Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-
Kwako muajiriwa
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko “busy” kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko “busy”??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??
Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??
Kwako wewe uliyejiajiri
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??
๐๐ฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??
๐๐ฟKwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??
๐๐ฟKwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??
๐๐ฟKwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??
๐๐ฟKwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???
๐๐ฟKwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??
๐๐ฟNi watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??
๐๐ฟWangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??
๐๐ฟKwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??
๐๐ฟKwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?
๐๐ฟKwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??
Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE