ROZARI YA MATESO SABA YA BIKIRA MARIA

Tumia Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria iliyo na mafungu 7 yaani mateso 7 yenye Salamu Maria saba kwa kila teso.

TESO LA KWANZA

Mzee Simeoni aliagua kuwa Moyo wa Mama Maria utachomwa kwa upanga.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

TESO LA PILI

Maria na Yosefu walikimbilia Misri usiku ili kumficha Mtoto Yesu asiuawe na Herodi.
Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

TESO LA TATU

Mama Maria aliona uchungu sana Mtoto Yesu alipopotea kwa siku tatu.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

TESO LA NNE

Mama Maria aliona uchungu sana alipokutana na Mwanae Yesu katika njia ya Msalaba.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

TESO LA TANO

Mama Maria aliona uchungu sana alipomwona Mwanae Yesu akisulibiwa Msalabani.
Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

TESO LA SITA

Mama Maria aliona uchungu sana alipopakata maiti ya Mwanae Yesu baada ya kushushwa Msalabani.
Tuombe neema ya kutotenda dhambi.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

TESO LA SABA

Mama Maria aliona uchungu sana aliporudi nyumbani baada ya kumzika Mwanae Yesu
Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria.
Mama wa mateso utuombee.
Baba Yetu ……… Salamu Maria x7. Atukuzwe Baba ……
Mateso na majonzi ya Mama Maria hayana mfano.

Melkisedeck Leon Shine

Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp

Read and Write Comments

1 thought on “ROZARI YA MATESO SABA YA BIKIRA MARIA”

  1. Rozari ya Mateso Saba ya Bikira Maria ni zana yenye nguvu katika imani ya Kikatoliki, ikionyesha utukufu na miujiza ya Bikira Maria. Mateso saba yanayojulikana kama “Mateso Matakatifu” ya Bikira Maria yanaashiria nyakati muhimu katika maisha ya Yesu Kristo. Kila matezo huleta mwangaza wa mwanga wa imani na upendo wa Mungu kwa wanadamu.

    Miujiza mingi imejulikana kuhusiana na Rozari ya Mateso Saba. Kuna hadithi nyingi za watu wanaoamini kuwa wameokolewa kutokana na shida za kiroho na kimwili kupitia sala ya Rozari hii. Wengine wametoa ushuhuda wa kuponywa kutokana na magonjwa, kushinda majaribu magumu ya maisha, na hata kuokolewa kutokana na hatari za kifo.

    Katika mafundisho ya Kikatoliki, Rozari ya Mateso Saba inaleta neema, ulinzi, na baraka kutoka kwa Mungu kupitia maombezi ya Bikira Maria. Sala hii inaunganisha waamini na maisha ya Yesu Kristo kwa njia ya kiroho, ikichochea mabadiliko na ukamilifu wa maisha ya Kikristo.

    Hivyo basi, Rozari ya Mateso Saba ni ishara ya nguvu ya sala na imani katika maisha ya Kikatoliki, ikionyesha utukufu wa Mungu na upendo wake usiokuwa na kipimo kwa wote wanaoitumia kwa moyo wa unyenyekevu na imani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart