Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya Pilau Ya Nyama ya Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu

Mahitaji

Mchele wa Par boiled au basmati – 5 vikombe

Nyama kondoo/mbuzi ya kusaga – 1 kikombe

Kitunguu – 2

Kitunguu saumu (thomu/galic) – 7 chembe

Adesi za brauni (brown lentils) – 1 kikombe

Zabibu – 1 kikombe

Baharaat/bizari mchanganyiko – 1 kijiko cha supu

Chumvi – kiasi

Pilipilii manga – ½ kijiko

Jiyra/bizari pilau/cummin – 1 kijiko cha chai

Supu ya nyama ng’ombe – Kiasi cha kufunikia mchele

Mafuta – ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha

Osha, roweka masaa 2 au zaidi.

Katakata (chopped)

Menya, saga, chuna

Osha, roweka, kisha chemsha ziive nusu kiini.

Osha, chuja maji

Namna Ya Kupika:

Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka vyekundu.
Tia kitunguu thomu, kaanga, tia baharati/bizari zote kaanga.
Tia nyama uchanganye vizuri, ukaange iwive..
Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu, koroga kidogo, funika uivie mchele.
Karibu na kuiva, tia adesi, zabibu, changanya, funika uendelee kuiva kama unavyopika pilau.
Epua pakua katika chombo, ongezea zabibu kupambia ukipenda

Mapishi Bora kwa Familia Yote Kupenda

Mapishi Bora kwa Familia Yote Kupenda 🍽️

Karibu tena kwenye makala ya AckySHINE ambapo leo tutajadili kuhusu mapishi bora ambayo yatapendwa na familia nzima. Tunafahamu kuwa kila familia ina ladha tofauti tofauti linapokuja suala la chakula, lakini tuko hapa kukusaidia kuandaa chakula ambacho kila mtu atakipenda! 🥘

  1. Kuku wa Kuchoma 🍗
    Kwa wale wapenzi wa nyama ya kuku, hakuna kitu kitakachowafurahisha zaidi kuliko kuku wa kuchoma. Unaweza kuandaa kuku huu kwa kutumia viungo kama vile tangawizi, kitunguu saumu, pilipili manga, na limau kwa ladha ya ziada. Hii ni njia nzuri ya kuhakikisha kuwa wewe na familia yako mnafurahiya chakula pamoja! 🍋

  2. Wali wa Maharage 🍚
    Wali wa maharage ni chakula ambacho hakina gharama nyingi na ni rahisi kuandaa. Unaweza kutumia mchele wa kawaida na maharage yoyote unayopenda kuandaa wali huu mzuri. Unaweza kuongeza viungo kama vile iliki, bizari na kitunguu saumu ili kuongeza ladha ya wali wako. Hakuna mtu atakayeweza kusimama kwa chakula hiki kitamu! 🍛

  3. Chapati za Nyama 🌯
    Chapati za nyama ni chakula kingine ambacho kitapendwa na familia yote. Unaweza kuandaa chapati hizi kwa kutumia nyama iliyosagwa, vitunguu, pilipili na viungo vingine vya kuchagua. Chapati hizi zinaweza kuliwa pekee yake au kwa kuiandaa na kachumbari na mchuzi wa nyanya. Utapata thawabu nyingi kutoka kwa familia yako! 🌮

  4. Samaki wa Kukaanga 🐟
    Ikiwa familia yako inapenda samaki, basi samaki wa kukaanga ni chaguo bora kwenu. Unaweza kutumia samaki kama vile dagaa, kambale au samaki wengine unaopenda. Tumia unga wa ngano kuwakaanga samaki wako na ongeza viungo kama vile pilipili na chumvi. Hakikisha samaki wako ni mzuri na laini ndani kabisa. Ni uhakika kuwa familia yako italamba vinywa vyao! 🐠

  5. Pilau ya Nyama 🍲
    Pilau ya nyama ni chakula kingine kizuri ambacho familia yako itapenda. Unaweza kuandaa pilau hii kwa kutumia nyama iliyokatwa vipande vidogo, mchele, vitunguu, pilipili na viungo vingine kama iliki, mdalasini na mchuzi wa nyanya. Pilau hii itajaza nyumba nzima na harufu nzuri na kumfurahisha kila mtu! 🍽️

