Mafundisho ya Katekisimu

Maswali na majibu kuhusu Katekesi

Katekista ni nani?
Katekista ni mlei aliyechaguliwa na Kanisa ili kumfanya Kristo ajulikane, apendwe, na kufuatwa na wale ambao hawajamfahamu na pia waamini


Waraka wa Baba Mtakatifu Unatafsiri vipi Makatekista?
Waraka unasema;
1. Makatekista ni Wafanyakazi maalimu
2. Mashahidi wa moja kwa moja, Wainjilishaji wasio na mbadala


Mkusanyo Sheria Kanuni za Kanisa unaelezaje kuhusu Makatekista?
Unaeleza kuwa – Makatekista ni Walei Wakristo ambao wamepewa malezi halisi na wanajitokeza vizuri katika maisha ya Ukristo wao.


Chini ya Uongozi wa Kanisa Katekista anafanya Kazi gani?
1. Yeye ni Kiungo cha Mapadre na waamini wa eneo lake
2. Kufikisha mafundisho ya Injili na kuhusika kwenye kazi za Ibada za kiliturujia na kazi za Huruma
3. Kuhubiri na kuwafundisha wakatekumeni
4. Kuelimisha vijana na watu wazima kkatika maswala ya Imani
5. Kuongoza Sala za Jumuiya hasa kwenye Ibada za Jumapili Ikiwa Padre hayupo
6. Kuwatembelea wagonjwa na kuwasaidia na kuongoza Ibada za Mazishi
7. Kufundisha dini mashuleni na kuwaandaa watoto katika kupokea Sakramenti mbalimbali
8. Kutembelea Jumuiya ndogondogo kuziendeleza na kuziimarisha

Maswali na Majibu kuhusu dhamira

Dhamiri adilifu ni nini?
Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu


Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?
Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu.


Twajenga na kutunza dhamira zetu namna gani?
Twajenga na kutunza dhamira zetu kwa;-
1. Kufuata sauti ya Roho Mtakatifu
2. Kuzingatia mafundisho ya dini
3. Kuzingatia mila na desturi njema tulizopata katika malezi.
4 Kufuata mifano na tabia njema ya wenzetu na ya Watakatifu


Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?
Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu


Dhamiri adilifu inaundwa namna gani iwe nyofu na ya kweli?
Dhamiri nyofu inayosema kweli inaundwa kwa;
1. Malezi
2. Upokeaji wa neno la Mungu
3. Upokeaji wa Mafundisho ya Kanisa
4. Sala
5. Utafiti wa dhamiri


Dhamiri adilifu inatengenezwa na kusaidiwa na nini?
Dhamiri adilifu inatengenezwa na vipaji vya Roho Mtakatifu na kusaidiwa na mashauri ya watu wenye busara.


Dhamiri inatakiwa kufuata daima masharti gani?
Dhamira inatakiwa kufuata daima masharti yafuatayo
1. Hairuhusiwi kutenda maovu kusudi yapatikane mema
2. Yoyote muyatakayo mtendewe na watu, ninyi watendeeni vivyo hivyo. (Mt 7:12)
3. Upendo hufuata daima nia na heshima kwa jirani na kwa dhamira yake

Mambo ya Msingi unayopaswa kufahamu kuhusu Ekaristi

Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?
Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.
Sisi ambao tulishiriki kifumbo kifo na ufufuko wake tukapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, tunaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapotulisha na kutunywesha Mwili na Damu yake ili tushiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi.
โ€œAulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimiโ€ (Yoh 6:56-57).
Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani mwetu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.

