Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaaliโ€ฆ mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mweziโ€ฆ?๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mafundisho makubwa ya Yesu Kristo

Heri

Basi Yesu alipoona makutano, alipanda
mlimani akaketi chini, nao wanafunzi
wake wakamjia. 2Ndipo akaanza kuwafundisha,
akisema:
3 โ€œWana heri walio masikini wa roho,
maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.
4Wana heri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.
5Wana heri walio wapole,
maana hao watairithi nchi.
6Wana heri wenye njaa na kiu ya haki,
maana hao watatoshelezwa.
7Wana heri wenye huruma,
maana hao watapata rehema.
8Wana heri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.
9Wana heri walio wapatanishi,
maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10Wana heri wanaoteswa kwa sababu ya haki,
maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.
11Mna heri ninyi watu watakapowashutumu
na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya
aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini
na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni
kuu.

Chumvi na Nuru

13โ€˜โ€˜Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini
chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje
kurudishiwa ladha yake tena ? Haifai tena kwa
kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na
watu.
14โ€˜โ€˜Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji
uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. 15Wala
watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli.
Badala yake, huiweka kwenye kinara chake,
nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani
ya ile nyumba. 16Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze
mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu
mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kutimiza Sheria

17โ€œMsidhani kwamba nimekuja kuondoa
Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza.
18Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu
na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja
ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo
yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe
kimetimia. 19Kwa hiyo, ye yote atakayevunja
mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri
hizi, naye akawafundisha wengine kufanya
hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa
Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na
kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika
Ufalme ya Mbinguni. 20Kwa maana nawaambia,
haki yenu isipozidi haki ya waandishi wa sheria
na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika
Ufalme wa Mbinguni.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Hasira

21โ€œMmesikia walivyoambiwa watu wa
zamani kwamba, โ€˜Usiue, ye yote atakayeua
atapasiwa hukumu.โ€™ 22Lakini mimi nawaambia
kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake
wa kiume au wa kike, atapasiwa hukumu. Tena,
ye yote atakayemwambia ndugu yake wa kiume
au wa kike, โ€˜Racaโ€™a, yaani kumdharau na
kumdhihaki, atapasiwa kufanyiwa baraza. Lakini
ye yote atakayesema โ€˜We mpumbavu ulaaniwe!โ€™
Atapasiwa hukumu ya moto wa jehanam.
23โ€œKwa hiyo, kama unatoa sadaka yako
madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako
ana kitu dhidi yako, 24iache sadaka yako hapo
hapo, mbele ya madhabahu, uende kwanza
ukapatane na ndugu yako wa kiume au wa kike,
kisha urudi na ukatoe sadaka yako.
25โ€œPatana na mshtaki wako upesi wakati
uwapo njiani pamoja naye kwenda
mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia
mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia
mikononi mwa walinzi, nawe ukatupwa
gerezani. 26Amin, nakuambia, hutatoka humo
mpaka umelipa hadi senti ya mwishoโ€

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Uzinzi

27โ€œMmesikia kwamba ilinenwa, โ€˜Usizini’.
28Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote
amtazamaye mwanamke kwa kumtamani,
amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29Jicho
lako la kuume likikufanya utende dhambi, ling’oe
ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza
kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako
mzima utupwe jehanam. 30Kama mkono wako
wa kuume ukikufanya utende dhambi, ukate
uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza
kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako
mzima utupwe jehanam.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Talaka

31โ€˜โ€˜Pia ilinenwa kwamba, โ€˜Mtu ye yote
amwachaye mkewe na ampe hati ya talaka.โ€™
32Lakini mimi nawaambia, ye yote amwachaye
mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati,
amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na ye yote
amwoaye yule mwanamke aliyeachwa azini.โ€™โ€™

