Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya kutunza kucha kujiepusha na maradhi shambulizi ya Kucha

Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.

Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.

Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.

Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.

Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.

Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.

Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.

Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.

Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.

Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.

Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)

Heshima za Liturujia kwa Bikira Maria

Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia ya Kiroma. Hapa zimepangwa kulingana na heshima zinavyozidiana:
Sherehe
8 Desemba – Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili 1 Januari – Bikira Maria Mama wa Mungu 25 Machi – Bikira Maria Kupashwa Habari 15 Agosti – Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni

Sikukuu

31 Mei – Maamkio ya Bikira Maria 8 Septemba – Kuzaliwa kwa Bikira Maria

Kumbukumbu

Juni – Moyo Safi wa Maria 15 Septemba – Mama Yetu wa Huzuni 22 Agosti – Bikira Maria Malkia 7 Oktoba – Bikira Maria wa Rozari 21 Novemba – Bikira Maria Kutolewa Hekaluni

Kumbukumbu za Hiari

11 Februari – Bikira Maria wa Lurdi 13 Mei – Bikira Maria wa Fatima 16 Julai – Bikira Maria wa Mlima Karmeli 5 Agosti – Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria 12 Septemba – Jina takatifu la Maria 12 Desemba – Bikira Maria wa Guadalupe
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu.
Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria: mashariki zinatumika tenzi na nyimbo mbalimbali, k.mf. Akatistos inayomuita “daraja linalounganisha dunia na mbingu”, “ngazi aliyoiona Yakobo” “kina kisichochunguzika kwa macho ya malaika” (Mwa 28:12); magharibi]] anaheshimiwa kwa rozari.
Wakristo wanaomheshimu Bikira Maria hawamuabudu hata kidogo, lakini wanamtolea heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Tofauti ni kwamba Mungu tu anastahili kuabudiwa (kwa Kigiriki, ‘latria’) watakatifu wanapewa heshima (‘dulia’) na Bikira Maria heshima zaidi (‘yuper-dulia’). Kanisa Katoliki linakiri neema zote za Mungu zinampitia Maria.

Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara

HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
💥Mama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.

💥Lakini kwa bahati mbaya akiwa amefika katikati ya mlima alizidiwa kiafya na hatimaye akashushwa mlimani akiwa amezirai hadi hospitalini.

💥Siku ya tatu alipozinduka hospitalini huku marafiki zake wakimpa pole, aliwajibu kuwa “Mlima Kilimanjaro hauwezi kuongezeka urefu, lakini mimi mwanadamu nina uwezo wa kuongeza maarifa, nguvu na mbinu za kupanda milima wowote duniani. Kwa hiyo nitarudi tena wakati mwingine mpaka nipande mlima Kilimanjaro hadi kileleni, ingawa nimepata changamoto wakati huu.”.

💥Alivyorudi kwao Marekani, alianza kufanya mazoezi tena ya kukimbia na kupanda vichuguu na vilima kwa muda wa mwaka mzima, na kisha mwaka uliofuata alirudi tena Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro mpaka kilele cha Kibo na mawenzi, na hatimaye akapewa cheti cha kupanda mlima Kilimanjaro!.

💥Je huyo mzungu angeamua kusubiri mlima Kilimanjaro upungue urefu ndipo aje Tanzania kuupanda, jambo hilo lingewezekana?

💥Je unataka maisha yawe rahisi ndipo uyamudu? Je unataka viwanja vishuke bei ndiyo ujenge nyumba yako? Je unataka ada za shule ziwe chini ndipo usome? Je unataka gharama za hospitali ziwe chini ndipo utibiwe? Je unataka mahari iwe chini ndipo uoe? Je unataka vitabu vya mafunzo ya biashara viwe bei chee ndiyo ununue? Unataka mshahara wako uwe mkubwa ndipo ufanikiwe? Je unataka shetani auwawe ndiyo umche Mungu? Je unataka dunia irudi nyuma, ndipo uweze kuyamudu maisha? Je, unataka urudi tumboni mwa mama yako ili uwe unakula na kulala bure? Ebo!🙊

💥Kama nia yako ni kufanikiwa hutakiwi kujionea huruma, nenda kwa wakati na ujitoe hadi kieleweke.

Kila la kheri na pia nakutakia MAFANIKIO makubwa sana wewe na kizazi chako! Siri ya utajiri ni ubahil asikudang’anye mtu tumia hela ikuzoee hakuna aliyezaliw kuwa maskin!

Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Mahitaji

Unga – 4 Vikombe

Sukari -10 Ounce

Siagi – 10 Ounce

Mdalasini ya unga – 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika – 4 ounce

Maziwa ya maji – 4 Vijiko vya supu

Maandalizi

Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Amri ya Kwanza ya Mungu: Mambo Muhimu ya Kuzingatia

Katika amri ya kwanza ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusadiki kuwa Mungu ni mmoja, ndiye Baba yetu na Mkubwa wetu: tumpende, tumwabudu yeye peke yake. (Mt 10:33, Kumb 6:4-9)


Wakatoliki tunamwabudu Mungu kwa namna gani?

Tunamwabudu Mungu kwa sala , sadaka na matendo mema


Katika amri ya kwanza ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa kumdharau Mungu na kuweka imani yetu katika viumbe badala ya Mungu.


Je, kuna viumbe ambavyo tunaviheshimu kwa kumtukuza Mungu?

Ndiyo twamuheshimu Bikira Maria, Malaika na Watakatifu.


Kwa nini yatupasa kuwaheshimu Watakatifu?

Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu.


Je, tuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu?

Hatuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu tunawaheshimu tu.


Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22).

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. Kutoka 25 :18-22.

Vile vile Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli Wachonge sanamu ya nyoka na yeyote atakayeumwa na nyoka akiiangalia atapona.


Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?

Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu.


Ni nanai ana kosa kumuabudu Mungu?

Anayekosa kumuabudu Mungu ni yule;

1. Anayeacha kusali au anayesali hovyo
2. Anayemkufuru Mungu
3. Anayeamini na kushika mambo ya kipagani


Mambo gani yanavunja amri ya kwanza ya Mungu?

Mambo hayo ni;

1. Kuabudu sanamu
2. Kufanya matambiko
3. Kwenda kwa waganga
4. Kupiga bao au ramli
5. Kuvaa hirizi
6. Kushiriki mambo ya kichawi n.k.


Ni nini maana ya kuabudu sanamu?

Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake.


Kutokumuabudu Mungu ni kwa namna gani?

Ni kuruhusu kitu chochote kimtawale mtu badala ya Mungu, mfano cheo, pombe, mali, shetani, tuisheni, kazi, na kutoadhimisha Jumapili au kutoshiriki.


Mkatoliki anaabuduje?

Mkatoliki anaabudu kwa kupiga goti au magoti mawili na ni mbele ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu tuu hasa wakati wa kuingia na kutoka kanisani


Je magoti yanayopigwa wakati mwingine tofauti na wakati wa kuabudu yana maana gani?

Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwa Mkao wa sala


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)

Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;

“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)

Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?

Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.

“BWANA akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).

Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.

Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.

Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.

Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.

Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.

Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.

Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.

FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.

Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Tunawaheshimu Watakatifu namna gani?

