Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.

Umuhimu wa kutifua udongo ni kama ifuatavyo
1. Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
2. Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
3. Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
4. Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
5. Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
6. Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo

Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute

Matatizo ni nini???

`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, `
πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’πŸ€’

Walahi haya ndo matatizoπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Angalia ndoto nyingine zilivyo na Majanga

Ndoto zingine bwana usiombe zikupate

Mimi usiku wa kuamkia Leo nikiwa nimelala nimeota naendesha gari Yangu aina ya BMW mpya Mara gafla ikakwama kwenye tope .hivyo ikabidi nishuke ili kuisukuma loh! Yani kudadeki ile kuamka nikakuta nimesukuma kitanda hadi sebleni Daaa ilinisikitisha sana jiangalie sana sese hivi ndio narudisha kitanda chumbani .angalizo angalia ndoto unazo ota unaweza kuota upo baharini ukaamka unajikukuta unaogelea kwenye Jaba la Maji shauri yako.

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji kitaalamu na kwa urahisi

Mbolea ya mboji hutokana na mabaki ya majani na miti. Majani na miti yanapooza hugeuka na kutengeneza virutubisho ambavyo husaidia kurutubisha udongo na kupunguza gharama.

Mboji ikichanganywa kwenye udongo huifanya mimea kustawi na kuwa na afya ya kujikinga na magonjwa yanayoshambulia mimea. Kwa kawaida wadudu waharibifu hutafuta mimea ambayo ni dhaifu. Udongo ambao umeimarishwa kwa mboji huwa na mimea michache dhaifu. Kwa hivyo, siyo rahisi kushambuliwa na wadudu.

Mbolea ya mboji ina madini yanayosaidia kuyeyusha madini mengine yaliyo kwenye udongo na kufanya yapatikane zaidi kwa ajili ya mimea kwa muda mrefu. Vijidudu ambavyo hujilisha kwa njia ya mbolea ya mboji kwa muda mfupi hushikilia udongo pamoja, na kuufanya udongo uwe bora na wenye afya.

Faida nyingine ya mbolea ya mboji ni kwamba mbolea hii hupunguza ama huondoa kabisa utumiaji wa mbolea za chumvichumvi na dawa za kuua wadudu ambazo zinaweza kuwa na madhara kwa afya za watu na udongo, ambazo pia ni gharama sana kununua.

Mahitaji ya kutengenezea mboji

Wakati wa kutengeneza mboji unahitajika kuwa na malighafi za kijani na kahawia.

Malighafi za kijani
Mimea yenye kijani kibichi na ambayo haijachanua inafaa zaidi katika kutengezeza mboji, na iwe imekatwa karibuni. Mabaki ya chakula na matunda pia yanajumuishwa katika kundi la malighafi za kijani.

Malighafi za Kahawia
Kundi la malighafi za kahawia ni pamoja na mimea ambayo imekauka baada ya kukatwa muda mrefu, pamoja na kinyesi cha wanyama wafugwao. Udongo na maji ni sehemu muhimu ya mahitaji kwa ajili ya kutengeneza mboji.

Vitu visivyotakiwa kwenye mboji

  • Mabaki ya mimea ambayo imeambukizwa magonjwa au imeshambuliwa na wadudu haitumiwi kwani inaweza kuwa na mayai ya wadudu na inaweza kuendelea kuzaliana.
  • Mimea yenye tindi kali kama vile migunga na Eucalyptus haifai, ijapokuwa kuna wakati inaweza kutumika kutengeneza mboji maalum kwa ajili ya kuongeza kiwango cha tindi kali kwenye udongo inapohitajika.
  • Magugu sugu kama sangare, mashona nguo na ukoka mgumu hayafai kwa kuwa yatasambaza mbegu za magugu katika shamba lako.
  • Usitumie kinyesi cha wanyama kama mbwa na paka.

Kutengeza mboji

Ili uweze kutengeneza mboji nzuri, unatakiwa kurundika rundo kwa matabaka. Kiwango cha wastani kinachofaa kutengeneza mboji ni chenye urefu wa mita moja, na mita moja upana. Rundo ambalo ni dogo kuliko hili haliwezi kuhifadhi joto la kutosha kuozesha malighafi. Hakuna kikomo cha ukubwa wa biwi la mboji, inategemea na ukubwa wa eneo ulilonalo na unataka mboji kiasi gani. Chakuzingatia ni kuwa lisiwe dogo.

Hatua za kufuata kutengeneza mboji

Hatua ya 1
Ondoa majani yote pamoja na vitu vingine vinavyoweza kuharibu mboji yako, kisha lainisha udongo kiasi cha inchi sita kwa kutumia rato au jembe. Hatua hii inasaidia maji kupenya chini
ya rundo la mkusanyiko wa kutengenezea mboji.

Hatua ya 2
Weka tabaka la kwanza kubwa kuliko matabaka mengine. Unaweza kutumia majani makavu, mabuwa ya mahindi na matawi madogo madogo ya miti. Vitu hivi pia ni vizuri kwa rundo la mboji na hurahisisha umwagiliaji maji. Weka rundo la tabaka la kwanza la mabuwa ya mahindi vijiti na matawi madogomadogo ili liwe tabaka lenye inchi sita kwa mita moja kila upande.

Hatua ya 3

Tengeneza tabaka la pili lenye ukubwa wa inchi mbili na malighafi za kijani. Kumbuka kwamba: Tabaka liwe jemjembamba kuliko tabaka la kwanza. Kama una mabaki ya chakula ongeza kwenye tabaka hili.

Hatua ya 4

Weka Tabaka la tatu la udongo lililochanganywa na mbolea au majivu. Tabaka hili liwe jembamba, kama unene wa robo inchi. Unahitaji kutumia kiasi kidogo tu cha mbolea kufunika sehemu ndogo tu katikati ya rundo la mboji kama vile futi moja kwa futi moja. Ni muhimu kutotumia mbolea nyingi kwenye rundo la katikati. Kama unatumia majivu, kiasi kidogo tu kitumiwe katikati ya rundo la mboji. Ukishaweka mbolea katikati, unaweza kuizungushia udongo kufunika tabaka la kwanza.

Hatua ya 5

Ongeza maji ya kutosha kila wakati kwenye rundo la mboji ili liwe na unyevunyevu, lakini yasiwe mengi kiasi cha kutota. Kumbuka, rundo la mboji liwe na unyevunyevu mfano wa sponji iliyowekwa kwenye maji na kukamuliwa.

