Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenziโ€ฆ

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mambo Mubimu kujua Kuhusu Tatizo la Shinikizo la damu (Tatizo la presha)

Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu. Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

  1. Uvutaji sigara
  2. Unene na uzito kupita kiasi
  3. Unywaji wa pombe
  4. Upungufu wa madini ya potassium
  5. Upungufu wa vitamin D
  6. Umri mkubwa
  7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
  8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

Uanishaji wa shinikizo la damu

Presha ya kawaida <120 <80
Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 โ‰ฅ180 โ‰ฅ110

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili zitakazokutokea unapokuwa na ugonjwa huu ni pamoja na;

  1. Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
  2. Kuchanganyikiwa,
  3. Kizunguzungu,
  4. Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
  5. Kutoweza kuona vizuri au
  6. Matukio ya kuzirai.
  7. Uchovu/kujisikia kuchokachoka
  8. Mapigo ya moyo kwenda haraka
  9. Kutokuweza kuona vizuri
  10. Damu kutoka puani
  11. Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.

Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.

Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo โ€˜reniniโ€™ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho โ€˜angiotensiniโ€™ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya โ€˜adrenoโ€™ kutoa homoni iitwayo โ€˜aldosteroniโ€™ ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.

Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.

Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo โ€˜vasopressiniโ€™ hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.

Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.

Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).

Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.

Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.

Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.

Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.

Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;

  1. Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
  2. Shambulio la moyo (heart attack)
  3. Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
  4. Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
  5. Kiharusi
  6. Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
  7. Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; โ€œSalt Your Way to Liveโ€, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika miili yao.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP.

Tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na la kuku wa kisasa

Kilishe mayai yote ni sawa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye yai la kuku wa kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya chuma na virutubishi vya aina nyingine, ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai la kuku wa kisasa.

Tatizo linaweza kutokea pale ambapo wafugaji wa kuku wa kisasa hawafuati taratibu za ufugaji na pengine hawawapi kuku vyakula muhimu wanavyohitaji au wanawapa dawa na vyakula visivyo bora kiafya, hivyo wakati mwingine kiini cha yai la kuku wa kisasa huonekana kupungua rangi ya njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.

Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni la kuku gani, kwa kutegemea ni yai lipi linapatikana kwa urahisi. Lakini nivizuri kula mayai ambayo yapo salama.

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

Zifutazo ndizo dalili za awali za mimba changa:

Kutokwa damu bila kutegemea.

“Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,โ€ iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

Kuchoka

Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

โ€œTambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingiziโ€

Chuchu kuwa nyeusi.

Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, โ€œWanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.โ€

Maumivu kwenye matiti

Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata โ€œrutubaโ€, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini

Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kuwa na hasira

“Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,โ€

Kuongezeka kwa joto mwilini.

Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna โ€œmtoto anakujaโ€.

Kichefuchefu.

Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

Mwili kuvimba

Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara.

Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali.

Kutokana na mwili kuwa na โ€œmzigoโ€ wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa

Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebish a na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo

Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Kanuni ya fedha ya matumizi na mipango ambayo itakusaidia ukiifuata

Jifunze kanuni za fedha
kama ilivyoainishwa hapo chini.
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kutumia
Hii kanuni inatumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani

Tuangalie hapa chini hizi kanuni๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Fungu la kumi 10%
Akiba 30%
Matumizi 40%
Dharura 10%
Msaada 5%
Sadaka 5%

๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†hii kanuni inafanya kazi katika kila hela unayopata kama faida

Mfano : mtu mwenye mshahara wa mil 1 unayoipata kila mwezi baada ya makato

Fungu la kumi 10% (Tithe) hii ni mali ya Mungu si yako!!

๐Ÿ‘‰itakuwa ni sh laki 1 unatakiwa uitoe sehemu unayoabudia kila mwezi na kama unabiashara zako faida yake ndani yake toa fungu la kumi
Pia hata kama ni hela unapewa kama zawadi itolee fungu la kumi

๐Ÿ‘‰faida ya hii

๐ŸŒธinalinda kazi au Biashara unayoifanya zidi ya adui
๐ŸŒธmagonjwa,ajali , ( vitu vitakavyokufanya utumie hela bila mpangilio),etc yanakuwa mbali nawe

Akiba 30%

๐Ÿ‘‰hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga,kusomesha,kulima, investment, etc
๐Ÿ‘‰unatenga laki 3 kwa mtu anaepokea mil 1

Matumizi 40%

๐Ÿ‘‰hii itatumika kwa matumizi ya kila siku ,chakula ,Maji, etc

๐Ÿ‘‰hapa unatenga laki 4 kwa ajili ya matumizi kwa mtu wa mshahara wa mil 1
๐Ÿ‘‰note : hapa ndio hela yako ya kustarehe inatoka
Angalia matumizi yasizidi hela uliyonayo
๐Ÿ‘‰wengi wao hapa watu ndio inamfanya awe na vyanzo vingi vya hela ili aweze kufanya starehe awezavyo
๐Ÿ‘‰pia hii ndio hela unayotoa kwa ajili ya mbegu (sadaka ya gharama) wanaoifahamu

