Ee Mama mbarikiwa na Bikira mwenye uchungu, Malkia wa Mashahidi, uliyesimama chini ya msalaba na uliyemtazama Mwana wako akifa, unitazame kwa huruma ya kimama ninayekusikitikia. Kwa sababu ya upanga uliochoma moyo wako, kwa mateso ya maisha yako nakuomba uniangalie kwa wema ukasikilize maombi yangu. Nakuomba, ee Mama, uniombee daima kwa Mwana wako, najua hawezi kukuvyima wewe kitu chochote. Basi, ufanye, Moyo wa Mwanao ukubali kunijalia ombi langu hili โฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆ(taja ombi lako). Maana nitamkimbilia nani katika mahitaji na misiba yangu isipokuwa kwako, ee Mama wa huruma? Wewe hasa unaweza kutusaidia sisi tulio bado katika bonde la machozi kwa sababu ulishiriki mateso ya Mwanao kutukomboa. Umtolee Yesu tone moja la Damu yake takatifu. Umkumbushe ya kuwa wewe ni matumaini, furaha na maisha yetu ukanipatie jambo ninalokuomba kwa Yesu Kristo, bwana wetu. Amina.
Sali Atukuzwe 7 kwa heshima ya Malaika 7 wateule ujipatie neema ya kuepa dhambi mbaya saba na kutujaza mapaji saba ya Roho Mtakatifu.
TUOMBE Ee Mungu Mwenyezi wa milele, kwa wema na huruma yako ya ajabu, umetaka watu wako waokoke, ukamweka Malaika Mkuu Mikaeli kuwa Mkuu wa Kanisa lako, Utukinge na adui zetu, wasitusmbue saa ya kufa kwetu, bali tuongozwe naye kwenye utukufu wako Mkuu. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana Wetu Yesu Kristo. Amina.
Utuombee Ee Mtukufu Mtakatifu Mikaeli Mkuu wa Kanisa la Yesu Kristo, tujaliwe ahadi za Kristo. Amina.
Kumheshimu Mungu wangu, Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike, Amri zake tu nishike, Wazo neno tendo lote, Namtolea Mungu pote, Roho, mwili chote changu, pendo na uzima wangu, Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda, Jina lako nasifia, Utakalo hutimia, Kwa utii navumilia, Teso na matata pia, Nipe Bwana neema zako, Niongezee sifa yako, Amina.
Novena ya Noeli (maarufu kama novena ya Mt. Andrea)
Husaliwa kuanzia tar 30 Nov hadi usiku wa Noeli, tar 24 Disemba. Inajulikana kama novena ya Mt. Andrea kwa sababu novena hii huanza kusaliwa katika siku ya kumbukumbu ya Mt. Andrea Mtume.
“IHESHIMIWE, NA IBARIKIWE, SAA ILE NA WAKATI ULE, AMBAO MWANA WA MUNGU, ALIZALIWA NA BIKIRA MBARIKIWA SANA, USIKU WA MANANE, KULE BETHLEHEM, WAKATI WA BARIDI KALI. WAKATI HUO, UPENDE E MUNGU WANGU, KUSIKIA MAOMBI YANGU, NA KUNIJALIA YALE NINAYOYAOMBA KWAKO, KWA NJIA YA MASTAHILI YA MWOKOZI WETU YESU KRISTO, NA YA MAMA YAKE MBARIKIWA. AMINA. (Sali mara 15 kwa siku).
Inasadikika kuwa chochote uombacho kwa imani kwa sala hii utakipata mradi kipatane na mapenzi ya Mungu. Sali na watoto/ familia kuwatafakarisha na kuwaongezea matazamio juu ya sikukuu ya Noeli.
Roho ya Kristo unitakase Mwili wa Kristo uniokoe Damu ya Kristo unifurahishe Maji ya ubavu wake Kristo yanioshe Mateso ya Kristo nguvu yanizidishie Ee Yesu mwema unisikilize Katika madonda yako unifiche Usikubali nitengwe nawe Na adui mwovu unikinge Saa ya kufa kwangu uniite Uniamuru kwako nije Na watakatifu wako nikutukuze Milele na milele. Amina.
