Uwe na maono
Uwe na maono au ndoto ya mambo unayotaka kufanya maishani naye Mungu atakubariki na kujidhihirisha katika ndoto zako.
Uwe na maono au ndoto ya mambo unayotaka kufanya maishani naye Mungu atakubariki na kujidhihirisha katika ndoto zako.
Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao ili wadumu katika mahusiano. Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hali kadhalika kama bado haupo Kwenye mahusiano kuna mambo ambayo ni ya msingi kufanya au kuwa nayo ili uweze kuwa na mvuto zaidi kwa wanawake.
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali wao kama wao, wanaojali kile wanachokifanya na watu wao wa karibu kama ndugu na wazazi. Wanapenda wanaume wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa amjali mpenzi wake kwa kila hali. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Vile vile kuonyesha kujali mambo yake na watu wake wa karibu kunamvutia mwanamke.
Mwanamke huvutiwa sana na mtu ambaye yupo karibu nae na ambaye anapatikana wakati anapohitajika. Kati ya vitu vinavyowapa wapendeza sana wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku na kushiriki katika mambo yake hata kwa mawazo kama ukishindwa kwa matendo. Ni vizuri kuwa naye au kuwasiliana naye wakati wa kula, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi na ambayo ni muhimu sana kwa wanawake. Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako, mfano kutembea pamoja, kuangalia movie pamoja, nakadhalika. Tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa kwani mwanamke anavutiwa sana na mtu aliye karibu nae.
Wanawake wanapenda kusifiwa na kuonekana kuwa bora. Mwanamke akisifiwa anahisi kupendwa kupita kiasi. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye. Vilevile kumsifia mwanamke kwake ni njia ya kuonyesha upendo na Ishara ya kuonyesha kumjali kupita kiasi.
Mwanamke anavutiwa zaidi na mtu anayeonyesha kumpa kipaumbele na kupewa nafasi. Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mwanamke akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya โmtoto wa dada amerudishwa ada shuleniโ.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.
Wanawake wanapenda mwanamme ambaye ni msafi, hii ni kwa sababu kiasili wamejaliwa kupenda usafi ndio maana ni nadra sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini yaani mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia pale anapotakiwa kufanya hivyo au wakati wowote ule. Siyo anayebabaika na kuyumba yumba. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia nguo mpya.
Mwanamke anapenda kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwanamke hapendi mtu anayebadilikabadilika Kwenye maamuzi na misimamo yake.
Mwanamke anapenda mwanaume mwenye malengo na anayemshirikisha katika mipango yake. Mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenye malengo katika maisha yake. Vilevile anapenda mtu anayemshirikisha katika malengo yake na kumuweka katika mipango yake. Faida ya kumshirikisha katika malengo yako ni pamoja na kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.
Mwanamke hupenda mwanamme anayeweza kujitetea. Mwanaume aliye โfitiโ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi. Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu โ anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote! Inapowezekana, uwe na uwezo wa โkuzichapaโ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.
Mwanamke anavutiwa zaidi na mwanamme anayeweza kumridhisha katika tendo la ndoa. Anataka mwanamme anayeweza kufanya kile anachotaka yeye na kile anachokipenda. Mwanamke hapendi mwanamme anayemkomoa katika tendo la ndoa au anayefanya mambo asiyoyapenda. Mwanamke anataka kuridhishwa na kujaliwa katika tendo la ndoa.
Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :ย Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :ย Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :ย Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:ย Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :ย Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
๐๐๐๐๐๐๐
ยท Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada
ya kutayarisha chakula
ยท Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa
kutayarisha na kula chakula
ยท Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula
ยท Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni
dakika kumi baada ya kuchemka
WIVU HUU NI NOMA
Mke: Hivi mume wangu una wanawake wangapi huko nje?
Mume: Kama nywele za kichwa changu.
Mke akachukua nguo zake akaondoka, Kufika njiani akakumbuka mumewe alikuwa na kipara Akaanza kurudi kwa mumewe.
Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu.
Uaminifu ni ishara ya Upendo na tunda la uvumilivu
Uaminifu ni alama ya ushirika na Umoja
Upendo haukamiliki bila Uaminifu.
Ni kwa kiasi cha Uaminifu wako Mungu atakuhukumu
Kama unaweza kuwa mwaminifu katika jambo dogo basi hata Makubwa utakua mwaminifu.
