Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kupika Mseto Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Nazi

Vipimo vya mseto

Tanbihi: Kiasi ya vipimo inategemea wingi wa watu, unaweza kupunguza au kuongeza. Hiki ni kiasi cha watu 6 takriban.

Chooko – 3 Vikombe

Mchele – 2 Vikombe

Samli – 2 vijiko Vya supu

Chumvi – kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Safisha na kosha chooko utoe taka taka zote.
Osha mchele kisha roweka pamoja na chooko kwa muda wa saa au zaidi.
Pika chooko na mchele ukiongeza maji inapohitajika, tia chumvi, funika pika moto mdogo mdogo huku unakoroga kwa mwiko kila baada ya muda huku unaponda ponda.
Karibu na kuwiva na kupondeka tia samli endelea kupika hadi karibu na kukauka. Epua.

Samaki

Vipande vya samaki (nguru) – 6 – 7 (4LB)

Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa – 2 vijiko vya supu

Pilipili ya unga nyekundu – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa ukipenda – 1 kijiko cha chai

Bizari ya samaki – 1 kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Ndimu – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutaysha Na Kupika

Changanya thomu/tangawizi, pilipili, bizari, chumvi pamoja na ndimu iwe masala nzito.
Paka vipande vya nguru kwa masala hayo weka akolee dakika kumi hivi.
Kaanga vipande vya nguru katika mafuta madogo kwenye kikaango (fyring pan) uweke upande.

Mchuzi Wa Nazi

Vitunguu maji – katakata vidogodogo – 4

Nyanya zilizosagwa (crushed) – 3- 4

Nyanya kopo – 1 kijiko cha chai

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Bizari ya mchuzi – 1 kijiko cha chai

Bamia zilizokatwa ndogo ndogo – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Ndimu – 2 vijiko vya supu

Tui la nazi – 3 Vikombe au 800 ml

Namna Ya Kupika

Katika karai au sufuria, tia mafuta ukaange vitunguu hadi vianze kugeuka rangi.
Tia nyanya zilizosagwa, nyanya kopo, uendelee kukaanga, kisha tia bizari, chumvi.
Tia nazi na mwisho tia bamia uache ziwive kidogo tu.
Tia vipande vya samaki vilivyokwisha kaangwa.
Tayari kuliwa na mseto upendavyo.

Vidokezo:

Bizari nzuri kutumia ni ya ‘Simba Mbili’ inaleta ladha nzuri katika mchuzi.
Ni bora kupika mchuzi kwanza kabla ya mseto kwani mseto ukikaa kwa muda unazidi kukauka.

Mapishi ya Samaki wa kuokwa

Mahitaji

Mackerel 2
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula
Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta 1 kijiko cha chai

Matayarisho

Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.

Lifahamu tatizo la maumivu chini ya kitovu

Tatizo hili huwakumba watu wengi sana kwenye jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadae hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.

Maumivu Chini Ya Kitovu Hutokea Kama Ifuatavyo:

Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.

Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi.

Maumivu chini ya Kitovu Yanaashiria Matatizo Gani Kwa Wanawake?

Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.

Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.

Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kunauwezekano akawa na PID hasa hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.

Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini?

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume liitwalo Prostatitis yaani kuvimba kwa tezi dume. Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa unaelekea miaka 50 au zaidi.

Dalili nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na maumivu ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na damu katika maji ya uzazi (semen)
Kwa wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kwa jina la Hernia ambapo waswahili tunaita ngiri.

Mwanaume anaposikia maumivu haya ya chini ya kitovu ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzalishwa chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vywa mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.

Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfumo wa haja ndogo yaani (Urinary Track Infection/UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za mwanamke hapo juu.

Vipimo na tiba vyahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula

Unachotakiwa kujua kuhusu Shinikizo la chini la damu

Ugonjwa wa Shinikizo la chini la damu ambao hujulikana kama hypotension kwa Kiingereza ni hali ambayo shinikizo la damu ya mtu linakuwa chini sana.

Dalili za ugonjwa wa shinikizo la chini la damu

  1. kizunguzungu,
  2. uchovu,
  3. udhaifu,
  4. kupumua kwa shida,
  5. kupungua kwa nuru ya macho nk

Shinikizo la kawaida la damu vipimo vinatakiwa visome 120/80 mm Hg.

Ikiwa vipimo vitasoma una 90/60 mm Hg au chini ya hapa, una shinikizo la chini la damu. Shinikizo la damu linapokuwa chini zaidi linasababisha msukumo ulio chini wa damu kwenye ogani kama ubongo, figo, na kwenye moyo.

Mambo yanayosababisha shinikizo la chini la damu

  1. kupungua kwa maji mwilini,
  2. kulala sana,
  3. lishe duni,
  4. kushuka kwa wingi wa damu,
  5. matatizo ya moyo,
  6. ujauzito,
  7. Baadhi ya dawa za hospitalini
  8. homoni kutokuwa sawa nk.

Unaposhughulika na shinikizo la chini la damu inashauriwa kuongeza matumizi ya chumvi na maji. Hata hivyo wasiliana na daktari wako wa karibu kabla kuamua lolote mwenyewe binafsi.

Ugonjwa huu unaweza kupona japo Kupona kabisa kunategemea na aina hasa ya chanzo chake.

Faida za Korosho Kiafya

Korosho zina faida hizi zifuatazo;

1. Zinakinga Maradhi ya Saratani Haswa kwenye matumbo mapana.

2. Korosho zinasaidia Afya ya moyo kufanya kazi vizuri.

3. Korosho zinasaidia Kuzifanya nywele na ngozi ya mwili kuwa na Afya nzuri.

4. Korosho zinasaidia mifupa yako kuwa imara na afya nzuri.

5. Korosho ni nzuri kula kwa ajili ya mishipa ya mwilini mwako.

6. Korosho zinakukinga usipatwe na mawe kwenye nyongo yako.

7. Korosho ukila zinapunguza uzito mwilini.

Angalia huyu mwalimu alichomfamya huyu mwanafunzi

*Hadith ya Shemdoe na Mwalimu wa English:*

*Teacher:* `Who is a pharmacist?`

*Shemdoe:* 👆🏿 _(raised up his hand.)_

*Teacher:* `So it’s only Shemdoe that can tell who a pharmacist is in this class? Thus, no body else to answer the question except Shemdoe?`

_(There was no reply from the students)_

*Teacher:* `Ok. now Shemdoe, chukua hii fimbo, charaza vilaza hawa wote kila mmoja viboko 3.`

*Shemdoe* _(akiwa amevimba kichwa, akawatwanga viboko vitatu vitatu vya kushiba darasa nzima)_

*Teacher:* `Now, my dear Shemdoe tell this dumb students, who a pharmacist is…?`

*Shemdoe:* `Yes, sir. a Pharmacist is a farmer who assists people.`

_*Shemdoe sasa hivi amelazwa MOI kwa wataalam wa mifupa*_😀😀😀

Hii ndio inaitwa mbinu ya biashara

Anakuja Mchina anasema anahitaji Paka🐈,
ananunua mmoja kwa bei ya 20,000/=, basi
wanakijiji wanahaha kusaka Paka🐈,
wanawaleta mchina ananunua wote anasepa
nao. Anarudi tena anasema vipi, naona
wameadimika, sasa ntanunua kwa bei ya
35,000 Paka🐈 mmoja, wanakijiji wanaenda
deep zaidi msituni, kamata Paka🐈, leta kwa
mchina, mchina anasepa nao.

Afu wiki
mnayofuatia Mchina anasema bado anataka
Paka🐈, saivi atanunua kwa Laki. Wanakijiji
macho yamewatoka, hawana tena paka🐈.
Mchina anasema basi ntaftieni kwa Laki na
Nusu. Keshoake inasikika kuwa kuna Mchagga
anauza Paka kijiji cha pili, anauza kwa
100,000/=, wanakijiji wanawahi fasta
wanaenda nunua Paka🐈🐈🐈🐈 wote wa kijiji cha
pili. Wanarudi kijijini hawana pesa ila wana
Mapaka 🐈🐈🐈 wakijua watamuuzia mchina fasta kwa
laki na nusu, Mchina hatokei Ng’oooo!!!!
Infact, yule mchina alikuwa anawakusanya tu
na kuwahifadhi kule kijiji cha pili akijua ataja
wauza kwa 100,000/= kwa hawa hawa wa kijiji
hiki.
This is what called business strategy.😃

Kutubu na Kusamehewa dhambi

Usiogope wala usisite kutubu na kuomba msamaha kwa Mungu. Uwe na Amani na Matumaini katika Huruma ya Mungu itokayo katika Upendo wake wa Mfano wa baba awapendavyo wanawe. Mungu anasubiri kukupokea kwenye mikono yake Ili akutunze kama mtoto wake kama utatubu na kumrudia yeye. Amua kumwendea leo! Anakungoja ni wewe tuu…

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About