Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya maji ya kunyunyiza kwenye majani

Mbolea ya kunyunyiza ni nzuri kwani inasaidia kuupa mmea virutubisho moja kwa moja kupitia kwenye majani au shina ambapo ndipo chakula kinahitajika.

Faida za mbolea ya maji ni pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha mavuno, uwezo wa mimea kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa, kuvumilia ukame, na kuongeza ubora wa mazao.

Jinsi ya kuandaa mbolea ya maji kwa kutumia samadi

Mbolea ya maji hutengenezwa kwa kuchukua kiroba kilichojazwa samadi, aina mbalimbali ya mimea yenye virutubisho na inayoaminika kuwa dawa ya mimea. Kiroba hicho kinafungwa kwenye kijiti, na kutumbukiza kwa kuningโ€™inia kwenye pipa lililojazwa maji.

Kiroba hicho ni lazima kichukue kati ya kilo 30-50 za samadi pamoja na aina nyingine za mimea kwa maji lita 200 (tazama mchoro). Unaweza kushika upande mmoja wa mti na kunyanyua na kushusha kila baada ya siku tano ili kuchanganya na kuharakisha kutolewa kwa virutubisho zaidi.

Kwa kawaida mchanganyiko huo unakuwa na harufu kali sana maana Nitrojeni nyingi inayopatikana hugeuka kuwa Amonia. Ni vizuri kufunika pipa ili kuzuia kuyeyuka kwa nitrojeni. Harufu ikishaisha, ujue mbolea yako ipo tayari kwa matumizi.

Ongeza maji na utingishe vizuri kabla ya kutumia. Nyunyizia mimea yako kila wiki mpaka utakapoona mabadiliko.

Jinsi ya kutengeneza mbolea ya maji kwa kutumia mimea peke yake (Majani fresh)

Mbolea hii hutengezwa kwa kuchukua majani mabichi na kuyakatakata na kisha kuyachanganya na maji kidogo.

Baada ya kuchanganya na maji unaacha kwa siku tatu au nne ambapo utatikisa mchanganyiko wako kila siku.

Baadae utatikisa na kuchanganya na maji na kunyunyiza shambani.

Vilevile Unaweza kutumia mbolea ya majani ambayo itakuwa kama dawa ya kuulia wadudu, kwa kutumia aina ya mimea kama vile mivule, mibangi mwitu, majani ya minyanya, mwarobaini, mashona nguo, pamoja na vitunguu saumu. Aina hii ya mimea inasaidia sana katika kuzuia magonjwa, wadudu na kutoa virutubisho muhimu kwa mimea vinavyosaidia mkulima kupata mazao bora bila gharama ya ziada ya kununua virutubisho.

Vigezo vya kunyunyiza mbolea ya maji

Ili upate matokeo mazuri wakati wa kunyunyiza mbolea ya maji unatakiwa kufuata vigezo vifuatavyo:
โ€ข Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
โ€ข Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
โ€ข Unatakiwa kutingisha vizuri mbolea yako ya maji kabla ya kunyunyiza. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
โ€ข Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
โ€ข Unatakiwa kunyunyizia mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.

Angalizo
Kabla ya kunyunyiza dawa au mbolea uliyoitengeneza mwenyewe shambani nyunyiza kwenye eneo dogo au mimea michache kwanza ili uone kama inaunguza au haiunguzi. Kumbuka kuwa mchanganyiko mwingine ukiwa cream au ukikolea sana unaweza kuchoma. Kwa hiyo kuepuka hili nyunyiza mahali padogo kwanza.

Jinsi ya kupika Wali wa hoho

Wali wa hoho ni chakula maalum kinachotumika katika hafla au sherehe. Ni chakula chenye ladha nzuri na kina muonekano wa kuvutia kinapokuwa mezani tayari kwa kuliwa.

Mara nyingi huandaliwa kama zawadi katika harusi hususan kwa watu wa pwani. Kwa kuwa zawadi hiyo au maarufu kama kombe huwa kuna vyakula vingi, ikiwamo chakula hiki ambacho hufanya kombe kuwa na muonekano wa kupendeza.

