Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Vipimo

Mchele vikombe 3

Karoti 1 ikune (grate)

Mchicha katakata kiasi

Adesi za brown

Kitunguu katakata (chopped)

Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2

Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia

Samli ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Vipimo Vya Samaki Wa Salmon

Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa

Tangawizi mbichi ilosagwa kijiko 1 cha kulia

Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia

Chumvi kiasi

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia

Ndimu 1 kamua

Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon

Changanya viungo vyote upake katika samaki.
Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake.
Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili.
Akiwa tayari epua.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori)
Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii.
Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia.
Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo.
Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu.
Tia chumvi ukoroge funika upike kama pilau.
Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon

Njia 8 za kupata mtaji kwa ajili ya Biashara yako

Njia hizo ni kama ifuatayo!!

1. Mtaji mbadala
Mtaji mbadala unarejelea rasilimali au mbinu ambazo zinaweza kutumika badala ya fedha katika kuendeleza biashara au mradi fulani. Ni muhimu kuelewa kwamba si kila hatua inahitaji matumizi ya fedha taslimu. Kuna nyakati ambapo unaweza kutumia rasilimali zingine ulizonazo ambazo zinaweza kuchukua nafasi ya fedha. Kwa mfano, mtu anaweza kutumia nguvu zake mwenyewe katika kutengeneza kitu kama bidhaa au katika kutoa huduma, hivyo kuokoa gharama ambayo angehitaji kulipa mtu mwingine kufanya kazi hiyo.

Ujasiriamali unahusisha pia kutumia maarifa na uzoefu ambao mtu amepata katika fani au sekta fulani. Maarifa haya yaliyotokana na mafunzo au uzoefu yanaweza kugeuzwa kuwa bidhaa au huduma bila ya gharama za ziada. Halikadhalika, mtaji mbadala unaweza kujumuisha kutumia umaarufu au jina lako kuvutia wateja au wabia bila haja ya matangazo ya gharama.

Kukopa au kuazima ni njia nyingine ya mtaji mbadala. Badala ya kutumia akiba yako ya fedha au kuchukua mkopo wa riba kubwa, unaweza kuazima vifaa au pata mikopo isiyo na riba kutoka kwa marafiki, familia, au taasisi zinazotoa mikopo midogo midogo.

Ubunifu ni sehemu muhimu ya mtaji mbadala. Kwa kutumia ubunifu, mtu anaweza kubuni njia mpya na tofauti za kutekeleza miradi ambazo hazihitaji fedha nyingi. Hii inaweza kujumuisha kufanya biashara kwa njia ya kubadilishana bidhaa na huduma (barter trade) au kuanzisha njia mpya ambazo zinapunguza gharama za uendeshaji.

Kipaji ni rasilimali nyingine ambayo inaweza kutumika kama mtaji mbadala. Kwa mtu mwenye kipaji kikubwa katika sanaa, muziki, riadha, au tasnia nyingine, kipaji hicho kinaweza kuwa njia ya kujipatia kipato bila haja ya kuwekeza fedha nyingi. Uwezo binafsi uliojengwa kama vile uongozi, mawasiliano na uwezo wa kushawishi watu, pia ni mali ambazo zinaweza kutumika kama mtaji mbadala.

Kwa ujumla, dhana ya mtaji mbadala inasisitiza umuhimu wa kuchangamkia rasilimali na vipawa tulivyonavyo, na kutafuta njia mbadala za kufanikisha malengo bila kutegemea fedha taslimu pekee.

2. Kupata mtaji kwa ndugu, jamaa na marafiki

Watu wengi wanakuwa kwenye umaskini wakati wamezungukwa na ndugu matajiri kisa wanaona aibu kuomba msaada, lakini amini usiamini watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki, mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria ndugu Dangote yeye alivyotaka kuanza ujasiriamali aliomba msaada toka kwa mjomba wake ambaye alimuazima kama milioni 3 hiv , kwa kuwa aliona fursa kwenye mambo ya ujenzi (cement) yeye akaanza kununua cement na kuuza leo hii ndugu Dangote amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika anauza cement, unga , mchele, mafuta, sukari na saa hivi anauza mafuta kule Africa Magharibi hata hapa Tanzania tuna kiwanda chake kule Mtwara,

Kuomba msaada sio ishara ua udhaifu bali ni ishara ya nguvu kwamba unajiamini ndio maana unaomba msaada. kumbuka kwenye neno UJASIRIAMALI kuna neno Jasiri pia, huwezi kuwa na mali bila kuwa jasiri.Umezungukwa na watu waliobarikiwa usisite kuwaambia wakusaidie ,.

3. Kwa kujiwekea akiba.

Watu wengi sana hapa kwetu Tanzania ukiwaambia weka akiba wanakwambia mimi siwezi kuweka akiba, sina utamaduni wa kuweka akiba, hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana kufika juu bila kuweka akiba kwa mfano kama umeajiriwa na unajua biashara fulani inataka milioni 2 ili kuifanya na wewe mshahara wako ni laki 4, kwa nini basi kila mwezi usiweke laki 1 pembeni, ndan ya miaka miwili utakuwa na milioni 2.4 huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.

Usisite kuanza kidogo kwa kuweka akiba polepole mpaka ufike huko unakoenda.

4. Pata kazi ya ziada
Kama kipato unachopata hakitoshi unaweza kujitafutia kazi ya ziada kwa muda wako wa jioni au weekend ili uweze kupata ziada ya akiba kwa ajili ya mtaji.

Watu wengi wanatumia muda vibaya, Je baada ya kazi yako unafanya nini? ile saa 10 hadi saa 4 usiku unatumiaje muda wako? Jinsi unavyotumia muda huu itakupelekea kuwa tajiri au maskini

5. Pata Mtaji kwa njia ya kudunduliza
Hii njia ya kudunduliza ndio njia ambayo ni nyepesi kabisa ambayo watu wengi hawaioni, ukiamua kutumia njia hii kamwe huwezi kukosa mtaji, hii ina maana unaanza katika hali ya chini kabisa ya kufanya kitu chochote halafu ile faida unayoipata hauitumii bali unaiwekeza kwenye biashara yako.Tuone mfano wa dada Christine ambaye ni mfano mzuri wa mtaji wa kudunduliza

Christine Momburi alikuwa amejifungua na mume wake walikuwa wamemuachisha kazi kwa hivyo maisha hayakuwa mazuri sana,

Sasa siku moja walitembelewa na mgeni nyumbani kwao yule mgeni alipotaka kuondoka alimpa Christina shilingi 700 ili anunue maziwa ya mtoto, baada ya yule mgeni kuondoka Christina alijiuliza Je aitumie ile sh 700 kununua maziwa au afanyie nini hasa ili iweze kubadili maisha yake? kwa hiyo alijiuliza sana baadae akaamua kuichukua ile hela aende sehemu akanunue nyanya chungu na mboga mboga kwa bei ya jumla. Akazinunua akaenda kuuza, kwa siku ya kwanza ikatoka sh 700 kwenda 1500 akaongeza mtaji wake, ilikufupisha stori baada ya wiki moja Christina akawa na mtaji wa sh 25000/=.

Siku moja akasikia kuna mahali wanajenga wanataka mama lishe wa kuwapelekea chakula akachukua ile tenda akawa anawapelekea chakula, baadae akasikia kuna sehemu wanataka mtu wa kuwapelekea sare za shule. akawa anazidi kukua na kukua na hivi sasa Christina amekuwa ni mjasiriamali mkubwa pale Moshi ana maduka makubwa sana na amehojiwa na vyombo vya habari mbalimbali na yeye amekiri kwamba kudunduliza ndio kuliko mtoa.

Sasa swali la msingi nalotaka nikuulize ni swali lifuatalo:

Swali, Ni je ni Sh 700 ngapi zimepita mikononi mwako? Je ni Sh 7000 ngapi zimepita mikononi mwako? Je ni Sh 70000 zimepita mikononi mwako? vipi kuhusu laki 7 au milioni 7 ngap zimepita mikononi mwako? mara nyingi tumeidharau fedha na kuona ni ndogo lakini kumbuka nilishasema siku za nyuma kuwa kila shilingi inayopita mikononi mwako ni itazame kwa jicho la kimilionea.

Nikukumbushe kuwa tajiri kuna maumivu ambayo utayapitia, watu wengi hawataki kupitia maumivu ndio maana watu wachache sana wanakuwa matajiri., watu wengi wanapenda utukufu lakini hawataki kubeba msalaba.

Hivyo usidharau pesa bali fikiria kwa ubunifu jinsi ya kuizalisha fedha hiyo.

6. Pata Mtaji mdogo kupitia wawekezaji

Wakati mwingine kutokana na mazingira uliyonayo unaweza ukagundua kwamba una wazo zuri sana la biashara lakini hauna mtaji, hapa jambo la msingi ni kuangalia unaweza kumpata vipi muwekezaji ambaye atataka faida, ni afadhali ukawa na wazo ukawashirikisha wengine wakakupa mtaji halafu mkagawana faida kuliko kufa na wazo lako zuri,.

Sisi watanzania tupo nyuma sana katika suala la kufanya biashara pamoja ( Partinership) tofauti na wakenya.
mfano mzuri ni rafiki yangu anaitwa Elisha Edson yuko Iringa, yeye aliwaza kuanzisha kiwanda cha mbao hizi nguzo za umeme, bahati mbaya hakuwa na mtaji wa kutosha akaamua kuongea na marafiki zake zaidi ya 10 akamshawishi kila rafiki yake awekeze kiasi kadhaa cha fedha na kumpatia hisa kwenye kile kiwanda chake, rafiki zake walikusanyika waktoa fedha na sasa kiwanda kimeanzishwa na kinakaribia kutoa nguzo wakati wowote kuanzia sasa.

