Mambo ya kutafakari unapokuwa katika shida kubwa, unapoelekea kukata tamaa

Leo tunatafakari kuhusu wakati wa shida
Maisha ya mtu yanabadilika wakati wowote kwa namna yoyote yanaweza yakawa mazuri mpaka ukashangaa au yanaweza yasiwe mazuri kama unavyotarajia. Yote hayo ni sehemu ya maisha.

Unapokua na matatizo makubwa katika maisha Kumbuka haya yafuatayo

  1. Mungu yupo na anakuona mwambie, Huo ndio wakati wake wa kuonyesha uwepo wake na nguvu zake kwa hiyo ni Wewe tuu kusema na Mungu. Utayari na uwazi wako ndio utakao kuwezesha kupata au kutatua tatizo lako.
  2. Maneno, vitendo na muamuzi yako ndiyo yanaweza yakawa njia ya kutatua matatizo yako.
  3. Tatizo lako sio mwisho wa maisha yako, sio mwisho wa yote mazuri yako ya jana ya leo na ya Kesho. Bado unayo mambo mengi mazuri yanakungojea.

Kumbuka tatizo lako linaweza likawa sio kubwa ila wewe ndio unaliona kubwa,

Wewe sio wa Kwanza kuwa na tatizo kama hilo, Wengine hayo ndo maisha yao.

Melkisedeck Leon Shine

Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp

Read and Write Comments

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart