Matendo ya Rozari Takatifu: Mchanganuo kwa siku zote za Saba za Juma
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
- Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
- Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
- Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
- Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
- Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
- Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
- Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
- Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
- Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
- Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
- Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
- Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
- Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
- Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
- Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
- Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
- Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
- Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
- Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
- Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
Karibu Vitatabu vya Kikatoliki
-
Vitabu Vya Dini
KITABU CHA SALA ZA KILA SIKU ASUBUHI NA JIONI
Original price was: Sh4,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Biblia Takatifu Agano Jipya
Original price was: Sh3,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
📕Kitabu cha Sala Muhimu: Mkusanyiko wa SALA, LITANIA NA NOVENA
Original price was: Sh12,500.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Mwongozo wa Sala na Nyimbo za Ibada ya Njia ya Msalaba
Original price was: Sh6,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Novena Ya Huruma ya Mungu
Original price was: Sh2,500.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
KITABU CHA NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Novena ya Roho Mtakatifu
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kwa nini Wakatoliki wanaweka Sanamu Kanisani?
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Mwongozo wa kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Original price was: Sh5,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Biblia Takatifu Agano la Kale
Original price was: Sh7,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now -
Vitabu Vya Dini
Kitabu cha Tafakari kwa Mkristu Mkatoliki (Sehemu ya I)
Original price was: Sh3,000.Sh0Current price is: Sh0. Download Now
Recent Comments