Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 ½ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa ½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito

Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu.

Kiungulia ni nini?

Kiungulia ni maumivu mithili ya moto yanayotokea kifuani sehemu ya katikat ya kifua. Maumivu haya hayana uhusiano na moyo.Yanatokea pale asidi ya kwenye tumbo inapopanda na kurudi kwenye koo la chakula.

Asidi hii ikiwa tumboni haisababishi madhara wala maumivu kwani inazalishwa muda wote na kuta za tumbo kumeng’enya chakula. Seli za kuta za tumbo haziathiriki na asidi hii ndio maana inapokuwa tumboni haileti shida yoyote.
Ila seli za kuta za koo la chakula haziwez kustahimili asidi hii ndiyo maana inapopanda kwenye koo la chakula unapata maumivu ya kiungulia.

Dalili ya kiungulia

Kiungulia mara nyingi hutokea wakati unakula au baada ya kula na kinaweza kuzidi makali wakati umelala.

Dalili ni kama, Kuhisi maumivu kama ya kuungua kwenye kifua au chembe moyopamoja na kujisikia radha ya uchachu mdomoni.

Saabu za kiungulia kwa wajawazito.

Sehemu mbali mbali za mwili hupata mabadiliko wakati wa ujauzito. Wakati wa ujauzito mwili hutengeneza kwa wingi hormone ya progesterone na relaxin ambazo huathiri mfumo wa chakula.

Progesterone hormone hii hufanya chakula kutembea na kufyonzwa kwa taratibu sana.
Relaxin hormone hufanya misuli laini ya mwili kulegea ikiwemo misuli inayobana sehemu ya juu ya tumbo (sphincter) inayozuia chakula au vitu vya tumboni visirudi kwenye koo la chakula .
Mabadiliko haya hufanya kuwa rahisi asidi na chakula vilivyomo tumboni kurudi kwenye koo la chakula na kusababisha kiungulia.

Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kiungulia kwa mama mjauzito ni;

  1. Kula chakula kingi sana
  2. Vyakula vyenye viungo
  3. Vyakula vyenye mafuta mengi
  4. Matunda jamii ya limao na machungwa
  5. Chocolate
  6. Soda
  7. Kahawa
  8. Sigara
  9. Pombe
  10. Baadhi ya madawa
  11. Stress
  12. Uzito uliopitiliza.

Jinsi ya kujikinga na kiungulia kwa wajawazito.

  1. Kuwa na uzito unaowiana na urefu wako
  2. Epuka vyakula vinavyosababisha kiungulia kama nilivyoainisha hapo juu
  3. Epuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja. Bali kula chakula kidogo kila baada ya muda.
  4. Kunywa maji ya kutosha. Angalau lita moja na zaidi kwa siku
  5. Epuka kuvaa nguo zinazobana sana tumbo na kiuno
  6. Usilale muda mfupi baada ya kula.
  7. Epuka kuwa na msongo wa mawazo /stress
  8. Onana na Daktari kupata ushauri wa dawa za kupunguza makali ya asidi hii ambazo ni salama kwa wajawazito

Mipango ya Mungu kwetu sisi wanadamu

Utangulizi

Mipango ya Mungu daima ni myema, Mungu anapanga Mema katika maisha ya mtu kama akifuata mapenzi yake. Tatizo ni kwamba watu wanafuata mapenzi yao wenyewe na kisha kukosa yale mema Mungu aliyopanga kwao.

Sio kila jambo jema unalofikiri kulifanya ni jema, kama halipo katika mipango ya Mungu halifai na linaweza kuzuia yale mema Mungu aliyopanga kwako.

Kwa hiyo, jitahidi kufahamu mapenzi ya Mungu na kuyafanya ili uwe katika mipango yake.

Mipango ya Mungu Daima ni Myema

Mipango ya Mungu ni kamilifu na inatufanyia mema ikiwa tutaifuata. Mungu anapanga mema kwa ajili ya maisha yetu, lakini mara nyingi tunashindwa kuona mema hayo kwa sababu tunafuata mapenzi yetu wenyewe badala ya mapenzi ya Mungu. Katika kila jambo tunalofanya, ni muhimu kutafuta kujua mapenzi ya Mungu na kuyatekeleza ili tuweze kuwa katika baraka na neema zake.

