Hadithi za Kiswahili

Stori inayogusa!!

Habari ya mama aliyeuguliwa ghafla na mtoto wake majira ya SAA 2 usiku, mtoto alibanwa na kifua(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda kuomba msaada kwa jirani yake aliyekuwa na gari, akamjibu gari haina mafuta, akaenda kwa mchungaji ili amsaidie, akamjibu nina wachungaji toka USA, hivyo sitaweza kuwaacha peke yao, mama hakuwa na jinsi aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije kufa kama baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo.

 

Huyo mama alikuwa na tatizo la mguu na mtoto alikuwa mzito, mama alianguka Mara kadhaa na akainuka kuendelea na safari. Njiani alikutana na watu waliotoka kazini aliomba wamsaidie walimpuuza na alijaribu kusimamisha magari hayakusimama. Kichaa mmoja mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani alipomuona yule mama anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali. Ma doctor walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura, wakamchukua mtoto na kumhudumia haraka, baada ya dk.10, mama wa mtoto akawasili, kisha ma doctor wakatoa taarifa kuwa, mtoto angecheleweshwa dk 5 angekufa. Mungu alimtumia yule kichaa mchafu kuokoa maisha ya mtoto. Hivyo usimteegemee Mch, jirani, wenye magari, matajiri nk. Mungu huweza kuinua MTU usiyemdhania kukubariki. Mwamini Mungu atakubariki. Usitumainie wanadamu hakuna baraka kwao. Mungu huinua vinyonge ilI kuangusha vyenye nguvu. Tuma ujumbe huu wa BARAKA kwa watu japo wanne ili kushiriki BARAKA hizi za Mungu, ujumbe huu waweza tena nitumia nami ktk kutakiana BARAKA za MUNGU WETU.

Huruma ya mama kwa mwanae ilivyomtesa

Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.

Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee, na ikitokea mama yake akamtembelea basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania. Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.

Lakini mama alimpenda mwanae na hakuonesha kukasirika hata pale mwanae alipomnyanyapaa waziwazi.

Badae mtoto akakuwa akamaliza masomo yake na kupata kazi nzuri. Akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake ‘chongo’ anayemtia aibu.

Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake. Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa ktk jamii yake.

Siku moja asubuhi akasikia wanae wakilia walipokua nje wakicheza.. Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha.. Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae. Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja (chongo). Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi.

Alipomtizama vizuri yule mwanamke akamgundua ni mama yake mzazi. Alikua amechoka na amezeeka sana. Amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa..

Mtoto kwa hasira akamuuliza “mama umekuja kufanya nini hapa? Kama una shida ungenipigia simu sio kuja? kwanza nani kakuonyesha ninapoishi? Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango? Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako”

Mama yake akasema “samahani mwanangu, sikujua naomba unisamehe”. Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.

Baada ya siku chache kupita, yule jamaa akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona. Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akasikie mama yake anataka kumwambia nini.

Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao. Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua sana bila msaada wowote.

Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake.. Barua ilisomeka hivi…

“Kwako mwanangu mpendwa wa pekee,
Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui kama nitapona.. Nimeugua nikakosa matibabu kwa kutokuwa na fedha. Sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida yangu zaidi yako wewe mwanangu wa pekee… Lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie matibabu ulinifukuza na kudai nawatisha wanao kwa chongo langu ! Uliniumiza sana mwanangu sitisahau maishani mwangu ila nimekusamehe.

Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana. Nami sikubahatika kupata mtoto mwingine. Nilikulea kwa nguvu zangu zote na umasikini niliokuwa nao ilikuwa nikitegemea badae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ! Hivyo unaona aibu kuwa nami….

Nisamehe kwa kuwatisha wanao kwa chongo langu, nisamehe kwa kuja kwako bila ya taarifa, nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio kwa kuwa mimi mama yako ni chongo….