Tunawaheshimu kwa kuadhimisha sikukuu zao, kwa kuomba maombezi yao, kufuata mifano yao na kuheshimu masalia na sanamu zao, kwa kuinama kichwa kidogo tunapopita mbele yake

Ujumbe mzuri wa kumtumia mpenzi wako kumtakia usiku mwema

“””””Yule””””” Anipendezae lazima nimkumbuke”” “”nimpe salamu “”moyo”” wangu “”uridhike”” “”Nimuombee kwa MWENYEZI “”MUNGU”” mabaya yamuepuke”” “”na kila lililo la kheri kwake lisiondoke”” “”nakutakia”” “ucku mwema”

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi

Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yy alialikwa. Akakuta mlango wa2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi yy hakuwa na zawadi. Mlango Wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto waume akapita kushoto akajikuta ametokea mtaani

😄😄😄😄😄😄😄😄. Tujifunze kutoa wandugu

*hatupendagi ujinga sisi*
🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿

Jinsi ya kupika Wali Wa Sosi Ya Tuna

Viambaupishi

Sosi Ya tuna

Tuna (samaki/jodari) 2 Vikopo

Vitunguu (kata kata) 4

Nyanya zilizosagwa 5

Nyanya kopo 3 Vijiko vya supu

Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo – cubes) 4

Dengu (chick peas) 1 kikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu

Hiliki 1/4 kijiko cha chai

Mchanganyiko wa bizari 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Pilipili manga 1 Kijiko cha chai

Vipande cha Maggi (Cube) 2

Wali

Mchele 3 Vikombe vikubwa (Mugs)

Mdalasini 2 Vijiti

Karafuu chembe 5

Zaafarani kiasi

*Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) 1/2 Kikombe

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Kosha Mchele na roweka.

2. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando.

3. Kaanga viazi, epua

4. Punguza mafuta, kaanga nyanya.

5. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi.

6. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi.

7. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali.

8. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu.

9. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven)

10. Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali.

11. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu).

12. Funika wali na upike katika jiko moto wa 450º kwa muda wa kupikika wali.

* Jirsh (komamanga) kavu zioshwe vizuri kutoa vumbi au tumia zabibu kavu (raisins)

Hii Ndiyo Namna Pekee ya Kuwa na Amani Katika Maisha Yako

Utangulizi

Namna pekee ya kuwa na Amani ni kuishi Mapenzi ya Mungu,

Kwa njia hii Moyo wako hautafadhaika, hautayumbishwa na hautajuta kwa kuwa utakua upo katika njia ya Mungu na njia ya Mungu haina Majuto kwa kuwa ni njema.

Njia zetu zinakua na Majuto kwa sababu hazifuati mapenzi njia na matakwa ya Mungu.

Namna Pekee ya Kuwa na Amani ni Kuishi Mapenzi ya Mungu

Katika dunia hii yenye changamoto na misukosuko mingi, kila mmoja wetu anatamani kuwa na amani ya kweli moyoni. Hata hivyo, amani hii haipatikani kwa wingi wa mali, umaarufu, au mafanikio ya kidunia. Namna pekee ya kuwa na amani ya kudumu ni kuishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Tunapochagua kuishi kwa mujibu wa mapenzi yake, tunapata utulivu wa ndani, furaha ya kweli, na uhakika wa maisha.

Moyo Wako Hautafadhaika

Tunapoishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu, moyo wetu unapata utulivu wa ajabu. Kila hatua tunayochukua inakuwa na uhakika kwa sababu tunajua tuko katika njia sahihi. Yesu alisema katika Yohana 14:27:

“Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; mimi nawapa, kama vile ulimwengu usivyotoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msione hofu.” (Yohana 14:27)

Amani anayotoa Yesu ni ya kudumu na ya kweli. Inatufariji na kutupa nguvu ya kuendelea mbele licha ya changamoto na magumu ya maisha.

Hautayumbishwa

Maisha yanapokuwa na misukosuko na mawimbi ya matatizo, wale wanaoishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu hawatayumbishwa. Imani yetu inatufanya tuwe na msingi imara ambao hautikisiki na dhoruba za maisha. Mithali 3:5-6 inasema:

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.” (Mithali 3:5-6)

Tunapomtumaini Mungu na kumtegemea katika kila jambo, anatuongoza na kutupatia mwongozo wa maisha ambao hautushawishi na mawimbi ya dunia.

Hautajuta

Kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu hakutaleta majuto. Njia ya Mungu ni njema, yenye baraka na inayotuelekeza kwenye uzima wa milele. Mungu ana mpango mzuri kwa kila mmoja wetu, na anataka tuishi kwa kufuata mapenzi yake ili tupate mema yote aliyoandaa kwa ajili yetu. Yeremia 29:11 inatukumbusha:

“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” (Yeremia 29:11)

Tunapomfuata Mungu na kuishi kwa mujibu wa mapenzi yake, tunapata uhakika wa kuwa katika mpango wake mzuri na hatutajuta.

Njia Zetu Zinakua na Majuto

Njia zetu binafsi zinaweza kuwa na majuto kwa sababu mara nyingi hazifuati mapenzi, njia na matakwa ya Mungu. Wakati tunapojaribu kufanya mambo kwa nguvu zetu wenyewe na bila kutafuta mwongozo wa Mungu, tunaweza kujikuta tunafanya makosa na kupata majuto. Isaya 55:8-9 inasema:

“Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu ziko juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.” (Isaya 55:8-9)

Njia za Mungu ni bora zaidi na zina mwongozo sahihi kwa ajili ya maisha yetu. Tunapomfuata Mungu na kuishi kwa mujibu wa mapenzi yake, tunajiepusha na majuto ya njia zetu binafsi.

Hitimisho

Amani ya kweli na ya kudumu inapatikana tu tunapoishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Kwa njia hii, moyo wetu hautafadhaika, hautayumbishwa na hautajuta kwa kuwa tutakuwa katika njia ya Mungu, ambayo ni njema na yenye baraka. Njia zetu za kibinafsi mara nyingi zinatupeleka kwenye majuto kwa sababu hazifuati mapenzi, njia na matakwa ya Mungu. Hivyo basi, tumtafute Mungu kwa moyo wetu wote, tumtumaini na kufuata njia zake ili tuwe na amani ya kweli na furaha ya milele.

Mambo ya Msingi Sana Kuhusu Kusali na Kuomba

Rafiki yangu, Omba utafute uso wa Mungu, Aonaye kwa Siri atakujibu kwa wazi.

Mungu ni Mwaminifu Sana hasa kwa wamwombao bila kukoma na kwa matumaini

Mungu yeye anasikia Sala zetu zote na kuzijibu zote.

Mungu hujibu na kutupa kile kilicho muhimu na kizuri kwetu kwa wakati huo.

Ni kama vile Mtoto anapomwomba mzazi wake wembe wa kukata kucha lakini mzazi hampi kwa kuwa anajua utamdhuru.

Vivyo hivyo Mungu hutupa Kile kilicho bora na sio tunachokitaka.

Uwezo wa Mungu ni mkuu na anaweza kutupa chochote tunachoomba.

Lakini kwa Upendo wake usio na mfano anatupa vile vilivyo vizuri kwetu.

Mtumainie Mungu kila wakati.

