Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya Pasta za cream na uyoga

Mahitaji

Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai)
Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai)
Cream (1 kikombe cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Kitunguu (onion 1)
Chumvi
Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho

Chemsha maji ya kutosha kisha tia chumvi na mafuta kidogo katika hayo maji na baadae tia pasta na uzichemshe mpaka ziive kisha uzichuje maji na uziweka pembeni. Baada ya hapo weka mafuta kidogo katika sufuria kisha tia uyoga uliokatwa na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia majani ya basil, chumvi na cream kisha acha ichemke kisha weka vitunguu na upike kwa muda wa dakika 4 kisha malizia kwa kutia pasta. Zichanganye vizuri na mchanganyiko wote kisha zipike kwa muda wa dakika 5. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Unaweza kupika nyama ya kuku (chiken breast) iliyokatwa vipande vidogo vidogo kama saizi na shape ya pasta. Vizuri kuikaanga pembeni mpaka iwe brown na kuiva alafu kuimix kwenye chakula baada ya uyoga na vitunguu kuiva alafu unamix cream kumalizia mapishi.

Jinsi ya kupika Biskuti Za Kopa Za Kunyunyuziwa Sukari Za Rangi

MAHITAJI

Unga vikombe 2 ยผ

Siagi 250g

Sukari kukaribia kikombe ยฝ (au takriban vijiko 10 vya kulia)

Baking powder ยฝ kijiko cha chai

Ute wa yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Sukari Ya Kunyunyizia na rangi mbali mbali.

MATAYARISHO

Kagawa sukari katika vibakuli utie rangi mbali mbali uweke kando.
Changanya siagi na sukari katika mashine ya kusagia keki upige mpaka ilainike iwe nyororo.
Tia ute wa yai vanilla uhanganye vizuri.
Tia unga na baking powder kidogo kidogo uchanganye upate donge.
Sukuma donge ukate kwa kibati cha shepu ya kopa.
Pakaza siagi katika treya ya kupikia kwenye oveni upange biskuti
Nyunyizia sukari za rangi rangi kisha pika katika oven moto mdogo wa baina 180 โ€“ 190 deg F kwa takriban robo saa.
Epua zikiwa tayari.

Mapishi ya Tende Ya Kusonga Ya Lozi Na Cornflakes

VIAMBAUPISHI

Tende zilizotolewa kokwa – 1 Kilo

Cornflakes – 1 ยฝ kikombe

Lozi Zilokatwa katwa – 1 kikombe

Siagi – ยผ kilo

MANDALIZI

Mimina tende na siagi kwenye sufuria bandika motoni moto mdogo mdogo mpaka zilainike. Kwa muda wa dakika 10.
Isonge kidogo kwa mwiko au kuikoroga ichanganyike vizuri.
Changanya Cornflakes na lozi kwenye tende mpaka zichanganyika vizuri.
Pakaza treya au sinia mafuta au siagi kidogo.
Mimina mchanganyiko wa tende, zitandaze vizuri na ukate vipande saizi unayopenda. Zikiwa tayari kuliwa kwa kahawa.

Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Viambaupishi

  1. Mchele (Basmati) – 3 vikombe
  2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) – 1 kikombe
  3. Kuku Kidari – 1 LB (ratili)
  4. Mayai – 2 mayai
  5. Vitunguu (vikubwa) – 2 au 3 vidogo
  6. Pili pili manga – 1 kijiko cha chai
  7. Paprika – 1 kijiko cha chai
  8. Chumvi – Kiasi
  9. Mafuta – 1/3 kikombe cha chai
  10. Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
  11. Tangawizi – 1 kijiko cha chai
  12. Kidonge cha supu – 1
  13. Soy sauce – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.

Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)

Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.

Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali

Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.

Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi

Wacha uchemke asilimia 70%

Chuja maji na weka kando

Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu

Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)

Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga

Kisha tia wali changanye vizuri

Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive

Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.

Jinsi ya kupika Keki Ya Maboga

Viamba upishi

Unga wa ngano vikombe vikubwa 3
Boga lililopondwa kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Sukari kikombe kikubwa 1
Blue band kikombe ยฝ
Vanilla kijiko kidogo 1
Mayai 2
Maji kiasi/ maziwa
(kama nilazima)

Hatua

โ€ข Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike.
โ€ข Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa.
โ€ข Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa.
โ€ข Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole.
โ€ข Ongeza sukari na changanya.
โ€ข Ongeza mayai na koroga na mwiko.
โ€ข Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike.
โ€ข (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo).
โ€ข Ongeza vanilla na koroga.
โ€ข Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano.
โ€ข Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea.
โ€ข Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive.
โ€ข Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.

Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori – 1 kilo moja

Vitunguu maji – 3

Karoti – 2

Siagi – 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) – 1 kimoja

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

ร“sha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala – kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.

Jinsi ya kupika Mitai

VIAMBAUPISHI

Unga wa ngano 1ย 1/2 Kikombe

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Baking soda ยผ Kijiko cha chai

Chumvi ยฝ kijiko cha chai

Sukari 1 kijiko cha supu

Hamira 1/2 Kijiko cha supu

Yai 1

Maziwa ยฝ Kikombe

Mafuta ya kukaangia

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari 1 Kikombe

Maji ยฝ Kikombe

Iliki au Mdalasini ยผ kijiko cha chai (ya unga)

MAANDALIZI NA JINSI YA KUPIKA

1. Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari na hamira.

2. Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.

3. Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga ; na ukande kama unga wa maandazi.

4. Ikisha fura, sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai .

5. Pasha moto mafuta na uchome hadi iwe rangi ya dhahabu, upande zote mbili.

6. Ipikie shira lakini isiwe nzito .

7. Tia mitai na upepete hadi sukari ienee kote na zitakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIPIMO:

Unga wa Visheti

Unga 4 Vikombe vya chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Hiliki ยฝ Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.

2. Changanya vizuri isiwe na madonge.

3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.

4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.

5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .

6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili

7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.

8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Shira:

Sukari 2 Vikombe vya chai

Maji 1 Kikombe cha chai

Vanilla ยฝ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma (Grilled)

Mahitaji

Mchele wa Basmati /Pishori – 4 vikombe

Kuku

Vitunguu – 3

Nyanya/Tungule – 2

Tangawizi mbichi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi nzima – 3

Ndimu – 2

Garama Masala/bizari mchanganyiko – 1 kijiko cha supu

Haldi/tumeric/bizari manjano – 1 kijiko cha chai

Pilipilu ya unga nyekundu – 1 kijiko cha chai

Mtindi /yoghurt – 3 vijiko vya supu

Mafuta ยฝ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele, roweka.
Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli.
Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu.
Punguza mchanganyiko kidogo weka kando.
Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi.
Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive.
Epua, weka kando.
Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando.
Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali.
Tia kuku uchaganye vizuri.
Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja.
Punguza masala nusu yake weka kando.
Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali.
Funika upike katika oveni hadi uive.
Changanya unapopakua katika sahani.

Mapishi mazuri ya Uji wa ulezi

Mahitaji

Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula)
Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe)
Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai)
Siagi (butter kijiko 1 cha chakula)
Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)

Matayarisho

Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.

Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Mahitaji

Muhogo – 3

Tui La Nazi – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko moja

Kitunguu maji – 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine

Jinsi ya kupika Biriyani Ya Nyama Ng’ombe

Viambaupishi Vya Masala

Nyama vipande – 3 LB

Mtindi – ยฝ kopo

Kitunguu (thomu/galic) – 1ยฝ kijiko cha supu

Tangawizi – 1ยฝ kijiko cha supu

Nyanya – 2

Pilipili mbichi – kiasi

Nyanya kopo – 4 vijiko vya supu

Vidonge supu – 2

Pilipili nyekundu paprika – kiasi

Bizari zote saga – 2 vijiko vya supu

Viazi – 4

Mafuta – 2 mug

Samli – ยฝ kikombe

Vitungu – 6

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika masala

Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni.
Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni.
Kanga viazi weka pembeni.
Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke.
Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.

Vipimo Vya Wali

Mchele – 5 mug

Maji – kiasi

Chumvi – kiasi

Mafuta uliyokaanga vitungu – kiasi

Rangi ya biriani – ยผ kijiko cha chai

*Zafarani – ยฝ kijiko cha chai

*roweka rangi na zafarani

Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali

Osha mchele roweka muda wa saa.
Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele.
Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja.
Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika.
Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.

Mapishi ya Wali Wa Zaafarani Na Kuku Wa Kupaka

Vipimo

Wali:

Mchele – 3 Vikombe

Kitunguu kiichokatwa – 1

Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande – 1

Mafuta – ยผ Kikombe

Zaafarani – 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka

Chumvi – 1 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown)
Tia pili pili boga.
Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi.
Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto.
Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.

Kuku

Kuku Mzima -1

Mayai ya kuchemsha – 6

Namna Ya Kupika Kuku

Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri.
Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu.
Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando

Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi

Kitunguu – 1

Nyanya iliyokatwa vipande – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Garam Masala – ยฝ kijiko cha supu

Bizari ya manjano – ยฝ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Pilipili masala ya unga – ยฝ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha supu

Nazi ya unga – 1 kikombe

Maji ya ukwaju – ยผ kikombe cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria
Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown).
Tia thomu na tangawizi.
Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa.
Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri.
Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri.
Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili.
Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui.
Mtie kwenye oveni kidogo.

