Kushindwa jambo sio Makosa
Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa.
Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa.
Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.
Kujaribu kufanya jambo kubwa la kipekee ni kushinda hata kama halijafanikiwa.
Biashara ya maisha ni kusonga mbele tuu. Maisha hayarudi nyuma wala hayafai kurudisha nyuma. Maisha yanasonga mbele.
Hakuna uwezo bila fursa. Huwezi kusema unauwezo wa kitu kama hauna fursa ya kukifanya.
Kukosa mtu, kitu au jambo fulani kunasababila Moyo kujenga upendo kwenye mtu, kitu au jambo ulilolikosa.
Ukitaka kufanya biashara kwa ufanisi; wakati wa kununua nunua ukiwa na mtazamo wa muuzaji kwa kufikiri kama wewe ungekua ndio unauza ungeuzaje, na Wakati wa kuuza uza ukiwa na mtazamo wa mnunuzi kwa kufikiri kama ungekua wewe ndiye mnunuzi ungenunuaje.
Uwe mzuri kwenye kufanya kama ulivyo kwenye kufikiri. Matendo yako yafanane na maneno na maneno na matendo.
Ukiona unaweza ukakaa siku nzima bila hata kuwa na wazo moja jipya ujue umezeeka akili tayari na kesho unaweza ukawa haupo
UMAKINI ni siri kuu ambayo wenye akili wote, wasomi na wanasayansi wanaitegemea.
Kitu chochote kinapofanywa vizuri mwanzoni ni sawa na kimefanywa nusu tayari.
Uzuri wa kitu huvutia MACHO lakini ubora wa kitu huuteka MOYO daima. Uzuri haudumu.
Ukiweza kutumia vizuri kipaji au uwezo mdogo ulionao itakufanya uwe bora na mwenye sifa nzuri kuliko yule mwenye uwezo mkubwa.
Kwenye dunia hii vitu haviwezi kusimama kama havijasimamishwa.
Unapokosa kitu ukipendacho kwa muda mfupi kinapungua thamani, ukikikosa kwa muda mrefu thamani yake yote hupotea.
Recent Comments