  6. Kachumbari ya Matango na Nyanya 🥗
    Kachumbari ya matango na nyanya ni sahani ya upande ambayo inawezesha kuongeza ladha kwa chakula chako. Unaweza kukata matango na nyanya vipande vidogo, kisha kuongeza pilipili, kitunguu saumu, chumvi, na limau. Kachumbari hii italeta uwiano na ladha nzuri kwa chakula chako na kufurahishwa na familia yote! 🥒

  7. Mkate wa Tandoori 🥖
    Mkate wa tandoori ni sahani inayopendwa sana na watu wengi. Unaweza kutumia unga wa ngano, chachu, maziwa, sukari na chumvi kuandaa mkate huu. Unaweza kuuandaa na mboga za kupenda au nyama na kufurahia kama kitafunio au kwa mlo wa jioni. Hakikisha kuwa unatumia moto wa kutosha kupata mkate uliopendeza! 🥐

  8. Tambi za Nyama 🍝
    Tambi za nyama ni chakula kingine ambacho kina ladha nzuri na rahisi kuandaa. Unaweza kutumia tambi za aina yoyote, nyama iliyokatwa vipande vidogo, vitunguu, pilipili, na viungo vingine kama iliki, bizari na chumvi. Pika tambi zako kwa muda mfupi ili ziwe laini na uchanganyike na nyama kwa ladha kamili. Hakuna mtu atakayeweza kusimama kwa tambi hizi! 🍜

  9. Kuku wa Kienyeji 🐔
    Kuku wa kienyeji ni chaguo bora kwa wale wanaopenda ladha ya kiasili na afya. Unaweza kuandaa kuku huu kwa kutumia viungo rahisi kama vile vitunguu, pilipili, bizari, chumvi na tangawizi. Pika kuku wako kwa muda mrefu ili iwe laini na inayeyuka mdomoni. Ukiwa na kuku wa kienyeji, familia yako itafurahia chakula chako kwa uhakika! 🍗

  10. Keki ya Chokoleti 🍰
    Keki ya chokoleti ni chakula kizuri cha tamu ambacho kitapendwa na watoto na watu wazima sawa. Unaweza kutumia unga wa ngano, sukari, maziwa, chokoleti na viungo vingine kuandaa keki hii. Unaweza kuiongezea pia glasi ya chokoleti au cream ya chokoleti kwa ladha zaidi. Keki hii itakuwa hit kwenye chakula cha jioni cha familia yako! 🍫

Hapa kuna mapishi kadhaa ambayo naamini yatakuwa ya kupendeza kwa familia yako. Njoo na jaribu mapishi haya na angalia jinsi familia yako itakavyofurahia! Je, una mapishi yako bora yanayopendwa na familia yote? Tungependa kusikia kutoka kwako! 🥘

Opinion: Je, ungependa kujua mapishi mengine ambayo familia yote itapenda?

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Viamba upishi

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Maziwa kikombe 1
Sukari kikombe 1
Blue band kikombe ½
Mayai 10-12

Hatua

• Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike.
• Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa.
• Ongeza sukari na changanya.
• Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike.
• Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga.
• Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo.
• Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo.
• Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.

Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)

Mahitaji

Mchele wa basmati – 4 cups

Samaki nguru (king fish) – 7 vipande au zaidi

Kitunguu – 5

Nyanya/tungule – 3

Njegere – 1 kikombe

Snuwbar (njugu za pine) – 1 kikombe

Viazi – 2 kata kata mapande makubwa

Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu – 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu – 1 kijiko cha chai

Bizari ya biriani/garama masala – 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kupika:

Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda.
Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili.
Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange.
Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere, njugu za snuwbar na ndimu kavu.
Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia.
Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki.
Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani.
Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.

Jinsi ya Kupika Kalmati

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Hamira (yeast kijiko 1 cha chai)
Sukari (sugar 2 vikombe vya chai)
Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
Maji kikombe1 na 1/2
Mafuta

Matayarisho

Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Labania Za Maziwa

MAHITAJI

Maziwa ya unga – 2 vikombe

Sukari – 3 vikombe

Maji – 3 vikombe

Unga wa ngano – ½ kikombe

Mafuta – ½ kikombe

Iliki – kiasi

MAPISHI

Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania
Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri
Kisha mimina mafuta koroga
Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka
Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza.
Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.

Tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na la kuku wa kisasa

Kilishe mayai yote ni sawa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye yai la kuku wa kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya chuma na virutubishi vya aina nyingine, ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai la kuku wa kisasa.

Tatizo linaweza kutokea pale ambapo wafugaji wa kuku wa kisasa hawafuati taratibu za ufugaji na pengine hawawapi kuku vyakula muhimu wanavyohitaji au wanawapa dawa na vyakula visivyo bora kiafya, hivyo wakati mwingine kiini cha yai la kuku wa kisasa huonekana kupungua rangi ya njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.

Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni la kuku gani, kwa kutegemea ni yai lipi linapatikana kwa urahisi. Lakini nivizuri kula mayai ambayo yapo salama.

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng’ombe Na Nyanya

Vipimo

Mchele (Basmati) – 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe – 1 kg

Pilipili boga – 1 kubwa

Nyanya – 2 kubwa

Vitunguu maji – 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Mafuta ya kupikia – ½ kikombe

Mdalasini – ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga – ½ Kijiko cha chai

Hiliki – ½ Kijiko cha chai

Namna ya kutayarisha na Kupika

Roweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIPIMO:

Unga wa Visheti

Unga 4 Vikombe vya chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Hiliki ½ Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.

2. Changanya vizuri isiwe na madonge.

3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.

4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.

5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .

6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili

7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.

8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Shira:

Sukari 2 Vikombe vya chai

Maji 1 Kikombe cha chai

Vanilla ½ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

Mapishi ya Boga La Nazi

Vipimo

Boga la kiasi – nusu yake

Tui zito la nazi 1 ½ gilasi

Sukari ½ kikombe

Hiliki ½ kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Menya boga kisha katakata vipande vya kiasi.
Weka katika sufuri tia maji kiasi ya kuchemshia na kuwiva bila ya kubakia maji mengi.
Changanya tui na sukari na hiliki kisha mimina juu ya boga wacha katika moto dakika chache tu bila ya kufunika.
Epua mimina katika chombo likiwa tayari.

Mapishi ya Ndizi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Ndizi – 15 takriiban

Nayma ya ng’ombe – 1 kilo

Kitunguu maji – 1

Nyanya – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilopondwa – 2

Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu.
Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria.
Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi.
Tia jira na chumvi.
Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa.
Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) 1/4
Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1
Yai (egg) 1
Chumvi (salt)
Mafuta (cooking oil)

Matayarisho

Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma Wa Tanduri

Mahitaji

Mchele – 4 vikombe

Kuku – 1

Vitunguu – 3

Nyanya/tungule – 4

Zabibu kavu – ½ kikombe

Tangawizi na kitunguu (thomu/galic) – 2 vijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) – 2 kijiko cha supu

Masala ya tanduri – 2 vijiko vya supu

Pilipili manga – 1 kijiko cha chai

Hiliki – ½ kijiko cha chai

Mdalasini – kijiti kimoja

Ndimu – 3 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Zaafarani (saffron) – 1 kijiko cha chai

Mafuta – ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Kuku:

Baada ya kumsafisha kuku, mkate vipande vikubwa vikubwa kiasi upendavyo, muoshe mchuje atoke maji.
Katika bakuli, tia tangawizi, kitunguu thomu ilosagawa, pilipili mbichi ilosagwa, chumvi, ndimu, mtindi, masala ya tanduri na uchanganye vizuri, kisha mtie kuku na uchanganye tena na acha arowanike kwa muda wa kiasi saa au zaidi.
Panga kuku katika sinia ya kuchoma ndani ya oveni. Kisha mchome (grill) hadi awive, mtoe acha kando. Mwagia juu yake masala yatakayobakia katika sinia baada ya kumchoma.

Namna Ya Kutayarisha Masala Ya Nyanya:

Weka mafuta katika karai, tia vitunguu ulivyokatakata, kaanga hadi vianze kugeuka rangi.
Tia nyanya ulizokatakata, tia pilipili manga, hiliki, mdalasini, chumvi, na zabibu. Kaanga kidogo tu yakiwa tayari.