Hatua ya 6

Kwa kufuata hatua zilizotangulia, kama unataka kuongeza matabaka, rudia kama ulivyofanya mwanzo. Tabaka la majani makavu, ya rangi ya kahawia lenye inchi mbili, likifuatiwa na tabaka la kijani la inchi mbili, likifuatiwa na tabaka jembamba la udongo uliochanganywa na mbolea au majivu au vyote. Endelea kuweka matabaka haya mpaka matabaka yako yawe na urefu wa futi tatu au nne kwenda juu.

Hatua ya mwisho

Weka tabaka la juu mwisho lenye majani makavu ya kikahawia lenye unene wa inchi tatu. Hii husaidia kuhifadhi harufu ambayo wakati mwingine hutokea wakati wa uozaji. Hii pia husaidia kufukuza wanyama ambao huvutiwa na kutaka kuona kuna nini kwenye rundo la mboji.

Baada ya muda Rundo la mboji litakapokuwa tayari, utabakiwa na mboji ambayo itaonekana kama udongo mweusi ulio na mbolea nzuri.

Matumizi ya mbolea ya Mboji

Chukua mboji ambayo ni tayari yani iliyo na udingo mweusi wenye mbolea nzuri na utandaza tabaka jembamba kwenye mazao yako na mimea itastawi, kunawiri vizuri na kutoa mazao bora.

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Angalia huyu mwalimu alichokifanya

Mwalimu aliingia darasani akiwa amechoka kinoma
akawambia wanafunzi.

‘leo tutajifunza kipindi cha
dini ” wanafunzi wakiwa wanajiandaa ili kuendelea
na kipindi mwalimu akajiegesha kwenye kiti klichokua
karibuu yake baada ya dakika kadhaa mwalimu alipitiwa
na usingizi, ghafla alingia mkurugenzi na
kusimama pembeni mwa kile kiti alichokalia mwalimu
ghafla kmya kikatawala darasani kiasi cha kunfanya
mwalimu ashtuke usingizini aliamka huku akipiga
miayo alpotupa jicho pembeni alimuona mkurugenzi
kasimama pemben! akiwa anababaika alifungua
kinywa na kusema ‘ Hivi ndivyo walivyolala wanafunzi
wa YESU walipokua wakimsubli kule mlimani, je
kuna mwenye swal? mkurugeni pale alipokua
akapiga makofi na kumsifia mwalimu kwa kufundisha
kwa vitendo.

Je % Ngapi unampa mwalimu kwa
kusolve kibarua chake.????

Mapishi ya Ugali, dagaa (wabichi) na matembele

Mahitaji

Dagaa wabichi (Fresh anchovies packet 1)
Unga wa ugali (corn meal flour 1/4 kilo) (unaweza kutumia unga wa choice uipendayo)
Matembele ya kukaushwa (dried sweet potato leaves, handful)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
Kitunguu maji (onion 2)
Limao (lemon 1/4)
Pilipili mbuzi nzima bila kukata (scotch bonnet pepper1, do not chop)
Chumvi (salt 1/2 ya kijiko cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Hoho (green pepper 1)
Kitunguu swaum (garlic 5 cloves)
Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
Binzari ya curry (Curry powder 1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho

Safisha dagaa kwa kutoa vichwa na utumbo kisha waoshe na uwakaushe na kitchen towel na uwaweke pembeni. Baada ya hapo katakata, vitunguu na hoho kisha weka pembeni. Baada ya hapo weka sufuria jikoni na utie mafuta yakisha pata moto tia dagaa na uwakaange mpaka wawe wa brown, kisha tia kitunguu swaum,curry powder na tangawizi, kaanga kidogo kisha malizia kwa kutia vitunguu maji, hoho,pilipili,chumvi na ukamulie limao. Kaanga kwa muda wa dakika 3-4 na hakikisha vitunguu na hoho haviivi sana na hapo dagaa watakuwa tayari.

Baada ya hapo yaoshe na uyaloweka matembele (kama ni makavu) kwa muda wa dakika 15, Kisha yatoe na uyaweke kwenye sufuria pamoja na kitunguu, nyanya, chumvi ,kamulia limao kidogo, pilipili na maji kiasi. acha matembele yachemke kwa muda wa dakika 20 na uhakikishe yameiva kwa kuwa laini. Baada ya hapo yapike mpaka maji yote yakauke na mafuta yatok na hapo matembele yatakuwa tayari.

Ukisha maliza kupika dagaa na matembele andaa chungu cha ugali. Kwanza unatakiwa kuchemsha maji ya moto, kisha koroga pembeni unga kiasi katika maji ya baridi na utie kwenye maji yanayochemka, Fanya kama unatengeneza uji, uji wa ugali ukishachemka tia unga na uanze kuusonga mpaka ugali uive. Ukisha iva pakua na usevu na mboga tayari kwa kuliwa.

Mambo ya Msingi kujua kuhusu uvaaji wa Tai

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi.

Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?

Wengine huwa hawafahamu jinsi ya kufunga tai na hivyo kuleta mushkeri wakati wa kuvaa tai na kusababisha tai kukaa upande. Unapoamua kuvaa tai na shati ambalo halijanyooshwa ambalo linakuwa kwenye mikunjo au kuvaa tai na ndala unakuwa umeua maananzima na kulivunjia heshima vazi hili.

Tai ni vazi lawatu walio maridadi kama huwezi kuwa maridadi basi vazi hili halikufai kabisa.
Unapovaa taa unatakiwa kuzingatia aina ya umbo lako kama wewe ni mnene vaa tai inayoendana na mtu mnene na kama wewe ni mwembamba basi vaa tai inayoendana na mtu mwembamba.

Kuna wengine huvaa tai zinazofika magotini na kuwa kichekesho anapopita mtaani
Tai ni vazi ambalo huongeza heshima na hadhi ya mvaaji cha muhimu ni jinsi gani unavaa tai yako na ikiwezekana jaribu kumechisha tai na suruali kwa vile ili tai upendeze ni laima iendane na nguo unayovaa.

Ni vyema ukahakikisha kuwa unakuwa na tai zenye rangi tofauti ambazo zitaendana na nguo unazovaa.

Amri za chuo

Ndio hizi sasa

1.Hicho ndicho chuo chako usiwe na chuo kingine ila hicho.
2.Usilitaje bure jna la chuo chako mana utawaumiza wengine.
3.Ikumbuke cku uliyochaguliwa na kuiheshimu.
4.Waheshimu tcu, bodi ya mkopo na uongoz wa chuo ili upate kuendelea kuwepo chuon.
5.Usisapu
6.Usidisko
7.Usitumie mkopo ovyo.
8.Usitaman chuo cha mwenzio
9.Usitamani fakat ya mwenzio
10. Usitaman bumu lake wala chochote alichonacho. hahaha chezea chuo weye!

