Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu.

Kula zaidi vyakula vyenye protini, vyenye vitamini B na C kwa wingi. Kula milo midogo midogo hata mitano kuliko kula miwili au mitatu lakini ya nguvu sana.

Unaweza kutumia kitunguu swaumu hasa kibichi ukitafuna punje 2 kila unapoenda kulala kadharika glasi moja ya juisi ya ubuyu kutwa mara 1.

Acha vilevi vyovyote mara tu unapogundulika na shinikizo la chini la damu. Epuka pia vyakula vyenye wanga sana kama tambi, mikate, viazi, wali nk

Upungufu wa baadhi ya vitamini hasa vitamini za kundi B na madini kunaweza pia kuleta shinikizo la chini la damu. Hivyo ili kudhibiti shinikizo la chini la damu unahitaji kula mlo sahihi kila siku.

Jinsi ya kuandaa Pilau ya sosi ya soya, nyama na mboga

Mahitaji

Nyama isiyokuwa na mifupa – 1 ยฝ Lb(ratili)
Mchele wa Basmati (rowanisha) – 3 Magi
Vitunguu maji – 2
Mchanganyiko wa mboga za barafu – 1 Magi
(karoti, mahindi, njegere)
Pilipili Mbichi – 3
Pilipili mboga kijani na nyekundu – 1
Pilipili manga – ยฝ kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Sosi ya soya (soy sauce) – 5 Vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 Kijiko cha supu
Mchanganyiko wa bizari (garam masala) – 1 Kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa – ยฝ Kikombe
Mafuta ya kukaangia – Kiasi

Namna Ya Kutaarisha

Ndani ya sufuria, tia mafuta yakipata moto kaanga vitunguu mpaka ziwe rangi ya hudhurungi.
Kisha tia nyama iliyokatwa vipande vidogo vidogo pamoja na maji ya kiasi na viungo vyote isipokuwa mchele, mboga zote na kotmiri. chemsha mpaka nyama iwive na maji yakauke.
Halafu changanya na mboga na iwache kwa muda wa dakika kumi kisha tia kotmiri na umimine kwenye bakuli au treya ya oveni na uweke kando.
Chemsha mchele na chumvi uwive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja, kisha umwagie juu ya ile treya ya nyama.
Nyunyizia mafuta na sosi ya soya na ipike katika oveni moto wa 350ยฐ kwa muda wa dakika 20 hivi.
Ukishawiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kutunza kucha kujiepusha na maradhi shambulizi ya Kucha

Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.

Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.

Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.

Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile โ€˜Formaldehyde na Tolueneโ€™ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.

Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.

Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.

Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.

Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia โ€˜nail cutterโ€™ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.

Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.

Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.

Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : ๐Ÿ—ฃJoniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: ๐Ÿ—ฃ we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: ๐Ÿ—ฃ Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Huyu mama mkwe kazidi sasa

Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na wengi. Gharama yake ni ndogo kiasi kulinganisha na mingine. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga Yya aina hii mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.

 

Mzinga wa Top bar

Faida ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
โ€ข Ni rahisi kukagua asali iliyo tayari.
โ€ข Ni rahisi kuvuna asali kuliko kuvuna toka kwenye mzinga wa kienyeji.
โ€ข Ni rahisi kuwatunza nyuki wakati wa kiangazi na inapokuwa hakuna maua. Kwa mfano unaweza kuwapatia nyuki chakula ili kuongeza uzalishaji wa asali.
โ€ข Ni rahisi kurina asali ukilinganisha na mizinga ya magogo inayotundikwa juu ya mti, kwa kuwa haihitaji vifaa maalumu.
โ€ข Aina hii ya mizinga huwekwa kwa kuninginia jambo ambalo siyo rahisi kushambuliwa na wadudu/wanyama wanaokula asali kwa kuwa Inajaa haraka sana wakati ambao ni msimu wa asali kutengenezwa kwa wingi.

Hasara ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
โ€ข Kichane kwenye mzinga wa boksi hakina kishikizo hivyo huvunjika kwa urahisi sana kama hakitashikwa kwa uangalifu.
โ€ข Masega huvunwa pamoja na asali, kwa hiyo nyuki wanalazimika kutengeneza tena masega mengine ambapo husababisha kupungua kwa uzalishaji wa asali.

Mzinga wa Langstroth

Mzinga wa Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi kulinganishwa na mizinga mingine Hii ni aina nzuri na rahisa sana ya mzinga. Mizinga hii hufahamika kama mzinga wa fremu, kwa kuwa ina fremu ambazo vichane vya masega hujishikiza. Chumba kikubwa ambacho malkia hutagia mayai. Malkia anazuiliwa kuhama kwenda chumba kingine kwa kutumia waya. Kwenye chemba maalumu ya kutagia juu yake pana chemba ya kuhifadhia asali.

