Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Soma hii Kabla hujafikiria kula nyama ya nguruwe tena

JEE NYAMA YA NGURUWE (KITI MOTO) NI SALAMA KWA BINADAMU???

Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu wa MEDICINE (Science)!!

Nguruwe ni mnyama anaeliwa na 38% ya watu wote duniani Na walaji wake ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Europe, Sub-Saharan Africa, America ya kaskazini , kusini mwa America, na Oceania.

Nguruwe ni mnyama ambae, Ana umbo la pekee sana, tukiangalia kuhusu madhara yake au faida yake , tunangalia vitu vinavyopatikana ktk mwili wake, tukilinganisha Na Faida.

FAIDA ZA NYAMA YA NGURUWE KITAALAMU

👉🏾Kunapatikna vitamini muhimu ktk mwili Wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12
👉🏾Unapata madini ya Chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
👉🏾Nyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako Na kuifanya iwe laini.
👉🏾Nyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida ktk mwili Wa binadamu
👉🏾Nyama ya nguruwe ina protein ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili
👉🏾Nyama ya nguruwe ina mafuta ambayo hutupa nguvu mwilini

HASARA YA NYAMA YA NGURUWE

Licha ya faida tajwa hapo juu, vile vile kuna hasara ya kutumia nyama hii.
👉🏾Nyama ya nguruwe ; ina sumu ya carcinogen ambayo inasababisha kansa; kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Na shirika la afya duniani ( WHO), Na The International Agency for Research on Cancer!! Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku 50gms basi uwezekano Wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa 18%
👉🏾Anasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na Centers for Disease Control and Prevention inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 ambaye anatokana Na Nguruwe(kiti moto) imeripotiwa kusababisha maradhi ya mripuko kwa nchi za MAREKANI
👉🏾Nyama ya nguruwe ina minyoo wajulilanao kwa jina la trichinella worm , ambao wadudu hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa joto Hata la 100C , utafiti uliofanyika 1998 Na WHO ukaonesha nyama ya Nguruwe iliopikwa kwa Joto la 104C , Huwa asilimia 52.37% ya trichinella worm wanabaki kuwa hai!! Wadudu hao wakiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; ambao huwa Na dalili kama ifuatavyo:
✅Homa kali sana
✅Kichwa kuuma
✅Kukosa nguvu
✅Maumivu ya nyama za mwili
✅Macho kuwa rangi ya pink(conjunctivitis)
✅Kuvimba uso Na kope
✅Kudhuriwa Na mwanga
👉🏾Nyama ya nguruwe ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambaye husababisha homa ya ini aina E
👉🏾Wadudu wengine ni kama;
🥄Nipah virus
🥄Menangle virus
🥄Viruses Ktk kundi Paramyxoviridae
Ambao wote hao; huwa wanaleta madhara kwa mwili Wa binadamu!!
👉🏾Nyama ya nguruwe husababisha Maradhi ambayo Yana resistance(ukinzani) Na ANTIBIOTICS
👉🏾Nyama ya nguruwe ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu ya shirika la Afya duniani(WHO) – Reference….open_http://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/taeniasis-cysticercosis
Wanasema; minyoo hii huwa;
👉Unaweza kuipata ikiwa hautapika nyama vizuri au Ukila nyama ya kuruwe ilioathirika(infected): Kwa hyo sio kila nyama ya Nguruwe iliopikwa vizuri, huwezi kupata minyoo hii.
👉Minyoo hii ikiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo Wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis
Mfano wake ni kifafa
👉30% ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa Na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe
👉🏾Watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa , huwa ni walaji wazuuri Wa Nguruwe.

JEE NG’OMBE, MBUZI, KONDOO NA WANYAMA WENGINE WALIWAO NA WENGI HAWANA MINYOO??

Ukweli ni kwamba Hata wanyama wengine nyama zao huwa zina minyoo aina ya Taenia saginata.
Ila minyoo ya Taenia saginata ni tofauti Na Taenia solium kwa sababu; Saginata wanakufa kwa joto Dogo sana, lakini solium wanahitaji 71C bila Hata kupungua!!
Swali langu kwako wewe msomaji Wa nakala hii;
👉🏾Nani anaepika huku akipima joto limefika au laa???

HITIMISHO

Tahadhari, sana Na nyama ya nguruwe , kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake!!!

Shared from;
Dr Isack

Sababu ya tatizo la Tumbo kujaa gesi na jinsi ya kujitibu

Tatizo la tumbo kujaa gesi husababishwa na kumeza chakula pamoja na gesi inayotolewa katika vyakula mbalimbali tunavokula ambayo hujaa tumboni na kwenye utumbo mdogo. Hali hii husababisha tumbo kujaa au kuvimba na mtu hutoa gesi hiyo kwa njia ya ushuzi na kubeua.

Nini husababisha.

Tatizo ili mara nyingi husababishwa na huambatana na mambo yafuatayo:
1. Kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo huchelewesha tumbo kufunguka kwa ajili ya usagaji wa chakula.

2. Kunywa vinywaji vyenye Carbonates, cola na kula vyakula vyenye gesi kama maharage, bigiji, vitunguu, kabichi n.k

3. Msongo wa mawazo na hasira.

4. Kula haraka haraka na kula unaongea.

5. Uvutaji wa Sigara

6. Magonjwa na maambukizi katika mfumo wa chakula asa kwenye tumbo na utumbo ambayo huzuia kusagwa na kufyonzwa kwa chakula.

Jinsi ya kujitibu.

· Kunywa chai ya tangawizi au karafuu itasaidia kupunguza gesi.

· Unaweza kunywa glasi moja ya juisi ya Limao baada ya kula.

· Tafuna mbegu za maboga zinasaidia kulainisha mfumo wa chakula

· Lalia ubavu wa kushoto na pumua kwa kasi ili kupunguza gesi tumboni.

· Kunja miguu na ikalie uku ukinyoosha mikono na kuinamia mbele itasaidia.

· kuongeza kasi ya mfumo wa chakula kufanya kazi na kuondoa gesi.

· Fanya mazoezi mepesi ya kutembea na kuruka ruka.

· Kula na tafuna chakula taratibu na epuka vyakula vyenye gesi na mafuta mengi,.

· Nenda hospitali kama tatizo ili linaambatana na kuharisha, kutapika, maumivu makali ya tumbo, kinyesi chenye rangi tofauti au damu na maumivu ya kifua.

Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka ‘Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina’.
Kugusa paji la uso tuna maana kukubali kwa akili, kugusa kifua maana yake ni kupokea na kuupenda msalaba moyoni na kugusa Mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba Msalaba kwa nguvu zetu zote.
Tunafanya njia ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu Mmoja katika Nafsi tatu. Pia Msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu.

Ishara ya Msalaba Juu ya Panda la uso, mdomo na kifua kabla ya injili
Hii ina maana Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu Kwa Akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa midomo yangu, na Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu Wote.

Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine

Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?

Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu

Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation

3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”

Mapishi ya tambi za mayai

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.

Mahitaji

  1. Tambi ½ paketi
  2. Vitunguu maji 2 vikubwa
  3. Karoti 1
  4. Hoho 1
  5. Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  6. Carry powder kijiko 1 cha chai
  7. Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  8. Mafuta kwa kiasi upendacho
  9. Mayai 2
  10. Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

Mahitaji

Ndizi mbichi – Kisia

Nyama ng’ombe – ½ kilo

Pilipili ya kusaga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi ya kusaga – 2 vijiko vya supu

Thomu (garlic/saumu) – 1 kijiko cha supu

Bizari mchuzi – 1 kijiko cha chai

Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) – 2 vijiko cha supu

Chumvi – Kiasi

Ndimu – 1 kamua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama ng’ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake
Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha.
Menya ndizi, ukatekate.
Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote.
Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu
Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.

Mapishi ya Supu ya makongoro

Mahitaji

Makongoro (miguu ya ng’ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Mzunguko wa elimu kiafrikaafrika

01.👉 Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.

02.👉 Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.👉 Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.👉 Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.👉 Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. 😂😂😂😂😉😆😆😆🏃🏃😜😜😜😜😜

Matumizi ya mbaazi kama dawa

Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza kutumika kama dawa kwa kutumia majani, mizizi na maua

MAANDALIZI

Chukua majani, maua au mizizi kiasi cha nusu kilo (ni vizuri kama utachanganya vyote) pondaponda na uloweke kwenye maji safi kiasi cha lita 2 kwa muda wa masaa 24.

Chuja na uweke dawa hii mbali na jua/joto, ni vizuri kama ataweka kwenye friji, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa siku 3

TIBA

Dawa hii inaweza kutibu magonjwa yafuatayo

1-Inauwezo mkubwa wa kushusha homa

2-Husaidia kuponesha vidonda.

3-Husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake.

4-Husaidia kupunguza uvimbe

5-Huponyesha kifua na kukohoa.

6-Husafisha kibofu/njia ya mkojo.

7- Huongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali

Jinsi ya kuishi maisha marefu (Mambo ya kuzingatia ili uishi maisha marefu)

Kuishi ukiwa na afya na kuishi maisha marefu kunawezekana kwa kubadili hali ya maisha unayoishi inayoharibu afya yako mfano uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi,kutokufanya mazoezi na kutokula matunda na mbogamboga.

Mambo yanayoweza kukusaidia kuishi maisha marefu ni kama yafuatayo

  1. Kuuandaa mwili kwa maisha marefu kwa kufanya mazoezi
  2. Kuwa makini kutambua na kutibu matatizo ya kiafya
  3. Kuepuka mazingira na kufanya kazi kwa namna au kazi zinazoweza kudhuru maisha yako. Mfano kuendesha gari bila kufuata utaratibu, kutokuvaa vifaa vya kujikinga wakati wa kazi
  4. Epuka vitu vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya yako na kukuletea matatizo ya kiafya kama dawa za mimea na mifugo, zitumie kama inavyotakiwa
  5. Usinywe pombe, usivute sigara wala kutumia dawa za kulevya
  6. Kula mlo kamili
  7. Usile vyakula vyenye chumvi na mafuta mengi
  8. Kunywa maji mengi ili kusafisha mwili
  9. Epuka msongo wa mawazo