Ee Baba yetu Mungu Mkuu, Umenilinda usiku huu, Ninakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho, Nilinde tena siku hii, Niache dhambi nikutii, Naomba sana Baba wee, Baraka yako nipokee, Bikira safi ee Maria, Nisipotee unisimamie, Mlinzi Mkuu Malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee, Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwake juu, Amina.
(Sala hii inafaa sana kwa ajili ya kutetea uhai wa watoto wachanga wakiwa tumboni mwa mama zao, dhidi ya utoaji mimba au hatari nyingine dhidi ya uhai wa binadamu)
Ee Mt. Yosefu, wewe ni Mchumba safi na Mpenzi wa Bikira Maria, u Baba Mlishi wa Yesu, mlinzi na mtunzaji wa Familia Takatifu, na wa familia zote. Tuna imani kabisa katika uangalizi wako uliojaa upendo, juu ya uhai mpya, na uaminifu wako kwa familia.
Tunaweka jitihada zetu chini ya ulinzi wa sala zako. Utusaidie daima katika kutetea zawadi ya uhai wa binadamu, ili ukue hadi uzima wa milele ulioahidiwa na kujaliwa kwetu na Mwanao, Ndugu yetu, Yesu Kristu. Amina.
Mwongozo wa namna ya Kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema โKwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Aminaโ.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, โTusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk).
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika: โMungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, โฆโฆ Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, โฆโฆ Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, โฆ..โ
Au;
โUtuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,โฆ. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,โฆ. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, โฆ..โ Au; โSalamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,โฆ.. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,โฆ.. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,โฆโฆโ Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi. Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Mariaโฆ, โAtukuzwe..โ, โEe Yesu wanguโฆโ na โTuwasifu mileleโฆโ kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuungโarisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,โฆโฆ Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia โฆโฆโฆ Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu โฆโฆ.. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja โฆโฆ.. Utuhurumie
Maria Mtakatifu โฆโฆโฆ. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu โฆโฆ.. utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira โฆโฆ.. utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,โฆโฆโฆโฆ..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Baba Yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe; ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina
Ee Moyo Mtakatifu sana wa Yesu, chemchemi ya kila baraka, ninakuabudu, ninakupenda, na kwa majuto halisi ya dhambi zangu, nakutolea moyo wangu dhaifu. Nifanye mnyenyekevu, mvumilivu na safi, nikikubali na kuyatii kabisa mapenzi yako. Ee Yesu mwema, unijalie niishi nawe na kwa ajili yako. Unilinde niwapo katikati ya hatari, unifariji katika mateso, unipe afya ya mwili na msaada katika mahitaji ya mwili, Baraka yako juu ya kila nilifanyalo, na neema ya kifo chema. Amina.
Ee Yesu uliyesema โKweli nawaambieni, ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, gongeni nanyi mtafunguliwaโ, tazama ninagonga, ninatafuta na kuomba โฆโฆ.. (Taja ombi lako) Baba Yetuโฆ.., Salamu Maria โฆโฆ.., Atukuzwe Babaโฆโฆ.. Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutumainia kwa moyo wote!
Ee Yesu uliyesema โKweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu mtapewaโ, tazama kwa jina lako ninaomba โฆโฆ. (Taja ombi lako) Baba Yetuโฆ.., Salamu Maria โฆโฆ.., Atukuzwe Babaโฆโฆ.. Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutumainia kwa moyo wote!
Ee Yesu uliyesema โKweli nawaambieni, mbingu na dunia zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamweโ, tazama, nikitiwa nguvu na maneno yako ya kweli ninaomba โฆโฆ.. (Taja ombi lako) Baba Yetuโฆ.., Salamu Maria โฆโฆ.., Atukuzwe Babaโฆโฆ.. Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutumainia kwa moyo wote!
Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambaye kwako ni kitu kimoja tu kisichowezekana, ambacho ni kutoacha kutowaonea huruma wenye huzuni, utuhurumie sisi wakosefu maskini na utujalie neema tukuombayo kwa njia ya Moyo Imakulata wa Maria, Mama yetu mpole.
Sali โSalamu Malkiaโ na kuongezea, โMtakatifu Yosefu Baba Mlishi wa Yesu, utuombeeโ.
P.S. โ Sala hii ya Novena ilisaliwa kila siku na PADRE PIO kwa ajili ya kuwaombea wale wote waliomwomba msaada wa sala zake. Unaweza kuisali kwa namna tofauti tofauti. Mfano, kama Novena ya siku tisa, ambapo unasali sala hii mara moja au zaidi kila siku kwa siku tisa, au unaweza kuifanya kama Novena ya masaa, ambapo unasali sala hii kila baada ya saa moja kwa masaa tisa kwa siku hiyo hiyo, hasa kama kitu unachokiomba ni cha haraka au umesongwa moyoni. Vilevile unaweza kuifanya sala hii kama sehemu ya sala zako za kila siku katika mwezi Juni ambao ni mwezi uliotengwa na Kanisa kwa ajili ya kuuheshimu Moyo Mtakatifu wa Yesu, na hapo utaitumia kuwaombea watu waliokuomba msaada wa sala zako kama alivyofanya Mtakatifu Padre Pio. Pia unaweza kuitumia kama sala yako ya siku zote au ya mara kwa mara kwa ajili ya mahitaji mbalimbali.
Tuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu Mwenyezi, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, milele na milele, Amina.
Ee Utatu Mtakatifu wa Mwenyezi Mungu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nasadiki kuwa upo hapa na mahali pote. Ee Mungu wangu, umeniumba, umenikomboa, umenifanya mkristo, umenizidishia neema zako hapa duniani, umenitayarishia makao yangu mbinguni, umenijalia na siku hii nikutumikie. Ee Mungu wangu! Nakuabudu, nakushukuru, nakuomba toba, nakupenda! Ee Mungu wangu, nakutolea roho yangu, na mawazo, na maneno, na kazi, na furaha, na mateso yangu: uyapokee unipe neema yako nisikutende leo dhambi!
Kwa ajili ya Baba Mtakatifu wetu ..(N); Bwana, umpe moyo wako wa uchungaji mwema Kwa ajili ya warithi wa Mitume; Bwana, uwape wawe na uangalifu uliojaa upendo kwa mapadre wao Kwa ajili ya Maaskofu wako waliochaguliwa na Roho Mtakatifu; Bwana, uwabakishe karibu na kondoo wako Kwa ajili ya wachungaji wako; Bwana, uwafundishe kutumikia kuliko kutafuta kutumikiwa Kwa ajili ya waungamishi na washauri wa kiroho; Bwana, uwafanye kuwa vyombo visikivu kwa Roho wako Mtakatifu Kwa ajili ya mapadre wanaotangaza neno lako; Bwana, uwawezeshe kushirikisha Roho wako na Uzima wako Kwa ajili ya mapadre wanaosaidia utume wa walei; Bwana, uwatie moyo wa kuwa mifano bora Kwa ajili ya mapadre wanaofanya kazi na vijana; Bwana, uwajalie wawakabidhi vijana kwako Kwa ajili ya mapadre wanaofanya kazi kati ya watu fukara; Bwana, uwajalie wakuone na wakutumikie kupitia hao Kwa ajili ya mapadre wanaoangalia wagonjwa; Bwana, uwajalie wawafundishe thamani ya mateso Kwa ajili ya mapadre fukara; – Uwasaidie ee Bwana Kwa ajili ya mapade wagonjwa; – Uwaponye ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wazee; – Uwapatie tumaini la raha ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wenye huzuni na walioumizwa; -Uwafariji ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wanaohangaishwa na wale wanaosumbuliwa; – Uwape amani yako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wanaodharauliwa na wanaonyanyaswa; – Uwatetee ee Bwana Kwa ajili ya mapadre waliokata tamaa; – Uwatie moyo ee Bwana Kwa ajili ya wale wanaosomea upadre; – Uwape