Mipango ya Mungu ni Kamilifu

Jeremia 29:11 inasema:
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” (Jeremia 29:11)

Mungu anatuwazia mema na anatupangia maisha yaliyojaa amani na mafanikio. Hata hivyo, ili tuweze kuona mipango ya Mungu ikitimia katika maisha yetu, tunahitaji kumfuata na kutii mapenzi yake.

Tatizo la Kufuata Mapenzi Yetu Wenyewe

Mara nyingi, tunachagua njia zetu wenyewe na kutozingatia mapenzi ya Mungu. Hii inatufanya tukose yale mema ambayo Mungu ameyapanga kwa ajili yetu. Mithali 14:12 inasema:
“Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.” (Mithali 14:12)

Hii inatukumbusha kwamba si kila jambo tunalofikiri ni jema linakubalika mbele za Mungu. Ni muhimu kujua mapenzi ya Mungu na kuyafuata.

Jitahidi Kufahamu Mapenzi ya Mungu

Warumi 12:2 inasema:
“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” (Warumi 12:2)

Tunapaswa kubadili mawazo yetu na kujua mapenzi ya Mungu kwa kusoma Neno lake na kuomba mwongozo wake. Kwa njia hii, tutaweza kutambua yale yaliyo mema na kukubalika kwake.

Mifano 10 ya Watu Waliopokea Mema kwa Kufuata Mapenzi ya Mungu

  1. Noa:
    Noa alifuata mapenzi ya Mungu kwa kujenga safina kama alivyoagizwa, na akawaokoa familia yake na wanyama wakati wa gharika. (Mwanzo 6:13-22)
  2. Ibrahimu:
    Ibrahimu alitii mapenzi ya Mungu alipomtoa mwanawe Isaka kama sadaka. Kwa imani yake, alibarikiwa na kuwa baba wa mataifa mengi. (Mwanzo 22:1-18)
  3. Yusufu:
    Yusufu alitii mapenzi ya Mungu hata alipouzwa utumwani na ndugu zake. Mwisho wa yote, Mungu alimtumia kuokoa Misri na familia yake kutokana na njaa. (Mwanzo 37-50)
  4. Musa:
    Musa alifuata mapenzi ya Mungu kwa kuwaongoza Waisraeli kutoka utumwani Misri kwenda kwenye nchi ya ahadi. (Kutoka 3:1-22)
  5. Yoshua:
    Yoshua alitii mapenzi ya Mungu alipowaongoza Waisraeli kuvuka mto Yordani na kushinda mji wa Yeriko kwa kuzunguka ukuta wake kama alivyoagizwa. (Yoshua 6:1-20)
  6. Gideoni:
    Gideoni alifuata mapenzi ya Mungu alipowachagua wanaume 300 kupigana dhidi ya jeshi kubwa la Wamidiani. Kwa imani yake, walipata ushindi mkubwa. (Waamuzi 7:1-25)
  7. Samueli:
    Samueli alitii mapenzi ya Mungu alipomteua Daudi kuwa mfalme wa Israeli, ingawa Sauli alikuwa bado anatawala. (1 Samweli 16:1-13)
  8. Daudi:
    Daudi alitii mapenzi ya Mungu alipompiga na kumuua Goliathi kwa jina la Bwana, na kuokoa Israeli kutoka kwa Wafilisti. (1 Samweli 17:45-50)
  9. Elia:
    Elia alifuata mapenzi ya Mungu alipotangaza njaa na mvua katika Israeli kulingana na amri ya Mungu. (1 Wafalme 17-18)
  10. Maria:
    Maria, mama wa Yesu, alitii mapenzi ya Mungu alipokubali kuwa mama wa Masiya, licha ya changamoto na aibu ambayo ingemkabili. (Luka 1:26-38)

