Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

JE, WAKATOLIKI WANABUDU SANAMU?

Mpenzi msomaji, kumekuwa na tuhuma nyingi dhidi ya wakatoliki kwamba wanaabudu sanamu. Je, tuhuma hizo zina ukweli gani? Hilo ndilo swali tunalotaka kujibu leo.
Amri ya kukataza ibada kwa sanamu imewekwa wazi katika Biblia Takatifu, Kutoka 20:4-5, “Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Sheria hiyo inapatikana pia katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:8-9: “Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Isivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Ni kutokana na vifungu hivyo vya Maandiko Matakatifu, Waamini wa Kikatoliki wamekuwa wakituhumiwa, kushtakiwa na kushambuliwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine kwamba wanapingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu, yanayokataza ibada kwa sanamu. Tuhuma hizo zinakuwa nzito zaidi, hasa zinapohusishwa na Ibada inayofanywa na Waamini Wakatoliki siku ya Ijumaa Kuu kila mwaka.

KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU

Mpenzi msomaji, kuna tofauti kubwa kati ya kuabudu na kuheshimu. Kamusi ya Kiswahili ya Maana na Matumizi, ya mwaka 1993, iliyoandikwa na SALIM K. BAKHRESSA, na kuchapishwa na OXFORD UNIVERSITY PRESS, DAR ES SALAAM, inaeleza kuwa neno “kuabudu” maana yake ni “kuomba au kufanya ibada”; na neno “kuheshimu” maana yake ni “kutukuza, kustahi au kuogopa.”
Katika maana yake ya ndani, anayeabudiwa na mwenye haki ya kuabudiwa ni Mungu peke yake. Hakuna mtu, kiumbe wala kitu chochote kinachopaswa kuabuduiwa na chenye haki ya kuabudiwa. Mtu, kiumbe au kitu hupewa heshima tu, tena ya kiwango maalum. Kwa mfano, Bikira Maria, kwa sababu ya nafasi yake katika kazi ya ukombozi, anapewa heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Watakatifu hao wengine hupewa heshima ya kadiri tu, chini ya heshima ile anayopewa Bikira Maria.

KWA NINI MUNGU PEKE YAKE ANASTAHILI KUABUDIWA?

Tumesema ni Mungu pekee yake, ndiye anayestahili kuabudiwa, kwa sababu ndiye MUUMBA wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana; ndiye anayevitawala na kuviongoza vitu vyote; ndiye mwenye uwezo juu yetu sisi wanadamu na viumbe vingine vyote; ndiye anayejua yote; ndiye aliye pote kwa ajili yetu; ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu; ndiye mkuu na Bwana wa wote.
Aidha, tunapomwabudu Mungu, tunakiri kwamba ndiye aliyetuumba na “ndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu na tuko!” (Mdo.17:28). Kwa kufahamu hilo, Wakatoliki hawawezi kumwabudu mtu, kiumbe au kitu chochote, isipokuwa Mungu tu.

MAMBO MAKUU NA MUHIMU KATIKA IBADA YA SANAMU

Ili kufahamu vema kinachofanywa na Wakatoliki ni vema kufuatilia na kutafakari yale wanayoyafundisha na kuyasadiki wao wenyewe, badala ya kuwahukumu kadiri watu wengine wanavyofikiri na kusema. Ukweli ni kwamba hakuna Ibada yoyote ya sanamu katika Kanisa Katoliki. Hilo ni dhahiri kwa sababu ili ibada ya sanamu iwe kweli kuabudu sanamu lazima yawepo mambo makuu na muhimu mawili: Kwanza, NIA KAMILI YA KUABUDU SANAMU INAYOHUSIKA;
Pili, KUWEPO NA IBADA YA DHATI YA KUABUDU SANAMU. Ikitazamwa kwa makini, hayo mambo mawili yanakosekana katika Kanisa Katoliki linapokuja suala la picha na sanamu. Kwa hiyo, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala picha. Kama ni hivyo, wakatoliki wanafanya nini na hizo sanamu au picha? Wanaziheshimu tu! Tukumbuke kuwa anayemwabudu mtu, kiumbe au kitu, ni sharti akihesabu na kukisadiki kuwa ndicho kinachomwezesha kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake (Rej. Mdo.17:28).

JE, BINADAMU TUNAHITAJI SANAMU AU PICHA?

NDIYO. Binadamu tunahitaji sananmu au picha, tena ni jadi yetu! Kwa sababu gani tunahitaji picha maishani mwetu? Kwa sababu katika udhaifu wetu, mara nyingi tunaweza kufikiri vema kwa kutumia vielelezo au vichokoo vyenye kuonekana na kugusika. Kwa njia ya vielelezo hivyo, binadamu tunaweza kuyafikia kwa urahisi mambo magumu na mafumbo yaliyo juu ya fikra zetu za kawaida. Ndiyo maana tukiona picha au sanamu ya Yesu au Mama Maria au Watakatifu wengine, akili zetu zinaweza kutafakari mambo matakatifu na kupata picha ya kina cha msamaha wa dhambi na mapendo ya Mungu kwetu wanadamu.

KWA NINI WAKATOLIKI HAWAABUDU SANAMU AU PICHA?

Wakatolikihawaabudu sanamu kwa sababu wanajua kwamba Mungu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa. Kwa hiyo, hawaziabudu sanamu au picha kwa sababu wanajua kwamba hivyo siyo Mungu. Zaidi hayo, wanajua kwamba Mungu mwenyewe amekataza kuziabudu sanamu na picha kwani hazina daraja la Muumba. Mungu amepiga marufuku kuzigeukia na kuzisujudia (Law.19:4). Aidha, wameaswa kuziepuka sanamu na Ibada kwa sanamu – “Watoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu!” (1Yoh.5:21). Pia wakatoliki wanajua kuwa sanamu na picha hazina uwezo wowote wa kimungu. “Mungu wetu yuko mbinguni, hufanya yote anayotaka. Miungu yao ni fedha na dhahabu; imetengenezwa na mikono ya wanadamu. Ina vinywa lakini haisemi. Ina macho lakini haioni. Ina masikio lakini haisikii. Ina pua lakini hainusi. … Wote wanaoitengeneza wanafanana nayo, kadhalika na wote wanaoitumainia. Enyi wa nyumba ya Israeli mtumainieni Mwenyezi Mungu, yeye ndiye msaada wenu na ngao yenu” (Zab.115:3-9). Pia kuziabudu sanamu ni jambo la kidunia, ambalo haliwezi kumpeleka mtu peponi (Rej. Isa.45:16; Isa.45:20; Gal.5:20). Kwa hiyo, Wakatoliki wanajua kuwa kuabudu sananmu na picha ni jambo haramu kabisa mbele ya Mungu, Mwumba wao (1Pet.4:3-4).