udumifu ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; – Uwape uaminifu kwako na kwa Kanisa lako ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; – Uwajalie utii na upendo kwa Baba Mtakatifu na kwa maaskofu wao ee Bwana Kwa ajili ya mapadre wote; – Uwajalie waishi katika umoja na maaskofu wao ee Bwana Tunawaombea mapadre wote; – Wawe wamoja kama Wewe na Baba mlivyo wamoja ee Bwana Tunawaombea mapadre wote; – Waishi na kuendeleza haki yako ee Bwana Tunawaombea mapadre wote; – Washirikiane katika umoja wa ukuhani wako ee Bwana Tunawaombea mapadre wote, wakiwa wamejawa na uwepo wako; – Waishi maisha yao ya useja kwa furaha ee Bwana Tunawaombea mapadre wote; – Wajalie ukamilifu wa Roho wako na uwageuze wafanane nawe ee Bwana Kwa namna ya pekee, ninawaombea mapadre wale ambao kwa njia yao nimepokea neema zako. Ninamwombea padre aliyenibatiza na wale walioniondolea dhambi zangu, wakinipatanisha na Wewe na Kanisa lako. Ninawaombea mapadre ambao nimeshiriki Misa walizoadhimisha, na walionipa Mwili wako kama chakula. Ninawaombea mapadre walionishirikisha Neno lako, na wale walionisaidia na kuniongoza kwako. Amina.
Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.
TESO LA KWANZA
Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga. Tuombe neema ya kuvumilia mateso. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA PILI
Maria na Yosefu walikimbilia Misri usiku ili kumficha Mtoto Yesu asiuawe na Herodi. Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA TATU
Mama Maria aliona uchungu sana Mtoto Yesu alipopotea kwa siku tatu. Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA NNE
Mama Maria aliona uchungu sana alipokutana na Mwanae Yesu katika njia ya Msalaba. Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA TANO
Mama Maria aliona uchungu sana alipomwona Mwanae Yesu akisulibiwa Msalabani. Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA SITA
Mama Maria aliona uchungu sana alipopakata maiti ya Mwanae Yesu baada ya kushushwa Msalabani. Tuombe neema ya kutotenda dhambi. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
TESO LA SABA
Mama Maria aliona uchungu sana aliporudi nyumbani baada ya kumzika Mwanae Yesu Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria. Mama wa mateso utuombee. Baba Yetu โฆโฆโฆ Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba โฆโฆ Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.
Salamu Maria Umejaa neema Bwana yu nawe Umebarikiwa kuliko wanawake wote Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa Maria Mtakatifu Mama wa Mungu Utuombee sisi wakosefu Sasa, na saa ya kufa kwetu. Amina.
Tusali kila siku sala hizi, angalau kwa mwezi wa saba (Julai) kila mwaka, mwezi wa kuheshimu Damu Takatifu ya Mkombozi wetu.
Yesu alimwahidi Mt. Brigita wa Sweden kwamba wale watakaosali Baba Yetu 7 na Salamu Maria 7 kwa miaka 12 kwa kuheshimu damu yake takatifu na kutafakari juu ya Kutahiriwa kwake, jasho lake la damu, kupigwa kwake mijeledi, kuvikwa taji la miiba, kuchukua kwake Msalaba, kusuliwa kwake na kuchomwa ubavuni; watapata neema 5 zifuatazo: (1) Hawataingia toharani, (2) Yesu atawapa cheo cha mashahidi waliomwaga damu yao kwa ajili ya imani, (3) Yesu atawadumisha jamaa zake watatu katika hali ya neema, (4) Roho za jamaa zake zitakingwa na Jehanam mpaka kizazi cha nne, (5) Mwezi kabla ya kufa, Yesu atawajulisha. Wakifa kabla ya kutimiza miaka ile, watahesabiwa wamemaliza.