Hitimisho

Mipango ya Mungu daima ni myema. Mungu anapanga mema katika maisha ya mtu kama akifuata mapenzi yake. Tatizo ni kwamba watu wanafuata mapenzi yao wenyewe na kisha kukosa yale mema Mungu aliyopanga kwao. Si kila jambo jema tunalofikiri kulifanya ni jema mbele za Mungu. Kwa hiyo, jitahidi kufahamu mapenzi ya Mungu na kuyafanya ili uwe katika mipango yake. Kwa kufuata mapenzi ya Mungu, tutapata mema yote aliyoyapanga kwa ajili yetu na kuishi maisha yenye baraka na amani.

Jinsi ya kupika Biriyani Ya Nyama Ng’ombe

Viambaupishi Vya Masala

Nyama vipande – 3 LB

Mtindi – ½ kopo

Kitunguu (thomu/galic) – 1½ kijiko cha supu

Tangawizi – 1½ kijiko cha supu

Nyanya – 2

Pilipili mbichi – kiasi

Nyanya kopo – 4 vijiko vya supu

Vidonge supu – 2

Pilipili nyekundu paprika – kiasi

Bizari zote saga – 2 vijiko vya supu

Viazi – 4

Mafuta – 2 mug

Samli – ½ kikombe

Vitungu – 6

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika masala

Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni.
Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni.
Kanga viazi weka pembeni.
Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke.
Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.

Vipimo Vya Wali

Mchele – 5 mug

Maji – kiasi

Chumvi – kiasi

Mafuta uliyokaanga vitungu – kiasi

Rangi ya biriani – ¼ kijiko cha chai

*Zafarani – ½ kijiko cha chai

*roweka rangi na zafarani

Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali

Osha mchele roweka muda wa saa.
Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele.
Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja.
Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika.
Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.

Jinsi ya kupika Visheti

Viamba upishi

Unga 2 Vikombe

Samli au shortening ya mboga 2 Vijiko vya supu

Maziwa ¾ Kikombe

Iliki Kiasi

Mafuta ya kukarangia Kiasi

Shira

Sukari 1 Kikombe

Maji ¾ Kikombe

Vanila ½ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda) Kiasi

Jinsi ya kupika na kuandaa

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya, kisha tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo kama kwenye picha.
Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Maana kamili ya Kwaresma

Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40). Mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu.
Kwaresma ni kipindi maalum ambacho wakristo wanakumbuka maisha ya Yesu kristo hapa duniani hususan mateso, kufa na kufufuka kwake.
Ni kipindi cha kutafakari maana na umuhimu wa dhabihu ya YESU kristo katika ukombozi wa dunia na kumrudia Mungu. Aidha ni kipindi ambacho wakristo wanakumbushwa kufanya toba na kumrudia Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Ingawa kipindi cha kwaresma ni kipindi cha mafungo kwa wakristo, watu wengi na hasa wa dini nyingine hushindwa kutambua funga inayofanywa na wakristo katika kipindi hiki na hasa kwa sababu wakristo wengi huonekana wakiendelea kula na kunywa wakati wa kwaresma. Wakristo walio wengi pamoja na kufuata kielelezo cha Yesu kristo ambae alifunga siku arobaini (usiku na mchana) huzingatia maagizo ya YESU mwenyewe na nabii Isaya ambao kwa kiasi kikubwa hufafanua aina ya funga ambayo wakristo wanapaswa kuizingatia.
Mwenyezi Mungu alitoa maagizo ya namna ya kufunga kupitia kwa nabii isaya akisema hivi
“Walakini wanitafuta kila siku, hupenda kujua njia zangu ; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao. Hutaka kwangu sheria za haki, humkaribia Mungu. Husema, mbona tumefunga lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. Je, kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je, ni siku ya mtu kujitabisha nafsi yake? je ni kuinamisha kichwa kama unyasi na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? je utasema ni siku ya kufunga na ya kukubaliwa na BWANA? Je, saumu niliyoichagua sio ya namna hii? Kufunguo vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaachia huru walio onewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia, utukufu wa BWANA (Mungu) utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita na BWANA ataitika, utalia nae atasema mimi hapa…” (Isaya 58: 2-9).
Mwenyezi Mungu alitoa maagizo haya baada ya kuona watu wengi wakipoteza muda mwingi na kujitabisha kuacha kula na kujitesa miili yao ili kumpendeza Mungu, huku wakisahau mambo muhimu zaidi ambayo Mungu anawataka wafanye ili kumpendeza. (Katika kipindi hicho wayahudi walikuwa wakifunga kwa kujitesa sana ikiwa ni pamoja na kuacha kula, kuvua nguo zao za thamani na kuvaa magunia, kujipaka majivu na wengine kujipiga na kujikata miili yao ili waone maumivu zaidi.
Aidha, watu walikuwa wakitumia kipindi cha kufunga kuuonesha umma jinsi walivyo wacha Mungu na hivyo kupewa heshima mtaani. Mtu asiyefunga alionekana mjinga, mtenda dhambi na asiyefaa katika jamii. Kufunga ilikuwa sehemu ya maisha na si suala la uhusiano binafsi kati ya mtu na Mungu).