Ekaristi maana yake nini? Je ni kweli Yesu yupo katika Maumbo ya Mkate na Divai?
Ekaristi maana yake ni shukrani, iliyokuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu.
23Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: Kwamba, usiku ule Bwana Yesu alipotolewa, alitwaa mkate, 24akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: โ€œHuu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.โ€ 25Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: โ€œHiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.โ€
26Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana.ย (1Kor 11:23-27).
Yesu alituambia nini kuhusu Mwili wake na damu yake?
Yesu alituambia hivi;
โ€œBaba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa. 50Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni, ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โ€™โ€™ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, โ€œMtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?โ€™โ€™ 53Hivyo Yesu akawaambia, โ€œAmin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu. 58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.โ€™โ€™ย (Yoh 6:49-58)
Damu na Mwili aliotupa Yesu ni nini? Ekaristi ni nini hasa?
Maana ya Damu na Mwili aliyoisemea Yesu tunaipata hapa;
โ€œWalipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi Wake akisema,ย โ€œKuleni, huu ndio mwili Wangu.โ€™โ€™ย 23Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa wanafunzi Wake, wote wakanywa kutoka humo. 24Akawaambia, โ€œHii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25Amin nawaambia, sitakunywa tena uzao wa mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika Ufalme wa Mungu.โ€™โ€™ 26Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda kwenye Mlima wa Mizeituni.ย (Marko 14:22-26).
Kwa hiyo Yesu alionyesha upi ni mwili wake na damu yake
Fundisho hili la mwili na damu ya Yesu (Ekaristi) lilikua Agizo tunalopaswa kulitii mpaka leo?
Ndiyo, Yesu alisema tufanye hivyo kwa ukumbusho wake
โ€œKisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, โ€œHuu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu,ย fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ€ย (Luka 22: 19).
Kwa hiyo aliwaagiza Mitume wafanye hivyo pia.
Mitume walitii Fundisho la Ekaristi na waliliishi?
Ndiyo, Kila walipokutana Walishiriki Meza ya Bwana Kama tunavyosoma Kwenye vifungu vifuatavyo;.
46Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe,ย (Mdo 2:46).
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate.ย (Mdo 20:7)
Je mkate na divai vilichukuliwa na Mitume kama nini hasa? walichukulia Ekaristi kama nini?
Mitume walichukua Mkate na divai kama mwili na damu ya Yesu Kristu na walishiriki kiaminifu na kwa usafi wa moyo.
16Je, kikombe cha Baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17(Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja)ย (1 Wakorinto 10:16)
27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. 31Lakini kama tungejipambanua wenyewe tusingehukumiwa. 32Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.ย (1Wakorinto 11:27-32)
21Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na cha mashetani pia. Hamwezi kuwa na sehemu katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani. 22Je, tunataka kuamsha wivu wa Bwana? Je, sisi tuna nguvu kuliko Yeye?ย (1 Wakorinto 10:21-22)
Je ni lazima Kwa Mkristu kupokea Mwili na damu ya Yesu (Ekaristi)?
Yesu alisema hivi;
53Hivyo Yesu akawaambia, โ€œAmin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.ย (Yohana 6:53โ€“56)
Je ni kwa nini madhehebu mengine hawakubali mafundisho haya ya Ekaristi Takatifu, Je ni mara ya kwanza watu kukataa?
Hii ni sababu ya ugumu wa mioyo na kutokuelewa maandiko ndio maana madhehebu mengine wanaukataa kwa dhati Mwili na Damu ya Yesu.
Hata wakati Yesu akiyasema maneno haya Wafuasi Wengi Walimwacha kama Biblia inavyosema;
60Wengi wa wafuasi Wake waliposikia jambo hili wakasema, โ€œMafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?โ€™โ€™ย (Yohana 6:60).
Haishangazi hata leo weni hawaamini mafundisho haya japokua ndio msingi wa Imani ya Kikristo.
Mitume walifundisha nini kuhusu Mwili na Damu ya Kristu (Ekaristi)?
23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema โ€œHuu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ€ 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, โ€œKikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.โ€ 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa.ย (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume waliwaasa Wakristu wa kwanza Kushiriki Mwili na Damu ya Yesu kila mara na kwa Uaminifu.
Je Yesu Yupo Mzima katika Ekaristi Takatifu? Na kwa nini Tunaabudu Ekaristi?
Ndiyo. Ekaristi Takatifu inamuwakilisha Yesu Mwenyewe aliye Mungu na aliyeamua Mwenyewe kuwepo katika Maumbo ya Mkate na Divai.
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โ€™โ€™ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, โ€œMtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?โ€™โ€™ 53Hivyo Yesu akawaambia, โ€œAmin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.ย (Yoh 6:51-57)
Mstari wa 51 Yesu alisema wazi Mkate huo ni Mwili wake.
Thamani na Uwepo wa Yesu Mwenyewe unaonekana katika Mstari wa 53 na wa 56. Kumbuka hapa amesema “Mimi nitakaa ndani yake” Hakusema Mwili wangu utakaa ndani yake. Kwa maana nyingine ni kwamba Ekaristi ni Yesu Mzima na Sio Mwili tuu.
54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
Wale Wanaopinga fundisho la Ekaristi wanafikiri Yesu alivyosema Mimi ni Chakula Kutoka Mbinguni hakumaanisha Mwili bali Maneno na Imani Kwake lakini Tukisoma 51 Yesu alisema wazi kuwa Mwili wake ndio Mkate wenyewe.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele.ย Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โ€™โ€™
Mitume wa Yesu walielewa hivi fundisho hili ndio Maana walishiriki Meza ya Bwana kila walipokutana na waliheshimu kama Mwili na Damu ya Kristo.
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate.ย (Mdo 20:7)
Ili kujua kuwa Mitume waliheshimu Mwili na Damu ya Yesu Biblia inatuambia hivi;
23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema โ€œHuu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ€ 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, โ€œKikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.โ€ 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa.ย (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume walisisitiza kuhusu Mwili na Damu ya Kristu kuwa ni Mtakatifu.
Kwa hiyo basi kama tunavyosoma katika Yoh 6:51; na
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โ€™โ€™
Yesu alisema Mimi ni Mkate wa Uzima ambao alimaanisha upo katika Mwili wake. Mwili tuu hauna uzima kama hauna Yesu ndani yake. Kwa sababu Mwili ni Mzima na Unaye Yesu ndani yake ndiyo maana unaweza kuleta uzima kwa Wengine.
Tunaelewa kwamba Yesu alijitoa Msalabani Mwili Wake na Damu yake na ndicho alichotupa ktk Ekaristi. Na Mwili wake huo Ulikua umembeba yeye aliye Mungu ndiyo maana tunaabudu Ekaristi alipo Yesu aliye Mungu.
Kwa kuwa Yesu ni Mungu Kama tunavyosoma katika Yoh 1:1-12
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watuโ€ฆโ€ฆ..14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.ย (Yoh 1:1-12)
Kwa hiyo Neno huyo huyo Ndiye aliyetukomboa kwa kuutoa mwili wake sadaka Msalabani na ndiye Aliyetupa Mwili Wake na Damu yake ktk Ekaristi na anaabudiwa kwa kuwa yupo katika mwili huo.
โ€œKisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, โ€œHuu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ€ย (Luka 22: 19).
Kwa namna hii alitupa mwili wake.
Alisema fanyeni kwa ukumbusho wangu na Sio wa mwili wangu.
Hivyo Ekaristi ni Yesu Mwenyewe aliye Mungu. Ndiyo sababu tunaabudu Ekaristi Takatifu.

Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu gani?
Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika utamaduni wake na katika Agano la Kale.
Vilikuwa chakula cha kawaida na kinywaji cha karamu.
โ€œDivai imfurahishe mtu moyo wakeโ€ฆ na mkate umburudishe mtu moyo wakeโ€ (Zab 104:15).
Vilitokana na chembe za ngano na matunda ya mzabibu ambavyo Yesu alijifananisha navyo.
โ€œAmin, amin, nawaambia: Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengiโ€ (Yoh 12:24).
โ€œMimi ni mzabibu, ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno loloteโ€ (Yoh 15:5).
Baada ya kulimwa, vilihitaji kusagwa au kushinikizwa, matendo yanayodokeza tena mateso yake pamoja na kazi ya binadamu. Pia wingi wa chembe na wa zabibu zinazoungana ziwe mkate na divai unamaanisha umoja wa waamini ndani ya Kristo. Kwa hiyo ni lazima tutumie daima mkate na divai, si vitu vingine.
Ikumbukwe piaย โ€œMelkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sanaโ€ย (Mwa 14:18),ย โ€œamefananishwa na Mwana wa Munguโ€ (Eb 3:7).ย Alimtolea Mungu kama sadaka

Mara nyingi waamini wanapokea umbo la mkate tu kwa lengo gani?, Kwa nini hatupokei mwili na damu, tunapokea mwili tuu?
Mara nyingi waamini wanapokea umbo la mkate tu kwa lengo la kukwepa umwagaji wa Damu ya Kristo na kurahisisha ibada, hasa kama washiriki ni umati (hata milioni 4 katika misa moja).
Yesu mwenyewe alizungumzia mkate kuliko divai, kwa sababu chakula ni muhimu kuliko kileo.
โ€œMimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwenguโ€ (Yoh 6:51).
Kwa maana hiyo hiyo, Mitume nao walizungumzia Mkate kuliko Divai.
โ€œKwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmojaโ€ (1Kor 10:17).
Mkate ni mwili na Divai ni Damu. Unaposema mwili umeshahusisha na Damu tayari.
Anayekula umbo la mkate hapokei sehemu tu ya Yesu, bali anampokea mzima, Mwili, Damu, Roho na Umungu. Pamoja na hayo, daima ni lazima walau padri anywe umbo la divai.
Hakuna nyama isiyokua na damu, damu hutoka kwenye nyama na sio nyama kwenye damu. Ukila nyama umekula na damu pia

Je, divai (pombe) ni halali?
Ndiyo, divai ni halali, mradi itumike kwa kiasi isije ikaleta madhara.
โ€œMelkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sanaโ€ (Mwa 14:18), โ€œamefananishwa na Mwana wa Munguโ€ (Eb 3:7).
โ€œBwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sanaโ€ (Isa 25:6).
โ€œNjoo, ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganyaโ€ (Mith 9:5-6).
Yesu alishiriki karamu nyingi na katika mojawapo ndipo alipoanza miujiza yake kwa kugeuza mapipa ya maji kuwa divai bora.
โ€œKila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasaโ€ (Yoh 2:10).
Tujihadhari na hoja za kibinadamu zinazoelekea kumlaumu kwa ajili hiyo, kama wengine walivyofanya zamani zake:
โ€œMwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, nanyi mwasema, โ€˜Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambiโ€ (Lk 7:34).

Hatimaye Yesu alitumia divai kufanyia nini?
Kama alivyofanya Melkizedeck anayefananishwa na Yesu. โ€œMelkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sanaโ€ (Mwa 14:18), โ€œamefananishwa na Mwana wa Munguโ€ (Eb 3:7). Alimtolea Mungu kama sadaka
Hatimaye Yesu alitumia divai kutuachia ishara ya damu yake tuweze kushiriki mateso yake. โ€œJe, mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?โ€ (Math 20:22). Kisha kushiriki kila mwaka karamu ya Pasaka, ambapo wote walikunywa divai mara nne, safari ya mwisho alikamilisha miujiza yake kwa kuigeuza iwe damu yake. โ€œโ€˜Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Munguโ€™. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, โ€˜Twaeni hiki, mgawanywe ninyi kwa ninyi; maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokujaโ€™. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, โ€˜Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wanguโ€™. Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula, akisema, โ€˜Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenuโ€™โ€ (Lk 22:15- 20). โ€œKikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo?โ€ (1Kor 10:16).

Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa nini?
Katika karamu ya Bwana tunakula na kunywa Mwili wa Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi padri anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai, Roho Mtakatifu anavigeuza kwa dhati: mkate si tena mkate, wala divai si tena divai, ingawa maumbo yanabaki yaleyale kwa hisi zetu.
โ€œAulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweliโ€ (Yoh 6:54-55).
โ€œBasi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwanaโ€ (1Kor 11:27).

Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi mpaka lini?
Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria.
Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni.
โ€œTomaso alijibu, akamwambia, โ€˜Bwana wangu na Mungu wangu!โ€™ Yesu akamwambia, โ€˜Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadikiโ€ (Yoh 20:28-29).

Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?
Ndiyo, ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu wetu.
โ€œYeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombeeโ€ฆ Kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoaโ€ (Eb 7:24-25; 8:3).
Katika ekaristi tunajiunga naye kwa kufanya ukumbusho wa kifo na ufufuko wake, tukimtolea tena Baba sadaka ya Mwili na Damu yake iliyolinganishwa na zile za Waisraeli na za Wapagani:
โ€œWaangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je, hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.ย Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetaniโ€ย (1Kor 10:18-21).

Kwa nini ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo?
Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila tunapofanya ukumbusho wa sadaka hiyo pekee tunazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesuย โ€œali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeoโ€ (Yoh 13:1).
Hivyo tunawezeshwa kutekeleza amri mpya aliyotuachia pamoja na ekaristi.
โ€œAmri mpya nawapa: Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyoโ€ (Yoh 13:34).
Ni sharti tujitoe kama Yesu, tukijiunga na sadaka yake katika ibada na katika maisha.
โ€œKatika hili tumelifahamu pendo: kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma yake, je, upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweliโ€ (1Yoh 3:16-18).

Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio gani?
Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio wa kupanda: tunalishwa Neno la Mungu katika mimbari, halafu Mwili na Damu ya Kristo katika altare. Vilevile sehemu ya kwanza (liturujia ya Neno) inatuletea masomo yakiwa na kilele katika Injili. Halafu katika sehemu ya pili (liturujia ya ekaristi) padri anafuata alichofanya Yesu katika karamu ya mwisho: anatwaa mkate na divai (kuandaa dhabihu zetu), anashukuru juu yake (sala kuu ya ekaristi inayogeuza dhabihu) na kuwapa waamini (komunyo, kilele cha yote, inayotugeuza ndani ya Kristo).
Yesu mfufuka โ€œaliwaeleza katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyeweโ€ฆ Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambuaโ€ (Lk 24:27,30-31).
โ€œWakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusaliโ€ (Mdo 2:42).
โ€œSiku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubuโ€ฆ akamega mkate, akalaโ€ (Mdo 20:7,11).
Tusipofuata vizuri hatua za awali, hatutafaidika kweli na sakramenti: ndiyo sababu ni muhimu tuwahi ibada.

Sakramenti ya Ekaristi ni nini?
Sakramenti ya Ekaristi ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo, aliye kweli katika Maumbo ya Mkate na Divai. (Yoh 6:1-17, Mt 26:26-28)

Yesu Kristo alianzisha lini Sakramenti ya Ekaristi?
Yesu Kristo alianzisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu jioni ya Alhamisi kuu yaani usiku ule kabla ya kukutwaliwa kwenye mateso na msalaba.
14 Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake. 15 Akawaambia, โ€œNimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16 Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.โ€
17 Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akasema, โ€œPokeeni, mgawane. 18Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.โ€
19 Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, โ€œHuu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu.ย 
Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.โ€ย 20 Akafanya vivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akisema, โ€œKikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenuย (Lk 22:14-20)
Mitume nao walilipokea Agizo la Ekaristi na kulifuata kwa Heshima huku wakiamini wanashiriki Mwili na Damu ya Yesu Kristu
23 Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: Kwamba, usiku ule Bwana Yesu alipotolewa, alitwaa mkate, 24 akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: โ€œHuu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.โ€ 25 Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe cha divai, akasema: โ€œHiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.โ€ 26ย Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi yaย Mwili na Damu ya Bwana.ย (1Kor 11:23-27)

Yesu Kristo alianzishaje Ekaristi Takatifu?
Yesu alitwaa mkate mikononi mwake, akashukuru, akaumega, akawapa mitume wake akisema: “TWAENI MLE WOTE: HUU NDIO MWILI WANGU UTAKAOTOLEWA KWA AJILI YENU”
Kisha akatwaa kikombe cha Divai mikononi mwake akawaambia: “TWAENI MNYWE WOTE HIKI NI KIKOMBE CHA DAMU YANGU: DAMU YA AGANO JIPYA NA LA MILELE ITAKAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU NA KWA AJILI YA WENGI KWA MAONDOLEO YA DHAMBI: FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU” (Mt 26:26, 1Kor 11:23-35)

Ni kwa nini ni Kweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai?
Nikweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai kwa sababu
1. Kwa kuwa hakuna kisichowezekana kwa Mungu (Lk 1:37)
2. Kwa kuwa Yesu aliahidi kutupatia chakula kutoka Mbinguni yaani Mwili na Damu yake Takatifu. (Yoh 6:41)
3. Kwa kuwa Yesu ni Mungu na akaita mkate ni mwili wake na divai ni damu yake basi lazima viwe hivyo. (Mt 26:26-27, Lk 22:14-20, Mk 14:22-26)
4. Kwa kuwa ni lazima anayetaka kuwa na uzima wa milele aule, hata leo katika maneno ya Padri Yesu huwa katika Maumbo hayo. (Yoh 6:53-56).

Ni wakati gani katika Misa Mkate na Divai vinageuka Mwili na Damu yake Kristo?
Ni katikati ya Misa padri asemapo maneno Matakatifu aliyosema Yesu mwenyewe: “HUU NDIO MWILI WANGU; HII NDIO DAMU YANGU”
26 Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akamshukuru Mungu, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, โ€œTwaeni mle; huu ni mwili wangu.โ€ 27 Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akawapa akisema, โ€œKunyweni nyote; 28 maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi. 29 Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.โ€
30 Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni.ย (Mat 26:26-30)

Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?
Majina haya;
1. Ekaristi Takatifu
2. Karamu ya Bwana
3. Misa Takatifu
4. Sakramenti Takatifu ya Altare
5. Komunyo Takatifu
6. Sadaka Takatifu
7. Kumega Mkate

Baada ya Mitume kufa ni nani wanafanya Sakramenti ya Ekaristi
Badaa ya Mitume kufa Maaskofu na Mapadri wanaendelea kuadhimisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu

Ni lini Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake?
Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake alipowafanya Mitume kuwa Mapadri katika karamu ya mwisho aliposema “FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU” (Lk 22:14-20)

Je, Divai iliyotumiwa na Yesu ilikua na Kilevi (pombe)?
Ndiyo, Divai aliyoitumia Yesu kuigeuza kuwa damu yake ilikua na kilevi kwa sababu kwa kawaida kipindi cha Pasaka sio msimu wa kuvuna zabibu na hakukuwa na njia yoyote ya kufanya juisi yake isiwe kilevi. Kwa hiyo hakukuwa na uwezekano wa kupata juisi ya zabibu isipokua mvinyo wa zabibu wenye kilevi. Vile vile Wayahudi walikua na desturi ya kutumia Mvinyo wa zabibu kama kinywaji cha sikukuu ya pasaka.
Hakuna sehemu kwenye Bilia tunaambiwa kwamba ulifanyika Muujiza wa Kufanya Divai isiwe kilevi. Biblia inatuambia kuwa Mitume kila walipokutana Walishiriki Meza ya Bwana. Haikutuambia walishiriki meza ya Bwana tuu Kipindi cha kukamua Zabibu.
Biblia inatuthibitishia kuwa Divai aliyotumia Yesu na Mitume ilikua na kilevi kwa kusema kuwa wengine walikuwa wakilewa katika Meza ya Bwana (Wakorinto 11:22).
Biblia haituambii kuwa Yesu alitumia Divai isiyo na kilevi. Wala Yesu hakuwahi kuonya kuhusu kutumia Divai yenye Kilevi. Yesu katika Umungu wake angeweza kujua kuwa miaka ijayo Divai ambayo ingetumika ingekuwa na Kilevi kwa hiyo angeonya Matumizi yake.
Divai iliyotumiwa na Yesu na Mitume ilikua na Kilevi ndio maana Mitume waliwaonya wakristo wa kwanza juu ya ya kushiriki vibaya Meza ya Bwana mfano kulewa kama tunavyosoma kwenye mistari ifuatayo.
17Basi katika maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu, kwa sababu mkutanikapo si kwa ajili ya faida bali kwa hasara. 18Kwanza, mnapokutana kama kanisa, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo. 19Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili kuonyesha ni nani anayekubaliwa na Mungu. 20Mkutanikapo pamoja si chakula cha Bwana mnachokula, 21kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine, huyu hukaa njaa naย mwingine analewa.ย 22Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha! 23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema โ€œHuu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ€ 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, โ€œKikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.โ€ 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. 31Lakini kama tungejipambanua wenyewe tusingehukumiwa. 32Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadabishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane. 34Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa. Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.(Wakorinto 11:17-29)
Kwa hiyo hata Mitume na Wakristu wa kwanza walitumia divai yenye kilevi kwenye Meza ya Bwana (Ekaristi) ndio maana kuna waliolewa.

Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu ngapi?
Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu tatu
1. Matayarisho ya vipaji
2. Sala ya Ekaristi
3. Ibada ya Komunyo

Ni vitu gani vya msingi na vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu?
Vitu vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu ni
1. Mkate wa Ngano
2. Divai ya mzabibu

Kabla ya Kupokea Ekaristi Takatifu Tunasali sala gani?
Tunasali “Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona”

Katika Ekaristi Takatifu Tunampokea nani?
Katika Ekaristi Takatifu Tunampokea Yesu Kristo Katika Maumbo ya Mkate na Divai na tunaungana naye (Yoh 6:57)

Mkristo awe katika hali gani kabla ya kupokea Ekaristi Takatifu?
1. Awe na Neema ya Utakaso yaani asiwe na dhambi ya mauti.
2. Awe na Imani, Ibada na Kumtamani Yesu.
3. Afunge chakula Muda wa saa Moja na Kileo zaidi ya masaa matatu.
4. Awe safi kimwili.
5. Awe na adabu na heshima.

