Matendo ya mtu
Matendo ya mtu ni tafsiri kuu ya mawazo yake.
Matendo ya mtu ni tafsiri kuu ya mawazo yake.
Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa.
UMAKINI ni siri kuu ambayo wenye akili wote, wasomi na wanasayansi wanaitegemea.
Uzuri wa kitu huvutia MACHO lakini ubora wa kitu huuteka MOYO daima. Uzuri haudumu.
Kukosa mtu, kitu au jambo fulani kunasababila Moyo kujenga upendo kwenye mtu, kitu au jambo ulilolikosa.
Kwenye dunia hii vitu haviwezi kusimama kama havijasimamishwa.
Kitu chochote kinapofanywa vizuri mwanzoni ni sawa na kimefanywa nusu tayari.
Kila mtu ni mrithi wake yeye mwenyewe. Mafanikio yako ya baadae ni urithi wako ulioutengeneza hapo awali. Utajiri wako wa sasa unatokana na uliyoyawekeza miaka ya nyuma na utajiri wako ujao ni yale unayoyawekeza sasa.
Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.
Sio kila kizuri ni chema, lakini kila chema ni kizuri. Uzuri wa chema ni wema wake.
Hakuna uwezo bila fursa. Huwezi kusema unauwezo wa kitu kama hauna fursa ya kukifanya.
Uwe mzuri kwenye kufanya kama ulivyo kwenye kufikiri. Matendo yako yafanane na maneno na maneno na matendo.
Huwezi kupata maendeleo kwa kusitasita na kuogopaogopa. Hata kobe anayesonga mbele ni yule anayetoa kichwa chake kwenye gamba/nyumba yake.
Tofauti ya maskini, tajiri na mwenye uchu/tamaa ni kwamba; Mtu maskini anafanyakazi ili apate chochote, tajiri anafanya kazi apate vitu vingi lakini mwenye uchu/tamaa anafanya kazi apate vitu vyote kitu ambacho hakiwezekani kwa hali ya kawaida.
Ukiona unaweza ukakaa siku nzima bila hata kuwa na wazo moja jipya ujue umezeeka akili tayari na kesho unaweza ukawa haupo
Recent Comments