Rafiki Yangu, Omba Utafute Uso wa Mungu

Rafiki yangu, omba utafute uso wa Mungu, kwa maana yeye aonaye kwa siri atakujibu kwa wazi. Mungu ni mwaminifu sana, hasa kwa wale wanaomwomba bila kukoma na kwa matumaini. Mungu husikia sala zetu zote na kuzijibu kwa hekima na upendo. Tunapomwomba Mungu kwa imani na uvumilivu, anatupa kile kilicho bora kwetu kwa wakati wake mwafaka.

Mungu Anasikia na Kujibu Maombi

Biblia inatufundisha kwamba Mungu husikia na kujibu maombi yetu. Yesu alisema katika Mathayo 6:6:
“Lakini wewe, uombapo, ingia katika chumba chako cha ndani, kisha funga mlango wako, uombe kwa Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujibu kwa dhahiri.” (Mathayo 6:6)

Mungu anapenda tuombe tukiwa na moyo wa unyenyekevu na uaminifu. Sala zetu zinazotoka moyoni humfikia Mungu, na kwa upendo wake mkuu, anatupatia majibu kwa njia ambazo ni bora kwetu.

Mungu Ni Mwaminifu

Mungu ni mwaminifu sana kwa wale wanaomwomba kwa matumaini. Biblia inasema katika 1 Yohana 5:14-15:
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kwamba, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Nasi tukijua ya kuwa atusikia katika lolote tuombalo, twaijua kwamba tumevipata vile vitu tulivyomwomba.” (1 Yohana 5:14-15)

Tunapoomba kwa kuzingatia mapenzi ya Mungu, tunakuwa na uhakika kwamba Mungu atasikia na kutujibu.

Mungu Anajibu Kulingana na Hekima Yake

Mungu hujibu maombi yetu kulingana na hekima yake kuu. Wakati mwingine tunapomwomba Mungu vitu fulani, hatupokei majibu tunayotarajia. Hii ni kwa sababu Mungu anajua zaidi kuhusu kile kilicho bora kwetu kuliko tunavyojua sisi wenyewe. Kama vile mzazi anavyomkatalia mtoto wake kitu hatari kwa ajili ya usalama wake, ndivyo Mungu anatupa kile kilicho bora zaidi kwetu. Yesu alisema katika Mathayo 7:9-11:
“Au ni nani miongoni mwenu, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akimwomba samaki, atampa nyoka? Basi, ikiwa ninyi, mlio wabaya, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba yenu aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa mema wao wamwombao?” (Mathayo 7:9-11)

Mungu, kwa hekima yake isiyo na kipimo, anatupatia kile kilicho bora zaidi kwa maisha yetu. Anajua mahitaji yetu halisi na hutupatia yale yatakayotusaidia kukua kiroho na kufanikisha kusudi lake maishani mwetu.

Uwezo wa Mungu ni Mkuu

Mungu ana uwezo mkuu na anaweza kutupa chochote tunachoomba. Yesu alisema katika Marko 11:24:
“Kwa hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.” (Marko 11:24)

Tunapomwomba Mungu kwa imani, tukiwa na uhakika kwamba atatupatia tunachohitaji, tunaweza kuwa na amani na utulivu tukijua kwamba Mungu anasikia na kujibu maombi yetu.

Mungu Anatupatia Kile Kilicho Bora

Kwa upendo wake usio na mfano, Mungu anatupatia vile vilivyo vizuri kwetu. Warumi 8:28 inasema:
“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.” (Warumi 8:28)

Mungu anafanya kazi kwa pamoja na sisi ili kutupatia mema. Hata wakati hatuelewi kwa nini maombi yetu hayajajibiwa kama tulivyotaka, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu anafanya kazi kwa ajili yetu, akituandalia mema makubwa zaidi.

Mtumainie Mungu Kila Wakati

Tunapaswa kumtumainia Mungu kila wakati, tukijua kwamba yeye anajua mahitaji yetu na anafanya kazi kwa ajili yetu. Mithali 3:5-6 inasema:
“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.” (Mithali 3:5-6)

Kumtumainia Mungu kwa moyo wetu wote inamaanisha kumwomba, kumtegemea, na kuamini kwamba anafanya kazi kwa ajili yetu kila siku. Mungu ni mwaminifu na anataka tuishi maisha ya furaha na amani, tukijua kwamba anatupatia kila tunachohitaji kwa wakati wake mwafaka.

Rafiki yangu, omba utafute uso wa Mungu, kwa maana yeye aonaye kwa siri atakujibu kwa wazi. Mungu ni mwaminifu sana hasa kwa wale wanaomwomba bila kukoma na kwa matumaini. Mungu husikia sala zetu zote na kuzijibu kwa hekima na upendo. Uwezo wa Mungu ni mkuu na anaweza kutupa chochote tunachoomba. Lakini kwa upendo wake usio na mfano, anatupa kile kilicho bora zaidi kwetu. Mtumainie Mungu kila wakati na utaona mema yake yakitimia katika maisha yako.

Angalia binadamu walivyo

Angalia Binadamu walivyo!,

“Ukitafuta sana anakuita MCHAWI,”

Ukifanikiwa sio BURE,

“Ukitulia MVIVU,”,

Usipovaa vizuri MCHAFU,

Ukidili sana na masomo unajifanya MSOMI,

Usipodili nayo MJINGA,

Ukisema sana MBEA,

Ukiwa mkimya JEURI,

Ukiwasaidia watu UNATAKA SIFA,

Usipowasaidia ROHO MBAYA,

Ukiwa na kazi UNAJISIKIA,

Usipokua nayo MZEMBE.

Hivyo BINADAMU ndivyo walivyo wewe jali MAISHA YAKO TU NA MAENDELEO YAKO.

MUNGU akulinde na shari zao.

MITAGUSO MIKUU YA KANISA KATOLIKI

MITAGUSO MIKUU

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo.

ORODHA YA MITAGUSO MIKUU

• Katika milenia ya kwanza ilifanyika mashariki (Uturuki wa leo):
1. Nisea I (mwaka 325)
2. Kostantinopoli I (381)
3. Efeso (431)
4. Kalsedonia (451)
5. Kostantinopoli II (553)
6. Kostantinopoli III (680-681)
7. Nisea II (787)
8. Kostantinopoli IV (869-870)
• Katika milenia ya pili ilifanyika magharibi (Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Vatikano ya leo):
9. Laterano I (1123)
10. Laterano II (1139)
11. Laterano III (1179)
12. Laterano IV (1215)
13. Lyon I (1245)
14. Lyon II (1274)
15. Vienne (1311-1312)
16. Konstanz (1414-1418)
17. Firenze (1431-1445)
18. Laterano V (1512-1517)
19. Trento (1545-1563)
20. Vatikano I (1869-1870)
21. Vatikano II (1962-1965)

HISTORIA YA MITAGUSO MIKUU

Mitaguso mikuu ya kwanza ilifanyika hasa ili kubainisha katika mafundisho yaliyogongana yapi yanalingana na imani sahihi. Mwisho wake ulikuwa kutangaza dogma fulani na kutenga na Kanisa watakaokataa kuiamini na watakaofundisha tofauti.
Mitaguso iliyofanyika baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la mashariki na la magharibi, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya, ilishughulikia zaidi urekebisho wa Kanisa katika ngazi na nyanja zote. Kwa namna ya pekee Mtaguso II wa Vatikano tangu uitishwe ulijulikana kuwa wa kichungaji, yaani usio na lengo la kufundisha dogma mpya wala kulaani mafundisho mengine.

Mtaguso I wa Nisea (325)

Mtaguso I wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa (tangu mwaka 338) mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya pekee kati ya mitaguso yote.
Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Washiriki walitokea hata nje ya dola hilo, kama vile Persia na Armenia. 2
Katika hali hiyo mtaguso ulianza tarehe 20 Mei 325; washiriki walikuwa kama 318, wengi wao wakitokea upande wa mashariki wa dola hilo. Upande wa magharibi uliwakilishwa na watu 4 kutoka Ulaya na 1 kutoka Afrika. Papa Silvesta I (314-335) aliwakilishwa na mapadri wawili.
Asili ya mabishano ilitokea katika Kanisa la Aleksandria (Misri), ambapo kasisi Arios alikuwa amekanusha umungu wa Yesu, na hivyo alihukumiwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 321, iliyoitishwa na askofu Aleksanda wa Aleksandria. Hata hivyo Arios hakuacha mafundisho yake, akakimbilia Palestina kwa rafiki yake Eusebio wa Nikomedia.
Basi, mtaguso ulikiri karibu kwa kauli moja kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwa maana ana ousìa (yaani dhati) ileile ya Kimungu aliyonayo Baba. Ndiyo kiini cha Kanuni ya imani ya Nisea iliyopitishwa na mtaguso.
Uamuzi mwingine wa mtaguso ulikuwa kupanga siku ya Pasaka, sherehe kuu ya Kanisa, iwe Jumapili inayofuata mbalamwezi ya kwanza ya majira ya Springi, tofauti na kalenda ya Kiyahudi. Pia zilitungwa kanuni 20 kuratibu mambo mbalimbali.
Mtaguso ulipomalizika tarehe 25 Julai 325, Konstantino alifikiri uamuzi juu ya dogma utamaliza mabishano, lakini haikuwa hivyo, kwa sababu Wagiriki wengi, ingawa hawakukubaliana na Arios, hawakuridhika na msamiati uliotumika kuelezea uhusiano wa Baba na Mwana.

Mtaguso I wa Konstantinopoli (381)

Mtaguso I wa Konstantinopoli ndio wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene yaliyofanyika wakati wa mababu wa Kanisa. Uliitishwa na kaisari Theodosius I ukafanyika Konstantinopoli mwaka 381.
Maaskofu 150 waliohudhuria walilaani aina mbalimbali za uzushi, hasa ule wa Masedoni wa Konstantinopoli aliyekanusha umungu wa Roho Mtakatifu, wakathibitisha maamuzi ya mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso I wa Nisea), uliofanyika mwaka 325.
Hivyo walikiri kwamba Roho Mtakatifu pia, kama vile Yesu Mwana wa Mungu, anachanga dhati ileile ya Baba.
Pamoja na hayo, walikamilisha kanuni ya imani ya Nisea ambayo kwa sababu hiyo inaitwa sasa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli na ambayo inatumika sana hata leo katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika liturujia.

Mtaguso wa Efeso (431)

Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosi II; Papa Selestini I (422-432) alimteua Sirili wa Aleksandria kuuendesha; washiriki walikuwa zaidi ya 150 na kujadili vikali hasa uzushi wa Nestori wa Konstantinopoli.
Patriarki huyo alikuwa anasisitiza ubinadamu wa Yesu Kristo kuliko umungu wake, akisema Bikira Maria alimzaa mtu Yesu, si Mungu, wala si Neno wa Mungu aliyehifadhiwa ndani ya nafsi ya Kristo kama hekaluni. Kwa hiyo Kristo alikuwa Theophoros, yaani “mbeba Mungu”, na Maria Christotokos, “Mama wa Kristo” si Theotokos, “Mama wa Mungu”.
Mtaguso huo ulilaani haraka mafundisho hayo ukikiri kwamba nafsi ya Yesu Kristo ni moja tu, ile ya milele ya Mwana wa Mungu, na kwamba nafsi hiyo ilitwaa ubinadamu kamili wenye mwili na roho. Hivyo Maria ni Theotokos kwa kuwa alimzaa Mungu kama binadamu.
Wajumbe wa Papa walipofika walithibitisha uamuzi huo, lakini maaskofu kutoka Antiokia hawakuridhika, na uzushi huo uliendelea Mesopotamia na kuenea hata Asia mashariki.
Mtaguso ulitangaza kuwa Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni kamili ukakataza isibadilishwe kwa namna yoyote. Pia ulilaani Upelaji, uzushi kutoka Ulaya magharibi kuhusu uwezo wa binadamu kutenda mema bila kusaidiwa na neema ya Mungu.

Mtaguso wa Kalsedonia (451)

Mtaguso wa Kalsedonia (leo katika nchi ya Uturuki) unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumeni iliyofanyika katika historia ya Kanisa.
Mtaguso huo uliitishwa na kaisari Marcianus wa Dola la Roma Mashariki pamoja na mke wake Pulkeria wa Bizanti miaka 20 baada ya Mtaguso wa Efeso.
Hao waliona haja ya kudumisha umoja wa Wakristo, uliokuwa msingi wa uimara wa dola hilo, hasa wakati huo ambapo makabila yasiyo na ustaarabu kutoka Asia yalikuwa yanajaribu kuteka Ulaya.
Umoja huo uliingia hatari ya kuvunjika kutokana na uamuzi wa mtaguso mkuu wa Efeso kuhusu imani sahihi juu ya Yesu Kristo kutoeleweka kwa namna moja.
Hasa baadhi ya walioshinda mtaguso huo walionekana kusisitiza mno umungu wake hata kutia shaka kama wanaamini sawasawa ubinadamu wake.
Vikao vilianza tarehe 8 Oktoba 451 vikiwa na washiriki zaidi ya 350: mara nyingi inatajwa idadi ya 600 hivi. Hatimaye mafundisho ya Eutike na Dioskoro wa Aleksandria yalilaaniwa.
Ufanisi wa mtaguso ulichangiwa na msimamo wa kaisari Valentiniano III wa Dola la Roma Magharibi, binamu wa Pulkeria. Kaisari huyo alimuunga mkono Papa Leo I (440-461) aliyekuwa ametoa msimamo wake na wa Kanisa la Roma tangu mwaka 449 katika Tomus ad Flavianum, yaani Waraka kwa Flaviano, Patriarki wa Konstantinopoli aliyeuawa na wafuasi wa Eutike. 3
Ingawa msimamo huo wa kati ulikubaliwa na wengi, wengine waliuona ni kinyume cha uamuzi wa Efeso, hivyo walishikilia sana mtazamo hao hata walipodhulumiwa na serikali. Ndiyo asili ya farakano la Misri, Syria, Armenia n.k. linalodumu hata leo.
Mtaguso huo ulitunga pia kanuni mbalimbali, kama vile kwa kumpatia Patriarki wa Konstantinopoli nafasi ya pili kati ya maaskofu wote.