Komunyo Takatifu Hutuletea neema gani?
1. Hulinda na kuongeza neema ya Utakaso iliyo uzima wa roho zetu.
2. Hutuondolea dhambi ndogo na kupunguza hatari ya kutenda dhambio kubwa.
3. Hututia bidii na nguvu ya kutenda mema kwa kutuongezea Imani, Matumaini na Mapendo.
4. Huleta Umoja katika Kanisa, sio sisi na Kristo tuu bali sisi kwa sisi.

Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi rohoni anatenda dhambi gani?
Mkristo akipokea Ekaristi Takatifu akiwa na dhambi anatenda dhambi kubwa yaani kufuru Sakramenti.
26 Maana kila mnapokula mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja. 27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana.ย (1 Kor 11;26 – 27)
28Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho; 29 maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe. 30 Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kadhaa wamekufa. 31 Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo. 32Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.ย (1 Kor 11;28 – 32)

Je, Kanisa linahimiza waamini wapokee Ekaristi wakati gani?
Kanisa linahimiza waamini wapokee Komunyo Takatifu kila siku wanaposhiriki Misa

Nani Mhudumu wa adhimisho la Ekaristi Takatifu?
Mhudumu wa adhimisho la Ekaristi Takatifu ni Askofu na Padre

Je, Mkristo akipokea kipande cha Hostia amempokea Yesu Mzima?
Ndiyo, Amempokea Yesu Mzima kabisa, Hata akipewa zaidi ya hostia moja amempokea Yesu Mzima

Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa wapi?
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa kwenye Tabernakulo

Tabernakulo ni nini?
Tabernakulo ni mahali Patakatifu anapokaa Yesu wa Ekaristi siku zote

Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa sababu gani
Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa ajili ya watu wote hasa wagonjwa

Ishara wazi ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni nini?
Ishara wazi ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni maumbo ya mkate na divai, na maneneo ya mageuzo ya Yesu mwenyewe Padri akiyatamka.

Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi tufanye nini?
Baada ya kumpokea Yesu wa Ekaristi: Tumwabudu,tumshukuru, tumwombe kwani yeye ni Mwenyezi. (Mt 2:11, Lk 17:11)

Komunyo pamba ndio nini?
Komunyo pamba ndio Ekaristi inayopokelewa na wale wanaokaribia kuaga maisha ya duniani na wanaojiandaa kuvukia uzima wa milele

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu tofauti za kijamii na uadilifu wa kijamii?

Kanisa Katoliki limekuwa likitetea uadilifu wa kijamii na tofauti za kijamii kama sehemu ya imani yake. Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki, kila mtu ana haki ya kuishi kwa heshima, kuheshimiwa na kuthaminiwa, bila kujali tofauti zao za kijamii. Tofauti za kijamii zinaweza kujumuisha mambo kama vile utajiri, umaskini, kabila, jinsia, au hata dini. Kuna mambo kadhaa yanayofundishwa na Kanisa Katoliki kuhusu tofauti za kijamii na uadilifu wa kijamii.

Kwanza, Kanisa Katoliki linatambua kuwa kila mtu ana thamani sawa mbele ya Mungu. Kwa hiyo, yeyote yule anayewakandamiza watu wengine kwa sababu ya tofauti zao za kijamii anakuwa anakiuka sheria za Mungu. Kama ilivyoelezwa katika Kitabu cha Mwanzo 1:27, "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba." Kwa sababu hiyo, tunapaswa kuwa wema kwa watu wa rangi ya ngozi, kabila, jinsia, umaskini, utajiri, na tofauti zingine zote za kijamii.

Pili, Kanisa Katoliki linaamini kuwa Mungu anatupenda sote sawa. Kama ilivyoelezwa katika Waraka wa Mtakatifu Paulo kwa Wagalatia 3:28, "Hakuna tena Myahudi wala Myunani; wala mtumwa wala huru; wala mwanamume wala mwanamke; kwa kuwa nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu." Kwa sababu hiyo, sisi sote ni sawa mbele ya Mungu, na hakuna mtu mwingine anayeweza kujivunia kuwa bora kuliko mtu mwingine.

Tatu, Kanisa Katoliki linaamini kuwa sisi sote ni majirani zetu, na tunapaswa kushirikiana kwa upendo na huruma. Kama alivyoeleza Yesu katika Injili ya Mathayo 22:39-40, "Na amri ya pili ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili zote hutegemea torati na manabii." Kwa hiyo, ni muhimu kwetu kuishi kwa amani na upendo na majirani zetu, bila kujali tofauti zetu za kijamii.