Uaminifu ni kipimo na kigezo cha ukamilifu na utakatifu katika maisha ya kiroho. Katika safari yetu ya kiroho, uaminifu ni msingi muhimu unaoonyesha ubora wa uhusiano wetu na Mungu na wanadamu wenzetu. Uaminifu ni zaidi ya neno; ni mtindo wa maisha ambao unaakisi ndani na nje ya matendo yetu ya kila siku.
“Mtu mwaminifu atafurika baraka; bali afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.” (Mithali 28:20)
“Tena asemacho ni hiki, Kama mtu akitamani kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejizuia, anayeheshimika, mkaribishaji, ajuaye kufundisha.” (1 Timotheo 3:1-2)
“Uaminifu wako hudumu kizazi na kizazi; uliifanya imara nchi, nayo idumu.” (Zaburi 119:90)
Uaminifu ni ishara ya upendo wa kweli na tunda la uvumilivu. Upendo wa kweli hauwezi kuwepo bila uaminifu. Ni kwa kupitia uaminifu ndipo tunathibitisha upendo wetu kwa Mungu na kwa watu tunaowapenda. Uaminifu unahitaji uvumilivu kwani mara nyingi tunakutana na majaribu na changamoto nyingi katika maisha yetu.
“Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.” (1 Wakorintho 13:7)
“Basi mnapaswa kuwa na uvumilivu, ili mweze kutimiza mapenzi ya Mungu na kupokea yale ahadi.” (Waebrania 10:36)
“Katika upendo wangu nitakuimarisha. Wakati upendo wako unapokuwa imara, ndipo uaminifu wako unapokuwa thabiti.” (Hosea 2:19-20)
Uaminifu ni alama ya ushirika na umoja. Katika jamii yoyote yenye mshikamano, uaminifu unachukua nafasi kubwa. Ni uaminifu unaotuwezesha kuishi kwa amani na kuelewana. Bila uaminifu, ushirika na umoja vinaporomoka, na matokeo yake ni migawanyiko na kutoelewana.
“Ni nani awezaye kukaa katika hema yako? Ni nani atakayekaa katika mlima wako mtakatifu? Ni yeye aendaye kwa ukamilifu, atendaye haki, asemaye kweli kwa moyo wake.” (Zaburi 15:1-2)
“Mimi ni mzabibu wa kweli, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote.” (Yohana 15:5)
“Tuzingatie basi jinsi tunavyoweza kuchocheana katika upendo na matendo mema, tusikose kuhudhuria mikutano yetu, kama wengine walivyo na desturi, bali tutiane moyo; na zaidi sana kwa kadri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.” (Waebrania 10:24-25)
Upendo haukamiliki bila uaminifu. Uaminifu ndio unaofanya upendo kuwa wa kweli na wa kudumu. Bila uaminifu, upendo unakuwa na mashaka na hauna msingi imara. Hivyo basi, ni muhimu kuzingatia uaminifu katika mahusiano yetu yote.
“Watu wawili wawezaje kwenda pamoja, wasipokubaliana?” (Amosi 3:3)
“Upendo na uaminifu hukutana pamoja; haki na amani hubusiana.” (Zaburi 85:10)
“Kila kitu mfanyacho na kiwe kwa upendo.” (1 Wakorintho 16:14)
Ni kwa kiasi cha uaminifu wako Mungu atakuhukumu. Uaminifu ni kipimo cha uadilifu wetu mbele za Mungu. Mungu huangalia jinsi tunavyoshughulikia majukumu yetu, madogo na makubwa, kwa uaminifu. Tunapokuwa waaminifu katika mambo madogo, tunadhihirisha kwamba tunaweza kuaminiwa na mambo makubwa.
“Yeye aliye mwaminifu katika lililo dogo, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na yeye aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.” (Luka 16:10)
“Bwana asema hivi, Tumaini la mtu ni Bwana, Uaminifu wake huonyesha tumaini lake kwa Mungu.” (Yeremia 17:7)
“Bwana akasema, Vema, mtumishi mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.” (Mathayo 25:21)
Kama unaweza kuwa mwaminifu katika jambo dogo basi hata makubwa utakua mwaminifu. Uaminifu unajengwa hatua kwa hatua, kuanzia mambo madogo tunayofanya kila siku. Hii ina maana kwamba tunapokuwa waaminifu katika majukumu madogo, tunajijengea msingi wa kuwa waaminifu katika mambo makubwa yanayokuja mbele yetu.