Je wewe una weza ukatumia njia hii? je una wazo ambalo unajua kabisa hili wazo nikipata wawekezaji wa nanmna hii? masharti yake yanaweza kuwa magumu sababu unaweza kuambiwa uandike mchanganuo wa biashara unao eleweka, na wazo lako la biashara lionekane limetulia kabisa.

Lakini ni afadhali ukapitia mchakato huu kuliko kuwa na wazo zuri halafu wewe huna fedha. na kumbe ungeweza kutoa ajira na kulipa kodi kwa nchi hii na kufanya wenzako wakanufaika na wazo ulilonalo.

7. Mtaji kwa njia ya Mgavi ( Supplier Financing)

Hii ni njia ya uhakika ya kupata mtaji wako. Naomba nitoe stori halisi , Miaka mingi iliyopita kijana mmoja anayeitwa Reginald alikuwa anatafuta kalamu za kuandikia mtaani kwake, lakin bahati mbaya baada ya kutafuta sana kwa muda mrefu alikosa kalamu pale mtaani kwake, jambo hilo lilimfanya aweze kushangaa sana na kujiuliza hivi kweli inawezekana vipi hakuna kalamu hapa mtaani? kwa hyo hilo likamfanya aanze kutafuta mbinu na maarifa ya yeye kuwa mtu ambaye analeta kalamu Tanzania. baada kufanya uchunguzi kwa marafiki mbalimbali wakati huo yeye alikuwa muhasibu tu, akaambiwa Mombasa kuna mtu ana kiwanda cha kalamu na baada ya kufanya mazungumzo na yule ndugu ikaonekana bwana Reginald angeweza kuwa anaingiza kalamu hapa Tanzania lakini hakuwa na mtaji, ndipo hapo ilibidi atumie mali kauli yaani awshawishi wale watu wampatie zile kalamu azilete hapa, aziuze halafu aweze kurejesha fedha na kuchukua faida yake.

Hivyo akaanza hiyo biashara kwenye chumba chake kidogo sebuleni akisaidiwa na familia yake baadae wahamia nje wakatengeneza banda la mabati tayari ikawa ndio kiwanda kwa ajili ya kupaki zile kalamu kwa pamoja. mwaka huo huo wa kwanza bwana Reginald alipata faida kubwa sana takriban bilion ya shilingi

8.Kupitia Taasisi za kifedha
Mada hii ni ndefu sana lakini tutajifunza huko mbele mada inayoitwa Jinsi ya kuishawishi benki ikukopeshe hata kama hukopesheki. hii mada tutaiongelea zaidi huko mbele , lakini nataka tu ujue ili benki ikukope inahitaji uwe na biashara ambayo imeshakuwepo kwa takribani miezi 6 au zaidi, pia watahitaji uwe na mzunguko mzuri wa fedha unaoeleweka, uwe na dhamana ambayo unaiweka ili kama unashindwa kulipa waweze kuichukua ile dhamana, watahitaji uwe umefanya usajili rasmi wa biashara yako., uwe na account ya benk n.k

Sasa basi kwa kuwa watu wanaogopa kwenda benki kutokana na yote haya ndipo unaweza kujaribu kutumia microfinances, hizi ni taasis za kifedha ambazo hutoa mikopo midogo midogo, kwa hiyo angalia kama huko ndiko unapoweza ukaponea. Zaidi ya hayo, taasisi hizi za kifedha zinajulikana kwa kutoa huduma zilizobinafsishwa zaidi, ambazo zinaweza kuwa na manufaa hasa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, watu binafsi, na biashara ndogo ndogo ambazo zinatafuta fursa za kukuza mitaji.

Microfinance institutions (MFI) zina sifa ya kuwa na mifumo inayoweza kufikiwa kwa urahisi, kwani mara nyingi hawana vikwazo vikali vya kielimu au kiuchumi kama vile benki kubwa. Wanaweza kutoa mikopo kwa riba nafuu na wakati huo huo kutoa mafunzo na ushauri wa kibiashara, ambayo yanaweza kuwa na manufaa makubwa kwa wakopaji.

Pia ni muhimu kufahamu kwamba MFI zinaweza kuwa na mitandao mikubwa inayowezesha huduma kufika hata vijijini ambako benki kubwa haziwezi kufika. Hii ina maana kwamba watu wanaoishi maeneo ya vijijini wanaweza kupata huduma za kifedha bila ya kuwa na ulazima wa kusafiri masafa marefu kwenda kwenye miji mikubwa.

Kwa kutumia huduma za microfinance, unaweza kupata fursa ya kuongeza mtaji, kuboresha biashara yako, na hata kupata elimu ya kifedha ambayo inaweza kusaidia katika kufanya maamuzi bora ya kibiashara na kifedha. Ni muhimu kuchunguza chaguzi zilizopo, kulinganisha tofauti za riba na masharti ya mkopo kabla ya kuchukua uamuzi wa kutumia taasisi fulani ya microfinance.

Ifahamu Saratani ya Tezi Dume, chanzo, Dalili, Uchunguzi na Tiba

Tezi Dume ni nini?

Tezi dume (prostate), ni tezi iliyo kwenye kizazi cha mwanaume inayozalisha maji maji yanayobeba manii/shahawa. Inaizunguka urethra, mrija unaotoa mkojo kwenye kibofu kwenda nje. Tezi dume ya kila mwanaume huongezeka ukubwa kadri umri unavyoongezeka. Kadri tezi inapokua na kuongezeka ukubwa,inaweza kukandamiza urethra na kusababisha matatizo ya kibofu na matatizo ya kukojoa. Tezi dume inapoongezeka ukubwa huitwa ”benign prostatic hyperplasia” kwa kifupi ”BPH”. Hii sio saratani, na haiongezi hatari ya kupata saratani ya tezi dume.

Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi.

Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour.
Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kibofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea.
Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake. Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya ’50 Plus Campaign’ anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.

VIHATARISHI VYA TEZI DUME

Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake:-

👉🏿Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea.

👉🏿Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo.

👉🏿Suala jingine ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo.
Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.

DALILI ZA TEZI DUME

Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH.
Dalili hizo ni pamoja na,

1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa.

2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa.

3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu.

4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote

6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
Pamoja na kueleza dalili hizo watu wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni.
Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.

UCHUNGUZI WA TEZI DUME

Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi.
Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee.
Mambo kama hayo hupelekea wanaume wengi kujinyanyapaa wenyewe na hata wengine kujitibu kwa uficho au kwa kutumia waganga wababaishaji mpaka pale mambo yanapokuwa yamewazidi ndipo hupelekwa mahospitalini na mara nyingine huwa wamechelewa na kupoteza maisha yao bure kwa ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa mapema.
Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla, na hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.
Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni “Digital Rectal Exam (DRE)” na cha pili ni “Prostate Specific Antigen (PSA)”. DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile transrectal ultrasound au prostate needle biopsy.

MATIBABU YA TEZI DUME

Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika. Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi.
Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.

Matumizi ya dawa

Alpha 1-blockers kama vile doxazosin, prazosin, tamsulosin, terazosin, na alfuzosin ni dawa zilizo kwenye kundi la dawa zinazotumika kutibu shinikizo la juu la damu. Dawa hizi hulegeza misuli ya shingo ya kibofu na tezi dume. Hii huruhusu mkojo kutoka kwa urahisi. Watu wengi wanatumia dawa ya Alpha 1-blockers, na husaidia sana kupunguza dalili zao.

Finasteride na dutasteride  ni dawa zinazopunguza kiwango cha homoni zinazotengenezwa na tezi dume,hupunguza ukubwa wa  tezi dume, huongeza kiwango cha mtiririko wa mkojo, na kupunguza dalili zinazotokana na ukubwa wa tezi dume kuongezeka. Inaweza kuchukua miezi 3 hadi 6 kabla ya kuona mabadiliko makubwa katika dalili zako. Kutumia finasteride na dutasteride kunaweza kuwa na athari kama vile, kupungua kwa nguvu za kiume na hata kuwa hanithi.

Daktari anaweza kuagiza upewe dawa za antibiotiki ili kutibu kuvimba kwa tezi dume (prostatitis), mara nyingi prostatitis huambatana na kuongezeka kwa ukubwa wa tezi dume.

Upasuaji

Upasuaji wa tezi dume unaweza kupendekezwa  iwapo :

  • Unajikojolea/ unashindwa kuzuia mkojo
  • Unakojoa mkojo wenye damu mara kwa mara
  • Unashindwa kukojoa mkojo wote,(Mkojo unabaki kwenye kibofu hata baada ya kukojoa)
  • Maambukizi ya mara kwa mara kwenye njia ya mkojo
  • Kushindwa kwa figo kufanya kazi
  • Mawe kwenye kibofu

Uchaguzi wa aina maalum ya upasuaji, mara nyingi hutegemea ukali wa dalili ,ukubwa na umbo la tezi dume.

  • Transurethral resection of the prostate (TURP): Hii ni aina ya upasuaji inayopendelewa zaidi kutibu ugonjwa wa tezi dume. TURP hufanyika kwa kuingiza kifaa chenye kamera kupitia kwenye uume na kisha kukata na kuondoa tezi dume kipande baada ya kipande.
  • Transurethral incision of the prostate (TUIP): Upasuaji huu unafanana kidogo na TURP, na hufanyika kwa wanaume walio na tezi dume isiyo kubwa sana. Kwa kawaida upasuaji hufanyika na kisha mgonjwa huruhusiwa kwenda nyumbani (hakuna kulazwa). Kama ilivyo kwa TURP, kifaa chenye kamera huungizwa kupitia kwenye uume mpaka kuifikia tezi dume. Kisha, badala ya  kukatakata na kuiondoa, daktari hufanya mkato mdogo kupanua urethra ili kuruhusu mkojo kupita.
  • Simple Prostatectomy : Mgonjwa hupewa dawa ya nusu kaputi na kisha daktari hupasua tumbo (chini ya kitovu) ili kuifikia tezi dume. Sehemu ya ndani ya tezi dume huondolewa . sehemu ya nje huachwa . Huu ni utaratibu unaochukua muda mrefu, mgonjwa huhitajika kulazwa hospitalini kwa siku 5 hadi 10.


Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

Tukumbuke kuwa, saratani ya tezi dume ni ugonjwa wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
😀😀😀😀

Mambo ya kutafakari unapokuwa katika shida kubwa, unapoelekea kukata tamaa

Tafakari Kuhusu Wakati wa Shida

Leo tunatafakari kuhusu wakati wa shida. Maisha ya mtu yanabadilika wakati wowote kwa namna yoyote. Yanaweza yakawa mazuri mpaka ukashangaa au yanaweza yasiwe mazuri kama unavyotarajia. Yote hayo ni sehemu ya maisha.

“Nimejifunza kuwa na kuridhika na hali yoyote niliyo nayo. Najua jinsi ya kuwa na hali duni, najua jinsi ya kuwa na hali ya wingi. Katika hali zote na mambo yote, nimefundishwa jinsi ya kushiba na jinsi ya kuwa na njaa, jinsi ya kuwa na wingi na jinsi ya kupungukiwa.” (Wafilipi 4:11-12)

Kumbuka Wakati wa Matatizo

Unapokua na matatizo makubwa katika maisha, kumbuka haya yafuatayo:

1. Mungu Yupo na Anakuona

Mungu yupo na anakuona. Mwambie matatizo yako, huo ndio wakati wake wa kuonyesha uwepo wake na nguvu zake. Wewe tu kusema na Mungu kwa utayari na uwazi, hivyo utakao kuwezesha kupata au kutatua tatizo lako.

“Naomba BWANA akujibu siku ya dhiki, jina la Mungu wa Yakobo likuinue.” (Zaburi 20:1)
“Mchungueni Bwana na nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote.” (1 Mambo ya Nyakati 16:11)
“Bwana ni ngome yao katika wakati wa shida.” (Zaburi 37:39)

2. Matendo na Maamuzi Yako

Maneno, vitendo, na maamuzi yako ndiyo yanaweza yakawa njia ya kutatua matatizo yako. Usiogope kuchukua hatua zinazohitajika. Tafuta hekima na uongozi kutoka kwa Mungu katika kila hatua unayochukua.

“Yehova atakuelekeza siku zote, na kukusibisha katika nchi yenye ukame, na kukuimarisha mifupa yako. Utakuwa kama bustani iliyomwagiliwa, na kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayatapungua.” (Isaya 58:11)
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.” (Mithali 3:5-6)
“Nawafundisha njia iliyo njema na adili; msiiachilie sheria yangu.” (Mithali 4:11-13)

3. Matatizo Hayako Sio Mwisho wa Maisha

Tatizo lako sio mwisho wa maisha yako, sio mwisho wa yote mazuri ya jana, leo, na kesho. Bado unayo mambo mengi mazuri yanakungojea. Mungu anapanga mambo mazuri kwa ajili ya wale wanaompenda na kumtumainia.

“Maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu, asema Bwana, ni mipango ya amani na si ya mabaya, ili niwape tumaini katika siku zenu za usoni.” (Yeremia 29:11)
“Na tusiache kutenda mema, kwa maana tutavuna kwa wakati wake tusipozimia roho.” (Wagalatia 6:9)
“Bwana atakamilisha mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; usiache kazi ya mikono yako.” (Zaburi 138:8)

4. Uangalizi wa Tatizo

Kumbuka tatizo lako linaweza likawa sio kubwa ila wewe ndio unaliona kubwa. Wewe sio wa kwanza kuwa na tatizo kama hilo, wengine hayo ndo maisha yao. Angalia kwa mtazamo wa matumaini na uombe hekima ya Mungu ili uweze kuona njia ya kutoka kwenye tatizo lako.

“Mkipungukiwa na hekima, na aombe kwa Mungu, naye atampa kwa ukarimu wala hachukii.” (Yakobo 1:5)
“Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.” (2 Wakorintho 4:16)
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:13)

Kwa hivyo, wakati wa shida, ni muhimu kujikumbusha kwamba Mungu yupo, anakusikiliza, na yupo tayari kukusaidia. Usiache matumaini, endelea kuamini na kutenda kwa hekima na imani, ukijua kwamba matatizo yako ni sehemu ya safari yako ya kiroho na Mungu anapanga mazuri mbele yako.

Karibu Ujitafakari: Kwa nini Unasali na Kumuabudu Mungu? Jifunze Kitu Hapa

Utangulizi

Embu tafakari kwa nini unasali na Kumuabudu Mungu!

Je unasali kwa hofu ya kutokua na uhakika na maisha?

Je unasali kwa sababu ya shida na matatizo katika maisha?

Je unasali kwa kuwa unaona wengine wanasali kwa hiyo unafikiri na wewe lazima usali?

Je unasali kwa kuwa unamwogopa Mungu?

Je unasali na kuabudu kama kutimiza wajibu katika dini au kanisa lako?

Je Unasali kutimiza wajibu kama kiumbe kwa Mungu?

Je unasali kwa kuwa unapenda Kusali?

Je unasali kwa kuwa Unampenda Mungu?

Je unasali kwa kuwa Unampenda Mungu na unaona ni wajibu wako Kusali?

Je unasali kwa kuwa Unampenda Mungu na unaona ni njia ya kujenga mahusiano na Mungu?

Je unasali na Kumuabudu Mungu kwa kuwa unajisikia vibaya kwa kuwa unaona wengine hawasali kwa hiyo unataka kumfariji Mungu kwa sala zako?

Tafakari uko wapi wewe?

Tafakari Maisha Yako ya Sala: Jiulize Maswali Haya

Katika maisha yetu ya kiroho, sala na ibada ni sehemu muhimu. Lakini je, umewahi kutafakari kwa nini unasali na kumwabudu Mungu? Hebu tuingie ndani ya mioyo yetu na kujitafakari kwa undani. Jiulize maswali haya ili kujielewa vizuri na kuboresha uhusiano wako na Mungu.

Je, Unasali kwa Hofu ya Kutokuwa na Uhakika na Maisha?

Wakati mwingine, tunaweza kujikuta tunasali kwa sababu ya hofu – hofu ya kesho, hofu ya hali ya kifedha, hofu ya magonjwa. Je, sala yako inachochewa na hofu hii? Ni muhimu kutambua kuwa Mungu anatuita tuje kwake si kwa sababu ya hofu, bali kwa sababu ya upendo na imani. Tafakari, je, sala zako zinakutoka kwa moyo wa hofu au moyo wa imani?

Je, Unasali kwa Sababu ya Shida na Matatizo Katika Maisha?

Mara nyingi, matatizo na changamoto za maisha zinatusukuma kuingia kwenye sala. Ni kawaida na ni sahihi kutafuta msaada wa Mungu wakati wa dhiki. Lakini je, sala zako ni za kudumu hata wakati mambo yakiwa mazuri? Mungu anataka uhusiano wa kudumu na wewe, si wakati wa matatizo tu bali pia wakati wa furaha. Tafakari, je, unasali tu unapokuwa na matatizo?

Je, Unasali kwa Kuwa Unaona Wengine Wanasali?

Katika jamii zetu, tunaweza kushawishika kufuata mkumbo. Unapoona wengine wakisali, je, unajikuta unasali kwa sababu tu na wewe unataka kuwa kama wao? Ni muhimu kujua kwamba sala ni uhusiano binafsi kati yako na Mungu. Sali kwa sababu unataka kuzungumza na Mungu, sio kwa sababu wengine wanasali. Tafakari, je, sala yako inatokana na msukumo wa ndani au ni kwa sababu ya wengine?

Je, Unasali kwa Kuwa Unamwogopa Mungu?

Hofu ya Mungu ni kitu cha kawaida, lakini Mungu hataki tuwe na hofu inayotutenga naye. Badala yake, anataka tuwe na hofu ya heshima inayotufanya tumkaribie zaidi. Je, unasali kwa kuwa unamwogopa Mungu au unamsali kwa sababu unampenda? Tafakari, je, hofu yako inakupeleka mbali na Mungu au inakukaribisha karibu naye?

Je, Unasali na Kuabudu Kama Kutimiza Wajibu Katika Dini au Kanisa Lako?

Wakati mwingine, tunaweza kujikuta tunatimiza wajibu wa kidini kama sehemu ya ibada zetu. Ni muhimu kutambua kuwa ibada na sala si tu wajibu, bali ni njia ya kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Je, unasali kwa sababu ni wajibu wa kidini au ni kwa sababu ya upendo wako kwa Mungu? Tafakari, je, sala zako ni sehemu ya utaratibu tu au zinatokana na moyo wako?

Je, Unasali kwa Kuwa Unapenda Kusali?

Sala inapaswa kuwa ni tendo la upendo na shauku. Unapenda kusali kwa sababu unapenda kuzungumza na Mungu. Kama unasali kwa sababu unapenda kusali, basi unafanya jambo sahihi. Tafakari, je, unasali kwa shauku na upendo au kwa sababu ya kawaida?

Je, Unasali kwa Kuwa Unampenda Mungu?

Upendo ni msingi wa imani yetu. Je, sala zako zinatokana na upendo wako kwa Mungu? Kama unampenda Mungu, basi sala zako zitakuwa na nguvu na maana zaidi. Tafakari, je, unasali kwa upendo wa dhati kwa Mungu?

