Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Maswali na Majibu kuhusu Ufufuko wa wafu

Ufufuko wa wafu maana yake nini?

Ufufuko wa wafu maana yake mwisho wa dunia watu wote watafufuka na miili yao na kwenda nayo katika furaha ya milele au moto wa milele. (Ayu 19:25-26, Mt 22:30-32, Yh 28-29)


Mbinguni ni mahali pa namna gani?

Mbinguni ni makao mema ya heri na furaha (2Kor 5:1, Ufu, 2:17).
Waendao mbinguni ni wale wanaokufa katika hali ya neema ya utakaso na urafiki na Mungu na waliotakaswa kikamilifu


Motoni ni nini?

Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15)


Uzima wa milele ni nini?

Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho.


Toharani ni mahali gani?

Toharani ni mahali pa mateso zinakosafishwa roho ambazo hazikutimiza kitubio vizuri baada ya kuungama dhambi. (1Kor 3:15, 1Pet 1:7).


Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?

Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)


Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?

Mambo hayo ni;
1. Kifo
2. Hukumu
3. Jehanamu (Motoni)
4. Paradiso. (Toharani/Mbinguni)


Je, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia?

Ndiyo, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia, kwa sababu kwa njia yake tu tunatiwa uzima: sasa rohoni kwa kuondolewa dhambi, na siku ya mwisho mwilini pia kwa kufufuliwa.
Mwenyewe alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele” (Yoh 11:25- 26).
“Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu” (1Kor 15:20-21).
“Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuka ili tupate kuhesabiwa haki” (Rom 4:25).


Je, ni muhimu tujiandae kufa?

Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Eb 9:27).
“Katika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatima” (YbS 7:36).
“Hamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka” (Yak 4:14).
“Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni” (Math 26:41).


Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?

Ndiyo, “ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” (Zab 116:15).
Hasa utiifu wa Yesu msalabani umegeuza laana ya kifo iwe baraka kwa waamini wake.
“Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” (Ufu 14:13).


Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake.
“Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3).
“Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet 1:3-4).
Sisi tuliobatizwa tunaitwa “wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!” (1Yoh. 3:1).
Kwa sababu tumesadiki kwamba “Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8) na kwamba “hakuna lisilowezekana kwa Bwana” (Lk 1:37).
“Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ‘Aba!’ yaani, ‘Baba!’ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu” (Gal 4:6-7).


Aliyezungumzia moto wa milele ni nani?

Aliyezungumzia moto wa milele ni hasa Yesu: akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee, alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo:
“Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake” (Math 25:41).
“Humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki” (Mk 9:48).
“Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku” (Ufu 14:11).


Toharani maana yake nini?

Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo “alichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zao” (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: “Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?” (1Kor 15:29).


Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > “hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42).
Siku ya ufufuo “ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi” (Lk 21:27).
“Saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu” (Yoh 5:28-29).
“Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele” (Math 25:46).


Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?

Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la.
“Imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyopenda, kwamba ni mema au mabaya” (2Kor 5:10).
“Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu” (1Kor 4:5).
“Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, ‘Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia… Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi’” (Math 25:31-36,40).
“Heri wenye rehema, maana hao watapata rehema” (Math 5:7).


Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?

Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa.
“Kama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake” (2Pet 3:13).
“Na Roho na Bibi arusi wasema, ‘Njoo!’ naye asikiaye na aseme, ‘Njoo!’… Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, ‘Naam, naja upesi’. Amina. Na uje, Bwana Yesu! Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina” (Ufu 22:17,20-21).

Salamu za kuaga mwaka na kukaribisha mwaka mpya

KWAHERI MWAKA JANA. UMENIFUNZA MENGI.

Mwaka umefika mwisho, zimebaki siku tatu tu
kuingia mwaka mwingine lakini yapo mengi
niliyojifunza mwaka huu na pengine ningepesha
kushare:

1. Kwamba si lazima sana kuwa na rundo la
marafiki kama hawaleti positive effects kwenye
maisha yako. Urafiki wa maongezi yasiyoleta
maendeleo ni uzamani chakavu.
2. Matumizi madogomdogo yasiyo ya lazima
huchelewesha maendeleo makubwa yenye kiu na
mimi. Nmekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na
ndio matundu hayo madogo yamezamisha meli.
3. Mungu ndio kila kitu. Anza na maliza siku na
Mungu. Ukikosacho hakukupangia, usiumie,
muombe akuletee atakacho.
4. Harusi zinaumiza. Usipojiwekea kiwango
maalum na idadi ya harusi za kuchangia kwa
mwaka na kwa umuhimu utakuja kujenga nyumba
kwenye harusi za wenzako.
5. Lawama ni muhimu sana ili maisha yaende,
usiogope hasa pale unapokuwa unasimamia lililo
la kimaendeleo kwako. Kumridhisha kila binadam
ni ngumu. Kuna muda ni kwa maendeleo yako
inabidi uwe mbinafsi.
6. Mapenzi ni mazuri ila yasikuzidi ‘kimo’, vipo
vyamaana vya kulilia sio mapenzi. Kikulizacho
ndicho ulichokipa kipaumbele. Mtu aamuapo
kukuliza na wewe ukalia basi umemtukuza.
Mapenzi yasiyosumbua na yaliyojaa mijadala ya
kimaendeleo ndiyo mapenzi yenye afya.
7. Watu waliowengi hasa kwenye mitandao ya
kijamii wana matatzo na ukichaa, usibishane nao
hasa kwenye mambo yasiyokuletea wewe
maendeleo. Usione hasara kuwafanya wajione
washindi.
8. Wazazi ni Muhimu sana, sala zao ni muhimu
kwako. Usipende kuhonga mpita njia akuachaye
siku yeyote ukawasahau wazazi wako. Wapo
watu sikukuu hizi wametumia maelfu ya shilingi
kuhudumia wanawake zao au wanaume zao
wapitaji wakasahau wazazi wao hata kwa pesa
ya dawa.
9. Kuahirisha mambo ni ugonjwa wa kuridhika na
dhiki. Uahirishapo atakaye uwe chini anafurahi.
Muaibishe shetani kwa mipango thabiti.
10. Panga kwaajili ya MWAKA kabla haUjafika,
kupanga kunakupa nafasi ya kujihakiki.
Mpya mwaka wa kucheza na ‘altenatives’.

SEASON GREETINGS…..HAPPY NEW YEAR.

Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju

Vipimo Vya Wali

Mchele Basmati – 4 vikombe

Vitunguu vya majani (Spring onions) – 5 miche

Pilipili mboga nyekundu (capsicum) – 1

Pilipili mboga manjano (capscimu) – 1

Nyanya kubwa – 1

Supu ya kidonge – 2

Siagi – 2 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha roweka kiasi masaa matatu takriban.
Katakata vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya vipande kiasi.
Weka siagi katika sufuria ya kupikia, weka katika moto iyayuke.
Tia vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya, kaanga kidogo tu.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji kiasi ya kuivisha mchele.
Tia supu ya kidogo au supu yoyote, funika wali upikike moto. mdogodogo.

Vipimo Vya Nyama Mbuzi Na Sosi Ya Ukwaju

Nyama mbuzi mapande makubwa kiasi – 7/8 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Ukwaju mzito ulokamuliwa – 1 kikombe cha chai

Jiyra/cummin/bizari pilau – 1 kijiko cha chai

Nyanya kopo – 2 vijiko vya supu

Siki – 2 vijiko vya supu

Mafuta – ½ kikombe cha chai

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Changanya vitu vyote pamoja katika kibakuli kidogo.
Weka nyama katika bakuli kubwa kisha tia mchanganyiko wa sosi, ubakishe sosi kiasi pembeni.
Roweka kwa muda wa masaa 3 – 5
Panga nyama katika bakuli au treya ya kuchomea katika oven.
Pika (bake) kwa moto wa kiasi kwa muda wa saa takriban.
Karibu na kuiva, epua, zidisha kuichangaya na sosi ilobaki.
Rudisha katika jiko uendelee kuipika muda kidogo tu.
Epua ikiwa tayari, weka juu ya wali uliopakuwa kisha mwagia sosi ya nyanya pilipili (chilii tomato sauce) ukipenda.

Ujumbe wa leo kwa mtu anayetaka kufanikiwa katika maisha kiuchumi

Kila mtu aliyefanikiwa ukifuatilia historia yake pengine unaweza kukata tamaa kabisa Na kusema mimi hii njia siiwez.

Lakin siri ya mafanikio ni uvumilivu Na kujituma ktk kazi uifanyao.

Ni kweli vijana wengi humaliza vyuo Na kusubiri ajira wanashindwa kusoma alama za nyakati, hawatambui kuwa sasa wasomi ni wengi sana ajira chache.

Mimi pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuuu lakini ni mjasiri amali vilevile.

Vijana wenzangu tubadilike fursa zipo tuache kuchagua kazi eti kisa unashule kichwani!

Tumia vyeti vinapo hitajika pia viweke pemben unapohitaji kutumia nguvu.

Jaman mungu ni wawote hana upendeleo utatoka tu!!! Tusijitenge eti kwasababu tumeingia darasan uonekane wakipekeee ila tujichanganye Na watu tuliowaacha mtaani tutaongeza maarifa Na watatuonesha fursa tusizozijua.

Shule ni nzuri sana ila pia ni mbaya hasa ya Tanzania maana haitufundishi kujitegemea bali inatufanya tuwe tegemezi cku zote

Chamsingi vijana wenzangu tuamini maarifa tuliyonayo kuwa ndo muhimu kuliko vyeti tulivyo navyo

“Tafuta maarifa ustafute shule tafuta pesa ustafute vyeti”

Kuna watu wameajiriwa lakn hadi Leo wanaishi nyumba za kupanga

Mwisho wa yote niambie uliwahi kuona wapi tajiri aliyeajiriwa? Wote wanamaisha ya kawaida tu.

Angalist ya matajiri Tanzania Na duniani kote hamna aliye ajiriwa hata mmoja.

Yatie akilini hayo jali mafanikio katika maisha yako

Huyu mwanamke ni noma cheki alichomwambia mme wake baada ya kumnunulia nguo za ndani

Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,

Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza

MUME:Watu gani hao watakaokuambia unachupi moje, inamaana unawaonyesha kitumbua changu? Leo utanambia’
Ungekuwa wewe ungefanya nini?

Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu

Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda.

Kama unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.

Usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.

Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

Mahitaji

Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa – 2 LB

Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa – 2 Vikombe

Kitungu maji (vikate vidogo) – 1

Mafuta – ¼ Kikombe

Nyana kata ndogo ndogo – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya haliym – 2 vijiko vya supu

Nyanya ya kopo – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha nyama na chumvi ½ kijiko mpaka iive, toa mafupa.
Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive.
Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, bizari ya haliym, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive.
Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo.
Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri
Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15.
Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

Zifutazo ndizo dalili za awali za mimba changa:

Kutokwa damu bila kutegemea.

“Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

Kuchoka

Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi”

Chuchu kuwa nyeusi.

Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

Maumivu kwenye matiti

Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini

Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kuwa na hasira

“Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”

Kuongezeka kwa joto mwilini.

Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.

Kichefuchefu.

Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

Mwili kuvimba

Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara.

Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali.

Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa

Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebish a na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo

Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?

Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”

Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”

Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”

Mapishi ya Wali, samaki, bilinganya na spinach

Mahitaji

Samaki
Spinach
Bilinganya
Nyanya ya kopo (Kopo 1)
Vitunguu maji
Vitunguu swaumu
Tangawizi
Pilipli mbuzi
Chumvi
Limao
Carry powder
Mchele
Mafuta ya kupikia
Coriander
Hiliki
Amdalasini
Karafuu

Matayarisho

Osha samaki na kisha wamarinate na vitunguu swaumu, tangawizi, limao, chumvi na pilipili kwa muda wa masaa matatu. Baada ya hapo wakaange samaki na uwaweke pembeni kwa ajili ya mchuzi.
Osha spinach na kisha zikatekate na ziweke pembeni
Osha mchele na kisha uloweke kwenye maji kwa muda wa dakika kumi
Osha bilinganya kisha likatekate vipande vidogo dogo

Jinsi ya kupika

Mchuzi

Saga pamoja vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi, nyanya.Kisha weka mchanganya katika sufuria na uinjike jikoni kwenye moto wa kawaida. Pika mchanganyiko mpaka ukauke kisha tia mafuta, chumvi na carry powder. pika kwa muda wa dakika kumi kisha tia samaki na tui la nazi. Acha mchuzi uchemke mpaka tui la nazi liive.kishaipua na tia coriander

Spinach

Kaanga vitunguu maji na mafuta, baada ya hapo tia spinach na chumvi acha ziive kidogo kisha ipua tayari kwa kuliwa.

Mabilinganya

Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka viwe vya brown kisha tia nyanya. Acha ziive kisha tiai mabilinganya na chumvi. Yakishaiva ipua weka pembeni tayari kwa kuliwa.

Wali

Chemsha maji ya wali kwenye sufuria, kisha tia hiliki, pilipili mtama mzima, karafuu na amdalasini, chumvi na mafuta. Kisha tia mchele na uufunike na uache uchemke mpaka utakapokauka maji. Geuza na uache mpaka uive. Kisha ipua. Tayari kwa kuliwa

SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye

Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe vya chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Hiliki ½ Kijiko cha chai

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari – 2 Vikombe vya chai

Maji – 1 Kikombe cha chai

Vanilla ½ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

JINSI YA KUTENGENEZA

Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
Changanya vizuri isiwe na madonge.
Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai.
Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Tabia za kuepuka ili uweze kuwa tajiri

UKIWA NA HIZI TABIA 9, JIANDAE KUFA MASKINI…………
By Kashindi Edson

“Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu” (Nelson Mandela, R.I.P)

“Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio”(Mwl Nyerere, R.I.P).

“Kile unahokifanya muda huu ndicho kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako”(Mahatma Gandhi, R.I.P)

“Ukizaliwa maskini sio kosa lako, ila ukifa maskini hilo ni kosa”(Bill Gate, The richest man in the world).

Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa, “mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini”. Mpaka leo sijaelewa alimaanisha nini.

Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo, uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na haya mambo 9 yafuatayo;

1. KUTOKUJARIBU.

Katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. “Chagua kufa, au kupambana”. “Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.

2. KUTOKUJIFUNZA.

Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima asome kitu kipya. “JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia, Hamasika.(Prof Jay)

3. WOGA & WASIWASI.

“Tunaweza tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa mchana”(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

4. KUJILINGANISHA.

Kuna baadhi ya watu, huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Usitamani kuwa Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu. Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi maisha yako yote.

*5. KUWEKA VINYONGO.**

“Kuweka chuki na konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine”. Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.

6. UONGO

“Uongo utakupa ushindi wa siku moja, ukweli utaishi milele”(WEUSI), “Muongo hata akiongoea ukweli usimuamini”(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja. “Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati wote”(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi kuvificha.

7. UVIVU & UZEMBE

“Nyumba yenye njaa ukisizi unapata zero”(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya. Neno “kazi” katika biblia limeandikwa mara 600. Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila siku. We kwepa majukumu tu, kesho utakula magodoro. “Uvivu unalipa muda huu, bidii & juhudi vinalipa baadae”.

8. STAREHE & ANASA KUPINDUKIA

Pombe, sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. “Sisi ni kile tunacho kula”. Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako”. Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. “Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana”(Nikki Mbishi,).

9. LAWAMA & UMBEA

“Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu” We upo kwenye kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la “wachawi”. Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako

Maswali na Majibu kuhusu Sala

Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;
“Niite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua”.(Yeremia 33:3)
Vile tunavyokuwa na juhudi ya kusali kwa kusema mbele ya Mungu ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa tuwe na juhudi ya kumsikiliza Mungu kile anachotuambia.
Tunaweza kumsikiliza Mungu ndani kabisa ya Mioyo yetu, mara nyingine kwa kupitia dhamira zetu, kupitia watu wengine na kupitia neno lake (Biblia). Tuombe neema ya kutambua sauti yake anaposema nasi ili tuweze kumsikiliza na kutengeneza mahusiano mazuri kati yetu na yeye.
Mungu ni Baba yetu, anatupenda sana na yupo tayari kutusikiliza wakati wote ndio maana Mungu anatualika kwa kutuambia;
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Tudumu katika sala daima kwa sababu njia ya sala ndipo tunaweza kusema yale tunayotaka mbele ya Mungu na kusikia yale anayotaka Mungu.


Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;
  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu

1. Kumwabudu Mungu

Tunasali ili kumwabudu Mungu, yaani kumpa heshima ya mwisho juu ya kila kitu. Kuonyesha kuwa ni mkuu na wa kipekee kuliko mtu au kitu chochote.

2. Kumshukuru Mungu

Tunasali ili kumshukuru Mungu kwa yale yote aliyokwisha kuyatenda, anayoyatenda na yale atakayoyatenda. Tunamshukuru Mungu kwa yote kwa kuwa yote anayoyafanya anayafanya kwa Mapenzi/ Matakwa yake Matakatifu. Nia ya Mungu ni njema daima ndio maana tunapoona ameruhusu mambo ambayo kwa akili zetu tunayaona ni magumu na sio mema tunapaswa kushukuru kwa sababu ameyafanya kwa makusudi mema.
Biblia inatuambia hivi;
16 Furahini siku zote; 17ombeni bila kukoma; 18shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. (1 Wathesalonike 5:16-18)
Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa Kila jambo na kumshukuru huku ni kwa njia ya sala.

3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu

Tunasali kwa kuomaba neema na baraka kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya wenzetu. Tunamuomba Mungu baraka na Mkono wake katika yale tunayoyafanya na kwa yale wanayoyafanya wengine.
Maombi yetu ili ykubalike mbele ya Mungu ni lazima yawe katika mapenzi yake na yawe na nia njema. Tunafundishwa hivi katika biblia;
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. (Yakobo 4:3)
Tunatakiwa tusali kwa kuomba mema na kwa nia njema ili tuweze kupata yale tunayoyaomba kwa Mungu.

4. Kuomba Msamaha

Tunasali ili kuomba msamaha mbele ya Mungu kwa yote mabaya tuliyoyafanya. Mungu ni mwaminifu hasa kwenye kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu.
9Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:9)
Vilevile Tunatakiwa kusali katika mapungufu yetu na kuwa na matumaini.
9Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. (2 Wakorinto 12:9)

6. Kumsifu na kumtukuza Mungu

Tunasali ili kusifu na kumtukuza Mungu. Mungu anapenda kusifiwa na kutukuzwa. Kwa njia ya sifa tunapokea neema na baraka hata ambazo hatujaziomba.
1Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (Zaburi 100:1-4)


Nani anapaswa kusali?

Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Sala ndiyo njia pekee ya kumuunganisha Mwanadamu na Mungu. Tunapaswa kusali Katika hali yoyote. Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali vivyo hivyo tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali.
Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kudumu katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona hali yetu ya kiroho ipo vizuri. Hatupaswi kuacha kusali kama tumepata neema ya kusimama vyema mbele ya Mungu.
Tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kurudi katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona tupo katika hali ya dhambi. Kwa njia ya sala ndipo tutakapoweza kutoka katika hali ya dhambi.
Mungu yupo tayari kusikiliza ukiwa katika hali ya neema au kama ukiwa katika hali ya dhambi. Ndio maana tunapaswa kumwelekea Mungu katika hali yoyote tulio nayo.
14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. (1 Yohane 5:15)
Tena Mungu anasubiri tumuombe ili furaha yetu itimilike.
24Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. (Yohane 16:24)
Hata kama tuna dhambi Mungu yupo tayari kutupokea na kutusikiliza.
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Mungu yupo tayari kutusikiliza hata tunapokuwa wadhambi kwa kuwa haziweki dhambi zetu na makosa yetu mbele yetu. Huruma yake ni kubwa kushinda dhambi zetu.
12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. (Zaburi 103:12-13)
Mungu anatuwazia mema daima ndio maana tunapaswa kusali kwake
11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 12Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. (Yeremia 29:11-13)


Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu.
Tunatakiwa tusali daima Kama Yesu alivyotuhimiza kwa mfano huu;
1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? 
(Lk 18:1-8)
Kwa hiyo basi, Tusali daima kila siku, kila saa na katika hali yoyote. Tusichoke kusali hata kama maombi Yetu hayajajibiwa. Mungu ni mwenye Hekima na anajua lini hasa akujibu kile unachokiomba kwa manufaa yako wewe. Usipopewa Leo kile ukiombacho unaweza kukipata kwa wakati ufaao tena bila ya Kukiomba.

Sala ni Hazina

Sala ni hazina. Kusali ni kujiwekea hazina. Sala unayosali leo inaweza kukunufaisha wakati usioutarajia.

Maana ya Sala kwa Mkristo Mkatoliki

Maana ya sala kwa Mristu Mkatoliki sio kuomba tuu. Sala kwa Mkatoliki ni zaidi ya kuomba. Kwa Mkatoliki sala inamaanisha kufanya haya;
  1. Tunasali kushukuru,
  2. Tunasali kuomba,
  3. Tunasali kusifu na Kutukuza,
  4. Tunasali kumshirikisha Mungu Furaha zetu na huzuni zetu,
  5. Tunasali kuomba Toba na Msamaha,
  6. Tunasali kumshirikisha Mungu Juhudi zetu na Mipango yetu,
  7. Tunasali kumshirikisha Mungu changamoto zetu.
Tuna kila sababu ya Kusali kila Siku na Kila saa. Maisha yetu yote yanatakiwa yawe Maisha ya Sala. Usifikiri kwamba Wakati wote unaposali lazima utamke maneno Mengi sana ili uwe umesali, Sala haipimwi kwa Maneno. Sala inapimwa kwa nia yake na Kujiweka wazi mbele ya Mungu.
Kila Usalipo Jijengee Tabia ya kunuia, kuwa wazi na kusali kwa ukweli wa Moyo wako. Hata kama ni sentesi Moja fupi Kabisa itamke kwa Upendo na Imani. Kwa Mfano, kuna wakati inatosha kabisa kusema Ee Mungu wangu ninakushukuru kwa hili, hii inaweza kuwa sala Yenye nguvu Kama imetamkwa kwa Imani, Shukrani na Mapendo ya Kweli. Maneno machache yanayotamkwa kwa Imani na Mapendo yanaweza kuzidi Mkesha wa Kusali Usiku Mzima huku unasinzia.
Pamoja na kwamba sala fupi ni nzuri na inafaa sana, kuna haja pia ya kujitengea Muda wa Kutosha Kusali na Kutafakari Huku tukiungana na Mungu. Kila siku tunanye mambo yote mengine lakini tusisahau kuwa Tunahitaji kuwa na Muda wa Kusali.
Tusali daima, Kila wakati na Maisha yetu yawe ni Maisha ya Sala.
Mungu Akubariki sana, Azijibu sala zako na Akujalie Neema ya Kuwa Mtu wa Sala.


Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;
9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 
Luka 18:9-14
Tunatakiwa tusali kwa nia njema na kwa kufuata Mapenzi ya Mungu ili sala zetu zipate kibali mbele za Mungu. Tunapoomba kwa nia mbaya ya tamaa na majivuno hatuwezi kupata kile tukiombacho.
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Yakobo 4:3
Mungu anajibu sala zetu kulingana na nia ya kile tunachokiomba. Watu wote waliofanikiwa Katika sala zao walifanikiwa kwa sababu ya nia ya kile walichokiomba.
Sala sio kutamka manano tuu, sala ni kutamka maneno kwa kunuia. Tena tusalipo yatupasa kujua kuwa tunaongea na Mungu na sio tuu kwamba tunatamka maneno. Tusisahau nia kuu ya kusali ambayo ni mawasiliano Yetu na Mungu.
Tunaposali Tunapaswa Kukumbuka na kuzingatia haya;
  1. Nia na Imani (Kuamini na Kuwa na Uhakika na Unachokifanya)
  2. Unyenyekevu wa Kweli
  3. Ibada na Uchaji
  4. Upendo na Uwazi (Honest)
  5. Matumaini na Saburi (Subira)
Kila unaposali jiulize unasali kwa kwa sababu gani? Kila ubapoomba, jiulize unamuomba Mungu ili nini? Sababu yako ndio kibali cha sala yako.
Mungu Akubariki kwa Kukujalia Imani, Unyenyekevu, Ibada, Uwazi na Matumaini Usalipo. Uwe na Amani.


Sala zipo za namna ngapi?

Sala zipo za namna tatu,
1. Sala ya sauti
2. Sala ya fikara
3. Sala ya taamuli


Sala ya Taamuli ni nini?

Sala ya taamuli ni sala ya kumtazama tuu Mungu kwa upendo mkubwa moyoni


Sala ya sauti ni nini?

Sala ya sauti ni sala asaliyo mtu au kundi kwa kutamka maneno


Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu


Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Ni nyakati gani zafaa kwa sala?

Nyakati zote zafaa kwa sala hasa:
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila Dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi


Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13)


Je, yatupasa kuombea wengine?

Ndiyo. Yatupasa kuwaombea watu wote hasa wenye shida, wakosefu na hata maadui zetu.


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,“Tazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’’ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: ‘‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, “Je, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41‘‘Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, “Baba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, “Katika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, ‘Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4“Kwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, ‘Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” 6Bwana akasema, “Sikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:1-8)


Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;
1. Misa Takatifu
2. Baraka ya Sakramenti Kuu
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari Takatifu
6.Novena


Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala


Mahali gani panafaa kwa sala?

Mtu anaweza kusali mahali popote lakini Kanisani ndipo mahali Rasmi pa sala


Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;
1. Mtawanyiko wa Mawazo
2.Ukavu wa moyo
3. Uvivu na Uregevu
Ndiyo maana kwa Wakatoliki sala nyingi zimeandikwa ili kutuongoza hasa tunapokuwa majaribuni katika sala.


Neno “Amina” katika sala lina maana gani?

Neno “Amina” katika sala lina maanisha “Na iwe Hivyo” (Hesabu 5:22)


“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maanisha “Msifuni Mungu”


Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?

Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?

Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?

Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili kushinda vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
“Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu” (Mk 5:8).
“Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!” (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
“Aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” (Mk 6:7).
“Paulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, ‘Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu’. Akamtoka saa ileile” (Mdo 16:18).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
“Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia” (1Sam 3:10).
“Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku” (Zab 63:6).
“Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zab 119:97).
“Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu” (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
“Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, ‘Bwana, tufundishe sisi kusali” (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
“Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yoh 17:1).
“Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
“Wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu” (Lk 2:41-42).
“Saa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, ‘Eloi, Eloi, lama sabakthani?’” (Mk 15:34).
“Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Lk 23:46).


Je, sala ya Yesu inatokana na utu wake tu?

Hapana, sala ya Yesu haitokani na utu wake tu, bali katika huo Mwana wa milele ndiye anayemuelekezea Baba yake sala kamili ya kitoto.
“Saa ileile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, ‘Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza” (Lk 10:21).
“Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote” (Yoh 11:41- 42).
“Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Lk 23:34).


Yesu alisali vipi?

Yesu alisali kila mahali na kila wakati, akidumisha ushirika wa upendo kati yake na Baba katika Roho Mtakatifu.
“Saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” (Yoh 4:23).
Pamoja na kushiriki kiaminifu ibada za taifa lake, mara nyingi alijitafutia mahali pa faragha.
“Aliongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani” (Lk 4:1).
“Alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba” (Lk 5:16).
“Aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu” (Lk 6:12).
Ndiyo sababu ametuambia,
“Wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini” (Math 6:6).
Tusipojua kuongea na Baba moyo kwa moyo, tutawezaje kuongea naye kati ya umati?


Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo.
“Upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako… Waombeeni wanaowaudhi… Msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu” (Math 5:24,44; 6:5).
“Mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, ‘Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi’. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki” (Lk 18:13-14).
Hasa ametutia Roho Mtakatifu atuongoze kama alivyomfanyia yeye.


Je, Yesu ametufundisha maneno ya sala pia?

Ndiyo, Yesu ametufundisha maneno ya sala ya ‘Baba Yetu’, kamili kuliko zote. Maombi yake saba yanategemea utangulizi ambao tunamuendea Mungu kwa ujasiri na furaha kama watoto wake, ndugu kati yetu.
Maombi matatu ya kwanza yanalenga atukuzwe, atawale, apate ushirikiano wetu. Maombi manne ya mwisho yanalenga tupate chakula cha roho na cha mwili, msamaha wa dhambi, ushindi katika vishawishi, usalama dhidi ya yule Mwovu.
“Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi…” (Math 6:8-9).


Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga
“juu ya imani… na kuomba katika Roho Mtakatifu” (Yud 20).
“Mkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana hao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi” (Math 6:7).
Hii haituzuii tusirudie maneno yetu kwa dhati zaidi na zaidi.
Yesu “alikwenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yaleyale” (Math 26:44).
Tunaweza kusali kimoyomoyo pia.
“Hana alikuwa akinena moyoni mwake, midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe… ‘Nimeimimina roho yangu mbele za Bwana’” (1Sam 1:13,15).
“Maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana” (Zab 19:14).


Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba.
“Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu” (Yoh 16:24).
Lakini Baba, kwa ujuzi na upendo usio na mipaka, anaweza akatupatia mambo tofauti na yale tuliyomuomba.
“Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, ‘Nipe maji ninywe’, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai” (Yoh 4:10).
“Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Lk 11:13).
Imani yetu ikubali kwamba aliyotupatia ni bora zaidi.


Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani.
Mhalifu alisema,
“‘Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako’. Yesu akamwambia, ‘Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (Lk 23:42-43).
Stefano aliomba,
“‘Bwana Yesu, pokea roho yangu’. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, ‘Bwana, usiwahesabie dhambi hii’” (Mdo 7:59-60).
“Roho na Bibi arusi wasema, ‘Njoo!’. Naye asikiaye na aseme, ‘Njoo!’… Na uje, Bwana Yesu!” (Ufu 22:17,20).


Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
“Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, ‘Aba!’ yaani, ‘Baba!’” (Gal 4:6).
“Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa… huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, ‘Njoo, Roho Mtakatifu!’ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.


Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
“Yeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu” (Ef 3:16-19).
“Huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.


Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote.
“Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Rom 8:38-39).
“Kwangu mimi kuishi na Kristo, na kufa ni faida… Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo” (Fil 1:21,23)
.
Kwa kuwa hao wako na Kristo mbinguni, wanatuombea mfululizo pamoja naye.
“Niliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, ‘Ee Mwenyezi, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini…’” (Ufu 6:9-10).
Tunawaomba wazidi kutuombea kwa Mungu, kama tunavyowaomba wenzetu waliopo duniani.
“Mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi” (Ef 6:18-19).


Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About