Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya choroko

Mahitaji

Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima

Matayarisho

Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.

Jinsi ya kutengeneza Nangatai

MAHITAJI

Unga wa ngano – 2 – 2 ยผ Vikombe

Siagi – 1 ยฝ Kikombe

Sukari – 1 Kikombe

Yai – 1

Vanilla -Tone moja

Baking Powder -kijiko 1 cha chai

Chumvi – Kiasi kidogo (pinch)

Unga wa Kastadi – 2 Vijiko vya supu

MATAYARISHO

Changanya vitu vyote isipokuwa unga.
Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa.
Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati.
Halafu zichome katika moto wa 300ยฐF kwa muda wa dakika 20 – 25 na zisiwe browni .
Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.

Jinsi ya kutengeneza Bisikuti Za Kaukau Na Kahawa (Cocoa Coffee Biscuits)

MAHITAJI

Maji baridi โ€“ kikombe 1

Biskuti za kawaida โ€“ paketi 2

Kaukau (cocoa) โ€“ vijiko 3 vya kulia

Kahawa ya unga โ€“ kijiko 1 cha kulia

Njugu mchanganyiko zilokatwakatwa โ€“ kikombe 1

Sukari โ€“ kiasi upendavyo

MAANDALIZI

Changanya maji na kaukau na kofi na sukari
Katakata biskuti kisha tia paketi moja na nusu uchanganye vizuri.
Kisha nusu ya biskuti zilobakia katakata vipande vikubwa na weka juu ya mchanganyiko, kisha changanya kidogo tu.
Weka katika foil paper na zungusha (roll)
Kisha fungua umwagie njugu au mkassaraat zilosagwa
Kisha roll katika foil paper na uweke katika freezer mpaka igande
Kisha kata kata slices na iko tayari

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu.
Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.

Hivyo basi kwa vyovyote vile unahitaji mtu wa kukuongoza au kuku Coach ili ufanikiwe katika pande zote za maisha.

Nitakwenda kuzungumzia sehemu kuu tatu za muhimu sana ambazo unatakiwa uwe na watu wa kukuongoza ili uweze kukua na kupanda viwango kila wakati.

Ni vitu vya kawaida sana lakini leo nitakwenda kuzungumzia uone ilivyo muhimu sana wewe kua na vitu hivi maana bila vitu hivi mafanikio yatakua magumu sana kufikia. Safari yako itakua ngumu zaidi kama utakosea sehemu hizi tatu.

Nitaomba tuelewane kwamba hapa huendi kuiga au kuwa hawa watu utakua wewe na utatimiza lile kusudi la Mungu ndani yako.

Kwanza kabisa uko hivyo ulivyo kwa sababu ya mazingira uliyokulia na watu ulioishi nao tangu ukiwa mtoto hadi hapo ulipo.

Kuna tabia nyingi sana unazo kutokana na mazingira uliyokulia.

(Hapa ndipo nakutana na kitu ambacho nakipenda sana kujifunza kwa wengine napenda kujifunza kwenye mazingira mapya na kwa watu wapya kwa kua wameishi maisha ambayo mimi siyajui na wanafahamu vitu vingi ambavyo mimi sifahamu. Watu wana utajiri mwingi sana ndani yao ukiweza kukaa na mtu ambaye humjui kabisa unaweza kujifunza mambo mengi ya ajabu kwake. )

Hawa ndio watu wa Muhimu sana kwenye safari yako usiwakose ili uweze kusonga mbele.

Sifa zao kabla hujawachagua ni za muhimu sana pia ili wasije wakakupoteza badala ya kukufikisha kule unakotaka kwenda.

(a)Awe na mafanikio (Amefika Mbali) kwenye hiyo sehemu.

(b)Awe na Tabia njema zinazokubalika na jamii yake na dini yake. (mfano hapa ukikutana na mtu ambaye anakuelekeza kuhusu biashara na ni mlevi na mzinzi hizi tabia lazima atakuambukiza kwasababu atakua mtu wako wa karibu sana)

(c)Awe amekuzidi sana kwenye kile unachotaka akulelee (akuongoze).