Je, Unasali kwa Kuwa Unaona Ni Wajibu Wako Kusali?

Kama kiumbe cha Mungu, ni wajibu wetu kusali na kumwabudu. Lakini wajibu huu unapaswa kutoka moyoni, si kwa kulazimishwa. Je, unahisi ni wajibu wako kusali kwa sababu unampenda Mungu? Tafakari, je, wajibu wako unakufanya usali kwa moyo mkunjufu?

Je, Unasali kwa Kuwa Unaona Ni Njia ya Kujenga Mahusiano na Mungu?

Sala ni njia bora ya kujenga na kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Unapozungumza na Mungu kupitia sala, unajenga daraja la upendo na imani. Tafakari, je, unasali kwa lengo la kujenga mahusiano ya karibu na Mungu?

Je, Unasali kwa Kuwa Unajisikia Vibaya kwa Kuona Wengine Hawasali?

Wakati mwingine, tunaweza kujisikia vibaya kuona wengine hawasali. Unaweza kujikuta unasali kwa bidii zaidi ili kumfariji Mungu kwa niaba ya wale ambao hawasali. Hii ni ishara ya upendo na kujali, lakini ni muhimu kuhakikisha kwamba sala zako zinatoka moyoni. Tafakari, je, unasali kwa bidii ili kumfariji Mungu au kwa sababu ya upendo wako binafsi?

Tafakari Uko Wapi Wewe

Tafakari maisha yako ya sala. Jiulize maswali haya kwa dhati na uone ni wapi ulipo katika uhusiano wako na Mungu. Sala ni uhusiano binafsi na Mungu. Ni njia ya kuzungumza na Yeye, kumshukuru, kumuomba msaada na kuelezea upendo wetu kwake. Jitafakari, jichunguze, na ujitahidi kuboresha maisha yako ya sala ili yawe na maana na nguvu zaidi. Mungu anakuita katika uhusiano wa dhati na wa kweli. Tafakari, uko wapi wewe?

Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.

Dalili

Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.

· Kushindwa kupumua vizuri

· Vidonda kwenye ulimi au mdomoni

· Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu

· Ngozi kuwa na rangi ya kijivu

· Kucha kuwa dhaifu

· Kusikia hasira na kuhamasika haraka

· Kuchoka sana kuliko kawaida

· Maumivu makali ya kichwa

· Kupungua kwa uwezo wa kufikiria

· Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama

· Miguu na mikono kuwa ya baridi sana

· Uchovu wa mara kwa mara

Matibabu.

Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.

Mambo ya Msingi Unayopaswa kufahamu kuhusu Ekaristi Takatifu: Mwili na Damu Ya Bwana Wetu Yesu Kristu

Ekaristi ni nini?

Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, katika
maumbo ya mkate na divai. Sakramenti hii
iliwekwa na Yesu Mwenyewe kwenye karamu ya mwisho, siku ya Alhamisi jioni kabla ya mateso
yake. (Yoh 6:1-71; Mt 26:26-28).

Maana ya jina Ekaristia

Tendo la shukrani na baraka.
Jina Ekaristi limetokana na neno la Kigiriki,
εύχαριστείν, maana yake ni “tendo la shukrani”,
“ kutoa shukrani*”, (Lk 22:19; 1Cor 11:24).
Ni tendo ambalo Yesu analifanya kwa Mungu.
Anamshukuru Mungu kwa kukamilisha kazi ya ukombozi. Tendo la baraka – εύλογείν
Kulingana na utamaduni wa Wayahudi baraka ilkua ikitolewa wakati wa mlo ikitukuza kazi za up mbaki za Mungu (Mt 26:26; Mk 14:22).

Injili zinazoongelea kuwekwa kwa Ekaristi

Injili tatu zinatueleza jinsi Yesu Kristo alivyoweka
Ekaristi Takatifu:
Mt 26:26-28.
Mk 14: 22-24
Lk 22:19-20
Mwinjili Yohane anaeleza Yesu Kristo mkate wa
uzima. Sura ya sita.
4. 1Kor 11:23-25
Mtume Paulo anatueleza jambo hilo katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho. 1Kor
11:23-25.

Tunajifunza kutoka kwa Yesu mambo yafuatayo

Lk 22:1. Saa ya Yesu (Lk 22:14). Hapa hamaanishi
saa ya kula, hapana. Bali saa ile ile ya kutimiliza tendo la wokovu. Yohane anapenda kusema saa ya kumtukuza Mungu, saa ya kupita kutoka ulimwengu huu kwenda kwa Baba. Sisi tunaweza kusema, tuna saa maalum ya kuingia katika ulimwengu wa
roho.Saa ya kukutana na Mungu, kutoka
ulimwengu huu kwenda kwa Mungu. (Sala au kifo).
2. Shukrani na masifu kwa Baba (Lk 22:17).
3. Kugawana sisi kwa sisi kikombe cha kwanza (Lk 22:17).
4. Kumbukumbu ya sadaka yake ya wokovu (Lk 22:19).
5. Uwepo wake (Lk 22:19).
6. Damu yake imemwagika kwa ajili yetu, kikombe cha pili (Lk 22:20).
Ekaristi ni Baraka kuu:
Yesu anabariki –kazi ya wokovu inabarikiwa na Yesu Mwenyewe. Hata vitu tunavyovitumia kila siku ni lazima kuviombea
baraka. Kabla ya mageuzo mkate na divai vinaombewa baraka (Mt 26:26).
Yesu anajitoa mwenyewe kwa watu –Yesu anajitoa kwa kila mshiriki (Mt 26:26).

Matunda ya Ekaristi katika maisha ya mkristo.

1. Muungano na Kristo:
Ekaristi inatuunganisha na Kristo kwa muungano wa ndani kabisa (Yoh 6:56).
2. Uzima wa milele : Ekaristi ni chanzo cha
uzima, maisha yetu yote yanapata uzima kwa kushiriki Mwili na damu ya Kristo, (Yoh 6:57).
3. Umoja: Ekaristi inaleta umoja wa kweli.
Tunafanywa kuwa mwili mmoja (1Kor 10:16-17).
4. Huondoa dhambi: Inatuondolea kwa
kuzifuta dhambi ndogo au inatutenga na dhambi ndogo (Mt 26:28; Yoh 1:29). Sakramenti ya
kitubio ndio hasa huondoa dhambi za mauti
(1Yoh 1:7; Yoh 20:22-23).
5. Dawa ya kutuponya kutoka katika umauti:
Ekaristi ni dawa ya kutokufa (Yoh 6:57-58).
6. Kufufuliwa siku ya mwisho: (Yoh 6:54).

Nguvu ya Ekaristi

–Kuponywa kwa
kuondolewa dhambi zetu.
Nguvu za Mungu zimo katika Ekaristi. Kabla ya kupokea Ekaristi tunasali Ee Bwana siesta hili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu
itapona. Bila shaka litakuwa kosa kubwa kwetu sisi kufikiri kwamba uponyaji unahusu masuala ya
mwili tu. Si kila uponyaji ni uponyaji wa mwili.
Mtume Paulo katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike sura ya 5:23 kuwa sisi wanadamu tu mwili, roho na nafsi . Hivyo tunaweza kuponywa nafsi zetu na roho zetu. Hata kama uponyaji haujanja katika mwili.
Lakini mara nyingi ukitokea uponyaji wa ndani basi matokeo
yake utayaona hata kimwili. (anima sana in
corpore sano) (Roho yenye afya katika mwili
wenye afya)
1. Ekaristi Takatifu inayalinda maisha ya
kimanga ya roho tuliyoyapokea wakati wa Ubatizo
, kwa kupata anayekomunika nguvu za kimungu za kupambana na vishawishi, na
kudhoofisha nguvu za tamaa. Inaimarisha uhuru wa mapenzi ya nafsi zetu wa kuhimili
mashambulizi ya shetani.
2. Ekaristi Takatifu inaongeza maisha ya
neema ambayo tayari tunayo. Hufanya hivyo kwa kuhuisha fadhila na vipaji vya Roho Mtakatifu
tulivyonavyo.
3. Ekaristi Takatifu inayatibu magonjwa ya kiroho ya nafsi kwa kuziondoa dhambi ndogo na kumkinga mtu na adhabu ndogo ndogo za kidunia
zitokanazo na dhambi. Ondoleo la dhambi ndogo na mateso ya muda yasababishwayo na dhambi hizi hufanyika mara moja kwa sababu ya upendo
kamili kwa Mungu ambao huamshwa kwa
kuipokea Ekaristi. Ondoleo la dhambi hizi
hutegemea kiasi cha upendo unaoelekezwa
kwenye Ekaristi (Lk 7:47).
4. Ekaristi Takatifu inatupa furaha ya kiroho tunapomtumikia Kristo, tunapotetea njia yake,
tunapotekeleza majukumu yetu ya maisha, na kufanya sadaka zetu zinazotukabili zile ni katika kuiga maisha ya Mwokozi wetu.
The ListPages module does not work recursively.

Je, hii ni kweli kwa wale wasichana wasiojibu meseji WhatsApp!!!?

Ukiona hivyo ujue ndio hivi

Mwanaume mwenzangu ukiona unamtext msg msichana WhatsApp kaisoma hajajibu, umetuma ya pili kasoma hajajibu, ukatuma ya tatu hajajibu mmmmmh😨😨 hapo ujue mwenzio kaangalia kwenye profile yako, kakagua picha weee mwishoni akajisemea tu “Huyu.mkaka hapana kwa kweli”🤣🤣🤣🤣🤣🤣

🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂🏃‍♂

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo.

Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.

Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida za kutembea kwa miguu.

  1. Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
  2. Huimarisha mifupa.
  3. Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
  4. Husaidia kupunguza uzito.
  5. Huzuia saratani ya utumbo mpana.
  6. Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
  7. Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
  8. Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito – BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
  9. Hukabili shinikizo la damu.
  10. Huondoa msongo wa mawazo.
  11. Huongeza utayari.
  12. Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
  13. Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
  14. Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
  15. Huimarisha misuli.
  16. Husaidia mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri.
  17. Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
  18. Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
  19. Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
  20. Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
  21. Hukuweka katika hali nzuri (mood).
  22. Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
  23. Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
  24. Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
  25. Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.

Naamini umeona jinsi ambavyo kutembea kwa miguu kuna manufaa makubwa sana kwenye afya, uchumi na hata mahusiano yako ya kijamii.

Inashauriwa kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku. Kwa njia hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.

Maswali na Majibu kuhusu Kanisa Katoliki

Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,“Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’’ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: ‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” 6Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:1-8)


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Umwilisho maana yake ni nini?

Umwilisho ni ile hali ya Yesu kama Mungu kujifanya mtu kwa Bikira Maria mzaa. (Yoh 1:14)


Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?

Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15)


Kanisa Katoliki ni nini?

Kanisa Katoliki ndio Jumuia ya Wakristu Wote pamoja na Maaskofu na Mapadri wanaoshiriki imani moja chini ya Baba Mtakatifu Mkuu wao


Ni nini Msingi wa Imani na Mafundisho ya Kanisa Katoliki?

Msingi wa Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki ni;
1. Biblia Takatifu
2. Mapokeo Matakatifu
3. Mamlaka ya Kanisa


Ni nani ameanzisha Kanisa Katoliki?

Yesu Kristo ameanzisha Kanisa Katoliki


Yesu aliweka makanisa mangapi? Yesu hakufanya makanisa mengi?

Hapana. Yesu alifanya Kanisa moja tuu.
Mungu ni Mmoja muumba na Baba wa wote, Mkombazi ni mmoja tuu, Yesu Kristo, Dini ni moja, Imani ni moja, Ubatizo ni mmoja, basi Kanisa ni moja kwa watu wote na nchi zote


Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20)


Kanisa linatimiza kusudi la Yesu Kristo kwa namna gani?

Kanisa linatimiza kusudi la Yesu Kristo kwa;
1. Kwa Ualimu wake yaani kuwafundisha watu
2. Kwa Ukuhani wake yaani kuwatakasa watu
3. Kwa Uchungaji wake yaani kuwaongoza watu.


Alama za kanisa la kweli ni zipi?

Alama za kanisa la kweli ni hizi;
1. Kanisa ni moja
2. Kanisa ni a Takatifu
3. Kanisa ni Katoliki
4. Kanisa ni la Kitume
5. Kanisa ni la Kimisionari


Kanisa ni Moja maana yake ni nini?

Kanisa ni moja maana yake ni la mahali popote na siku zote lina mafundisho yale yale, Sakramenti zile zile na mkubwa mmoja


Kanisa ni Takatifu maana yake ni nini?

Kanisa ni Takatifu maana yake:-
1. Limeanzishwa na Mungu mwenyewe aliye Mtakatifu
2. Kristo aliye Mtakatifu alijitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake ili kulitakasa
3. Roho Mtakatifu hulihuisha kwa upendo wake
4. Ndani yake wamo Bikira Maria na Watakatifu wengi wanaoliombea


Kanisa ni Katoliki maana yake ni nini?

Kanisa ni Katoliki maana yake ni la watu wote mahali pote na nyakati zote.


Kanisa ni la Kitume maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kitume maana yake wakubwa wake yaani Baba Mtakatifu na Maaskofu nimahalifa wa Mitume


Kanisa ni la Kimisionari maana yake ni nini?

Kanisa ni la Kimisionari maana yake limetumwa kupeleka habari njema kwa mataifa yote. (Mt 28:19-20)


Yesu amemweka nani kuwa mkubwa wa Kanisa?

Yesu amemweka Mtume Petro kuwa Mkubwa wa Kanisa zima. (Mt 16:18-19). Halifa wa Mtume Petro ni Baba Mtakatifu.


Kanisa Katoliki laweza kudanganya katika mafundisho yake?

Hapana. Kanisa Katoliki haliwezi kudanganya katika mafundisho yake kwa sababu Roho Mtakatifu analilinda daima lisikosee na analiongoza. (Yoh 14:26).


Jimbo Katoliki ni nini?

Jimbo Katoliki ni Jumuiya ya Wakristo ambao katika Imani na Sakramenti wana ushirika na Askofu aliye halifa wa Mitume.


Tuwaonaje Wakristo ambao sio Wakatoliki?

Ingawa wamejitenga katika ushirika kamili wa Kanisa Katoliki, tunawatambua kuwa ndugu zetu kutokana na ubatizo wao.


Nje ya Kanisa Katoliki hakuna Wokovu maana yake ni nini?

Nje ya Kanisa Katoliki hakuna wokovu maana yake ni Mkatoliki akijiondoa katika kanisa au mtu akukataa kuingia wakati anajua Yesu ameanzisha limuokoe atapotea Motoni Milele.


Taifa la Mungu limeundwa kwa namna gani?

Taifa la Mungu limeundwa kwa Maklero yaani Maaskofu, Mapadri, Mashemasi, Watawa na Walei.


Maklero ni wakina nani?

Maklero ni watu wote wenye daraja Takatifu yaani Maaskofu, Mapadri na Mashemasi.


Watawa ni akina nani?

Watawa ni Waamini, Walei au Maklero waliowekwa wakfu kwa Mungu katika Kanisa kwa ajilli ya wokovu wao na wa dunia:-
1. Kwa kufunga rasmi nadhiri za Kitawa mbele ya Kanisa
2. Kwa kuishi masharti ya injili, utii, ufukara na useja mtakatifu.
3. Kwa kufuata mtindo wa maisha uliokubalika na Kanisa


Walei ni wakina nani?

Walei ni wote katika Kanisa wasio na Daraja Takatifu


Ushirika wa Watakatifu ni nini?

Ushirika wa Watakatifu ni:-
1. Umoja na ushirikiano kati ya Wakristo Duniani, Watakatifu Mbinguni, na marehemu toharani.
2. Ni muungano wa Waamini wote katika Ekaristi Takatifu.


Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu? Na kwa nini aheshimiwe?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu kwa sababu amemzaa Yesu na Yesu ni Mungu.
“Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, 27kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. 28Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!” 29Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 30Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” 34Maria akamwuliza huyo malaika, “Maadam mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” 35Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu Zake Yeye Aliye Juu zitakufunika kama kivuli, kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 36Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana. 38Maria akasema, “Tazama, mimi ni mtumisi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka akamwacha.”(Lk 1:26-38).
Yesu ni Mungu ndio maana Bikira Maria akaitwa Mama wa Mungu kwa sababu ndiye aliyemzaa Yesu. Yaani Bikira Maria ni Mama wa Mungu tuu kwa sababu ya kumleta Yesu Duniani kama mzazi wa kimwili.

Je, Bikira Maria kuitwa Mama wa Mungu maana yake ni kwamba yeye ndiye chanzo cha Yesu na Bila yeye Yesu asingekuwepo?

Hapana, haimaanishi kwamba Bikira Maria ni chanzo cha Yesu. Hii haimaanishi kwamba Bikira Maria ni Mama wa Yesu kabla ya Yesu kuja Duniani kwa maana Yesu Alikuawepo kabla ya kuzaliwa kwake.
“Baba yenu Abrahamu alishangilia kwamba angaliiona siku Yangu, naye akaiona na akafurahi.’’ 57Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, Wewe wasema umemwona Abrahamu?’’ 58Yesu akawaambia, ‘‘Amin, amin, nawaambia, kabla Abrahamu hajakuwako, ‘Mimi niko.’’’ (Yohane 8:56-58)
Inamaana kuwa Yesu alikuwepo kabla ya Mama yake. Kwa sababu hiyo Umama wa Bikira Maria ni wa Kimwili tuu na sio Umungu. Bikira Maria hajatangulia kuwepo kabla ya Yesu Bali Yesu ndiye alikuwepo kabla na ni Mungu wake pia. Yesu kama Mungu alimuumba Bikira Maria na kumfanya Mama yake wa kimwili.
“Usiogope, Maria, umepata upendeleo kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele na ufalme Wake hautakuwa na mwisho.” (Luka 1:31-33)
Bikira Maria alipewa nafasi ya kipekee na Mungu kuwa Mama yake na ingewezekana nafasi hii apewe mwanamke mwingine kama Bikira Maria Asingekuwepo au asingekuwa tayari kupokea heshima hii. Ndiyo maana Bikira Maria katika unyonge wake alitambua kuwa ni nafasi ya upendeleo wa Mungu aliyopewa na hivyo alimshukuru na kumtukuza Mungu kwa nafasi hii.
41Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. 43Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45Amebarikiwa yeye aliye amini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.” 46Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, 48kwa kuwa ameangalia kwa fadhili unyonge wa mtumishi wake, hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita mbarikiwa, 49kwa maana, Yeye Mwenye Nguvu, amenitendea mambo ya ajabu, Mtakatifu ndilo Jjina Lake.” (Luka 1:41-49)

Je Bikira Maria anamwonaje Yesu? Bikira Maria Anamchukulia Yesu kama nani Kwake?

Bikira maria anamwita Yesu Mwanae wa kumzaa kwa kuwa Bikira Maria ndiye aliyemzaa Yesu Duniani na kumlea kama mtoto wake. Vilevile Bikira Maria anamwita Yesu Bwana na Mungu wake kwa kuwa ni Mungu wake pia. Kwa sababu hivyo Bikira Maria ni mdogo mbele ya (Yesu) Mungu kama kiumbe cha Mungu (Yesu).