Kupakuwa katika Sinia

Pakuwa wali kwanza katika sinia
Muweke kuku juu ya wali.
Pambia mayai

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Na Mtindi

MAHITAJI

Nyama iliyokatwa vipande – 1 Ratili(LB)

Mchele Basmati – 2 Magi

Chumvi ya wali – kiasi

Kitungu kilichokatwa katwa – 1 kikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yogurt) – ยฝ kikombe

Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari – 2 vijiko vya supu

Mafuta kidogo yakukaangia

Rangi ya manjano (ukipenda)

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Osha mchele na roweka nusu saa .

Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).

Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.

Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga hadi nyama isiwe nyekundu tena.

Tia maji gilasi 1ยฝ- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.

Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.

Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.

Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza rangi (ukipenda) kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.

Changanya wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa.

Kuandaa Chakula kwa Kupunguza Uzito: Vidokezo na Mapishi

Kuandaa Chakula kwa Kupunguza Uzito: Vidokezo na Mapishi ๐Ÿฝ๏ธ๐Ÿ’ช

Kupunguza uzito ni lengo ambalo wengi wetu tunalipigia debe, lakini mara nyingi tunapata changamoto kubwa ya jinsi ya kuandaa chakula kinachosaidia katika mchakato huu. Kwa bahati nzuri, kuna njia nyingi za kuandaa chakula ambazo zitakusaidia kufikia lengo lako la kupunguza uzito. Katika makala hii, nitaenda kukushauri jinsi ya kuandaa chakula kinachofaa kwa ajili ya kupunguza uzito wako. Kama AckySHINE, mtaalam katika masuala haya, ninafahamu jinsi ya kukusaidia kupata matokeo bora.

Hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kuandaa chakula kwa kupunguza uzito na mapishi ambayo yatakuwezesha kufurahia chakula chenye afya na bado ufikie lengo lako la kupunguza uzito.

  1. Chagua vyakula vyenye kiwango cha chini cha mafuta: Ni muhimu kuzingatia kiwango cha mafuta katika chakula chako. Badala ya kukaanga, jaribu kupika kwa kutumia njia kama kuchemsha, kuchoma au kupika kwa mvuke. ๐Ÿฅฆ๐Ÿ—

  2. Punguza matumizi ya sukari: Sukari ni tishio kubwa katika mchakato wa kupunguza uzito. Badala ya kutumia sukari ya kawaida, jaribu kutumia mbadala kama vile asali au sukari mbadala yenye kiwango cha chini cha kalori. ๐Ÿฏ๐Ÿฐ

  3. Ongeza mboga kwenye milo yako: Mboga ni tajiri katika virutubisho na hupunguza kalori katika mlo wako. Hakikisha unaongeza mboga kwenye sahani yako ili kuongeza ladha na thamani ya lishe ya chakula chako. ๐Ÿฅ•๐Ÿฅฌ

  4. Pika kwa kutumia viungo vya asili: Kuandaa chakula chako mwenyewe kunakupa udhibiti wa viungo unavyotumia. Tumia viungo vya asili kama vile tangawizi, vitunguu, pilipili, na viungo vingine vyenye afya ili kuongeza ladha bila ya kuongeza kalori nyingi. ๐ŸŒถ๏ธ๐Ÿง…

  5. Punguza matumizi ya chumvi: Chumvi inaweza kusababisha umeng’enyaji usiofaa na kuongeza shinikizo la damu. Jaribu kutumia chumvi kidogo au badala yake tumia viungo vingine kama vile pilipili, tangawizi na jani la bay kwa ladha zaidi. ๐Ÿง‚๐Ÿฅ˜

  6. Pika sahani ndogo: Kula kwa kiasi kidogo kunaweza kukusaidia kupunguza ulaji wako wa kalori. Jaribu kutumia sahani ndogo wakati wa kuandaa chakula chako ili udhibiti kiasi unachokula. ๐Ÿฝ๏ธ๐Ÿฅ—

  7. Subiri kabla ya kula tena: Mara nyingi tunapokula, tunahisi kushiba haraka. Kabla ya kukimbilia kula tena, subiri angalau dakika 20 ili kutoa nafasi kwa mwili wako kujua ikiwa umekula vya kutosha. ๐Ÿ•’๐Ÿ™‡โ€โ™€๏ธ

  8. Jaribu kupika kwa kutumia mafuta ya asili: Mafuta ya asili kama vile mafuta ya zeituni, mafuta ya alizeti, na mafuta ya avocado yana mafuta yenye afya ambayo yanaweza kukusaidia kupunguza uzito wako. Epuka mafuta ya trans na mafuta ya wanyama. ๐Ÿฅ‘๐Ÿณ

  9. Fanya chakula kiwe na rangi: Chakula chenye rangi nyingi huwa na virutubisho vingi na huongeza hamu ya kula. Jaribu kuchanganya matunda na mboga za rangi tofauti ili kuongeza ladha na mchanganyiko wa lishe katika milo yako. ๐ŸŒˆ๐Ÿ“

