Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya Biriani Ya Kuku Wa Kuchoma (Grilled)

Mahitaji

Mchele wa Basmati /Pishori – 4 vikombe

Kuku

Vitunguu – 3

Nyanya/Tungule – 2

Tangawizi mbichi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi nzima – 3

Ndimu – 2

Garama Masala/bizari mchanganyiko – 1 kijiko cha supu

Haldi/tumeric/bizari manjano – 1 kijiko cha chai

Pilipilu ya unga nyekundu – 1 kijiko cha chai

Mtindi /yoghurt – 3 vijiko vya supu

Mafuta ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele, roweka.
Safisha kuku vizuri, mkate vipande vya saizi ya kiasi weka katika bakuli.
Katika kibakuli kidogo, changanya tangawizi mbichi, thomu, bizari zote, pilipili nyekundu ya unga, chumvi, mtindi, kamulia ndimu.
Punguza mchanganyiko kidogo weka kando.
Mchanganyiko uliobakia, tia katika bakuli la kuku uchanganye vizuri arowanike (marinate) kwa dakika chache hata nusu saa au zaidi.
Weka kuku katika treya ya kuoka au kuchoma katika oveni kisha mchome (grill) uwe unageuzageuza hadi aive.
Epua, weka kando.
Katakata vitunguu, nyanya/tungule, pilipili boga weka kando.
Katika sufuria ya kupikia biriani, tia mafuta, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Tia nyanya na pilipili mbichi, pilipili boga na mchanganyiko uliopunguza awali.
Tia kuku uchaganye vizuri.
Wakati unakaanga vitunguu ili uokoe muda, huku chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji, chuja.
Punguza masala nusu yake weka kando.
Mimina wali kiasi juu ya masala, kisha mimina masala yaliyobakia kisha juu yake tena mimina wali.
Funika upike katika oveni hadi uive.
Changanya unapopakua katika sahani.

Jinsi ya kupika Biskuti Za Ufuta Na Jam

Viamba upishi

Unga 2 Viwili

Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe

Siagi 250 gms

Jam kisia

Ufuta Kisia

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Tia kwenye mashine ya kusaga (blender) au mashine ya keki, siagi, yai, sukari na vanilla uchanganye hadi ichanganyike vizuri.

2. Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.

3. Paka siagi sinia ya kupikia ya oveni.

4. Tengeneza viduara vidogo vidogo.

5. Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unynyuzie ufuta.

6. Pika katika moto wa chini 350ºF kwa muda wa dakika 20-25.

7. Tayari kwa kuliwa.

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂

Mapishi ya Biriani Ya Tuna

MAHITAJI

Mchele Basmati – Mugs 2 ½

Vitunguu (Vikubwa kiasi) – 3

Tuna – Vibati 3

Carrot – 2 kubwa

Tomatoe paste – 1 kikopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 2 Vijiko vya supu

Tangawizi – 2 Vijiko vya supu

Uzile (Bizari ya pilau ya unga) (cummin powder )

(Jeera) – ½ Kijiko cha supu

Mdalasini – ½ Kijiko Cha supu

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Tuna carrots (grate) ziwe kama chicha weka kando.

Kaanga vitunguu 2 mpaka viwe brown weka pembeni.

Kaanga Kitunguu cha 3 halafu changanya na tangawizi, thomu, na tuna huku unakoroga.

Changanya na tomatoe, uzile (cummin powder) na mdalasini, koroga vizuri (hakikisha umeweka mtoto mdogo mdogo kwani ni rahisi kuungua)

Ikiwiva epua weka pembeni.

Chemsha wali wako kwa maji mengi na uuchuje kabla haujawiva vizuri na uugawe sehemu

Chukua trey au sufuria ambayo itaweza kuingia vitu vyote uilivyoandaa, tandaza fungu la kwanza la wali halafu utandaze carrot juu yake.

Tandaza fungu la pili la wali halafu utandaze vitunguu juu yake.