“Kuwa mwaminifu hadi mauti, nami nitakupa taji ya uzima.” (Ufunuo 2:10)
“Tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu yawe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.” (2 Wakorintho 4:7)
“Nawaambia kweli, kama hamjageuka na kuwa kama watoto wadogo, hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.” (Mathayo 18:3)
Uaminifu ni kipimo na kigezo cha ukamilifu na utakatifu. Ni ishara ya upendo wa kweli na tunda la uvumilivu, na ni alama ya ushirika na umoja. Mungu atakuhukumu kwa kiasi cha uaminifu wako, na kama unaweza kuwa mwaminifu katika mambo madogo, basi hata makubwa utakua mwaminifu. Kwa hivyo, tujitahidi kuishi maisha ya uaminifu katika yote tunayofanya, tukijua kwamba tunamtumikia Mungu mwaminifu ambaye daima yupo nasi, akitubariki na kutuongoza katika njia zake za haki.
Mungu alimpenda sana binadamu hata akauvaa Mwili wa Binadamu akashuka duniani na kuishi kama Binadamu ili amkomboe Mwanadamu na hata akaamua kufa kwa ajili ya Binadamu kwa malipizi ya dhambi za Binadamu na kwa maondoleo ya dhambi.
Ni watu wachache sana duniani wanaouona upendo huu mkuu wa Mungu, wengi hawaoni wala hawataki kuona. Wapo hata wacha Mungu lakini hawaelewi upendo huu.
Mungu alimpenda sana binadamu hata akaamua kuuvaa mwili wa binadamu na kushuka duniani ili amkomboe mwanadamu. Alishuka na kuishi kama binadamu, akakubali kuteseka na kufa kwa ajili ya malipizi ya dhambi za wanadamu. Huu ni upendo mkuu ambao Mungu ametufanyia, na ni muhimu kuelewa kwa kina ukubwa wa tendo hili la ajabu.
Mungu, kwa upendo wake usio na kifani, aliona mateso na maumivu ya wanadamu na akaamua kushuka duniani kama binadamu kupitia Yesu Kristo. Aliacha utukufu wake wa mbinguni na kuja kuishi kati yetu. Yohana 1:14 inasema:
“Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:14)
Yesu alikuja na kuishi kama binadamu, akakutana na changamoto zote tunazokutana nazo, ili aweze kutuelewa na kutukomboa kikamilifu.
Upendo wa Mungu ulionyeshwa kwa namna ya ajabu pale Yesu alipokubali kuteseka na kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Alibeba mzigo wa dhambi za ulimwengu mzima na kutoa maisha yake kama sadaka takatifu. Warumi 5:8 inasema:
“Lakini Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Warumi 5:8)
Yesu hakufa kwa ajili ya wenye haki, bali kwa ajili ya wenye dhambi, ili kutupa nafasi ya kupokea msamaha na uzima wa milele.
Mungu ametufanyia kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya wokovu wetu. Alitoa mwanawe wa pekee, Yesu Kristo, ili afe kwa ajili yetu na kutuondolea dhambi zetu. Ni nini zaidi tunachoweza kumwomba Mungu ambacho hajakifanya? Hakuna upendo mkuu zaidi ya huu ambao Mungu ametufanyia. Kama ilivyoandikwa katika Yohana 15:13:
“Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.” (Yohana 15:13)
Hata kama Yesu angeendelea kuishi duniani mpaka leo, bado kungekuwa na watu wasiomwamini na kumchukia. Hii ni kwa sababu mioyo ya watu wengi imejaa ugumu na kutokuamini. Yesu mwenyewe alisema katika Yohana 15:18:
“Kama ulimwengu ukiwachukia ninyi, kumbukeni ya kwamba ulinichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.” (Yohana 15:18)
Hii inaonyesha kwamba kuna watu ambao hata wakiweka wazi upendo wa Mungu, bado watakataa na kumwona Yesu kama adui.
Ni watu wachache sana wanaoona na kuthamini upendo huu mkuu wa Mungu. Wengi hawaoni wala hawataki kuona. Wengine ni wacha Mungu lakini hawaelewi kabisa kina cha upendo huu. Hata hivyo, wale wanaoona upendo huu na kuukubali wanapata uzima wa milele na uhusiano wa karibu na Mungu. Yesu alisema katika Yohana 3:16:
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16)
Upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni mkubwa sana na umedhihirishwa kwa Yesu Kristo kushuka duniani, kuishi kama binadamu na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Mungu ametufanyia kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya wokovu wetu. Ni jukumu letu kutambua na kuthamini upendo huu, na kuishi maisha yanayodhihirisha imani na shukrani zetu kwake. Tunapoona upendo huu wa ajabu, mioyo yetu inapaswa kujazwa na furaha na amani, tukijua kwamba Mungu ametupenda sana na anataka tuwe na uzima wa milele.
