Nilichokifanya baada ya kualikwa na mchumba wangu kwao
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuโฆ
Nikaamua kuvaa glovesโฆ
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.๐๐๐
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuโฆ
Nikaamua kuvaa glovesโฆ
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.๐๐๐
1. Kutushawishi tuache kusali maaana njia kuu ya mawasiliano kati yetu na MUNGU.Hivyo akifanikiwa hapo kwisha habari yako
2. Kufanya umwogope shetani na nguvu zake kuliko unavyompenda MUNGU. Wakristo wengi leo hii husali na kuomba kwa nguvu mno siyo sababu wanampenda MUNGU mno hapana ni sababu wanamwogopa shetani na majeshi yake na muda mwingine hata watumishi wa MUNGU wanamsaidia kwa kuhubiri mno na muda mwingine kuongeza jumvi juu ya nguvu za giza kuna wahubiri huambatanisha kila kitu na vifungo vya nguvu za giza na kusahau kuhubiri uzuri na wema wa MUNGU kwetu.
3.Kutufanya tusahau uwepo wake au kuupuzia. pale tunapokuwa hatupay attention existance ya shetani yeye ndio hupata wakati mzuri wa kutupiga ,sababu ni rahisi mno kutouutambua ubaya wa dhambi kama hatutaamini uwepo wa shetani ktk uovuโฆhii hutupelekea kutenda dhambi na kuziona siyo dhambi mfano kwa wasomi wengi hupuuzia baadhi ya mambo kama kujilinda na zinaa wakiamini ni kupitwa na wkt kama utakuwa hauna mahusiano ya kingono mpaka umefika chuo kikuu tena huchukulia wasiokuwa hivyo ni wagonjwa.hapo ni kuwa wengi wameignore uwepo wa shetani “no devil no evil” hivyo watu ndio hupotea.
4.KUTUTIA MOYO WAKATI WA KUTENDA DHAMBI NA KUTUKATISHA TAMAA YA KUSAMEHEWA. nitatoa mfano huu mtu ambaaye anataka kufanya uzinzi shetani humtia moyo kuwa MUNGU anajua kuwa sisi ni binadamu dhaifu na yeye husamehe dhambi zetu daima lakini ifikiapo wakati ukataka kutubu hafanya kila njia kukukatisha tamaa ya kusamehewa na hututia aibu hata kutsmka kwa padri kuwa nimedhini maana huanza kufikiria padre atanionaje mimi.
BASI NDUGU TUSISINZIE BALI TUWE MACHO DAIMA MSHITAKI WETU YU MACHO KUTUJARIBU.
House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani.
Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza ‘what happened to my plate?
House girl akajbu: ‘The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjeeโฆโฆthe pasuka paaaaaaaa
๐๐๐๐hadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika
Ukitaka kufanya biashara kwa ufanisi; wakati wa kununua nunua ukiwa na mtazamo wa muuzaji kwa kufikiri kama wewe ungekua ndio unauza ungeuzaje, na Wakati wa kuuza uza ukiwa na mtazamo wa mnunuzi kwa kufikiri kama ungekua wewe ndiye mnunuzi ungenunuaje.
Takribani kila mtu angependa kuwa na ngozi laini, au hata laini zaidi. Watu wengi wamekuwa wakiitafuta ngozi nzuri au kujitahidi kuitunza ili isiharibike. Lakini je, wamefanikiwa?
Wachache hufanikiwa na wengi hushindwa. Na hata hao waliofanikiwa wengi wao hutumia vipodozi vikali ambavyo vingi huchubua na kuharibu ngozi zao na kuwaletea madhara makubwa sana baadae.
Vipi wewe, ungependa kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako? Karibu somo la leo ili uweze kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako.
Ngozi laini ni nzuri na inaongeza mvuto wa mwili. Ulaini wa ngozi hupotezwa na mambo mbalimbali kama vile seli za ngozi kupungukiwa na maji na kuanza kusinyaa na kunyauka, seli za ngozi kujeruhiwa, na seli za ngozi kufa. Matokeo yake ni michirizi, makunyanzi, makovu, chunusi, madoa, ngozi kufubaa na kuzeeka.