Haya mapenzi jamani! Umewah kumpenda kwa kihivi??

Sijui Kama ushawai fall in love ile haswaa..

yani unampenda mtoto hadi akikupigia ile sauti ilivo tamu unajiskia kutafuna na kuimeza hiyo simu

Akikuita tu “my love”unajiskia tu kuvua nguo mwenywe
..
hicho kiupendo ukiwa nae unajskia unaweza piga wanaume 8 kwa pamoja

Yani ile love mtashinda pamoja kutwa nzima afu usiku unakopa salio umpigie muongee

Yani yale mapenz kiasi ukiona love story za romeo na Juliet unaona hakuna wanachofanya coz mapenz yao hayafikii yenu..

ile true love akikuangalia machoni akuguse mashavu afu akwambie,”I love u”
Unajishikilia kwenye ukuta usizimie..

yani ukimfikiria unaweza kulala chini ya kitanda Ku dilute hiyo feeling coz ni too much..

Umewahi kufeel hivyo??

Kama ushawai experience hivyo?? Basi HIYO SIYO “LOVE” NI “BANGI” PLZ ACHA KUTUMIA!
#ishakua_biashara_kichaa

Namna ya kutengeneza Visheti Vya Nazi Na Njugu (Sudani)

VIAMBAUPISHI

Unga – 3 mug za chai

Samli – Β½ mug ya chai

Maziwa – 1ΒΌ mug ya chai

Baking powder – 2 vijiko vya chai

VIAMBAUPISHI VYA MJAZO

Njugu zilizomenywa vipande vipande – 2 vikombe cha chai

Sukari – Β½ kikombe cha chai

Iliki – 1 kijiko cha chai

Nazi iliyokunwa – 2 vikombe vya chai

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari – 2 vikombe vya chai

Maji – 1 kikombe cha chai

Ndimu – 1

JINSI YA KUVIANDAA

1-Changanya unga na samli kisha tia baking powder na maziwa. Ukande ulainike kisha

uwache kama dakika 5 uumuke.

2-Kwenye bakuli nyingine changanya njugu, sukari na iliki.

3-Kata madonge madogo dogo sukuma kila donge duara jembamba, kisha tia kijiko cha mchanganyiko wa njugu juu yake ifunikie juu yake na ibane pembeni.

4-Panga kwenye treya isiyoganda (non stick) kisha choma kwenye oven kwa moto wa chini

(bake) 350Β° C kwa dakika kama 15-20.

5-Chemsha maji na sukari katika sufuria ndogo kisha tia ndimu acha ichemke mpaka inatenate unapoigusa.

6-Kwenye sahani ya chali mimina nazi iliyokunwa.

7-Vibiskuti vikiwa tayari vya motomoto chovea kwenye shira kisha zungushia katika nazi iliyokunwa,

panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Wali na kuku wa kienyeji

Mahitaji

Kuku wa kienyeji (boiler chicken 1)
Mchele (rice 1/2 kilo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
Vitunguu (onion 2)
Vitunguu swaum (garlic cloves 6)
Tangawizi (ginger)
Carry powder
Binzari ya njano (Turmaric 1/2)
Njegere(peas 1/2kikombe)
Carrot iliyokwanguliwa 1
Limao (lemon 1)
Bilinganya (aubergine 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Loweka mchele kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka uive.
Chemsha kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali.

Jinsi ya kuandaa Wali Wa Hudhurungi Na Kabeji

VIPIMO VYA WALI

Mchele wa hudhurungi (brown rice)

na (wild rice kidogo ukipenda)Osha na Roweka – 2 Vikombe

Kitungu maji – 1 Kiasi

Kitunguu saumu – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano – 1/2 Kijiko cha chai

Mdalasini nzima – 1 kijiti

Iliki iliyosagwa – 1/4 Kijiko cha chai

Chumvi – Kiasi

Pilipili manga – 1/4 Kijiko cha cha

Mafuta – 2 Vijiko vya supu

Majani ya Bay(bay leaves) – 1

Mbegu ya giligilani iliyoponwa (coriander seeds) – 1 Kijiko cha chai

Supu ya kuku ya vidonge – 1

Maji ya wali – 4 vikombe

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kaanga kitungu, kabla ya kugeuka rangi tia thomu.
Kisha weka bizari zote na ukaange kidogo.
Tia mchele kisha maji na ufunike upike katika moto mdogo.
Na ikishawiva itakuwa tayari kwa kuliwa na kabeji na kuku wa tanduuri.

VIPIMO VYA KABEJI

Kabeji iliyokatwa katwa – 1/2

Karoti iliyokwaruzwa – 1-2

Pilipili mboga kubwa – 1

Figili mwitu (celery) iliyokatwa – 1 au 2 miche

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi – 1

Kisibiti (caraway seed) – 1/4 Kijiko cha chai

Bizari ya manjano ya unga = 1/2 Kijiko cha chai

Giligani ya unga – 1 Kijiko cha chai

Chumvi – Kiasi

Kitungu maji kilichokatwa -1

Kotmiri – upendavyo

Mafuta ya kukaangia – Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kwenye sufuria kaanga kitungu, figili mwitu kisha tia thomu na pilipili zote.
Halafu tia bizari zote na ukaange kidogo.
Kisha weka kabeji na chumvi, ufunike moto mdogo ilainike kidogo na sio sana
Tia karoti na usiwache motoni sana, kisha zima moto na inyunyizie kotmiri juu.

Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele

Faida ya Mafuta Ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele.

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara

2. Yanasaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa

3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele

4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.

5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.

NAMNA YA KUZIHUDUMIA NYWELE:

Unaweza kuchanganya na Mdalasini pamoja na Asali.

1. Olive oil vijiko 2 vya chakula

2. Asali kijiko 1 cha chakula

3. Mdalasini kijiko 1 cha chai

Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja pakaa kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka.

Ninashauri utumie mafuta haya kwenye nywele na ngozi ni mazuri sana. Ukiwa na mba pakaa kwenye ngozi mba itaisha na muwasho utaondoka.

JE, WAKATOLIKI WANABUDU SANAMU?

