
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema โKwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Aminaโ.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, โTusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk).
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:
โMungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, โฆโฆ Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, โฆโฆ Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, โฆ..โ
Au;
โUtuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,โฆ. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,โฆ. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, โฆ..โ Au;
โSalamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,โฆ.. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,โฆ.. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,โฆโฆโ
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi.
Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Mariaโฆ, โAtukuzwe..โ, โEe Yesu wanguโฆโ na โTuwasifu mileleโฆโ kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuungโarisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
- Bwana utuhurumie
- Bwana utuhurumie
- Kristo utuhurumie
- Bwana utuhurumie
- Bwana utuhurumie
- Kristo utusikie
- Kristo utusikilize
- Mungu Baba wa Mbinguni,โฆโฆ Utuhurumie
- Mungu Mwana Mkombozi wa dunia โฆโฆโฆ Utuhurumie
- Mungu Roho Mtakatifu โฆโฆ.. Utuhurumie
- Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja โฆโฆ.. Utuhurumie
- Maria Mtakatifu โฆโฆโฆ. utuombee
- Mzazi Mtakatifu wa Mungu โฆโฆ.. utuombee
- Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira โฆโฆ.. utuombee
- Mama wa Kristo โฆโฆโฆ utuombee
- Mama wa Neema ya Mungu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mama Mtakatifu sana โฆโฆโฆ utuombee
- Mama mwenye usafi wa Moyo โฆโฆโฆ.. utuombee
- Mama mwenye ubikira โฆโฆโฆ.. utuombee
- Mama usiye na doa โฆโฆโฆ.. utuombee
- Mama mpendelevu โฆโฆโฆ. utuombee
- Mama mstajabivu โฆโฆโฆ. utuombee
- Mama wa Muumba โฆโฆโฆ. utuombee
- Mama wa Mkombozi โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mama wa Kanisaโฆโฆโฆ.. utuombee
- Bikira mwenye utaratibu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Bikira mwenye heshima โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Bikira mwenye sifa โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Bikira mwenye uwezo โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Bikra mweye huruma โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Bikra mwaminifuโฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Kioo cha haki โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Kikao cha hekima โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Sababu ya furaha yetu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Chombo cha neema โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Chombo cha kuheshimiwa โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Chombo bora cha ibada โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Waridi lenye fumbo โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mnara wa Daudi โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mnara wa pembe โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Nyumba ya dhahabu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Sanduku la Agano โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mlango wa Mbingu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Nyota ya asubuhi โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Afya ya wagonjwa โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Kimbilio la wakosefu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mtuliza wenye huzuni โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Msaada wa waKristo โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Malaika โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Mababu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Manabii โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Mitume โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Mashahidi โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Waungama dini โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Mabikira โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Watakatifu wote โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia uliyepalizwa Mbinguni โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa Rozari takatifu โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Malkia wa amani โฆโฆโฆโฆ.. utuombee
- Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utusamehe ee Bwana.
- Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utusikilize ee Bwana
- Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,โฆโฆโฆโฆ..Utuhurumie.
- Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,โฆโฆโฆโฆ..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Karibu Vitatabu vya Kikatoliki
-
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Novena ya Roho Mtakatifu
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Tafakari kwa Mkristu Mkatoliki (Sehemu ya I)
Original price was: Sh3,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
KITABU CHA NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
๐Kitabu cha Sala Muhimu: Mkusanyiko wa SALA, LITANIA NA NOVENA
Original price was: Sh12,500.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Biblia Takatifu Agano la Kale
Original price was: Sh7,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Mwongozo wa Sala na Nyimbo za Ibada ya Njia ya Msalaba
Original price was: Sh6,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Mwongozo wa kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Biblia Takatifu Agano Jipya
Original price was: Sh3,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
KITABU CHA SALA ZA KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI
Original price was: Sh4,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Novena Ya Huruma ya Mungu
Original price was: Sh2,500.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kwa nini Wakatoliki wanaweka Sanamu Kanisani?
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now
๐๐ Mbarikiwe sana
Katika imani, yote yanawezekana
Mwamini Bwana; anajua njia
๐๐ Mungu akujalie amani
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia