Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Kichekesho cha mwalimu na wanafunzi

Mtoto: Mwalimu mimi nataka nisome darasa la nne kwani hili la3 halinifai.

Mwalimu: Kwa nini unasema hivyo?

Mtoto: Nina akiliโ€ฆ

Basi mwalimu akamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni hayaโ€ฆ.

Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 20 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?

Dogo: Yatabaki 19.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.

Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani kwenye friji.

Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.

Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?

Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka kwenye friji.

Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?

Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.

Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani ni kwanini alikufa?

Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.

Mwalimu mkuu: Huyu dogo akasome chuo kikuuโ€ฆ.
๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†

Uvaaji wa Tai kulingana na Umbo lako

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi. Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?

Wengine huwa hawafahamu jinsi ya kufunga tai na hivyo kuleta mushkeri wakati wa kuvaa tai na kusababisha tai kukaa upande. Unapoamua kuvaa tai na shati ambalo halijanyooshwa ambalo linakuwa kwenye mikunjo au kuvaa tai na ndala unakuwa umeua maananzima na kulivunjia heshima vazi hili.

Tai ni vazi lawatu walio maridadi kama huwezi kuwa maridadi basi vazi hili halikufai kabisa.
Unapovaa taa unatakiwa kuzingatia aina ya umbo lako kama wewe ni mnene vaa tai inayoendana na mtu mnene na kama wewe ni mwembamba basi vaa tai inayoendana na mtu mwembamba.

Kuna wengine huvaa tai zinazofika magotini na kuwa kichekesho anapopita mtaani
Tai ni vazi ambalo huongeza heshima na hadhi ya mvaaji cha muhimu ni jinsi gani unavaa tai yako na ikiwezekana jaribu kumechisha tai na suruali kwa vile ili tai upendeze ni laima iendane na nguo unayovaa.

Ni vyema ukahakikisha kuwa unakuwa na tai zenye rangi tofauti ambazo zitaendana na nguo unazovaa.

Mapishi ya Dagaa wa nazi, nyanya chungu na bamia

Mahitaji

Dagaa waliokaushwa (dried anchovy 2 kikombe cha chai)
Bamia (okra 5)
Nyanya chungu (garden egg 5)
Tui la nazi (coconut milk 1 kikombe cha chai)
Nyanya (fresh tomato 2)
Kitunguu (onion 1)
Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
Turmeric powder 1/2 kijiko cha chai
Limao (lemon 1/2)
Chumvi (salt kiasi)
Pilipili (scotch bonnet 1)
Mafuta (veg oil)

Matayarisho

Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange kidogo kisha tia chumvi, pilipili, curry powder, turmeric, bamia na nyanya chungu, koroga vizuri mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri kisha tia nyanya na ufunike. Pika mpaka nyanya iive kisha kamulia limao,na pia hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva kidogo(usiache mpaka ziive sana manake zitavurugika pindi utakapotia tui la nazi) kisha malizia kwa kutia tui la nazi na uache lichemke mpaka rojo ibakie kidogo. Hakikisha nyanya chungu na bamia zimeiva ndo uipue. Na hapo dagaa wako watakuwa tayari kwa kuliwa na wali au ugali.

Faida ya kupanda maharagwe katikati ya kabichi

Maharagwe yanapandwa kwenye kabichi yanafanya kazi zifuatazo;

Kudhibiti wadudu (mtego).

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Kuboresha udongo.

Maharagwe yanaongeza nitrojeni kwenye udongo

Chakula cha mifugo.

Maharagwe yanaweza kutumika kulishia mifugo kama ng’ombe mbuzi na kondoo.

Matandazo.

Maharage yanaweza yakatumika kama matandazo kwenye shamba kusaidia kulinda unyevu.

Kutengenezea mbolea.

Maharagwe yakioza yanaweza kuwa mbolea nzuri ya shamba lako

Hizi ndizo sababu kwa nini ule Tende kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Kitaalamu chakula unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni. Na ni muhimu sana kuzingatia ulaji bora wa chakula na si kula ilimradi umekula. Wataalamu wa lishe wanatuambia kuwa ulaji unaofaa hutokana na kula chakula mchanganyiko kulingana na wakati.

Lakini hata ulaji huo, unatakiwa kutazamwa ni ulaji gani unaofaa kulingana na mchanganyiko kulingana na mahitaji ya mwili. Na pia, wanasema mlo kamili unaofaa ni ule ulio na virutubisho vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora.

Leo katika makala haya, yataangazia ulaji wa tende, na kwa kuzingatia kuwa huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tende ndiyo tunda pekee linaloliwa kwa wingi, pengine kuliko tunda lingine lolote.

Inaelezwa kuwa kisayansi, tunda hilo limethibitika kusheheni madini na vitamini nyingi kiasi cha kulifanya liwe na faida nyingi kiafya.

Ulaji wa tende kwa waliofunga

Mtaalamu wa Lishe, Juliana Majaliwa anasema mtu aliyekwenye mfungo, mara zote huwa kiwango chake cha sukari mwilini hupungua na kutakiwa airejeshe tena kwa kula vyakaula vitakavyosaidia kufanya mara tu anapotakiwa kufuturu.

Majaliwa anasema aina ya kwanza ya sukari itumikayo mwilini ni ya glukosi. Lakini sukari inayoshuka kwa watu ambao hawajala wala kula kwa muda mrefu, inaweza kuwasababishia kupatwa na kizunguzungu au kulegea.

Hivyo, anasema ulaji wa tende mara mtu anapotakiwa kufuturu, humfanya aliyefunga asijihisi kuchoka sana na huwa na nuru zaidi ya macho. Pia tende zitamsaidia kuimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo ataondokana na matatizo ya ukosefu wa choo au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

Hivyo, mfungaji akila tende zitamsaidia kupata virutubisho vya โ€˜amino acidsโ€™ ambavyo ni muhimu mwilini, pia mwili wake utapata aina mbalimbali za madini na vitamin za kutosha, ambazo zinapatikana kwenye tunda hili maarufu ambalo lina kiasi kidogo cha mafuta yasiyo na lehemu. Majaliwa anasema sukari inapoliwa kwa njia ya chakula au kinywaji, mara zote viwango vya glukosi ya mwili hujisawazisha yenyewe na kumfanya mlaji aliyefunga asijihisi.

Ingawaje tende mara nyingi si chakula kinachopendelewa sana na watu wenye njaa, lakini ndicho chakula kisicho na mafuta na ni chanzo madhubuti cha sukari.

Wataalamu wa lishe wanasema mfungaji akila tende, atajipatia kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili kwa ujumla.

Faida zaidi za tende

Wale walio kwenye mfungo, muda wa kufuturu ukiwadia, wanashauriwa pia kuchanganya tende na maziwa halisi kisha wale. Na kama wanajisikia uchovu, badala ya kunywa vinywaji baridi vinavyodaiwa kuongeza nguvu, wale tende hata punje tatu tu zinatosha.

Wataalamu wa lishe wanawashauri kuanza kufungua kwa kula tende ili kuurejeshea mwili nguvu iliyopotea kwa siku nzima.

Kwa sababu tende pia ina madini aina ya potasium na kiasi kidogo cha chumvi.

Madini haya husaidia uimarishaji wa mishipa ya fahamu. Watafiti wamegundua kwamba ulaji kiasi wa madini ya potasium husaidia kumwepusha mtu na maradhi ya kiharusi. Pia tende husaidia kupunguza lehemu mwilini.

Wenye matatizo ya kukauka damu

Wataalamu wanasema kwa mfungaji mwenye tatizo la kukauka damu mwilini (anemia), anaweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi ambayo ina kiwango cha kutosha cha madini ya chuma ambayo huhitajika katika utengenezaji wa damu mwilini. Wakati vitu vingine vitamu vinadaiwa kuwa huozesha meno, lakini wataalamu wa tiba lishe wanasema utamu wa tende huzuia uozaji wa meno.

Faida zingine za tende

Kwa mtu aliye na tatizo sugu la kukosa choo, anatakiwa kuloweka tende za kutosha kwenye maji kiasi cha lita moja kwa muda ili kupata juisi nzito, muathirika anywe na atapata choo laini.

Kwa matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume, mchanganyiko maalum wa tende, maziwa, asali na unga wa hiriki vinaweza kuondoa tatizo hilo. Chukua kiasi cha kiganja kimoja cha tende, loweka kwenye maziwa ya mbuzi kiasi cha lita moja, ziache zilowane kisha zisage kwenye maziwa hadi zichangayike, weka vijiko vitatu au vinne vikubwavya asali pamoja na nusu kijiko cha chai cha hiriki, kisha kunywa mchangayiko huo kila siku hadi utakapoona mabadiliko ya kuridhisha.

Tende ni dawa

Tunaelezwa kuwa tende ni dawa ya unene na kwa wale wenye matatizo ya wembamba wa kupindukia na wanataka kuongeza uzito, ulaji wa tende kila siku unaweza kuwasaidia. Lakini hii ina maana wale wanaohitaji kupunguza uzito, ulaji wa tende kwa wingi hauwezi kuwafaa.

Mtaalamu wa tiba ya mimea, Japhet Lyatuu, anasema tende hutibu pia saratani ya tumbo na husaidia pia kuondoa hali ya ulevi kwa wale wanaokunywa pombe.

Anasema tende tiba ni na haina madhara yoyote kwa sababu ni dawa ya asili na inafanyakazi vizuri kuliko dawa za โ€˜kizunguโ€™.

Laytuu anasema tunda hilo husaidia pia kuimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku. Anasema faida za tende ni nyingi na mtu anaweza kuila kwa namna mbalimbali.

Maswali ya kijinga yakijibiwa vizuri

Haya ndiyo majibu mazuri๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Q: Umenyoa nywele?

A: *Hapana, nimebadilisha kichwa.*

Q: Hiyo simu umenunua?

A: *Hapana nimeitengeneza mwenyewe.*

Q: Utakula mboga na nini?

A: *Mdomo*

(Simu inaita usiku,then aliyepiga anauliza) Q: Nimekuamsha?

A: *Hapana nilikuwa naota jua hapa nje.*

Q: Gazeti la leo linasemaje?

A: *Sijaongea nalo.*

Q: Gari limejaa, nitakaa wapi?

A: *Usijali dereva anashuka kituo kinachofata utapata kiti.*

Q: Hiyo ni ajali?

A: *Hapana ni driver ameamua kupark gari upside down* .

Q: Umepause movie?

A: *Hapana wamechoka kuact wanarest.*
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚๐Ÿƒโ€โ™‚

