Karibu AckySHINE Charity

Kuhusu AckySHINE charity

AckySHINE charity ni programu ya kampeni na misaada ya kiutu yenye lengo la kuhamasisha amani na umoja, kulinda mazingira, na kudumisha afya na maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

AckySHINE charity inajumuisha kampeni mbalimbali kama vile Kampeni za Amani, Kampeni za Mazingira, Kampeni za Afya, na Kampeni za Maendeleo, ambazo zote zimeundwa kwa ajili ya kuboresha maisha na ustawi wa watu.

Kupitia jitihada hizi, AckySHINE charity inalenga kuimarisha mshikamano na uelewano miongoni mwa watu, huku ikihimiza uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo. Pia, inalenga kuleta maendeleo endelevu kwa kuboresha afya na kukuza mipango ya maendeleo ambayo itaongeza ubora wa maisha kwa kila mmoja katika jamii.

Kampeni zote za AckySHINE charity zinatangazwa na kupatikana kupitia tovuti yao rasmi, ackyshine.com, ambako watu wanaweza kujifunza zaidi kuhusu kampeni mbalimbali na kushiriki katika kampeni hizo.

Lengo la AckySHINE Charity

Lengo la misaada na kampeni hzi ni kudumisha utu na mshikamano katika jamii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho, kwa kutunza mazingira ya asili, kulinda amani, kuhamasisha maendeleo na kudumisha afya ya mtu mmoja mmoja na ya jamii kwa ujumla.

Mwanziliahi wa AckySHINE Charity

AckySHINE Charity ilianzishwa na inasimamiwa na Melkisedeck Leon Shine tangu 2011 hadi leo.

1. Kuhamasisha jamii Kudumisha Amani, upendo, umoja na Uelewano

Kufanikisha lengo hili kampeni hizi zinaendelea

 1. Wafanye Watabasamu
 2. Umoja wa Imani
 3. Amani na Upendo

2. Kuhamasisha jamii kutunza mazingira na kutumia mali asili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo

Kampeni zifuatazo zinaendeshwa

 1. Wanyama pori
 2. Vyanzo vya maji
 3. Miti na misitu
 4. Usafi na Utunzaji wa Mazingira

3. Kuhamasisha jamii kusaidia na Kutetea makundi yenye uhitaji zaidi katika jamii

Kampeni hizi zinaendeshwa

 1. Wajane
 2. Wazee
 3. Watoto na Vijana wadogo
 4. Watu wenye Ulemavu
 5. Watoto Yatima

4. Kuhamasisha jamii kutunza afya zao kwa maendeleo ya mtu momoja mmoja na ya jamii kwa ujumla

Kufanikisha lengo hili kampeni hii inaendelea

 1. Usafi Binafsi

Jinsi AckySHINE Charity inavyofanya Kazi

AckySHINE charity inatoa misaada na kufanya kampeni zake online kupitia website ya ackyshine.com. Ndani ya website hiyo matangazo ya kampeni za AckySHINE Charity yanatangazwa ili kusomwa na watembeleaji wa tovuti hiyo na hatimaye ujumbe kuwafikia.

AckySHINE Charity haifungamani wala hailengi itikadi, nchi au jamii fulani. Misaada na kampeni ni kwa watu wote kutoka nchi yoyote, kutoka jamii yoyote wenye itikadi yoyote.

AckySHINE Charity haipo kwa ajili ya kujipatia faida yoyote kifedha na haichangishi fedha, ipo kwa ajili ya kuwawezesha wanajamii kufahamu na kutenda mambo yote kwa ushirikiano katika amani na upendo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na cha baadae.

Jinsi ya Kushiriki

Unaweza kushiriki kwa namna hizi;

 1. Kuufanyia kazi ujumbe wa kampeni husika
 2. Kusambaza ujumbe wa kampeni husika kwa kuwaambia watu wengine moja kwa moja au kusambaza kwenye mitandao ya Kijamii

Mafanikio Kwa Sasa

Kwa sasa kampeni zinawafikia watu zaidi ya 10,000 kila mwezi.

AckySHINE Charity inalenga kuwafikia watu zaidi ya 25,000 kila mwezi ifikapo mwaka 2025

Misaada ya AckySHINE Charity

Kutangaza Viyuo Misaada kwa Kijamii: Tunawezesha Watoa Misaada na Wenye Vituo Kukutana

Kwenye Tovuti ya AckySHINE, tunawaunganisha watu wanaotoa misaada kwa jamii kama yatima, walemavu wasiojiweza, na wazee, pamoja na vituo vya misaada. Tunatoa nafasi kwa vituo vya misaada kutangaza huduma zao bure bila kukusanya michango. Kama una kituo cha kutoa msaadawasiliana nasi.

Mawasiliano

AckySHINE Charity

Barua Pepe: charity@ackyshine.com

Views: 15

Shopping Cart