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kuapa

33โ€œTena mmesikia walivyoambiwa watu wa
zamani kwamba, โ€˜Usiape kwa uongo, bali
timizeni, nadhiri zile ulizofanya kwa Bwanaโ€™
34Lakini mimi nawaambia,โ€™โ€™Msiape kabisa, ama
kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha
Mungu, 35au kwa nchi, kwa kuwa ndipo mahali
pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu,
kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36Nanyi
msiape kwa vichwa vyenu kwa kuwa hamwezi
kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe
au mweusi. 37โ€˜Ndiyo,โ€™ yenu iwe โ€˜Ndiyoโ€™ na
โ€˜Hapanaโ€™, yenu iwe โ€˜Hapana.โ€™ Lo lote zaidi ya hili
latoka kwa yule mwovu.โ€™โ€™

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kulipiza Kisasi

38โ€œMmesikia kwamba ilinenwa, โ€˜Jicho kwa
jicho na jino kwa jino.โ€™ 39Lakini mimi nawaambia,
msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu
akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na
la pili pia, 40Kama mtu akitaka kukushtaki na
kuchukua shati lako, mwachie achukue na koti
pia. 41Kama mtu akikulazimisha kwenda
kilometa moja, nenda naye kilometa mbili.
42Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie
kisogo yeye atakaye kukukopa.โ€™โ€™

Mafundisho ya Yesu kuhusu Upendo Kwa Adui

43โ€˜โ€˜Mmesikia kwamba ilinenwa, โ€˜Mpende
jirani yako na umchukie adui yako.โ€™ 44Lakini
mimi ninawaambia : Wapendeni adui zenu na
waombeeni wanaowatesa ninyi, 45ili mpate
kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa
maana Yeye huwaangazia jua lake watu waovu
na watu wema, naye huwanyeshea mvua
wenye haki na wasio haki. 46Kama mkiwapenda
wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani?
Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?
47Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je,
mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu
wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 48Kwa hiyo
iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni
alivyo mkamilifu.โ€™โ€™

Mafundisho ya Yesu kuhusu Kuwapa Wahitaji

โ€˜โ€˜Angalieni msitende wema wenu mbele ya
watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya
hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu
aliye mbinguni.
2โ€˜โ€˜Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige
panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki
katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na
watu. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha
kupokea thawabu yao. 3Lakini ninyi mtoapo
sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa
kushoto usijue mkono wako wa kuume
unachofanya, 4ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo
Baba yako wa mbinguni, Yeye aonaye sirini
atakupa thawabu kwa wazi.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu kusali

5โ€œNanyi msalipo, msiwe kama wanafiki,
maana wao hupenda kusali wakiwa
wamesimama katika masinagogi na kando ya
barabara ili waonekane na watu. Amin, amin
nawaambieni, wao wamekwisha kupata
thawabu yao. 6Lakini wewe unaposali, ingia
chumbani mwako, funga mlango na umwombe
Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye
sirini atakupa thawabu yako. 7โ€œNanyi mnaposali
msiseme maneno kama wafanyavyo watu
wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani
kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa
maneno yao. 8Msiwe kama wao, kwa sababu
Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla
hamjamwomba.โ€™โ€™
9โ€˜โ€˜Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba :
โ€œBaba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
10Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike hapa duniani
kama huko mbinguni.
11Utupatie leo riziki zetu za kila siku.
12Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tulivyokwisha
kuwasamehe wadeni wetu.
13 Usitutie majaribuni,
bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu,
kwa kuwa Ufalme ni Wako na nguvu
na utukufu hata milele. Amen.โ€
14Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine
wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe pia na ninyi. 15Lakini
msipowasamehe watu wengine makosa yao,
wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa
yenu.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kufunga

16โ€œMnapofunga, msiwe wenye huzuni kama
wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja
nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba
wamefunga. Amin, amin nawaambia wao
wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu.
17Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani
na kunawa nyuso zenu 18ili kufunga kwenu
kusionekane na watu wengine ila Baba yenu
aliye sirini, naye Baba yenu aonaye sirini
atawapa thawabu yenu kwa wazi.โ€