Kuifanya ngozi kuwa laini unahitaji kuupatia mwili virutubisho vyote vya kujenga mwili vizuri na kunywa maji ya kutosha ili seli zisikauke, kusinyaa wala kunyauka. Kula mlo kamili, matunda mengi na kunywa maji ya kutosha.
Pia unahitaji kuepuka jua kali ambalo litaunguza ngozi, kuikausha na kuifanya iwe na makunyanzi na vitu vingine vinavyoota kwenye ngozi kutokana na jua.
Tumia vipodozi vizuri vinavyosaidia ngozi kuwa laini bila kuidhuru. Hapa kuna vipodozi vya aina mbali mbali na vinavyofanya kazi kwa njia mbali mbali. Vipodozi vya muhimu ni
Tumia sabuni zenye uwezo mkubwa wa kuondoa uchafu kutoka kwenye ngozi, na ukiweza tumia โface washโ au โfacial cleansersโ. Hivi husaidia kusafisha kabisa ngozi na kuondoa uchafu.
Kwa upande wa seli zilizokufa na kubaki juu ya ngozi tumia โscrubโ. Scrub hufanya kazi kwa kuondoa seli zilizoharibika na zilizokufa na kuacha seli changa na ngozi nzuri.
USHAURI:
MIKUNJO katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi.
Tofauti na mikunjo ya uzee, mikunjo hii hutokana na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na mambo mablimbali.
Katika kupambana na tatizo hilo, wadau wa urembo wa asili wamegundua njia mbalimbali zinazoweza kutumika kutatua tatizo hili.
Wadau hao wanashauri kumwona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi wa matumizi ya njia hizo za asili kabla ya kuanza kutumia njia za asili kwani hata kama ni vipodozi asilia, haina maana kama ni salama kwa watu wote.
Kwa mujibu wa wadau hao, unaweza kutumia viungo vinavyopatikana jikoni kwako kupambana na mikunjo katika ngozi. Baadhi ya viungo hivyo ni pamoja na:
Karoti
Tumia juisi ya karoti kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika.
Karoti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako. Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi.
Si hivyo tu, karoti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo ya
ngozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maeneo kama hayo.
Namna ya kufanya
Chukua karoti, saga kwenye mashine kisha kamua ili kupata juisi yake.
Tumia pamba kupaka katika maeneo yaliyoathirika, fanya hivyo mara kwa mara, itakusaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.
Maziwa
Maziwa yana virutubisho vinavyochochea kunawiri kwa ngozi. Pia yana chembechembe za ‘Alfa-Hydroxide Acid’ ambazo zina uwezo mkubwa kuondoa seli zilizokufa mwilini.
Yote haya husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la mikunjo katika ngozi.
Unachotakiwa kufanya
Kuchukua maziwa kiasi na chovya pamba ndani yake, kisha paka maeneo yaliyoathirika.
Aloe Vera
Jeli ya Alovera ndiyo hasa inayotakiwa katika zoezi hili. Chukua jani lake na kisha likate ili kupata utomvu wake.
Chukua utomvu au jeli hiyo kama wengine wanavyoita na kisha pakaa sehemu iliyoathirika, itapunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.
Parachichi
‘Mask’ ya Parachichi husaidia kuifanya ngozi iwe na mng’ao. Siyo hivyo tu, bali huchangia kwa kiasi kikubwa pia kuifanya ngozi iwe laini na nyororo.
Unachotakiwa kufanya
Chukua parachichi liloiva vizuri, kisha saga hadi lilainike.
Baada ya hapo pakaa sehemu iliyoathirika na acha kwa muda wa dakika 10, kisha osha sehemu hiyo uikaushe.
Papai
Mask ya Papai pia husaidia kuondoa tatizo hili.
Unachotakiwa kufanya
Chukua kipande cha papai kilichoiva na kuchanganya na kijiko kimoja cha unga wa ngano.
Pakaa sehemu iliyoathirika na kaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi. Mbali na kupaka pia unaweza ukatumia kula kwani lina vitamin E kwa wingi, ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa ngozi.
Danzi
Juisi ya tunda hili husaidia katika uzalishaji wa sehemu ya juu ya ngozi ‘collagen’. Danzi lina kiwango kikubwa cha vitamini C. Na kwa kawaida aina hii ya vitamin husaidia kuchochea ukuaji wa โcollagenโ, hivyo kuifanya ngozi yako kunawiri.
Maji
Kunywa maji mengi kwani husaidia kuifanya ngozi yako iwe na unyevu muda wote.
Ikiwa utazingatia zoezi hili mikunjo kati ngozi yako itakuwa ni historia.
Kitendawili…
Nikizidi nalaumiwa, nikipungua nadharauliwa
JIBU: Chumvi
Mbongo, Mganda, na Mkenya walikamatwa na makosa Uchina.
Wakaambiwa adhabu ni ama kifo cha moja kwa moja au adhabu nyingine ambayo atakayeifaulu atakuwa huru, atakayeshindwa atauawa.
Basi wao wakaomba wapewe hiyo adhabu nyingine wajaribu bahati yao.
Wakapelekwa msituni wakaambiwa kila mmoja aende kwa njia yake halafu arudi na matunda kumi ya kufanana.
Wakaingia msituni kila mtu njia yake.
โฆ Mganda akarudi wa kwanza na machungwa kumi. Akaambiwa adhabu yake ni kumeza moja moja likiwa zima bila kufumba macho bila kulia wala kucheka wala kujitikisa mpaka yote kumi yaishe. Akameza la kwanza. Safi. Kumeza la pili, akashindwa kuvumilia akafumba macho. Akapigiwa risasi akafa.
Mkenya akaja. Ana vitunda vidogo vidogo kama pili vilaini. Akasomewa masharti. Akaanza kumeza bila kufumba macho wala kulia, wala niniโฆ alipofika cha tisa akashindwa kuvumilia akaangua kicheko! Akapigwa risasi pia akafa.
Wakiwa kuzimu Mganda akamwuliza Mkenya, โVipi, mbona ulishindwa kuvumilia wakati kilibaki kitunda kimoja tu?โ
Mkenya akamjibu: โMkuu, nilishindwa kuzuia kicheko maana nilimwona Mbongo anakuja na matikiti maji!โ
Mbangi mwitu au kwa kisayansi ni African marigold / (Tagetes erecta) Unazuia Bakteria, fungusi na wadudu kama vile Siafu, bungo pamoja na aina nyingine za wadudu.
Alipelekwa Hospitali na baba yake, baada ya vipimo Doctor akawa anamuandikia dawa, baba yake akatoka nje kuongea na cm.
Mtoto akamwinamia Doctor na kusema kwa sauti ya chini:- “Doctor Kwenye dozi ya dawa niandikie na FANTA BARIDII, CHIPS na MISHIKAKI kutwa mara 2 kwa siku 30.
Sala yoyote ili iwe SALA lazima itolewe kwa Imani, Upendo, Unyenyekevu na kwa Matumaini. Sala kama hii ndiyo ipendezayo mbele ya Mungu.
Boss;-ย kwa nini umechelewa kazini
Juma;-ย kuna mtu njiani alidondosha elfu1
Boss;-ย ohhoh kwa hiyo ulikuwaunamsaidia kuitafuta
Juma;-ย hapana nilikuwa nimeikanyaga
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Upendo wa Mungu hauna kikomo. Mama anaweza kumchoka na kumtelekeza mwanae lakini Mungu kamwe hamchoki mtu.
Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia.
Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa.
Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume. Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi.
Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji.
Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa โkuonaโ. Endapo mtumiaji ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae.
Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika. Ukwepaji wa gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye hatari zaidi.
Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.
Ni kwa nini tunapata Mateso na shida katika Maisha? Kwa nini Mungu ameruhusu tuteseke?
Mungu hapendi mtu Ateseke lakini ni kwa njia ya ya Mateso mtu anaweza akapimwa IMANI yake, UNYENYEKEVU, UTII na Matumaini yake kwa Mungu.
Mateso na shida katika maisha ni nafasi ya kujifunza na Kuonyesha unyenyekevu, Imani na Matumaini ya mtu.
