Mafundisho ya Katekisimu

Maswali yanayoulizwa sana kuhusu Ibada ya Kanisa Katoliki

Masifu ni nini?

Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, โ€œTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.โ€™โ€™ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Tumuadhimishe nani?

Tumuadhimishe Mungu pekee siku zote za maisha yetu kwa tumaini la kumuadhimisha milele.
โ€œEe Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, nitalihimidi jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, nitalisifu jina lako milele na mileleโ€ (Zab 145:1-2).
โ€œKwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Aminaโ€ (Rom 11:36).


Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa.
Pamoja na viumbe vyote tuwaimbie usiku na mchana, โ€œMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!โ€ (Ufu 4:8).
โ€œMungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweliโ€ (Yoh 4:24).


Tumuadhimishe Mungu kwa jinsi alivyo au kwa maajabu anayotutendea?

Tumuadhimishe Mungu kwa jinsi alivyo, halafu kwa maajabu anayotutendea tangu awali, ambayo anatujulisha kidogo jinsi alivyo.
โ€œMshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za mileleโ€ (Zab 136:1).


Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu gani?

Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu aliyoyatenda katika Yesu, lakini pia katika Maria na wengine ambao wamefanana naye na kutuonyesha uwezo wa neema yake kwetu.
โ€œKwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwaโ€ (Ef 1:5-6).
Yeye atakuja โ€œili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadikiโ€ (2Th 1:10).


Tumuadhimishe Mungu kwanza kwa njia gani?

Tumuadhimishe Mungu kwanza kwa kumsikiliza kwa makini na kumuitikia kwa imani.
โ€œMasikio ya watu wote yalikisikiliza kitabu cha toratiโ€ฆ watu wote walilia, walipoyasikia maneno ya toratiโ€ (Ne 8:3,9).
Kunyamaza ni sehemu ya ibada yoyote: tunahitaji kimya ili tuelewe tunachoambiwa na tunachosema.
โ€œNisikieni nyote na kufahamuโ€ (Mk 7:14).
โ€œHamjui mnaloliombaโ€ (Mk 10:38).


Je, ibada zetu ziishie katika kusadiki?

Hapana, ibada zetu zisiishie katika kusadiki, kwa kuwa tangu Agano la Kale Mungu aliagiza matendo mbalimbali ya ibada yanayolisha imani.
โ€œHili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako: Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwaโ€ฆ Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenuโ€ (Mwa 17:10,12).
โ€œMwanakondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmojaโ€ฆ Kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioniโ€ฆ Ni Pasaka ya Bwanaโ€ฆ Siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwanaโ€ (Kut 12:5,6,11,14).
Kwetu sisi Wakristo ni yale tuliyoagizwa na Yesu ili yatuletee wokovu.
โ€œAaminiye na kubatizwa ataokokaโ€ (Mk 16:16).


Kanisa linaitaje ibada hizo tulizoagizwa na Yesu?

Kanisa linaita ibada hizo tulizoagizwa na Yesu sakramenti, yaani mafumbo. Ziko saba: Ubatizo, Kipaimara, Ekaristi, Kitubio, Mpako wa Wagonjwa, Daraja na Ndoa. Ndiyo โ€œmafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikonoโ€ (Eb 6:2) tuliyoyapata kupitia Mitume.
Tujihadhari na madhehebu yaliyopunguza sakramenti hizo saba tulizoachiwa na wema wa Yesu kwa kuwa alijua tunavyozihitaji.


Je, tuishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo?

Hapana, tusiishie katika kusadiki na kuadhimisha mafumbo, kwa kuwa imani na sakramenti zinadai kutekelezwa maishani.
โ€œSisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?โ€ฆ Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maanaโ€ (Rom 6:2-3; 12:1).
โ€œNuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguniโ€ (Math 5:16).


Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake nini?

Matendo yetu yasipomtukuza Mungu, maana yake mafumbo hayakuadhimishwa vizuri.
โ€œMaana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufaโ€ (Yak 2:26).


Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?

Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa kuzingatia umbile letu, kwamba binadamu ni umoja wa roho na mwili, hivyo anahitaji mwili na hisi zake ili kuingiza chochote rohoni na kutokeza yaliyomo katika roho yake isiyoonekana.
Ndiyo sababu Yesu alipoletewa kiziwi mwenye utasi โ€œakatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, โ€˜Efathaโ€™, maana yake, โ€˜Funguka!โ€™โ€ (Mk 7:33-34).
Hizo zote ni ishara wazi kwa milango yetu ya fahamu.


Je, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo?

Ndiyo, hisi zetu zote zinaweza kutumika kuadhimishia mafumbo, kila moja kadiri ya uwezo wake: macho kwa kuona, pua kwa kunusa, kinywa kwa kuonja na kusema, mwili mzima kwa kugusa na kutenda, lakini hasa masikio kwa kupokea maneno yaletayo uzima wa Kimungu.
โ€œManeno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzimaโ€ (Yoh 6:63).
โ€œKila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikiaโ€ฆ Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristoโ€ (Rom 10:13-14,17).


Kwa nini maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo?

Maneno ndiyo muhimu zaidi kuadhimishia mafumbo kwa sababu yanafafanua ishara nyingine na kuzitia nguvu ya kututakasa.
โ€œKama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika nenoโ€ (Ef 5:25-26).
Pasipo maneno hapana sakramenti yoyote.


Ishara za mafumbo zimetokana na nini?

Ishara za mafumbo zimetokana na viumbe (maji, mafuta, mkate, divai n.k.) na maisha ya jamii (kuosha, kupaka, kula na kunywa pamoja n.k.) na historia ya wokovu (kunyunyiza na kuzamisha, kuwekea mikono, kula Pasaka, n.k.),
lakini ni kwa kuagizwa na Yesu kwamba zinabeba kazi yake ya kuokoa na kutakasa.
โ€œFanyeni hivi kwa ukumbusho wanguโ€ (Lk 22:19).


Maneno na ishara kwenye ibada vinaweza kubadilishwa na nani?