Akiba Ya Mbinguni

19โ€œMsijiwekee hazina duniani, mahali
ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi
huvunja na kuiba. 20Lakini jiwekeeni hazina
mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu
haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba.
21Kwa sababu mahali akiba yako ilipo, hapo
ndipo pia moyo wako utakapokuwa.โ€™โ€™

Jicho Ni Taa Ya Mwili

22โ€˜โ€˜Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni
nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru.
23Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote
utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru
iliyomo ndani yako ikiwa giza, hilo ni giza kuu
namna gani ! โ€

Mungu Na Mali

24โ€˜โ€˜Hakuna mtu ye yote awezaye
kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama
atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine,
au atashikamana sana na huyu na kumdharau
huyu mwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia
Mungu na malia.โ€™โ€™

Msiwe Na Wasiwasi

25โ€˜โ€˜Kwa hiyo nawaambia, msiwe na
wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au
mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa
nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili
zaidi ya mavazi? 26Waangalieni ndege wa
angani, wao hawapandi wala hawavuni au
kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni
huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi
kuliko hao ndege? 27Ni nani miongoni mwenu
ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza
kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha
yake au kuongeza dhiraa mojab kwenye kimo
chake ?
28โ€˜โ€˜Nanyi kwa nini kujitaabisha kwa ajili ya
mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo.
Hayafanyi kazi wala hayafumi. 29Lakini
nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari
yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo
maua. 30Lakini ikiwa Mungu anayavika hivi
majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho
yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri
zaidi, enyi wa imani haba? 31Kwa hiyo msiwe na
wasiwasi, mkisema, โ€˜Tutakula nini?โ€™ Au
โ€˜Tutakunywa nini?โ€™ Au โ€˜Tutavaa nini?โ€™ 32Kwa
maana watu wasiomjua Mungu ndio
wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa
mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo
yote. 33Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa
Mungu na haki yake na haya yote
mtaongezewa. 34Kwa hiyo msiwe na wasi wasi
kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia
yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.โ€™โ€™

Mafundisho ya Yesu kuhusu Kuwahukumu Wengine

โ€œUsihukumu ili usije ukahukumiwa. 2Kwa
maana kwa jinsi ile unavyowahukumu
wengine, ndivyo utakavyohukumiwa na kwa
kipimo kile utakachotoa ndicho utakachopokea.
3โ€˜โ€˜Kwa nini unatazama kibanzi kidogo
kilichomo kwenye jicho la ndugu yako na wala
huoni boriti iliyoko kwenye jicho lako? 4Au
unawezaje kumwambia ndugu yako, โ€˜Acha nitoe
kibanzi kwenye jicho lako wakati kuna boriti
kwenye jicho lako mwenyewe ?โ€™ 5Ewe mnafiki,
toa kwanza boriti kwenye jicho lako mwenyewe,
nawe ndipo utakapoona wazi ili kuondoa kibanzi
kilichoko kwenye jicho la ndugu yako.
6โ€˜โ€˜Msiwape mbwa vitu vilivyo vitakatifu, wala
msitupie nguruwe lulu zenu. Kama mkifanya
hivyo, watazikanyaga kanyaga na kisha
watawageukia na kuwararua vipande vipande. โ€

Omba, Tafuta, Bisha

7โ€œOmbeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi
mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
8Kwa maana kila aombaye hupewa, naye
atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa
mlango.
9โ€˜โ€˜Au ni nani miongoni mwenu ambaye
mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe?
10Au mwanawe akimwomba samaki atampa
nyoka? 11Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua
jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi
sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu
vizuri wale wamwombao ? 12Kwa hiyo cho chote
ambacho mngetaka mtendewe na watu, ninyi
nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii
ndiyo Torati na Manabii.โ€™โ€™