Hizo ni sifa za muhimu tu za kuangalia zipo nyingine nyingi sana utajifunza mwenyewe.

1. Mlezi wako wa Kiroho

Huyu ni mtu wa muhimu sana na nimemweka wa kwanza.

Bila roho hakuna mwili.

Bila roho mwili wako unakua umekufa.

Unahitaji ukue kiroho na upande viwango kila wakati ili uweze kuvutia mafanikio ya nje.

Ukishindwa hapa hata ukiwa bilionaire inaweza kuwa kazi bure.

Hutaweza kuzifurahia hizo pesa.

Tafuta mtu wa kukulelea kiroho.

Mtu wa kukufundisha kumcha Mungu.

Kama huna katafute mtu wa kukulea kiroho sifa nimezitaja hapo juu.

Mtu huyu anatakiwa akufahamu vizuri na wewe umfahamu vizuri.

Yaani muwe na mahusiano ya karibu sana.

Mtu huyu awe anafuatilia maendeleo yako ya kiroho kwa karibu sana.

Haijalishi uko Dini gani lazima umpate mlezi wa roho yako.

Dini ndio inahusika kulisha roho zetu.
Ndio maana hatufundishwi biashara kule.

2. Mlezi wa Mahusiano/Uchumba/Ndoa

Hapa ni kwa muhimu sana.

Ukiwa vizuri kiroho mahusiano yakawa na tatizo hutafika mbali.

Ukiwa vizuri kiroho ndoa ikasumbua nayo ni tatizo.

Tafuta mtu wa kukulea kwa upande huu pia mtu aliefika mbele zaidi yako.

Aliefanikiwa zaidi yako.

Kama unatafuta mchumba tafuta mtu aliye kwenye ndoa na amefanikiwa.

Ukimtafuta single mwenzako atakupoteza๐Ÿ˜€.

Mtu huyu awe karibu yenu kabisa kulea mahusiano/ uchumba au ndoa yenu.

Hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu tunajifunza hapa duniani kwa waliotutangulia na waliopo pia.

3. Mlezi wa Maono yako/Ndoto zako/Malengo yako/Biashara Yako/Pesa. (Coacher).

Mtu huyu ni wa muhimu pia katika maisha yako.

Unataka kumiliki utajiri wa dollar billion moja lazima utafute mtu wa kukulelea na kukuwezesha ufikie huko.

Huwezi kwenda mwenyewe.

Unahitaji mtu wa kukuongoza kwenye kila unachotaka kukifanya.

Wengi wanakata tamaa kwa kua hawana watu hawa wa kuwalelea.

Mtu huyu anatakiwa awe anakufuatilia hatua kwa hatua kwenye kile unachokifanya.

Awe anapata taarifa za maendeleo yako kila wakati ikiwezekana hata kila week.

Ukipata mafanikio yeyote ajue pia ukipata changamoto ajue.

Mtu huyu anatakiwa awe amekupita kwenye kile unachokitaka na hapa huendi kuwa Follower,anakwenda kukutengeneza wewe uwe kiongozi.

Uweze kusimama mwenyewe na hatimae uongoze wengine.

Kwa Tanzania wapo watu wanaofanya kazi hizi kwa malipo pia.

Lakini hapa unaweza kuanza na mtu ambaye una mahusiano nae ya karibu awe anakulelea.

Siku hizi teknolojia imekua rahisi sana unaweza kuwa na mawasiliano na mtu yeyote unayemtaka popote alipo duniani.

Unaweza kujifunza pia vitu vingi sana kupitia mitandao hii kama hapa facebook.

Unaweza kusoma vitabu na vitu vingi sana vile unavyovitaka.

Naomba nimalizie kwa kusema kwamba.
Kwa hiki ulichokipata leo ukikifanyia kazi.

Utakua mshindi uliyezaliwa kuwa.

Utafikia Hatma yako kwa kufuata haya, namaanisha wewe uliyesoma hapa.

I will see you at the top!

Mapishi ya Kabichi

Mahitaji

Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.