Mtaguso II wa Konstantinopoli (553)

Mtaguso II wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.
Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu (Teodoro wa Mopsuestia, Teodoreto wa Kiro na Iba wa Edesa) yaliyochukiwa sana na Wamisri.
Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.
Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili (537-555) na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.
Hatimaye Papa Gregori I (590-604) aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa tano kati ya mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa Mtaguso wa Kalsedonia.

Mtaguso III wa Konstantinopoli (680-681)

Mtaguso III wa Konstantinopoli unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa sita kati ya Mitaguso ya kiekumeni.
Kaisari Konstantino IV wa Konstantinopoli ndiye aliyeuitisha na kuuendesha kuanzia tarehe 7 Novemba 680 hadi tarehe 16 Septemba 681.
Suala kuu lililosumbua Wakristo wa karne VII lilimhusu Yesu Kristo upande wa utashi. Ulikuwa unaenea mtazamo wa kwamba hakuwa na utashi wa kibinadamu, bali ule wa Kimungu tu.
Lakini wamonaki Sofronio wa Yerusalemu na Maksimo Muungamadini walipinga vikali jaribio hilo la kuleta upatanisho wa Waorthodoksi wa Mashariki (Wamisri n.k.) kwa kumpunguza Yesu katika ubinadamu wake kamili uliosisitizwa na Mtaguso wa Kalsedonia (451).
Vilevile Papa Martin I (649-655), katika mtaguso uliofanyika Laterani, alilaani mtazamo huo, kinyume cha Kaisari na Patriarki wa Konstantinopoli.
Konstantino IV alikubaliana na Papa Agatoni (678-681), na hivyo Mtaguso III wa Konstantinopoli ulilaani rasmi mtazamo wa kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu.

Mtaguso II wa Nisea (787)

Mtaguso II wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787 ili kujadili matumizi ya sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la Papa Adrian I (772-795).
Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa saba kati ya Mitaguso ya kiekumeni. Ni wa mwisho kufanyika wakati wa mababu wa Kanisa.
Mtaguso mkuu huo ulihitajika ili kumaliza mabishano makali kuhusu sanamu za Kikristo yaliyochukua zaidi ya miaka 100 hasa katika Dola la Roma Mashariki yakimalizika mwaka 843 tu.
Chanzo ni uamuzi wa kaisari Leo III wa Konstantinopoli (717-741) wa kuteketeza sanamu zote ili kujilinganisha na Waislamu waliotishia utawala wake.
Patriarki wa Konstantinopoli alilazimika kujiuzulu, lakini uamuzi wa kaisari ulizidi kupingwa hasa na wamonaki na mwanateolojia Yohane wa Damasko. Mapapa wa Roma pia walipinga uamuzi huo.
Sera ya dola ilibadilika aliposhika uongozi Irene kwa niaba ya mtoto wake mdogo Konstantino VI.
Mtaguso ulianza Konstantinopoli mwaka 786, lakini ulipoingiliwa na jeshi waliowaunga mkono maaskofu wengi waliopinga sanamu, Irene aliuhamishia Nisea ambapo vilifanyika vikao 7 kuanzia tarehe 28 Septemba 787. Cha mwisho kilifanyika katika ikulu tarehe 23 Oktoba 787.
Pamoja na maaskofu 300 hivi wa dola hilo, walihudhuria wamonaki wengi. Papa alituma mabalozi wake wawili na barua moja.
Mtaguso ulitofautisha heshima inayokubalika kwa sanamu na ibada isiyovumilika. Hoja kuu ni kwamba sanamu si kitu, ila inamwakilisha yule aliyechorwa ndani yake. Kimsingi sanamu zinakubalika kutokana na umwilisho wa Mwana wa Mungu uliomfanya atwae sura na kuonekana.
Mtaguso ulichukua pia maamuzi mbalimbali ili kurekebisha Kanisa.

Mtaguso IV wa Konstantinopoli (869-870)

Mtaguso IV wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani.
Kanisa Katoliki linahesabu kuwa Mtaguso Mkuu IV wa Konstantinopoli ule uliofanyika tangu tarehe 5 Oktoba 869 hadi 28 Februari 870.
Uliitishwa na Kaisari Basili I wa Konstantinopoli na Papa Adrian II (867-872), kwa sababu mwisho wa ikonoklastia katika sinodi ya mwaka 843 ulikuwa umeacha athari kubwa katika Kanisa la Mashariki. 4
Patriarki Metodi wa Konstantinopoli (843-847) alijitahidi kutuliza pande zote, lakini hakufaulu.
Alipofariki, malkia Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto Mikaeli III, alilazimisha nafasi yake ishikwe na Ignas I, mmonaki mwenye msimamo mkali, ambaye hatimaye aliondoshwa.
Badala yake alichaguliwa mlei msomi Fosyo ambaye kwa siku chache alipewa daraja na kutawazwa, lakini kufikia Februari 859 lililotea farakano kati ya waliomkubali yeye na waliomkubali Ignas I.
Ndipo Fosyo alipojitahidi kuungwa mkono na Papa Nikolaus I (858-867), ambaye kwanza alimkubali pamoja na pendekezo la Kaisari Mikaeli III la kuitisha mtaguso uliofanyika Konstantinopoli kati ya Aprili na Agosti 861 wakihudhuria maaskofu zaidi ya 300.
Papa hakupendezwa na maamuzi ya mtaguso huo, akashindana na Kaisari kimaandishi kwa sababu za kiutamaduni na za kisiasa pia.
Hapo Fosyo alipata nguvu dhidi ya Papa akaitisha mtaguso uliovunja umoja kati ya Makanisa ya Mashariki na yale ya Magharibi mwaka 867, akithubutu kwa mara ya kwanza kumhukumu Papa kama mzushi na kutaka kumuondoa madarakani.
Kumbe Kaisari mpya alimrudisha Ignas I kuwa Patriarki na pamoja naye akamuomba Papa atume mabalozi kwa mtaguso mwingine wa kufanyika Konstantinopoli.
Mtaguso ulipoanza tarehe 5 Oktoba 869 walikuwepo tu maaskofu wakuu 5 na maaskofu wengine 7, lakini walikuwepo mabalozi wa Mapatriarki wa Antiokia na Yerusalemu (wale wa Aleksandria walifika baadaye).
Waliokuwa upande wa Fosyo walikubaliwa kuhudhuria kuanzia tarehe 7 Oktoba wakamtetea sana dhidi ya msimamo wa Papa, lakini wakashindwa na kutengwa (29 Oktoba).
Baada ya miezi mitatu mtaguso uliendelea tarehe 12 Februari 870, wakiwepo maaskofu 67 walioongezeka tena hadi kufikia 103 siku ya mwisho (28 Februari), lilipotolewa tamko la imani pamoja na kanuni 26 kuhusu teolojia na sheria, bila kutoa mafundisho mapya. Pamoja na idadi yenyewe kutokuwa kubwa sana, ni muhimu kwamba walikuwepo maaskofu wakuu 37 kati ya 40.
Kwa kuwa mtaguso huu haukukubaliwa sana huko Konstantinopoli (hasa baada ya Fosyo kurudia Upatriarki mwaka 877), na pande mbili zilishindwa zaidi na zaidi kuelewana, uliitishwa mtaguso mwingine, ambapo wafuasi wa Fosyo walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya Waorthodoksi wanahesabu mtaguso huo mpya (879-880), uliofuta maamuzi dhidi ya Fosyo, kuwa wa kiekumeni na kuukataa ule wa miaka 10 ya nyuma. Lakini wengine hawakubali kuwa wa kiekumeni kwa sababu haukutoa mafundisho ya imani.
Ingawa wajumbe wa Papa Yohane VIII (872-882) walikubali kwanza maamuzi wa mtaguso huo ili kudumisha amani, na labda hata yeye mwenyewe, waandamizi wake waliukataa, na Fosyo mwenyewe aliondoshwa tena mwaka 886.