Kwa nini Bikira Maria anapewa Heshima kubwa

Tunamuheshimu Bikira Maria kwa sababu ya nafasi yake ya kipekee ya upendeleo aliyopewa na Mungu ya Kuwa Mama wa Mungu. Tunapomuita Bikira Maria Mama wa Mungu tunaheshimu nafasi yake ya kipekee ya kuizalia Dunia Yesu aliye Mungu na Mkombozi wetu.

Je, Bikira Maria anastahili kuabudiwa? Je Tunamwabudu Maria?

Hapana, Bikira Maria hastahili kuabudiwa na wala hatumuabudu Maria. Kwa kuwa Bikira Maria ni kiumbe wa Mungu na ni Mdogo kuliko Mungu kwa hiyo hana Umungu wowote hivyo haabudiwi kama Mungu au pamoja na Mungu.

Kwa nini tunamuheshimu Bikira maria na kusali kwake?

Tunamuheshemu Bikira Maria na Kumuomba atuombee kwa Mungu mwanaye Yesu kwa sababu anayo nafasi ya kipekee mbele ya Mungu mwanaye Yesu kama Mama yake wa kumzaa Duniani na kama mlezi wake akiwa duniani tangu kuzaliwa mpaka kufa Msalabani wakiwa pamoja.
Yesu mwenyewe alimtii na kumsikiliza Mama yake ndio maana muujiza wa kwanza aliofanya aliambiwa na mama yake. Bikira Maria ndiye aliyemwomba Yesu Afanye muujiza wake wa kwanza.
1 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. 2Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. 3Hata divai ilipowaishia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai. 4 Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia, fanyeni. 6 Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kunawa, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. 7Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza mpaka juu. 8Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa sherehe. Wakapeleka. 9Naye mkuu wa sherehe alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa sherehe alimwita bwana arusi, 10akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; na watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa. 11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. Yohana 2:1-11


Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa kwa sababu ni yeye aliyemzaa Yesu Kristo ambaye amelianzisha Kanisa.


Bikira Maria anafaida yeyote kwa Kanisa?

Ndiyo. Bikira Maria ni mwombezi Mkuu wa Kanisa.


Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria inafuata baada ya Heshima kwa Utatu Mtakatifu


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Je, inafaa tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi?

Hapana, haifai tushike neno lolote la Agano la Kale kama Wayahudi wasiozingatia jinsi Yesu alivyolitimiliza kwa maneno na matendo hata wakamshutumu kutenda kinyume:
“Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato” (Yoh 9:16).
Alipofafanua amri 10 za Mungu alikariri:
“Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa… lakini mimi nawaambieni…” (Math 5:21,27,31,33,38,43).
Alipouliziwa unajisi wa vyakula kadhaa, alisisitiza,
“’Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni?’ Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote” (Mk 7:18- 19).
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16-17).
Hakika, mwili ni mzito kuliko kivuli chake.
Vile vile katika Warumi 4:16. Tunasoma “Kwa sababu hiyo, jambo hili lategemea imani, hivyo kwamba ahadi hiyo yatokana na neema ya Mungu, na kwamba ni hakika kuwa ahadi hiyo ni kwa ajili ya wote:si kwa wale tu wanaoishika sheria, bali kwa wale waishio kwa Imani kama Abrahamu. Yeye ni Baba yetu sote.”
Wakristo wengine wanachanganywa na wale wasioyajua maandiko na kuwataka washike sheria na Torati,basi tukisema ni lazima kushika sheria tutakua tunakataa kua Abrahamu hakuwa mtu wa Mungu maana kwa Abrahamu hatukuwa na Sheria wala Torati na alipata kibali machoni Pa Mungu tuu kwa Imani. Kumbuka pia Abrahamu alitahiriwa baada ya Kuwa tayari mtu wa Mungu kwa Imani yake na sio kwamba Kutahiriwa ndio kulifanya mtu wa Mungu.
Tumekombolewa kwa Imani na sio kwa Sheria. Wagalatia 5:18 “Lakini Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”
Hatumtumikii Mungu ili tuwe watu wa Mungu bali tukishakua watu wa Mungu ndio tunamtumikia Mungu.


Je, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na kila mtu?

Hapana, ufunuo wa Mungu unaweza kufafanuliwa rasmi na umoja wa Maaskofu tu, kwa kuwa ndio waandamizi wa Mitume 12 wa Yesu.
“Au je, neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?” (1Kor 14:36).
“Hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu” (2Pet 1:20-21).
Tunahitaji unyenyekevu wa Mwafrika ambaye shemasi Filipo alimsikia “anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, ‘Je, yamekuelea haya unayosoma?’ Akasema, ”Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza?’ Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye” (Mdo 8:30-31).


Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,
“Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16).
“Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).


Tunaweza kusadiki vipi?

Tunaweza kusadiki kwa msaada wa Roho Mtakatifu tu, anayetuelekeza kwa Mungu, akituangazia Neno lake na kutuvuta tulikubali kwa moyo.
“Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu” (Yoh 7:17).
“Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu kweli, nanyi mnajua nyote” (1Yoh 2:20).
Kumbe, “Mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni” (1Kor 2:14).


Je, miujiza inaweza kutusaidia tusadiki?

Ndiyo, miujiza inaweza kutusaidia tusadiki, lakini inaweza kutudanganya pia.
“Wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo yupo hapa’, au, ‘Yuko kule’, msisadiki. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu, wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule” (Math 24:23- 24).
“Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru” (2Kor 11:13-14).
Alipomshawishi Yesu alitumia hata maneno ya Biblia “akamwambia, ‘Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini, kwa maana imeandikwa: Atakuagizia malaika zake, na mikononi mwao watakuchukua, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe” (Math 4:6).


Kanisa linahusika vipi na imani?

Kanisa linahusika na imani kama mama wa waamini wote, kwa sababu imani yake inatangulia, inazaa, inategemeza na kulisha imani yetu: lenyewe ni “nguzo na msingi wa kweli” (1Tim 3:15).
Tukiondoa nguzo na msingi, nyumba ya ukweli haiwezi kusimama.
“Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa?… Basi imani, chanzo chake ni kusikia” (Rom 10:13-15,17).
Hivyo wokovu unategemea kupokea kwa imani maneno ya watu hai waliotumwa rasmi, sio Biblia peke yake. Mitume waliandika tu kwa kutegemeza mahubiri yao:
“Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wowote utokao katika hiyo kweli” (1Yoh 2:21).
“Nitakuwa tayari kuwakumbusha hayo sikuzote, ijapokuwa mnayajua na kuthibitishwa katika kweli mliyo nayo” (2Pet 1:12).


Je, tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki?

Ndiyo, tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki kwa moyo mmoja tupate uzima wa milele, kwa kuwa Yesu aliwaambia Mitume,
“Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” (Mk 16:16).


Tunapaswa kusadiki hasa nini?

Tunapaswa kusadiki hasa Utatu wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Milele yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuvia Roho Mtakatifu, kama vile jua linavyotoa mwanga na joto lisitenganike navyo.
Mwana, ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Eb 1:3), alisema: “Nimekuja kutupa moto duniani” (Lk 12:49).
Naye Roho aliwashukia wafuasi wake “kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” (Mdo 2:3-4).


Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

Hapana, Mungu hagawanyiki hata kidogo, bali daima ni Umoja kamili.
“Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” (Mk 12:29).
Tumuabudu yeye peke yake katika nafsi tatu, na Utatu wa nafsi katika Umoja wa hali yake, tusichanganye nafsi wala kugawa Umungu. Baba si Mwana wala Roho Mtakatifu. Mwana si Baba wala Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si Baba wala Mwana. Lakini milele yote nafsi hizo tatu ni Mungu yuleyule pasipo tofauti ya kuzitenganisha: kila moja imo ndani ya nyingine.
“Mimi na Baba tu umoja” (Yoh 10:30).


Kwa nini Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu”?

Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu” kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: “Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
” (Lk 1:42-43).

Je, Bikira Maria ni kama Bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu Duniani au anayo thamani zaidi?

Bikira Maria sio kama bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu duniani. Yesu ametokana na Bikira Maria katika ubinadamu wake. Mwili wa Yesu wa kiubinadamu ni sehemu au uzao wa Bikira Maria. Bikira Maria anayo uhusiano wa damu na Yesu Kristu. Ndiyo maana Mungu alimtakasa Bikira Maria Ili atakayezaliwa kutoka kwake awe na yeye mtakatifu.
Mungu alimtakasa Bikira Maria kabla ya Kuamua kuzaliwa kupitia yeye kwa kuwa Mungu ni Mtakatifu. Ubinadamu wa Yesu (MWILI – Nyama na Damu) asili yake ni Bikira Maria.


Kanisa maana yake nini?

Kanisa maana yake ni “kusanyiko”: ndani yake Roho Mtakatifu anaunganisha na Yesu na kati yao wale waliopokea Neno la Mungu na sakramenti zake.
“Bwana alilizidisha Kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa… Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja” (Mdo 2:47; 4:32).
Ndio tokeo la ombi la Yesu:
“Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako, hao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma” (Yoh 17:21).
Kumbe utitiri wa madhehebu yaliyotenganika unaleta picha ya “tawanyiko” ambayo inakwaza ulimwengu usisadiki.
“Kila mtu wa kwenu husema, ‘Mimi ni wa Paulo’, na, ‘Mimi ni wa Apolo’, na, ‘Mimi ni wa Kefa’, na, ‘Mimi ni wa Kristo’. Je, Kristo amegawanyika?” (1Kor 1:12-13).