Maneno na ishara vinaweza kubadilishwa na waandamizi wa Mitume, waliokabidhiwa na Yesu mamlaka ya kuendeleza kazi yake katika mazingira mbalimbali hata mwisho wa dunia.
โ€œAmin, nawaambieni: Yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni, na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguniโ€ (Math 18:18).
Hao Maaskofu wanakiri hawawezi kamwe kuyabadilisha yale ambayo Yesu aliyaweka kuwa ya lazima kama yalivyo mafumbo yenyewe.
โ€œKwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyiโ€ (1Kor 11:23).
Mengine yote wanaweza kuyapanga na kuyarekebisha kadiri ya mazingira, kuanzia lugha, wakilenga daima wokovu wa watu.


Faida ya kupanga taratibu za ibada ni ipi?

Faida ya kupanga taratibu za ibada ni hasa kuhakikisha yote yafuate usahihi wa imani na maadili, yakidumisha umoja na upendo, badala ya kumuachia kiongozi au mwingine yeyote aseme na kufanya anavyotaka. Mitume wenyewe walianza kazi hiyo, wakidhibiti hata karama.
โ€œMambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamazeโ€ฆ Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana. Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjingaโ€ฆ Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibuโ€ (1Kor 14:26-30,37-38,40).
Polepole taratibu ziliongezeka na ibada zikapata mtiririko rasmi wa kueleweka: ndizo liturujia za mashariki na za magharibi ambazo zinaweza kuwa mbalimbali mradi zisipishane upande wa imani.


Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni nani?

Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni Mungu ambaye kwa njia hiyo anazidi kutufanyia maajabu alivyoyafanya Yesu alipokuwa duniani. Kama tunda la kutukomboa kwa kifo na ufufuko wake, Baba anatujaza humo Roho Mtakatifu kama advansi ya uzima wa milele.
โ€œNanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi yake aliye Mtakatifu. Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wakeโ€ (Ef 1:13-14).


Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama nani?

Sisi tunahusika na mafumbo hayo kama walengwa ambao tuyatumie vema ili yazae matunda yote yaliyokusudiwa na Mungu.
Ndiyo kiini cha ukuhani wetu ambao tunashiriki ule wa Kristo tangu tubatizwe.
โ€œMmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristoโ€ (1Pet 2:4-5).


Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?

Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa kwa kuwa ndivyo anavyotufanya โ€œtuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendoโ€ฆ tupate kuwa sifa ya utukufu wakeโ€ (Ef 1:4,12).
Tukipokea neema hiyo tunampatia ibada, sifa na shukrani na tunazidi kumuomba atujaze Roho Mtakatifu kwa njia ya Mwanae.
โ€œBasi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Aminaโ€ (Ef 3:20-21).


Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu.
Ubatizo, kipaimara na ekaristi vinatuingiza katika fumbo la Pasaka tuweze kuishi upya kama wana wa Mungu.
Kitubio na mpako wa wagonjwa vinatuponya roho na hata mwili. Daraja na ndoa zinatufanya wahudumu wa Kanisa na wa familia.
Ni muhimu tujue tunachohitaji na tukipate vipi.
โ€œMaana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwaโ€ (1Kor 11:29-31).


Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna โ€œubatizo mmojaโ€ (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya โ€œkwa maji na kwa Rohoโ€ (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa.
Vilevile katika kipaimara na daraja, karama inayopatikana kwa kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume haifutiki, inadai kuchochewa tu.
โ€œNakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yanguโ€ (1Tim 1:6).
Kumbe tunahitaji ekaristi mara nyingi, kwa sababu ni chakula cha roho.
โ€œBwana, sikuzote utupe chakula hikiโ€ (Yoh 6:34).
โ€œMaana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapoโ€ (1Kor 11:26).


Je, mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote?

Hapana, si mafumbo yote yanaweza kuadhimishwa na yeyote, bali mengine yanahitaji mhudumu wake awe amepewa daraja inayoshirikisha uwezo ambao Yesu aliwapa Mitume wake.
โ€œIkawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu. Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitumeโ€ (Lk 6:12-13).
โ€œYesu aliwaambia tena, โ€˜Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyiโ€™. Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, โ€˜Pokeeni Roho Mtakatifuโ€™โ€ (Yoh 20:21-22).
Kwa kuwa Waprotestanti hawana sakramenti ya daraja, kati yao zinapatikana sakramenti zile mbili tu zisizohitaji padri, yaani ubatizo na ndoa.


Je, tunapoadhimisha mafumbo hayo tuko peke yetu?

Hapana, tunapoadhimisha mafumbo hayo hatuko peke yetu, bali tunashiriki ibada ambayo Yesu anamtolea Baba milele.
โ€œKwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yaoโ€ (Math 18:20).
Kwa kuungana na Kristo Kichwa, tunaungana na viungo vyote vya Mwili wake, vya duniani, toharani na mbinguni.
โ€œNinyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu wa kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habiliโ€ (Eb 12:22-24).


Je, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, kuna nyakati za kufaa zaidi kumuadhimishia Mungu. Yesu aliyesema, โ€œSikuja kutangua, bali kutimilizaโ€ (Math 5:17), alifuata kalenda ya dini ya Kiyahudi, halafu kwa kufa na kufufuka amekuwa kiini cha ibada zetu zote. Hivyo Mitume waliadhimisha siku aliyofufuka kama โ€œsiku ya Bwanaโ€ (Ufu 1:10) ambapo wakutane โ€œili kumega mkateโ€ (Mdo 20:7) wa ekaristi.
Vilevile kwenye Pasaka hawakuadhimisha tu kazi ya Musa, bali ukumbusho wa Yesu.
โ€œPasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristoโ€ (1Kor 5:7).
Fumbo hilo ndio moyo wa mwaka wa liturujia, yaani wa mpangilio wa maadhimisho katika mzunguko wa mwaka.
โ€œBasi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristoโ€ (Kol 2:16).


Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali.
โ€œMungu je, atakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama, mbingu hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii niliyoijenga!โ€ (1Fal 8:27).
โ€œMungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikonoโ€ (Mdo 17:24).
Hata hivyo sisi watu tunahitaji mahali maalumu kwa matendo yetu mbalimbali, na kumwekea Mungu mahali patakatifu.
โ€œMwambieni mwenye nyumba, โ€˜Mwalimu asema: Ki wapi chumba changu cha wageni, niile Pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu?โ€™ Naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieniโ€ (Mk 14:14-15).


Hekalu ndiyo nini?

