Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku (Chicken Breast) Wa Kukausha

Viambaupishi

Vipimo vya Wali:

Mchele 3 vikombe

*Maji ya kupikia 5 vikombe

*Kidonge cha supu 1

Samli 2 vijiko vya supu

Chumvi kiasi

Hiliki 3 chembe

Bay leaf 1

Viambaupishi: Kuku

Kidari (chicken breast) 1Kilo

Kitunguu 1

Tangawizi mbichi ½ kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) 7 chembe

Pilipili mbichi 3

Ndimu 2

Pilipilimanga 1 kijiko cha chai

Mdalasini ½ kijiko cha chai

Jira/Cummin ya unga 1 kijiko cha chai

Maji ¼ kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

Wali:

Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.

Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.

Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.

*Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.

  • Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.

Kuku:

Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.

Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.

Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.

Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)

Zawadi ya Kipekee kwa Mtu Ambayo Inadumu Milele

Kuna Zawadi moja ya Kipekee ya kumpa mtu ambayo ni Kusali na Kuomwombea Mtu aweze kuingia Mbinguni. Je, ulishawahi kutoa zawadi hii hasa kwa wale unaowapenda? Kila kitu kitabaki hapa duniani na kitapita na kusahauliwa lakini hili halina mwisho

Zawadi ya Kipekee: Kusali na Kuombea Wapendwa Wetu

Kuna zawadi moja ya kipekee ambayo unaweza kumpa mtu, nayo ni kusali na kumuombea ili aweze kuingia Mbinguni. Katika maisha haya ya kidunia, mara nyingi tunatafuta zawadi za kuwafurahisha wapendwa wetu, lakini zawadi ya sala ina thamani kubwa kuliko zawadi yoyote ya kidunia. Je, ulishawahi kutoa zawadi hii hasa kwa wale unaowapenda?

Thamani ya Zawadi ya Sala

Kusali na kumuombea mtu ni tendo la upendo wa kweli. Ni njia ya kuonyesha kwamba unajali sana kuhusu hali ya kiroho ya mtu huyo na unataka kumwona akifurahia maisha ya milele. Sala ni mazungumzo na Mungu, na kwa kuomba kwa ajili ya wengine, tunawaweka mikononi mwa Mungu mwenye uwezo wote. Biblia inatufundisha umuhimu wa kuombeana.

“Basi, aombeeni hivyo na kusema, Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.” (Mathayo 6:9)
“Kwa sababu hii tena, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kuomba kwa ajili yenu, na kusiomba kwamba mjazwe na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho.” (Wakolosai 1:9)
“Sasa basi, waombeeni kila siku ili wasimame imara katika imani yao.” (Waebrania 13:18)

Kila Kitu Kitabaki Hapa Duniani

Katika maisha haya, tunaweza kumiliki vitu vingi: nyumba, magari, fedha, na mali nyingine nyingi. Hata hivyo, kila kitu kitabaki hapa duniani na kitabakia kuwa mali isiyo na thamani tunapovuka kwenda kwenye maisha ya milele. Mali ya kidunia inapitiliza na kusahaulika, lakini zawadi ya sala inaendelea hata baada ya kifo.

“Hatujaingia na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu.” (1 Timotheo 6:7)
“Usiweke hazina zenu duniani, ambako nondo na kutu vinaharibu, na wevi huvunja na kuiba; bali wekeni hazina zenu mbinguni, ambako hakuna nondo wala kutu viiharibuyo, na wevi hawavunji wala kuiba.” (Mathayo 6:19-20)
“Mna haja moja, nayo ni hii; utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa.” (Mathayo 6:33)

Zawadi ya Sala Haina Mwisho

Sala ni zawadi ya kudumu. Inapotolewa kwa nia safi, inaweza kubadilisha maisha ya mtu na kumwongoza kwenye njia ya wokovu. Kwa kumwombea mtu, tunasaidia roho yake kupata nafasi ya kumkaribia Mungu na kuishi maisha matakatifu. Hii ni zawadi ambayo haitaisha au kupotea, bali itaendelea kuwa na athari milele.

“Naomba kwa ajili yao. Siombi kwa ajili ya ulimwengu, bali kwa ajili ya wale ulionipa, kwa maana wao ni wako.” (Yohana 17:9)
“Kwa hiyo, ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” (Yakobo 5:16)
“Basi nakuomba, kama ambavyo hujaacha kumwombea Mtakatifu huyo; unapoomba usife moyo, bali uongeze juhudi.” (Wakolosai 4:12)

Hitimisho

Je, ulishawahi kutoa zawadi hii kwa wale unaowapenda? Kusali na kuwaombea wapendwa wako ni tendo la upendo na kujali ambalo lina thamani kubwa sana kuliko zawadi yoyote ya kidunia. Kila kitu kingine kitabaki hapa duniani na kitapita na kusahauliwa, lakini zawadi ya sala ina athari za milele. Kwa kumwombea mtu, unampa nafasi ya kuingia Mbinguni, na hiyo ni zawadi ya pekee zaidi unayoweza kumpa mtu yeyote.

Kila wakati unapomwomba Mungu kwa ajili ya wapendwa wako, kumbuka kwamba unawawekea hazina mbinguni, ambako hazina hizo hazitaharibika kamwe. Ni tendo lenye upendo na lenye kuleta baraka zisizo na mwisho.

“Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwana wake pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16)
“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.” (Mathayo 7:7)
“Na imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” (Waebrania 11:1)

Jinsi ya kupika Baklawa Za Pistachio Na Lozi

VIAMBAUPISHI

Philo (thin pastry) manda nyembamba – 1 paketi

Siagi – ¼ Kikombe cha chai

Baking powder – 2 Vijiko vya chai

Pistachio/ lozi – 2 vikombe vya chai

Mafuta – ½ Kikombe

VIAMBAUPISHI VYA SHIRA

Sukari – 2 Vikombe vya chai

Maji – 2 ½ Vikombe vya chai

ndimu – ½ kijiko cha chai

JINSI YA KUANDAA

Tafuta treya iliyokuwa sawa na ukubwa wa hizo manda nyembamba (philo) au zikate hizo manda kwa ukubwa wa treya (mraba au mstatili)
Kisha yeyusha siagi changanya na mafuta.
Kisha panga manda moja pakaza mafuta juu yake kisha weka manda nyingine juu yake kisha pakaza mafuta tena weka manda nyingine juu yake, endelea kufanya hivyo mpaka ziwe kama sita au saba kisha nyunyizia pistachio na lozi halafu panga tena manda na mafuta manda na mafuta tena sita au saba kisha nyunyizia tena pistachio na lozi.
Panga namna hivyo mpaka treya ijae inapofika manda ya mwisho kata vipande vya mraba vidogodogo humo humo kwenye treya kisha nyunyizia mafuta yaliyobaki.
Washa moto wa oven 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi rangi ibadilike kidogo (isikauke sana)
Chemsha syrup yako kama shira ya majimaji lakini isiwe nzito sana ikishakuwa tayari mwisho tia ndimu acha ipoe kidogo kisha miminia juu ya treya yote halafu malizia kunyunyizia pistachio na lozi zilizobaki.
Zikishakuwa tayari zipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

ANGALIZO

Ukishatoa treya kwenye oven wacha ipoe kidogo na syrup yako pia wacha ipoe kidogo kabla hujamimina, ukitia ya motomoto zitalainika.
Manda nyembamba za baklawa zinauzwa tiyari madukani kwenye pakiti.

Ushauri kuhusu mwanamke wa kufaa kuoa

Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara. Yote hayo ni ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Wekeni wivu pembeni na Yafuateni haya;

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia “Mimi ni mume wa mtu” au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, “wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao”

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.
MBARIKIWE SANA WANAUME WOTE WENYE BUSARA..

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE ili uweze kuwafahamu zaidi wanawake

Mapishi ya Maharage na spinach

Mahitaji

Maharage yaliyochemshwa kiasi
Spinach zilizokatwa kiasi
Vitunguu maji 2
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi

Matayarisho

Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.

Jinsi ya kupika vizuri Wali Wa Karoti Na Nyama

MAHITAJI YA WALI

Mchele – 3 Magi

Mafuta – 1/4 kikombe

Karoti unakata refu refu – 3

Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa – 1 kikubwa

Pilipli manga – 1/2 kijicho chai

Hiliki – 1/2 kijiko chai

Karafuu ya unga – 1/4 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga – 1/2 kijiko cha chai

Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji – 1 kijiko cha chai

Zabibu kavu (ukipenda) – 1/4 kikombe

Chumvi kiasi

KUPIKA WALI

Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo.
Tia vitunguu kisha tia bizari zote.
Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi
Tia mchele upike uwive.
Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda.
Funika endelea kuupika hadi uwive.

MAHITAJI KWA NYAMA

Nyama – 2 Ratili (LB)

Chumvi – Kiasi

Mafuta – 1/4 kikombe

Kitunguu (kata virefu virefu) – 1 Kikubwa

Pilipili mboga kubwa – 2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.

Figili mwitu (celery) kata vipande virefu virefu- Miche miwili.

KUPIKA NYAMA

Chemsha nyama hadi iwive
Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu
Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu
Kaanga kidogo tu kama dakika moja.
Tayari kuliwa na wali.

Soma huyu mtoto anachosema sasa, Ndoto za watoto bwana! Kazi ipo!

Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?

ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Nehemiah ??
Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!

Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

Viamba upishi

Nyanya 1 kg
Maji Iita ½
Chumvi kijiko kidogo 1
Sukari

Hatua

• Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike.
• Chuja juisi.
• Pima juisi – vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka
kwenya sufuria safi .
• Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke.
• Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa
kunywa.

Angalia huyu mwanafunzi anachomjibu huyu mwalimu wake

1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamilia….Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”

ZUZU:”Sunguramilia.”

2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTA…Je rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”

3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGE…Je samaki yuko katika jamii ya nini?”

ZUZU:”MELI.”

4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINI….Je wa
Liverpool anaitwaje?

ZUZU:”LIVER.”

5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”

ZUZU:”Hasira nyingi sana!”

Mapishi ya Ndizi mzuzu

Mahitaji

Ndizi tamu (plantain) 3-4
Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai

Matayarisho

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About