  10. Kula kwa polepole: Kula polepole kunaweza kukusaidia kuhisi kushiba haraka na kula kwa kiasi kidogo. Chakula huchukua muda kufika kwenye tumbo, kwa hiyo jaribu kula kwa taratibu ili kujisikia kushiba haraka. ๐Ÿข๐Ÿฝ๏ธ

  11. Epuka vinywaji vyenye sukari: Vinywaji vyenye sukari kama vile soda na juice ya kutoka kwenye pakiti huongeza kiasi kikubwa cha kalori zisizo na faida kwenye lishe yako. Chagua maji, juisi ya limau au chai zisizoongeza sukari. ๐Ÿฅค๐Ÿน

  12. Tumia sahani nyembamba: Kutumia sahani nyembamba kunaweza kukufanya uhisi kama una sahani kamili hata kama umechukua kiasi kidogo cha chakula. Hii inaweza kukusaidia kudhibiti sehemu unazochukua. ๐Ÿฝ๏ธ๐Ÿ›

  13. Panga milo yako mapema: Kupanga milo yako mapema kunaweza kukusaidia kuepuka kula chakula kisicho na afya au kupita kiasi. Jipange vizuri na andika orodha ya unachotaka kula kwa kila siku ili kudumisha mpangilio mzuri wa lishe yako. ๐Ÿ“†๐Ÿ“

  14. Jaribu mapishi mapya: Kupika chakula kipya kunaweza kuwa na furaha na inaweza kukusaidia kupunguza monotoni ya chakula chako. Tafuta mapishi mapya na jaribu vitu vipya ili kuongeza mshangao na ladha mpya kwenye milo yako. ๐Ÿ‘ฉโ€๐Ÿณ๐Ÿฝ๏ธ

  15. Usiwe mkali kwako mwenyewe: Kupunguza uzito ni mchakato na hakuna njia ya mkato. Usikate tamaa ikiwa unaanguka kutoka kwenye mstari wako. Badala yake, jikumbushe lengo lako na endelea kujitahidi. Kila hatua ndogo inakaribishwa na inakusaidia kufikia lengo lako la mwisho. ๐Ÿ’ช๐Ÿ’ซ

Kwa hiyo, hapa ndio vidokezo na mapishi ya jinsi ya kuandaa chakula kwa kupunguza uzito wako. Kumbuka, chakula ni muhimu katika mchakato huu na inaweza kufanya tofauti kubwa katika matokeo yako. Jaribu vidokezo hivi na uone jinsi yanavyofanya kazi kwako. Je, una vidokezo vyovyote au mapishi unayopenda kutumia wakati wa kupunguza uzito? Tuambie katika sehemu ya maoni hapa chini. ๐Ÿ—ฃ๏ธ๐Ÿ‘‡

Jinsi ya Kupika skonzi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
Baking powder 1/2 kijiko cha chai
Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)

Matayarisho

Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200ยฐC ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones au maskonzi yatakuwa tayari

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) 1/4
Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1
Yai (egg) 1
Chumvi (salt)
Mafuta (cooking oil)

Matayarisho

Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Chicken Curry

Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).

Mahitaji

Kuku mzima
Nyanya kubwa 3
Karoti mbili
Pilipili hoho
Kotmiri
Tangawizi
Kitunguu maji
Kitunguu saumu kidogo
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Chumvi (pilipili ukipenda)

Matayarisho

1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja.
2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu).
3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni.
4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni.
5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni.
6. Andaa kikaango na jiko.

Mapishi

1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui).
2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi.
3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana.
4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.

Mapishi ya viazi mbatata Vya Nazi Kwa Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Mbatata / viazi – 2 kilo

Nyama ngโ€™ombe – ยฝ kilo

Kitunguu maji – 2

Tungule/nyanya – 2

Nazi /tui zito – 2 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

pilipili shamba/mbichi ilosagwa – kiasi

Mdalasini – 1 kipande

Bizari ya manjano – ยฝ kijiko cha chai

Bizari ya pilau/jiyrah/cummin – ยฝ kijiko cha chai

Ndimu/limau – 1

Namna Ya Kupika:

Chemsha nyama kwa kutia; chumvi, tangawizi, kitunguu thomu, mdalasini, na bizar zote.

Ipike nyama mpaka iwive na ibakishe supu yake kidogo.

Changanya tui la nazi pamoja na supu ilobakia.

Panga mbatata katika sufuria.

Tia nyama

Mwagia vitunguu na nyanya ulizotayarisha, tia pilipili.

Mwagia supu ulochanganya na tui

Funika upike mpaka viwive .

Tia ndimu

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About