Mtaguso I wa Laterano (1123)

Mtaguso I wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi ukamalizika tarehe 11 Aprili 1123.
Mahali pake ni kwenye Kanisa Kuu la Roma (Italia) katika mtaa wa Laterano, alipokuwa anaishi askofu wake. Hukohuko baadaye ilifanyika mitaguso mingine minne ya Karne za Kati, halafu umuhimu wake ukapungua Papa alipohamia Vatikano.
Mtaguso uliitishwa na Papa Kalisti II (1119-1124) mnamo Desemba 1122, mara baada ya Mapatano ya Worms, ya kwanza kufanyika kati ya Papa na Dola Takatifu la Kirumi, iliyofurahisha sana wanakanisa, hata mwaka huo ulitajwa kuwa mwanzo wa kipindi kipya.
Mapatano hayo yalikomesha desturi ya walei kuteua viongozi wa Kanisa na wa utawa, yakitenganisha shughuli za kiserikali na zile za kidini, na kukubali kwamba mamlaka ya kiroho inatokana na daraja takatifu.
Ili kuthibitisha mapatano hayo, Papa alialika Roma maaskofu wote wa Magharibi. Waliohudhuria kweli walikuwa zaidi ya 900 kati ya maaskofu zaidi ya 300 na maabati 600 hivi). Papa mwenyewe aliendesha vikao.
Hakuna hati za mtaguso, ila matunda yake. Tunachojua ni kwamba Mapatano hayo yalisomwa yakapitishwa rasmi, pamoja na kanuni 22 au 25, ambazo nyingi zilikuwa zimeshapitishwa zamani.

Mtaguso II wa Laterano (1139)

Mtaguso II wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II (1130-1143), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi. Ni wa pili kufanyika Magharibi, kwenye Kanisa kuu la Roma (Italia).
Mtaguso ulihitajika kutokana na farakano lililotokea mwaka 1130 alipofariki Papa Honori II (1124-1130): hapo makardinali waligawanyika kuhusu Mapatano ya Worms, ambayo mwaka 1122 yalikuwa yamekomesha mashindano kuhusu uteuzi wa maaskofu.
Isitoshe, kulikuwa na ushindani kati ya koo mbili za Roma, yaani Frangipane na Pierleoni.
Tarehe 14 Februari 1130, makardinali 16 waliosimama upande wa familia ya Frangipane walimchagua Gregorio Papareschi, aliyejiita Papa Inosenti II. Saa chache baadaye, Pietro Pierleoni alichaguliwa na makardinali wengine na kujiita Anakleti II.
Hatimaye, kwa msaada wa Bernardo wa Clairvaux, Inosenti II alishinda na kukubaliwa na wengi, ingawa hakuweza kuhamia Roma mpaka baada ya mpinzani wake kufa (1138). 5
Mtaguso ulipaswa kurekebisha matokeo ya farakano hilo. Basi, Inosenti II alifungua kikao na kuondoa madarakani maaskofu waliomfuata mpinzani wake.
Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso I wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa za kurudia zile za zamani kuhusu usimoni, mapadri wenye wake n.k.

Mtaguso III wa Laterano (1179)

Mtaguso III wa Laterano uliitishwa na Papa Aleksanda III (1159-1181) ufanyike huko Roma mwaka 1179, kutokana na Amani ya Venezia kati ya Kaisari Federiko I wa Ujerumani na Lega Lombarda ya Italia kaskazini.
Unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na moja. Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu uchaguzi wa Papa, ukidai thuluthi mbili za kura za makardinali wote, bila kutofautisha haki za makundi yao matatu.

Mtaguso IV wa Laterano (1215)

Mtaguso IV wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.
Uliitishwa na Papa Inosenti III (1198-1216) kama kilele cha kazi yake.
Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 (wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria), na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.
Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani (kuhusu ekaristi n.k.) na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.
Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

Mtaguso I wa Lyon (1245)

Mtaguso I wa Lyon uliitishwa na Papa Inosenti IV (1243-1254) tarehe 24 Juni 1245 akiwa huko Lyon (Ufaransa), alipokimbilia usalama. Waliushiriki karibu viongozi 150 wa Kanisa Katoliki, ambalo linauhesabu kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tatu.
Baada ya mashindano makali kati ya mamlaka ya kiroho ya Papa na ile ya kisiasa ya kaisari huko Ulaya, mtaguso huo uliitishwa ili kumhukumu moja kwa moja kaisari Federiko II kuwa Mpinga Kristo.
Mtaguso ulianza tarehe 28 Juni 1245 wakiwepo maaskofu 144, halafu ukawa na vikao viwili vingine tena tarehe 5 Julai na 17 Julai. Hatimaye maaskofu walikuwa 225.
Mwanzoni papa alitangaza matatizo 5 yanayotesa Kanisa:
• kuharibika kwa imani na maadili;
• kushindwa kuikomboa Nchi takatifu (Yerusalemu ulitekwa tena na Waturuki mwaka 1244);
• kudumu kwa farakano la Waorthodoksi;
• kujitokeza hatari ya kuvamiwa na Watartari;
• kupambana na Federiko II.
Maamuzi yalitangazwa tarehe 25 Agosti tu, baada ya papa na wasaidizi wake kurekebisha miswada, yakapokewa na kufafanuliwa na vyuo vikuu. Lakini uamuzi wa kumuondoa madarakani kaisari haukuweza kutekelezwa hata kwa vita.

