🌻Bikira Maria ni Mama wa uhai, mlei, muuguzi wa kwanza/ muhudumu wa kwanza alienda kwa haraka kuanzisha kliniki ndogo nyumbani mwa Zakaria amhudumie Elizabeti Mama wa Yohane Mbatizaji aliyekuwa mjamzito
-Mama wa watoto wa kesho
-Baba wa watoto wa kesho
-Padre wa kesho
-Mtawa wa kesho
-Raisi wa kesho n.k
🌻Bikira Maria alikombolewa kwaajili ya mastahili ya mwanae tena kwa namna ya pekee sana, aliangaliwa na…..
-Baba kama Binti yake Mpenzi
-Mwana, mama mheshimiwa
-Roho Mtakatifu, hekalu lake
2. Pili ni kuwa Yesu aliyemzaa Ni Mungu.
Malaika akamwambia ‘ usiogope Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu, tazama utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume na jina lake utamwita Yesu kwahiyo ni dhahiri kwamba huyu ni mama halisi wa Yesu ambae sisi tunamuimba kila leo.
kuzaliwa kwake Yesu Kristu kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu huu ni ushahidi tosha kuwa Bikira Maria ni Mama halisi wa Yesu kwani ndiye aliye pewa hadhi zaidi ya wanawake wote kuzaa kitakatifu Mwana wa Mungu.
yaani habari za mwanawe, aliye zaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili ikikumbuka wakati tunasali nasadiki kama sehemu ya kuikiri imani yetu kuna maneno huwa tunatamka kwamba akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu hivyo ni connection nzurii sana kwetu kuendelea kumheshimu Mama yetu Maria kwa kutuunganisha na Mungu kwa ubinadamu wetu!
kwahiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara, tazama , Bikira atachukua mimba , atazaa mtoto mwanamume naye atamwita jina lake Imanueli(yaani Mungu pamoja nasi tazama maneno haya yalitabiliwa na Nabii huyu juu ya mama huyu Mtakatifu atakavyo tuletea ukombozi kwann tusimheshimu na kumtetea mpaka tunapotoshwa?
hawa wote walikuwa wakidumu kwa Moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake na mariamu mama yake Yesu na ndugu zake wanawake wengine walihesabiwa pamoja lakini mama Maria anasemwa kwa upeke yake ktokana na uzito wake kupita wanawake wengine kwani ndiye mama wa Yesu Kristu ni heshima kubwa!!!
hapo mwanzo kulikuwako Neno naye Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu Huyo Mwanzo alikuwako kwa Mungu kwa maneno hayo na ukiendelea kusoma ukitafakari utaona anaezungumziwa na Yesu Kristu ambaye ndie nuru halisi ya ulimwengu ni ndie uzima wetu kwa Mungu na huyu Yesu basi alizaliwa na Bikira Maria hivyo alichozaa Maria ni Mungu kweli.
ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya Mwili, ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu mwenye kuhimidiwa milele. Amina hayo ni maneno yanayo tambulisha koo ya kibinadamu kwamba ndiko pamoja ubinadamu wetu amezaliwa Mungu soma injili ya mtakatifu Mathayo sura ya kwanza aya ya kwanza na kuendelea habari za ukoo wa Yesu naamini hapa Tmcs tunapasikia sana!!!
nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu nakuendelea……….. maneno hayo yanaonyesha kuwa Kristo ndie mambo yote katika kuupata uzima wa milele na huyu anae onekana ni mwisho wa yote amaezaliwa na Mwanamke Maria.
Tomaso akajibu, akamwambia Bwana wangu na Mungu wangu kutokana na matendo na kazi ya Yesu Kristu iliwafanya mitume waone kuwa ufalme wake sio wa dunia hii tu bali ni wa milele na kazi yake ni Takatifu na sio hapo tu kumbuka pia wale wanafunzi walio kuwa wanasema yatufaa sasa tujenge vibanda vitatu kimoja cha Musa na kingine cha Eliya mara sauti ikasikika ikisema huyu ni mwanangu mpendwa wangu msikieni yeye na mara akageuka sura maneno hayo ilikuwa ni uthibitisho juu ya umungu wa Yesu Kristu ambaye huyu alizaliwa na Bikira Maria.
Malaika akajibu akamwambia “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako , na nguvu zake aliyejuu zitakufunika kama kivuli, kwasababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu mwana wa Mungu” haya maneno ni dhahiri yanatufundisha kwamba Bikira Maria alimzaa Mungu katika ubinadamu wake.
huyu ni mwana wa Mungu, ni mwana wa mwanamke, huyo mwana wa Mungu, pia ni mwana wa Maria tuseme nn sasa tusiyumbishwe yumbishwe na maneno yasiyo na tija juu ya mama Maria kwani kupitia yeye tunakuwa salama katika Roho na Mwili
hakuna jambo kubwa zaidi ya hili kuwa Bikira Maria alipata kuwa Mama wa Mungu ambalo kwalo zinatoka zawadi(heri) kubwa na Nyingi ambazo amepewa inakuaje leo tusione umhimu wa heshima kwa mama huyu?
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Baraka kwako na familia yako.
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao