Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Vipimo

Mchele vikombe 3

Karoti 1 ikune (grate)

Mchicha katakata kiasi

Adesi za brown

Kitunguu katakata (chopped)

Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2

Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia

Samli ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Vipimo Vya Samaki Wa Salmon

Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa

Tangawizi mbichi ilosagwa kijiko 1 cha kulia

Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia

Chumvi kiasi

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia

Ndimu 1 kamua

Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon

Changanya viungo vyote upake katika samaki.
Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake.
Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili.
Akiwa tayari epua.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori)
Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii.
Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia.
Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo.
Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu.
Tia chumvi ukoroge funika upike kama pilau.
Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon

Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto

Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili mtoto aweze kuwa na afya. Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea wakina mama wengi kushindwa kuzalisha maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto zao. Hata hivyo kama wewe ni mama na una tatizo hilo basi unatakiwa kufanya yafuatayio ili utengeneze maziwa kwa wingi;

1. Nyonyesha mara kwa mara.

Nyonyesha angalau mara nane kwa siku. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.

2.Tumia vinywaji vya kutosha na kula zaidi.

Epuka kukosa mlo wowote wa siku.

3. Pumzika mara kwa mara.

Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.

4. Hakikisha maziwa yametoka yote wakati wa kunyonyesha au unapokamua.

Usiache maziwa yako kujaa kwa muda mrefu. Hata kama uko mbali na mtoto hakikisha unakamua maziwa.

5. Hakikisha mtoto amenyonya maziwa yote mara mbili kila unaponyonyesha
6. Kwa kina mama ambao hawana maziwa ya kutosha wanaweza kuongea na daktari akawaandikia dawa za kusaidia kuzalisha maziwa.

Huyu mke kwa kupenda hela! Cheki anachomwambia mume wake

Jamaa karudi toka kazini mpole na hana furaha!
MKE; Vipi leo mbona mpole?
MUME; Ofisi yetu imeungua na watu wote waliokuwemo wamekufa.
MKE; Ilikuaje wewe ukapona?
MUME; Nilikua chooni jirani na ofisi najisaidia.
MKE; Loh maskini, familia zao itakuaje?
MUME; Watalipwa million 100 kila mfiwa.
MKE; KWA HASIRA, Ona sasa na wewe kunya kunya kwako umetukosesha mihela.. Ungeenda kunya akhera.

Jinsi ya kutengeneza Labania Za Maziwa

MAHITAJI

Maziwa ya unga – 2 vikombe

Sukari – 3 vikombe

Maji – 3 vikombe

Unga wa ngano – ½ kikombe

Mafuta – ½ kikombe

Iliki – kiasi

MAPISHI

Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania
Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri
Kisha mimina mafuta koroga
Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka
Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza.
Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.

Jinsi ya kutengeneza saladi

Mahitaji

Tango 1/2
Kitunguu 1/2
Cherry tomato 8
Lettice kiasi
Green olives kidogo
Black olives kidogo
Hoho jekundu 1
Carrot
Giligilani kidogo

Salad dressing
Yogurt 1/2 kikombe
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Olive oil kiasi

Matayarisho

Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu Ishara ya Msalaba

Ishara ya msalaba ni nini?
Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?
Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?
Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?
Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?
Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?
Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.

Jinsi ya kufanya nywele zako ziwe na mvuto na kuvutia zaidi

Mwanamke unywele hasa ukiwa nao, hii ni kauli upya ambayo Muungwana blog inakupa siku ya leo. Miongoni mwa maswali ambavyo huwa tunaulizwa na wasamoaji wetu ni pamoja ni kwa jinsi gani naweza kutengeneza nywele zangu ili ziwe za kuvutia?

Basi nasi bila ya haiana yeyote ile tunakuletea somo hili maalum kwa ajili ya watu wote ambao wanatamani kujua namna ya kuzifanya nywele zako zivutie. Kwanza kabisa kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto

Hivyo zifuatazo ndizo njia ya kufanya nywele zako zivutie:

Tumia shampoo inayoendana na nywele zako

Tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

Usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.

Jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

Kula vyakula venye protin na matunda

kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

Kata ncha za nywele zako

kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

Osha nywele zako angalau mara moja kwa wiki

kuosha nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. Hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuonsha nywele zako.

Zifunge nywele zako kabla ya kulala

Unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika

Tumia mafuta asili

Badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka nywele zako.

Zilinde nywele zako na jua

W akati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. Pia unaweza kuzipaka sunscreen.

Faida za kiafya za Kula Matunda

Matunda yote yana faida mwilini kiafya lakini matunda yanatofautiana kifaida. Zifuatazo ni faida za kula matunda ya aina Mbalimbali;

FAIDA ZA TANGO

1. Kuzuia kisukari, kuboresha mfumo wa damu na kuondoa kolesteroli mwilini.
2. Chanzo kikubwa cha Vitamin B.
3. Kusaidia kutunza ngozi.
4. Kuongeza maji mwilini.
5. Kukata hangover.
6. Kuimarisha mmeng’enyo wa chakula mwilini.
7. Kuzuia saratani mwilini.
8. Kusaidia kupungua uzito.
9. Kuondoa maumivu na kuboresha viungo vya mwili.
10. Kuondoa harufu mbaya ya kinywa.

FAIDA ZA PAPAI

1. Kuua na kuondoa mazalia ya minyoo mwilini.
2. Kusaidia kutibu vidonda vya tumbo.
3. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula.
4. Majani yake huleta ahueni kwa wagonjwa wa saratani.
5. Kupunguza uvimbe (anti-inflammatory).
6. Kuboresha misuli na neva mwilini.
7. Kusaidia kumeng’enya protini.
8. Kuboresha kinga ya mwili.
9. Kuboresha macho.
10. Kuboresha mfumo wa hewa

FAIDA ZA UBUYU

1. Kuzuia uhalibifu na mikunjo ya ngozi.
2. Kusaidia katika kupunguza uzito wa mwili.
3. Kuimarisha moyo.
4. Kusafisha ini na kuondoa sumu.
5. Kiwango kikubwa cha vitamin C.
6. Chanzo cha madini ya Calcium.
7. Kuimarisha kinga ya mwili.
8. Kuimarisha figo.
9. Kuimarisha mifupa na meno.
10. Kuimarisha mfumo wa fahamu

FAIDA ZA EMBE

1. Kupunguza kiwango cha asidi mwilini.
2. Kuboresha mmeng’enyo wa chakula.
3. Kurekebisha kiwango cha insulin.
4. Kuboresha macho.
5. Kusafisha damu.
6. Kuboresha ngozi.
7. Kuzuia saratani.
8. Kuimarisha kinga mwilini.
9. Kutibu joto kiharusi (heat stroke).
10. Kupunguza kiwango cha kolesteroli.

FAIDA ZA NANASI

1. Chanzo kikubwa cha vitamin A.
2. Kusaidia kumeng’enya chakula.
3. Inarekebisha mapigo ya moyo.
4. Kuimarisha mifupa ya mwili.
5. Ina kiwango kidogo cha kalori.
6. Inasaidia kuzuia mafua na homa.
7. Kuimarisha mfumo wa kinga.
8. Chanzo cha vitamin C.
9. Inapunguza uvimbe.
10. Kupunguza spidi ya kuzeeka kwa seli mwilini

FAIDA ZA NJEGERE

1. Kuzuia saratani ya tumbo.
2. Kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.
3. Chanzo kizuri cha protini.
4. Kuboresha ufanyaji kazi wa ini.
5. Ina kiwango kidogo cha kalori.
6. Kuboresha kinga ya mwili.
7. Inaleta nguvu mwilini.
8. Ina virutubisho vya nyuzi nyuzi.
9. Inazuia kuzeeka haraka.
10. Imejaa virutubishi vingi muhimu mwilini.

FAIDA ZA PILIPILI HOHO

1. Husaidia kupunguza uzito.
2. Kuboresha mzunguko wa damu.
3. Inapunguza kolesteroli mwilini
4. Kuzuia shinikizo la damu.
5. Ina kiwango kidogo cha kalori.
6. Nzuri kwa kuboresha macho.
7. Kuimarisha mfumo wa kinga.
8. Inatibu anemia.
9. Inazua saratani.
10. Kuboresha moyo.

Huyu panya wa tatu ni noma

🐀 🐀 🐀 Panya watatu walikua wakibishana nani Ni noma zaidi

Panya 1: jamani mimi ni noma Wiki hii nimekula rat rat(sumu ya panya) mara tatu na sijadedi !!!

Panya 2 Wewe unasema nini, mimi nimekula nyama ikiwa
kwa mtego mara 5 nasijawahi dakwa

RAT 3 Mmemaliza? Mie hata sijui mnabishana nini? Mimi hii mimba niliyo nayo ni ya paka !!!

Panya WA 1 na 2 wakazimia😆😆😆😆😆
Panya wa 3 huwa hapendi ujinga kabisa

Jielewe, kipato chako kinakusaidia nini?

ASSET AND LIABILITY
Asset ni kitu chochote kinacho kuingizia pesa mfukoni uwepo au usiwepo.

Liability ni kitu kinachotoa pesa mfukoni kwako.
Ukitaka kuwa tajiri,hiki ndio kitu pekee unacho hitaji kukijua na kukifanyia kazi.
Matajiri wote wananunua Assets,lakini Masikini na wenye wenye maisha ya saizi ya kati wananunua Liabilities wanazodhani kua ni Assets.

Watu wengi ukiwauliza una Asset gan unayomiliki atakutajia vitu kama,nyumba,gari,simu,laptop, duka.
Ni sawa kama tu hivyo vitu vinakuingizia pesa,lakini kama havikuingizii chochote hivyo sio Assets bali ni Liabilities.

Hebu tuangalie nyumba,kama una nyumba yako ya kuishi mwenyewe hiyo ni Liability kubwa sana,maana haikuingizii hata mia,badala yake inakutolea pesa,utalipa umeme,maji,ukarabati na malekebisho ya vitasa,taa,furniture n.k,hayo yoote yanatoa pesa mfukoni.

Lakini kama nyumba umepangisha,hiyo ni Asset. Gari,kama unaitumia kwa matumizi yako binafsi ya kila siku hiyo ni Liability kubwa,itahitaji mafuta,service,na kama umenunua kwa mkopo wa Bank ndio balaa zaidi,ila kama ni la biashara hiyo ni Asset.
Simu ambayo haikuingizii pesa yoyote zaidi ya kukumalizia vocha na kuishia kuchart,hiyo ni Liability, Tv na radio hata duka pia,maana siku umelifunga huingizi chochote,matumizi yoote unategemea dukani,badala ya duka kukupa faida,unachukua mshahara unaongeza mtaji.

Wasomi wengi walioajiliwa wanakufa masikini kwasababu mishahara yao na mikopo wanayochukua inaishia kununua liabilities kama furniture, TV,radio,simu kubw,gari,fridge,nguo,viatu, badala ya Asset ambazo zingewaingizia pesa zingine,mwisho wanaishia kuuza liabilities zao na kubaki masikini kabisa.

Watu wengi wanadhani wakiongezewa mshahara wata tatua matatizo yao,badala yake matatizo yanaongezeka maana mshahara(Income) ukiongezeka,matumizi(Expenses) pia yanaongezeka hivyo kuongeza column ya Liabilities. Na hii yote ni kwasababu hatufundishwi elimu ya pesa dalasani.

Matajiri woote wana kuza upande wa kipato(Income) na kupunguza upande wa matumizi(Expenses) kwa kununua Assets nyingi na kupunguza Liabilities,wananunua Luxuries kama gari,tv ,sm kubwa pale tu Assets au vitu walivyowekeza vinapowapatia faida,hivyo faida ndio inanunua magari,nyumba,TV nnk, ndio maana wanasema siri ya utajiri ni ubahili,lakini watu wengine kadri kipato kinapoongezeka na matumizi yanaongezeka.
Kama unataka kua tajiri lazima ujue pia maana halisi ya neno utajiri(Wealth).

Wealth is a person’s ability to survive so many numbers of days toward, or if you stopped working today,how long could you survive?
Maana yake,kama leo utaacha kufanya kazi ambazo zinakuingizia kipato,una uwezo wa kuendelea kuishi kwa muda gani??
Ukiona ukiacha kufanya kazi huna uwezo wa kumudu mahitaji ya kila siku kwa muda hata wa mwaka mmoja ujue wewe bado huna Mali(wealth) maana huna Assets zinazoweza kukuingizia kipato cha kuweza kukufanya uendelee kuishi pindi uachapo kazi.

Jiulize msharaha wako unanunua Assets au Liabilities, na pia ujiulize are you Wealth or not?

Jinsi ya kuandaa Vileja Vya Tambi

MAHITAJI

Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2

Siagi – 4 Vijiko vya supu

Maziwa (condensed) 300Ml

Lozi zilizokatwakatwa – 1 kikombe

Zabibu kavu – 1 Kikombe

Arki (essence) – 1 Kijiko cha supu

MAPISHI

Weka karai kwenye moto kiasi
Tia siagi
Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu.
Weka lozi na zabibu huku unakoroga
Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono.
Tia arki
Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze.
Kipindue kwenye sahani utoe kileja.
Fanya hivyo mpaka umalize vyote.

Mapishi ya Wali Wa Karoti Na Kuku Wa Kukaanga

Vipimo Vya Wali

Mchele wa Basmati/Pishori – 1 kilo moja

Vitunguu maji – 3

Karoti – 2

Siagi – 3 vijiko vya supu

Kidonge cha supu (stock) – 1 kimoja

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili
Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando.
Kwaruza karoti (grate) weka kando.
Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke
Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu.
Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu.
Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo.
Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.

Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga

Kuku alokatwakatwa – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari ya mchanganyiko/garam masala – kijiko cha supu

Mtindi/Yoghurt – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote.
Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo.
Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban.
Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.

Utaratibu wa Mkristo Mkatoliki Kanisani

Ninapoingia kanisani nachovya maji ya baraka na kusema;
“Unitakase Ee Bwana mimi na uovu wangu wote, ili nipate kustahili kushiriki ibada takatifu’ Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” Amina!
Ninapiga goti huku nikisema
“Mungu wangu na Bwana wangu”
🙋🏽Nikiinuka nasema
“Nitakusifu na kukuabudu katika Ekaristi takatifu”
🙋🏽Naenda mpaka kwenye bench, napiga magoti au nakaa nikiwa mimeinamisha kichwa (kama mabenchi yameisha nabaki nimejisimamia) huku nikitoa nia yangu ya kusali misa siku hiyo, mfano
“Ee Mungu, ninaungana nawe na jeshi lote la mbinguni, pamoja na Mama Bikira Maria, nikiwa na nia ya kumwombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, jirani yangu ambaye mpaka sasa hatuelewani na pia familia yetu ambayo haina amani, Mungu kupitia misa hii rejesha hali ya mama yangu, rejesha uelewano na jirani yangu, na pia rejesha amani ya familia yetu pamoja na familia zote ambazo hazina amani”
🙋🏽Ninaendelea na misa na Kushiriki litrujia kikamilifu
🙋🏽Wakati wa komunyo nikikumbuka kuwa nina dhambi kubwa huwa nakominika kwa sala ya tamaa wala siendi mbele, huwa najikalia tu kwenye bench naangalia wenye moyo safi wanaenda mbele kumpokea Yesu (Kweli huwa najisikia wivu sana, itanibidi katikati ya wiki nifanye kitubio ili nisikae tena)”
🙋🏽Mwisho wakati wa kuondoka nachovya maji ya baraka nikisema
“Unilinde Ee Mwenyezi Mungu, nikapate kuwa mfano katika jamii yangu, na nikushuhudie katika matendo yangu”
(Hapo nachovya maji ya baraka na kufanya ishara ya msalaba) “Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, amina”
Usiku mwema wapendwa. Malaika awalinde
Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About