Lakini naomba nikupe siri ambayo hukua unaijua ewe mwanangu, wewe ndiye uliyezaliwa ukiwa chongo. Ulikua na jicho moja tu. Nikaumia sana kuona mwanangu ana jicho moja, atawezaje kuishi na kukabiliana na changamoto za maisha.. Nikaomba madaktari wanitoe jicho langu moja wakupe wewe, Niliona ni heri mimi niwe chongo kwa kuwa nimeshaona mengi sana duniani kuliko wewe..

Na ulipowekewa jicho langu nilifurahi kukuona una macho mawili nikajua utaweza kuzikabili vema changamoto za dunia hii… Na hakika jicho langu limekusaidia kwani wewe ni mtu mashuhuri na tajiri sana kwa sasa…

Lakini kwa jinsi ninavyoumwa najua nitakufa. Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu. Kwa kutumia jicho langu umeweza kuwa msomi mzuri na tajiri unayeheshimika na jamii yote.. Wasalimie wajukuu zangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu.. Please take care of my eye…

Akupendaye,
Mama”

Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana. Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema wake aliomtendea.. Lakini haikuwezekana, it was TOO LATE.!

MORAL OF THE STORY.!

Nyuma mafanikio ya kila mwanaume yupo mwanamke. Anaweza kuwa mama yako, mke wako, dada yako au mchumba wako.. Je unatambua nafasi yake katika mafanikio yako au unampuuza tu?

Wapo wanawake ambao walijitoa sadaka ili uweze kuwa hapo ulipo. Jiulize mama yako amefanya mangapi kukufikisha hapo.

Hadithi hapo juu inatueleza juu ya mama aliyetoa jicho lake kwa mwanae.. lakini jicho ni kielelezo tu cha yale wanayofanya mama zetu.

Kuna wengine jicho lao ni vibarua alivyokua anafanya ili wewe usome.. Pengine jicho lake ni namna alivyokua akijinyima kwa kuvaa nguo moja mwaka mzima ili upate ada ya shule na mahitaji mengine.. Je umewahi kumshukuru mama yako kwa kutoa jicho lake kwa ajili yako??

Mpende sana mama yako.. Wapende wanawake wote, waheshimu, walinde, wajali. Wanapitia magumu mengi sana ili kutufanya sisi wanaume tuwe kama tulivyo.

Kisa cha kusisimua cha mama mjane

Mimi ni mwanamke mjane ninaishi mjini Arusha. Huu ni ushuhuda wangu wa maisha yangu.

Miaka 21 iliyopita nilifunga ndoa na mume wangu mpendwa kanisani, baadaye tukajaliwa kuwa na watoto wa2 mmoja wa kiume Alfred na mwingine wa kike Minza. Mimi nimesomea mambo ya uuguzi MD, nimefanya kazi muda mrefu ktk hospitali za wilayani karatu na Arusha mjini mpk nilipolazimika kuacha kutokana na udhaifu wa mwili na mambo yaliyonipata katika maisha. Mume wangu alikua ni askari polisi mpk baadaye alipojiunga na ajira zingine mpaka alipokutwa na mauti kama nitakavyoeleza baadaye hapo chini.

Tulipooana na mume wangu,maisha yalikua ya furaha sana na tulikua na mipango mingi mizuri ya kujiendeleza kiuchumi na kihuduma kwani tulikua tunampenda Mungu na tulikua waimbaji na waombaji kanisani. Baada ya muda mrefu katika maisha ya ndoa na familia, baadaye maisha yalianza kuwa magumu kutokana na mishahara yetu kuwa midogo ukilinganisha na mahitaji. Mume wangu alijisikia vibaya sana zaidi yangu hasa pale alipoona wengine hasa marafiki zake wanafanikiwa lkn yeye hafanikiwi. Kuna maaskari walikua wakipandishwa vyeo haraka na kuhamishiwa mijini ikiwemo Daressalaam na Arusha- hali hiyo ilimpa shida sana akawa anaomba na kufunga kwa muda mrefu lkn hakuona mafanikio.

Wakati fulani ilitokea akakutana na rafiki yake askari mwenzie, akamualika nyumbani kwake. Mume wangu aliporudi akaja akiwa mwenye mawazo makubwa sana, sikujua ni kwanini na hukuniambia hata nilipomuuliza.