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”ย ๐๐๐ย Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoย *Sipendagi Ujinga mimi* ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฝ
Huwezi kupata maendeleo kwa kusitasita na kuogopaogopa. Hata kobe anayesonga mbele ni yule anayetoa kichwa chake kwenye gamba/nyumba yake.
Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.
โKuna vitu sita unatakiwa uvitambue, โ Aliiambia penseli,
โKabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.โ
Alisema muumbaji wa penseli.
โMoja,โ alianza kuvitaja,โutakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wakoโ
โMbiliโ aliendelea kutoa nasaha, โutapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.โ
โTatu, utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya.โ
โNne, kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika.โ
โTanoโ alisisitiza mtengenezaji penseli, โkwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki.
โNa sitaโ, alimalizia muumbaji yule wa penseli, โipo siku utaisha na kupotea. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu uliombiwa kuufanyaโ
Penseli ilielewa na kuahidi kukumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.
Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.
Moja, una uwezo wa kufanya mambo mengi na makubwa, kama utajiweka kwenye mikono ya Mungu.
Mbili, utakutana na magumu mengi ya kuumiza, lakini hayo ndiyo yatakufanya uwe mtu imara na bora, usiyakimbie.
Tatu, una uwezo wa kurekebisha makosa yote uliyoyafanya. Usijilaumu.
Nne, sehemu yako ya muhimu ni ile iliyo ndani yako kwani ndiyo inayoandika maisha yako. Ilinde.
Tano, kila sehemu utakayopita, acha alama yako kwa kufanya mazuri yatakayokufanya ukumbukwe daima, bila kujali mazingira. Timiza wajibu wako kwa kiwango cha juu.
Sita, tambua kuwa ipo siku utakufa. Usiwe na hofu yoyote juu ya kifo kwani ukiogopa kifo hutafanya lolote hapa duniani.
Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumba wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza dhamira uliyotumwa na Muumba.
UBARIKIWE SANA.
Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza.
Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili.
Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: “Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka”?
Siku moja wakati nasoma biblia niliona Mungu alipotaka kumtumia Mussa kuokoa wana wa Israel akamuuliza-
โUna nini mkononi mwakoโ-
Mussa akajibu
kwa kudharau alichonacho kuwa โNina fimbo kavu tu ya kuchungia mifugoโ.
Ndipo Mungu alianza kumuonyesha miujiza kutumia fimbo ambayo siku zote
alikuwa nayo na kujidharau ndiyo ambayo ikatumika kwenda kuokoa wana wa Israel.
Watu wengi sana wanashindwa kuanza kwa sababu huwa wanajiuliza-
“Hivi ninakosa nini ili niweze kuanza”
badala ya ‘Hivi nina nini cha kuanzia’.
Cha kuanzia sio lazima iwe pesa-Inawezekana ni uwezo wa kufanya jambo fulani la kipekee,inawezekana ni
mahusiano mazuri uliyonayo na watu fulani(mtandao wako),inawezekana ni uzoefu ulionao,inawezekana ni kipaji n.k
Leo unapoanza siku yako naomba ijiulize-
โNina nini mkononi mwangu ambacho naweza kutumia katika
hatua ya kwanzaโ?.
Kumbuka hakuna mtu ambaye hana
kitu kabisa-KITAFUTE HADI UKIPATE NA ANZA KUKITUMIA KUCHUKUA HATUA.
Share ili wengine wajifunzeโฆ..uwe na Jumatatu njemaโฆโฆ..
Hakuna Maisha ya Kikristo bila Kusali. Kama kuna Mkristo anaishi bila kusali huyo siyo Mkristo bali Mkristo mfu. Sala ndiyo uhai wa Mkristo. Hakuna Njia nyingine yoyote ya kumfikia Mungu isipokua sala.
Muhogo Inazuia Minyoo na vidukari.
Angalizo:ย Tafuta ushauri wa mtaalamu wa kilimo kabla ya kutumia dawa yoyote ya asili
Sala za kila siku katika maisha ndiyo hazina kubwa na msaada hasa wakati wa kufa. Adumuye katika sala Mungu hatomwacha saa ya mwisho. Tusali, tusali, tusali daimaโฆ
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallahโฆ!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendeleaโฆ huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiโฆ
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
Binti: Hallow mpenzi, Mambo
Jamaa: Poa baby
Binti:Uko wapi?
Jamaa: Niko town napata lunch
Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Binti: Kwanini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!
Recent Comments