 
 

Mzinga wa Langstroth

Vichane vya masega vinatengezwa kwenye fremu na si kwenye nguzo kama ilivyo kwenye Top bar. Ili kuvuna asali, mfugaji akiwa na masega yaliyojaa asali, hutumia vifaa maalum kwa ajili ya urinaji na kuhifadhi asali bila kupata tabu.

Mzinga wa Langstroth ni gharama kiasi kulinganisha na mizinga mingine.Unaweza kuipata kutoka katika taasisi zinazojiusisha na uuzaji wa mizinga, taasisi na karakana binafsi, au wakala wa Serikali.

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.

Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?

Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24???
Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyoโ€ฆ.katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.

Tuseme katika Masaa 8 kwa ajili ya mambo yako mengine labda masaa manne yanapotea katika foleni au purukushani za maisha kama kula nk.
Je haya mengine manne yanaenda wapi?Tunayapotezea wapi?
Kwenye mpira?kwenye movie?kwenye TV?kwenye mitandao ya kijamii?kukaa na kuwajadili wengine na mashosti?

Hivi unajua kwa siku una wastani Wa kupoteza masaa manne kwenye masaa yako 24??
Kwa wiki unapoteza masaa 28 hali kadhalika masaa 112 kwa mwezi hupotea.
Kwa mwaka mmoja wenye masaa 8760 una wastani Wa kupoteza masaa 1344 ambayo ni sawa na siku 56 kwa mwaka kwa makadirio ya haraka haraka.

Kwa maana nyingine kwa kutumia hii “concept” kila miezi 12 ya mwaka mzima unapoteza miezi miwili kwa mambo ambayo sio “productive”.
Hii ni sawasawa na kupoteza mwaka mmoja ndani ya miaka 6โ€ฆkwa maana nyingine kwa “the same concept” ya masaa 4 kwa siku kupotea ni kwamba unapoteza mwaka mmoja kwa mambo ambayo hayakusaidii chochote.

Hebu jiulize hapo ulipo una umri gani?umeshapoteza miaka mingapi kwa mambo ambayo sio productive??
Kama wewe ni mfanyakazi au muajiriwa ukifanya kazi kwa muda Wa miaka 40 au kwa muda Wa miaka 40 unapoteza miaka 6.6.

Je hebu jiulize muda wote huo unaoupoteza kwenye mambo ambayo sio “productive” ungekuwa ni muda ulioutumia vizuri kwa mambo ya uzalishaji mfano kuanza kidogo kidogo kujenga biashara yako sasaivi tungekuwa na mamilionea na mabilionea wangapi?
Ili uweze kujenga biashara ambayo ni “strong” inakuhitaji angalau uijenge kwa muda Wa miaka mitano kwa maana nyingine kwa kutumia masaa manne tu kwa siku ndani ya miaka 40 utakuta tayari wewe ni milionea na baada ya kustaafu ajira usingeanza kuangaishana na pensheni (kwanza ni shilingi ngapi) au kuanza kubembeleza kuomba uongezewe mkataba au kwenda kufanya tena part time employmentโ€ฆ..kwa concept hiyo ni mamilionea wangapi tumewapoteza??

Ndio maana katika hii dunia yetu tunayoishi matajiri wote ni 3% na 97% ya watu waliobakia wanawafanyia kazi matajiri.
Matajiri waliweza kuiona hii concept kwa jicho la Tatu na wakaanza kuifanyia kazi and the rest is history.
Huwezi kumkuta tajiri anapoteza muda wake kwa mambo ya kizembe yasiyomuingizia chochote ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini wanaendelea kuwa maskini.

Lakini bado muda na nafasi unayo sasa ukiamua na ukianza kuutumia muda wako ulio nao kwa ajili ya kuyatengeneza maisha yako.
Watu wengi hawako tayari kuumia na kujifunza biashara na kuielewa ndani ya miaka mitano itakayowapelekea kuwa matajiri na kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao lakini wapo tayari kuajiriwa na kufa maskini ndani ya miaka 40.

Muda mzuri ndio sasa Wa kufanya maamuzi sahihi Wa kuyawekeza masaa manne kwenye biashara ili uje upate matokeo chanya.

Mapishi ya Bagia dengu

Mahitaji

Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho

Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Kukataliwa ni mtaji

Hakuna mtu duniani ambaye hajawahi kukutana na hali ya kukataliwa. Yaani kukataliwa katika hali yoyote ile. Waweza kuwa umekataliwa katika kupata ajira, umekataliwa katika mahusiano, umekataliwa kupata nafasi ya kusoma, umekataliwa kupata mtaji wa biashara, umekataliwa tuu..umekataliwa.

