MAFUNDISHO MUHIMU KUHUSU MWILI NA DAMU YA YESU KRISTU | BIBLIA INAVYOELEZA KUHUSU EKARISTI
Yesu alituambia nini kuhusu Mwili wake na damu yake?
Damu na Mwili aliotupa Yesu ni nini? Ekaristi ni nini hasa?
Fundisho hili la mwili na damu ya Yesu (Ekaristi) lilikua Agizo tunalopaswa kulitii mpaka leo?
Mitume walitii Fundisho la Ekaristi na waliliishi?
Je mkate na divai vilichukuliwa na Mitume kama nini hasa? walichukulia Ekaristi kama nini?
16Je, kikombe cha Baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17(Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja) (1 Wakorinto 10:16)
Je ni lazima Kwa Mkristu kupokea Mwili na damu ya Yesu (Ekaristi)?
Je ni kwa nini madhehebu mengine hawakubali mafundisho haya ya Ekaristi Takatifu, Je ni mara ya kwanza watu kukataa?
Hata wakati Yesu akiyasema maneno haya Wafuasi Wengi Walimwacha kama Biblia inavyosema; 60Wengi wa wafuasi Wake waliposikia jambo hili wakasema, โMafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?โโ (Yohana 6:60). Haishangazi hata leo weni hawaamini mafundisho haya japokua ndio msingi wa Imani ya Kikristo.
Mitume walifundisha nini kuhusu Mwili na Damu ya Kristu (Ekaristi)?
Je, Divai iliyotumiwa na Yesu na mitume pamoja na Wakristu wa Kwanza ilikua na Kilevi (pombe)?
Kwa hiyo hata Mitume na Wakristu wa kwanza walitumia divai yenye kilevi ndio maana kuna waliolewa na walionywa kuhusu hilo.
Je Yesu Yupo Mzima katika Ekaristi Takatifu? Na kwa nini Tunaabudu Ekaristi?
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โโ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, โMtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?โโ 53Hivyo Yesu akawaambia, โAmin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.
Mstari wa 51 Yesu alisema wazi Mkate huo ni Mwili wake.
Thamani na Uwepo wa Yesu Mwenyewe unaonekana katika Mstari wa 53 na wa 56. Kumbuka hapa amesema “Mimi nitakaa ndani yake” Hakusema Mwili wangu utakaa ndani yake. Kwa maana nyingine ni kwamba Ekaristi ni Yesu Mzima na Sio Mwili tuu.
54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
Wale Wanaopinga fundisho la Ekaristi wanafikiri Yesu alivyosema Mimi ni Chakula Kutoka Mbinguni hakumaanisha Mwili bali Maneno na Imani Kwake lakini Tukisoma 51 Yesu alisema wazi kuwa Mwili wake ndio Mkate wenyewe.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โโ
Mitume wa Yesu walielewa hivi fundisho hili ndio Maana walishiriki Meza ya Bwana kila walipokutana na waliheshimu kama Mwili na Damu ya Kristo.
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. (Mdo 20:7)
Ili kujua kuwa Mitume waliheshimu Mwili na Damu ya Yesu Biblia inatuambia hivi;
23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema โHuu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, โKikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.โ 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume walisisitiza kuhusu Mwili na Damu ya Kristu kuwa ni Mtakatifu.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โโ
Yesu alisema Mimi ni Mkate wa Uzima ambao alimaanisha upo katika Mwili wake. Mwili tuu hauna uzima kama hauna Yesu ndani yake. Kwa sababu Mwili ni Mzima na Unaye Yesu ndani yake ndiyo maana unaweza kuleta uzima kwa Wengine.
Tunaelewa kwamba Yesu alijitoa Msalabani Mwili Wake na Damu yake na ndicho alichotupa ktk Ekaristi. Na Mwili wake huo Ulikua umembeba yeye aliye Mungu ndiyo maana tunaabudu Ekaristi alipo Yesu aliye Mungu.
Kwa kuwa Yesu ni Mungu Kama tunavyosoma katika Yoh 1:1-12
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watuโฆโฆ..14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Kwa hiyo Neno huyo huyo Ndiye aliyetukomboa kwa kuutoa mwili wake sadaka Msalabani na ndiye Aliyetupa Mwili Wake na Damu yake ktk Ekaristi na anaabudiwa kwa kuwa yupo katika mwili huo.
โKisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, โHuu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ (Luka 22: 19). Kwa namna hii alitupa mwili wake.
Alisema fanyeni kwa ukumbusho wangu na Sio wa mwili wangu.
Hivyo Ekaristi ni Yesu Mwenyewe aliye Mungu. Ndiyo sababu tunaabudu Ekaristi Takatifu.
Recent Comments