IBADA YA KWELI YA SANAMU INAKUWAJE?

Ibada ya kweli ya sanamu siyo rahisi hivyo, kama baadhi ya watu wanavyodhani! Ibada ya kweli ya sanamu siyo kitu cha mchezomchezo, kama baadhi ya watu wanavyofikiri na kusema. Ibada ya Sanamu ni suala la kuabudu, na kuabudu siyo suala la kuwa na kitu au kikiheshimu tu, bali ni kwenda mbali zaidi ya hapo! Hivyo kumiliki sanamu au picha, mathalani majumbani au kanisani, hakusemi lolote juu ya uwepo wa ibada ya sanamu kwa wale wanaohusika nazo. Kwa hiyo, ikiwa watu hawazipi sanamu au picha hizo mahali pa Mungu wa kweli, basi hawana hatia yoyote.
Jambo muhimu hapa ni kwamba wamiliki wa sanamu au picha hizo wanaziheshimu tu huku wakijua kuwa wenyewe wanaowakilishwa na sanamu au picha hizo hawapo pale kwa hali halisi. Katika maana hiyo, inakuwa sahihi kabisa kuziheshimu picha za marais, ndugu na marafiki wetu tunaowapenda, ambao hawapo karibu nasi. Picha zao hatuzikejeli wala hatuzibwagi chini na kuzikanyaga au kuzitia vumbi. Hatufanyi hivyo, siyo kwa sababu tunawaabudu watu hao au vitu hivyo, bali kwa sababu tunawapenda na kuwathamini wenyewe katika hali zao halisi.
Kwa mfano ikiwa tuna kitabu cha picha (Album) chumbani, chenye picha 100 za ndugu, rafiki na jamaa zetu, hatusemi tuna miungu 100 tunaowaabudu nyumbani mwetu! Vinginevyo, mambo yangetisha sana majumbani mwetu! Wenye picha hizo hatuwaabudu kamwe, ila tunawapa heshima tu kwa sababu tunawajali na kuwapenda. Kwa nini tusiwape heshima hiyo, ambayo ni kitu cha bure! Ukweli huo pia unahusu Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, nk.

JE, MUNGU ANACHUKIA KILA SANAMU NA PICHA?

Mungu hachukii kila sanamu au picha. Hapa inafaa ieleweke vema kwamba Mungu alipopiga marufuku sanamu katika Kitabu cha Kut. 20:3-5 na Kumb. 5:7-10, hakupiga marufuku kila sanamu. Yeye mwenyewe anaonesha kwamba anazichukia sanamu zinazotengenezwa kusudi zichukue nafasi yake tu. Kama sanamu au picha hazihatarishi nafasi yake, hana maneno nazo! Ndiyo maana, basi, baada ya kumwagiza MUSA awaambie watu wasizitengeneze sanamu na kuziabudu kama miungu (Kut.20:4-5), alimwagiza MUSA huyo huyo azitengeneze sanamu zisizokuwa hatari, ambazo hazikupewa daraja la Mungu. Mungu alimwagiza MUSA kutengeneza sanamu katika nafasi mbili:
(i) Musa anaagizwa atengeneze sanamu mbili za Makerubi azibandike kwenye Sanduku la Agano wakifunike kiti chake cha rehema. “Utatengeneza pia mfano wa viumbe hai viwili kwa kufua dhahabu, uwaweke kwenye miisho miwili ya kiti hicho; kiumbe kimoja mwisho mmoja na kiumbe mwingine mwisho mwingine. Waweke viumbe hao kwenye miisho ya hicho kiti, lakini wawe kitu kimoja na hicho kiti. Viumbe hao wataelekeana, mabawa yao yamekunjuka kukifunika kiti cha rehema, nyuso zao zitakielekea kiti hicho” (Kut.25:18-20; Rejea pia Ebr.9:5).
(ii) Mungu alimwagiza pia Musa atengeneze Nyoka wa Shaba kama dawa kwa wale ambao waling’atwa na nyoka wa moto kule Jangwani. Musa alielezwa wazi kwamba wale ambao wangemtazama huyo nyoka wa shaba kwa imani kwa Mungu wa Israeli wangepona. “Ndipo naye Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: Tengeneza Nyoka wa shaba, umtundike juu ya mlingoti. Mtu yeyote atakayeumwa na nyoka, akimtazama nyoka huyo wa shaba, atapona. Basi, Musa akatengeneza nyoka wa shaba, akamtundika juu ya mlingoti. Kila mtu aliyeumwa na nyoka alipomtazama huyo nyoka wa shaba, alipona” (Hes. 21:8-9; Rejea pia Yoh.3:14-15).
Basi, Musa alitekeleza maagizo hayo ya Mwenyezi Mungu, naye alifurahia. Kwa maagizo hayo mawili ni dhahiri kwamba Mungu hachukii kila sanamu au picha. Mungu anachukizwa na sanamu zile ambazo zimekusudiwa kuchukua daraja la umungu wake, maana ni yeye tu ndiye anayestahili kuabudiwa. Yule nyoka wa shaba alikuwa dawa kwa wale walioumwa na nyoka wa moto. Watu hao hawakumwabudu nyoka wa shaba, lakini walipona, siyo kwa sababu ya nguvu zake, ila kwa nguvu za mwokozi zilizokuwa nyuma yake. “Kama mtu akiitazama alama hiyo aliponywa, lakini kilichomponya siyo hicho kitu alichokiona, bali wewe uliye Mwokozi wa watu wote” (Hek.16:7).
Hapa ni vifungu vingine vya Maandiko Matakarifu, vinavyoonesha kuwa Mungu hachukii kila sanamu au picha.
1Fal. 7:29 “kulikuwa na sanamu za simba, mafahali na viumbe vyenye mabawa. Sanamu hizo za simba na mafahali zilikuwa, zimefunikwa na kutandikwa mapambo yaliyosokotwa vizuri”.
2Nyak.3:10 “Alitengeneza sanamu mbili za viumbe wenye mabawa kwa mbao, akazifunika kwa dhahabu na kuziweka mahali patakatifu sana”
Ezek.41:17-18 “… kwenye ukumbi palikuwepo na michoro iliyofanana na mitende na picha za viumbe vyenye mabawa. Kila baada ya mtende kulichorwa picha ya kiumbe chenye mabawa kukizunguka chumba chote”.
Yoh. 3:14-15 “Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka wa shaba kule Jangwani, naye Mwana wa mtu atainuiliwa juu vivyo hivyo, ili kila anayemwamini awe na uhai wa milele.”
Ebr.9:5 “Juu ya hilo sanduku kulikuwa na viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi huondolewa”

UBAYA WA SANAMU AU PICHA UKO WAPI?

Ubaya wa sanamu au picha upo katika kuzipa sanamu au picha daraja la Mungu. Hatari na ubaya wa sanamu au picha vimo katika kitendo cha binadamu kuzipa sanamu au picha hizo daraja la Mwenyezi Mungu. Kama sanamu au picha hazipewi daraja la Mungu, haziwi hatari na wala hazina ubaya wowote mbele ya Mungu. Kwa sababu hiyo, basi, mtu anaweza kuwa na sanamu au picha ndani ya nyumba yake au kanisani, lakini bila kumkasirisha Mungu.
Zaidi ya hayo, Mungu mwenyewe anajua fika kuwa sanamu au picha fulani imepewa daraja lake au siyo. Kwa nini Mungu akasirike pale ambapo sanamu au picha haziingilii daraja na ukuu wake? Mungu mjinga wa aina hiyo hayupo! Mungu wa kweli hawezi kukasirikia picha na sanamu ambazo zinaheshimiwa tu, na wala haziabudiwi. Aidha, Mungu mwenye haki hawezi kumwadhibu na kumtupa Jehanamu mtu ambaye anamiliki picha au sanamu duniani lakini bila kuziabudu, yaani pasipo kuzipa daraja la Mungu.

BIBLIA INAWEZA KUTUSAIDIA KUIELEWA IBADA YA SANAMU?

Jibu ni ndiyo! Biblia inatoa maelezo ya kina na ufafanuzi mzuri juu ya ibada ya sanamu. Tumesema hapo juu kuwa ibada ya sanamu siyo jambo la mzaha au mchezo wa kitoto! Ni suala la kuabudu, na kuabudu siyo tu jambo la kuwa na sanamu au picha na kuiheshimu tu. Ni zaidi ya hapo! Kuna mambo muhimu ambayo lazima sanamu zitendewe, ndipo ihesabike kuwa ni ibada ya sanamu.
a) Tukitaka kujua kama kitendo fulani mbele ya sanamu ni kuabudu au sivyo, kwanza lazima iwepo nia thabiti ya mtu anayehusika katika kitendo hicho kinachofanyika. Ibada inakuwa ya kuabudu sanamu ikiwa mtu anayefanya kitendo hicho anaamini moyoni mwake kwamba hiyo sanamu au picha inayofanyiwa kitendo hicho inachukua daraja na nafasi ya Mwenyezi Mungu. Katika kitendo hicho, mtu anaamini kuwa sanamu au picha hiyo ndiyo inayomwezesha kwenda, kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake hapa duniani.
b) Jambo la pili ni kuangalia kama kitendo hicho kinachofanyika katika ibada hiyo ni Liturujia ya kueleweka/maalum. Baada ya kubaini nia thabiti ya mtendaji, tunaweza kuitambua ibada ya sanamu kwa kuangalia yale yanayofanyika mbele ya sanamu au picha kwa kufuatilia mambo ambayo waabudu sanamu huyafanya. Mambo hayo, ambayo waabudu sanamu wanayafanya tunaweza kuyakusanya kutoka katika Biblia yetu. Agano la Kale linaonesha kuwa Ibada ya Kuabudu Sanamu inajumuisha mambo makuu yafuatayo:
i. Kuzitolea sadaka: za kuteketezwa: Rej. Hos.4:13; nafaka na vyakula 2Fal.5:17.
ii. Kuzitolea ubani kwa heshima kamili: Rej. 1Fal.11:8; Isa. 57:6; Yer.7:18.
iii. Kuzimwagia matambiko: Rejea Isa. 57:6
iv. Kuzitolea zaka ya sehemu ya kumi ya mapato ya mwaka ya mazao ya mashambani: Rejea Hosea 2:8
v. Kuziandika meza mbele yao: Rejea Isa. 65:11
vi. Kuzibusu sanamu kwa kuzisujudia kama viumbe vyenye enzi.
Rejea 1Fal. 19:18; Hos.13:2; Ayu. 31:2.
vii. Kuziinulia sanamu mikono katika kuzisujudia: Rejea Isa.44:20
viii. Kuziangukia sanamu kifudifudi ama kuzipigia magoti kwa kuziabudu: Rejea 1Fal.18:26,28.
ix. Kuzichezea ngoma na wakati mwingine kujikatakata kwa visu kama kitendo cha ibada kwa sanamu: Rejea 1Fal.18:26,28.
Hayo yote yakichunguzwa kwa makini, tutaona wazi kuwa hakuna Ibada ya kuabudu sanamu katika Kanisa Katoliki. Kwa hiyo, shutuma kwamba Wakatoliki wanaabudu sanamu siyo za kweli, hazina msingi, na ni uchochezi wa bure wenye lengo la kuleta mafarakano na magomvi. Jambo hilo ni dhahiri kwa sababu Wakatoliki hawana nia thabiti ya kuabudu sanamu wanapotoa heshima kwa sanamu au picha mbalimbali. Pili, matendo ya kiliturujia yanayofanywa na wakatoliki katika kuheshimu sanamu hayalingani na matendo ya kiliturujia yanayofanywa na waabudu sanamu, kama ilivyoelezwa katika Biblia Takatifu, hususan Agano la Kale. Kifupi, wakatoliki hawana nia thabiti moyoni ya kuziabudu sanamu au picha, tena hawazifanyii liturujia yoyote sanamu au picha walizo nazo majumbani au makanisani.
Ni wapi ambapo Kanisa Katoliki linafanya au kuwafundisha rasmi na kuwahimiza wafuasi wake wafanye matendo hayo tisa ya kiliturujia kwa ajili ya kuabudu sanamu? Hakuna! Kwa hiyo, Wakatoliki hawana hatia yoyote ya kuabudu sanamu mbele ya Mungu. Kama mtu mmoja akifanya hivyo, hilo ni shauri lake binafsi, siyo shauri au utaratibu wa Kanisa lote. Aidha, afanyaye hivyo amepotoka peke yake, kwa sababu hajafundishwa na Kanisa Katoliki afanye hivyo. Hilo ni kweli kwa sababu mambo binafsi, siyo mambo rasmi ya Kanisa lote!
Kwa hiyo, tunaona wazi kwamba Wakatoliki hawaabudu sanamu kamwe, kama inavyodaiwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine ya kikristo. Wanaotoa shutuma hizo inafaa wajiangalie kwanza wao wenyewe, maana imeandikwa: “… mtu akidhani kwamba kitu fulani ni najisi, basi, kwake huwa najisi” (Rom.14:14).