Mpenzi msomaji, kumekuwa na tuhuma nyingi dhidi ya wakatoliki kwamba wanaabudu sanamu. Je, tuhuma hizo zina ukweli gani? Hilo ndilo swali tunalotaka kujibu leo.
Amri ya kukataza ibada kwa sanamu imewekwa wazi katika Biblia Takatifu, Kutoka 20:4-5, β€œUsijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Sheria hiyo inapatikana pia katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 5:8-9: β€œUsijifanyie sanamu za miungu za kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Isivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu.”
Ni kutokana na vifungu hivyo vya Maandiko Matakatifu, Waamini wa Kikatoliki wamekuwa wakituhumiwa, kushtakiwa na kushambuliwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine kwamba wanapingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu, yanayokataza ibada kwa sanamu. Tuhuma hizo zinakuwa nzito zaidi, hasa zinapohusishwa na Ibada inayofanywa na Waamini Wakatoliki siku ya Ijumaa Kuu kila mwaka.

KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU

Mpenzi msomaji, kuna tofauti kubwa kati ya kuabudu na kuheshimu. Kamusi ya Kiswahili ya Maana na Matumizi, ya mwaka 1993, iliyoandikwa na SALIM K. BAKHRESSA, na kuchapishwa na OXFORD UNIVERSITY PRESS, DAR ES SALAAM, inaeleza kuwa neno β€œkuabudu” maana yake ni β€œkuomba au kufanya ibada”; na neno β€œkuheshimu” maana yake ni β€œkutukuza, kustahi au kuogopa.”
Katika maana yake ya ndani, anayeabudiwa na mwenye haki ya kuabudiwa ni Mungu peke yake. Hakuna mtu, kiumbe wala kitu chochote kinachopaswa kuabuduiwa na chenye haki ya kuabudiwa. Mtu, kiumbe au kitu hupewa heshima tu, tena ya kiwango maalum. Kwa mfano, Bikira Maria, kwa sababu ya nafasi yake katika kazi ya ukombozi, anapewa heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Watakatifu hao wengine hupewa heshima ya kadiri tu, chini ya heshima ile anayopewa Bikira Maria.

KWA NINI MUNGU PEKE YAKE ANASTAHILI KUABUDIWA?

Tumesema ni Mungu pekee yake, ndiye anayestahili kuabudiwa, kwa sababu ndiye MUUMBA wa vitu vyote, vinavyoonekana na visivyoonekana; ndiye anayevitawala na kuviongoza vitu vyote; ndiye mwenye uwezo juu yetu sisi wanadamu na viumbe vingine vyote; ndiye anayejua yote; ndiye aliye pote kwa ajili yetu; ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu; ndiye mkuu na Bwana wa wote.
Aidha, tunapomwabudu Mungu, tunakiri kwamba ndiye aliyetuumba na β€œndani yake yeye sisi tunaishi, tunajimudu na tuko!” (Mdo.17:28). Kwa kufahamu hilo, Wakatoliki hawawezi kumwabudu mtu, kiumbe au kitu chochote, isipokuwa Mungu tu.

MAMBO MAKUU NA MUHIMU KATIKA IBADA YA SANAMU

Ili kufahamu vema kinachofanywa na Wakatoliki ni vema kufuatilia na kutafakari yale wanayoyafundisha na kuyasadiki wao wenyewe, badala ya kuwahukumu kadiri watu wengine wanavyofikiri na kusema. Ukweli ni kwamba hakuna Ibada yoyote ya sanamu katika Kanisa Katoliki. Hilo ni dhahiri kwa sababu ili ibada ya sanamu iwe kweli kuabudu sanamu lazima yawepo mambo makuu na muhimu mawili: Kwanza, NIA KAMILI YA KUABUDU SANAMU INAYOHUSIKA;
Pili, KUWEPO NA IBADA YA DHATI YA KUABUDU SANAMU. Ikitazamwa kwa makini, hayo mambo mawili yanakosekana katika Kanisa Katoliki linapokuja suala la picha na sanamu. Kwa hiyo, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala picha. Kama ni hivyo, wakatoliki wanafanya nini na hizo sanamu au picha? Wanaziheshimu tu! Tukumbuke kuwa anayemwabudu mtu, kiumbe au kitu, ni sharti akihesabu na kukisadiki kuwa ndicho kinachomwezesha kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake (Rej. Mdo.17:28).

JE, BINADAMU TUNAHITAJI SANAMU AU PICHA?

NDIYO. Binadamu tunahitaji sananmu au picha, tena ni jadi yetu! Kwa sababu gani tunahitaji picha maishani mwetu? Kwa sababu katika udhaifu wetu, mara nyingi tunaweza kufikiri vema kwa kutumia vielelezo au vichokoo vyenye kuonekana na kugusika. Kwa njia ya vielelezo hivyo, binadamu tunaweza kuyafikia kwa urahisi mambo magumu na mafumbo yaliyo juu ya fikra zetu za kawaida. Ndiyo maana tukiona picha au sanamu ya Yesu au Mama Maria au Watakatifu wengine, akili zetu zinaweza kutafakari mambo matakatifu na kupata picha ya kina cha msamaha wa dhambi na mapendo ya Mungu kwetu wanadamu.

KWA NINI WAKATOLIKI HAWAABUDU SANAMU AU PICHA?

Wakatolikihawaabudu sanamu kwa sababu wanajua kwamba Mungu pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa. Kwa hiyo, hawaziabudu sanamu au picha kwa sababu wanajua kwamba hivyo siyo Mungu. Zaidi hayo, wanajua kwamba Mungu mwenyewe amekataza kuziabudu sanamu na picha kwani hazina daraja la Muumba. Mungu amepiga marufuku kuzigeukia na kuzisujudia (Law.19:4). Aidha, wameaswa kuziepuka sanamu na Ibada kwa sanamu – β€œWatoto wangu, epukaneni na sanamu za miungu!” (1Yoh.5:21). Pia wakatoliki wanajua kuwa sanamu na picha hazina uwezo wowote wa kimungu. β€œMungu wetu yuko mbinguni, hufanya yote anayotaka. Miungu yao ni fedha na dhahabu; imetengenezwa na mikono ya wanadamu. Ina vinywa lakini haisemi. Ina macho lakini haioni. Ina masikio lakini haisikii. Ina pua lakini hainusi. … Wote wanaoitengeneza wanafanana nayo, kadhalika na wote wanaoitumainia. Enyi wa nyumba ya Israeli mtumainieni Mwenyezi Mungu, yeye ndiye msaada wenu na ngao yenu” (Zab.115:3-9). Pia kuziabudu sanamu ni jambo la kidunia, ambalo haliwezi kumpeleka mtu peponi (Rej. Isa.45:16; Isa.45:20; Gal.5:20). Kwa hiyo, Wakatoliki wanajua kuwa kuabudu sananmu na picha ni jambo haramu kabisa mbele ya Mungu, Mwumba wao (1Pet.4:3-4).

IBADA YA KWELI YA SANAMU INAKUWAJE?