Je, Kanisa ni kundi la binadamu tu?

Hapana, Kanisa si kundi la binadamu tu, tunaloweza kulianzisha kama vile chama, timu n.k.
Kanisa ni fumbo la Mwili wa Kristo unaohuishwa na Roho Mtakatifu. Kama Yesu linaonekana upande wa ubinadamu tu, kumbe linaunganisha utu na Umungu.
Baba “alivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote” (Ef 1:22-23).


Je, tunaweza kuambatana na Yesu tukilikataa Kanisa?

Hapana, hatuwezi kuambatana na Yesu kwa kulikataa Kanisa, kwa kuwa hao wawili ni mwili mmoja, kama Bwanaarusi na Bibiarusi.
“Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, ‘Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Math 19:4-6).
“Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa” (Ef 5:32).


Je, Kanisa ni muhimu kwa wote?

Ndiyo, Kanisa ni muhimu kwa wote kwa kuwa ndilo ishara na chombo cha umoja wa watu na Mungu na kati yao.
“Aliwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja” (Ef 2:16- 18).


Wokovu unapatikana wapi?

Wokovu unapatikana kwa Yesu tu, anayeishi katika Kanisa lake. Hata hivyo Roho Mtakatifu anaweza akaongoza mtu asiyewajua bila ya kosa lake aungane nao kiroho kwa kumlenga Mungu na kujitahidi kumtii kwa moyo wote.
“Tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio” (1Tim 4:10).
“Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye… Twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vilevile kama wao” (Mdo 10:34-35; 15:11).


Mtu akijua Kanisa ni la lazima kwa wokovu asiingie au ajitenge nalo, itakuwaje?

Mtu akijua Kanisa ni la lazima kwa wokovu asiingie au ajitenge nalo hawezi kuingia mbinguni.
“Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe” (1Tim 4:1-2).
“Watoto, ni wakati wa mwisho. Na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu” (1Yoh 2:18-19).


Je, anayejiunga na Kanisa na kudumu ndani yake ana hakika ya kuingia mbinguni?

Hapana, anayejiunga na Kanisa na kudumu ndani yake lakini haongozwi na Roho Mtakatifu kuishi kadiri ya ubatizo wake atahukumiwa na Mungu vikali zaidi kwa kuchezea neema kubwa hivi.
“Kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi” (Lk 12:48).


Sifa kuu za Kanisa ni zipi na zinapatikana wapi?

Sifa kuu za Kanisa ni kuwa moja, takatifu, katoliki na la Mitume. Sifa hizo zinalitambulisha kati ya madhehebu mengi Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu kumpitia Mtume aliyembadilishia jina aitwe Petro, yaani Mwamba wa Kanisa lake lisilokoma wala kupotoka kamwe:
“Wewe u Simoni, mwana wa Yohane; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro)” (Yoh 1:42).
Siku ya Pentekoste, “waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu” (Mdo 2:41).
Ndiye aliyekaribisha hata wasio Wayahudi: “Tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini” (Mdo 15:7).
Baada ya kuongoza Mitume wenzake na Kanisa lote, aliuawa msalabani huko Roma kama alivyotabiriwa:
“’Utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka’. Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu” (Yoh 21:18-19).


Kanisa kuwa moja maana yake nini?

Kanisa kuwa moja maana yake ni “mwili mmoja na Roho mmoja”: lina “Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Ef 4:4-5).
Yesu alisema, “Na kondoo wengine ninao. Ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja” (Yoh 10:16).
Hakuna Kanisa lingine, isipokuwa matawi ambayo yamekatika kwa kiasi tofauti, na yana uhai kadiri yanavyounganika bado na shina. Hata leo Kanisa Katoliki peke yake lina waamini wengi kuliko jumla ya madhehebu mengine ya Kikristo.


Kanisa kuwa takatifu maana yake nini?

Kanisa kuwa takatifu maana yake ni kazi ya Mungu mtakatifu inayong’aa katika watakatifu wa mbinguni, hasa Bikira Maria.
“Ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu” (1Pet 2:9-10).
“Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa” (Ef 5:25-27).
Hata hivyo hapa duniani linaundwa na wakosefu pia:
“Ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya wa kila namna. Hata lilipojaa, walilivuta pwani, wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa” (Math 13:47-48).


Kanisa kuwa katoliki maana yake nini?

Kanisa kuwa katoliki maana yake linaweza kuwatolea watu wote wa mahali pote na wa nyakati zote kweli zote za imani na vifaa vyote vya kufikia wokovu wa milele.
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18- 20).


Kanisa kuwa la Mitume maana yake nini?

Kanisa kuwa la Mitume maana yake limejengwa juu ya Mitume 12 wa Yesu na kuongozwa na waandamizi wao.
“Ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwanakondoo” (Ufu 21:14).
“Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Yesu Kristo mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Ef 2:20-22).


Kanisa limepewa na Yesu muundo gani?

Kanisa limepewa na Yesu wahudumu wenye daraja takatifu wanaoitwa makleri; waamini wengine wanaitwa walei. Kutoka pande hizo mbili wanapatikana watawa waliowekwa wakfu kwa namna ya pekee kwa kushika mashauri ya Kiinjili.
Yesu “alipanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri” (Mk 3:13-14).
“Walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake” (Mdo 1:13- 14).


Je, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya mwamba?

Ndiyo, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya Mtume Petro, alichunge lote kwa niaba yake. Papa kama Askofu wa Roma ndiye mwandamizi wa Petro na mkuu wa kundi zima la Maaskofu, waandamizi wa Mitume.
“Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, wala milango ya kuzimu haitalishinda” (Math 16:18).
“Atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba” (Math 7:24-25).
Historia ya miaka elfu mbili sasa imedhihirisha ukweli wa maneno hayo.


Papa amejaliwa na Mungu mamlaka gani?

Papa amejaliwa na Mungu mamlaka kamili juu ya waamini wote awafungulie ufalme wa mbinguni, kama Yesu alivyomuambia Petro: “Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Math 16:19).
“Nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako” (Lk 22:32).
“Lisha wanakondoo wangu… Chunga kondoo zangu… Lisha kondoo zangu” (Yoh 21:15-17).


Maaskofu wote wamerithi mamlaka gani?

Maaskofu wote wamerithi mamlaka ya Mitume kwa kufundisha, kutakasa na kuongoza Kanisa lote pamoja na Papa na chini yake.
Wale waliokabidhiwa jimbo fulani ni msingi wa umoja kwa waamini wao na kati yao na Kanisa lote duniani.
“Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Mdo 20:28).


Maaskofu wanasaidiwa na nani?

Maaskofu wanasaidiwa kwanza na mapadri katika uchungaji, halafu na mashemasi katika utumishi.
“Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye: lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia” (1Pet 5:1-2).
“Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na Maaskofu na mashemasi” (Fil 1:1).


Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao.
“Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja” (1Kor 10:16-17).
Bila ya ekaristi tusingekuwa Kanisa, bali jumuia tu, kama madhehebu mengi yaliyojichagulia viongozi wasioshirikishwa hizo daraja takatifu kwa kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume.
“Uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu” (2Tim 1:6).
“Nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru” (Tit 1:5).
“Usimwekee mtu mikono kwa haraka” (1Tim 5:22).


Walei wanaitwa na Mungu kufanya nini?

Walei wanaitwa na Mungu kuratibu malimwengu yote yafuate matakwa yake.
“Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima” (Rom 13:7).
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema” (Tit 3:1).
“Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu” (1Pet 2:15-16).


Watawa wanashika mashauri gani ya Kiinjili?

Watawa wanashika hasa mashauri ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu ambayo msingi wake ni maisha na mafundisho ya Yesu kadiri ya Injili.
“Wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee” (Math 19:12).
“Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate” (Math 19:21).
“Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo” (Yoh 15:14).


Ushirika wa watakatifu maana yake nini?

Ushirika wa watakatifu maana yake sisi, kwa kushiriki mafumbo matakatifu tunaunda ndani ya Kristo mwili mmoja, ambamo waadilifu waliopo duniani, marehemu wa toharani na wenye heri wa mbinguni tunaunganishwa na upendo tufaidike na mema ya kila mmoja.
“Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana. Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia” (Rom 14:8-9).
“Kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor 12:26-27).
Dhambi yoyote kubwa inatutenga na ushirika huo kama Yesu alivyosema,
“Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa” (Yoh 15:1-2).
Lakini “Mungu aweza kuwapandikiza tena… Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake” (Rom 11:23,29).


Je, Kanisa linaweza kutuondolea dhambi yoyote?

Ndiyo, Kanisa linaweza kutuondolea dhambi yoyote katika ubatizo na kitubio kwa kutumia mamlaka ambayo Yesu mfufuka aliwashirikisha Mitume wake alipowavuvia akisema:
“Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23).
“Mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu” (1Kor 6:11).


Ekaristi maana yake nini? Je ni kweli Yesu yupo katika Maumbo ya Mkate na Divai?

Ekaristi maana yake ni shukrani, iliyokuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu.
23Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: Kwamba, usiku ule Bwana Yesu alipotolewa, alitwaa mkate, 24akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” 25Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
26Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana. (1Kor 11:23-27).

Yesu alituambia nini kuhusu Mwili wake na damu yake?

Yesu alituambia hivi;
“Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. 50Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ 53Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. 58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.’’ (Yoh 6:49-58)

Damu na Mwili aliotupa Yesu ni nini? Ekaristi ni nini hasa?

Maana ya Damu na Mwili aliyoisemea Yesu tunaipata hapa;
“Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi Wake akisema, “Kuleni, huu ndio mwili Wangu.’’ 23Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa wanafunzi Wake, wote wakanywa kutoka humo. 24Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25Amin nawaambia, sitakunywa tena uzao wa mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika Ufalme wa Mungu.’’ 26Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni. (Marko 14:22-26).
Kwa hiyo Yesu alionyesha upi ni mwili wake na damu yake

Fundisho hili la mwili na damu ya Yesu (Ekaristi) lilikua Agizo tunalopaswa kulitii mpaka leo?

Ndiyo, Yesu alisema tufanye hivyo kwa ukumbusho wake
“Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” (Luka 22: 19).
Kwa hiyo aliwaagiza Mitume wafanye hivyo pia.

Mitume walitii Fundisho la Ekaristi na waliliishi?

Ndiyo, Kila walipokutana Walishiriki Meza ya Bwana Kama tunavyosoma Kwenye vifungu vifuatavyo;.
46Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, (Mdo 2:46).
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. (Mdo 20:7)

Je mkate na divai vilichukuliwa na Mitume kama nini hasa? walichukulia Ekaristi kama nini?

Mitume walichukua Mkate na divai kama mwili na damu ya Yesu Kristu na walishiriki kiaminifu na kwa usafi wa moyo.
16Je, kikombe cha Baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17(Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja) (1 Wakorinto 10:16)
27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. 31Lakini kama tungejipambanua wenyewe tusingehukumiwa. 32Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. (1Wakorinto 11:27-32)
21Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22Je, tunataka kuamsha wivu wa Bwana? Je, sisi tuna nguvu kuliko Yeye? (1 Wakorinto 10:21-22)

Je ni lazima Kwa Mkristu kupokea Mwili na damu ya Yesu (Ekaristi)?

Yesu alisema hivi;
53Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. (Yohana 6:53–56)

Je ni kwa nini madhehebu mengine hawakubali mafundisho haya ya Ekaristi Takatifu, Je ni mara ya kwanza watu kukataa?

Hii ni sababu ya ugumu wa mioyo na kutokuelewa maandiko ndio maana madhehebu mengine wanaukataa kwa dhati Mwili na Damu ya Yesu.
Hata wakati Yesu akiyasema maneno haya Wafuasi Wengi Walimwacha kama Biblia inavyosema;
60Wengi wa wafuasi Wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?’’ (Yohana 6:60).
Haishangazi hata leo weni hawaamini mafundisho haya japokua ndio msingi wa Imani ya Kikristo.

Mitume walifundisha nini kuhusu Mwili na Damu ya Kristu (Ekaristi)?

23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema “Huu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.” 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume waliwaasa Wakristu wa kwanza Kushiriki Mwili na Damu ya Yesu kila mara na kwa Uaminifu.

Je Yesu Yupo Mzima katika Ekaristi Takatifu? Na kwa nini Tunaabudu Ekaristi?

Ndiyo. Ekaristi Takatifu inamuwakilisha Yesu Mwenyewe aliye Mungu na aliyeamua Mwenyewe kuwepo katika Maumbo ya Mkate na Divai.
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?’’ 53Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. (Yoh 6:51-57)
Mstari wa 51 Yesu alisema wazi Mkate huo ni Mwili wake.
Thamani na Uwepo wa Yesu Mwenyewe unaonekana katika Mstari wa 53 na wa 56. Kumbuka hapa amesema “Mimi nitakaa ndani yake” Hakusema Mwili wangu utakaa ndani yake. Kwa maana nyingine ni kwamba Ekaristi ni Yesu Mzima na Sio Mwili tuu.
54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
Wale Wanaopinga fundisho la Ekaristi wanafikiri Yesu alivyosema Mimi ni Chakula Kutoka Mbinguni hakumaanisha Mwili bali Maneno na Imani Kwake lakini Tukisoma 51 Yesu alisema wazi kuwa Mwili wake ndio Mkate wenyewe.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’
Mitume wa Yesu walielewa hivi fundisho hili ndio Maana walishiriki Meza ya Bwana kila walipokutana na waliheshimu kama Mwili na Damu ya Kristo.
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. (Mdo 20:7)
Ili kujua kuwa Mitume waliheshimu Mwili na Damu ya Yesu Biblia inatuambia hivi;
23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema “Huu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.” 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume walisisitiza kuhusu Mwili na Damu ya Kristu kuwa ni Mtakatifu.
Kwa hiyo basi kama tunavyosoma katika Yoh 6:51; na
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.’’
Yesu alisema Mimi ni Mkate wa Uzima ambao alimaanisha upo katika Mwili wake. Mwili tuu hauna uzima kama hauna Yesu ndani yake. Kwa sababu Mwili ni Mzima na Unaye Yesu ndani yake ndiyo maana unaweza kuleta uzima kwa Wengine.
Tunaelewa kwamba Yesu alijitoa Msalabani Mwili Wake na Damu yake na ndicho alichotupa ktk Ekaristi. Na Mwili wake huo Ulikua umembeba yeye aliye Mungu ndiyo maana tunaabudu Ekaristi alipo Yesu aliye Mungu.
Kwa kuwa Yesu ni Mungu Kama tunavyosoma katika Yoh 1:1-12
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu……..14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. (Yoh 1:1-12)
Kwa hiyo Neno huyo huyo Ndiye aliyetukomboa kwa kuutoa mwili wake sadaka Msalabani na ndiye Aliyetupa Mwili Wake na Damu yake ktk Ekaristi na anaabudiwa kwa kuwa yupo katika mwili huo.
“Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.” (Luka 22: 19).
Kwa namna hii alitupa mwili wake.
Alisema fanyeni kwa ukumbusho wangu na Sio wa mwili wangu.
Hivyo Ekaristi ni Yesu Mwenyewe aliye Mungu. Ndiyo sababu tunaabudu Ekaristi Takatifu.


Je, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa?

Ndiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa kwa sababu kazi ya wokovu haimtegemei binadamu, bali Mungu.
“Hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu” (Eb 5:4-5),
Yesu alisisitiza alivyopewa na Baba uwezo wa kutuokoa. “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake” (Yoh 3:35).
“Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele” (Yoh 17:2)
.
Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki:
“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” (Math 28:18-20).
Mpaka mwisho wa dunia uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa mamlaka. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.


Je, wenye daraja wanastahili heshima?

Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo.
“Amin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipeleka” (Yoh 13:20).
“Jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesu” (Gal 4:14).
“Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii” (Tito 3:1).
Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia.
“Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha” (1Tim 5:17).


Kanisa linaheshimu marehemu kwa namna gani?

Kanisa linaheshimu marehemu kwa kuwafanyia mazishi huku likiwaombea kwa Mungu.
“Watu watauwa walimzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu” (Mdo 8:2).
Yeye kama mfiadini, aliyefikia upeo wa upendo kwa kutoa uhai wake, hakuhitaji kuombewa. Lakini wafu wengine walitolewa sala na sadaka tangu Israeli ilipoanza kusadiki ufufuo.
“Kama asingalitumaini kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi yao” (2Mak 12:44-46).
“Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?” (1Kor 15:29).


Je, Kanisa linahimiza waamini wapokee Ekaristi wakati gani?

Kanisa linahimiza waamini wapokee Komunyo Takatifu kila siku wanaposhiriki Misa


Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.

Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.

Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.

Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?

Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.

Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?

Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.

Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?

Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.

Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia

Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.

Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?

Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.

Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu

Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.

Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?

Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu “…
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

TAFAKARI KUHUSU NAFASI YA MATESO NA SHIDA KATIKA MAISHA

Ni kwa nini tunapata Mateso na shida katika Maisha? Kwa nini Mungu ameruhusu tuteseke?

Mungu hapendi mtu Ateseke lakini ni kwa njia ya ya Mateso mtu anaweza akapimwa IMANI yake, UNYENYEKEVU, UTII na Matumaini yake kwa Mungu.


Mateso na shida katika maisha ni nafasi ya kujifunza na Kuonyesha unyenyekevu, Imani na Matumaini ya mtu.


Mateso yanaweza kuwa malipizi ya dhambi kama adhabu au Majitoleo .


Mtu anaweza kujitesa au kukubali Mateso huku akiyachukulia kama malipizi ya dhambi zake au dhambi za wengine.


Sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kukubali au kujitesa kwa ajili ya dhambi hasa kwa dhambi zisizokua zake, Ni watu wachache Wenye fadhila hii. Mfano Watakatifu kama Mt. Faustina aliweza kuchukua Mateso kama malipizi ya dhambi hasa za watu wengine ambapo alikubali magonjwa shida na Kudharauliwa kama malipizi ya dhambi.


Yesu mwenyewe pamoja na Umumgu na Enzi yake alikubali Mateso kama Malipizi ya dhambi za watu na Kama njia ya Kuonyesha Unyenyekevu na Upendo.

Kumbuka, Mateso ni njia ya Kuonyesha unyenyekevu, Upendo na Kujitolea kwa hiyo ni kama malipizi na majitoleo hivyo sio lazima mtu ateseke au Ajitese ili aokolewe au aingie Mbinguni.


Mungu hapendi mtu ateseke ila anakubali Mateso kama njia ya kupima mtu na kumtakatifuza.

Mateso = Malipizi = Majitoleo = Kipimo cha Imani na Matumaini kwa Mungu

KUMBUKA: Ni kwa njia ya Mateso na Kifo cha Bwana wetu Yesu Kristo sisi tuliokolewa. Mababu wote Kwenye Biblia na Manabii walipitia dhiki na Mateso, Hata mitume nao waliteseka


Sio mara zote Mateso na Shida maana yake ni kuachwa na Mungu au Kuadhibiwa na Mungu, mara nyingine mateso ni majaribu, kipimo cha Imani na njia ya kujivika Utakatifu.


Mungu anakupenda sana, mtumainie yeye. Yote yanapita lakini yeye atasimama milele.

Mungu na Akubariki na kukupa Faraja.
Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About