Mapishi โ€“ Saladi ya Matunda

Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora. Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula kizuri sana.

Mahitaji

Embe iliyoiva kiasi
Nanasi
Tango
Tikiti maji
Zabibu
Papai

Matayarisho

1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba

2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.

3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo

4. Saladi yako tayari kwa kuliwa

Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Mafundisho ya Msingi kuhusu Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni nini?

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu

Majina mengine ya Roho Mtakatifu ni yapi?

Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji wa kweli, Roho wa Bwana, Roho wa Kristu

Ni alama zipi zinawakilisha Roho Mtakatifu?

Alama zinazowakilisha Roho Mtakatifu ni hizi; Maji, Mpako wa mafuta, Moto, wingu, tendo la kuweka mikono, njiwa

Neno Manabii maana yake ni nini?

Neno Manabii maana yake ni waliovuviwa na Roho Mtakatifu waseme kwa jina la Mungu

Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku gani?

Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku ya Pentekoste, yaani siku ya hamsini toka Pasaka. (Mdo 2:1-4)

Roho Mtakatifu aliwafanyia nini Mitume?

Roho Mtakatifu aliwatia Mitume Mwanga wa nguvu ili waweze kuhubiri Injili na kueneza Kanisa kote duniani

Roho Mtakatifu anatufanyia nini sisi Wakristo?

Roho Mtakatifu anatufanyia haya;
1. Anatuangaza tufahamu mafundisho ya dini
2. Anatuimarisha tutende mema na kuacha mabaya
3. Anatutakasa na kutututia uzima rohoni mwetu
4. Analiongoza Kanisa. (Yoh 16:13-15)

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa namna gani?

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa;
1. Neema ya utakaso
2. Fadhila za Kimungu na vipaji vyake

Maandiko Matakatifu ndiyo nini?

Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la โ€œBibliaโ€, yaani โ€œVitabuโ€.
Hao โ€œwanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifuโ€ (2Pet 1:21).

Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana.
โ€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisiโ€ (Rom 5:5).
Ametumwa kwetu atufanyie kazi pasipo kuonekana.
โ€œUpepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Rohoโ€ (Yoh 3:8).
โ€œWote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Munguโ€ (Rom 8:14).

Je, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu?

Ndiyo, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu na kulenga hasa kuandaa watu wampokee, wamfuate na kumshuhudia katika umoja wa kundi lake, Kanisa.
โ€œAjapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. Nanyi pia mnashuhudiaโ€ (Yoh 15:26-27).

Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake nini?

Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake ni kuja kuongozwa naye badala ya kutawaliwa na shetani.
โ€œKwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwetu, aliaye, โ€˜Aba!โ€™ yaani, โ€˜Baba!โ€™ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miunguโ€ฆ Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Rohoโ€ (Gal 4:6-8; 5:25).
โ€œIkiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wakeโ€ (Rom 8:9).

Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia nini?

Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia adili kuu la upendo:
โ€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisiโ€ (Rom 5:5).
Tena tunapokea vipaji vyake ambavyo Yesu alikuwa navyo kikamilifu.
โ€œRoho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana. Na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwanaโ€ (Isa 11:2-3).
Mambo hayo, tofauti na karama, ni ya lazima kwa yeyote apate wokovu wa milele.

Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?

Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo.
โ€œWengi wataniambia siku ile: Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovuโ€ (Math 7:22-23).
โ€œNijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kituโ€ (1Kor 13:1-3).

Je, karama ni zile za kushangaza tu?

Hapana, karama si zile za kushangaza tu, tena zile muhimu zaidi si hizo, bali zile zinazojenga zaidi Kanisa, kama zile za uongozi:
โ€œMungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lughaโ€ (1Kor 12:28).
โ€œBasi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furahaโ€ (Rom 12:6-8).

Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kufanya nini?

Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kuishi kwa useja kama Yesu na Paulo, au kwa ndoa:
โ€œNipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane; ni heri wakae kama mimi nilivyoโ€ (1Kor 7:7-8).
โ€œSi wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwaโ€ (Math 19:11).
Tunavyoona katika historia ya watawa, mara nyingi karama ya useja inaendana na nyingine katika maisha ya sala, ya kijumuia na ya kitume. Hivyo Filipo โ€œalikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiriโ€ (Mdo 21:9).

Karama zinagawiwa vipi?

Karama zinagawiwa na Roho Mtakatifu jinsi anavyotaka, si kwa sifa au faida ya binafsi, bali kwa ustawi wa taifa la Mungu.
โ€œKazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeyeโ€ฆ Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?โ€ฆ Kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisaโ€ฆ Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amaniโ€ (1Kor 12:11,29-30; 14:12,33). Kwa ajili hiyo mitume walipambanua na kuratibu karama katika ibada na katika maisha ya jumuia zisije zikavuruga Kanisa.

Karama za kushangaza zina hatari gani?

Karama za kushangaza zina hatari mbalimbali, hasa zikitiwa maanani mno. Hapo ni rahisi zilete majivuno, kijicho na mafarakano.
โ€œIkiwa kwenu kuna husuda na fitina, je, si watu wa tabia ya mwili ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?โ€ฆ Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemilikiโ€ฆ Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asiangukeโ€ (1Kor 3:3; 4:8; 10:12).
Katika mambo yasiyothibitika ni rahisi kudanganyika kuwa yametoka kwa Mungu, kumbe sivyo. Kisha kudanganyika ni vigumu kuachana nayo hata yakiwa na madhara kwa mhusika au kwa Kanisa.
โ€œWapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea dunianiโ€ (1Yoh 4:1).

Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni lipi?

Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni umoja wa Kanisa unaotokana na ustawi wa upendo na vipaji ndani ya waamini.
โ€œWote walijaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho mojaโ€ (Mdo 4:31-32).
โ€œTunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheriaโ€ (Gal 5:22-23).
โ€œLakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi; tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafikiโ€ (Yak 3:14-17).
Madhehebu yanapozidi kufarakana ni lazima tujiulize kama kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
โ€œMungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, โ€˜Aba!โ€™ yaani, โ€˜Baba!โ€™โ€ (Gal 4:6).
โ€œRoho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwaโ€ฆ huwaombea watakatifu kama apendavyo Munguโ€ (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, โ€˜Njoo, Roho Mtakatifu!โ€™ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
โ€œYeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Munguโ€ (Ef 3:16-19).
โ€œHuyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yoteโ€ (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.

Sakramenti ya Kipaimara ni nini?

Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa

Nini maana ya Roho Mtakatifu?

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26)

Je, Roho Mtakatifu Katika mfano wa ndimi za Moto Maana yake nini?

Maana yake ni kupata nguvu ya Kuhubiri Injili, Neno la Mungu linalopenya kwenye Moyo Kama Moto.

Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini nini?

Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini haya.
1. Anawatakasa
2. Anawaangaza na kuwavuta ili waende kwenye uzima wa milele

Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu Anatutakasa?

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa njia ya Sakramenti, Visakramenti, Fadhila za Kimungu na vipaji vyake. (Yoh 16:8)

Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anatenda kazi zake?

Roho Mtakatifu anatenda kazi zake kwa njia hizi;
1. Anatuangaza kwa Mwanga wake tupate kuelewa mafundisho ya dini
2. Anatupatia neema za msaada za kutusaidia kutunza utakatifu wetu
3. Anatuvuta kwa mapendo yake tuzitumie Neema na kufika kwenye uzima wa milele.
4. Anatufariji katika shida zote. Ndio maana Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji

Kwa nini Sakramenti hii inaitwa Kipaimara?

Inaitwa Sakramenti ya Kipaimara kwa sababu inaimarisha na kukamilisha neema ya Ubatizo

Roho Mtakatifu anakuja kufanya nini rohoni mwetu kwa Kipaimara?

Anakuja kufanya yafuatayo;
1. Anakuja kutuongezea Neema ya Utakaso
2. Anatuletea pia ukamilifu wa mapaji yake saba na msaada wa kuungama imani yetu mbele za watu

Mapaji Saba ya Roho Mtakatifu ndio nini?

Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni msaada wake wa kuimarisha na kuzoesha akili na moyo wetu kwa mambo ya utumishi wa Mungu

Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni yapi?

Mapaji Hayo ni;
1. Hekima
2. Akili
3. Shauuri
4. Nguvu
5. Elimu
6. Ibada
7. Uchaji wa Mungu (Isaya 11:2)

Hekima ni nini?

Ni upendaji wa Mambo ya Mungu na Machukio ya Mambo ya Dunia

Akili ni nini?

Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu

Shauri ni nini?

Ni utaratibu wa Kuchagua Siku zote mambo yenye kufaa kwa sifs ya Mungu na kwa Wokovu wetu

Nguvu ni nini?

Ni moyo wa kushika sana Amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu, matukano, mateso wala kufa. (Rum 8:38-39)

Elimu ni nini?

Ni maarifa ya kutambua werevu na udanganyifu wa shetani; anaposhawishi mwenyewe au kwa kutumia vitu au watu. (1Pet 5:8-9)

Ibada ni nini?

Ni roho ya kupenda utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na Heshima

Uchaji wa Mungu ni nini?

Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake.

Roho Mtakatifu hutajwa wapi katika Rozari?

Roho Mtakatifu hutajwa katika fungu la tatu la Matendo ya Utukufu tusemapo; Aliyepeleka Roho Mtakatatifu. (Mdo 2:1-4)

Kabla ya Kupaa mbinguni Yesu aliwaahidi nini Mitume?

Kabla ya kupaa mbinguni Yesu aliwaahidia Mitume kuwapelekea Roho Mtakatifu; ndiye nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu. (Yoh 16:7)

Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Matunda ya kuongozwa na Roho Mtakatifu ni yapi?

Matunda ya Roho Mtakatifu ni;
1. Upendo
2. Furaha
3. Amani
4. Uaminifu
5. Uvumilivu
6. Utu wema
7. Fadhila
8. Upole
9. Kiasi
(Wagalatia 5:22, 23)

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.

Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.

Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.

Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?

Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.

Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?

Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.

Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?

Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.

Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia

Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hiviโ€ฆโ€Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.โ€โ€ฆKwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.

Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?

Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.

Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu

Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.

Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?

Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..โ€Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu โ€œโ€ฆ
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

Jinsi ya kuandaa biskuti za Siagi Na Jam

MAHITAJI

Unga – 2 Vikombe
Sukari ya icing – 1 Kikombe
Siagi – 250 gm
Yai – 1
Vanilla – 2 Vijiko vya chai
Baking powder -1 Kijiko cha chai
Jam – ยผ kikombe
Lozi – ยผ kikombe

JINSI YA KUPIKA

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi.
Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia.
Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa.
Pika (bake) katika oven moto wa 375ยฐ F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama

Mambo makubwa yanayosababisha kulazimika kulima au kutifua udongo

Kutifua udongo ni jambo la muhimu sana ili kuufanya udongo kuwa bora.

Umuhimu wa kutifua udongo ni kama ifuatavyo
1. Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
2. Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.
3. Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
4. Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
5. Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
6. Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia limau au limao

Dawa nyingine nzuri kwa ajili ya chunusi usoni na mwilini ni limau. Limau linajitokeza kwenye vyakula vingi tunavyokula kila siku mathalani limau halikosekani pakiwepo supu au mapishi yoyote ya samaki.

Limau lina kiasi kingi cha vitamini C ambayo inaweza kutumika kama antibiotiki inayozuia kuongezeka na kukua kwa bakteria wanaosababisha chunusi.

Limau pia ina tindikali maalumu inayohamasisha chunusi kutoka katika ngozi.

Unachotakiwa kufanya ni kukata limau pande mbili au nne na upake majimaji yake moja kwa moja kwenye chunusi pole pole kwa dakika 10 hivi kasha jisafishe na maji safi.

Tindikali katika limau inaweza kuzidhuru seli zilizopo juu ya ngozi yako hivyo tumia dawa hii mara 1 au 2 tu kwa wiki na siyo kila siku.