Baada ya siku kadhaa mume wangu akaacha kwenda kanisani wala huduma hakufurahia tena. Akawa ni mkimya na mwenye mawazo mengi sana. Siku moja akaniambia atasafiri kikazi kwa muda wa siku tatu. Baada ya siku tatu akarudi akiwa hoi sana na mgonjwa km mtu mwenye malaria. Nikajaribu kumshawishi twende hospitali hakukubali kbs akaniambia ni uchuvo tu wa safari na kazi na atakuwa salama. Kesho yake, kweli akaamka vzr na kwenda kazini bila kuugua km hapo jana. Ikapita muda mrefu bila kujua hasa nini kinachoendelea kwa mume wangu kwani hakuniambia chochote hata nilipomuuliza.

Baada ya muda, mume wangu akapata nafasi ya kwenda masomoni Moshi. Alipomaliza masomo hayo,haikuchukua muda mrefu tukapata barua ya uhamisho wa mume wangu kikaz kuelekea Arusha mjini.

Binafsi nilifurahi sana, nikajua Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya siku nyingi. Kwa hiyo na mimi nikaanza mipango ya uhamisho. Tulipofika Arusha tukapata makazi mapya na kanisa zuri la kuabudia. Baada ya muda niligundua mume wangu hakupenda mambo ya Mungu km siku za zamani. Wakati huu mimi nilikua mjamzito nikijandaa kupata mtoto wa pili.

Tulizungumza sana na mwenzangu lkn sikujua hasa kitu gani kulikua kinamsumbua. Baada ya muda niligundua mume wangu alikua mlevi wa pombe na tabia yake ilibadilika sana hasa kuhusu mambo ya kiimani na kushirikishana mipango. Aligeuka kuwa mtu wa mambo mengi,kuamrisha na msiri sana- kutokana na aina ya kazi zao nikajua ni kawaida.

Nilipojifungua mtoto wetu wa pili akaniletea zawadi ya gari mark2-mimi nilikua miongoni mwa wanawake wachache kuendesha mark2 wakati miaka ya90 mwishoni. Tulijisikia vzr sana na mambo ni kama yalikua yananyooka.

Mwaka 2001 mume wangu alipata nafasi ya kwenda tena chuoni kusoma kwa muda mfupi huko Dar, nikabaki na familia na nikawa naendelea vzr na kazi zangu. Alipomaliza masomo akarudi na maisha yakaendelea kwa muda km kawaida. Baada ya miezi km sita kutoka chuo ni, mume wangu akaniambia anataka kuacha kazi- nilishangaa sana nikamuuliza maswali mengi lkn hukunijibu vzr. Wiki moja baadaye akaniambia ameacha kazi na ameajiriwa shirika moja kubwa la UN hapa Arusha.

Kweli akaanza kuvaa sare mpya za kazi hiyo mpya. Kazi hiyo mpya ilituletea mafanikio makubwa sana ya kifedha na kujieneza kwa mali. Wakati huo pia mimi nilipata nafasi ya kwenda kusoma chuoni muhimbili Dar kwa muda wa miaka mitano. Nikaenda Dar nikaiacha familia ikiendelea vzr kbs.

Nikiwa Dar chuoni nilipata nafasi ya kwenda nje ya nchi kufanya seminar ya health exhibitions (mafunzo ya maonesho)- nikiwa huko nilipigiwa simu kuwa mtoto wetu mdogo amefariki dunia. Nilichanganyikiwa nikarudi nyumbani kwa kuchelewa, nikakuta wameshamzika Alfred mwanangu sikumuona tena. Ilisemekana alifariki ghafla sana bila kujua hasa ni ugonjwa gani au alipatwa na nini mwanangu. Niliongea na madaktari, wakanieleza kuwa mwanangu alitokwa na damu nyingi sana mpk ndani ya jeneza. Uchungu mkubwa na kuchanganyikiwa vilinipata bila kujua hasa nini cha kufanya.

Niliporudi msibani nilishangaa kumkuta mume wangu akiwa na pete kubwa ya dhahabu yenye kinakshi cha tanzanite katikati mkono wa kuume. Nilipomuuliza akaniambia amenunua mjini bei ghali sana na pia ameninulia na mimi aina km hiyo ya pete. Sikujua chochote nikaipokea ile pete km zawadi nikawa naivaa. Pia akaniambia kuna kanisa jipya limeanzishwa hapa mjini ndio tutakua tunasali. Huko tulikutana na watu mbalimbali wa mataifa mengine na ibada zilikua ni za kiingereza. Tulienda kutambulishwa na mume wangu kwa mchungaji ambaye nayepia alikua amevaa pete km ya mume wangu-sikujali sana kwa siku hiyo. Nilijisikia vzr sana kwani huko nilimuona mume wangu akifurahia na kujitoa km zamani. Pia tulipata marafiki wengi akiwemo familia moja ya wakameruni waliokua karibu sana sisi. Tukahamia huko.

Baada ya muda baada ya kuipata ile pete na kurudi chuoni na kujiunga kanisa jipya huku Arusha, sikupenda tena kwenda kanisani wala kujishughulisha na mambo ya huduma kama awali. Nilijiona mwenye majukumu mengi sana na sina muda wa mambo ya kanisani na huduma. Wenzangu waliponiuliza, niliwajibu kuwa niko bize sana na masomo na shughuli za kikazi. Nikawa mzembe sana ktk mambo ya imani na huduma.

Lkn siku moja Nikiwa Dar wakati wa fellowship za chuoni, ndugu mmoja alitutembelea akahubiri kwa nguvu sana akatuambia kuna mtu amezingirwa na roho mbaya za kichawi zinazotafuta kumuangamiza na familia yake-sikuelewa hata kidogo wala hakupita mtu yeyote mbele siku hiyo. Yule muhuburi alilia sana kwa uchungu mpk mwisho wa ibada.

Baada ya kumaliza masomo mwaka 2007 nilirudi Arusha. Nikapata marafiki wengi na mitandao mbalimbali ya kibiashara ndani na nje ya nchi. Pesa ilikuwa nyingi mpk nikashangaa kuwa ni baraka za namna gani.

Mwaka 2009 siku moja nilishtuka na kitu kimoja pale mume wangu aliposahau pete yake (ile nyingine anayovaa mkono wa kuume sio ya ndoa) nyumbn. Mimi bila kujua nilipoiona niliihifadhi kwenye mkoba wangu nikaondoka nayo. Kumbe nyuma yangu, mume wangu alirudi nyumbn ghafla na kuitafuta sana pete akanipigia simu nikamwambia ninayo kwenye mkoba aje nilipo aichukue. Cha ajabu alipokuja ili nimpe ile pete haikuwepo tena kwenye mkoba. Nilijikagua na kuwauliza wafanyakzi wenzangu lkn pete haikuonekana. Mume wangu alichanganyikiwa na kunishambulia kwa makofi na matusi akiwa mwenye hasira kubwa- sikuwahi kumuona mume wangu akiwa mwenye hasira na ghadhabu kubwa kiasi kile. Alinidhalilisha hadharani mbele ya wafanyakazi wenzangu na kuniamrisha twende nyumbn haraka. Ofisi yao ilikua nikaribu na ofisi kwangu lkn alinipandisha gari yake na tukaelekea nyumbn bila kupitia ofisini kwao. Kwenye gari tulikua tunagombezana kwani nilijisikia kudhalilishwa kwa hali ya juu sana.

Tulipofika nyumbani, ugomvi ulikua mkubwa sana na sana mume wangu alinipiga kweli. Baadaye watu walikuja lkn hawakuweza kuingia ndani kwani kulikua kumefungwa. Mume wangu alinifungia kwenye chumba kimoja na nikamsikia akiwapigia simu watu kadhaa huku akilia km mtoto. Sikuelewa kwa kweli. Mchungaji wa kule kwenye kanisa letu alikuja na mtu mmoja ambaye alikua ni rafiki wa karibu wa familia yetu lkn foreigner.

Walipofika waliongea na mume wangu kwa muda afu wakaondoka. Mume wangu akaja akanifungulia mlango akaniambia tuongee- wakati huo alikua mpole na mkimya asiyelia tena.

Akaniambia kuwa ile pete iliyopotea ilikua ndio pete ya maisha yetu. Alipewa na huyo mchungaji na ilikua inamasharti makubwa kuwa lazima aivae yeye tu na isikae muda mrefu nje ya kidole chake. Kwa ufupi pete hiyo haikuwa ya kawaida na ile pete ilikua ni yule mtoto wetu (Alfred) aliyekufa miaka kadhaa iliyopita. Nilishtuka kujua hata ile pete niliopewa mimi haikuwepo mkononi mwangu wakati huo. Ilikua imetoweka, nikazimia kusikia maneno hayo. Nilipozinduka nilijikuta nyumbn kwa mchungaji nikiwa nimelazwa kitandani. Kumbe nilipozimia nilipelekwa hospitali na pia mume wangu akakamatwa na polisi akawekwa lokap lkn akaachiwa bady kutokana na ushawishi wake pale polisi na alipowaelezea anavyojua yeye. Alipotoka akaja hospitali wakanichukua mpk nyumbn kwa mchungaji. Nilipozinduka nikamuona mchungaji na yule rafiki yetu mkameruni walikua wamevaa pete km ile ya mume wangu iliyopotea. Hawakunisemesha kitu wala hawa kuomba lkn waliondoka kule chumbani wakiniacha na mume wangu mara baada ya kupata ufahamu.

Mume wangu alinichukua mpk nyumbn, tulipofika hatukuongea kitu mpk asbh. Yeye alienda mjini baadaye akarudi akiwa bado mwenye mawazo na wasiwasi mkubwa. Siku hiyo ikapita na kesho yake. Marafiki zangu walikuja kunitembelea ili kunipa pole lkn hawakuruhusiwa. Kumbe mume wangu aliwaambia watu pamoja na ndugu zangu kuwa nimemuibia mali nyingi sana nimeficha kusikojulikana. Ndugu zangu walipokuja aliwaruhusu kwa masharti kuwa nisiwaambie ukweli. Akanitisha kuwa nikisema ukweli tutakufa wote.

Maisha yaliendelea kwa siku kadhaa, nikaendelea na kazi lkn nikiwa mwenye mawazo makubwa. Nikaomba off kazini kwa muda ili nipate ahueni. Mume wangu naye akaomba off pia tukawa tunashinda ndani tu. Nyakati za usiku nikiwa nimelala mara nyingi niliota ndoto kuwa Alfred mwanangu ananiita yuko barabarani anahangaika akiwa analia. Nikimwambia mume wangu ananiuliza ni wapi eneo gani hasa, nikimtajia eneo nilipoota ananiambia hapo ndipo pete ilipo kwa hiyo ataifuata- nakweli mara nyingi alikua anaamka anaondoka eti kuifuata hilo eneo nilipomuona mtoto wangu kwenye ndoto.

Pete ile haikuwahi kuonekana na maisha yetu yalianza kuporomoka siku hadi siku. Mume wangu hakufurahi tena. Alikua ni mtu mwenye majonzi na wasiwasi sana juu ya maisha yetu siku zijazo. Wakati huo aliwafukuza wafanyakazi wote wa nyumbn na alininyanganya simu zote na alifungia ndani nisitoke nje

Siku moja ikitokea mjini katika mizunguko yake alinijia na habari mpya akidai kuwa ndio suluhisho la tatizo letu. Aliniambia kuwa ili turejee ktk maisha yetu ya kawaida inabidi tumuue mtoto wetu Minza pia kwa siku zote za maisha yetu kuanzia siku hiyo itakua ni marufuku kufanya mapenzi kwa njia ya kawaida ila tu kinyume na maumbile (yaani awe ananiingilia kinyume na maumbile ya mwanamke). Akaniambia hakuna namna nyingine ya kurejesha maisha yetu zaidi ya hivyo. Nilishtuka sana nikaogopa mno. Nilimlaumu sana mume wangu kwanini alijiingiza ktk maisha hayo- ndipo akanieleza hbr kamili kuwa mafanikio yetu yote yametokana na mfumo huo wa maisha tangu siku ile aliporudi ile safari tukiwa Karatu. Kumbe siku ile alikua ametoka kwa mganga aliyepelekwa na yule rafiki yake.