Mbali na kuliwa kama kombe chakula hiki kinaweza kuandaliwa kama mlo wa usiku.

Mahitaji:

โ€ข Mchele ยฝ kg
โ€ข Nyanya 3
โ€ข Mafuta ya kupika ยผ kikombe cha chai
โ€ข Chumvi kiasi
โ€ข Kitunguu swaumu kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
โ€ข Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
โ€ข Hoho 4
โ€ข Nyama ya kusaga ยผ
โ€ข Tangawizi kijiko 1 cha chakula
โ€ข Limao au ndimu kipande

Maadalizi:

โ€ข Chukua mchele uoshe vizuri kasha chuja maji
โ€ข Chukua nyama ya kusaga na kamulia ndimu, weka chumvi na tangawizi, changanya vizuri na weka jikoni.iache ichemke hadi ikauke maji yote.
โ€ข Chukua maji na kiasi cha robo tatu lita chemsha na weka pembeni
โ€ข Chukua sufuria kavu yenye uwezo wa kupika kiasi cha kilo moja
โ€ข Weka mafuta ya kupika kiasi cha vijiko vitatu na acha yapate moto
โ€ข Weka vitunguu maji, menya nyanya na katakata halafu weeka katika sufuria hiyo.
โ€ข Weka chumvi na kanga hadi vilainike kabisa
โ€ข Baada ya kuiva weka vitunguu swaumu na baadaye mchele
โ€ข Koroga hadi uchanganyike na weka nyama. Endelea kukoroga, baada ya hapo weka maji kiasi cha kuivisha mchele huo. Acha vichemke hadi vikaukie.
โ€ข Palia mkaa juu yake au kama unatumia jiko la gesi au umeme weka kwenye oven hadi maji yakauke kabisa.
โ€ข Baada ya hapo chukua hoho na kasha kata upande wa juu kama vifuniko. Kasha ondoa matunda ya ndani yake. Funika na kasha zipange kwenye sufuria yenye maji na chumvi na mafuta kidogo kiasi cha kijiko kimoja. Chemsha jikoni hadi ziive.
โ€ข Baada ya kuiva, chukua hoho zako na kasha chota wali kw akutumia kijiko kasha jaza katika kila hoho na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
โ€ข Unaweza kupamba na salad ukipenda.

Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)

Viamba upishi

Mboga za majani makavu ยผ kg
Mafuta vijiko vikubwa 3-4
Karanga zilizosagwa kikombe ยฝ
Maziwa au tui la nazi kikombe 1
Kitunguu 1
Nyanya 2
Chumvi (kama kuna ulazima)
Maji baridi

Hatua

โ€ข Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15.
โ€ข Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu.
โ€ข Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike.
โ€ข Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike.
โ€ข Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto.
โ€ข Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5.
โ€ข Onja chumvi, pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Weka nyanya kidogo.
Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa.
Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.

Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori – 1 kilo moja

Vitunguu maji – 3

Karoti – 2

Siagi – 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) – 1 kimoja

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

ร“sha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala – kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.

Maisha ya Wasichana Wa facebook na instagram

Wiki ya kwanza
Status:”Location flani amazing”
“Having fun”
“I love my life”
“sijali mnayosema nafanya nachotaka”

BAADA YA MIEZI MIWILI
STATUS:”Binadamu wengi ni wasaliti”
“trust nobody”
“Na hili nalo litapita”
BAADA YA MIEZI SITA
Status:”Yesu wewe ndio rafiki wa kweli”
“Bwana ndiye mchungaji wangu”
BAADA YA MIEZI TISA NA KIDOGO
STATUS: “Nakupenda mwanangu๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜€๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜„

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

THERE IS NO FUTURE IN THE PAST.** Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho.

Bahati nzuri Mungu alitujalia kusahau, ivyo siku zote sahau ya nyuma na waza yale ya mbele yako.

