Matendo ya mtu
Matendo ya mtu ni tafsiri kuu ya mawazo yake.
Matendo ya mtu ni tafsiri kuu ya mawazo yake.
Siri kuu ya kuishinda hasira yako ni kusubiri kabla ya kutenda unapokuwa na hasira.
Huwezi kupata maendeleo kwa kusitasita na kuogopaogopa. Hata kobe anayesonga mbele ni yule anayetoa kichwa chake kwenye gamba/nyumba yake.
Kitu chochote kinapofanywa vizuri mwanzoni ni sawa na kimefanywa nusu tayari.
Kukosa mtu, kitu au jambo fulani kunasababila Moyo kujenga upendo kwenye mtu, kitu au jambo ulilolikosa.
Tunatakiwa tujithaminishe wenyewe kwa yale tunayoona tunauwezo wa kuyafanya japokuwa watu wengine wanatuthamanisha kwa yale wanayoyaona tumeshayafanya
Uzuri wa kitu huvutia MACHO lakini ubora wa kitu huuteka MOYO daima. Uzuri haudumu.
Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.
Kujaribu kufanya jambo kubwa la kipekee ni kushinda hata kama halijafanikiwa.
Unapokosa kitu ukipendacho kwa muda mfupi kinapungua thamani, ukikikosa kwa muda mrefu thamani yake yote hupotea.
Tamaa ni tabia ya kiasili ya kila mtu, tofauti ya mtu na mtu ni namna ya kukabili tamaa.
Sio kila kizuri ni chema, lakini kila chema ni kizuri. Uzuri wa chema ni wema wake.
Kuacha kitu chochote kabisa moja kwa moja ni rahisi sana kuliko kufanya kitu hicho kidogokidogo kwa wastani. Usijidanganye utafanya kidogo au utaacha kidogo. Acha Kabisa na usifanye tena.
Ukiona unaweza ukakaa siku nzima bila hata kuwa na wazo moja jipya ujue umezeeka akili tayari na kesho unaweza ukawa haupo
UMAKINI ni siri kuu ambayo wenye akili wote, wasomi na wanasayansi wanaitegemea.
Recent Comments