Mtaguso II wa Lyon (1274)

Mtaguso II wa Lyon unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na nne. Ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika karne XIII yote.
Mnamo Februari 1274, katika ikulu ya Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV (1265-1268).
Ndipo Papa Gregori X (1271-1276) alipoitisha mtaguso huko Lyon, ambao uhudhuriwe na wawakilishi wa Waorthodoksi ili kukamilisha umoja.
Papa Gregori X alifungua mtaguso tarehe 7 Mei 1274 akitangaza tena malengo yake matatu:
• kusaidia Wakristo wa Nchi takatifu,
• kuungana tena na Waorthodoksi,
• kurekebisha maadili ndani ya Kanisa.
Vilifuata vikao viwili tarehe 18 Mei na 4 Juni. Halafu tarehe 24 Juni ulifika na kupokewa kwa shangwe ujumbe kutoka Ugiriki, ukiundwa na maaskofu 2 na katibu wa kaisari.
Tarehe 6 Julai kilifanyika kikao cha nne kwa ajili ya muungano na hatimaye tarehe 16 Julai kile cha mwisho kilichopitisha hati mbalimbali za urekebisho. Kesho yake mtaguso ulifungwa.
Muungano haukuweza kudumu, kwa sababu, alivyoandika Papa Paulo VI (1963-1978) tarehe 19 Oktoba 1974, ulifanyika «bila kulipatia Kanisa la Kigiriki nafasi ya kutokeza kwa hiari mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Wakristo wa Kilatini ndio waliotunga hati na matamko kufuatana na mafundisho juu ya Kanisa yaliyofafanuliwa na kupangwa magharibi». 6
Mikaeli VIII alijaribu kulazimisha raia zake wapokee mambo wasiyoyakubali kwa moyo, hata akatumia nguvu kuwadhulumu waliokataa; akilaumiwa na watu wa Roma kwa kushindwa kufanikisha muungano, akaja kutengwa na Kanisa. Alipokufa (1282), mwanae Androniko II aliyemrithi, alifuta maamuzi ya baba yake kwa ajili ya muungano.
Vilevile mipango kwa ajili ya vita vya msalaba haikutekelezwa, na hatimaye (1291) Waturuki waliteka Akri, mji wa mwisho kubaki mikononi mwa Wakristo huko Mashariki ya Kati.
Maamuzi mengine yalihusu utaratibu mpya wa kumchagua Papa kwa lengo la kuzuia uchelewaji uliojitokeza hapo nyuma, na katazo la mashirika mapya ya kitawa.

Mtaguso wa Vienne (1311-1312)

Mtaguso wa Vienne unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.
Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Bonifas VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314) alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa), karibu na himaya ya mfalme huyo.
Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:
• suala la Wahekalu;
• vita vya msalaba;
• hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
• urekebisho wa Kanisa.
Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Kuhusu Wahekalu, mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Kuhusu Vita vya Msalaba, uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.
Kuhusu imani, ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Kuhusu urekebisho, ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.

Mtaguso wa Konstanz (1414-1418)

Mtaguso wa Konstanz (Ujerumani) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na sita. Uliitishwa na antipapa Yohane XXIII kwa ombi la kaisari Sigismund wa Ujerumani ukathibitishwa na Papa Gregori XII (1406-1415).
Lengo kuu lilikuwa kumaliza Farakano la Magharibi lililofikia hatua ya kuona maaskofu watatu kujidai Papa kwa wakati mmoja. Malengo mengine yalikuwa kung’oa uzushi na kurekebisha Kanisa “katika kichwa na viungo vyake”.
Hatimaye Papa Gregori XII alikubali kujiuzulu, wapinzani wake wawili waliondolewa, na Papa Martin V akachaguliwa.
Ulikuwa mtaguso muhimu kwa wingi wa waliohudhuria (makardinali 29, maaskofu 186, maabati zaidi ya 100 na wataalamu 300 hivi), muda (vikao 55) na mafanikio, ingawa majaribio yake ya mapinduzi yalishindikana, hasa ulipodai kuwa na mamlaka ya juu kuliko Papa.
Kati ya maamuzi mengine kuna hukumu dhidi ya John Wyclif na Jan Hus kama wazushi.

Mtaguso wa Firenze (1431-1445)

Mtaguso wa Firenze uliitishwa na Papa Martin V (1417-1431) mwaka wa mwisho wa uongozi wake ili kutekeleza shingo upande agizo la Mtaguso wa Konstanz la kwamba mtaguso ufanyike mara kwa mara.
Mtaguso ulianza Basel (Uswisi) chini ya Papa Eugenio IV (1431-1447), ukiwa na maaskofu wachache kulingana na mapadri na walei wenye haki ya kupiga kura.
Ingawa mtaguso ulifaulu kupatanisha wafuasi wa Hus na Kanisa, na kutoa sheria kadhaa za urekebisho kwa kibali cha Papa, baadaye ulianza kumshambulia yeye pamoja na makardinali, ukionyesha wazi wengi waliuona una mamlaka ya juu kuliko Papa, kinyume cha mapokeo.
Hapo Eugenio IV aliuvunja halafu akauhamishia Ferrara (Italia), ulipokutanika tarehe 8-1-1438, bila kujali upinzani wa wale ambao walibaki Basel na kumchagua antipapa wa mwisho, Felix V.
Huko Italia ulifika ujumbe mkubwa kutoka Konstantinopoli kwa ajili ya kurudisha umoja kati ya Kanisa Katoliki na Waorthodoksi. Kati ya wajumbe 700 kulikuwa na kaisari na patriarki wa Konstantinopoli, walioogopa Waturuki watateka mji wao (kama ilivyotokea kweli tarehe 29 Mei 1453); hivyo walihitaji msaada wa Wakristo wenzao wa magharibi.
Ferrara iliachwa kutokana na uhaba wa majengo na hofu ya tauni. 7
Mwaka 1439 mtaguso ulihamia Firenze ukafikia makubaliano ya kurudisha umoja (6-7-1439), ingawa uamuzi ukashindwa kutekelezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na upinzani wa waumini wa Konstantinopoli.
Vilevile tarehe 22-11-1439 yalifikiwa makubaliano na Waarmenia na tarehe 4-2-1440 yale na Wamisri.
Hatimaye tarehe 24-9-1443 mtaguso ulihamia Roma kwenye Laterano. Huko yalifikiwa makubaliano ya kurudisha umoja na Wasiria kadhaa (30-4-1444) na Wakaldayo na Wamaroni wa Kupro (7-8-1445).
Hakuna hati kuhusu mwisho wa mtaguso. Lakini waliobaki Basel na kujitenga na Papa, kufikia tarehe 19-4-1449 walimkubali Nikolaus V na siku sita baadaye walifunga mkutano wao.
Mtaguso huo ulichochea Wakristo wa magharibi kutamani mawasiliano na wenzao wa Ethiopia na India, jambo lililowafanya waanze zile safari za mbali kupitia baharini zilizowafikisha Afrika Kusini na Mashariki, China na Amerika.

Mtaguso V wa Laterano (1512-1517)

Mtaguso V wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma. Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.
Uliitishwa na Papa Julius II (1503-1513) ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X (1513-1521) hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.
Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.
Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.
Kabla yake kilifanyika “Kitaguso” cha Pisa: kwa kuwa Papa Julius II alikuwa hatekelezi kiapo chake cha kuitisha mtaguso kwa ajili ya urekebisho, baadhi ya makardinali, wakihimizwa na watawala wa Ujerumani na Ufaransa, waliuitisha huko Pisa (Italia) kuanzia tarehe 1 Septemba 1511. Walikusanyika wachache tarehe 1 Oktoba, halafu katika kikao cha nane walimsimamisha Papa wakahamia Lyon (Ufaransa).
Papa aliitikia “kitaguso” hicho kwa hati ya tarehe 18 Julai 1511, ambayo pamoja na kukipinga na kujitetea aliitisha mtaguso mkuu ukusanyike tarehe 19 Aprili 1512 huko Laterano.
Vita vilichelewesha mwanzo wa mtaguso wenyewe hadi tarehe 3 Mei 1512, walipokusanyika katika basilika la Laterano makardinali 15, mapatriarki 2, maaskofu wakuu 10, maaskofu 56, maabati na wakuu wa mashirika ya kitawa wachache pamoja na mabalozi wa nchi 3. Mwisho walikuwepo makardinali 23 na maaskofu 122.
Upande wa matokeo, utekelezaji wa maagizo ya mtaguso ulikuwa mdogo sana, la sivyo pengine Matengenezo ya Kiprotestanti yasingetokea. Ukweli ni kwamba Martin Luther aliyaanzisha miezi sita tu baada ya mtaguso kwisha.

