Chemsha Bongo: Maswali na Majibu, Na Melkisedeck Leon Shine
Amekufa lakini anasaidia mgonjwa
Je, glasi itakuwa vipande vingapi?
SWALI: Mtoto alikua amebeba glasi mkono mmoja na mkono mwingine mpira. Kwa bahati mbaya mpira ukaanguka chini na kudunda mara tatu. Je, glasi imebaki vipande vingapi?
Onesha Jibu
JIBU: Glasi bado ni nzima. Mpira ndio ulianguka. Glasi haikuanguka
Read and Write Comments
Nikizidi nalaumiwa, nikipungua nadharauliwa
Kitendawili…
Nikizidi nalaumiwa, nikipungua nadharauliwa
Onesha Jibu
JIBU: Chumvi
Read and Write Comments
Kivipi unaweza kusimama nyuma ya Baba yako wakati huo huo amesimama nyuma yako?
SWALI: Inawezekanaje kusimama nyuma ya mtu huku na yeye amesimana nyuma yako?
Onesha Jibu
JIBU: Inawezekana kama wote mmegeuziana MigongoUnanitizama nimekupiga?
Tano inawezaje kuwa ndani ya nne?
SWALI: Tano inawezaje kuwa ndani ya nne?
Onesha Jibu
JIBU: Inaweza kuwa ndani ya nne kama ukiziandika kwa Kirumi.
IV = Nne
V = Tano
V ni Tano japokuwa ipo ndani aya Nne (IV)
Read and Write Comments
Ni herufi gani tatu zinafuata baada ya hizi?
SWALI: Ni herufi gani tatu zinafuata baada ya MMTNTSS
Onesha Jibu
MMTNTSSNTK: Herufi ya kwanza ya namba Moja mpaka Kumi. Yaani Moja, Mbili, Tatu, Nnne, Tano, Sita…
Read and Write Comments
Nilienda kwa mjomba akanichinjia Jogoo mwenye mguu mmoja
Kitendawili…
Nilienda kwa mjomba akanichinjia Jogoo mwenye mguu mmoja
Onesha Jibu
JIBU: Uyoga
Read and Write Comments
Recent Comments