Nilimshauri mume wangu twende kwa mchungaji tukaombewe lkn akasema kuwa tukisema tu kwa watu tutakufa wote. Pia akasisitiza kuwa sisi wote tuko katika mtandao huo kwa hiyo sio rahisi kujiokoa tena. Kesho yake mume wangu alinikumbushia tena akasema ni lazima tufanye hivyo na pia sio kwa kulazimisha inatakiwa iwe kwa hiari ili tupate faida kwa haraka. Bado nilikataa, sikuwa tyr kufanya hivyo. Nilimuomba mungu usiku na mchana atusaidie. Lkn mume wangu Alinitisha sana na kunifinya mwili ili nikubali kwani alikua mwenye hasira na ghadhabu kubwa. Pia alinifungia ndani ili nisitoke nje. Pia alisisitiza nisiombe kbs. Maisha yaligeuka kuwa jehanam.

Siku km mbili zililizofuata tulipigiwa simu kutoka shuleni kwao na mtoto wetu kuwa Minza ametoweka shuleni hajulikani alipo. Tulikwenda haraka kujua hatma ya mtoto wetu. Niliogopa zaidi kwani nilijua labda ndio keshapatikana- japo mume wangu alionekana kuwa si mwenye wasiwasi ht kidogo. Nilianza kukumbuka kukemea na kuomba Mungu atusaidie lkn mume wangu alinikataza nisiombe kbs. Akanizabua kibao kikubwa mdomoni tukiwa kwenye gari mpk damu ikatoka mdomoni. Nikisikia uchungu mkubwa zaidi kwanini maisha yalikua yanaenda hivyo ghafla au nini faida ya kuishi basi.

Tulisafiri siku nzima mpk kufika shuleni kwa Minza mwanangu. Kitu cha ajabu ni kwamba tulimkuta mtoto akiwa hospitali amelzwa haongei wala hajitambui- na taarifa zinasema alikutwa chumbani(hostel) kwao mchana huo akiwa anatokwa na damu nyingi.

Siku kadhaa bdye tulipewa mtoto wetu baada ya kupata nafuu tukarudi naye nyumbn kwa matibabu zaidi. Minza aliendelea kuugua sana bila nafuu na hakuweza kuzungumza kitu alikua ni mtu wa kulala kitandani na kutazama tu.

Ilipita miezi kadhaa maisha hayo yakawa yamechukua sura ya familia yangu. Miradi kadhaa tuliyoifungua mjini ilikua imefungwa, pia kazini kwangu nilikua nakwenda kwa shida sana. Uwezo wangu wa akili na kiutendaji ulipooza sana. Nilijiingiza kwenye chama cha ulevi wa pombe km mume wangu ili kupoteza machungu na kupunguza mawazo. Lkn hai kusaidia. Lkn kule kanisani tuliendelea kwenda na mume wangu aliendelea na kazi kule UN.

Siku moja mume wangu aliniambia tunakwenda shambani kwa siku kadhaa twende wote- tulijiandaa tulikwenda pamoja. Tulipofika huko, tulijumuika pamoja na mchungaji na yule rafiki yetu mkameruni. Tulifurahi na kunywa na kula mpk usiku kwa siku hiyo ya kwanza. Kesho yake asubuhi na mapema niliitwa na mume wangu kuwa kuna kikao- Cha ajabu ni kwamba asbhu hiyo mchungaji na yule mkameruni walikua wamevalia mavazi ya kitamaduni kupitiliza kawaida yao. Tulikwenda mpk vichakani zaidi kwani walisema kuna maongezi muhimu sana.