Angalia huyu bibi alichotufanyia kwenye gari

​tulikua kwenye gari kibao ad wengne mlangon likasmimama kituo kimoja kulikua kuna bibi anataka kupanda​

Konda- bibi twende sit kibao ata utalala

Bibi – oooh sawa mjukuu

Konda – simama tu apo wanashuka mbele

Bibi – akacheka sana tu

Konda- mbona unacheka bibi

Bibi – mjukuu hawa wote hawashuki wanakufa apo mbele

Watu- simamisha gar

Saiv bibi kabaki mwenyewe amelala sit ya nyuma😆😆😅😂😂

Yafahamu Mawazo na Mipango ya Mungu Kwako

Utangulizi

Mungu daima anawaza Mema na Anampangia Mtu Mambo mema.

Kama mtu ataenda katika njia ambayo Ipo katika mipango na mapenzi ya Mungu basi atapokea yale mema Mungu aliyopanga Kwake.

Lakini kama mtu ataishi kwa kufuata mapenzi yake mwenyewe basi atapoteza yale mema Aliyopangiwa.

Mbele ya mtu kuna njia nzuri na mbaya, ni shauri yako sasa uchague nzuri au Mbaya. Nzuri ni kuchagua kuishi kama Mungu anavyotaka na Mbaya ni Kutokuishi kama Mungu anavyotaka.

Mungu Daima Anawaza Mema na Anampangia Mtu Mambo Mema

Mungu ni mwenye upendo, huruma, na hekima isiyo na kifani. Anatufikiria na kutupangia mema kila wakati. Hili ni jambo ambalo linaonekana wazi katika maandiko matakatifu. Mungu anataka tuishi maisha ya baraka, amani, na furaha. Hata hivyo, ili tuweze kupokea baraka hizi, ni muhimu tuishi kulingana na mapenzi na mipango yake.

Mungu Anawaza Mema Kila Wakati

Jeremia 29:11 inatukumbusha upendo na nia njema ya Mungu kwa watu wake:
“Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.” (Jeremia 29:11)

Hii inathibitisha kwamba Mungu anafikiria mema kwa ajili yetu. Anataka tuishi kwa amani na matumaini, lakini ni lazima tufanye sehemu yetu kwa kufuata njia zake.

Kufuata Mipango ya Mungu

Tunapochagua kuishi kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, tunajiweka katika nafasi ya kupokea baraka zake zote. Zaburi 37:4 inasema:
“Jifurahishe kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako.” (Zaburi 37:4)

Hii inaonyesha kwamba Mungu anajali haja zetu na anataka kutubariki. Ni lazima tuweke furaha yetu kwake na kuishi kulingana na mapenzi yake.

Hatari ya Kufuatilia Mapenzi Yetu Wenyewe

Mithali 14:12 inasema:
“Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.” (Mithali 14:12)

Tunapofuata mapenzi yetu wenyewe, tunaweza kupotea na kujikuta katika hali mbaya. Kila wakati tunahitaji mwongozo wa Mungu ili kuepuka njia zinazoweza kuleta matatizo na maafa katika maisha yetu.

Uchaguzi ni Wetu

Kila mmoja wetu ana uchaguzi wa kufanya: kufuata njia nzuri au mbaya. Njia nzuri ni kuchagua kuishi kama Mungu anavyotaka. Kumbukumbu la Torati 30:19 inasema:
“Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako.” (Kumbukumbu la Torati 30:19)

Mungu anatupatia uchaguzi wa kufuata njia zake na kupokea uzima na baraka, au kuishi kwa kufuata mapenzi yetu na kupata mauti na laana.

Mifano Halisi ya Watu Waliopokea Mema kwa Kufuata Mapenzi ya Mungu

  1. Noa:
    Noa alitii amri ya Mungu ya kujenga safina, na kwa kufanya hivyo, alilinda familia yake na wanyama wakati wa gharika. (Mwanzo 6:13-22)
  2. Ibrahimu:
    Ibrahimu alionyesha imani kuu kwa kumtii Mungu alipomtoa mwanawe Isaka kama sadaka. Mungu alimbariki na kumfanya kuwa baba wa mataifa mengi. (Mwanzo 22:1-18)
  3. Yusufu:
    Yusufu alikumbana na mateso mengi, lakini alibaki mwaminifu kwa Mungu. Mwishowe, Mungu alimwinua na kumfanya kuwa mfalme wa pili kwa ukubwa katika Misri, akiponya familia yake kutokana na njaa. (Mwanzo 37-50)
  4. Musa:
    Musa alitii wito wa Mungu wa kuwaongoza Waisraeli kutoka utumwani Misri hadi nchi ya ahadi. Kwa utii wake, Mungu aliwapa Waisraeli uhuru. (Kutoka 3:1-22)
  5. Yoshua:
    Yoshua alifuata maagizo ya Mungu kwa ujasiri na kuwaongoza Waisraeli katika ushindi dhidi ya Yeriko. (Yoshua 6:1-20)
  6. Gideoni:
    Gideoni aliongoza jeshi dogo la wanaume 300 dhidi ya jeshi kubwa la Wamidiani kwa ujasiri na utii kwa Mungu, na walipata ushindi mkubwa. (Waamuzi 7:1-25)
  7. Daudi:
    Daudi alimtumaini Mungu alipompiga Goliathi kwa imani. Mungu alimwinua kuwa mfalme wa Israeli na kumbariki kwa namna nyingi. (1 Samweli 17:45-50)
  8. Danieli:
    Danieli aliendelea kumwomba Mungu licha ya amri ya mfalme kinyume na maombi. Mungu alimlinda katika tundu la simba na kumwinua juu katika utawala wa Babeli. (Danieli 6:10-23)
  9. Esta:
    Esta alionyesha ujasiri na imani kwa kuwaomba Waisraeli wafunge na kuomba kabla ya kwenda kwa mfalme kuomba ulinzi kwa watu wake. Mungu aliokoa Waisraeli kupitia yeye. (Kitabu cha Esta)
  10. Maria:
    Maria alikubali kuwa mama wa Yesu kwa utii na unyenyekevu, akichukua jukumu kubwa la kumlea Mkombozi wa ulimwengu. (Luka 1:26-38)

