Ufunuo 12:17
17Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo.
Kwa hiyo Bikira Maria ni Mama wa Wakritu wote yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo
Ukisoma kwa urefu inasomeka hivi
Ufunuo 12:1-18
1 Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake. 2Alikuwa na mimba naye akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kuzaa. 3Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: Likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. 4Mkia wake ukakokota theluthi ya nyota zote angani na kuziangusha katika nchi. Ndipo lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kuzaa ili lipate kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. 5Yule mwanamke akazaa mtoto mwanamume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo yake ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti Chake cha enzi. 6Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku 1,260. 7 Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao. 8Lakini joka na malaika zake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni. 9Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. Ushindi 10Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, “Sasa Wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana. 11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa. 12Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo Shetani ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!’ 13Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanamume. 14Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko nyikani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu wakatia ambako yule joka hawezi kufika. 15Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. 16Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake. 17Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari. 18Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari.
Tunajifunza nini
Mwanamke ni Bikira Maria
Mwanamke aliyetukuzwa Uf 12:1
1 Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake.
Anamzaa mtoto
Analindwa nyoka asimdhuru
Nyoka anapambana na wanawe
IShara ya joka kama Shetani
Akisubiri kuzaliwa kwa mtoto ili amdhuru kisha alishindwa na kutupwa duniani na kutaka kupambana na yule mwanamke Akashindwa na kuishia kupambana na watoto wa Yule mwanamke yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo Uf 12:17
Mtoto Aliyezaliwa mwenye mamlaka
Ambaye ndiye Yesu Kristu
Hata chembe ya haradali ya imani inaweza kusogeza milima
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
Dumu katika Bwana.
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Katika imani, yote yanawezekana
Neema na amani iwe nawe.
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
Mwamini Bwana; anajua njia
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Mwamini katika mpango wake.
Wakati wa Mungu ni kamilifu
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
Rehema hushinda hukumu
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
Mungu ni mwema, wakati wote!
Nguvu hutoka kwa Bwana
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
Tumaini ni nanga ya roho
Tembea kwa imani, si kwa kuona
Mungu akubariki!
Rehema zake hudumu milele
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
Baraka kwako na familia yako.
Neema ya Mungu inatosha kwako
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
Nakuombea 🙏
Imani inaweza kusogeza milima
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Sifa kwa Bwana!
Endelea kuwa na imani!
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini