Tuwe wenye Hodari na wenye uwezo
Tunatakiwa tujenge uhodari na uwezo utakaotusaidia kutumia fursa zilizo wazi mbele yetu.
Tunatakiwa tujenge uhodari na uwezo utakaotusaidia kutumia fursa zilizo wazi mbele yetu.
Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.
Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima.
Kujaribu kufanya jambo kubwa la kipekee ni kushinda hata kama halijafanikiwa.
Uzuri wa kitu huvutia MACHO lakini ubora wa kitu huuteka MOYO daima. Uzuri haudumu.
Ukiweza kutumia vizuri kipaji au uwezo mdogo ulionao itakufanya uwe bora na mwenye sifa nzuri kuliko yule mwenye uwezo mkubwa.
Sio kila kizuri ni chema, lakini kila chema ni kizuri. Uzuri wa chema ni wema wake.
Tunatakiwa tujithaminishe wenyewe kwa yale tunayoona tunauwezo wa kuyafanya japokuwa watu wengine wanatuthamanisha kwa yale wanayoyaona tumeshayafanya
Biashara ya maisha ni kusonga mbele tuu. Maisha hayarudi nyuma wala hayafai kurudisha nyuma. Maisha yanasonga mbele.
Uwe mzuri kwenye kufanya kama ulivyo kwenye kufikiri. Matendo yako yafanane na maneno na maneno na matendo.
Kuacha kitu chochote kabisa moja kwa moja ni rahisi sana kuliko kufanya kitu hicho kidogokidogo kwa wastani. Usijidanganye utafanya kidogo au utaacha kidogo. Acha Kabisa na usifanye tena.
Siri kuu ya kuishinda hasira yako ni kusubiri kabla ya kutenda unapokuwa na hasira.
Changamoto na ugumu wa jambo upo kwa wale wanaolifanya. Huwezi kukaa na kutazama jambo bila kulifanya na kisha kujua changamoto zake.
Kwenye dunia hii vitu haviwezi kusimama kama havijasimamishwa.
Kama vile moto unavyozimwa na maji ndivyo vivyo hivyo hasira inamalizwa na maneno ya upole.
Recent Comments