Hitimisho

Mungu daima anawaza mema na anampangia mtu mambo mema. Kama mtu ataenda katika njia ambayo ipo katika mipango na mapenzi ya Mungu, basi atapokea yale mema Mungu aliyopanga kwake. Lakini kama mtu ataishi kwa kufuata mapenzi yake mwenyewe, basi atapoteza yale mema aliyopangiwa. Mbele ya kila mmoja wetu kuna njia nzuri na mbaya. Uchaguzi ni wetu sasa kuchagua nzuri au mbaya. Njia nzuri ni kuishi kama Mungu anavyotaka, na njia mbaya ni kutokuishi kama Mungu anavyotaka. Kumbuka, Mungu ana mipango myema kwa ajili yetu, na ni kwa kufuata mapenzi yake ndipo tunapoweza kuzipokea baraka zote ambazo ametuandalia.

Utajuaje kama una upungufu wa maji mwilini? Dalili ni hizi

Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini;

Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto.

Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.

Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

  1. Kukojoa mara chache sana
  2. Mdomo na ulimi kukauka
  3. Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.
  4. Mtoto kutokuwa mchangamfu
  5. Macho, tumbo au mashavu kubonyea

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee.

Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.
Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito.

Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:

  1. Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
  2. Kuumwa na kichwa.
  3. Mwili kukosa nguvu.
  4. Kichefuchefu na kutapika.
  5. Kukaukwa na mdomo.

Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?

Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora

Ufanyialo wengine ndilo utakalofanyiwa

Siku niliposoma hili andiko kwa mara ya kwanza nakumbuka, kwanza nilipata mshtuko flani baada ya kulisoma, halafu nikajikuta nikitafakari vitu vingi sana.

Hebu kwanza tusome pamoja andiko hili

ZABURI 109

17 Naye alipenda kulaani, nako kukampata.Hakupendezwa na kubariki, kukawa mbali naye

▶Huu mstari wa 17 umenishangaza sana, halafu ukanifungua na kunifundisha vitu vya msingi sana katika haya maisha tunayoishi

Ngoja tuuchambue kidogo hapa ili tuelewane vizuri

_Alipenda kulaani?………………………….Nako (laana/kulaaniwa) kukampata_

_Hakupendezwa na kubariki……………………(Kubarikiwa) kukawa mbali nae_

NET BIBLE inasema hivii

“He loved to curse others, so those curses have come upon him, He had no desire to bless anyone, so he has experienced no blessings” Kumbe the more ninakuwa na shauku ya kuona wengine wakibarikiwa, the more baraka zinanijia mimi and vice versa

Hapa nikajifunza kwamba kumbe yale mabaya tunayowafanyia au kuwawazia watu kuna uwezekano mkubwa sana yakatupata sisi wenyewe

Na tunapotamani kubarikiwa na kuinuliwa wakati hatufurahii kuona wengine wakiinuliwa, kuinuliwa kutakuwa mbali nasi

Huu mstari unaniongezea maarifa na kunifundisha namna ya kuishi katika ulimwengu huu

Nimewaza pia inawezekana wakati mwingine kuna vitu hatupati ni kwasababu tuu hatufurahii wala hatuombi wengine wapate hivyo

Kumbe kubarikiwa kwangu kunategemea na namna ambavyo ninakuwa baraka kwa wengine na kutamani kuona wengine wakibarikiwa

Shauku yangu ya kutamani wengine wabarikiwe na kuinuliwa ndio nyenzo ya kuinuliwa kwangu na moyo mbovu wa kufurahi kuona wengine wakikwama ndio sababu ya kukwama kwangu?

_”Hii ni kanuni ya ajabu”
Ndugu yangu, unajua hapa najifunza kwamba kumbe kuna uwezekano mkubwa kwamba mikwamo mingine tumekuwa tukijikwamisha sisi wenyewe

Ni kweli ninataka kubarikiwa, lakini ni mara ngapi nimefurahi au kuombea wengine ili wabarikiwe?

Unatamani kupandishwa cheo sawa, lakini wengine wakipandishwa vyeo unanuna? Au ukiona ofisini ndio anapewa safari nyingi za nje unakasirika?

Unatamani kuoa/kuolewa halafu wengine wakioa na kuolewa unaona uchungu juu yao, unawanunia, unapunguza ukaribu?

Unatamani kupata gari zuri lakini wengine wakipata unakasirika?

Nikiwa mtoto mdogo nakumbuka mwalimu mmoja aliwahi fundisha kwamba nisipende sana kujiombea mwenyewe, na akasema kama unahitaji kitu, waombee wengine wasionacho wapate, nawe utajibiwa pia, andiko hili limenifanya nielewe kwanini mwalimu yule alifundisha vile

Na wakati mzaburi anaongea maneno haya hapa chini sikumuelewaga, nilijua ni kawaida tuu, nilisoma kikawaida tuu, lakini sasa ndio nimefunguka ufahamu zaidi

*ZABURI 35*

13 Bali mimi, walipougua wao, Nguo yangu ilikuwa gunia. Nalijitesa nafsi yangu kwa kufunga; Maombi yangu yakarejea kifuani mwangu

Bila kujali watu walikuwa wakimuwazia na kumfanyia nini, alipowaombea tuu, maombi yale yalirejea, yalifanya kazi na katika maisha yake. Kumbe kuomba kwaajili ya wengine wafanikiwe, wainuliwe, wabarikiwe na wapandishwe kunarejesha matunda kwetu pia

Ubaya unaomfanyia mwingine si ajabu ukakupata

Kuanguka unakomuombea mwingine kutakujia wewe

Kanuni hii inanifundisha pia kuwa YESU aliposisitiza tupendane alikuwa na maana kuu

Alijua kwamba ukiwa na chuki kwa mwingine chuki ile itakuathiri wewe

Ukiwa na moyo wa kufurahi wengine wanaposhindwa, kushindwa kutakupata wewe

Kwanini sasa tusichague kubariki wengine ili baraka zile zitupate na sisi pia?

Kwanini tusiwaombee mema wengine ili maombi yale ya mema yatutendee mema sisi?
Ni vyema sasa tukachagua kuwa na moyo wa upendo, moyo utakaowawazia na kuwatendea mema wengine kwasababu mema yale tuwafanyiayo wengine yatatuletea mema maishani mwetu pia

Jipime, jiangalie, jichunguze

Waza mema kwaajili ya wengine, mema yaje kwaajili yako

MITHALI 17

13 Yeye arudishaye mabaya badala ya mema,Mabaya hayataondoka nyumbani mwake

If you love to curse others, those curses will come upon you

If you have NO desire to bless others, then you will experience NO blessings

CHOOSE TO BLESS OTHERS,BLESSING WILL FOLLOW YOU

Maswali yanayoulizwa sana kuhusu Ibada ya Kanisa Katoliki

Masifu ni nini?

Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Tumuadhimishe nani?

Tumuadhimishe Mungu pekee siku zote za maisha yetu kwa tumaini la kumuadhimisha milele.
“Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, nitalisifu jina lako milele na milele” (Zab 145:1-2).
“Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina” (Rom 11:36).


Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa.
Pamoja na viumbe vyote tuwaimbie usiku na mchana, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!” (Ufu 4:8).
“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24).


Tumuadhimishe Mungu kwa jinsi alivyo au kwa maajabu anayotutendea?

Tumuadhimishe Mungu kwa jinsi alivyo, halafu kwa maajabu anayotutendea tangu awali, ambayo anatujulisha kidogo jinsi alivyo.
“Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele” (Zab 136:1).


Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu gani?

Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu aliyoyatenda katika Yesu, lakini pia katika Maria na wengine ambao wamefanana naye na kutuonyesha uwezo wa neema yake kwetu.
“Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa” (Ef 1:5-6).
Yeye atakuja “ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki” (2Th 1:10).


Tumuadhimishe Mungu kwanza kwa njia gani?

Tumuadhimishe Mungu kwanza kwa kumsikiliza kwa makini na kumuitikia kwa imani.
“Masikio ya watu wote yalikisikiliza kitabu cha torati… watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya torati” (Ne 8:3,9).
Kunyamaza ni sehemu ya ibada yoyote: tunahitaji kimya ili tuelewe tunachoambiwa na tunachosema.
“Nisikieni nyote na kufahamu” (Mk 7:14).
“Hamjui mnaloliomba” (Mk 10:38).


Je, ibada zetu ziishie katika kusadiki?

Hapana, ibada zetu zisiishie katika kusadiki, kwa kuwa tangu Agano la Kale Mungu aliagiza matendo mbalimbali ya ibada yanayolisha imani.
“Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako: Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa… Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu” (Mwa 17:10,12).
“Mwanakondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja… Kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni… Ni Pasaka ya Bwana… Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana” (Kut 12:5,6,11,14).
Kwetu sisi Wakristo ni yale tuliyoagizwa na Yesu ili yatuletee wokovu.
“Aaminiye na kubatizwa ataokoka” (Mk 16:16).


Kanisa linaitaje ibada hizo tulizoagizwa na Yesu?

Kanisa linaita ibada hizo tulizoagizwa na Yesu sakramenti, yaani mafumbo. Ziko saba: Ubatizo, Kipaimara, Ekaristi, Kitubio, Mpako wa Wagonjwa, Daraja na Ndoa. Ndiyo “mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono” (Eb 6:2) tuliyoyapata kupitia Mitume.
Tujihadhari na madhehebu yaliyopunguza sakramenti hizo saba tulizoachiwa na wema wa Yesu kwa kuwa alijua tunavyozihitaji.


Je, tuishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo?

Hapana, tusiishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo, kwa kuwa imani na sakramenti zinadai kutekelezwa maishani.
“Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?… Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana” (Rom 6:2-3; 12:1).
“Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Math 5:16).


Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?

Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake mafumbo hayakuadhimishwa vizuri.
“Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa” (Yak 2:26).


Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?

Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa kuzingatia umbile letu, kwamba binadamu ni umoja wa roho na mwili, hivyo anahitaji mwili na hisi zake ili kuingiza chochote rohoni na kutokeza yaliyomo katika roho yake isiyoonekana.
Ndiyo sababu Yesu alipoletewa kiziwi mwenye utasi “akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, ‘Efatha’, maana yake, ‘Funguka!’” (Mk 7:33-34).
Hizo zote ni ishara wazi kwa milango yetu ya fahamu.


Je, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo?

Ndiyo, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo, kila moja kadiri ya uwezo wake: macho kwa kuona, pua kwa kunusa, kinywa kwa kuonja na kusema, mwili mzima kwa kugusa na kutenda, lakini hasa masikio kwa kupokea maneno yaletayo uzima wa Kimungu.
“Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima” (Yoh 6:63).
“Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia… Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rom 10:13-14,17).


Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?

Maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo kwa sababu yanafafanua ishara nyingine na kuzitia nguvu ya kututakasa.
“Kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno” (Ef 5:25-26).
Pasipo maneno hapana sakramenti yoyote.


Ishara za mafumbo zimetokana na nini?

Ishara za mafumbo zimetokana na viumbe (maji, mafuta, mkate, divai n.k.) na maisha ya jamii (kuosha, kupaka, kula na kunywa pamoja n.k.) na historia ya wokovu (kunyunyiza na kuzamisha, kuwekea mikono, kula Pasaka, n.k.),
lakini ni kwa kuagizwa na Yesu kwamba zinabeba kazi yake ya kuokoa na kutakasa.
“Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Lk 22:19).


Maneno na ishara kwenye ibada vinaweza kubadilishwa na nani?

Maneno na ishara vinaweza kubadilishwa na waandamizi wa Mitume, waliokabidhiwa na Yesu mamlaka ya kuendeleza kazi yake katika mazingira mbalimbali hata mwisho wa dunia.
“Amin, nawaambieni: Yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni, na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni” (Math 18:18).
Hao Maaskofu wanakiri hawawezi kamwe kuyabadilisha yale ambayo Yesu aliyaweka kuwa ya lazima kama yalivyo mafumbo yenyewe.
“Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi” (1Kor 11:23).
Mengine yote wanaweza kuyapanga na kuyarekebisha kadiri ya mazingira, kuanzia lugha, wakilenga daima wokovu wa watu.


Faida ya kupanga taratibu za ibada ni ipi?

Faida ya kupanga taratibu za ibada ni hasa kuhakikisha yote yafuate usahihi wa imani na maadili, yakidumisha umoja na upendo, badala ya kumuachia kiongozi au mwingine yeyote aseme na kufanya anavyotaka. Mitume wenyewe walianza kazi hiyo, wakidhibiti hata karama.
“Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze… Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga… Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu” (1Kor 14:26-30,37-38,40).
Polepole taratibu ziliongezeka na ibada zikapata mtiririko rasmi wa kueleweka: ndizo liturujia za mashariki na za magharibi ambazo zinaweza kuwa mbalimbali mradi zisipishane upande wa imani.


Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni nani?

Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni Mungu ambaye kwa njia hiyo anazidi kutufanyia maajabu alivyoyafanya Yesu alipokuwa duniani. Kama tunda la kutukomboa kwa kifo na ufufuko wake, Baba anatujaza humo Roho Mtakatifu kama advansi ya uzima wa milele.
“Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi yake aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:13-14).


Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama nani?

Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama walengwa ambao tuyatumie vema ili yazae matunda yote yaliyokusudiwa na Mungu.
Ndiyo kiini cha ukuhani wetu ambao tunashiriki ule wa Kristo tangu tubatizwe.
“Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo” (1Pet 2:4-5).


Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?

Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa kwa kuwa ndivyo anavyotufanya “tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo… tupate kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:4,12).
Tukipokea neema hiyo tunampatia ibada, sifa na shukrani na tunazidi kumuomba atujaze Roho Mtakatifu kwa njia ya Mwanae.
“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina” (Ef 3:20-21).


Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu.
Ubatizo, kipaimara na ekaristi vinatuingiza katika fumbo la Pasaka tuweze kuishi upya kama wana wa Mungu.
Kitubio na mpako wa wagonjwa vinatuponya roho na hata mwili. Daraja na ndoa zinatufanya wahudumu wa Kanisa na wa familia.
Ni muhimu tujue tunachohitaji na tukipate vipi.
“Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa” (1Kor 11:29-31).


Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna “ubatizo mmoja” (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya “kwa maji na kwa Roho” (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa.
Vilevile katika kipaimara na daraja, karama inayopatikana kwa kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume haifutiki, inadai kuchochewa tu.
“Nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu” (1Tim 1:6).
Kumbe tunahitaji ekaristi mara nyingi, kwa sababu ni chakula cha roho.
“Bwana, sikuzote utupe chakula hiki” (Yoh 6:34).
“Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo” (1Kor 11:26).


Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?

Hapana, si mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote, bali mengine yanahitaji mhudumu wake awe amepewa daraja inayoshirikisha uwezo ambao Yesu aliwapa Mitume wake.
“Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume” (Lk 6:12-13).
“Yesu aliwaambia tena, ‘Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi’. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu’” (Yoh 20:21-22).
Kwa kuwa Waprotestanti hawana sakramenti ya daraja, kati yao zinapatikana sakramenti zile mbili tu zisizohitaji padri, yaani ubatizo na ndoa.


Je, tunapoadhimisha mafumbo hayo tuko peke yetu?

Hapana, tunapoadhimisha mafumbo hayo hatuko peke yetu, bali tunashiriki ibada ambayo Yesu anamtolea Baba milele.
“Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao” (Math 18:20).
Kwa kuungana na Kristo Kichwa, tunaungana na viungo vyote vya Mwili wake, vya duniani, toharani na mbinguni.
“Ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu wa kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili” (Eb 12:22-24).


Je, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu. Yesu aliyesema, “Sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Math 5:17), alifuata kalenda ya dini ya Kiyahudi, halafu kwa kufa na kufufuka amekuwa kiini cha ibada zetu zote. Hivyo Mitume waliadhimisha siku aliyofufuka kama “siku ya Bwana” (Ufu 1:10) ambapo wakutane “ili kumega mkate” (Mdo 20:7) wa ekaristi.
Vilevile kwenye Pasaka hawakuadhimisha tu kazi ya Musa, bali ukumbusho wa Yesu.
“Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo” (1Kor 5:7).
Fumbo hilo ndio moyo wa mwaka wa liturujia, yaani wa mpangilio wa maadhimisho katika mzunguko wa mwaka.
“Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo” (Kol 2:16).


Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali.
“Mungu je, atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!” (1Fal 8:27).
“Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono” (Mdo 17:24).
Hata hivyo sisi watu tunahitaji mahali maalumu kwa matendo yetu mbalimbali, na kumwekea Mungu mahali patakatifu.
“Mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu asema: Ki wapi chumba changu cha wageni, niile Pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu?’ Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni” (Mk 14:14-15).


Hekalu ndiyo nini?

Hekalu ndipo tunapomuendea Mungu kwa ibada. Vilevile sisi wenyewe ni Mahekalu.
Yesu aliheshimu na kutakasa hekalu pekee la taifa lake kama “nyumba ya Baba” yake (Yoh 2:16), lakini alitabiri kuwa litabomolewa moja kwa moja, na kuwa watu watapaswa kuabudu ndani yake aliye hekalu hai. “Wayahudi walisema, ‘Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?’ Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake” (Yoh 2:20-21).
“Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Ef 2:22).
“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi” (1Kor 3:16-17).


Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu kwa sababu tunapaswa kutumia kwa utukufu wake vipawa alivyotujalia, kama vile vya kujenga, kupamba, kuchonga, kuchora na kucheza. Kwa njia hizo tutokeze na kukoleza imani yetu na ya wenzetu.
Mungu “amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi za kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu. Basi, Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye Bwana amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote Bwana aliyoyaagiza” (Kut 35:35-36:1).
“Maskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi!” (Zab 84:1).


Kati ya sanaa kwenye ibada/kumuadhimisha Mungu, muhimu zaidi ni ipi?

Kati ya sanaa, muhimu zaidi ni uimbaji, kwa kuwa unahusiana zaidi na Neno la Mungu, ukilitia maanani kwa uzuri wa muziki. Katika Agano la Kale, kitabu cha Zaburi ni nyimbo tupu za kutumia katika ibada.
“Msifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi! Msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi! Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana!” (Zab 150:3-5).
Agano Jipya pia linatuletea nyimbo nyingi.
“Mjazwe Roho, mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu” (Ef 5:18-19).
Mbinguni washindi wana “vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo” (Ufu 15:2-3).


Kuimba wakati wa ibada ni kazi ya nani?

Kuimba ni kazi ya kusanyiko lote, yaani ya kila mwamini. Kwaya ziimbishe watu wamwadhimishe Mungu, zisiwaimbie tu na kuwanyima nafasi ya kuimba.
“Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote, mtumikieni Bwana kwa furaha, njoni mbele zake kwa kuimba” (Zab 100:1-2).
“Kila kiumbe kilichopo mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, ‘Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwanakondoo, hata milele na milele’” (Ufu 5:13).


Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie nini?

Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie utakatifu na ukweli, si uzuri tu. Zisiigeuze kamwe kuwa igizo wala tamasha, kwa kuwa lengo si kuchangamsha watu bali kumtukuza Mungu.
Ziinue mioyo kwake, zitokeze na kuchangia maisha safi, zilete ujumbe sahihi kadiri ya imani na maadili, kama ilivyo lazima kwa mahubiri na mafundisho.
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu” (Math 15:8-9).


Je, ni halali kuheshimu sanamu?

Ndiyo, ni halali kuheshimu sanamu kama viwakilishi vya Yesu, Mama yake na watakatifu wake, ambao zinaleta sura zao.
Kwa msingi huo walimsihi Yesu “waguse hata pindo la vazi lake tu. Na wote waliogusa wakaponywa kabisa” (Math 14:36).
“Mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote il msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo” (Gal 6:14).


Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu.
“Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki, kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote” (Math 23:27).
“Akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri, kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, ‘Keti wewe hapa mahali pazuri’, na kumwambia yule maskini, ‘Simama wewe pale’, au ‘Keti miguuni pangu’, je, hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?” (Yak 2:2-4).
“Wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani, bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu” (1Tim 2:9-10).
Kanisa si mahali pa mashindano: hatuendi kupendeza watu, ila Mungu.
“Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu?” (1Kor 11:22).


Mbali ya sakramenti, Kanisa linamuadhimisha Mungu vipi?

Mbali ya sakramenti, Kanisa linamuadhimisha Mungu hasa kwa Liturujia ya Vipindi, yaani kwa sala rasmi zinazotolewa mara kadhaa kwa siku, kufuatana na ratiba ya binadamu ya usiku na mchana. Hivyo linajitahidi kutimiza agizo la kusali daima.
“Imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa” (Lk 18:1).
“Kesheni ninyi kila wakati, mkiomba” (Lk 21:36).
“Ombeni bila kukoma, shukuruni kwa kila jambo” (1Thes 5:17).
“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” (Ef 6:18).
“Huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku” (1Tim 5:5).


Kanisa linamuadhimishaje Mungu tena?

Kanisa linamuadhimisha Mungu tena kwa visakramenti ambavyo kwa mamlaka ya Kristo linawatia watu neema zake katika nafasi yoyote ya maisha. Kati yake muhimu zaidi ni baraka na mazinguo, ambavyo vipo tangu zamani, hata nje ya taifa la Israeli.
Melkisedek alisema, “Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako” (Mwa 14:19-20).
Farao aliomba, “Mkanibariki mimi pia” (Kut 12:32).
Balaam alisifiwa, “Najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa” (Hes 22:6).
“Ikawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwacha” (1Sam 16:23).
“Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je, wana wenu huwatoa kwa nani?” (Math 12:27).


Maana ya baraka ni ipi?

Maana ya baraka ni kumsifu Mungu kwa yale aliyokwishatujalia na kumuomba azidi kutujalia kadiri ya mahitaji ya wahusika. Mara nyingi inatolewa na mtu mwenye daraja au mamlaka fulani.
Yesu aliletewa “watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea” (Math 19:13).
Siku ya kupaa mbinguni “aliinua mikono yake akawabariki” (Lk 24:50).
“Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao” (Mdo 13:3).
Pengine vinabarikiwa vitu vinavyotumiwa na watu, au mahali wanapoishi.
“Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano” (Lk 9:16).


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
“Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu” (Mk 5:8).
“Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!” (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
“Aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” (Mk 6:7).
“Paulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, ‘Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu’. Akamtoka saa ileile” (Mdo 16:18).


Je, ni halali kwa Wakristo kujitungia ibada nyingine?

Ndiyo, ni halali kwa Wakristo kujitungia ibada nyingine, mradi wakubali zipimwe na Maaskofu kama zinalingana na imani, maadili na taratibu za Kanisa.
“Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure… Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu” (Kol 2:18,23).
“Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao” (2Tim 3:14).


Ni halali kujitungia ibada kwa sababu gani?

Ni halali kujitungia ibada kwa sababu sala ni hasa maongezi ya Mungu na mtu.
Adamu na Eva “walisikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga” (Mwa 3:8).
Yeye hachoki kumvuta kila mmojawetu kwake na kumtia hamu ya kumhimidi na kumuabudu, kumuomba kwa ajili yake na ya wengine, kumshukuru na kumsifu.
“Ee Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yako” (Zab 143:1).
Hata tukisali pamoja, uhusiano wa kila mmojawetu na Mungu ni wa pekee. Tusiposali kwa moyo, ibada ni ya bure.
“Watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami” (Isa 29:13).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
“Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia” (1Sam 3:10).
“Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku” (Zab 63:6).
“Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zab 119:97).
“Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu” (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, ‘Bwana, tufundishe sisi kusali” (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
“Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yoh 17:1).
“Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
“Wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu” (Lk 2:41-42).
“Saa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, ‘Eloi, Eloi, lama sabakthani?’” (Mk 15:34).
“Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Lk 23:46).
Shopping Cart
24
    24
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About