Chemsha Bongo: Maswali na Majibu, Na Melkisedeck Leon Shine
Nilienda kwa mjomba akanichinjia Jogoo mwenye mguu mmoja
Kitendawili…
Nilienda kwa mjomba akanichinjia Jogoo mwenye mguu mmoja
Onesha Jibu
JIBU: Uyoga
Je, glasi itakuwa vipande vingapi?
SWALI: Mtoto alikua amebeba glasi mkono mmoja na mkono mwingine mpira. Kwa bahati mbaya mpira ukaanguka chini na kudunda mara tatu. Je, glasi imebaki vipande vingapi?
Onesha Jibu
JIBU: Glasi bado ni nzima. Mpira ndio ulianguka. Glasi haikuanguka
Je, glass ina Maji kiasi gani?
SWALI: Glasi imewekwa juu ya Meza na imejaa Maji. Kwa bahati mbaya upepo ukataka kuidondosha. Je glasi inamaji Kiasi gani?
Onesha Jibu
JIBU: Glasi bado imejaa Maji kwa sababu haikuanguka. Upepo ulitaka tuu kuiangusha.
Ni herufi gani tatu zinafuata baada ya hizi?
SWALI: Ni herufi gani tatu zinafuata baada ya MMTNTSS
Onesha Jibu
MMTNTSSNTK: Herufi ya kwanza ya namba Moja mpaka Kumi. Yaani Moja, Mbili, Tatu, Nnne, Tano, Sita…
Nikizidi nalaumiwa, nikipungua nadharauliwa
Kitendawili…
Nikizidi nalaumiwa, nikipungua nadharauliwa
Onesha Jibu
JIBU: Chumvi
Kivipi unaweza kusimama nyuma ya Baba yako wakati huo huo amesimama nyuma yako?
SWALI: Inawezekanaje kusimama nyuma ya mtu huku na yeye amesimana nyuma yako?
Onesha Jibu
JIBU: Inawezekana kama wote mmegeuziana MigongoTano inawezaje kuwa ndani ya nne?
SWALI: Tano inawezaje kuwa ndani ya nne?
Onesha Jibu
JIBU: Inaweza kuwa ndani ya nne kama ukiziandika kwa Kirumi.
IV = Nne
V = Tano
V ni Tano japokuwa ipo ndani aya Nne (IV)
Recent Comments