MAPISHI YA LADU

VIAMBAUPISHI

Unga – 6 vikombe

Samli – ยฝkikombe

Baking Powder – ยฝkijiko cha chai

Maziwa- 1 kikombe

Maji -Kisia kiasi kama unga bado mzito

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari – 5 vikombe

Maji – 2ย 1/2 vikombe

Vanilla – 2 vijiko vya chai

Rangi ya orange – 1 kijiko cha chai

Iliki ya unga – 1 Kijiko cha chai

MAANDALIZI

Changanya unga wa dengu, samli, baking powder pamoja na maziwa katika mashine ya keki (cake mixer).
Ukisha changanya angalia kama mchanganyiko wako umekua mwepesi kidogo kuliko wa keki, kama bado mzito basi ongeza maji kiasi.
Kisha weka mafuta kiasi kwenye karai,weka na samli kikombe kimoja, weka kwenye moto wa kiasi.
Mafuta yakisha pata moto, chukua kijiko kikubwa cha matundu chota mchanganyiko wako na kijiko cha kawaida tia kwenye kijiko cha matundu. Hakikisha kijiko cha matundu kiwe juu ya karai ili mchanganyiko wako uchuruzike ndani ya mafuta yalio pata moto.
Pika ndani ya mafuta mpaka iwive, ila usiache ikawa brown.
Toa mchanganyiko ulowiva tia ndani ya shira uliyo pika. Hakikisha shira iwe imepoa kabla ya kutia mchanganyiko huo.
Endelea kupika mchanganyiko wako mpaka uishe, kila ukitoa katika mafuta hakikisha unatia ndani ya shira.
Ukishamaliza wote kanda huo mchanganyiko ulokua ndani ya shira mpaka uone shira yote imekauka (yaani iwe imeingia ndani ya mchanganyiko).
Tupia zabibu kavu na lozi zilizo katwa, changanya na mkono.
Wacha mchanganyiko katika bakuli, funika na foil mpaka siku ya pili.
Siku ya pili chukua mchanganyiko kiasi katika mkono tengeneza mviringo (round).

MAANDALIZI YA SHIRA

Katika sufuria, tia sukari, maji, iliki, vanilla na rangi.
weka kwenye moto wacha ichemke mpaka itowe povu (bubbles) juu.
Kisha toa povu, wacha shira kwenye moto kama dakika 3.
Hakikisha shira yako iwe inanata kiasi kwenye vidole, lakini iwe nyepesi kidogo kuliko shira ya kaimati.

Cheki hawa wachungaji

CHEKA KIDOGO

Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.

MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.

WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.

WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:

We vp unatatizo gani mbona unalia???

AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ‘†๐Ÿป๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Jinsi ya kupika Slesi Za Chokoleti Na Karameli

Viamba upishi

Unga 1 Magi (vikombe vya chai)

Sukari ya browni ยฝ Magi

Siagi iliyoyayushwa 125ย g

Nazi iliyokunwa ยฝ Magi

Mjazo wa karameli (Caramel filling)

Syrup 1/3 kikombe cha chai

Siagi iliyoyayushwa 125ย g

Maziwa matamu ya mgando 2 vikopo (condensed milk)

Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)

Chokoleti 185ย g (dark chocolate)

Mafuta 3 Vijiko vya chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.

2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30ย cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.

3. Choma kwenye moto 325หšC kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.

4. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.

5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.

6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa

Jinsi Bikira Maria anavyoelezwa Katika dini ya Kiislamu

Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili.
Hata hivyo anapewa heshima ya pekee, kama inavyoonekana katika sura ya 3:43: โ€œNa kumbukeni malaika waliposema, โ€˜Ewe Mariamu, kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa walimwenguโ€. Tena katika aya 3:46: โ€œNa kumbukeni waliposema malaika: โ€˜Ewe Mariamu, bila shaka Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za Neno litokalo kwake, jina lake Masihi Isa mwana wa Mariamu, mwenye heshima katika dunia na ahera, na yu miongoni mwa waliokaribishwaโ€™โ€.
Aliambiwa amefanywa โ€œisharaโ€ pamoja na mwanae, ingawa haisemwi ni ishara ya nini. Sura ya 19, yenye jina lake, inaeleza kwamba Malaika Jibrili (Gabrieli) akimpasha habari ya mimba alisema, โ€˜Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifuโ€™. Akasema, โ€˜Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote, wala mimi si mwasherati?โ€™ Akasema, โ€˜Ni kama hivyo; Mola wako amesema: Haya ni rahisi kwangu, na ili tukufanya ishara kwa mwanadamu na rehema itokayo kwetu, na ni jambo lililokwisha hukumiwaโ€™ โ€ (19:19-21). โ€œNa mwanamke yule aliyejilinda tupu yake na tukampulizia roho yetu na tukamfanya yeye na mwanawe ishara kwa walimwenguโ€ (21:91).
Pamoja na kusifiwa kwa usafi wake, anaongezewa sifa za imani na unyenyekevu: โ€œNa Mariamu binti Imrani aliyejilinda uchi wake, na tukampulizia humo Roho yetu na kayasadikisha maneno ya Mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevuโ€ (66:12).