Maisha bora ya mbele hayawezi kuja kama akili yako imebeba kushindwa kwa nyuma.

Binadamu yeyote anayeweza kupoteza muda wake wa leo kwa kulaumu mabaya ya jana, kesho atapoteza muda akilaumu mabaya ya leo.

Tambua ya kuwa, “hakuna awezaye kurudi nyuma na kuanza upya, bali waweza kuanza leo na kutengeneza maisha yako ya kesho”

Kadri unavyofikiria ya nyuma ndivyo unavyochelewa kufika mbele zaidi. Penda zaidi ndoto yako ya kesho kuliko historia yako ya jana,maana hatima yako siku zote iko mbele na sio nyuma.

Siku zote utashindwa kwa kuendekeza mambo yaliopitwa na wakati maana utakuwa unatumia ujuzi uliopitwa na wakati.

“Habari njema ya siku ni leo, na siku nzuri yako ni ya kesho “

Ukiona umesononeka kwa maisha kuwa magumu jua unaumia kwaajili ya maisha yako ya nyuma, maana unawaza jinsi ulivyo shindwa kulipa kodi ya nyumba,ulivyoshindwa kulipa umeme, maji, ada za watoto na ulivyoshindwa kuendesha biashara yako au ulivyoshindwa kuitetea ajira yako. Usipoteze Muda wako kwa kuwaza yaliopita badala yake waza kesho yako itakuwaje.

Waswahili wanasema yaliopita si ndwele, tugange yajayo. Huwezi kubadilisha jana, Bali waweza kubadilisha kesho yako kwa kufanya maamuzi leo.

Usipoteze Muda kwa kugeuza shingo yako kutazama ya nyuma, utajikuta unadumbukia katika shimo la maisha magumu.

“You can’t have a better tomorrow if you are thinking about yesterday all the time “

Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana. Anza sasa.

Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe

Viamba upishi

Unga wa ngano 1 Kilo

Siagi ยผ kilo

Mayai 2

Kastadi (custard) 3 vijiko vya supu

Baking powder 1 kijiko cha chai

Maziwa 1 ยฝ gilasi

Mafuta Ya kukaangia kiasi katika karai

Maandalizi na upikaji

Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder.
Tia siagi uchanganye vizuri.
Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana.
Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake.

5- Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana.

6- Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira.

Vipimo Vya Shira

Sukari ยฝ kilo

Hiliki ilosagwa 1 kijiko cha chai

โ€˜arki (rose flavor) 5 matone

Maji 1 gilasi

Namna Ya Kutyarisha

Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito.
Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na โ€˜arki .
Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari.

Jinsi vitunguu swaumu vinavyosaidia kuzuia wadudu shambani

Vitungu saumu vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi ya magonjwa kutokana na kuwa na harufu kali inayosaidia kuwafukuza wadudu kama vidukari, bungo na hata panya.

Hatua za kufuata kutengeneza dawa ya kitunguu saumu

  1. Saga kitunguu saumu kimoja,
  2. Changanyakwenye lita moja ya maji
  3. Nyunyizia kwenye mazao.

Namna nyingine ya kutengeneza dawa

  1. Unaweza pia kusaga vitunguu saumu 3,
  2. kishachanganya na mafuta taa,
  3. acha ikae kwa siku tatu,
  4. kisha ongeza lita 10 za maji ya sabuni na unyunyizie.

Hii itaondoa aina nyingi sana ya wadudu wanaosababisha magonjwa.

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri

Mahitaji

Mchele – 4 vikombe

Kuku – 1

Vitunguu – 3

Nyanya/tungule – 4

Zabibu kavu – ยฝ kikombe

Tangawizi na kitunguu (thomu/galic) – 2 vijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) – 2 kijiko cha supu

Masala ya tanduri – 2 vijiko vya supu

Pilipili manga – 1 kijiko cha chai

Hiliki – ยฝ kijiko cha chai

Mdalasini – kijiti kimoja

Ndimu – 3 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Zaafarani (saffron) – 1 kijiko cha chai

Mafuta – ยฝ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Kuku:

Baada ya kumsafisha kuku, mkate vipande vikubwa vikubwa kiasi upendavyo, muoshe mchuje atoke maji.
Katika bakuli, tia tangawizi, kitunguu thomu ilosagawa, pilipili mbichi ilosagwa, chumvi, ndimu, mtindi, masala ya tanduri na uchanganye vizuri, kisha mtie kuku na uchanganye tena na acha arowanike kwa muda wa kiasi saa au zaidi.
Panga kuku katika sinia ya kuchoma ndani ya oveni. Kisha mchome (grill) hadi awive, mtoe acha kando. Mwagia juu yake masala yatakayobakia katika sinia baada ya kumchoma.

Namna Ya Kutayarisha Masala Ya Nyanya:

Weka mafuta katika karai, tia vitunguu ulivyokatakata, kaanga hadi vianze kugeuka rangi.
Tia nyanya ulizokatakata, tia pilipili manga, hiliki, mdalasini, chumvi, na zabibu. Kaanga kidogo tu yakiwa tayari.

Namna Ya Kutayarisha Wali:

Osha na roweka mchele wa basmati.
Roweka zaafarani kwa maji ya moto kiasi robo kikombe weka kando.
Chemsha maji, tia chumvi, kisha tia mchele uive nusu kiini.
Mwaga maji uchuje mchele kisha rudisha katika sufuria au sinia ya foil. Nyunyizia zaafarini, na rudisha katika moto upike hadi uive kamili.
Epua, kisha pakua wali katika sahani au chombo upendacho, mwagia juu yake masala ya nyanya. Kisha weka vipande vya kuku ulivyochoma, biriani ikiwa tayari

Jinsi ya kupika Pilau Ya Nyama Ya Ng’ombe Na Nyanya

Viambaupishi

Mchele (Basmati) 3 vikombe

Nyama ya ngoโ€™mbe 1 kg

Pilipili boga 1 kubwa

Nyanya 2 kubwa

Vitunguu maji 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Ndimu 1

Mafuta ya kupikia ยฝ kikombe

Mdalasini ยฝ kijiko cha chai

Binzari nyembamba 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ยฝ Kijiko cha chai

Hiliki ยฝ Kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

Loweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;

JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi

Wadada acheni hizo

Mfalme Sulemani alikuwa na wake 700 na alichepuka(cheated)na vimada 300 . Mpenzi wako/Mume wako unamfumania na kimada mmoja tu ugomvi na amani imapotea ndani ya nyumba,unasimulia kuanzia padri,mchungaji,ukoo wako mzima,mashoga, stress,vidonda vya tumbo,inapelekea mpaka unaokoka,eti kisa kamuonjesha mmojaโ˜ sasa akionjesha 700 si utakutwa Mirembe๏ฟฝ

Wadada acheni HIZO
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.

Mavazi ya Ofisini kwa Wadada

Wengi wetu tunashindwa kutofautisha mavazi ya sehemu husika mfano Ofisini, michezoni, na yale ya usiku na sehemu nyinginezo leo nitagusia vazi la ofisini kwa akina dada.

Unapotaka kuvaa vazi ,lazima uangalie vazi unalolivaa mda gani na mahala unapokwenda,siyo vazi la kutokea usiku au la kimichezo unalivaa ofisini,utakuwa kichekesho mbele za watu hata kwa wafanyakazi wenzio.

Mavazi ya kiofisi yanaeleweka lakini hasa kwa mwanamke basi vaa sketi fupi au ndefu na blauzi ya heshima iliyofunika kitovu chako, au suti ya heshima na koti na hata suruali ambayo haijakubana sana inafaa sana kwa ofisi.

Kama utapendelea kuvaa gauni basi angalia mkao wa hilo gauni ukoje maana mara nyingi gauni huwa halipendezi kuwa vazi la ofisini bali vazi la jioni.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About