Hekalu ndipo tunapomuendea Mungu kwa ibada. Vilevile sisi wenyewe ni Mahekalu.
Yesu aliheshimu na kutakasa hekalu pekee la taifa lake kama โ€œnyumba ya Babaโ€ yake (Yoh 2:16), lakini alitabiri kuwa litabomolewa moja kwa moja, na kuwa watu watapaswa kuabudu ndani yake aliye hekalu hai. โ€œWayahudi walisema, โ€˜Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?โ€™ Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wakeโ€ (Yoh 2:20-21).
โ€œKatika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Rohoโ€ (Ef 2:22).
โ€œHamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyiโ€ (1Kor 3:16-17).


Je, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu?

Ndiyo, sanaa zinafaa kumuadhimishia Mungu kwa sababu tunapaswa kutumia kwa utukufu wake vipawa alivyotujalia, kama vile vya kujenga, kupamba, kuchonga, kuchora na kucheza. Kwa njia hizo tutokeze na kukoleza imani yetu na ya wenzetu.
Mungu โ€œamewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi za kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu. Basi, Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi, na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye Bwana amemtia akili na hekima ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote Bwana aliyoyaagizaโ€ (Kut 35:35-36:1).
โ€œMaskani zako zapendeza kama nini, Ee Bwana wa majeshi!โ€ (Zab 84:1).


Kati ya sanaa kwenye ibada/kumuadhimisha Mungu, muhimu zaidi ni ipi?

Kati ya sanaa, muhimu zaidi ni uimbaji, kwa kuwa unahusiana zaidi na Neno la Mungu, ukilitia maanani kwa uzuri wa muziki. Katika Agano la Kale, kitabu cha Zaburi ni nyimbo tupu za kutumia katika ibada.
โ€œMsifuni kwa mvumo wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi! Msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi! Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana!โ€ (Zab 150:3-5).
Agano Jipya pia linatuletea nyimbo nyingi.
โ€œMjazwe Roho, mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenuโ€ (Ef 5:18-19).
Mbinguni washindi wana โ€œvinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondooโ€ (Ufu 15:2-3).


Kuimba wakati wa ibada ni kazi ya nani?

Kuimba ni kazi ya kusanyiko lote, yaani ya kila mwamini. Kwaya ziimbishe watu wamwadhimishe Mungu, zisiwaimbie tu na kuwanyima nafasi ya kuimba.
โ€œMfanyieni Bwana shangwe, dunia yote, mtumikieni Bwana kwa furaha, njoni mbele zake kwa kuimbaโ€ (Zab 100:1-2).
โ€œKila kiumbe kilichopo mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, โ€˜Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwanakondoo, hata milele na mileleโ€™โ€ (Ufu 5:13).


Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie nini?

Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie utakatifu na ukweli, si uzuri tu. Zisiigeuze kamwe kuwa igizo wala tamasha, kwa kuwa lengo si kuchangamsha watu bali kumtukuza Mungu.
Ziinue mioyo kwake, zitokeze na kuchangia maisha safi, zilete ujumbe sahihi kadiri ya imani na maadili, kama ilivyo lazima kwa mahubiri na mafundisho.
โ€œWatu hawa huniheshimu kwa midomo, ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamuโ€ (Math 15:8-9).


Je, ni halali kuheshimu sanamu?

Ndiyo, ni halali kuheshimu sanamu kama viwakilishi vya Yesu, Mama yake na watakatifu wake, ambao zinaleta sura zao.
Kwa msingi huo walimsihi Yesu โ€œwaguse hata pindo la vazi lake tu. Na wote waliogusa wakaponywa kabisaโ€ (Math 14:36).
โ€œMimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote il msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristoโ€ (Gal 6:14).


Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu.
โ€œOle wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki, kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu woteโ€ (Math 23:27).
โ€œAkiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri, kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, โ€˜Keti wewe hapa mahali pazuriโ€™, na kumwambia yule maskini, โ€˜Simama wewe paleโ€™, au โ€˜Keti miguuni panguโ€™, je, hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?โ€ (Yak 2:2-4).
โ€œWanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani, bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Munguโ€ (1Tim 2:9-10).
Kanisa si mahali pa mashindano: hatuendi kupendeza watu, ila Mungu.
โ€œAu mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu?โ€ (1Kor 11:22).


Mbali ya sakramenti, Kanisa linamuadhimisha Mungu vipi?

Mbali ya sakramenti, Kanisa linamuadhimisha Mungu hasa kwa Liturujia ya Vipindi, yaani kwa sala rasmi zinazotolewa mara kadhaa kwa siku, kufuatana na ratiba ya binadamu ya usiku na mchana. Hivyo linajitahidi kutimiza agizo la kusali daima.
โ€œImewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaaโ€ (Lk 18:1).
โ€œKesheni ninyi kila wakati, mkiombaโ€ (Lk 21:36).
โ€œOmbeni bila kukoma, shukuruni kwa kila jamboโ€ (1Thes 5:17).
โ€œKwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu woteโ€ (Ef 6:18).
โ€œHuyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usikuโ€ (1Tim 5:5).


Kanisa linamuadhimishaje Mungu tena?

Kanisa linamuadhimisha Mungu tena kwa visakramenti ambavyo kwa mamlaka ya Kristo linawatia watu neema zake katika nafasi yoyote ya maisha. Kati yake muhimu zaidi ni baraka na mazinguo, ambavyo vipo tangu zamani, hata nje ya taifa la Israeli.
Melkisedek alisema, โ€œAbramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwakoโ€ (Mwa 14:19-20).
Farao aliomba, โ€œMkanibariki mimi piaโ€ (Kut 12:32).
Balaam alisifiwa, โ€œNajua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwaโ€ (Hes 22:6).
โ€œIkawa, ile roho mbaya kutoka kwa Mungu ilipomjilia Sauli, ndipo Daudi akakishika kinubi, akakipiga kwa mkono wake, naye Sauli akaburudishwa, na ile roho mbaya ikamwachaโ€ (1Sam 16:23).
โ€œNa mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je, wana wenu huwatoa kwa nani?โ€ (Math 12:27).


Maana ya baraka ni ipi?