Mambo 5 ya muhimu kuzingatia kuhusu mahali unapotaka kuweka mizinga ya nyuki

Ukitaka kujua kuwa eneo unalotaka kuweka mizinga ya nyuki ni sahihi unatakiwa kuzingatia yafuatayo:

1. Haishauriwi kuweka mzinga shambani au karibu na shamba. Unatakiwa uweke umbali wa mita 150-200 kutoka kwenye mazao au nyumbani. Hii ni Kulingana na hali ya kujilinda ya nyuki wa Afrika

2. Mzinga ni lazima uwekwe sehemu ambayo haitasababisha upotevu wa nyuki wanaporudi kutoka nje ya mzinga. Mfano wasiingie kwenye kundi lisilokuwa lao.

3. Mizinga inatakiwa isiwekwe mbalimbali sana ili kuepusha usumbufu wa kutembea mbali kwa mfugaji wakati anapokagua.

Sifa ya eneo la kuweka mizinga
โ€ข Iwe Kimya na mbali ya jumuia kama vile hospitali, shule, na viwanja vya michezo vile vile isiwe karibu na maeneo ya biashara au viwanda.
โ€ข Karibu na maji masafi-kandokando ya mto, mabwawa ya samaki, mabeseni ya maji au sehemu ya matone.
โ€ข Sehemu ya kuweka mizinga Iwe ni karibu na chakula cha nyukimimea inayochanua, miparachichi, nazi, euculptus, migunga n.k
โ€ข Iwe sehemu ambayo ni kavu na isiwe sehemu ya tindiga kwani unyevu unyevu husababisha ugonjwa wa ukungu (magonjwa ya fangasi yaani fungal disease) na pia huzuia utengenezaji mzuri wa asali.
โ€ข Mahali pa mizinga pawe mbali na watu waharibifu na iliyojificha kuepuka waharibifu.
โ€ข Sehemu ya kuweka mizinga ni lazima iwe inafikika kirahisi kwa kipindi chote cha mwaka ili iwe rahisi kuhamisha nyuki pale inapohitajika.
โ€ข Panatakiwa pawe kivuli cha kutosha hasa wakati wa mchana jua linapokuwa kali, na kusiwe na upepo mkali.

4. Mizinga ya nyuki Iwe mbali na mashamba, ambapo dawa za kuulia wadudu zinatumika.

5. Vichaka au wigo unaotenganisha mizinga na kuzuia wavamizi ni muhimu ili kupunguza ukali wa nyuki.

Jinsi ya kupika Wali Wa Sosi Ya Tuna

Viambaupishi

Sosi Ya tuna

Tuna (samaki/jodari) 2 Vikopo

Vitunguu (kata kata) 4

Nyanya zilizosagwa 5

Nyanya kopo 3 Vijiko vya supu

Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo – cubes) 4

Dengu (chick peas) 1 kikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu

Hiliki 1/4 kijiko cha chai

Mchanganyiko wa bizari 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Pilipili manga 1 Kijiko cha chai

Vipande cha Maggi (Cube) 2

Wali

Mchele 3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Mdalasini 2 Vijiti

Karafuu chembe 5

Zaafarani kiasi

*Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) 1/2 Kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Kosha Mchele na roweka.

2. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando.

3. Kaanga viazi, epua

4. Punguza mafuta, kaanga nyanya.

5. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi.

6. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi.

7. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali.

8. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.

9. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven)

10. Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali.

11. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu).

12. Funika wali na upike katika jiko moto wa 450ยบ kwa muda wa kupikika wali.

* Jirsh (komamanga) kavu zioshwe vizuri kutoa vumbi au tumia zabibu kavu (raisins)

Mapishi ya tambi za mayai

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.

Mahitaji

  1. Tambi ยฝ paketi
  2. Vitunguu maji 2 vikubwa
  3. Karoti 1
  4. Hoho 1
  5. Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  6. Carry powder kijiko 1 cha chai
  7. Njegere zilizochemshwa ยฝ kikombe
  8. Mafuta kwa kiasi upendacho
  9. Mayai 2
  10. Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About