JE, IJUMAA KUU WAKATOLIKI WANAABUDU NINI?

Je, ni kweli kwamba Siku ya IJUMAA KUU Wakatoliki wanaabudu Sanamu au Mti wa Msalaba? HAPANA! WANAMWABUDU WOKOVU-YESU! Kiini cha utata hapa ni “NINI MAANA YA IBADA YA KUABUDU MSALABA” inayoendeshwa siku ya Ijumaa Kuu? Madhehebu hayo yanayofanywa na Wakatoliki Siku ya IJUMAA KUU siyo Ibada ya Kuabudu Sanamu. Labda hapa ni tatizo la lugha au maneno yanayotumika, ndiyo yanayowachanganya watu! Hilo ni kweli kwa sababu jina la madhehebu yenyewe halisemi wazi kitu gani hasa kinanuiwa kufanywa katika ibada hiyo.
Wengi hawajui nini hasa kinanuiwa kufanyika siku ya Ijumaa Kuu katika “Ibada ya Kuabudu Msalaba” – jina ambalo nimesema halitoi picha halisi ya jambo linalokusudiwa kufanyika. Mtu mwenye akili timamu akijua kitu halisi kinachofanyika siku ya Ijumaa Kuu, hawezi kusema madhehebu hayo ni Ibada ya Sanamu au kuabudu mti. Tatizo hapo ni lugha tu inayotumika katika kuieleza ibada hiyo. Labda jina hilo lichunguzwe upya na wataalamu wetu katika Kanisa na ikiwezekana kulirekebisha ili kuondoa utata kwa baadhi ya watu wenye uelewa mdogo, wenye wanaokwazwa nalo!

NINI HASA KINAFANYIKA SIKU YA IJUMAA KUU?

Wanachofanya Wakatoliki Siku ya Ijumaa Kuu ni KUUHESHIMU MTI WA MSALABA na KUMWABUDU WOKOVU. WOKOVU ni nani? WOKOVU NI YESU KRSITO BWANA WETU. Basi, kinachofanyika siku ya Ijumaa Kuu ni kumwabudu WOKOVU yaani YESU KRISTO, ambaye alitundikwa msalabani. Hivyo ndivyo anavyotangaza Kiongozi wa Ibada hiyo ya Ijumaa Kuu, pale anapotoa mwaliko kwa waamini mara tatu, ili kila muumini ausikie na kuelewa vema: “HUU NDIO MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA DUNIA UMETUNDIKWA JUU YAKE, NJOONI TUUABUDU.” Waamini wanaalikwa kiimani kuuabudu WOKOVU, na hilo ndilo linalofanyika, yaani kuuabudu WOKOVU – YESU KRISTO. Waamini wote wanaalikwa kujongea mbele kwa imani kwenda kumwabudu YESU. Watu wanamwabudu YESU kwa sababu WOKOVU maana yake ni YESU.
Jina YESU ambalo linatokana na Kiebrabia “YESHUA”, maana yake “WOKOVU” (Rej. Mt.1:21;1:25; Lk.1:31). Ikiwa wokovu ni YESU, basi Ijumaa Kuu Wakatoliki hawaabudu sanamu au mti, bali wanamwabudu YESU KRISTO. Kwa sababu hiyo, yote yanayofanyika Siku ya Ijumaa Kuu, yanafanyika kihalali na kwa haki kwa sababu YESU KRISTO, ambaye ni WOKOVU ni MUNGU, na MUNGU peke yake ndiye mwenye haki na anayepaswa kuabudiwa. Ikiwa mkristo hataki kumwabudu YESU KRISTO, aliye Mwana wa Mungu na Mungu kamili, na ambaye ameeleta wokovu, anafanya makosa makubwa!
Basi, nasisitiza kuwa Siku ya Ijumaa Kuu, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala mti. Wanamwabudu WOKOVU, yaani YESU KRISTO, Nafsi ya Pili ya MUNGU. Kutomwabudu YESU KRISTO ni sawa na kumkana Mungu, kukana wokovu ulioletwa naye. Basi, tujiepushe na ukanaji Mungu wa aina hiyo. Nawaalika wote Siku ya Ijumaa Kuu tufungue mioyo yetu kwa imani kubwa ili tumwone WOKOVU aliyetundikwa msalabani, apate kuukomboa ulimwengu. Kwa imani, wote tumsujudie YESU ili apate kutukumbuka katika Ufalme wake wa milele.
Hatimaye, niseme kwamba ingawa Mungu ametoa amri ya kukataza sanamu na picha (Kut. 20:4-5; Kumb. 5:6-10), lakini hachukizwi na kila sanamu au picha. Sanamu na picha ambazo hazipewi daraja la Mungu, Yeye hazichukii, kwa sababu hazichukui nafasi yake kama Muumba. Basi, Wakatoliki hawaendi kinyume na Biblia kwa kuziheshimu sanamu na picha zilizoko kwenye majumba yao na makanisani.