Namna Ya Kutayarisha Wali:

Osha na roweka mchele wa basmati.
Roweka zaafarani kwa maji ya moto kiasi robo kikombe weka kando.
Chemsha maji, tia chumvi, kisha tia mchele uive nusu kiini.
Mwaga maji uchuje mchele kisha rudisha katika sufuria au sinia ya foil. Nyunyizia zaafarini, na rudisha katika moto upike hadi uive kamili.
Epua, kisha pakua wali katika sahani au chombo upendacho, mwagia juu yake masala ya nyanya. Kisha weka vipande vya kuku ulivyochoma, biriani ikiwa tayari

Jinsi ya kupika Roast ya biringanya na mayai

Mara nyingi biringanya hutumika kama kiungo cha nyongeza katika mchuzi. Hata hivyo, kiungo hiki kinaweza kupikwa chenyewe na kutoa mchuzi wenye ladha ya kipekee.

Baadhi ya wapishi wameweza kubuni aina hii ya upishi ambayo huweza kupikwa kwa dakika tano tu na kukupa chakula kitamu chenye ladha ya kuvutia.

Uzuri wa chakula hi ni kwamba kinaweza kuliwa wakati wowote na kwa chakula chochote kulingana na matakwa ya mlaji.

Kwa mujibu wa wataalamu wa maswala ya mapishi, biringanya ni miongoni mwa vyakula vyenye mapishi mengi kama ilivyo kwa mchele.
Hapa tutaenda kuona jinsi ya kupika roast ya biringanya na mayai.

Mahitaji:

Biringanya 2 kubwa
Nyanya 4 kubwa
Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
Mayai 2
Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya mezani
Chumvi kiasi
Pilipili 1 (kama unatumia)
Hoho 1
Karoti 1
Kitunguu swaumu kilichosagwa 1
Kotimili fungu 1

Maadalizi:

Chukua biringanya ioshe vizuri na kasha katakata vipande vidogo vidogo.
Osha na menya nyanya hapafu katakata. Fanya hivyo kw akaroti na hoho pia.
Weka mafuta kwenye sufuria na weka jikoni kwenye moto kiasi
Yakishachemka maji na kasha weka kitunguu maji na kasha swaumu huku ukikaanga taratibu.
Weka hoho na karoti huku ukiendelea kukaanga. Baada ya hapo weka nyanya na baadae chumvi. Funika hadi ziive kabisa na kasha weka majani ya kotimili.
Weka biringanya. Acha vichemke hadi viive. Koroga ili kuruhusu mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Kwa kuwa biringanya ina majimaji huhitaji kuweka maji ya ziada, weka pilipili.
Acha kwa muda wa dakika tatu hadi dakika tano. Pasua mayai na kisha miminia huku ukikoroga taratibu. Fanya hivyo hadi yaive kabisa na kuwa mchuzi mzito. Roast yako ya biringanya iko tayari kwa kuliwa
Unaweza kula aina hii ya mboga na mikate, maandazi na hata ugali

Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry

MAHITAJI

Unga kikombe 1 ½

Siagi ½ kikombe

Sukari ½ kikombe

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jam ya peach na raspberry

MAANDALIZI

Wash oven moto wa takriban 180 – 190 Deg F
Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla.
Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon).
Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam.
Panga katika treya uliyopakaza siagi.
Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry
Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light.
Epua vikiwa tayari

Mapishi ya Samaki wa kuokwa

Mahitaji

Mackerel 2
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula
Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta 1 kijiko cha chai

Matayarisho

Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.

Mchemsho wa samaki na viazi

Mahitaji

Samaki mbichi (1)
Viazi mbatata (3)
Nyanya (1)
Kitunguu maji
Limao
Kitunguu saumu
Tangawizi
Chumvi
Pilipili
Vegetable oil

Matayarisho

Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza saladi

Mahitaji

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo

Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho

Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Mapishi ya Bokoboko La Kuku

Mahitaji

Ngano nzima (shayiri) – 3 Vikombe

Kuku – ½ (3 LB takriban)

Thomu na tangawizi iliyosagwa – 1 kijko cha supu

Pilipili manga ya unga – ½ kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) – ½ kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Kidonge cha supu – 1

Samli ya moto – ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Roweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.
Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi viungo vyote. Mchemeshe awive na ibakie supu yake.
Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.
Chemisha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iwive na kukauka maji.
Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemechambua. Tia kidonge cha supu.
Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha songa mchanganyiko uchanganye hadi ivurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
Mimina katika sahani, mwagia samli imoto ilyobakia likiwa tayari.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About