Ee Yesu, sasa ninataka kusali Baba yetu mara saba nikiungana na ule upendo ambao kwao uliitakasa sala hii katika Moyo wako. Uichukue kutoka mdomoni mwangu hadi moyoni mwako. Uiboreshe na kuikamilisha hivyo kwamba iupatie heshima na furaha kwa Utatu Mtakatifu kama vile Wewe ulivyoupatia kupitia sala hii wakati ulipokuwa bado hapa duniani. Utukuzwe ee Yesu, itukuzwe Damu Yako Takatifu sana uliyoimwaga kutoka katika Majeraha Yako Matakatifu.
1. Yesu anatahiriwa.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, kupitia mikono safi ya Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutolea Majeraha ya kwanza, maumivu ya kwanza na Damu ya kwanza aliyomwaga Mwanao mpenzi, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu na dhambi za dunia nzima, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya dhambi ya kwanza ya mauti, hasa kati ya ndugu zangu.
2. Yesu anatokwa Jasho la Damu bustanini Gethsemane.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, kupitia mikono safi ya Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutolea mateso na mahangaiko makali sana ya moyoni, ya Bwana wetu Yesu Kristu katika mlima wa mizeituni na kila tone la jasho lake la damu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu za kimoyomoyo, na dhambi za namna hiyo zinazotendwa na dunia nzima, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya dhambi za moyoni na kwa ajili ya kueneza upendo wa kiMungu na wa kindugu.
3. Yesu anapigwa mijeledi.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, kupitia mikono safi ya Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutolea majeraha elfu elfu aliyopata, maumivu makali sana na Damu Takatifu sana aliyomwaga, alipopigwa mijeledi, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu za tamaa ya mwili, kwa malipizi ya dhambi za tamaa ya mwili za wanadamu wote, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya dhambi za tamaa ya mwili, na kwa kulinda usafi wa moyo, hasa kati ya ndugu zangu.
4. Yesu anavikwa taji la miiba.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, kupitia mikono safi ya Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutolea majeraha, maumivu na Damu Takatifu kutoka katika Kichwa Kitakatifu cha Yesu wakati alipovikwa taji la miiba, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu za rohoni, kwa malipizi ya dhambi za rohoni za wanadamu wote, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya dhambi za rohoni, na kwa ajili ya kueneza Ufalme wa Kristu hapa duniani.
5. Yesu anachukua Msalaba.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, kupitia mikono safi ya Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutolea mateso ya njia ya Msalaba, hasa donda lake la begani na Damu Takatifu iliyomwagika, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu za ukaidi dhidi ya msalaba, na dhambi za ukaidi dhidi ya msalaba za wanadamu wote, malalamiko yote dhidi ya mipango yako mitakatifu na dhambi zote za ulimi, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya dhambi za ulimi na kwa ajili ya upendo wa kweli kwa Msalaba.
6. Yesu anasulibiwa.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, kupitia mikono safi ya Maria na Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakutolea Mwanao Msalabani, kupigwa kwake misumari na kuinuliwa kwake, madonda yake mikononi na miguuni na mifereji mitatu ya Damu yake Takatifu iliyomwagika kutoka katika majeraha haya, mateso yake makali sana ya mwili na roho, kifo chake kitakatifu, ukumbusho usio wa kumwaga wa damu wa kifo hiki katika Misa zote Takatifu ulimwenguni, kwa ajili ya majeraha yote yanayosababishwa na ukaidi wa nadhiri na kanuni katika madaraja matakatifu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zangu zote na za ulimwenguni mzima, kwa ajili ya wagonjwa na wanaokufa, kwa ajili ya mapadre watakatifu na walei, kwa ajili ya nia za Baba Mtakatifu za kukarabati familia za kikristu, kwa ajili ya kuimarika kwa imani ya kikristu ulimwenguni, kwa ajili ya nchi yetu na muungano kati ya mataifa ndani ya Kristu na Kanisa lake, na kwa ajili ya wokovu wa dunia nzima.
7. Yesu anachomwa kwa mkuki moyoni.
Tafakari fupi (kimya kidogo). Baba Yetu โฆ. Salamu Maria โฆ. Baba wa Milele, ukubali kupokea, kwa ajili ya mahitaji ya Kanisa Takatifu na kwa ajili ya malipizi ya dhambi za wanadamu wote, Damu na Maji Takatifu vilivyomwagika kutoka jeraha la Moyo Mtakatifu wa Yesu. Utuhurumie. Damu Takatifu ya Yesu, tone lile la mwisho lililomwagika kutoka katika Moyo wake Mtakatifu, unioshe mimi na wengine wote dhambi zetu zote! Ee Maji kutoka katika Moyo Mtakatifu wa Yesu, unioshe na adhabu zote za dhambi zangu na uizime miale ya moto wa toharani kwa ajili yangu na kwa ajili ya roho zote zilizomo toharani. Amina.
Katika mwaka wa Kanisa wa kiliturjia, mwezi Julai ni wa kuiheshimu Damu Takatifu ya Yesu.
Ee uliye Mkuu, Mt. Yosefu, uliyatii kabisa maongozi ya Roho Mt. Unijalie neema ya kufahamu aina ya maisha ambayo Mungu anapenda mimi niishi. Usiniache nidanganyike katika jambo muhimu kama hili, ambalo furaha yangu hapa duniani inalitegemea, na hata pia wokovu wa roho yangu.
Unijalie, nikiangazwa na matakwa matakatifu na nikiwa mwaminifu katika kuyatimiza, nikumbatie aina ya maisha ambayo Mungu ameniandalia na yatakayoniongoza kwenye furaha ya milele. Amina.
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,โฆโฆโฆโฆ..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Ee Moyo Mtakatifu wa Yesu, ninakukimbilia, ninakuja kwako katika mikono yako yenye huruma. Ndiwe tegemeo langu na tumaini langu dhabiti. Ndiwe mwenye dawa ya maovu yangu yote, malipizi ya makosa yangu yote. Waweza kunipatia haja zangu na neema ninazoziomba mimi na wengine. Wewe uko ili kutusaidia sote, ndiwe mwanga mkuu usiozimika, ndiwe chanzo cha nguvu, uvumilivu, amani na faraja. Nina hakika kuwa maombi yangu hayatakuchosha, nawe hutaacha kunisaidia, kunilinda, kunipenda, kwani, ee Moyo Mtakatifu , upendo wako hauna mwisho. Ee Moyo Mtakatifu, unihurumie, kwa ajili ya maombi yangu, kadiri ya huruma yako. Nawe katika sisi, na kwa ajili yetu, ufanye lolote unalolihitaji, kwani tunajitoa kwako kwa imani na uhakika thabiti kwamba kamwe hautatuacha, kwa milele. Amina.
Please note that AckySHINE Swahili Website is not active.ย
Because of unavoidable circumstances AckySHINE Swahili Website will not be updated starting from May 2018. No new post will be published from May 2018.
However, You can view/read old pages (public pages) which were created before May 2018 and shared to public.
With hundreds of old public pages, we believe Swahili Website service can still be useful to the public users.
“๐Kitabu cha Sala Muhimu: Mkusanyiko wa SALA, LITANIA NA NOVENA” has been added to your cart. View cart
Login
Register
Application Legal Notice
We, the Operators of this Application, provide it as a public service to our users.
Terms of Use
Please carefully review theย Terms of Use that govern your use of the Application and Website. Please note that your use of the Application constitutes your unconditional agreement to follow and be bound by these Terms and Conditions of Use. If you (the “User”) do not agree to them, do not use the Application, provide any materials to the Application or download any materials from it.
Privacy Policy
Theย Privacy Policy explains what we may do, and will not do, with your personal data that might be collected while you use this application and its services. Please read this policy and if you do not agree with it, please do not use this application or any of the services on it.