Madhara ya kutumia dawa bila ushauri wa Dakitari

Mara nyingi watu wanaugua maradhi mbalimbali, lakini wengi wao hawapendi kwenda hospitali kufanya vipimo au kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari. Kutokana na uwepo wa maduka ya dawa baridi, watu wengi wanapojisikia kuwa wagonjwa, hununua dawa kwenye maduka hayo na kuanza kuzitumia.

Ni ukweli usiopingika kuwa dawa zimetengenezwa ili kutibu maradhi fulani ambayo yatabainika kwa mgonjwa baada ya uchunguzi wa kitaalamu.

Hivyo matumizi ya dawa bila kufanya uchunguzi wa kitaalamu yanaweza kuwa na madhara makubwa kwenye afya yako

Yafuatayo ni madhara yatokanayo na kutumia dawa bila ushauri wa dactari:

1. Huweza kusababbisha kifo.

Kama nilivyoeleza kwenye hoja zilizotangulia, dawa ni sumu zinazokabili vimelea vya magonjwa. Hivyo kutumia dawa vibaya kunaweza kusababisha kifo.

Ikumbukwe pia watu wenye matatizo maalumu kama vile maradhi ya moyo pamoja na shinikizo la damu, wanapaswa kuwa makini na dawa wanazozitumia kwani zinaweza kuchochea matatizo yao na hatimaye kifo

2. Huweza kusababisha saratani.

Dawa zinapoingia mwilini mwako kimakosa na kushindwa kufanya kazi yake, zinaweza kuharibu baadhi ya seli za mwili na kuzifanya kugeuka seli za saratani. Hivyo hakikisha dawa unayoitumia ni sahihi na inalenga ugonjwa husika.

3. Husababisha usugu wa maradhi

Mtaalamu wa afya hukupa kiwango (dosage) cha dawa kulingana na vipimo alivyovifanya; hivyo kutumia dawa bila vipimo vya kitaalamu kunaweza kusababisha vimelea vya ugonjwa vizoee dawa husika na kusababisha ugonjwa huo usitibike tena.

Hili ndilo linalosababisha maradhi kama vile malaria sugu au UTI sugu. Hivyo kabla ya kutumia dawa ni vyema ukafanya uchunguzi wa kitaalamu

4. Husababisha tatizo la mzio. Allegy.

Kuna watu wenye tatizo la mzio au wengi huita “aleji” kwa lugha isiyo sanifu, watu hawa wanapaswa kuwa makini na kuepuka kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu.

Hili ni kutokana na baadhi ya dawa kutokuendana na afya zao, hivyo kusababisha tatizo lao la mzio kuibuka. Ni vyema ukamwona mtaalamu wa afya na umweleze aina ya mzio uliyo nayo ili akupe dawa stahiki.

5. Huongeza sumu mwilini.

Dawa zimetengenezwa kwa kutumia kemikali mbalimbali ambazo kimsingi ni sumu zinazoua vimelea vya magonjwa.

Hivyo kutumia dawa bila vipimo kunakusababishia kuongeza sumu za dawa hizo mwilini mwako kwani umetumia dawa ambazo mwili hauzihitaji kukabili ugonjwa husika.

Sumu hizi zinapokusanyika mwilini mwako zinaweza kukuletea athari mbalimbali za muda mfupi au hata mrefu.

Ni muhimu ukumbuke kuwa dalili za ugonjwa mmoja zinaweza kuwa dalili za ugonjwa mwingine pia. Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi pamoja na kutafuta ushauri wa kitabibu kabla ya kutumia dawa zozote kutibu maradhi yanayokukabili.

Vyakula vinavyosaidia macho kuongeza uwezo wa kuona

Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.

Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.

Mboga za majani

Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.

Mayai

Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).

Samaki

Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.

Matunda jamii ya mchungwa na zabibu

Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.

Karanga na jamii zake

Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.

Vyakula vya jamii ya kunde

Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.

Alizeti

Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.

Matunda ya rangirangi

Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.

Nyama ya ng’ombe

Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.

Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.

Zawadi ya Kipekee kwa Mtu Ambayo Inadumu Milele

Kuna Zawadi moja ya Kipekee ya kumpa mtu ambayo ni Kusali na Kuomwombea Mtu aweze kuingia Mbinguni. Je, ulishawahi kutoa zawadi hii hasa kwa wale unaowapenda? Kila kitu kitabaki hapa duniani na kitapita na kusahauliwa lakini hili halina mwisho

Zawadi ya Kipekee: Kusali na Kuombea Wapendwa Wetu

Kuna zawadi moja ya kipekee ambayo unaweza kumpa mtu, nayo ni kusali na kumuombea ili aweze kuingia Mbinguni. Katika maisha haya ya kidunia, mara nyingi tunatafuta zawadi za kuwafurahisha wapendwa wetu, lakini zawadi ya sala ina thamani kubwa kuliko zawadi yoyote ya kidunia. Je, ulishawahi kutoa zawadi hii hasa kwa wale unaowapenda?

Thamani ya Zawadi ya Sala

Kusali na kumuombea mtu ni tendo la upendo wa kweli. Ni njia ya kuonyesha kwamba unajali sana kuhusu hali ya kiroho ya mtu huyo na unataka kumwona akifurahia maisha ya milele. Sala ni mazungumzo na Mungu, na kwa kuomba kwa ajili ya wengine, tunawaweka mikononi mwa Mungu mwenye uwezo wote. Biblia inatufundisha umuhimu wa kuombeana.

“Basi, aombeeni hivyo na kusema, Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.” (Mathayo 6:9)
“Kwa sababu hii tena, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kuomba kwa ajili yenu, na kusiomba kwamba mjazwe na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho.” (Wakolosai 1:9)
“Sasa basi, waombeeni kila siku ili wasimame imara katika imani yao.” (Waebrania 13:18)

Kila Kitu Kitabaki Hapa Duniani

Katika maisha haya, tunaweza kumiliki vitu vingi: nyumba, magari, fedha, na mali nyingine nyingi. Hata hivyo, kila kitu kitabaki hapa duniani na kitabakia kuwa mali isiyo na thamani tunapovuka kwenda kwenye maisha ya milele. Mali ya kidunia inapitiliza na kusahaulika, lakini zawadi ya sala inaendelea hata baada ya kifo.

“Hatujaingia na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu.” (1 Timotheo 6:7)
“Usiweke hazina zenu duniani, ambako nondo na kutu vinaharibu, na wevi huvunja na kuiba; bali wekeni hazina zenu mbinguni, ambako hakuna nondo wala kutu viiharibuyo, na wevi hawavunji wala kuiba.” (Mathayo 6:19-20)
“Mna haja moja, nayo ni hii; utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa.” (Mathayo 6:33)

Zawadi ya Sala Haina Mwisho

Sala ni zawadi ya kudumu. Inapotolewa kwa nia safi, inaweza kubadilisha maisha ya mtu na kumwongoza kwenye njia ya wokovu. Kwa kumwombea mtu, tunasaidia roho yake kupata nafasi ya kumkaribia Mungu na kuishi maisha matakatifu. Hii ni zawadi ambayo haitaisha au kupotea, bali itaendelea kuwa na athari milele.

“Naomba kwa ajili yao. Siombi kwa ajili ya ulimwengu, bali kwa ajili ya wale ulionipa, kwa maana wao ni wako.” (Yohana 17:9)
“Kwa hiyo, ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” (Yakobo 5:16)
“Basi nakuomba, kama ambavyo hujaacha kumwombea Mtakatifu huyo; unapoomba usife moyo, bali uongeze juhudi.” (Wakolosai 4:12)

Hitimisho

Je, ulishawahi kutoa zawadi hii kwa wale unaowapenda? Kusali na kuwaombea wapendwa wako ni tendo la upendo na kujali ambalo lina thamani kubwa sana kuliko zawadi yoyote ya kidunia. Kila kitu kingine kitabaki hapa duniani na kitapita na kusahauliwa, lakini zawadi ya sala ina athari za milele. Kwa kumwombea mtu, unampa nafasi ya kuingia Mbinguni, na hiyo ni zawadi ya pekee zaidi unayoweza kumpa mtu yeyote.

Kila wakati unapomwomba Mungu kwa ajili ya wapendwa wako, kumbuka kwamba unawawekea hazina mbinguni, ambako hazina hizo hazitaharibika kamwe. Ni tendo lenye upendo na lenye kuleta baraka zisizo na mwisho.

“Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwana wake pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16)
“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.” (Mathayo 7:7)
“Na imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” (Waebrania 11:1)

Madhara ya kunywa maji baridi na faida za kunywa maji moto na asali

UNYWAJI wa maji baridi, hasa katika joto kali kama la Dar es Salaam, ni kiburudisho kikubwa cha koo na huleta faraja kubwa mwilini. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu kuhitaji kunywa maji hayo mara baada ya kula mlo, iwe mchana au usiku.

MADHARA YA KUNYWA MAJI BARIDI

Pamoja na ukweli kwamba maji baridi ni;matamu’, lakini siyo mazuri kwa afya yako na katika makala ya leo tutaangalia ukweli kwa nini maji haya siyo mazuri.

Kwa mujibu wa utafiti uliokwisha fanywa na wataalamu wetu wa masuala ya lishe, mtu anapokunywa maji baridi mara baada ya kula chakula, maji yale yanapopita kwenye utumbo huchangia kugandisha mafuta yaliyomo kwenye chakula.

Kitendo hicho, husababisha usagaji wa chakula kuwa wa taratibu sana na hivyo kuchangia ukosefu wa choo. Mbali na ukosefu wa choo, ambao ni madhara yanayojionesha kwa muda mfupi, lakini pia kuna madhara ya muda mrefu yanayoweza kujitokeza baadaye sana.

Inaelezwa zaidi kuwa, wakati chakula kinapochelewa kusagwa kwa sababu ya kuganda kulikosababishwa na maji baridi, chakula hicho hukutana na ;acid’ iliyoko tumboni ambayo huanza kuyayusha mafuta hayo haraka na kufyonzwa na utumbo kabla ya chakula chenyewe.

Hali hii inapoendelea kwa muda mrefu, tabaka la mafuta (fats) hujijenga kwenye utumbo na baadaye huweza kusababisha saratani ya utumbo. Hali kadhalika, huweza kuwa chanzo kingine cha ugonjwa wa moyo ambao madhara yake ni pamoja na kupatwa na Kiharusi na hatimaye kifo.

Ili kuepuka hatari hii, unachotakiwa kufanya ni kuacha tabia ya kunywa maji baridi na badala yake pendelea kunywa maji ya uvugu-vugu mara baada ya kula chakula. Vile vile zingatia ushauri wa kukaa kwa muda usiopungua nusu saa ndiyo unywe maji.

MAJI MOTO NA ASALI KAMA DAWA

Kujiweka katika mazingira mazuri ya kuhakikisha unasafisha tumbo lako kila siku kabla ya kulala, weka utatartibu wa kunywa maji moto kiasi, yaliyochanganywa na asali.