Kwa vile Mwenyezi Mungu wetu ni wa upendo na huruma, alimtuma nabii isaya kuwaambia watu hao kuachana na funga hiyo isiyo na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika mambo muhimu ambayo Mungu anaangalia katika kutathimini utu wa mtu. Mambo hayo ni upendo, huruma na kujitoa kama ilivyoelezwa hapo juu na kuachana uovu wa aina zote.. Kwa msingi huo, mtu mwenye upendo na anaejitoa kusaidia wengine ana thamani kubwa mbele za Mungu kuliko mtu anaeshinda njaa siku 300 za mwaka pasipo kuonesha upendo wa kweli kwa wengine.
Yesu kristo alipokuja ulimwenguni, alisisitiza maneno ya nabii Isaya kwa kutaka watu waache tabia ya funga za kujionesha kwa watu, na badala yake wajitahidi kumpendeza Mugu.
Yesu alisema “Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye nyuso za kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amini nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako (Mungu) aliye sirini; na baba yako aonae sirini atakujazi” (Mathayo 6:16)
Kumbe tabia ya kujionesha mbele za watu kwamba tumefunga inamuudhi Mungu na kutufanya tukose thawabu. Mtu anaejionesha au kujisifu kwamba anafunga huambulia kusifiwa na watu wa kidunia ambao wanadhani mtu huyo ni mtakatifu sana, lakini kwa mujibu wa maandiko matakatifu mtu huyo anajisumbua na kupoteza muda wake bure kwani hakuna thawabu anayo pata kwa Mwenyezi Mungu.
Tumuombe Mungu sana atuongoze na kutusaidia katika kipindi hiki cha Kwaresma na baada ya hapo.Ni wajibu wetu kujitahidi kuachana na maovu yote, kufanya toba ya kweli na kumpokea Yesu katika mioyo yetu badala ya kumuabudu kwa midomo tu. Tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu wetu ni yule yule kabla, wakati na baada ya kipindi cha Kwaresma na hivyo kipindi hiki kiwe kipindi cha kutukumbusha na kutuandaa kwa ajili ya wakati mrefu ujao baada ya Kwaresma.

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia

Mahitaji

Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
Hamira (dried yeast 3/4 kijiko cha chakula)
Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
Ute wa yai 1(egg white)
Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200°C kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake mafuta na umimine mchanganyiko. Kisha utie katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.

Kisa cha mzaramo na mchaga

MZARAMO V/S MCHAGA.
Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote
kwa tsh. 100,000/=
Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki
yako nakukuongeza laki nyingine.
MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa.
MZARAMO: “unaumwa nini?”
MCHAGA: “Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa..”
MZARAMO: “sawa, toa laki kabisa..”
Mchaga akatoa.
MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; “Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu..”
MCHAGA akanywa akatema faster; “Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?”
MZARAMO: “Umepona karibu tena..”
Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake.
MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau
sanaaaaa..”
MZARAMO akamwambia “hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..’
MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..’
MZARAMO: “nesi naomba kikopo no.27..”
MCHAGA: “ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?”
MZARAMO: “UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.

