Mafundisho ya Katekisimu

Mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu kuhusu Sakramenti ya Daraja

Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?
Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani.
โ€œJitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyeweโ€ (Mdo 20:28).
โ€œHakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisaโ€ (Ef 5:29-32).


Je, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa?
Ndiyo, daraja takatifu zinahitajiwa kabisa na Kanisa kwa sababu kazi ya wokovu haimtegemei binadamu, bali Mungu.
โ€œHapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni. Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuuโ€ (Eb 5:4-5),
Yesu alisisitiza alivyopewa na Baba uwezo wa kutuokoa. โ€œBaba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwakeโ€ (Yoh 3:35).
โ€œKama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa mileleโ€ (Yoh 17:2)
.
Kisha kufufuka alitumia mamlaka hiyo kuwatuma wanafunzi kumi na mmoja waliobaki:
โ€œNimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahariโ€ (Math 28:18-20).
Mpaka mwisho wa dunia uwezo huo wa Kimungu utatolewa tu kwa sakramenti ya daraja, inayounganisha mtu na Mitume kupitia mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono ili kushirikishwa mamlaka. Bila yake, kuna upungufu katika ufundishaji, utoaji wa sakramenti na uongozi.


Je, wenye daraja wanastahili heshima?
Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo.
โ€œAmin, amin, nawaambieni: Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenipelekaโ€ (Yoh 13:20).
โ€œJaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Kristo Yesuโ€ (Gal 4:14).
โ€œUwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutiiโ€ (Tito 3:1).
Wenye daraja wanaotimiza kazi zao vizuri wanastahili heshima kwa uaminifu wao pia.
โ€œWazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu, hasa hao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundishaโ€ (1Tim 5:17).


Je, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi?
Ndiyo, wenye daraja wanaweza wakatenda dhambi kwa sababu ni binadamu kama sisi sote. Yesu alionja ukosefu wa Mitume hasa wakati wa mateso.
โ€œJe, mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?โ€ (Yoh 6:70).
โ€œTazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao, na kuniacha mimi peke yanguโ€ (Yoh 16:32).
Paulo alionya mapadri, โ€œKatika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie waoโ€ (Mdo 20:30).


Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa kufanya nini?
Ili tuwe na wachungaji wengi waaminifu tunapaswa hasa kusali.
โ€œMwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yakeโ€ (Math 9:38).
Halafu yanahitajika maandalizi ya muda mrefu, juhudi na ushirikiano wa kidugu.
โ€œAsiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisiโ€ฆ Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao piaโ€ฆ Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengineโ€ (1Tim 3:6; 4:16; 5:22).


Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?
Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote.
โ€œPetro, na Yohane, na Yakobo, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo wa Alfayo, na Simoni Zelote, na Yuda wa Yakobo. Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zakeโ€ฆ Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiyaโ€ฆ kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmojaโ€ (Mdo 1:13-14,23,26).
โ€œWalimchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yaoโ€ (Mdo 6:5-6).


Je, kutoa daraja kwa wanaume tu ni kuwakosea haki wanawake?
Hapana, kutoa daraja kwa wanaume tu si kuwakosea haki wanawake, kwa kuwa hizo ni huduma zinazofaidisha wote.
โ€œMaana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikayeโ€ (Lk 22:27).
Mwenye daraja anahudumia Kanisa kwa kumwakilisha Yesu; hivyo anatakiwa kuwa mwanamume kama yeye mbele ya Bibiarusi wake. Kukubali mgawanyo wa majukumu maishani ni kusifu hekima ya Mungu aliyetuumba watu wa jinsia mbili tofauti ili kustawisha familia, jamii na Kanisa.
โ€œWalakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwanaโ€ฆ Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yakeโ€ (1Kor 11:11; 12:27).


Je, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa?
Ndiyo, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa.
โ€œHatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?โ€ (1Kor 9:5).
Paulo, akiwa mseja, hakudai kila mmojawao aoe, ila asiwe ameoa mara mbili, bali โ€œmume wa mke mmojaโ€ (1Tim 3:2; Tit 1:6), kama alivyoagiza mjane aandikishwe akiwa tu โ€œmke wa mume mmojaโ€ (1Tim 5:9).
Polepole mangโ€™amuzi yakaelekeza Kanisa kubana nafasi hiyo kwa Maaskofu, na katika majimbo mengi kwa mapadri pia. Useja mtakatifu unawalinganisha zaidi na Yesu na kuwaachia uhuru wa moyo na wa muda kwa ajili ya huduma.
โ€œWako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokeeโ€ (Math 19:12).