Njia Nyembamba Na Njia Pana

13โ€˜โ€˜Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba,
kwa maana lango ni pana na njia ni pana
ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa
kupitia lango hilo. 14Lakini mlango ni
mwembamba na njia ni finyo ielekayo kwenye
uzima, nao ni wachache tu waionao.โ€™โ€™

Mti na Tunda lake

15โ€œJihadharini na manabii wa uongo,
wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya
kondoo, lakini ndani wao ni mbwa mwitu
wakali.16Mtawatambua kwa matunda yao. Je,
watu huchuma zabibu kwenye miiba au tini
kwenye michongoma? 17Vivyo hivyo, mti
mwema huzaa matunda mazuri na mti mbaya
huzaa matunda mabaya. 18Mti mwema hauwezi
kuzaa matunda mabaya wala mti mbaya
hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19Kila mti
usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa
motoni. 20Hivyo, kwa matunda yao,
mtawatambua.โ€™

Mwanafunzi Wa Kweli

21โ€œSi kila mtu aniambiaye, โ€˜Bwana, Bwana,โ€™
atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni
yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye
mbinguni. 22Wengi wataniambia siku ile,
โ€˜Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako
na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza
mingi? 23Ndipo nitakapowaambia wazi,
`โ€™Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi
watenda maovu!โ€™

Msikiaji Na Mtendaji

24โ€˜โ€˜Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya
maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu
mwenye busara aliyejenga nyumba yake
kwenye mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko
yakaja na upepo ukavuma ukaipiga hiyo
nyumba, lakini haikuanguka kwa sababu msingi
wake ulikuwa kwenye mwamba. 26Naye kila
anayesikia haya maneno yangu wala
asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga
nyumba yake kwenye mchanga. 27Mvua
ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo
ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo
ikaanguka kwa kishindo kikubwa.โ€™โ€™
28Yesu alipomaliza kusema maneno haya,
makutano ya watu wakashangazwa sana na
mafundisho yake, 29kwa sababu alifundisha
kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama
walimu wao wa sheria.

Mafundisho Kuhusu Bikira Maria

DOGMA ZA KANISA KATOLIKI KUHUSU BIKIRA MARIA.

Kuna mafundisho makuu manne
kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima
kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na
ufunuo wa Mungu: 1. B. Maria
mkingiwa dhambi ya asili 2. B. Maria
Mama wa Mungu 3. B. Maria Bikira
daima 4. B. Maria kupalizwa mbinguni
mwili na roho

MKINGIWA DHAMBI YA ASILI

Malaika alimsalimia Maria โ€œumejaa
neemaโ€ (Lk 1:28) maana ndiye tunda
bora la ukombozi ulioletwa na Yesu. Ni
imani ya Wakatoliki kwamba kwa stahili
za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi
dhambi ya asili na madonda
yanayotokana nayo, wala asitende
dhambi maisha yake yote. Kwa maneno
mengine, Bikira Maria tangu atungwe
mimba Mungu alimkinga na kila doa la
dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu
Kristo aliye Mkombozi wa binadamu
wote. Ndiye aliyekombolewa kwa namna
bora kushinda viungo vyote vya Kanisa.
Maisha yake yote hakutenda dhambi
hata moja. Mapokeo ya mashariki
yanamuita โ€œA Panagiaโ€ = โ€œMtakatifu tuโ€.
Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX
mwaka 1854, halafu mwaka 1858 Bikira
Maria alijitambulisha kama Mkingiwa
kwa Bernadeta Soubirous huko Lurdi
( Ufaransa ). Tena mwaka 1917 huko
Fatima ( Ureno ) aliwafunulia Lusia,
Fransisko na Yasinta Marto moyo wake
safi usio na doa.