😄😄😄😄😁😁😁😁😁😁

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.

Kwa tabasamu, alijibu “Wako mbele yetu 3-0”!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?

“Kukata tamaa?
“Yule mvulana aliuliza kwa mshangao….”!?

Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho?

Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda!

Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele!

Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa, mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; such beautiful faith;

Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi:
“Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?”

Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja wako?

Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako?

Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?

Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho.

Lakini maadamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.

Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.

Usijipulizie kipenga chako cha mwisho we mwenyewe.

JIPE MOYO USIKATE TAMAA!

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

KAMWE USIKATE TAMAA.

Makonda wana mambo, Kila mtu ni ndugu yao

Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.

Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,

Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apande…

Duh… makonda noma…!!

Dalili na matibabu ya tatizo la upungufu wa damu

Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.

Dalili

Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.

· Kushindwa kupumua vizuri

· Vidonda kwenye ulimi au mdomoni

· Sehemu nyeupe ya jicho kuwa bluu

· Ngozi kuwa na rangi ya kijivu

· Kucha kuwa dhaifu

· Kusikia hasira na kuhamasika haraka

· Kuchoka sana kuliko kawaida

· Maumivu makali ya kichwa

· Kupungua kwa uwezo wa kufikiria

· Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama

· Miguu na mikono kuwa ya baridi sana

· Uchovu wa mara kwa mara

Matibabu.

Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.

Amri ya Saba ya Mungu: Usiibe – Tambua mali ya mtu na kuheshimu

Je, Amri ya Saba ya Mungu inafundisha nini?

Amri ya saba ya Mungu inafundisha kuitambua mali ya mtu na kuiheshimu.


Mali ya mtu ni ipi?

Mali ya mtu ni ile aliyoipata kwa njia halali yaani kwa haki.


Lengo la mali ya binafsi ni lipi?

Kutosheleza mahitaji yake mtu binafsi, ya familia, ya wenye shida na ya kanisa.


Mtu awatendeje wanyama?

Mtu anatakiwa kuwatendea wanyama kwa wema kama viumbe wa Mungu


Amri ya saba ya Mungu inakataza nini?

Inakataza haya;

1. Wizi
2. Kulangua
3. Kutapeli
4. Kughushi
5. Kufuja mali
6. Kutoa au kupokea rushwa
7. Ufisadi
8. Kuharibu mali ya mtu au jamii


Anayejipatia mali kwa njia isiyo ya halali yampasa kufanya nini?

Anayejipatia mali kwa njia isiyo ya halali yampasa kurudisha gharama yake kwa mwenye mali


Anayeharibu mali ya mwingine lazima afanye nini?

Anayeharibu mali ya mwingine lazima alipe hasara aliyosababisha. (Lk 19:8)


Je yatupasa kufanya kazi?

Ndiyo, kwa sababu:

1. Kazi inampa mwanadamu heshima
2. Kufanya kazi ni wajibu wa haki. (Mwa 1:28)


Je ni lazima kuwasaidia masikini na fukara?

Ndiyo, Kuwatendea Masikini mema ni kumtendea Yesu mwenyewe. (Mt 25:40)

Mapishi ya Maini ya ng’ombe

Mahitaji

Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho

Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

MAHITAJI

Nyama iliyokatwa vipande – 1 Ratili(LB)

Mchele Basmati – 2 Magi

Chumvi ya wali – kiasi

Kitungu kilichokatwa katwa – 1 kikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yogurt) – ½ kikombe

Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari – 2 vijiko vya supu

Mafuta kidogo yakukaangia

Rangi ya manjano (ukipenda)

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Osha mchele na roweka nusu saa .

Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).

Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.

Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.

Tia maji gilasi 1½- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.

Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.

Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.

Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.

Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.

Shopping Cart
22
    22
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About