Chemsha maji moto au chukua maji moto yaliyopo kwenye chupa ya chai, acha yapoe kidogo na kuwa ya uvuguvugu, kisha weka kijiko kimoja cha asali mbichi kunywa kisha lala. Kunywa maji hayo nusu saa au zaidi baada ya kula chakula cha mwisho.

Kitendo hicho kitakuwezesha kuyeyusha mafuta, kusadia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kukuwezesha kutoa uchafu na sumu mwilini kwa njia ya haja kubwa. Kwa utaratibu huu, hutakaa na uchafu tumboni wala mrundikano wa mafuta mabaya mwilini.

Ni jambo lisilo shaka kuwa iwapo kila mmoja wetu atazingatia kanuni za ulaji na unywaji sahihi, bila shaka matatizo ya moyo na shinikizo la damu yanaweza kupungua kwa kiwango kikubwa, kama siyo kutoweka kabisa.

Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana

1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda. Soma sana utafanikiwa…

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa. Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.

3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora

4. Jifunze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja. Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali

6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.

7. Weka falsafa yako katika maisha na uiishi. Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mfano unataka kumiliki nini katika maisha? Unataka mke au mume wa aina gani? Aina gani ya maisha unaipenda? Hiyo ndiyo falsafa…

8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. (Kwa wale wa ndoa) Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi, kijana au binti wa moyo wako, mpende… Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..

9. Kuwa na marafiki imara, jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta kwaa urafiki m’baya uliowapoteza… a

10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu. Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako, usimsahau Mungu. Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.

11. Jitume katika kazi, watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma. Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona

12. Zingatia kujiweka safi. Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo, muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..

13. Kula kwa afya, wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba, ila ukila kwa afya, ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..

14. Vaa kwa heshima, usivae kama mcheza disko au teja. Kumbuka thamani yako kwa Mungu. Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo? Vaa kwa heshima..

15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze! Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi. Penda kusafiri, tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.

16. Kumbuka kupumzisha mwili. Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika. Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..

17. Jifunze kuamua mwenyewe. Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue. Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yako mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi. Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.

18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri. Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.

19. Jfunze na zitawale hisia zako. Hisia ziwe za hasira, mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo…

20. Jitolee kwaajili ya wengine, fundisha kemea saidia. Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk. Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji. Wewe ni yatima, mzee, au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema

21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri. Usijione mzuri au HB sana ukadharau wengine. Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wanakuchukia..

22. Tunza muda, muda ni mali huwezi kuurudisha, kuusimamisha au kuuzuia. Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..

23. Pendelea kusoma hasa vitabu vya dini, kuhusu mali, elimu, mchumba, afya, maisha, uongozi, hekima, busara, utu, uchaji, utii, maarifa, utajiri, heshima, uvumilivu, matumaini, upendo, na kila kitu vimo katika Biblia na Qur’an ..soma uchote hekimaa…

24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache, kama unajifunza acha na kama kuna mtu anakushawishi kataa. Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya…

Inafaa ukishare kwa wengine wajifunze maarifa haya..
*Maisha ni maamuzi yako wewe*
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..

Hapo sasa patamu, cheki jamaa alivyowezwa na huyu dogo

Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia:

Mkulima: Baba yako yupo?

Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini.

Mkulima: Mama yako?

Mtoto: Nae kaenda mjini na baba.

Mkulima: Kaka yako Howard yupo?

Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa.
Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu.

Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng’ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba.

MADHARA YA SHISHA

Yafuatayo ni madhara ya shisha;

1.Kansa
Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu.

2.Matatizo ya Moyo
Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba, Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake.

3.Huharibu Fizi (periodontal disease)
Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya meno.

4. Fangasi na Kifua kikuu (TB)
Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha (hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria.

5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo)
Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji.

6. “Nicotine Addiction”
Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila kutumia shisha au sigara.

7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana.
Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa nguvu za kiume.

8.Kuchakaa kwa ngozi.
Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia.

9.Asthma na Allergy Zingine
Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma.

10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!

Je, Kuangalia Picha za Ngono ni dhambi?

Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
“Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya “AIBU” wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni.
Wanaume wamejikuta wakipiga punyeto (Mastubation) na Wanawake wakijisaga ( wanatumia mikono yao na viungo vyao vingine kama njia ya kujikidhi hali zao za tamaa mbaya waliloziamsha wao wenyewe). Haipaswi kamwe kuwa hivyo. Biblia inasema tusiyachochee wala kuyaamsha “mapenzi” mpaka yatakavyoona yenyewe (Wimbo ulio bora 2:7, 3:5). Naomba tufuatane pamoja kwenye somo hili muhimu sana ambalo litakuweka huru mbali na “utumwa wa fikra za kingono”

1. MAANA YA PICHA ZA NGONO

Neno PICHA ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. PICHA si kitu halisi bali ni kivuli chake. Unaweza ukapewa PICHA ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako. NGONO ni kitendo cha mtu, watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama. Kuangalia picha za ngono ni kitendo cha kuangalia watu wakifanya Matendo ya kujamiana iwe kwa njia ya asili, kinyume na maumbile au kufanya na wanayama. Kitendo hicho huleta kuchochea tamaa ya miili kiasi ambacho watu wengine hufanya mambo ya “AIBU” katika nyumba zao (Warumi 1:24-28). PICHA za NGONO zimeenea kila mahali kwa sasa, kwenye simu yako unaweza ukakutana na “uchafu” wa namna hiyo. Wahindi wao picha za ngono huziita “kachumbali” na unaweza ukamkuta Mhindi amekaa na familia yake anaangalia “kachumbali” wanadai inanogesha utamu wanapofika kitandani. Huko ni kujidanganya Mungu hakumletea Adamu PICHA ya NGONO bali alimletea mke ambaye watashirikiana naye kwenye Tendo Takatifu (Mwanzo 2:18, 21-25). Wakati mmoja Mfalme Daudi wakati watu wake wa vita wamekwenda vitani yeye akawa yuko ghorofani anaangalia “PICHA LIVE” ya NGONO mwanamke alikuwa akioga matokeo yake yakawa ni kufanya kitendo chenyewe na kuamua kumuua mume wa Bathsheba (2Samweli 11:2-27).
“Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?”………..
Kile kitendo cha Daudi “kuona” lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya. Ndivyo ilivyo kwa PICHA ZA NGONO lazima ukiangalia upate “UKICHAA” wa muda ukajikuta umeng’ang’ania sabuni au ndizi ukiwa unapiga punyeto. Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako kama wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika sabuni, godoro au toy la jinsia ya kiume.

2. JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI?

Kuangalia picha za ngono “NI DHAMBI” kwa herufi kubwa. Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika. Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha “kutamani” tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28). Tamaa mbaya ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16). Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha “FIKRA” nzuri za mtu alizonazo. Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi “USHUSHE” huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee. Wewe unayengalia picha za ngono Kama ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako “unakuwa zezeta wa akili” Biblia inasema “taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza..”(Mathayo 6:22-23). Kwa wale wanandoa ni “MWIKO” kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa. Wewe mume unaye hapo “chombo” unakiona “live” na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum kama ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako. Mungu ameweka sehemu ya “haja kubwa” kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga “zege” hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).
Warumi 1:26:27
“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”

3. JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako. Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi. Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue. Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)

USHAURI WAKIVITENDO:

I) Yatie Nuru macho yako – Zaburi 13:3, 19:8 – Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu. Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.
II) Tazama mambo ya Adili(mema) – Zaburi 17:2-3 – Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema. Vipindi vizuri vya neno la Mungu. PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.
III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako – Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.
IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako – Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.
V) Macho yako yatazame Mbele – Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono. Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako. Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema “anaona ufito wa mlozi” anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).
VI) Pendezwa na njia za Mungu – Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako. Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.
VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe – Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.
VIII) Omba rehema na neema ya Yesu – Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.
Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine

Jinsi ya kupika Vileja

VIPIMO

Unga wa mchele 500g

Samli 250g

Sukari 250g

Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai

Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai

Baking powder 1 kijiko cha chai

Mayai 4

Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai

NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA

1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.

2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.

3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.

4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.

5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.

6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa

Mchemsho wa samaki na viazi

Mahitaji

Samaki mbichi (1)
Viazi mbatata (3)
Nyanya (1)
Kitunguu maji
Limao
Kitunguu saumu
Tangawizi
Chumvi
Pilipili
Vegetable oil

Matayarisho

Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.

Madhara ya Kuvaa viatu virefu

NI wazi kuwa viatu virefu huvutia sana vinapo kuwa vimevaliwa.Tulio wengi hasa mabinti au wanawake tunaokwenda na wakati hupenda kuvaa viatu virefu ilikuongeza muonekano wa umbile lako nikiwa na maana kuwa miguu huonekana yenye kuvutia zaidi unapo kuwa umevaa viatu virefu.

Kutokana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku.Visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa kuliko kawaida, huku vikikunyima raha ya kutembea kwa uhuru kiasi kwamba wengine hufikia hatua ya kuvua na kutembea peku.

Leo hii napenda kukujuza madhara ya uvaaji wa wa viatu virefu.Kwa kawaida, miguu ya binadamu hasa visigino, vimeumbwa ili kuuzuia uzito wa mwili juu ya ardhi.Uvaaji wa viatu virefu hufanya uzito wa mwili kubebwa na kisigino, hivyo uzito wa mwili kushindwa kuhimili uzito wote.

Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya miguu, kiuno, mgongo na shingo kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito.Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino.Tatizo hilo hupelekea kiuno,Miguu na mgongo kuwa katika hatari ya matatizo ya kiafya pamoja na kuteguka na kuvunjika miguu.

Visigino virefu hubadili muundo wa mifupa ya miguu, hivyo hupelekea magoti na misuli ya mapaja kufanya kazi ya ziada ili kuupa mwili usawa.Kwa kuwa misuli inafanya kazi kubwa, uwezekano wa kupatwa na maumivu makali ya miguu na kushindwa kutembea katika siku za baadae huwa mkubwa zaidi. Visigino virefu husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya miguu, mpangilio wa mifupa ya vidole kuvurugika, mishipa na misuli ya mapaja kuuma, neva za fahamu kufungana na kushindwa kufanya kazi yake.

Tatizo huendelea kwa vifundo vya miguu, magoti, na mifupa ya kwenye mapaja kushindwa kujivuta na kulegea na hivyo kusuguana wakati wa kutembea.

Jambo la kuzingatia kwa wale wanaopenda kuvaa viatu virefu,ni vema kama unapenda kuvaa viatu virefu hakikisha hutembei umbali mrefu kama una usafiri sio mbaya ukivaa viatu virefu,na kwa wale wanao kwenda ofisini jitahidi kuwa na viatu flati ndani ya mkoba wako ili unapokuwa umechoka unavua na kuvaa viatu vyako pia ukiwa ofisini waweza kuvua viatu virefu.

Mpenzi msomaji kama huwezi kutembelea viatu virefu nivema ukipitwa na wakati kuliko kujiabisha barabarani na kuonekana rimbukeni ikiwa wewe ni mjamzito epuka uvaaji wa viatu virefu.Usikose kujumuika nami katika safu hii ya urembo na mitindo.

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Ukitaka kujua Simu ya Kichina utajua tu jinsi ilivyo na makelele mengiiiii sana wakati wa kuita….

Sasa ukitaka kujua relationship feki ya kichina utaona tu makelele yalivyo mengi kama ile simu…

Watu hawatulii kwenye wall,mara I miss my baby,mara baby come back,mara baby this,ooh my man/Girl is special,mara picha…

Mi and my baby,full kujishaua..ukiona wall zenye hayo makelele asilimia 90 ni penzi la kichina na lazima lina double line.

Relationship serious na Original hazina makeke wala mikelele mingi kama hiyo yako na milio mikubwa ya ajabu na vibration ambazo zinaweza kufyeka hata majani.

TULIA, hatuhitaji kujua who is ur baby au umemmiss, ukimmiss mpigie simu hukooo! Ebooo!!!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About