โ€”-= Unaweza kuwa umekataliwa katika ajira moja kumbe kuna ajira nyingine tena yenye maslahi zaidi inakusubiri.

โ€”-= Umekataliwa na mteja mmoja na kumbe kuna wateja wengi wanakusubiri.

โ€”-= Umekataliwa katika chuo kimoja mwaka huu kumbe mwakani kuna nafasi yako inakusubiri.

โ€”โ€”= Umekataliwa na mpenzi ulioamini kabisa atakua wako wa maisha kumbe aliye wako haswaa anakusubiri ufike.

Watu wengi kinachowarudisha nyuma, “ni kuacha kuboresha fikra zao ili kuwa watatuzi wa matatizo_(problem solvers)_ ila wameamua kuwa walalamikaji tu kila siku, ili tuendelee ni lazima tujikite katika kutafuta majibu ya matatizo yanayotuzunguka.” Yaani, mara zote jiulize ” *sasa nifanye nini? Na sio kwa nini mimi?”*

Mtaalamu mmoja aliwahi kusema ” _Life is 10% of what happens to you and 90% of how you respond to it_”. Yaani _yale yanayokutokea maishani yanachangia asilimia kumi tu kuboresha au kuharibu maisha yako na asilimia 90 ya maisha yako ni jinsi wewe unavyoyachukulia maisha hayo_. Kwa nini ukate tamaa baada ya kukataliwa. Yape maisha yako maana sana thamani ya juu kabisa ili kukataliwa kwako iwe ni kukupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi. Tambua utakacho na unachoweza kukifanya. Jifunze vizuri na ubobee ili kuuhakikishia ulimwengu kwamba wewe sio mzigo ila ni sehemu ya wenye majibu ya matatizo yanayotuzunguka.

Kukataliwa, ni mtaji. Kila jambo lina wakati wake.

Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-

Kwako muajiriwa

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko “busy” kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko “busy”??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??

Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??

Kwako wewe uliyejiajiri

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟNi watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟWangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??

Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 ยฝ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ยฝ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo.
Ndoto uliyonayo ina thamani kubwa kuliko fedha wala kitu chochote kile. Ndoto uliyonayo ina nguvu kubwa ya kubadilisha maisha yako na kukufikisha sehemu ambayo ulitaka ufike ama zaidi ya pale ulipotarajia kufika.

Ndoto yako inaweza kukupeleka sehemu mbalimbali duniani ukazunguka kufanya mambo yako si kwa sababu una fedha sana, bali ni kwa sababu una ndoto. Ni vyema utambue nguvu ya ndoto uliyonayo ni kubwa kuliko fedha.

Ndoto inaweza kuzaa fedha kwa maana matunda yake yanaweza kuwa fedha, lakini katu fedha haiwezi kuzaa ndoto. Kwa hiyo bais, ndoto ni kubwa kuliko fedha.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, mtu maskini kuliko wote duniani ni yule asiyekuwa na ndoto!

Hivyo utakubaliana naye kuwa kila mwenye ndoto ni tajiri na si maskini, maana ana kitu cha thamani, cha pekee na cha tofauti ambacho hakuna mwenye nacho isipokua wewe mwenyewe.

Tatizo kubwa ni kwamba, watu wengi wameua ndoto zao kwa kisingizio cha kukosa fedha lakini wanashindwa kutambua kwamba hakuna fedha inayozidi ndoto isipokuwa ndoto inazidi fedha.

Tatizo lingine ni kwamba, watu wengi hawajui kuwa ndoto zao zina nguvu kubwa kufanikisha maisha yao kijamii, kiuchumi, kisiasa na kila nyanja.

Ndani ya ndoto zako kuna kila kitu unachokitaka ama unachokihitaji โ€“ iwe fedha, utajiri, umaarufu, familia nzuri, mume mzuri, mke mzuri, watoto wazuri, kazi nzuri, afya nzuri โ€“ hivyo ukiacha kutafuta fedha ukatafuta kutimiza ndoto zako utapata kila kitu ikiwemo utoshelevu na amani ya moyo.

Lakini tatizo lipo kwenye kufanya ndoto zako zitimie na zikuzalie mafanikio. Haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani, kama hutaitimiza ikaja kwenye uhalisia tambua kwamba utakufa maskini ukiwa na utajiri wa ndoto, jambo ambalo linaumiza na linatesa maisha ya watu wengi wanaoishi maisha ya chini tofauti na walivyopaswa wawe.