Tandaza fungu la tatu la wali halafu utandaze tuna (masalo) juu yake.

Mwisho tandaza fungu la nne la wali, ufunike vizuri na upike kwenye oven (bake) 350 Deg C kwa muda wa dakika 20

Epua ikiwa tayari kuliwa

Mapishi ya Chicken Curry

Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).

Mahitaji

Kuku mzima
Nyanya kubwa 3
Karoti mbili
Pilipili hoho
Kotmiri
Tangawizi
Kitunguu maji
Kitunguu saumu kidogo
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Chumvi (pilipili ukipenda)

Matayarisho

1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja.
2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu).
3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni.
4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni.
5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni.
6. Andaa kikaango na jiko.

Mapishi

1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui).
2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi.
3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana.
4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.

AHADI 15 ZA ROZARI TAKATIFU

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.

1. Yeyote yule atakayesali kwa imani rozari hii takatifu atapokea neema kuu zenye nguvu
2. Naahidi ulinzi wa kipekee na neema za kipekee kwa yule atakayesali rozari hii
3. Rozari itakuwa silaha kubwa dhidi ya nguvu za kuzimu, itaharibu maovu, itapunguza dhambi na kushinda kutofautiana
4. Itafanya fadhila kukua, kazi nzuri kuongezeka, itapatia roho huruma tele toka kwa MUNGU, itaondoa hamu ya wanadamu kupenda mambo ya dunia na majivuno yake na kufanya wapende zaidi mambo ya mbinguni. Ooh, ni kwa namna gani roho hizo zitajifurahisha na kubarikiwa kwa namna hii.
5. Roho zitakazojikabidhi kwangu kwa njia ya kusali rozari, kamwe hazitapotea.
6. Yeyote atakayesali rozari kwa uaminifu huku akiyatafakari matendo makuu ya rozari, kamwe hatashindwa na ubaya. MUNGU hatamwadhibu katika hukumu yake, hatapotea katika kifo asichopangiwa na atabaki katika neema za MUNGU na kustahili kupata uzima wa milele.
7. Yeyote atakayekuwa mwaminifu katika kusali rozari, kamwe hatakufa bila ya kupokea Sakramenti takatifu za Kanisa.
8. Wote watakaokuwa waaminifu katika kusali rozari watadumu katika mwanga wa MUNGU katika maisha yao na saa yao ya kufa na kupata neema zake tele; katika saa yao ya kufa watashiriki fadhila za watakatifu waliopo peponi
9. Nitawatoa toharani wale wote waliokuwa waaminifu katika kusali rozari
10. Watoto wangu waaminifu katika kusali rozari watapata fadhila kuu ya utukufu Mbinguni.
11. Utapata yale yote unayoniomba kwa kusali rozari
12. Wote wale wanaoeneza rozari hii takatifu nitawasaidia katika mahitaji yao
13. Nimepata toka kwa mwanangu Mtukufu kuwa mawakili wote wa rozari takatifu watapata
waombezi toka baraza lote kuu la Mbinguni wakati wa maisha yao na wakati wa saa yao ya kufa.
14. Wote wanaosali rozari hii takatifu ni wanangu, na kaka na dada wa mwanangu wa pekee YESU KRISTO
15. Ibada kwa rozari takatifu ni ishara kuu ya kuelekea ukombozi

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.

Chemsha maji kwenye sufuria jikoni funika na uache nafasi kidgo ya mvuke uwe unatoka, kisha chukua taulo na ujifunike usoni huku ukisogelea karibu na mvuke unapokea na uruhusu mvuke huo ukupate kwa mbali.

Baki hapo kwa dakika 5 mpaka 10 hivi huku ukiwa umetulia (relaxed). Huu mvuke utakusaidia pia kujisikia mtulivu na kukuondolea mfadhaiko wa akili.

Mwishoni mwa zoezi jisafishe uso wako na maji ya baridi.

Endelea kusoma makala hii kujifunza zaidi dawa nyingine za asili za kutibu chunusi.

Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Unapotokwa na damu puani fanya yafuatayo;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusimama itakusaidi kupunguza kasi na presha katika mishipa ya damu puani wakati unapoinamisha kichwa kwa mbele huzuia kumeza damu ambayo italeta shida tumboni.

2. Weka pamba au kitambaa chenye uwezo wa kufyonza damu nje ya pua na bana pua kwa muda wa dakika 15 huku ukitumia mdomo kupumua, kubana pua hurudisha damu katika mishipa ya pua na kuzuia kuvuja.

3. Kuzuia damu isitoke tena usichokonoe pua wala kuinamisha kichwa mbele kwa nguvu na kwa muda mrefu.

4. Kama damu inaendelea kutoka bana pua kwa kutumia kitambaa chenye ubaridi au barafu itasaidia kusinyaa kwa mishipa ya damu na kuzuia damu.

5. Nenda hosipitali kama damu puani inatoka na kuumia kichwani, haijakata kwa muda wa dakika 20 na kama pua imeumia au kuvunjika

KUMBUKA: Kutokwa na damu puani ni jambo la kawaida sana kwa kila mtu na mara nyingi huwa sio hatari sana isipokuwa kama linaambatana na dalili nyingine hatari. Tatizo ili huweza kusababishwa na kuumia ndani au nje ya pua, kuchokonoa pua mara kwa mara, shinikizo la damu, matumizi dawa za aspirini, ukosefu wa vitamini K, pombe kupita kiasi, na mabadiliko ya hormoni kwa wajawazito

Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-

Kwako muajiriwa

👉🏿Umeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko “busy” kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko “busy”??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???

👉🏿Umeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??

Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??

Kwako wewe uliyejiajiri

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??

👉🏿Kwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??

👉🏿Kwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??

👉🏿Kwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??

👉🏿Kwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???

👉🏿Kwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??

👉🏿Ni watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??

👉🏿Wangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??

👉🏿Kwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??

👉🏿Kwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?

👉🏿Kwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??

Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia Uwatu (Fenugreek)

Uwatu ni dawa nyingine ya asili inayotumika kutibu chunusi. Uwatu unaondoa sumu na maambukizi mbalimbali.

Hizi ni hatua chache za kutibu chunusi kwa kutumia uwatu

a)Chukua kijiko kidogo cha unga wa mbegu za uwatu
b)Ongeza maji kidogo kupata uji mzito (paste)
c)Pakaa mchanganyiko huu sehemu yenye chunusi
d)Acha kwa dakika 20 au kwa usiku mzima
e)Kisha jisafishe a maji safi
f)Fanya zoezi hili mara 2 au 3 kwa wiki

Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka

Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C, magnesiamu na potasiamu, vilevile dawa hii husaidia kuweka sawa akili na kuondoa msongo wa mawazo (stress).

Matumizi

  1. Chukua majani 10 mpaka 15 ya mrehani mbichi
  2. Saga au twanga kupata maji maji yake (juisi).
  3. Weka asali kijiko kidogo kimoja ndani yake.
  4. Kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa tupu.

Vile vile unaweza kutafuna tu moja kwa moja majani kadhaa ya mrehani kila siku asubuhi.

Namna ya kutunza kuku na kuwakinga na magonjwa

1. Zingatia chanjo muhimu kwa kuku ili kuzuia magonjwa kama utakavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo.
Chanjo huanza katika wiki ya kwanza (mfano chanjo ya kuzuia sotoka) na inaweza kurudiwa baadaye.

2. Epuka kuweka kuku wengi mahali pamoja.
Ni rahisi magonjwa kuenea kwa haraka kuku wanaporundikana.

3. Kumbuka kutenganisha vifaranga na kuku wakubwa (isipokuwa kutoka kwa mama) kwa sababu vifaranga ni rahisi na wepesi sana kushambuliwa na magonjwa.

4. Hakikisha unaweka mipaka na madaraja ya sehemu za kuku kuzunguka/kucheza.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About