MAMA WA MUNGU

Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo,
โ€œHapo mwanzo kulikuwako Neno, naye
Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno
alikuwa Munguโ€ (Yoh 1:1). Huyo Mungu
Mwana alitwaa ubinadamu katika Bikira
Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu,
maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni
binadamu kama sisi katika yote
isipokuwa dhambi. Ubinadamu wa Yesu
unategemea Nafsi yake ya Kimungu:
akisema, โ€˜Mimiโ€™, ni kwa Nafsi yake hiyo.
Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi,
โ€œKweli nawaambia, kabla Abrahamu
hajazaliwa, nalikuwepoโ€ (Yoh 8:50).
โ€œKama vile Baba alivyo asili ya uhai,
ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili
ya uhaiโ€ (Yoh 5:26).
Mtume Paulo akaeleza, โ€œWakati
maalumu ulipotimia Mungu alimtuma
Mwanae aliyezaliwa na mwanamkeโ€ (Gal
4:4). Bikira Maria ni Mama wa Mungu
kwanzia wakati huo: tangu Bikira Maria
alipojaliwa kumchukua mimba, kumzaa,
kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye
kwa asili ni Mungu. Cheo hicho
kimemuinua juu kuliko hata malaika.
โ€œMalaika alimwambia, โ€˜Hicho
kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu,
Mwana wa Munguโ€™โ€ (Lk 1:35).
Dogma ilitangazwa mwaka 431 kwenye
Mtaguso wa Efeso uliomuita โ€œMzazi wa
Munguโ€, ukisema Maria anastahili
kuitwa hivyo kwa sababu Mwana wa
milele wa Mungu, ambaye ni Mungu
sawa na Baba, alifanyika mtu toka
kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa:
โ€œUmebarikiwa wewe katika wanawake,
naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Limenitokeaje neno hili, hata mama wa
Bwana wangu anijilie mimi?โ€ (Lk
1:42-43). Ungamo hilo la Elizabeti
likakamilishwa na Mtume Thoma
aliyemuambia Yesu mfufuka: โ€œBwana
wangu na Mungu wangu!โ€ (Yoh 20:28).

BIKIRA NA MAMA

Wakristo na Waislamu wote wanakiri
kuwa Yesu alitungwa bila ya mchango
wa mwanamume. La ajabu zaidi katika
imani hiyo ni kwamba hata uzazi
wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali
uliutakasa: ni Bikira daima. Ingawa akili
inasita, ni lazima kukiri na malaika,
โ€œHakuna lisilowezekana kwa Munguโ€ (Lk
1:38). Yosefu , ingawa kisheria alikuwa
mume wake, hakutenda naye tendo la
ndoa.
Ni imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi
kuwa Mama wa Yesu anastahili kuitwa
โ€œBikira daimaโ€ kwa sababu alimchukua
mimba akiwa bikira, akamzaa bila ya
kupotewa na ubikira, akabaki bikira hadi
mwisho wa maisha yake. Hamu yake ya
kuwa bikira hata kisha kuchumbiwa
inajitokeza katika jibu alilompa malaika
aliyemtabiria mimba: โ€œLitakuwaje neno
hili, maana sijui mume?โ€ (Lk 1:35). Ni
kielelezo cha Wakristo ambao Mtume
Paulo aliwaandikia: โ€œNawaonea wivu,
wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea
mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira
safiโ€ (2Kor 11:2), โ€œmpate kumhudumia
Bwana pasipo kuvutwa na mambo
mengineโ€ (1Kor 7:35).
Wanaosemwa katika Injili โ€œndugu zake
Yesuโ€ si watoto wa Bikira Maria, bali
ndugu wa ukoo waliokuwa jirani sana
na familia hiyo takatifu. Kama Bikira
Maria angekuwa na watoto wengine,
Yesu angekuwa amefanya kosa la
kuwanyangโ€™anya Mama yao na
kumfanya awe Mama wa mtume
Yohane alipomkabidhi msalabani,
โ€œโ€˜Mwana, tazama Mama yakoโ€™. Na tangu
saa ile huyo mwanafunzi alimchukua
akae nyumbani kwakeโ€ (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo
anayeitwa na mtume Paulo โ€œndugu yake
Bwanaโ€ (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa
maarufu katika Kanisa la Yerusalemu
(Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal
2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo
kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni
Yakobo ndugu yake Yose na mama yao
kwenye Injili anaitwa โ€œMaria mwingineโ€,
si Maria Mama wa Yesu. โ€œWalikuwepo
pia wanawake waliotazama kwa mbali.
Miongoni mwao akiwa Maria
Magdalena , Salome na Maria mama wa
akina Yakobo mdogo na Yoseโ€ (Mk
15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida
kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa
wengi hivyo, tujue kuwatofautisha
kwenye Injili, ambazo zinamtaja Bikira
Maria kama โ€œMama wa Mungu”