Mtu anaweza kujitesa au kukubali Mateso huku akiyachukulia kama malipizi ya dhambi zake au dhambi za wengine.
Sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kukubali au kujitesa kwa ajili ya dhambi hasa kwa dhambi zisizokua zake, Ni watu wachache Wenye fadhila hii. Mfano Watakatifu kama Mt. Faustina aliweza kuchukua Mateso kama malipizi ya dhambi hasa za watu wengine ambapo alikubali magonjwa shida na Kudharauliwa kama malipizi ya dhambi.
a)Binzari ya unga
b)Maziwa fresh
c)Asali
d)Bakuli
e)Kijiko cha chai
a)Weka kijiko kidogo kimoja cha binzari ya unga ndani ya bakuli
b)Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali ndani yake
c)Ongeza tena kijiko kidogo kimoja au viwili vya maziwa fresh
d)Changanya vizuri mchanganyiko huu upate uji mzito
e)Pakaa pole pole sehemu yenye chunusi mchanganyiko huu
f)Baada ya dakika 5 au 7 hivi jisafishe uso wako
g)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 tu kwa wiki
Binti: Hallow mpenzi, Mambo
Jamaa: Poa baby
Binti:Uko wapi?
Jamaa: Niko town napata lunch
Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Binti: Kwanini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!
Inafahamika kuku kutaga mayai mengi hutokana na aina ya mbegu ya kuku, ila jua kwamba hata aina ya mbegu ya kuku yenye sifa ya kutaga mayai mengi kama haitapewa matunzo mazuri ย basi sifa yake ya utagaji itapotea.
Kwa kawaida Tetea anatumia muda wa masaa 24 – 27 (siku moja) kutengeneza yai. Hakuna njia ya kupunguza muda huu (yaani atengeneze mayai miwili katika siku moja). Hiyo ndio asili yake. Njia Nzuri ya kumfanya kuku atage muda mrefu ni kumfanya awe na furaha na afya.
1. Wape chakula bora chenye virutubisho vya kutosha. Usichakachue chakula chao hawatataga.
2. Viota vyao viwe safi. Safisha viota vyao mara kwa mara ili watage sehemu safi.
3. Wawe na sehemu ya wazi ya kuzunguka zunguka na kuparua parua.
4. Wawekee calcium ya kutosha kwenye chakula chao ili mayai wanayotaga yawe na gamba gumu.
5. Wachunguze mara kwa mara
kama wana dalili za kuumwa, na endapo dalili zipo watibu mara moja.
6. Wapatie maji safi kila siku. Pia safisha vyombo vyao kwa sabuni kila siku.
7. Hakikisha banda lao ni safi muda wote ili kusiwe na wadudu kama viroboto, chawa na papasi. Wadudu hawa huwasumbua kuku na kuwafanya wapunguze kutaga.
8. Hakikisha kuku hawapati msongo/stress, mfano kusiwe na wanyama wa kuwatisha wanaopita au kuingia bandani kwao.
9. Chagua aina ya kuku wanaotaga mayai mengi.
10. Umri wa kuku. Kuku wenye umri wa miezi 6 – 18 wanataga sana. Wakiwa na miezi 19 – 24 wananyonyoka manyoya (Annual Molt), hivyo hupunguza kutaga, na wakianza kutaga tena, wanataga mayai makubwa na machache kuliko mwanzo.
11. Wasihamishwe hamishwe banda. Kuku hutaga vizuri zaidi wakiwa kwenye mazingira waliyoyazoea.
12. Walishe mboga za majani za kutosha.
Kumbuka: Kuku wenye furaha na afya ndio watakaotaga sana kwenye maisha yao.
Note: Wakati mwingine inadhaniwa kwamba Jogoo anaweza kumsaidia Tetea kutaga mayai mengi. Jogoo hawezi kuongeza utagwaji wa mayai, lakini anahitajika kuyarutubisha mayai (kuyafanya yawe na mbegu). Kama kuku wako anataga mayai machache, kuongeza Jogoo hakutamfanya Tetea atage mayai mengi.
Recent Comments