Vitamini C iliyomo kwenye limau husaidia kukinga mwili dhidi ya magonjwa mengi sababu ndiyo vitamini inayosaidia kuongeza kinga ya mwili.

Kinga ni bora kuliko tiba!

Hivyo tumia vitamini C mara kwa mara au kunywa juisi ya limau kila siku ili kuweka mwili wako katika afya bora zaidi muda wote.

Jinsi ya kupika Keki Ya Maboga

Viamba upishi

Unga wa ngano vikombe vikubwa 3
Boga lililopondwa kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Sukari kikombe kikubwa 1
Blue band kikombe ยฝ
Vanilla kijiko kidogo 1
Mayai 2
Maji kiasi/ maziwa
(kama nilazima)

Hatua

โ€ข Osha boga, Kata, ondoa mbegu, kisha kata vipande vikubwa, chemsha na maji mpaka vilainike.
โ€ข Kwangua boga la ndani ukiacha maganda na ponda sawasawa.
โ€ข Chekecha unga (kila kikombe 1, vijiko vidogo 2 vya baking powder) kwenye bakuli kubwa.
โ€ข Ongeza blue band na changanya sawasawa na vidole.
โ€ข Ongeza sukari na changanya.
โ€ข Ongeza mayai na koroga na mwiko.
โ€ข Ongeza boga lililopondwa na koroga njia moja mpaka ilainike.
โ€ข (Kama haikulainika ongeza yai /mayai au maziwa/ maji kidogo).
โ€ข Ongeza vanilla na koroga.
โ€ข Paka mafuta chombo cha kuokea au sufuria kisha chekecha unga kidogo wa ngano.
โ€ข Mimina rojo la keki kwenye sufuria au chombo cha kuokea.
โ€ข Oka kwenye oven au tumia sufuria na weka mkaa wa moto juu na chini moto kidogo mpaka iive.
โ€ข Jaribu kuchoma kisu katikati, kama ni kavu keki imeiva, epua, pozesha kata tayari kwa kula, kama kitafunio.

Dondoo muhimu za afya

Tafadhali soma na uwapelekee wengine.

Dr. Chriss Mosby wa Tanzania amegundua kensa mpya kwa binadamu inayosababishwa na Silver Nitro Oxide. Unaponunua kadi ya simu usiichune kwa kucha kwani imo hiyo Silver Nitro Oxide na inaweza kusababisha kensa ya ngozi. Watumie ujumbe huu wale uwapendao.

Nukuu muhimu za afya

  • sikiliza simu kwa sikio la kushoto.
  • usimeze dawa na maji baridi
  • usile chakula kizito baada ya saa kumi na moja jioni.
  • kunywa maji mengi asubuhi na kidogo usiku.
  • wakati mzuri wa kulala ni kuanzia saa nne hadi kumi usiku. usilale mara baada ya kula dawa au chakula.
  • ikiwa chagi imebakia kijino cha mwisho usipokee simu kwani mionzi inakuwa na nguvu kwa mara 1000 zaidi.

unaweza kuwatumia haya wale unaowajali?
Mie nimeshafanya.
Huruma haigharimu kitu lakini elimu ni nuru.

MUHIMU
Jumuiya ya uchunguzi ya marekani imetoa majibu mapya. Usinywe chai kwenye vikombe vya plastic. Na usile Chochote kwenye mifuko ya plastic. Plastic ikikutana na joto inatoa vitu vinavyo sababisha aina 52 za kensa. Kwa hiyo ujumbe huu ni bora kuliko mijumbe 100 isiyo na maana. Tafadhali wapelekee unaowajali.

Mapishi ya Viazi, samaki na asparagus

Mahitaji

Viazi (potato 1/2 kilo)
Samaki (fish 2)
Asparagus 8
Kitunguu kilichokatwa (chopped onion 1)
Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic 4 cloves)
Tangawizi iliyosagwa kiasi (ginger paste)
Limao (lemon 1)
Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander)
Curry powder (kijiko 1 cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Safisha samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About