Further
If you have questions regarding these policies pleaseย contactย us.
Enjoying?
Hey there! ๐
I’m so happy you’re here! ๐ฅณ
If you’re enjoying yourself, please leave a comment๐ฌ.
Thanks for reaching out! Send me a message on WhatsApp via the link below or email through the form. I prefer messages over calls, so please avoid calling. Thanks!
AckySHINE is a Platform that support provision of both Online and Offline Services.
We provide the following Services
Research Consultancy– Active Offline Service We offer consultation services in Research, including research concept development, designing, data collection and processing and report writing.
Monitoring and evaluation Consultancy– Active Offline Service We offer consultation services in M&E Planning, Process Evaluation and In Impact Evaluation.
Training and facilitation Consultancy– Active Offline Service We offer consultation services inย Training and Facilitation. This include Training Planning, Session Plan and Management as well as Conduction of Training andย facilitationย session.
English – Swahili Translationย services– Active Offline Service We translate Short Texts, Documents and webpage from English to Swahili and vise versa. We provide live human support, translation is done by native speaking translators, no automatic translation.
Web designing and development– Active Offline Service We offer WordPress Set up service and Customization Services. Free Templates, SEO optimization, One Year Assistance, Responsive Design, Mobile Friendly.
AckySHINE Dedications– Pending Online Service This is a special place for sendingย dedicationsย to the person you love. Via WhatsApp and SMS.
AckySHINE Shop– Pending Online Service This is anย Digital shopping serviceย aim at sharing of knowledge and skills through soft copy books.
AckySHINE Library– Pending Online Service Welcomeย AckySHINE Libraryย where you can get unlimited Books. Feel Free to Download our Books.
English Website– Pending Online Service This isย English multi-category websiteย special designed for information, entertainment and motivation
Swahili website– Pending Online Service This isย Swahili multi-category websiteย special designed for information, entertainment and motivation
Advertising and marketing– Active Online Service We Display banner, image & links on our website. For ads we offer freeย translationย (English to Swahili), free Landing page, you can embed forms on your landing page and embed HTML Codes. You can also publish your posts on our website with unlimited words, unlimited pictures, unlimited videos and free translation service. Your posts will be intergraded in post categories.
[rpt name=”research-assistance”]
Our Spring Sale Has Started
You can see how this popup was set up in our step-by-step guide: https://wppopupmaker.com/guides/auto-opening-announcement-popups/
Sh3,000Original price was: Sh3,000.Sh0Current price is: Sh0.Download Now
AckySHINE Development Changelog
Welcome AckySHINE, We are still developing AckySHINE platform. Almost all services are not available for now because of reprogramming state. However, some services might be available from time as we are occasionally testing our services before full launching. We are sorry for any inconvenience.
Share your ideas and suggestions for our services here. We will be happy to hear from you.
Because of unavoidable circumstances this website (ackyshine.com) will not be updated starting from May 2018 till further notice.
No new post will be published. However you can only view/read old pages (public pages), which are pages created before May 2018 and shared to the public.
With thousands of old public pages, this website can still be useful and active to the public users.
AckySHINE is a consultancy office operating in Tanzania and providing professional services in the areas of Community development issues, Social science research and Project planning, monitoring and evaluation.
Main Consultation Services
Research methodology
Research Design/Planning
Data collection
Data Processing and analysis
Project/Programme management and evaluation
(M&E) Monitoring and Evaluation Project/Programme
Planning and implementation
Web design and Development
And Other relating services
You are Always Welcome
We are well placed to ensure optimum solutions for numerous clientsโ projects. We prefer a relationship based on mutual trust, co-operation, and communication
For us, the trust between the consultant and client is paramount. Enjoy the friendly atmosphere of his office when visiting.
Welcome AckySHINE Charity
AckySHINE charity is a program for humanitarian campaigns and aid aimed at promoting peace and unity, protecting the environment, and maintaining the health and development of individuals and the community as a whole. These campaigns are advertised through ackyshine.com.
Recent Comments