Mtaguso wa Trento (1545-1563)

Mtaguso wa Trento (uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa.
Mtaguso huo, uliochukua muda mrefu kuliko yote ya historia, ulieneza urekebisho wa Kanisa na kuchukua msimamo kuhusu mafundisho ya Waprotestanti waliojitokeza katika hiyo karne XVI.
Mtu wa kwanza kulilia mtaguso ambao uamue kati yake na papa alikuwa Martin Luther (1517): huko Ujerumani ombi lake liliungwa mkono na wengi, pamoja na kaisari Karolo V aliyeuona kuwa njia ya kurekebisha Kanisa lakini pia ya kujiimarisha kimamlaka. Ndiyo sababu kuu iliyomfanya Papa Klementi VII (1523-1534), aliyesimama upande wa Ufaransa, kukataa kabisa kuuitisha.
Wazo hilo lilipata nguvu tena chini ya mwandamizi wake, Papa Paulo III (1534-1549), ambaye mwaka 1536 aliitia kwanza Mantova halafu Vicenza maaskofu na maabati wote, pamoja na wafalme wadogo wengi wa Dola takatifu la Kijerumani.
Baada ya juhudi mbalimbali kushindikana, mwaka 1542 uamuzi ulifikiwa wa kuitisha mtaguso huko Trento kwa sababu ni mji wa Italia lakini ulikuwa ndani ya mipaka ya dola hilo. Hatimaye (Novemba 1544) papa aliweza kutoa hati ya kuitisha mtaguso inayoitwa Laetare Jerusalem.
Mtaguso ulifunguliwa rasmi tarehe 13 Desemba 1545 katika kanisa kuu la Mt. Vigilio.
Mwanzoni mtaguso ulikuwa na maaskofu wachache, karibu wote kutoka Italia, ukatawaliwa na wajumbe wa papa. Kati ya makardinali wapya (Contarini, Sadoleto, Carafa, Fisher na huyo Pole) wengi walipenda urekebisho.
Zilijadiliwa na kupitishwa hasa dogma dhidi ya mafundisho ya Waprotestanti, kama vile kuhusu utakaso na wokovu. Pamoja na kupitisha tafsiri rasmi ya Biblia katika Kilatini iliyo maarufu kwa jina la Vulgata, kati ya maamuzi muhimu zaidi upo ule wa kudai maaskofu waishi katika majimbo yao ili kufanya uchungaji uliowapasa.
Baada ya mtaguso kuhamishiwa Bologna, Papa Paulo III aliusimamisha mnamo Septemba 1549.
Papa Julius III (1550-1555) aliuitisha tena kuanzia tarehe 1 Mei 1551 na zikatolewa hati juu ya sakramenti za Ekaristi, Kitubio na Mpako wa wagonjwa. Polepole waliohudhuria waliongozeka, 8
wakiwemo Waprotestanti wengi pia, wakidai wanateolojia wao wawe na haki ya kupiga kura na hati zilizokwishatolewa zifutwe. Ndipo ilipoonekana wazi kwamba tofauti katika imani ni kubwa mno.
Majeshi ya Kiprotestanti yalipokaribia Trento, Papa alikubali kusimamisha tena mtaguso tarehe 28 Aprili 1552.
Sehemu ya mwisho ya mtaguso baada ya kuitishwa ilichelewa kuanza hadi tarehe 18 Januari 1562, tena ilikabili matatizo mengi, lakini iliokolewa na kutawaliwa na askofu wa Milano Karolo Borromeo, mpwa wa Papa Pius IV (1559-1565) aliyemalizia haraka mtaguso wakiwemo wajumbe 255.
Katika sehemu hiyo yalitolewa mafundisho rasmi kuhusu Misa, Daraja takatifu na Ndoa, Toharani, sala kwa watakatifu, heshima kwa masalia na rehema. Pia Kanisa la Roma lilikubaliwa kama mama na mwalimu wa makanisa yote. Maaskofu wote walitakiwa kuahidia utiifu kwa Papa, ambaye peke yake ana haki ya kuitisha mtaguso mkuu. Kwa msingi huo, mtaguso ulimuachia Papa kuthibitisha maamuzi yote, naye alifanya hivyo bila kujali upinzani wa maofisa wake huko Roma.
Isitoshe, mwishoni, maamuzi mbalimbali yaliachwa mikononi mwa Papa na ofisi zake, yakachukuliwa miaka iliyofuata; kati yake, urekebisho wa Breviari na Misale, kwa kusawazisha liturujia za majimbo ya magharibi (isipokuwa chache, kama ya Milano na Lyon) kulingana na mapokeo ya Roma. Halafu ikatolewa Katekisimu ya Trento na Orodha ya vitabu vilivyokatazwa (Index librorum prohibitorum).

Mtaguso I wa Vatikano (1869-1870)

Mtaguso I wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa ishirini katika historia yake.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX (1846-1878) mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870, kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.
Walishiriki maaskofu na mapadri 774 (kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria), ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.
Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati Dei Filius juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.
Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani (kwa kifupi: akisema “ex cathedra”, yaani “kutoka ukulu).
Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.

Mtaguso II wa Vatikano (1962-1965)

Malengo ya Mtaguso II wa Vatikano

Muda mfupi baada ya kuchaguliwa Papa, mwenye heri Yohane XXIII alitangaza uamuzi wake wa kuitisha mtaguso mkuu akiamini kwamba utaweza kuandaa na kusababisha ustawi mpya wa maisha ya Kanisa. Lengo kuu la mtaguso lilikuwa kuliamsha Kanisa likumbuke wito wake na kwa kujifanya upya kwa ndani lipate msukumo mpya wa kimisionari ili kuwatangazia watu wote ujumbe wa milele wa wokovu, amani na umoja.
Tangazo hilo lilitolewa tarehe 25-1-1959. Baada ya maandalizi, Mtaguso II wa Vatikano ulifunguliwa tarehe 11-10-1962. Vikao vinne vikafanyika mpaka ulipofungwa tarehe 8-12-1965. Kila kikao kilianza Oktoba na kumalizika Desemba ya miaka hiyo.
Kwa kuwa Yohane XXIII alifariki tarehe 2-6-1963, vikao vitatu vya mwisho viliongozwa na mwandamizi wake, Paulo VI, na hati zote kumi na sita zikatolewa chini yake pia kwa kupigiwa kura ya ndiyo karibu kwa kauli moja. Maaskofu na wakuu wa mashirika kadhaa wenye haki ya kupiga kura walikuwa kama elfu tatu, wakiwakilisha karibu Kanisa lote duniani, isipokuwa nchi zile zenye kuwadhulumu Wakristo.
Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About