Nne, Kanisa Katoliki linatambua kuwa kuna tofauti za kijamii, lakini linataka kuona usawa wa kijamii unaotokana na uwajibikaji wa kijamii. Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, "Katika jamii ya binadamu, kuna tofauti za kiuchumi, utamaduni, na kijamii; na kwa hiyo, ni wajibu wa raia na serikali kuweka sheria na mipango ya kijamii inayolinda haki za binadamu, inapigania ustawi wa pamoja wa jamii, na inahakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii." Kwa hiyo, Kanisa Katoliki linataka kuona kila mtu anapata haki sawa kwa maendeleo, na kwamba hakuna mtu mwingine anayeonewa kwa sababu ya tofauti za kijamii.

Hatimaye, Kanisa Katoliki linataka kuona ulimwengu unaishi kwa amani na upendo. Kwa kufuata mafundisho ya Yesu, tunaweza kuishi kwa amani na upendo, na kuheshimu tofauti za kijamii. Kama ilivyoelezwa katika Injili ya Luka 10:27, "Naye akajibu, akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako; na jirani yako kama nafsi yako." Kwa hiyo, kwa kufuata amri hizi mbili, tunaweza kuishi kwa amani na upendo na kuheshimu tofauti za kijamii.

Kwa ufupi, Kanisa Katoliki linatetea uadilifu wa kijamii na tofauti za kijamii kwa sababu ya imani yake katika Mungu wa upendo na huruma. Kwa kufuata mafundisho ya Kanisa Katoliki, tunaweza kuishi kwa amani na upendo, na kuheshimu tofauti za kijamii. Kwa hiyo, ni muhimu kwetu kuelewa tofauti za kijamii na kujitahidi kuishi kwa amani na upendo na majirani zetu, bila kujali tofauti zetu za kijamii.

Maswali na Majibu kuhusu Mafumbo ndani ya Kanisa Katoliki

Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?
Laitwa fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk, 3:21-22)


Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?
Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15)


Nini maana ya neno “Fumbo”?
Fumbo ni ukweli ambao hatuwezi kuelewa kikamilifu, lakini tunasadiki kwa kuwa Mungu hutufumbulia. (Math 11:27)


Katika dini yetu yapo mafumbo hasa mangapi?
Mafumbo matatu
1. Fumbo la Utatu Mtakatifu
2. Fumbo la Mungu Kujifanya mtu
3. Fumbo la Ukombazi wetu

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu Ishara ya Msalaba

Ishara ya msalaba ni nini?
Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?
Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?
Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?
Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?
Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?
Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki katika jamii?

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki katika jamii? Jibu ni ndiyo! Kanisa Katoliki linaamini kuwa uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki ni sehemu muhimu ya imani ya Kikristo. Kama Wakatoliki, tunapaswa kuishi kwa mfano wa Yesu Kristo, ambaye alikuwa mshikamano na watu wote, na aliwajali wote bila ubaguzi.

Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, kila mtu ni mwenye heshima kwa sababu yeye ni waumba wa Mungu. Kwa hiyo, tunapaswa kuwatendea wote kwa heshima na upendo. Hii inamaanisha kwamba hatupaswi kuwabagua watu kwa msingi wa jinsia zao, rangi ya ngozi, au hali yao ya kiuchumi. Badala yake, tunapaswa kuwajali wote, na kuwapa haki sawa, upendo, na msaada wanaohitaji.

Bible inakumbusha kwetu kuwa "Basi, kwa sababu ya hili, ni lazima kumtii mtawala, si kwa sababu ya adhabu tu, bali kwa sababu ya dhamiri yako pia. Kwa sababu hii pia mliwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakishughulikia kazi yao kwa bidii. Mlipeni kila mtu kodi yake; yeye ambaye kodi, kodi; yeye ambaye ushuru, ushuru; yeye ambaye hofu, hofu; yeye ambaye heshima, heshima" (Warumi 13:5-7). Kwa kufuata kanuni hizi, tunaweza kuishi kwa amani na kwa kufurahia maisha mema na mazuri.

Kanisa Katoliki pia linatuhimiza kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki. Kwa mujibu wa Catechism, "ubaguzi ndio upinzani wa Mungu kwa sababu ni kukiuka heshima ya watu wengine kama waumba wa Mungu" (CCC1935). Tunapaswa kushughulikia ubaguzi katika jamii kwa kuelewa kuwa ubaguzi una madhara makubwa kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla.

Kama Wakatoliki tunafundishwa kupigana dhidi ya ubaguzi na ukosefu wa haki. Biblia inatufundisha kuwa "Mungu hana upendeleo" (Matendo ya Mitume 10:34), na tunapaswa kuishi kwa mfano wa Kristo, ambaye alikuwa mshikamano na watu wote, bila ubaguzi. Hii inamaanisha kwamba tunapaswa kupinga ubaguzi wa aina yoyote, iwe ni ubaguzi wa rangi, jinsia, kabila, au hali ya kiuchumi.

Kwa ufupi, Kanisa Katoliki linawaalika waamini wake kuishi kwa uadilifu wa kijamii na kupinga ubaguzi na ukosefu wa haki katika jamii. Tunapaswa kuishi kwa mfano wa Kristo, ambaye alikuwa mshikamano na watu wote, na aliwajali bila ubaguzi. Kwa kufuata kanuni hizi, tunaweza kuishi kwa amani na kwa kufurahia maisha mema na mazuri.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu utunzaji wa mazingira?