Ibada ya kweli ya sanamu siyo rahisi hivyo, kama baadhi ya watu wanavyodhani! Ibada ya kweli ya sanamu siyo kitu cha mchezomchezo, kama baadhi ya watu wanavyofikiri na kusema. Ibada ya Sanamu ni suala la kuabudu, na kuabudu siyo suala la kuwa na kitu au kikiheshimu tu, bali ni kwenda mbali zaidi ya hapo! Hivyo kumiliki sanamu au picha, mathalani majumbani au kanisani, hakusemi lolote juu ya uwepo wa ibada ya sanamu kwa wale wanaohusika nazo. Kwa hiyo, ikiwa watu hawazipi sanamu au picha hizo mahali pa Mungu wa kweli, basi hawana hatia yoyote.
Jambo muhimu hapa ni kwamba wamiliki wa sanamu au picha hizo wanaziheshimu tu huku wakijua kuwa wenyewe wanaowakilishwa na sanamu au picha hizo hawapo pale kwa hali halisi. Katika maana hiyo, inakuwa sahihi kabisa kuziheshimu picha za marais, ndugu na marafiki wetu tunaowapenda, ambao hawapo karibu nasi. Picha zao hatuzikejeli wala hatuzibwagi chini na kuzikanyaga au kuzitia vumbi. Hatufanyi hivyo, siyo kwa sababu tunawaabudu watu hao au vitu hivyo, bali kwa sababu tunawapenda na kuwathamini wenyewe katika hali zao halisi.
Kwa mfano ikiwa tuna kitabu cha picha (Album) chumbani, chenye picha 100 za ndugu, rafiki na jamaa zetu, hatusemi tuna miungu 100 tunaowaabudu nyumbani mwetu! Vinginevyo, mambo yangetisha sana majumbani mwetu! Wenye picha hizo hatuwaabudu kamwe, ila tunawapa heshima tu kwa sababu tunawajali na kuwapenda. Kwa nini tusiwape heshima hiyo, ambayo ni kitu cha bure! Ukweli huo pia unahusu Bendera ya Taifa, Wimbo wa Taifa, nk.

JE, MUNGU ANACHUKIA KILA SANAMU NA PICHA?

Mungu hachukii kila sanamu au picha. Hapa inafaa ieleweke vema kwamba Mungu alipopiga marufuku sanamu katika Kitabu cha Kut. 20:3-5 na Kumb. 5:7-10, hakupiga marufuku kila sanamu. Yeye mwenyewe anaonesha kwamba anazichukia sanamu zinazotengenezwa kusudi zichukue nafasi yake tu. Kama sanamu au picha hazihatarishi nafasi yake, hana maneno nazo! Ndiyo maana, basi, baada ya kumwagiza MUSA awaambie watu wasizitengeneze sanamu na kuziabudu kama miungu (Kut.20:4-5), alimwagiza MUSA huyo huyo azitengeneze sanamu zisizokuwa hatari, ambazo hazikupewa daraja la Mungu. Mungu alimwagiza MUSA kutengeneza sanamu katika nafasi mbili:
(i) Musa anaagizwa atengeneze sanamu mbili za Makerubi azibandike kwenye Sanduku la Agano wakifunike kiti chake cha rehema. β€œUtatengeneza pia mfano wa viumbe hai viwili kwa kufua dhahabu, uwaweke kwenye miisho miwili ya kiti hicho; kiumbe kimoja mwisho mmoja na kiumbe mwingine mwisho mwingine. Waweke viumbe hao kwenye miisho ya hicho kiti, lakini wawe kitu kimoja na hicho kiti. Viumbe hao wataelekeana, mabawa yao yamekunjuka kukifunika kiti cha rehema, nyuso zao zitakielekea kiti hicho” (Kut.25:18-20; Rejea pia Ebr.9:5).
(ii) Mungu alimwagiza pia Musa atengeneze Nyoka wa Shaba kama dawa kwa wale ambao waling’atwa na nyoka wa moto kule Jangwani. Musa alielezwa wazi kwamba wale ambao wangemtazama huyo nyoka wa shaba kwa imani kwa Mungu wa Israeli wangepona. β€œNdipo naye Mwenyezi Mungu akamwambia Musa: Tengeneza Nyoka wa shaba, umtundike juu ya mlingoti. Mtu yeyote atakayeumwa na nyoka, akimtazama nyoka huyo wa shaba, atapona. Basi, Musa akatengeneza nyoka wa shaba, akamtundika juu ya mlingoti. Kila mtu aliyeumwa na nyoka alipomtazama huyo nyoka wa shaba, alipona” (Hes. 21:8-9; Rejea pia Yoh.3:14-15).
Basi, Musa alitekeleza maagizo hayo ya Mwenyezi Mungu, naye alifurahia. Kwa maagizo hayo mawili ni dhahiri kwamba Mungu hachukii kila sanamu au picha. Mungu anachukizwa na sanamu zile ambazo zimekusudiwa kuchukua daraja la umungu wake, maana ni yeye tu ndiye anayestahili kuabudiwa. Yule nyoka wa shaba alikuwa dawa kwa wale walioumwa na nyoka wa moto. Watu hao hawakumwabudu nyoka wa shaba, lakini walipona, siyo kwa sababu ya nguvu zake, ila kwa nguvu za mwokozi zilizokuwa nyuma yake. β€œKama mtu akiitazama alama hiyo aliponywa, lakini kilichomponya siyo hicho kitu alichokiona, bali wewe uliye Mwokozi wa watu wote” (Hek.16:7).
Hapa ni vifungu vingine vya Maandiko Matakarifu, vinavyoonesha kuwa Mungu hachukii kila sanamu au picha.
1Fal. 7:29 β€œkulikuwa na sanamu za simba, mafahali na viumbe vyenye mabawa. Sanamu hizo za simba na mafahali zilikuwa, zimefunikwa na kutandikwa mapambo yaliyosokotwa vizuri”.
2Nyak.3:10 β€œAlitengeneza sanamu mbili za viumbe wenye mabawa kwa mbao, akazifunika kwa dhahabu na kuziweka mahali patakatifu sana”
Ezek.41:17-18 β€œβ€¦ kwenye ukumbi palikuwepo na michoro iliyofanana na mitende na picha za viumbe vyenye mabawa. Kila baada ya mtende kulichorwa picha ya kiumbe chenye mabawa kukizunguka chumba chote”.
Yoh. 3:14-15 β€œKama vile Musa alivyomwinua yule nyoka wa shaba kule Jangwani, naye Mwana wa mtu atainuiliwa juu vivyo hivyo, ili kila anayemwamini awe na uhai wa milele.”
Ebr.9:5 β€œJuu ya hilo sanduku kulikuwa na viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya mahali ambapo dhambi huondolewa”

UBAYA WA SANAMU AU PICHA UKO WAPI?