Maana ya baraka ni kumsifu Mungu kwa yale aliyokwishatujalia na kumuomba azidi kutujalia kadiri ya mahitaji ya wahusika. Mara nyingi inatolewa na mtu mwenye daraja au mamlaka fulani.
Yesu aliletewa โ€œwatoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombeaโ€ (Math 19:13).
Siku ya kupaa mbinguni โ€œaliinua mikono yake akawabarikiโ€ (Lk 24:50).
โ€œNdipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zaoโ€ (Mdo 13:3).
Pengine vinabarikiwa vitu vinavyotumiwa na watu, au mahali wanapoishi.
โ€œAkaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutanoโ€ (Lk 9:16).


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
โ€œEwe pepo mchafu, mtoke mtu huyuโ€ (Mk 5:8).
โ€œEwe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!โ€ (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
โ€œAliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafuโ€ (Mk 6:7).
โ€œPaulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, โ€˜Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyuโ€™. Akamtoka saa ileileโ€ (Mdo 16:18).


Je, ni halali kwa Wakristo kujitungia ibada nyingine?

Ndiyo, ni halali kwa Wakristo kujitungia ibada nyingine, mradi wakubali zipimwe na Maaskofu kama zinalingana na imani, maadili na taratibu za Kanisa.
โ€œMtu asiwanyangโ€™anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bureโ€ฆ Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kituโ€ (Kol 2:18,23).
โ€œBali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwaoโ€ (2Tim 3:14).


Ni halali kujitungia ibada kwa sababu gani?

Ni halali kujitungia ibada kwa sababu sala ni hasa maongezi ya Mungu na mtu.
Adamu na Eva โ€œwalisikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupungaโ€ (Mwa 3:8).
Yeye hachoki kumvuta kila mmojawetu kwake na kumtia hamu ya kumhimidi na kumuabudu, kumuomba kwa ajili yake na ya wengine, kumshukuru na kumsifu.
โ€œEe Bwana, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu, kwa uaminifu wako unijibu kwa haki yakoโ€ (Zab 143:1).
Hata tukisali pamoja, uhusiano wa kila mmojawetu na Mungu ni wa pekee. Tusiposali kwa moyo, ibada ni ya bure.
โ€œWatu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana namiโ€ (Isa 29:13).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
โ€œNena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiaโ€ (1Sam 3:10).
โ€œNakutafakari Wewe makesha yote ya usikuโ€ (Zab 63:6).
โ€œSheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwaโ€ (Zab 119:97).
โ€œManeno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wanguโ€ (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
โ€œIkawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, โ€˜Bwana, tufundishe sisi kusaliโ€ (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
โ€œBaba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze weweโ€ (Yoh 17:1).
โ€œAba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo weweโ€ (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
โ€œWazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuuโ€ (Lk 2:41-42).
โ€œSaa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, โ€˜Eloi, Eloi, lama sabakthani?โ€™โ€ (Mk 15:34).
โ€œEe Baba, mikononi mwako naiweka roho yanguโ€ (Lk 23:46).

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa kuheshimu uhuru wa dini na kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali?

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa kuheshimu uhuru wa dini na kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali? Ndio! Kanisa Katoliki linapenda kuhimiza kila mtu kuheshimu uhuru wa dini na kuheshimu imani ya wengine, na kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali. Kama Wakatoliki, tunapaswa kuwa mfano wa amani na upendo kwa wengine, hata kwa wale ambao hawana imani yetu.

Katika Injili, Yesu Kristo alipenda kutangaza amani na upendo kwa kila mtu. Yeye alisema katika Mathayo 5:9 "Heri wenye amani, kwa kuwa wao watapewa na Mungu jina lao la kuwa wana." Hii inaonyesha jinsi Mungu anavyopenda amani na upendo, na hivyo tunapaswa kuwa wakazi waadilifu wa dunia hii, wakipenda amani na kuheshimu wengine.

Kanisa Katoliki linafundisha kuwa kila mtu ana haki ya uhuru wa dini na kukubaliwa kwa imani yake, bila kujali ni dini gani. Hii inamaanisha kwamba kila mtu anapaswa kuheshimiwa kwa imani yake na kuheshimu imani ya wengine. Wakatoliki tunapaswa kuwa na heshima ya wengine, hata kama kuna tofauti za kidini.

Kanisa Katoliki linapendekeza kwamba sisi sote tunapaswa kuchangia katika kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali. Hii inaweza kufanywa kwa njia ya majadiliano, kutembeleana, na kushirikiana kwa malengo mema. Kwa mfano, tunaweza kuwaalika wenzetu wa dini nyingine kwa misa zetu au hata kushiriki katika shughuli za kijamii na za kimaendeleo.

Kanisa Katoliki linasema pia katika Catechism of the Catholic Church kwamba "uhuru wa dini unahusisha haki ya kila mtu ya kufuata dhamiri yake katika mambo yote yanayohusiana na dini" (CCC 2106). Hii ni sehemu ya haki ya binadamu ambayo inapaswa kulindwa kote ulimwenguni. Kwa hiyo, kama Wakatoliki, tunapaswa kuongoza kuwa mfano wa kulinda haki hii ya binadamu.

Katika Wagalatia 5:13, Paulo anasema "Kwa maana ninyi, ndugu, mliitwa kwa ajili ya uhuru; lakini msitumie uhuru wenu kuwa sababu ya kufanya mambo maovu, bali tumikianeni kwa upendo." Hii inaonyesha kwamba uhuru unapaswa kutumika kwa njia ya upendo na kuheshimu wengine. Tunapaswa kutumia uhuru wetu kwa kusaidiana kwa upendo na kuheshimiana wengine.

Mwisho, tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya dini mbalimbali. Kwa kweli, tunapaswa kujua imani yetu kwa undani, lakini pia tunapaswa kuelewa imani za wengine. Hii itatusaidia kuheshimu imani ya wengine na kuwa mfano wa amani na upendo.

Kwa hiyo, tunapaswa kuheshimu uhuru wa dini na kuheshimu imani ya wengine, kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali, na kuwa mfano wa upendo na amani kwa wengine. Neno la Mungu linasema, "Bwana wa amani mwenyewe awape amani kwa njia zote. Bwana na awe pamoja ninyi nyote" (2 Wathesalonike 3:16).

Amri ya Kwanza ya Mungu: Mambo Muhimu ya Kuzingatia

Katika amri ya kwanza ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusadiki kuwa Mungu ni mmoja, ndiye Baba yetu na Mkubwa wetu: tumpende, tumwabudu yeye peke yake. (Mt 10:33, Kumb 6:4-9)


Wakatoliki tunamwabudu Mungu kwa namna gani?