Kanisa Katoliki limekuwa likitangaza utunzaji wa mazingira kama jukumu la kikristo kwa miaka mingi. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba tunalinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo. Utunzaji wa mazingira ni kazi yetu sote na inatokana na imani yetu ya kikristo na maadili tunayoyafuata.

Katika kitabu cha mwanzo 2:15, Mungu anamwamuru Adamu awatunze na kuilinda bustani ya Edeni. Kwa hivyo, imani ya Kanisa Katoliki inaamini kwamba sisi ni wasimamizi wa mazingira na tunapaswa kulinda kila aina ya uhai uliopo. Kwa kufanya hivyo, tunawajibika kwa Mungu na kwa vizazi vijavyo.

Kanisa Katoliki linategemea falsafa ya kiekumene katika kutunza mazingira. Falsafa hii inasema kwamba binadamu na mazingira ni sehemu moja ya ulimwengu mmoja. Tunapata maisha yetu kutoka kwa mazingira na kwa hivyo, tunapaswa kuilinda mazingira kama sehemu ya jukumu letu la kibinadamu.

Vilevile, imeandikwa katika KKK 2402, "uharibifu wa mazingira ni kinyume cha maadili na inaweza kuathiri maisha ya watu." Kwa hivyo, Kanisa linasisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kama sehemu ya maadili yetu.

Katika Mkutano wa Mazingira wa Vatican uliofanyika mnamo 2019, Baba Mtakatifu Francis aliwataka watu wote kuchukua hatua za kuhifadhi mazingira. Aliwataka wakristo kuhakikisha kwamba wanawajibika kwa kufuata mafundisho ya kanisa na kuishi maisha yenye kuheshimu mazingira.

Kwa hivyo, tunapaswa kulinda mazingira kwa kufuata kanuni za utunzaji wa mazingira kama vile kupunguza utumiaji wa plastiki na kukuza utumiaji wa nishati mbadala. Tunapaswa pia kuhakikisha kwamba tunatumia rasilimali za dunia kwa njia yenye uwajibikaji na kwa kuzingatia mahitaji ya vizazi vijavyo.

Kwa kuhitimisha, Kanisa Katoliki linatukumbusha kwamba utunzaji wa mazingira ni jukumu letu kama wakristo. Tunapaswa kuhakikisha kwamba tunatumia rasilimali za dunia kwa njia yenye uwajibikaji na kuheshimu kila aina ya uhai uliopo. Tunapaswa kuwa wasimamizi wa mazingira na kutoa mfano wa maisha yenye kuheshimu mazingira kwa vizazi vijavyo.

Je, Kanisa Katoliki linapinga utoaji mimba na kuhimiza kulinda na kuheshimu uhai wa watoto wachanga?

Karibu kwenye makala hii, ambapo tutajadili suala la utoaji mimba na jinsi Kanisa Katoliki linavyolipinga. Katika maandiko matakatifu, tunaambiwa kuwa kila uhai ni takatifu na kwamba hatuna haki ya kuutoa kwa namna yoyote ile. Hivyo, Kanisa Katoliki linahimiza kulinda na kuheshimu uhai wa watoto wachanga kwa kila njia.

Suala la utoaji mimba ni suala tata sana ambalo limegawanya jamii kwa muda mrefu sasa. Kwa upande wa Kanisa Katoliki, utoaji mimba ni dhambi kubwa, kwani kila mtoto aliyeumbwa na Mungu ana haki ya kuishi. Tunaambiwa katika Kitabu cha Zaburi 139:13-14 kuwa "wewe ndiwe uliyeniumba viungo vyangu, wewe umenifuma tumboni mwa mama yangu. Nitakusifu kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha; maana ya matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana."

Kwa hivyo, kila mtoto aliyeumbwa tumboni mwa mama yake ana thamani na haki ya kuishi, na hatuna haki ya kumnyima uhai wake. Hii ndiyo sababu Kanisa Katoliki linapinga utoaji mimba kwa nguvu zote.

Vile vile, Kanisa Katoliki linahimiza kulinda uhai wa watoto wachanga kwa kila njia. Kulingana na Katekisimu ya Kanisa Katoliki, kila mtoto aliyezaliwa ana haki ya kuwa na heshima na kulindwa, kwani kila mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Tunasoma katika Kitabu cha Isaya 44:24 kuwa "Bwana, Mkombozi wako, ndiye aliyekuumba tangu tumboni, asema hivi: Mimi ndiye Bwana, nifanyaye vitu vyote."

Kwa hiyo, kama Wakatoliki, tunapaswa kuheshimu na kulinda uhai wa watoto wachanga, kwani wanathaminiwa sana na Mungu. Tunapaswa kuwasaidia na kuwapa upendo wote wanahitaji ili kufikia ukuaji wao kamili.

Kwa kuhitimisha, Kanisa Katoliki linapinga utoaji mimba na kuhimiza kulinda na kuheshimu uhai wa watoto wachanga. Kwa kuzingatia maandiko matakatifu na kanuni za Kanisa, tunajifunza kwamba kila uhai ni takatifu na thamani yake ni kubwa. Kama Wakatoliki, tunapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda uhai wa watoto wachanga na kuwasaidia katika safari yao ya maisha.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About