Tukiwa huko yule mchungaji alitueleza waziwazi kuwa yeye ni mtu mwenye nguvu nyingi sana na amewasaidia wengi sana. Na pia hata zile mali za kwanza na kufanikiwa kwetu ni yeye ndiye aliyetusaidia kwa nguvu zake. Na nguvu hizo ni zilitokana pete yake. Pete yake ndio inayompa nguvu na kumletea bahati na mvuto kwa watu.

Kwa kuwa tulikua tumeshindwa kutekeleza sharti la kwanza la kumuua Minza na muda ulikua umepita basi, kuna sharti lingine la mwisho

Kwa hiyo, akasema anao uwezo wa kutupatia pete nyingine lkn ndio kwa masharti. Na leo hapo yuko tyr kutusaidia tena ili tufanikiwe na tusife- kwani tulikua tumefanya makosa makubwa sana kupoteza ile pete ya awali.

Akatoa masharti ili tupate pete nyingine inabidi mimi nikubali pale niingiliwe kimwili nao wote watatu. (yaani nifanye mapenzi na wote watatu pale kichakani hadharani na mmoja baada ya mwingine akianza mume wangu). Vinginevyo mume wangu atapoteza maisha pale pale na mimi pia ningekufa siku zijazo au ningekua kichaa. Nilishtuka nikaogopa sana, nikaanza kupiga mayowe huku nilikimbia kuelekea kwa mume wangu- nililia sana kwa uchungu huku nikitaja jina la mume wangu kwa kumlaumu kwanini alijiingiza kwenye mambo hayo. Mume wangu alinisihi nikubali ili tusife kwani hakukua na namna nyingine.

Sikukubali. Nilianza kukimbia kuelekea barabarani kuhofia usalama wangu kwani niligundua mume wangu hakuwa na uwezo tena wa kunisaidia au kujiokoa. Nilpofika mahala tulipopark magari yetu sikuona gari ht moja. Nikiwa ktk hali ya kukimbia na kujiokoa huku nikipiga mayowe niliwaona yule mchungaji na yule mkameruni wamenitokea nyuma na mbele yangu. Ghafla yule mchungaji aliniwekea mkono kichwani nikaanguka chini nikapoteza fahamu.

Niliporejea fahamu zangu ni siku nilipojikuta niko katikati ya kundi la watu walinisimamia na kuniangalia kwaumakini mkubwa sana. Kumbe ilikua ni kwenye maombezi. Fahamu zangu zilinirejea na kujitambua japo nilikua nimeharibika mwili na mavazi machakavu pia nikiwa nimefungwa kwa kamba ngumu sana. Nikifanikiwa kuwatambua baadhi ya ndugu jamaa na marafiki waliokuwepo pale.

Kwa masaa kadhaa nilijisikia kupumbaa kama mjinga bila kujua nifanye nini. Alitokea mtu mmoja akaniambia pole. Akaniuliza kama ninajisikiaje kwa wakati huo. Nikamuelezea. Kisha nikamuhoji kuwa hapo ni wapi- akaniambia kuwa ni kituo cha maombezi na yeye ndiye mchungaji.

Inasemekana kuwa siku hiyo nilikua nimefunguliwa kutoka katika ukichaa ulionisumbua kama miaka mitatu na nusu. Katika muda wote huo niliishi msituni km mnyama. Nilitafutwa na ndugu zangu kwa muda mrefu sana bila mafanikio. Hakuna mtu alijua mimi au mume wangu tulikua wapi.

Baadaye Nilipouliza kuhusu mwanangu Minza na mume wangu, nijibiwa kuwa waliokufa miaka mitatu na nusu iliyopita. Ndipo nikakumbuka mambo magumu ya maisha yaliyonipata. Nilitunga msiba mkubwa upya kabisa. Nililia sana na kujionea huruma kama yatima asiye na msaada. Sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote. Hata uhai nilionao leo ni Mungu tu amenisaidia.

Shopping Cart
Scroll to Top