Kinga ya magonjwa na madhara yote
Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima.
Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima.
Huwezi kuona thamani ya kitu ambacho hujakigharamia. Faida haina thamani kama haijagharamiwa.
Matendo ya mtu ni tafsiri kuu ya mawazo yake.
Tamaa ni tabia ya kiasili ya kila mtu, tofauti ya mtu na mtu ni namna ya kukabili tamaa.
Kwenye dunia hii vitu haviwezi kusimama kama havijasimamishwa.
Kujaribu kufanya jambo kubwa la kipekee ni kushinda hata kama halijafanikiwa.
Kuacha kitu chochote kabisa moja kwa moja ni rahisi sana kuliko kufanya kitu hicho kidogokidogo kwa wastani. Usijidanganye utafanya kidogo au utaacha kidogo. Acha Kabisa na usifanye tena.
Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.
Sio kila kizuri ni chema, lakini kila chema ni kizuri. Uzuri wa chema ni wema wake.
Usimpe mtu ushauri ambao unahisi ataukubali sana, mpe mtu ushauri wenye manufaa kwake japo ni mgumu kuukubali.
Tunatakiwa tujenge uhodari na uwezo utakaotusaidia kutumia fursa zilizo wazi mbele yetu.
UMAKINI ni siri kuu ambayo wenye akili wote, wasomi na wanasayansi wanaitegemea.
Unapokosa kitu ukipendacho kwa muda mfupi kinapungua thamani, ukikikosa kwa muda mrefu thamani yake yote hupotea.
Uwezo wa kuwa makini katika jambo bila kuyumbishwa na kitu chochote ni ishara kuu ya mtu mwenye akili na mwenye mafanikio.
Kukosa mtu, kitu au jambo fulani kunasababila Moyo kujenga upendo kwenye mtu, kitu au jambo ulilolikosa.
Recent Comments