KUPALIZWA MBINGUNI MWILI NA ROHO

Baada ya maisha haya ya duniani Bikira
Maria alipalizwa mbinguni mwili na
roho, ishara ya mwanamke mshindi.
โ€œIshara kubwa ikaonekana mbinguni,
ambapo mwanamke aliyevikwa jua , pia
na mwezi chini ya miguu yake, na taji la
nyota kumi na mbili juu ya kichwa
chakeโ€ (Ufu 12:1). Maneno ya shangilio
lake yametimia: Mungu โ€œamewaangusha
wakuu katika viti vyao vya enzi; na
wanyonge amewakwezaโ€ (Lk 1:52).
Imani hiyo ya mapokeo ya kale,
yanavyoshuhudiwa na Mababu wa
Kanisa, ilitangazwa rasmi na Papa Pius
XII kwa niaba ya ma askofu wote mwaka
1950.

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi mazuri ya Uji wa ulezi

Mahitaji

Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula)
Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe)
Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai)
Siagi (butter kijiko 1 cha chakula)
Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)

Matayarisho

Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.

Jinsi ya kupika Biskuti Za Tende Na Ufuta

Viambaupishi

Unga 3 Vikombe vya chai

Baking powder 1 ยฝ Vijiko vya chai

Sukari 1 Kikombe cha chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Mayai 2

Maji kiasi ya kuchanganyia

Tende 1 Kikombe

ufuta ยผ kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli

2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.

3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.

4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.

5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande kama katika picha.

6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.

7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Kama una miaka 24 hadi 29 huu ni ujumbe wako, Soma hii tafadhali

ITAKUSAIDIA KIJANA PLEASE ISOME NA UITAFAKARI

SINTOFAHAMU MAISHANI KATI YA MIAKA 24 HADI 29
1. Umri mgumu zaidi katika maisha yako ni kati ya miaka 24 hadi 29 hivi. Presha ya kuwa mtu wa aina fulani au levo fulani ya maisha katika umri huo ni kubwa sana.

2. Kila ukitazama unaona watu wengine wanaishi vizuri sana, tena maisha unayoyatamani na wanayafurahia. Wewe unahisi kama unasukuma siku tu.

3. Umeomba kazi sehemu kibao lakini kila ukijibiwa ni jibu la kwamba umekosa na tena sehemu nyingine hata jibu hupati.

4. Bahati mbaya sana huu ndio muda au umri ambao wengi wanachanganyikiwa kabisa. Muda ambao kama mtu hana subira au umakini wa kutosha anajikuta katika ulevi wa kupindukia au madawa ya kulevya au kilevi chochote.

5. Kwa sababu kukata tamaa kunakuwa kwingi unajikuta unatafuta njia mbadala za kukimbia uhalisia. Unatafuta ulevi wako. Pombe! Madawa! Bangi! Kamari! Mwanamke!

