Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Vipimo

Mchele vikombe 3

Karoti 1 ikune (grate)

Mchicha katakata kiasi

Adesi za brown

Kitunguu katakata (chopped)

Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2

Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia

Samli ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Vipimo Vya Samaki Wa Salmon

Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa

Tangawizi mbichi ilosagwa kijiko 1 cha kulia

Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia

Chumvi kiasi

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia

Ndimu 1 kamua

Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon

Changanya viungo vyote upake katika samaki.
Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake.
Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili.
Akiwa tayari epua.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori)
Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii.
Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia.
Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo.
Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu.
Tia chumvi ukoroge funika upike kama pilau.
Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Kama mzazi au mlezi, mara nyingine inaweza kuwa changamoto kubwa kuwapa watoto wako vitafunio vyenye afya, hasa pale ambapo wana tabia ya kuchagua vyakula visivyo na lishe. Lakini usijali! Kama AckySHINE, nina vidokezo 10 vya vitafunio vya afya ambavyo vitawafurahisha watoto wako na kuwapa lishe bora wanayohitaji. Soma ili kugundua!

  1. Matunda yenye rangi:
    Matunda kama vile tufaa, ndizi, au zabibu ni vitafunio bora kwa watoto. Wanaweza kula matunda haya kama yalivyo au kutengeneza saladi ya matunda yenye rangi mbalimbali kwa kuongeza limau kidogo ili kuongeza ladha. 🍎🍌🍇

  2. Karanga:
    Karanga kama vile njugu, karanga za pekee au karanga za kawaida zina protini nyingi na mafuta yenye afya. Unaweza kuzitoa kama vitafunio vya kati au kuzichanganya na matunda yaliyokatwa ndogo kwa kitafunio bora zaidi. 🥜

  3. Jibini:
    Jibini ni chanzo kizuri cha protini na madini ya kalsiamu. Unaweza kuwapa watoto wako vipande vidogo vya jibini pamoja na matunda au karanga kama vitafunio vyenye afya. 🧀

  4. Yoghurt:
    Yoghurt yenye asili ya maziwa ni chanzo bora cha protini na kalsiamu. Unaweza kuongeza asali au matunda yaliyokatwa ndani yake ili kuongeza ladha na kufanya iwe vitafunio bora zaidi. 🥛

  5. Mtindi:
    Mtindi ni chanzo kingine bora cha protini na kalsiamu. Unaweza kuongeza matunda yaliyokatwa kidogo au karanga zilizokatwa ndani ya mtindi ili kuongeza ladha na virutubisho vyenye afya. 🍓

  6. Sandvihi za mboga:
    Badala ya kutumia mkate wa kawaida, tumia mkate wa ngano nzima au mkate wa mboga kama karoti au matango. Weka mboga zingine kama nyanya au pilipili kwenye sandvihi na uwape watoto wako. Ni vitafunio vyenye lishe bora na rahisi kuandaa. 🥪

  7. Ndizi za kukaanga:
    Ndizi za kukaanga ni vitafunio vya afya na tamu ambavyo watoto wengi hupenda. Unaweza kuzikaanga kwa mafuta ya mizeituni au jibini kidogo ili kuongeza ladha. 🍌

  8. Kabeji:
    Kabeji ni mboga yenye lishe na inayoambatana vizuri na vitafunio vingine. Unaweza kutoa vipande vidogo vya kabeji pamoja na dipu ya jibini au mtindi. 🥬

  9. Barafu ya matunda:
    Kufanya barafu ya matunda ni njia nzuri ya kuwapa watoto wako kitafunio cha baridi na kitamu. Changanya matunda yaliyosagwa na maji, weka kwenye tray ya barafu na weka kwenye friji hadi itenge. Ni kitafunio bora cha majira ya joto! 🍧

  10. Chapati za nafaka:
    Badala ya kutumia unga wa ngano, tumia unga wa nafaka kama vile unga wa mtama au ulezi. Chapati za nafaka ni vitafunio bora vyenye lishe na rahisi kuandaa. Unaweza kuzitumia kama sahani ya kando au kuzikata vipande vidogo na kuwapa watoto wako. 🌾

Hivyo basi, kama AckySHINE ninaamini kwamba vitafunio vyenye afya ni muhimu sana kwa watoto wetu. Kwa kufuata vidokezo hivi, unaweza kuwapa watoto wako vitafunio vyenye lishe bora na kuwajenga kwenye tabia ya kula afya. Kumbuka, kuwapa watoto wako vitafunio vyenye afya ni njia bora ya kuwaweka na afya bora na kuwapa nguvu ya kukua na kufanikiwa!

Je, una maoni gani kuhusu vidokezo hivi? Je, umewahi kujaribu vitafunio hivi na kama ndivyo, ni vitafunio vipi ulivyopenda zaidi? Asante kwa kusoma na natarajia kusikia maoni yako! 🌟

Mapishi ya Ndizi na Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Ndizi mbichi – 10-12

Nyama ng’ombe – 1 kilo moja

Kitunguu maji – 2

Nyanya/tungule – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 7

Tangawizi mbichi – 1 kipande

Ndimu – 2 kamua

Chumvi – kiasi

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Tui la nazi – 3 vikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi.
Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive.
Menya ndizi ukatekate
Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga.
Tia tangawizi na thomu ilobakia.
Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake.
Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.

Jinsi ya kupika Keki Ya Maboga

Viamba upishi

Unga wa ngano vikombe vikubwa 3
Boga lililopondwa kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Sukari kikombe kikubwa 1
Blue band kikombe ½
Vanilla kijiko kidogo 1
Mayai 2
Maji kiasi/ maziwa
(kama nilazima)

Hatua

• Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike.
• Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa.
• Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa.
• Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole.
• Ongeza sukari na changanya.
• Ongeza mayai na koroga na mwiko.
• Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike.
• (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo).
• Ongeza vanilla na koroga.
• Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano.
• Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea.
• Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive.
• Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.

Mapishi ya Viazi vya nyama

Mahitaji

Viazi (potato) 1 kilo
Nyama ya ng’ombe 1/2 kilo
Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin
Vitunguu maji 2
Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Chumvi
Coriander
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha na katakata nyama ktk vipande vidogovidogo kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama, swaum/ tangawizi, chumvi na limao. Ichanganye vizuri kisha funika na uipike mpaka iive na maji yote yakauke yani yabaki mafuta tu. Baada ya hapo tia viazi vilivyokatwa vipande vya wastani vikaange kwa muda wa dakika 10 kisha tia pilipili na curry powder na nyanya. Funika na punguza moto.Pika mpaka nyanya iive vigeuze kisha tia vimaji kidogo vya kuivishia viazi. Viazi vikikaribia kuiva(hakikisha vinabaki na rojo kidogo) tia hoho na upike kwa muda wa dk 5 kisha malizia kwa kutia coriander. Changanya vizuri kisha ipua na viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.

JINSI YA KUANDAA VILEJA

MAHITAJI

Unga wa mchele – 500g

Samli – 250g

Sukari – 250g

Hiliki iliyosagwa – 1/2 kijiko cha chai

Arki (rose flavour) – 1/2 kijiko cha chai

Baking powder – 1 kijiko cha chai

Mayai – 4

Maji ya baridi – 1/2 kikombe cha chai

MAANDALIZI

Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
23
    23
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About