Ubaya wa sanamu au picha upo katika kuzipa sanamu au picha daraja la Mungu. Hatari na ubaya wa sanamu au picha vimo katika kitendo cha binadamu kuzipa sanamu au picha hizo daraja la Mwenyezi Mungu. Kama sanamu au picha hazipewi daraja la Mungu, haziwi hatari na wala hazina ubaya wowote mbele ya Mungu. Kwa sababu hiyo, basi, mtu anaweza kuwa na sanamu au picha ndani ya nyumba yake au kanisani, lakini bila kumkasirisha Mungu.
Zaidi ya hayo, Mungu mwenyewe anajua fika kuwa sanamu au picha fulani imepewa daraja lake au siyo. Kwa nini Mungu akasirike pale ambapo sanamu au picha haziingilii daraja na ukuu wake? Mungu mjinga wa aina hiyo hayupo! Mungu wa kweli hawezi kukasirikia picha na sanamu ambazo zinaheshimiwa tu, na wala haziabudiwi. Aidha, Mungu mwenye haki hawezi kumwadhibu na kumtupa Jehanamu mtu ambaye anamiliki picha au sanamu duniani lakini bila kuziabudu, yaani pasipo kuzipa daraja la Mungu.

BIBLIA INAWEZA KUTUSAIDIA KUIELEWA IBADA YA SANAMU?

Jibu ni ndiyo! Biblia inatoa maelezo ya kina na ufafanuzi mzuri juu ya ibada ya sanamu. Tumesema hapo juu kuwa ibada ya sanamu siyo jambo la mzaha au mchezo wa kitoto! Ni suala la kuabudu, na kuabudu siyo tu jambo la kuwa na sanamu au picha na kuiheshimu tu. Ni zaidi ya hapo! Kuna mambo muhimu ambayo lazima sanamu zitendewe, ndipo ihesabike kuwa ni ibada ya sanamu.
a) Tukitaka kujua kama kitendo fulani mbele ya sanamu ni kuabudu au sivyo, kwanza lazima iwepo nia thabiti ya mtu anayehusika katika kitendo hicho kinachofanyika. Ibada inakuwa ya kuabudu sanamu ikiwa mtu anayefanya kitendo hicho anaamini moyoni mwake kwamba hiyo sanamu au picha inayofanyiwa kitendo hicho inachukua daraja na nafasi ya Mwenyezi Mungu. Katika kitendo hicho, mtu anaamini kuwa sanamu au picha hiyo ndiyo inayomwezesha kwenda, kuishi, kujimudu na kuwa na uhai wake hapa duniani.
b) Jambo la pili ni kuangalia kama kitendo hicho kinachofanyika katika ibada hiyo ni Liturujia ya kueleweka/maalum. Baada ya kubaini nia thabiti ya mtendaji, tunaweza kuitambua ibada ya sanamu kwa kuangalia yale yanayofanyika mbele ya sanamu au picha kwa kufuatilia mambo ambayo waabudu sanamu huyafanya. Mambo hayo, ambayo waabudu sanamu wanayafanya tunaweza kuyakusanya kutoka katika Biblia yetu. Agano la Kale linaonesha kuwa Ibada ya Kuabudu Sanamu inajumuisha mambo makuu yafuatayo:
i. Kuzitolea sadaka: za kuteketezwa: Rej. Hos.4:13; nafaka na vyakula 2Fal.5:17.
ii. Kuzitolea ubani kwa heshima kamili: Rej. 1Fal.11:8; Isa. 57:6; Yer.7:18.
iii. Kuzimwagia matambiko: Rejea Isa. 57:6
iv. Kuzitolea zaka ya sehemu ya kumi ya mapato ya mwaka ya mazao ya mashambani: Rejea Hosea 2:8
v. Kuziandika meza mbele yao: Rejea Isa. 65:11
vi. Kuzibusu sanamu kwa kuzisujudia kama viumbe vyenye enzi.
Rejea 1Fal. 19:18; Hos.13:2; Ayu. 31:2.
vii. Kuziinulia sanamu mikono katika kuzisujudia: Rejea Isa.44:20
viii. Kuziangukia sanamu kifudifudi ama kuzipigia magoti kwa kuziabudu: Rejea 1Fal.18:26,28.
ix. Kuzichezea ngoma na wakati mwingine kujikatakata kwa visu kama kitendo cha ibada kwa sanamu: Rejea 1Fal.18:26,28.
Hayo yote yakichunguzwa kwa makini, tutaona wazi kuwa hakuna Ibada ya kuabudu sanamu katika Kanisa Katoliki. Kwa hiyo, shutuma kwamba Wakatoliki wanaabudu sanamu siyo za kweli, hazina msingi, na ni uchochezi wa bure wenye lengo la kuleta mafarakano na magomvi. Jambo hilo ni dhahiri kwa sababu Wakatoliki hawana nia thabiti ya kuabudu sanamu wanapotoa heshima kwa sanamu au picha mbalimbali. Pili, matendo ya kiliturujia yanayofanywa na wakatoliki katika kuheshimu sanamu hayalingani na matendo ya kiliturujia yanayofanywa na waabudu sanamu, kama ilivyoelezwa katika Biblia Takatifu, hususan Agano la Kale. Kifupi, wakatoliki hawana nia thabiti moyoni ya kuziabudu sanamu au picha, tena hawazifanyii liturujia yoyote sanamu au picha walizo nazo majumbani au makanisani.
Ni wapi ambapo Kanisa Katoliki linafanya au kuwafundisha rasmi na kuwahimiza wafuasi wake wafanye matendo hayo tisa ya kiliturujia kwa ajili ya kuabudu sanamu? Hakuna! Kwa hiyo, Wakatoliki hawana hatia yoyote ya kuabudu sanamu mbele ya Mungu. Kama mtu mmoja akifanya hivyo, hilo ni shauri lake binafsi, siyo shauri au utaratibu wa Kanisa lote. Aidha, afanyaye hivyo amepotoka peke yake, kwa sababu hajafundishwa na Kanisa Katoliki afanye hivyo. Hilo ni kweli kwa sababu mambo binafsi, siyo mambo rasmi ya Kanisa lote!
Kwa hiyo, tunaona wazi kwamba Wakatoliki hawaabudu sanamu kamwe, kama inavyodaiwa na baadhi ya waamini wa madhehebu mengine ya kikristo. Wanaotoa shutuma hizo inafaa wajiangalie kwanza wao wenyewe, maana imeandikwa: β€œβ€¦ mtu akidhani kwamba kitu fulani ni najisi, basi, kwake huwa najisi” (Rom.14:14).

JE, IJUMAA KUU WAKATOLIKI WANAABUDU NINI?

Je, ni kweli kwamba Siku ya IJUMAA KUU Wakatoliki wanaabudu Sanamu au Mti wa Msalaba? HAPANA! WANAMWABUDU WOKOVU-YESU! Kiini cha utata hapa ni β€œNINI MAANA YA IBADA YA KUABUDU MSALABA” inayoendeshwa siku ya Ijumaa Kuu? Madhehebu hayo yanayofanywa na Wakatoliki Siku ya IJUMAA KUU siyo Ibada ya Kuabudu Sanamu. Labda hapa ni tatizo la lugha au maneno yanayotumika, ndiyo yanayowachanganya watu! Hilo ni kweli kwa sababu jina la madhehebu yenyewe halisemi wazi kitu gani hasa kinanuiwa kufanywa katika ibada hiyo.
Wengi hawajui nini hasa kinanuiwa kufanyika siku ya Ijumaa Kuu katika β€œIbada ya Kuabudu Msalaba” – jina ambalo nimesema halitoi picha halisi ya jambo linalokusudiwa kufanyika. Mtu mwenye akili timamu akijua kitu halisi kinachofanyika siku ya Ijumaa Kuu, hawezi kusema madhehebu hayo ni Ibada ya Sanamu au kuabudu mti. Tatizo hapo ni lugha tu inayotumika katika kuieleza ibada hiyo. Labda jina hilo lichunguzwe upya na wataalamu wetu katika Kanisa na ikiwezekana kulirekebisha ili kuondoa utata kwa baadhi ya watu wenye uelewa mdogo, wenye wanaokwazwa nalo!

NINI HASA KINAFANYIKA SIKU YA IJUMAA KUU?

Wanachofanya Wakatoliki Siku ya Ijumaa Kuu ni KUUHESHIMU MTI WA MSALABA na KUMWABUDU WOKOVU. WOKOVU ni nani? WOKOVU NI YESU KRSITO BWANA WETU. Basi, kinachofanyika siku ya Ijumaa Kuu ni kumwabudu WOKOVU yaani YESU KRISTO, ambaye alitundikwa msalabani. Hivyo ndivyo anavyotangaza Kiongozi wa Ibada hiyo ya Ijumaa Kuu, pale anapotoa mwaliko kwa waamini mara tatu, ili kila muumini ausikie na kuelewa vema: β€œHUU NDIO MTI WA MSALABA, AMBAO WOKOVU WA DUNIA UMETUNDIKWA JUU YAKE, NJOONI TUUABUDU.” Waamini wanaalikwa kiimani kuuabudu WOKOVU, na hilo ndilo linalofanyika, yaani kuuabudu WOKOVU – YESU KRISTO. Waamini wote wanaalikwa kujongea mbele kwa imani kwenda kumwabudu YESU. Watu wanamwabudu YESU kwa sababu WOKOVU maana yake ni YESU.
Jina YESU ambalo linatokana na Kiebrabia β€œYESHUA”, maana yake β€œWOKOVU” (Rej. Mt.1:21;1:25; Lk.1:31). Ikiwa wokovu ni YESU, basi Ijumaa Kuu Wakatoliki hawaabudu sanamu au mti, bali wanamwabudu YESU KRISTO. Kwa sababu hiyo, yote yanayofanyika Siku ya Ijumaa Kuu, yanafanyika kihalali na kwa haki kwa sababu YESU KRISTO, ambaye ni WOKOVU ni MUNGU, na MUNGU peke yake ndiye mwenye haki na anayepaswa kuabudiwa. Ikiwa mkristo hataki kumwabudu YESU KRISTO, aliye Mwana wa Mungu na Mungu kamili, na ambaye ameeleta wokovu, anafanya makosa makubwa!
Basi, nasisitiza kuwa Siku ya Ijumaa Kuu, Wakatoliki hawaabudu sanamu wala mti. Wanamwabudu WOKOVU, yaani YESU KRISTO, Nafsi ya Pili ya MUNGU. Kutomwabudu YESU KRISTO ni sawa na kumkana Mungu, kukana wokovu ulioletwa naye. Basi, tujiepushe na ukanaji Mungu wa aina hiyo. Nawaalika wote Siku ya Ijumaa Kuu tufungue mioyo yetu kwa imani kubwa ili tumwone WOKOVU aliyetundikwa msalabani, apate kuukomboa ulimwengu. Kwa imani, wote tumsujudie YESU ili apate kutukumbuka katika Ufalme wake wa milele.
Hatimaye, niseme kwamba ingawa Mungu ametoa amri ya kukataza sanamu na picha (Kut. 20:4-5; Kumb. 5:6-10), lakini hachukizwi na kila sanamu au picha. Sanamu na picha ambazo hazipewi daraja la Mungu, Yeye hazichukii, kwa sababu hazichukui nafasi yake kama Muumba. Basi, Wakatoliki hawaendi kinyume na Biblia kwa kuziheshimu sanamu na picha zilizoko kwenye majumba yao na makanisani.

MAANA YA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA MASUALA YA LISHE

1. Chakula

ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na kuupatia mwili virutubishi mbalimbali Chakula huupatia mwili nguvu, kuulinda na kuukinga dhidi ya maradhi mbalimbali .Mfano wa chakula ni ugali, wali, maharagwe, ndizi, viazi, mchicha, nyama, samaki.

2. Lishe

ni mchakato unaohusisha hatua mbalimbali za jinsi mwili unavyokitumia chakula kilicholiwa, hatua hizi ni kuanzia chakula kinapoliwa, jinsi mwili unavyokisaga na kukiyeyusha, umetaboli, na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini.

3. Virutubishi

ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishi vya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.

4. Mlo kamili

ni ule ambao hutokana na chakula mchanganyiko kutoka katika makundi yote ya chakula na una virutubishi vyote muhimu kwa ajili ya lishe na afya bora. Mlo huu unapoliwa kwa kiasi cha kutosha kulingana na mahitaji ya mwili angalau mara tatu kwa siku huupatia mwili virutubisho vyote muhimu.