6. Mbaya zaidi unakuta baadhi ya watu uliosoma nao wamepata bahati ya kupata kazi nzuri. Jinsi muda unavyoenda unahisi idadi ya marafiki zako inapungua โ€“

7. Sio kwamba marafiki wanakutenga lakini wewe mwenyewe tu unaona bora ujitenge kwa namna hali ilivyo.

8. Hebu fikiria utafanya nini ukiwa katika WhatsApp group na marafiki zako wanajadili kuhusu safari ya kula starehe Zanzibar wiki ya wiki iliyopita

9. na hapo wanaendelea kujadili mipango ya kuchagua wikiendi fulani wakavinjari Ngorongoro au Serengeti na wake au wapenzi wao. Wewe utachangia nini wakati hata hujui mlo wako kesho utatoka wapi?

10. Mara nyingi unajikuta chat za kwenye group WhatsApp kama hizo unazisoma kimyakimya mwenyewe kama msalaba kwenye kaburi.

11. Kidogo kidogo unagundua hao watu na hili group la WhatsApp sio saizi yangu

12. kwa sababu kadiri unavyokaa karibu na group kama hilo au watu wa aina hiyo ndivyo jinsi ambavyo unazidi kupata au kujipa presha.

13. Si unajua zile stori za kwenye magroup ya WhatsApp za house party zikianza inabidi ujifanye bubu maana unawaza ikifika zamu yako hili kundi la watu 15 litaenea wapi katika chumba chako kimoja ulichopanga Sinza kwa Remi.

14. Ushawahi kukaa kwenye kundi la watu wanajadili iPhone mpya au jinsi ambavyo Fastjet wanatoa huduma mbovu?

15. hapo unasikia moyo wako unakwambia โ€œkijana, huu ni ule muda wa maumivu ya moyo, huwezi kutafuta group ambalo wanajadili bodaboda?

16. Ila unabaki tu katika hilo group, unatulia kimya unatazama raia wanavyojadili maisha yao bora na wewe unakuwa kama secretary anavyoandika summary za vikao.

17. Unasahaulika kabisa kama kilema aliyesinzia kwenye daladala (huwa hadi wanapitishwa vituo)

18. Mara moja moja unakuta mmoja ya marafiki zako anakuuliza kama unahitaji bia nyingine

19. unawaza sijui niseme hapana niondoke zangu niende home? Ila unawaza tena home nikafanye ishu gani mida hii?

20. Unajikuta unajibu: โ€œYes kaka, ngoja ninywe moja ya mwishoโ€. Mwongo!

21. Kosa kubwa unaloweza kufanya kipindi kama hiki bro ni kujaribu kuwa na mpenzi.

22. ukweli ni kwamba mtu ambaye anapitia nyakati kama hizi kwenye mapenzi ataleta tafrani tu. Mapenzi ni furaha na ili umpe mtu furaha lazima kwanza wewe mwenyewe uwe na furaha. Huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna.

23. Huu ndo ule wakati ambao utaona wasichana ambao ungetamani kuwa nao wanatoka au wanaolewa na wanaume waliokuzidi umri zaidi ya miaka 10.

24. Halafu ndugu yangu huwezi hata kuwalaumu. Ni kwamba tu spidi ya maisha yako haiendani na malengo yao. So inabidi tu uelewe.

25. Wasichana wengi ambao utakuta nao muda kama huu tena kama una bahati sana wanaweza kukuvumilia mpaka utimize miaka 28 au 29,

26. na ukitimiza 29 maisha yako bado hayasomeki jiandae kuachwa.

27. Lakini katika umri huu unajifunza mengi sana kuhusu maisha.

28. Maisha yanakufunza mengi kuhusu uvumilivu, na kushukuru Mungu wako kwa kile unachopata kila siku,

29. yanakufundisha kitu kuhusu urafiki, mapenzi, kazi na kujitambua mwenyewe.

30. Huu daima ndio wakati wako wa kuamka au kuanguka moja kwa moja kwenye maisha kutegemea nini utaamua kufanya.

31. Namna utakavyoishi maisha yako kati ya miaka 30 hadi 39 na kuendelea itategemea sana namna ambavyo utayashinda maisha haya ya majaribu mengi kati ya miaka 24 hadi 29.

Never giv upโ€ฆ.

๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ™ˆ

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About