Dharura 10%

๐Ÿ‘‰hii fedha unaitunza kwa ajili ya vitu usivyotarajia kama msiba, ndugu kuumwa au kukwama etc
๐Ÿ‘‰unatunza laki 1 kwa mtu wa mshahara wa mil 1

Msaada 5%

๐Ÿ‘‰hii inawahusu watoto yatima, wajane na wasiojiweza kama vilema
๐Ÿ‘‰unatoa elfu 50 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
๐Ÿ‘‰unaigawa kama unamagroup yote hayo

Sadaka 5%

๐Ÿ‘‰hii unatoa elfu 50 kwa mtu wa mshahara wa mil 1
๐Ÿ‘‰igawe mara NNE coz mwezi una jumapili 4 ambayo utapata ni elfu 12500 ivyo basi kila jumapili peleka sadaka elfu 12500

Note:
๐Ÿ‘‰Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku 2 au 3 ndio uitoe
sadaka
๐Ÿ‘‰nakama unahitaji kitu mfano Nguo peleka nguo kwa waitaji uone utakavyopata Nguo
Nyingi
๐Ÿ‘‰chukua mfano Bakhresa na Mengi wanavyojitolea mbona hawaishiwi, siri yao iko kwenye nidhamu hii ya pesa!!

Jaribu na wewe anza hata na kidogo kidogo kuwa na nidhamu na fedha uone nayo itakavyokuheshimu

Jinsi ya kutengeneza saladi

Mahitaji

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo

Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho

Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Jaribu kufikiria haya

1. Uelekeo ni muhimu kuliko kasi. Ni heri kwenda taratibu katika Uelekeo sahihi, kuliko kwenda kwa kasi katika Uelekeo usio sahihi.

2. Kulalamika mambo hayaendi wakati wewe mwenyewe hujui unakokwenda ni kuwa na matatizo ya akili.

3. Kasi yako inaamuliwa sana na umbali unaoweza kuona. Kama huoni chochote mbele ya maisha yako, basi huna chochote.

4. Sayansi inadai kuwa kazi ni nguvu inayotumika kusukuma kitu kwa umbali fulani kwenye Uelekeo maalumu. Kwa hiyo kama unatumia nguvu kusukuma mambo, lakini hayana Uelekeo maalumu jua kwamba hufanyi kazi yoyote, unapoteza nguvu tu.

5. Masaa yanaenda, siku zinapita, miaka inaongezeka, umri wako ndio unaenda hivyo, unafanya nini katika maisha?

Jifunze kupitia mfano huu Ili uishi kwa amani na watu

Siku moja nilichukua taxi aina ya UBER nikiwa naelekea uwanja wa Ndege Mwl. Nyerere Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu.

Pasipo kutegemea dereva wa gari la taka akaanza kufoka na kutoa matusi kwa kelele kubwa!

Katika hali ya kushangaza dereva wa taxi alitabasamu na kuwapungia mkono waliokuwa kwenye gari la taka na ndipo kwa mshangao nilimuuliza; “Inakuwaje ufanye hivyo wakati walitaka kutuua na hata kuharibu mali yako?”

Akajibu kwa upole akinitazama kwa tabasamu akasema. โ€œKatika maisha yetu, kuna watu wako kama gari la taka. Wamejaa misongo, hasira, maumivu, wamechoka kifikra, kiuchumi na kimaisha, na wamejaa masikitiko mengi. Watu hao takataka zao zinazopowazidi hutafuta mahali pa kuzitupa na haijalishi mazingira wanakozitupia.

FUNZO!
Jifunze kutogombana nao. Wapungie mkono, wape tabasamu, songa mbele. Haikupunguzii kitu. Wala usiruhusu takataka zao zikupate.”

Uliumbwa kuyafurahia maisha. Usiyafupishe kwa kuamka asubuhi na kinyongo, na hasira, na ghadhabu kwa sababu ya mtu fulani.

Watafiti wanasema 10% ya maisha ni vile ulivyoyatengeneza lakini 90% ya maisha ni vile unavyochukuliana nayo.

Jifunze kuchukuliana na maisha kuliko vile unavyoyatengeneza huku ukimtegemea Mungu.

ANGALIZO!
Ukiona umeanza kueleweka, kukubalika, kutambulika, kufahamika, kuheshimika na kupata nafasi zaidi kwa kile unachokifanya kumbuka kuendelea kuzingatia misingi, nguzo, miiko na nidhamu iliyokuwezesha kufika hapo ulipo ili uende mbali zaidi.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe vya chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Hiliki ยฝ Kijiko cha chai

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari – 2 Vikombe vya chai

Maji – 1 Kikombe cha chai

Vanilla ยฝ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

JINSI YA KUTENGENEZA

Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
Changanya vizuri isiwe na madonge.
Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai.
Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Duh! Tamaa mbaya, cheki kilichompata Huyu