Ndoto yako ndiyo imebeba kusudi la maisha yako. Kama hutaishi katika ndoto yako maana yake utakuwa hujaishi maisha yako ambayo kwa kiasi kikubwa yapo kwenye ndoto zako.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa, watu wengi duniani hawaishi, bali wapo tu. Kuna tofauti kati ya kuishi na kuwepo. Kuishi ni kutimiza ndoto zako na ndani ya kusudi la maisha yako, lakini kama hutimizi ndoto hizo uko nje ya kusudi la maisha yako. Wewe utakuwa hauishi bali upo upo tu.

Anaamka asubuhi kwa sababu watu wanaamka. Ukimuuliza kwanini umeamka anasema ni kwa sababu watu wameamka! Hana sababu za msingi. Kataa kuishi bila agenda, bila kuwa na ndoto ambayo kila siku unapiga hatua kuifikia ama uko ndani yake sasa katika kuitimiza na kuifanikisha kwa kiwango cha juu.

Kila kitu kipo kwenye ndoto zako, tafuta kutimiza ndoto zako kuliko kutafuta fedha kwa sababu fedha ni moja kati ya bidhaa iliyomo ndani ya ndoto zako.

Sisemi watu wasitafute fedha, la hasha. Wazitafute, tena kwa bidi, ila wasisahau kutafuta kutimiza ndoto zao na kutumia fedha kama moja kati ya nyenzo za kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Ukweli ni kwamba, fedha daima huwa hazitoshi, hata kama ni nyingi kiasi gani. Kama unabisha waulize matajiri kama wamewahi kuridhika. Lakini katika kutimiza ndoto zako kuna utoshelevu kiasi na kuridhika kiasi fulani (satisfaction) hata kama si kwa asilimia 100.

Mwandishi mashuhuri wa vitabu, Myles Munroe, aliwahi kusema kuwa โ€œWatu wenye kusumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo ni wale ambao ndoto zao hazijatokea kwenye uhalisia, zinawasumbua.โ€

Inawezekana unasumbuka sana kwenye maisha yako kwa sababu hujatimiza ndoto zako, maana ndoto huwa haimwachi mtu akatulia, inampa mahangaiko, mfadhaiko wa kutaifuta.

Kila mtu anapaswa azae, ndoto yako izae, uwezo ulionao uzae. Unaweza kukuzalia mafanikio makubwa, hivyo usikubali kufa na kitu cha thamani kilichoko ndani yako.

Hakuna ndoto kubwa wala ndogo. Fikiria mtu aliyegundua lipstick, leo hii wanawake dunia nzima wanapaka lipstick, si jambo dogo tena.

Hukuja duniani kuwa mtu wa kuhangaikia fedha, inatakiwa fedha ikuhangaikie wewe, ikupende na ikutamani na si wewe utamani fedha.

Tengeneza miundombinu ya fedha na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako, maono yako, kipaji

Namna ya kupika Biskuti Za Kuchoveya Chokoleti

VIAMBAUPISHI

Unga 300gm

Siagi 225gm

Icing Sugar 60gm

Chokoleti iliyokoza (Dark Chocolate) – 225gm

Vanilla โ€“ Vijiko 2 vya chai

Yai -1

Baking Powder ยฝ kijiko cha chai

Njugu za vipande ยฝ kikombe cha chai

Njugu zilizosagwa ยผ kikombe cha chai

JINSI YA KUTAYARISHA

Piga sukari na siagi katika mashine ya keki mpaka iwe laini
Kisha mimina yai na vanilla koroga vizuri
Mwisho mimina unga na baking powder polepole mpaka ichanganyike.
Kata kata umbo (shape) lolote unavyopenda (kama nyota, pembetatu,duara, kopa n.k)
Panga kwenye treya na choma kwa moto wa 350ยฐC , vikibadilika rangi kidogo tu vitoe
Yayusha chokoleti tia kwenye bakuli ndogo.
kisha paka kwa kijiko au chovyea upande mmoja mmoja wa biskuti kisha nyunyizia njugu za kipande na njugu ya unga.
Panga kwenye sahani tiyari kunywewa na chai ya maziwa au kahawa.

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziโ€ฆ

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Namna ya kutibu chunusi kwa kutumia Binzari, maziwa na asali

Unahitaji vitu vifuatavyo:

a)Binzari ya unga
b)Maziwa fresh
c)Asali
d)Bakuli
e)Kijiko cha chai

Hatua kwa hatua namna ya kutumia:

a)Weka kijiko kidogo kimoja cha binzari ya unga ndani ya bakuli
b)Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali ndani yake
c)Ongeza tena kijiko kidogo kimoja au viwili vya maziwa fresh
d)Changanya vizuri mchanganyiko huu upate uji mzito
e)Pakaa pole pole sehemu yenye chunusi mchanganyiko huu
f)Baada ya dakika 5 au 7 hivi jisafishe uso wako
g)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 tu kwa wiki

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About