Mbinu 9 za kuwavutia na kuwateka wanawake kimapenzi

Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao ili wadumu katika mahusiano. Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hali kadhalika kama bado haupo Kwenye mahusiano kuna mambo ambayo ni ya msingi kufanya au kuwa nayo ili uweze kuwa na mvuto zaidi kwa wanawake.

Yafuatayo ni mambo yakufanya ili kumvutia mwanamke.

1. Kuonyesha kuwa unamjali

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali wao kama wao, wanaojali kile wanachokifanya na watu wao wa karibu kama ndugu na wazazi. Wanapenda wanaume wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa amjali mpenzi wake kwa kila hali. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Vile vile kuonyesha kujali mambo yake na watu wake wa karibu kunamvutia mwanamke.

2. Kuonyesha kuwa karibu na kupatikana unapohitajika

Mwanamke huvutiwa sana na mtu ambaye yupo karibu nae na ambaye anapatikana wakati anapohitajika. Kati ya vitu vinavyowapa wapendeza sana wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku na kushiriki katika mambo yake hata kwa mawazo kama ukishindwa kwa matendo. Ni vizuri kuwa naye au kuwasiliana naye wakati wa kula, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi na ambayo ni muhimu sana kwa wanawake. Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako, mfano kutembea pamoja, kuangalia movie pamoja, nakadhalika. Tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa kwani mwanamke anavutiwa sana na mtu aliye karibu nae.

3. Kumsifia na kumuonyesha kuwa ni bora

Wanawake wanapenda kusifiwa na kuonekana kuwa bora. Mwanamke akisifiwa anahisi kupendwa kupita kiasi. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye. Vilevile kumsifia mwanamke kwake ni njia ya kuonyesha upendo na Ishara ya kuonyesha kumjali kupita kiasi.

4. Kupewa kipaumbele

Mwanamke anavutiwa zaidi na mtu anayeonyesha kumpa kipaumbele na kupewa nafasi. Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mwanamke akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

5. Usafi binafsi

Wanawake wanapenda mwanamme ambaye ni msafi, hii ni kwa sababu kiasili wamejaliwa kupenda usafi ndio maana ni nadra sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

6. Anavutiwa na mwanamme anayejiamini

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini yaani mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia pale anapotakiwa kufanya hivyo au wakati wowote ule. Siyo anayebabaika na kuyumba yumba. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia nguo mpya.
Mwanamke anapenda kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwanamke hapendi mtu anayebadilikabadilika Kwenye maamuzi na misimamo yake.

7. Malengo ya maisha

Mwanamke anapenda mwanaume mwenye malengo na anayemshirikisha katika mipango yake. Mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenye malengo katika maisha yake. Vilevile anapenda mtu anayemshirikisha katika malengo yake na kumuweka katika mipango yake. Faida ya kumshirikisha katika malengo yako ni pamoja na kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

8. Anayeweza kujitetea

Mwanamke hupenda mwanamme anayeweza kujitetea. Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi. Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote! Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.

9. Anayemtosheleza tendo la ndoa

Mwanamke anavutiwa zaidi na mwanamme anayeweza kumridhisha katika tendo la ndoa. Anataka mwanamme anayeweza kufanya kile anachotaka yeye na kile anachokipenda. Mwanamke hapendi mwanamme anayemkomoa katika tendo la ndoa au anayefanya mambo asiyoyapenda. Mwanamke anataka kuridhishwa na kujaliwa katika tendo la ndoa.

Ili kufahamu mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu wanawake, Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Melkisedeck Leon Shine

Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp

Read and Write Comments
Shopping Cart