HAHAHAHAHAAAAAA DUH TAMAA MBAYA

Muokota makopo katika uokotaji wake wa makopo akaona chupa ambayo ndani kuna ki2, alipoifungua likatoka jitu la ajabu. Huku akitetemeka lile jitu likamwambia kijana asante sana kwa kuniokoa omba vi2 viwili sasa hivi. Kijana kwa hofu akaomba pesa za kumiliki magari na majumba ya kifahari. Ghafla fuko la hela na pete ya bahati vikadondoka. Akaambiwa ombi la pili,akasema nibadilishe niwe kivutio ili nipendwe sana nakina dada Hapohapo akageuzwa akawa chipsi yai.!!๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimuโ€ฆ.kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

Kwa nini watu wanapenda pesa

Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia njia sahihi kuzipata na tunapozipata hatuna Akili ya kuweza kuwa nazo muda mrefu zisiondoke.
Kama tujuavyo katika maisha yetu haya Pesa ndio kila kitu,tunahitaji Pesa ili tuweze kufanya mambo mengi mazuri na makubwa.Kitu kinachotukwamisha hatujui tufanye nini ili tuweze kuzipata hizi Pesa na tunapozipata tunakosea tena cha kuzifanyia ili zisipotee tena au zisiishe.

Kitu kikubwa kinachotugharimu ni kwamba hatuna elimu ya Pesa.Wengi wetu tumesoma tena sana lakini huko shuleni na vyuoni hatufundishwi jinsi gani ya kuzitafuta Pesa,uzifanyie nini,na nini kifanyike ili zisiishe.
Elimu hii kuhusu Pesa haitolewi shuleni zaidi ni ya kujifunza kutoka mtaani hasa kwa watu wanaomiliki Pesa nyingi au ambao wamefanikiwa ndio watakupa utaalam halisi na elimu kuhusu Pesa.

Kuna watu wengi sana tumeshawahi kuwasikia wamepata Pesa nyingi sana lakini sasaivi hawana kitu.Wengi tumewasikia kwenye bahati nasibu wamejishindia Pesa nyingi,wengine kwenye mashindano mbalimbali wamejishindia Pesa kibao lakini cha kujiuliza hao watu mpaka sasa wapo wapi?hela zao ziko wapi?wamezifanyia kitu gani?bado wanazo??Jibu rahisi ni hapana na hii ni kutokana na kwamba hawakupata elimu ya Pesa ndio maana.

Inatakiwa kabla ya kuwapa watu Pesa lazima wapate elimu kuhusiana na Pesa hapo ndipo watakapokuwa na ujuzi Wa kuweza kuzifanyia kazi na kuziongeza.
Matajiri wote unaowafahamu wana elimu juu ya Pesa ndio maana Pesa zinazidi kuwafuata wao na sisi ambao hatuna elimu ya Pesa tunazidi kuhangaika kuzitafuta.

Lakini sifa nyingine ya Pesa kadiri unavyotoa ndivyo unavyozidi kuzipata yaani ni kama vile unabarikiwaโ€ฆ.kama unajua au unavyoona matajiri wengi sana ni watoaji Wa hela kusaidia sehemu mbalimbali hasa kwa wasiojiweza au miradi ya kimaendeleo ndio maana unaona wanazidi kufanikiwa.

Watu wengi tunazifanyia Pesa kazi badala ya Pesa kutufanyia sisi kazi. Hii ni kutokana na kwamba hatujaelewa au hatujui jinsi gani ya kutengeneza mfumo utakaokuwa unakuingizia tu Pesa hata kama haupo.Umeshawahi kujiuliza hicho unachokifanya kama ukipumzika kwa muda Wa kama miezi sita utaendelea kupata kiasi kilekile cha Pesa ulichokuwa unakipata kabla ya kupumzika?Kama huwezi hivyo basi wewe unazifanyia Pesa kazi.

Kwa muajiriwa ukipumzika miezi sita utaendelea kulipwa mshahara wako?
Kwa mfanyabiashara labda Wa duka ukipumzika wiki moja bila kufungua duka lako utapata kipato kile kile unachokitengeneza kila siku?Kama hauwezi basi ujue unazifanyia Pesa kazi.

Tukiangalia kwa upande mwingine wafanyabiashara wakubwa wanaweza kupumzika hata mwaka mzima na wakaendelea kupata hela zilezile kwani wameshatengeneza mfumo ambao sisi wengi hatunao na ndio watu ambao Pesa zinawafanyia kazi.Ana uwezo Wa kwenda kupumzika Marekani mwaka mzima na Pesa zikaendelea kuingia huu ndio Uhuru Wa Pesa.

Jiulize wewe unazifanyia Pesa kazi au Pesa zinakufanyia wewe kazi?
Unaufanyia mfumo kazi au mfumo unakufanyia wewe kazi?
Kipato chako ni endelevu au sio endelevu?
Ukipumzika mwaka mzima bila kufanya au kugusa chochote utaendelea kupata kipato hichohicho?

Kama jibu ni hapana basi ni muda muafaka Wa kubadilika na kubadilisha unachokifanya.

โ€ฆโ€ฆShtuka na changamkia fursaโ€ฆโ€ฆ

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About