5. Ulaji unaofaa

hutokana na kula chakula mchanganyiko na cha kutosha (mlo kamili) ili kukidhi mahitaji ya mwili. Ulaji unaofaa pia huzingatia matumizi ya kiasi kidogo cha chumvi, mafuta, sukari, ulaji wa nyama nyekundu kwa kiasi kidogo. Ni muhimu kuzingatia ulaji wa mboga mboga, matunda, na vyakula vya jamii ya kunde kwa wingi ili kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

6. Nishati- lishe

ni nguvu inayopatikana baada ya virutubishi (kabohaidreti, mafuta) kuvunjwa vunjwa mwilini. Mwili huitumia nguvu hiyo kufanya kazi mbalimbali Kama kulima, kutembea, kupumua, kuziweka seli za mwili katika hali inayotakiwa n.k.

7. Kalori au kilo kalori

ni kipimo kinachotumika kupima nishati -lishe

8. Makapi mlo

ni sehemu ya chakula ambayo mwili hauwezi kuyeyusha lakini ni muhimu katika uyeyushwaji wa chakula. Mfano wa vyakula venye makapi mlo kwa wingi ni mboga za majani, matunda( maembe, machungwa, mapera, machenza, mafenesi, unga usiokobolewa( dona) na vyakula vya jamii ya kunde.

9. Lehemu

ni aina ya mafuta yanayopatikana hasa kwenye vyakula vya asili ya wanyama na pia hutengenezwa mwilini. Lehemu inayotokana na vyakula ikizidi mwilini huleta madhara ya kiafya. Vyakula venye lehemu kwa kiasi kikubwa ni pamoja na maini, figo, mayai, nyama iliyonona kama nundu, nyama ya nguruwe yenye mafuta, mkia wa kondoo, samli, siagi, ngozi ya kuku n.k.

10. Utapiamlo

ni hali ya kupungua au kuzidi kwa baadhi ya virutubishi mwilini ambapo husababisha lishe duni au unene uliozidi.

11. Antioxidants

ni viini ambavyo vina uwezo wa kukinga seli za mwili zisiharibiwe na chembe chembe haribifu (free radicals) ambazo huweza kusababisha saratani. Viini hivyo huungana na chembechembe hizo haribifu na kuzidhibiti ili zisisababishe madhara. Mifano ya antioxidants ni pamoja na beta-carotene, lycopene, vitamin C, E, na A.

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia baking soda

Moja ya sababu za kutokea chunusi katika ngozi yako ni kuwepo kwa takataka au uchafu juu ya ngozi yako na njia rahisi ya kusafisha taka hizo ni kwa kutumia baking soda hivyo kuifanya ngozi ipumuwe vizuri.

Kwahiyo ukiwa na chunusi hebu fikiri kuhusu baking soda. Baking Soda husaidia kubandua seli za ngozi zilizokufa na kufanya mafuta yaliyozidi kuondoka.

Ni rahisi zaidi kutumia baking soda kutibu chunusi. Chukua baking soda na uchanganye kidogo na vijiko vinne vidogo vya maji au vya maji maji ya limau na upake uji huo moja kwa moja kwenye chunusi. Subiri kwa dakika 10 na ujisafishe na maji ya moto.

Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka

πŸ‘‰Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chumvi

Kunywa Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kwenye chumvi hupandisha juu shinikizo la damu. Usizidishe dawa hii kwa sababu chumvi nyingi kuzidi ina madhara kiafya.

Matumizi:

Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ndani ya maji glasi moja (robo lita) na unywe mchanganyiko huu mara 1 au 2 kwa siku


πŸ‘‰Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda.

Kama unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.

Usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.


πŸ‘‰Matumizi ya zabibu kavu kutibu shinikizo la chini la damu

Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo

1. Chukua zabibu kavu Loweka zabibu 30 mpaka 40 ndani ya kikombe cha maji kwa usiku mzima.

2. Asubuhi kabla ya kula wala kunywa chochote kula zabibu moja baada ya nyingine na unywe pia maji yake

3. Rudia zoezi hili kila siku kwa majuma kadhaa hata mwezi.


πŸ‘‰Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu

Hatua za kufuata

  1. Chukua Kijiko kikubwa kikubwa cha tangawizi mbichi iliyoparuzwa
  2. Changanya na Kikombe kimoja cha maji ya moto
  3. Chemsha katika moto kwa dakika 12 hivi
  4. Kisha ipua na uchuje
  5. Ikipoa kidogo kunywa yote,
  6. fanya hivi mara 2 kwa siku kila siku

πŸ‘‰Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka

Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C, magnesiamu na potasiamu, vilevile dawa hii husaidia kuweka sawa akili na kuondoa msongo wa mawazo (stress).

Matumizi

  1. Chukua majani 10 mpaka 15 ya mrehani mbichi
  2. Saga au twanga kupata maji maji yake (juisi).
  3. Weka asali kijiko kidogo kimoja ndani yake.
  4. Kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa tupu.

Vile vile unaweza kutafuna tu moja kwa moja majani kadhaa ya mrehani kila siku asubuhi.


πŸ‘‰Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Hatua za kufuata

1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti

2. Weka vijiko vikubwa viwili vya asali ndani yake na kisha changanya vizuri

3. Kunywa yote asubuhi tumbo likiwa tupu na jioni glasi nyingine kwa majuma kadhaa


πŸ‘‰Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.

Hii ni kwa sababu Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa.

Kwa hiyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.

Mishipa ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu.

Maji yanapopungua kwenye mwili hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu.

Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.

Kwa sababu hii, ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.

Hii inasaidia kuongeza vimiminika katika mishipa ya damu.


πŸ‘‰Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu

Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.

Lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.


πŸ‘‰Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu.

Kula zaidi vyakula vyenye protini, vyenye vitamini B na C kwa wingi. Kula milo midogo midogo hata mitano kuliko kula miwili au mitatu lakini ya nguvu sana.

Unaweza kutumia kitunguu swaumu hasa kibichi ukitafuna punje 2 kila unapoenda kulala kadharika glasi moja ya juisi ya ubuyu kutwa mara 1.

Acha vilevi vyovyote mara tu unapogundulika na shinikizo la chini la damu. Epuka pia vyakula vyenye wanga sana kama tambi, mikate, viazi, wali nk

Upungufu wa baadhi ya vitamini hasa vitamini za kundi B na madini kunaweza pia kuleta shinikizo la chini la damu. Hivyo ili kudhibiti shinikizo la chini la damu unahitaji kula mlo sahihi kila siku.


πŸ‘‰Matumizi ya Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu

Unaweza kutumia Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo;

  1. Loweka lozi 5 mpaka 6 kwenye kikombe cha maji kwa usiku mmoja
  2. Asubuhi menya hizo lozi na uzisage
  3. Chukua hizo lozi ulizosaga na uweke ndani ya kikombe cha maziwa
  4. Chemsha mchanganyiko huu kwa dakika kadhaa
  5. Kunywa kinywaji hiki kila siku asubuhi
Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About