Tunamwabudu Mungu kwa sala , sadaka na matendo mema


Katika amri ya kwanza ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa kumdharau Mungu na kuweka imani yetu katika viumbe badala ya Mungu.


Je, kuna viumbe ambavyo tunaviheshimu kwa kumtukuza Mungu?

Ndiyo twamuheshimu Bikira Maria, Malaika na Watakatifu.


Kwa nini yatupasa kuwaheshimu Watakatifu?

Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu.


Je, tuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu?

Hatuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu tunawaheshimu tu.


Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22).

18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. Kutoka 25 :18-22.

Vile vile Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli Wachonge sanamu ya nyoka na yeyote atakayeumwa na nyoka akiiangalia atapona.


Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?

Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu.


Ni nanai ana kosa kumuabudu Mungu?

Anayekosa kumuabudu Mungu ni yule;

1. Anayeacha kusali au anayesali hovyo
2. Anayemkufuru Mungu
3. Anayeamini na kushika mambo ya kipagani


Mambo gani yanavunja amri ya kwanza ya Mungu?

Mambo hayo ni;

1. Kuabudu sanamu
2. Kufanya matambiko
3. Kwenda kwa waganga
4. Kupiga bao au ramli
5. Kuvaa hirizi
6. Kushiriki mambo ya kichawi n.k.


Ni nini maana ya kuabudu sanamu?

Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake.


Kutokumuabudu Mungu ni kwa namna gani?

Ni kuruhusu kitu chochote kimtawale mtu badala ya Mungu, mfano cheo, pombe, mali, shetani, tuisheni, kazi, na kutoadhimisha Jumapili au kutoshiriki.


Mkatoliki anaabuduje?

Mkatoliki anaabudu kwa kupiga goti au magoti mawili na ni mbele ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu tuu hasa wakati wa kuingia na kutoka kanisani


Je magoti yanayopigwa wakati mwingine tofauti na wakati wa kuabudu yana maana gani?

Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwa Mkao wa sala


Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)

Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;

“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)

Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?

Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.

“BWANA akamwambia Mose, โ€œTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.โ€™โ€™ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.” (Hesabu 21:8-9).

Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.

Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.

Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.

Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.

Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.

Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani: Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki: Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22)Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.

Kwenye Agano jipya: Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.

FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.

Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.


Tunawaheshimu Watakatifu namna gani?

Tunawaheshimu kwa kuadhimisha sikukuu zao, kwa kuomba maombezi yao, kufuata mifano yao na kuheshimu masalia na sanamu zao, kwa kuinama kichwa kidogo tunapopita mbele yake

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya sala?

Kanisa Katoliki linathamini sana maombi kama sehemu muhimu ya maisha yetu ya kiroho. Imani yetu inatufundisha kuwa kupitia maombi tunawasiliana na Mungu na kuimarisha uhusiano wetu naye. Hii ni kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na tunaishi kwa neema yake.

Maombi ni mawasiliano ya moyo na Mungu, ambayo yanatuwezesha kumwomba msamaha kwa dhambi zetu na kupata nguvu za kushinda majaribu. Kwa hivyo, sala ni sehemu muhimu ya maisha ya Kikatoliki na inahitajika kwa maendeleo yetu ya kiroho.

Tunapata mafundisho haya kutoka kwa Yesu mwenyewe, ambaye aliwaambia wanafunzi wake kuwa wasali daima na kutokata tamaa (Luka 18: 1). Katika Yohana 15: 7, Yesu anatuambia kuwa ikiwa tunakaa ndani yake na neno lake linakaa ndani yetu, tunaweza kuomba chochote tunachotaka, na Mungu atatupa.

Kanisa Katoliki pia linatupa mfano wa sala kwa kufundisha kwamba sala ya Bwana ni muhimu sana. Sala hii inatufundisha kumwomba Mungu kwa njia ya kinafiki na kutambua kwamba yeye ndiye muumba wetu. Tunamuomba Mungu kwa mahitaji yetu ya kila siku, pamoja na kupata nguvu za kushinda dhambi.

Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunaambiwa kuwa sala ya Kanisa ni muhimu sana. Sala hii inaundwa na sala za Wakristo wote na inaunganisha Kanisa kama mwili wa Kristo. Sala hii inatupa nguvu za kuishi maisha ya Kikristo kwa kupata nguvu zetu kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Kwa hivyo, kama Wakatoliki, tunahimizwa kuomba kwa nguvu zetu zote na kwa moyo wote. Tunatafuta kumjua Mungu vizuri zaidi na kukuza uhusiano wetu naye kupitia sala. Kwa njia hii, tunaweza kuwa na maisha yenye furaha, amani, na raha ya ndani.

Kwa hiyo, tunakuhimiza, mpendwa msomaji, kuanza maisha ya sala na kujitolea kwa Bwana wetu. Kwa kufanya hivyo, utapata furaha ya kweli na utaishi maisha yenye maana. "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; pigeni hodi, nanyi mtafunguliwa" (Mathayo 7: 7).

Amri ya Tatu ya Mungu: Tumeamriwa kuheshimu siku ya Mungu

Katika amri ya tatu ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa kuheshimu siku ya Mungu:-

1. Kushiriki Misa Takatifu siku ya Jumapili na Sikukuu zote za Amri
2. Kuacha kazi nzito na
3. Kutenda matendo mema


Siku ya Mungu kwa Mkristo ni lini?

Siku ya Mungu kwa Mkristo ni siku ya Dominika, ndio siku aliyofufuka Bwana na huitwa pia Siku ya Bwana


Nani analazima kuhudhuria Misa Takatifu, Dominika na Sikukuu zilizoamriwa?

Kila Mkatoliki aliyetimiza umri wa Miaka saba na kuendelea ana lazima kuhudhuria Misa Takatifu, Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.


Katika amri ya tatu ya Mungu tumekatazwa nini?

Katika Amri ya tatu ya Mungu tumekatazwa kufanya kazi nzito siku ya Dominika/Jumapili.


Kazi nzito zilizokatazwa kufanyika siku ya Bwana ni zipi?

Kazi nzito ni zile za kuchosha mwili na zisizo za lazima kama vile kulima, kujenga, kubeba mizigo mizito, biashara n.k.


Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?

NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa.


Nani atenda dhambi dhidi ya Amri ya tatu ya Mungu?

Anayetenda dhambi dhidi ya amri ya tatu ya Mungu ni yule:-

1. Asiyeshiriki Misa Takatifu Dominika na sikukuu zilizoamriwa kwa uvivu au uzembe
2. Anayefanya kazi ngumu Dominika na sikukuu zilizoamriwa
3. Anayechelewa sehemu kuu ya Misa Takatifu
4. Anayekaa nje ya kanisa bila sababu wakati wa Misa Takatifu na Ibada. (Neh 13:15-22, Kut 20:8-11)


Anayevunja Amri ya Tatu ya Mungu yampasa nini?

Yampasa atubu na aungame kabla ya kushiriki Sakramenti nyingine

Maswali na majibu kuhusu Katekesi

Katekista ni nani?
Katekista ni mlei aliyechaguliwa na Kanisa ili kumfanya Kristo ajulikane, apendwe, na kufuatwa na wale ambao hawajamfahamu na pia waamini


Waraka wa Baba Mtakatifu Unatafsiri vipi Makatekista?
Waraka unasema;
1. Makatekista ni Wafanyakazi maalimu
2. Mashahidi wa moja kwa moja, Wainjilishaji wasio na mbadala


Mkusanyo Sheria Kanuni za Kanisa unaelezaje kuhusu Makatekista?
Unaeleza kuwa – Makatekista ni Walei Wakristo ambao wamepewa malezi halisi na wanajitokeza vizuri katika maisha ya Ukristo wao.


Chini ya Uongozi wa Kanisa Katekista anafanya Kazi gani?
1. Yeye ni Kiungo cha Mapadre na waamini wa eneo lake
2. Kufikisha mafundisho ya Injili na kuhusika kwenye kazi za Ibada za kiliturujia na kazi za Huruma
3. Kuhubiri na kuwafundisha wakatekumeni
4. Kuelimisha vijana na watu wazima kkatika maswala ya Imani
5. Kuongoza Sala za Jumuiya hasa kwenye Ibada za Jumapili Ikiwa Padre hayupo
6. Kuwatembelea wagonjwa na kuwasaidia na kuongoza Ibada za Mazishi
7. Kufundisha dini mashuleni na kuwaandaa watoto katika kupokea Sakramenti mbalimbali
8. Kutembelea Jumuiya ndogondogo kuziendeleza na kuziimarisha

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya watoto wachanga?

Katika Kanisa Katoliki, watoto wachanga ni baraka kubwa kutoka kwa Mungu. Imani yetu inaamini kuwa kila mtoto anapewa uhai na Mwenyezi Mungu, na hivyo wanastahili heshima na upendo. Watoto wachanga ni zawadi kubwa kwa familia zao, na wanapaswa kuheshimiwa na kulindwa kwa kila hali.

Kanisa limeelezea kwa undani jinsi maisha ya mtoto wachanga yanapaswa kulindwa. Kwa mfano, kwa mujibu wa Catechism of the Catholic Church, "Maisha yote ni takatifu, tangu kuanzia mimba, mpaka kifo cha asili kinapotokea" (2258). Hii ina maana kwamba mtoto anayekua kwenye tumbo la uzazi anastahili heshima na kulindwa kama mtu mzima.

Kwa hiyo, Kanisa linapinga vitendo vyote vinavyoleta madhara kwa mtoto wachanga. Hii ni pamoja na utoaji mimba, ambao unaharibu uhai wa mtoto kabla hata hajazaliwa. Kanisa pia linapinga utoaji mimba kwa sababu yoyote ile, hata kama ni kwa ajili ya afya ya mama. Kanisa linatetea haki ya mtoto wa kuishi, na kuheshimu maisha yake kutoka mwanzo hadi mwisho.

Kanisa pia linawahimiza wazazi kuwa waangalifu katika jinsi wanavyokabiliana na watoto wachanga. Wazazi wanapaswa kuwa na upendo, uvumilivu, na subira katika kuwalea watoto wao. Kama ilivyoelezwa katika Catechism, "Wazazi wanapaswa kuwa mfano bora kwa watoto wao, na kuwafundisha jinsi ya kuishi kwa kumtegemea Mungu na kuwapenda wengine" (2225). Kwa hiyo, wazazi wanapaswa kuwa waangalifu katika kuchagua maneno yao na vitendo vyao wanapokuwa karibu na watoto wao.

Kanisa pia linawahimiza wazazi kuwabatiza watoto wao mara wanapozaliwa. Kupitia ubatizo, mtoto anapokea Roho Mtakatifu na anakuwa sehemu ya familia ya Kanisa. Ubatizo pia unafuta dhambi ya asili ya mtoto na kumweka katika njia ya kumfuata Kristo. Kwa hiyo, ubatizo ni muhimu sana katika maisha ya mtoto wachanga.

Kwa ufupi, maisha ya watoto wachanga ni muhimu sana katika imani ya Kanisa Katoliki. Watoto wachanga wanapaswa kulindwa kwa kila hali, na kutambuliwa kama zawadi kutoka kwa Mungu. Wazazi wanapaswa kuwa waangalifu katika jinsi wanavyowalea watoto wao, na kuhakikisha kuwa wanawafundisha jinsi ya kuishi kwa kumtegemea Mungu. Kupitia ubatizo, mtoto anakuwa sehemu ya familia ya Kanisa, na anapokea Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, watoto wachanga ni baraka kubwa katika Kanisa, na wanapaswa kutunzwa kwa kila hali.

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa haki na kulinda haki za binadamu?

Kanisa Katoliki ni moja kati ya makanisa makubwa duniani ambayo yamejikita katika kufundisha na kuhubiri umuhimu wa haki na kulinda haki za binadamu. Katika mafundisho yake, Kanisa Katoliki linaamini kuwa kila binadamu ana thamani sawa mbele za Mungu, na hivyo kila mtu anastahili kulindwa, kuheshimiwa na kupewa nafasi ya kuishi maisha yenye haki na amani.

Kwa mujibu wa Catechism of the Catholic Church, haki ni "sifa za haki ya kila mtu kupewa nafasi ya kuishi, kupata chakula, mavazi, makazi, elimu, afya, na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya maisha yake." Kanisa Katoliki linasisitiza kuwa haki hizi zinastahili kupewa kipaumbele na kuhakikishwa na serikali na jamii kwa ujumla.

Katika Injili, Yesu Kristo pia alisisitiza umuhimu wa haki na kulinda haki za wengine. Kwa mfano, katika Mathayo 25:31-46, Yesu anaelezea jinsi atakavyowahukumu watu wakati wa mwisho wa dunia. Atawauliza kama walishiriki katika kuwalisha wenye njaa, kuwapa maji wenye kiu, kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji wafungwa. Maandiko haya yanasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa haki za wengine zinalindwa na kuheshimiwa.

Katika mafundisho yake, Kanisa Katoliki pia linaamini kuwa kulinda haki za binadamu ni sehemu ya wajibu wa kila mmoja wetu. Kila mtu ana wajibu wa kusimama kwa ajili ya haki na kuwalinda wengine, na kuwa mstari wa mbele katika kupinga dhuluma na ubaguzi. Hii inamaanisha kuwa lazima tufanye kazi pamoja kushughulikia ubaguzi, unyanyasaji, na kila aina ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kwa kumalizia, Kanisa Katoliki linasisitiza umuhimu wa haki na kulinda haki za binadamu. Ni wajibu wetu kama waumini wa Kanisa Katoliki kufuata mafundisho haya na kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za wengine. Kama ilivyoelezwa katika Mathayo 25:31-46, tunapaswa kuwa na huruma kwa wengine na kuhakikisha kuwa haki zao zinalindwa na kuheshimiwa. Hii ni sehemu muhimu ya kufuata mafundisho ya Kristo na kuishi maisha yenye amani na haki.

Mambo ya muhimu kujua kuhusu Sakramenti ya Kipaimara

Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku gani?
Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku ya Pentekoste, yaani siku ya hamsini toka Pasaka. (Mdo 2:1-4)


Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?
Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake.
โ€œWaliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yaoโ€ (Mdo 19:5-6).
Sakramenti hizo ni kama pande mbili za pesa moja. Zinahusiana kama Pasaka na Pentekoste, ambayo ni utimilifu wake, kwa kuwa siku alipofufuka Yesu aliwapulizia Mitume Roho Mtakatifu, ambaye siku hamsini baadaye akawajia kama
โ€œupepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yoteโ€ (Mdo 2:2).


Pamoja na kuwekewa mikono na mwandamizi wa Mitume, mtu anapewa kipaimara vipi?
Pamoja na kuwekea mikono na mwandamizi wa Mitume, mtu anapewa kipaimara kwa kupakwa krisma kama mhuri wa kuwa mali ya Bwana. Ndiyo inayotufanya tuitwe Wakristo nyuma ya Yesu aliyeitwa Kristo.
โ€œKwa sababu huyo ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Munguโ€ (Yoh 6:27).
โ€œYeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetuโ€ (2Kor 1:21-22).


Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake nini?
Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake ni kuja kuongozwa naye badala ya kutawaliwa na shetani.
โ€œKwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwetu, aliaye, โ€˜Aba!โ€™ yaani, โ€˜Baba!โ€™ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miunguโ€ฆ Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Rohoโ€ (Gal 4:6-8; 5:25).
โ€œIkiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wakeโ€ (Rom 8:9).


Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia nini?
Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia adili kuu la upendo:
โ€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisiโ€ (Rom 5:5).
Tena tunapokea vipaji vyake ambavyo Yesu alikuwa navyo kikamilifu.
โ€œRoho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana. Na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwanaโ€ (Isa 11:2-3).
Mambo hayo, tofauti na karama, ni ya lazima kwa yeyote apate wokovu wa milele.


Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?
Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo.
โ€œWengi wataniambia siku ile: Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovuโ€ (Math 7:22-23).
โ€œNijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kituโ€ (1Kor 13:1-3).


Je, karama ni zile za kushangaza tu?
Hapana, karama si zile za kushangaza tu, tena zile muhimu zaidi si hizo, bali zile zinazojenga zaidi Kanisa, kama zile za uongozi:
โ€œMungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lughaโ€ (1Kor 12:28).
โ€œBasi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furahaโ€ (Rom 12:6-8).


Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kufanya nini?
Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kuishi kwa useja kama Yesu na Paulo, au kwa ndoa:
โ€œNipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane; ni heri wakae kama mimi nilivyoโ€ (1Kor 7:7-8).
โ€œSi wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwaโ€ (Math 19:11).
Tunavyoona katika historia ya watawa, mara nyingi karama ya useja inaendana na nyingine katika maisha ya sala, ya kijumuia na ya kitume. Hivyo Filipo โ€œalikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiriโ€ (Mdo 21:9).


Karama zinagawiwa vipi?
Karama zinagawiwa na Roho Mtakatifu jinsi anavyotaka, si kwa sifa au faida ya binafsi, bali kwa ustawi wa taifa la Mungu.
โ€œKazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeyeโ€ฆ Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?โ€ฆ Kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisaโ€ฆ Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amaniโ€ (1Kor 12:11,29-30; 14:12,33). Kwa ajili hiyo mitume walipambanua na kuratibu karama katika ibada na katika maisha ya jumuia zisije zikavuruga Kanisa.


Karama za kushangaza zina hatari gani?
Karama za kushangaza zina hatari mbalimbali, hasa zikitiwa maanani mno. Hapo ni rahisi zilete majivuno, kijicho na mafarakano.
โ€œIkiwa kwenu kuna husuda na fitina, je, si watu wa tabia ya mwili ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?โ€ฆ Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemilikiโ€ฆ Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asiangukeโ€ (1Kor 3:3; 4:8; 10:12).
Katika mambo yasiyothibitika ni rahisi kudanganyika kuwa yametoka kwa Mungu, kumbe sivyo. Kisha kudanganyika ni vigumu kuachana nayo hata yakiwa na madhara kwa mhusika au kwa Kanisa.
โ€œWapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea dunianiโ€ (1Yoh 4:1).


Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni lipi?
Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni umoja wa Kanisa unaotokana na ustawi wa upendo na vipaji ndani ya waamini.
โ€œWote walijaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho mojaโ€ (Mdo 4:31-32).
โ€œTunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheriaโ€ (Gal 5:22-23).
โ€œLakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi; tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafikiโ€ (Yak 3:14-17).
Madhehebu yanapozidi kufarakana ni lazima tujiulize kama kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu.


Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.
Sisi ambao tulishiriki kifumbo kifo na ufufuko wake tukapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, tunaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapotulisha na kutunywesha Mwili na Damu yake ili tushiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi.
โ€œAulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimiโ€ (Yoh 6:56-57).
Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani mwetu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.


Sakramenti ya Kipaimara ni nini?
Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa


Nini maana ya Roho Mtakatifu?
Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26)


Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini nini?
Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini haya.
1. Anawatakasa
2. Anawaangaza na kuwavuta ili waende kwenye uzima wa milele


Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu Anatutakasa?
Roho Mtakatifu anatutakasa kwa njia ya Sakramenti, Visakramenti, Fadhila za Kimungu na vipaji vyake. (Yoh 16:8)


Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anatenda kazi zake?
Roho Mtakatifu anatenda kazi zake kwa njia hizi;
1. Anatuangaza kwa Mwanga wake tupate kuelewa mafundisho ya dini
2. Anatupatia neema za msaada za kutusaidia kutunza utakatifu wetu
3. Anatuvuta kwa mapendo yake tuzitumie Neema na kufika kwenye uzima wa milele.
4. Anatufariji katika shida zote. Ndio maana Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji


Kwa nini Sakramenti hii inaitwa Kipaimara?
Inaitwa Sakramenti ya Kipaimara kwa sababu inaimarisha na kukamilisha neema ya Ubatizo


Roho Mtakatifu anakuja kufanya nini rohoni mwetu kwa Kipaimara?
Anakuja kufanya yafuatayo;
1. Anakuja kutuongezea Neema ya Utakaso
2. Anatuletea pia ukamilifu wa mapaji yake saba na msaada wa kuungama imani yetu mbele za watu


Mapaji Saba ya Roho Mtakatifu ndio nini?
Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni msaada wake wa kuimarisha na kuzoesha akili na moyo wetu kwa mambo ya utumishi wa Mungu


Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni yapi?
Mapaji Hayo ni;
1. Hekima
2. Akili
3. Shauuri
4. Nguvu
5. Elimu
6. Ibada
7. Uchaji wa Mungu (Isaya 11:2)


Hekima ni nini?
Ni upendaji wa Mambo ya Mungu na Machukio ya Mambo ya Dunia


Akili ni nini?
Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu


Shauri ni nini?
Ni utaratibu wa Kuchagua Siku zote mambo yenye kufaa kwa sifs ya Mungu na kwa Wokovu wetu


Nguvu ni nini?
Ni moyo wa kushika sana Amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu, matukano, mateso wala kufa. (Rum 8:38-39)


Elimu ni nini?
Ni maarifa ya kutambua werevu na udanganyifu wa shetani; anaposhawishi mwenyewe au kwa kutumia vitu au watu. (1Pet 5:8-9)


Ibada ni nini?
Ni roho ya kupenda utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na Heshima


Uchaji wa Mungu ni nini?
Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake.


Ni nani mhudumu rasmi wa Sakramenti ya Kipaimara?
Ni Askofu halali wa Kanisa Katoliki au anaweza kumtuma Padre kutoa Sakramenti ya Kipaimara.
Katika hatari ya kufa kila padre anatoa Sakramenti ya Kipaimara. (Mdo 8:1, 1Kor 12:1-11)


Askofu ampaje Mkristo Kipaimara?
Kwanza ananyoosha Mikono juu yake akimwombea mapaji saba ya Roho Mtakatifu.
Anamwandika ishara ya msalaba katika panda la uso kwa mafuta ya Krisma Takatifu akitaja maneneo ya Sakramenti “Pokea Mhuri wa paji la Roho Mtakatifu” halafu anampiga kofi kidogo.


Ishara wazi ya Sakramenti ya Kipaimara ni nini?
Ishara wazi ya Sakramenti ya Kipaimara ni Askofu kumwekea Mkristo mikono na kumpaka Krisma Takatifu na Kusema maneneo, “Pokea muhuri wa Paji la Roho Mtakatifu”


Ina maana gani kupaka mafuta ya Krisma katika panda la uso wakati wa Kipaimara?
Inamaana kuwekwa wakfu (Yh 17:16-17).
Inamaana kuwa aliyepokea Sakramenti ya Kipaimara anapaswa kuwa tayari Kuteswa kwa kuungama Imani yake na kuishi bila woga. (Mdo 7:54-55).


Kwa nini Askofu anampiga kofi kidogo shavuni wakati akitoa Kipaimara?
Askofu anampiga kofi Kidogo Shavuni ili kumkumbusha awe mvumilivu, imara na tayari kuteseka hata kama ni kifo kwa ajili ya Yesu Kristo.


Mwenye kupokea Sakramenti ya kipaimara Yampasa nini?
Ajue mafundisho makuu ya dini na awe katika hali ya neema


Mkristo Hupokea Sakramenti ya Kipaimara Mara ngapi?
Mkristo Hupokea Sakramenti ya Kipaimara Mara moja tuu, kwa sababu Kipaimara hupiga rohoni chapa isiyofutika milele.


Je, Baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima kuendelea kujifunza Dini?
Ndiyo, Baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima kuendelea kujifunza Dini ili tuweze kuelewa na kulinda Imani yetu na kutumia vema neema ya Kipaimara.


Je, Ni lazima kila Mkristo kupokea Sakramenti ya Kipaimara?
Ni lazima kila Mkristo kupokea Sakramenti ya Kipaimara kwa sababu ni Ukamilisho wa Sakramenti ya Ubatizo. (Mdo 8:14-17)


Sakramenti ya Kipaimara inaleta manufaa gani rohoni mwa Mbatizwa?
Manufaa ya Kipaimara ni;
1. Miminiko la pekee la Roho Mtakatifu, kama la siku ya Pentekoste
2. Inachapa rohoni alama isiyofutika milele
3. Inakamilisha neema ya Ubatizo
4. Kufanya hali ya kuwa wana wa Mungu itie mizizi mirefu zaidi
5. Inaunganisha zaidi na Kristo na Kanisa lake.
6. Inastawisha vipaji vya Roho Mtakatifu rohoni
7. Inatia nguvu ya pekee kwa kushuhudia Imani ya Kristo
Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About