Ni zipi Sakramenti za Huduma ya ushirika na utume?
Ni Sakramenti mbili ambazo ni Sakramenti ya Daraja na Sakramenti ya Ndoa


Sakramenti ya Daraja ndiyo nini?
Sakramenti ya Daraja ndiyo Sakramenti ambayo mwanamme mkatoliki aliyeitwa na Mungu hupata mamlaka na neema ya kuendeleza ndani ya Kanisa Utume Kristo aliowakabidhi Mitume wake


Ni kwa nini inaitwa Sakramenti ya Daraja?
Inaitwa Sakramenti ya Daraja kwa sababu mtu anapata Sakramenti hii kwa kuweka wakfu kwa ibada ya pekee inayomwezesha kwa nguvu ya Roho Mtakatifu atumie uwezo Mtakatifu kwa niaba na mamlaka ya Yesu Kristo ili kuhudumia Taifa la Mungu


Sakramenti ya Daraja ina ngazi ngapi?
Sakramenti ya Daraja inazo ngazi tatu, nazo ni Ushemasi, Upadre, Uaskofu


Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo gani?
Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo yafuatayo;
1. Inampa utimilifu wa SSakramenti ya Daraja Takatifu
2. Askofu anakuwa Mwandamizi rasmi wa Mitume
3. Inampa Askofu ushirika na Papa na maaskofu wengine wa kuwajibikia Makanisa yote
4. Inampa uwezo wa kufundisha, kutakasa na kuongoza


Askofu ni nani?
Askofu ndiye mchungaji mkuu wa kanisa Mahalia au Jimbo lake


Askofu ana kazi gani katika Jimbo lake?
Askofu katika Jimbo lake anamwakilisha Kristo akitimiza kazi ya kichungaji akisaidiwa na mapadri na mashemasi wake.
Askofu ni kiongozi wa kiroho katika jimbo mahalia. Na sio mambo ya kiroho tu ila hata ya kijamii lakini watu/mtu akiitaji ufafanuzi na msaada toka kwake.
Kazi zake ni:-
1. Kuliongoza taifa la Mungu alilopewa yaani wakristo/wengineo pia
2. Kusimamia na kuongoza Litrujia katika eneo husika.
3. Kueneza amani kwa kupitia karama na wadhifa aliopewa na Mungu.
4. Kueneza upendo katika eneo/jimbo mahalia.
5. Mtoa kauli ya mwisho kwa mambo ya kikanisa katika jimbo.
6. Kusimamia miito ya kanisa na kuchochea bila kukata tamaa
7. Kusimamia baraza la walei na kulishauri kwa kutolea kauli ya Mwisho kabla ya kwenda kwingine
8. Kuwashauri watu waliokata tamaa au kushindikana katika ngazi za chini
NB. Hivyo ndani ya kanisa kuna miogozo ili kupata nafasi zisizokinzana


Ni nani ampaye padri Daraja la Uaskofu?
Ni Baba Mtakatifu pekee au humteua Askofu mmoja akisaidiwa na maaskofu wengine wawili humweka wakfu Padri huyo kuwa Askofu (Mt 13:2-3)


Baba Mtakatifu ni nani?
1. Ndiye Askofu Mkuu wa Maaskofu wote
2. Ndiye mchungaji mkuu wa Wakatoliki wote hapa duniani
3. Ni Wakili wa Yesu Kristo hapa duniani. (Mt 16:18-19; Yoh 21:15-17).


Ibada ya Daraja inachapa alama gani nafsini mwa aliyepewa?
1. Ibada ya Daraja inatia rohoni alama isiyofutika
2. Inamlinganisha mpokeaji na Kristo Kuhani
3. Inamwezesha mwenye Daraja kutenda kwa Jina la Yesu aliye Kichwa cha Kanisa


Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka gani?
Kwa Sakramenti ya Daraja Padri anapata mamlaka ya
1. Kuadhimisha sadaka ya Misa Takatifu na kutakasa watu kwa njia ya Sakramenti.
2. Kuhubiri neno la Mungu
3. Kuwaongoza watu (Ebr 5:1-4)


Ni nani wenye uwezo wa kutoa Sakramenti ya Daraja?
Wanaotoa Sakramenti ya Daraja Katika ngazi tatu Uaskofu, Upadre, Ushemasi ni Maaskofu waliopewa Daraja halisi kama waandamizi wa Mitume.


Ni nani aweza kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu?
Mwenye kupewa kihalali Sakramenti ya Daraja Takatifu ni Mwanaume peke yake aliyebatizwa, akiwa na wito nasifa zinazotakiwa na kukubaliwa na Mamlaka ya Kanisa. Ndivyo Yesu Kristu alivyotaka mwenyewe


Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ni kuweka mikono juu ya yule anayepewa Daraja na kutamka maneneo ya sala ya wakfu.


Anayetaka kuwa padri yampasa nini?
Yampasa;
1. Awe na tabia njema, akili za kutosha na afya nzuri.
2. Apende sana wokovu wa watu na kujitolea kwa huduma ya Mungu
3. Awe tayari kuishi hali ya useja maisha yake yote


Kwa sababu gani cheo cha Padri ni kikubwa sana?
Kwa sababu Padri anashiriki Upadri wa Yesu Kristo na ni mjumbe kati ya Mungu na Mwanadamu


Yatupasa nini kwa wenye Daraja Takatifu?
Yatupasa
1. Kuwaheshimu
2. Kuwasikiliza na kufuata mafundisho yao
4. Kuwasaidia katika utumishi wao kwa Sala na sadaka zetu


Matokeo ya Sakramenti ya Daraja ni yapi?
1. Inaleta mmiminiko wa kipekee wa Roho Mtakatifuambao unamlinganisha mhusika na Kristo
2. Inatia alama ya kiroho isiyofutika. kwa hiyo haiwezi kurudiwa au kutolewa kwa muda tuu.

Maswali na majibu kuhusu Katekesi

Katekista ni nani?
Katekista ni mlei aliyechaguliwa na Kanisa ili kumfanya Kristo ajulikane, apendwe, na kufuatwa na wale ambao hawajamfahamu na pia waamini


Waraka wa Baba Mtakatifu Unatafsiri vipi Makatekista?
Waraka unasema;
1. Makatekista ni Wafanyakazi maalimu
2. Mashahidi wa moja kwa moja, Wainjilishaji wasio na mbadala


Mkusanyo Sheria Kanuni za Kanisa unaelezaje kuhusu Makatekista?
Unaeleza kuwa – Makatekista ni Walei Wakristo ambao wamepewa malezi halisi na wanajitokeza vizuri katika maisha ya Ukristo wao.


Chini ya Uongozi wa Kanisa Katekista anafanya Kazi gani?
1. Yeye ni Kiungo cha Mapadre na waamini wa eneo lake
2. Kufikisha mafundisho ya Injili na kuhusika kwenye kazi za Ibada za kiliturujia na kazi za Huruma
3. Kuhubiri na kuwafundisha wakatekumeni
4. Kuelimisha vijana na watu wazima kkatika maswala ya Imani
5. Kuongoza Sala za Jumuiya hasa kwenye Ibada za Jumapili Ikiwa Padre hayupo
6. Kuwatembelea wagonjwa na kuwasaidia na kuongoza Ibada za Mazishi
7. Kufundisha dini mashuleni na kuwaandaa watoto katika kupokea Sakramenti mbalimbali
8. Kutembelea Jumuiya ndogondogo kuziendeleza na kuziimarisha

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu Ishara ya Msalaba

Ishara ya msalaba ni nini?
Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?
Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?
Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?
Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?
Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?
Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.

Kuhusu Ubatizo, Haya ndiyo mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu

Kwa nini ubatizo unafanyika kwa maji?

Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo ishara ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
โ€œNami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenuโ€ (Ez 36:26-27).
โ€œKisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kungโ€™aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwanakondooโ€ (Ufu 22:1).


Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu lini?

Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo Yesu ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha waamini walivyotekeleza agizo hilo katika mazingira mbalimbali, sio tu yalipopatikana maji mengi. Hivyo Paulo alipokuwa ndani ya nyumba โ€œakasimama akabatizwaโ€ (Mdo 9:18).
Kumbe Yohane Mbatizaji hakusogea mbali na mto Yordani, akisubiri watu wamuendee kutoka maeneo yote ya nchi ile kame.
โ€œAlikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji teleโ€ (Yoh 3:23).


Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?

Hapana, ubatizo uliotolewa na Yohan Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu, mwanzilishi wa sakramenti zote.
โ€œKweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa motoโ€ (Math 3:11).
Paulo aliuliza watu, โ€œโ€˜Mlibatizwa kwa ubatizo gani?โ€™ Wakasema, โ€˜Kwa ubatizo wa Yohaneโ€™. Paulo akasema, โ€˜Yohane alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesuโ€™. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesuโ€ (Mdo 19:3-5).


Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni zipi?

Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni kwamba sakramenti inategemea imani kwa Kristo na kutushirikisha kifo na ufufuko wake.
โ€œMaana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristoโ€ (Gal 3:27).
Ndivyo inavyoondolea dhambi zote na kuingiza katika uzima wa Utatu Mtakatifu. Kwa sababu hiyo Yesu aliagiza tubatize โ€œkwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifuโ€ (Math 28:19).
Maneno hayo ndiyo muhimu zaidi katika sakramenti hiyo. Maji peke yake, hasa yakiwa mengi, yanaweza kuosha mwili, lakini si roho. Kumbe ubatizo unaotuokoa
โ€œsiyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Munguโ€ (1Pet 3:21).


Je, watoto wachanga wanaweza kubatizwa?

Ndiyo, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai neema ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwake โ€œalichukizwa sana, akawaambia, โ€˜Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisaโ€ (Mk 10:14-15).
Yeremia aliambiwa,
โ€œKabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifaโ€ (Yer 1:5).
Yohane Mbatizaji alitabiriwa โ€œatajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamayeโ€ (Lk 1:15).
Mitume walipokea katika Kanisa familia nzima, si wazazi tu.
Walibatizwa โ€œyeye na nyumba yakeโ€, โ€œyeye na watu wake woteโ€ (Mdo 16:15,33);
โ€œwatu wa nyumbani mwa Stefanaโ€ (1Kor 1:16).
Kwa hiyo tunaona kuwa tangu wakati wa Mitume sio watu wazima tuu waliokua wakibatizwa bali na watoto pia.


Mbona watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika wakati wa ubatizo halafu wanabatizwa?

Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani.
โ€œVinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao umeiweka misingi ya nguvuโ€ (Zab 8:2).
โ€œElisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lakeโ€ฆ kwa shangweโ€ (Lk 1:41,44).
โ€œNakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zakoโ€ (Math 11:25-26).


Je, watu wazima wanaweza kuelewa sakramenti kwa dhati?

Hapana, watu wazima hawawezi kuelewa sakramenti kwa dhati, kwa kuwa zote ni mafumbo yanayotuzidi. Basi, kama Petro alipooshwa miguu, tumuachie Bwana atufanyie kazi anavyojua yeye.
โ€œNifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadayeโ€ (Yoh 13:7).
Kisha kuoshwa tuzidi kuchimba mafumbo hayo kwa mwanga wa Neno na wa Roho Mtakatifu.
โ€œJe, mmeelewa na hayo niliyowatendea?โ€ฆ Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyoโ€ (Yoh 13:12,15).


Je, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto?

Ndiyo, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto kama wengine pia.
Walimletea Yesu โ€œmtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanneโ€ฆ Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, โ€˜Mwanangu, umesamehewa dhambi zakoโ€ (Mk 2:5).
Yesu aliiona imani yao akamponya. Imani ya watu wengine ndio ilivyopelekea kuponywa kwa huyu mtu. Vivyo hivyo Imani ya Mzazi inaweza kumsaidia mtoto.
Kwa ubatizo watoto wanaunganishwa naye na kuanza kuponywa madonda ya dhambi ya asili.
โ€œTazama, mimi naliumbwa kati hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatianiโ€ (Zab 51:5).
โ€œIkiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristoโ€ (Rom 5:19).


Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?

Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba Wayahudi walipokea watoto katika dini yao kwa kuwatahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa.
โ€œHata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesuโ€ (Lk 2:21).
Watu wa mataifa walipoongokea dini hiyo, walioshwa na kutahiriwa pamoja na watoto wao. Mitume pia walipokea katika Kanisa familia nzima, si wazazi tu. Walibatizwa โ€œyeye na nyumba yakeโ€, โ€œyeye na watu wake woteโ€ (Mdo 16:15,33); โ€œwatu wa nyumbani mwa Stefanaโ€ (1Kor 1:16).
Kwa hiyo tunaona kuwa tangu wakati wa Mitume sio watu wazima tuu waliokua wakibatizwa bali na watoto pia.
Kwa Kanisa Katoliki, ubatizo sio ukamilifu wa kuwa Mkristo. Ubatizo ni Sakramenti ya kwanza ambayo inakamilishwa na Sakramenti ya Kipaimara ambayo humfanya Mkristo kuwa mkamilifu kwa kukiri na kuahidi mwenyewe kuwa Mfuasi wa Yesu Kristu kwa kumkataa Shetani na Mambo yake yote. Kwa maana hiyo, watoto wanapobatizwa wazazi wanamtoa au wanamwalika mtoto katika Imani ya Kikristu wakiahidi kumtumza na kumwelekeza katika njia ya Imani kwa Yesu Kristu mpaka atakapokua mkubwa na kuwa na ufahamu na Elimu ya kutosha kuhusu Imani yake ndipo na yeye atakiri na kuahidi mwenyewe wakati wa Sakramenti ya Kipaimara.


Je, ubatizo tuu unatosha?

Hapana, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula.
Sakramenti hizo tatu kwa pamoja ni msingi wa maisha ya Wakristo wote, kumbe nyingine zinahitajika tu katika hali na nafasi maalumu. Mitume waliwaendea Wasamaria
โ€œwakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifuโ€ (Mdo 8:15-16).
โ€œAmin, amin, nawaambieni: Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndaniyenuโ€ (Yoh 6:53).


Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?

Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake.
โ€œWaliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yaoโ€ (Mdo 19:5-6).
Sakramenti hizo ni kama pande mbili za pesa moja. Zinahusiana kama Pasaka na Pentekoste, ambayo ni utimilifu wake, kwa kuwa siku alipofufuka Yesu aliwapulizia Mitume Roho Mtakatifu, ambaye siku hamsini baadaye akawajia kama
โ€œupepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yoteโ€ (Mdo 2:2).


Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?

Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.
Sisi ambao tulishiriki kifumbo kifo na ufufuko wake tukapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, tunaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapotulisha na kutunywesha Mwili na Damu yake ili tushiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi.
โ€œAulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimiโ€ (Yoh 6:56-57).
Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani mwetu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.


Sakramenti ya ubatizo ni nini?

Sakramenti ya Ubatizo ni Sakramenti yenye kuondoa dhambi ya asili pamoja na dhambi nyingine zote tulizotenda, kufufua roho zetu kwa kututia uzima wa Mungu, Kutuandika Wakristu Watoto wateule wa Mungu na wa Kanisa.


Ubatizo ni nini?

Ubatizo ni Sakramenti inayotuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa Maji na Roho Mtakatifu, ni mlango (Kiingilio) kwa Sakramenti nyingine zote na ni ufunguo wa uzima wa milele. (Yoh 3:3, Mt28:19)


Sakramenti ya Ubatizo yatuletea nini?

Sakramenti ya Ubatizo yatuletea;
1. Maondoleo ya dhambi ya asili
2. Maondoleo ya dhambi zote za binafsi na adhabu zake
3. Neema ya Utakaso kwa mara ya kwanza
4. Yatutia alama isiyofutika (1Kor 6:11, 12:13)


Kuna Ubatizo wa namna ngapi?

Kuna Ubatizo wa namna tatu;
1. Ubatizo wa maji – Ubatizo wa kawaida
2. Ubatizo wa tamaa – Mfano mtu akifa akiwa na nia ya kubatizwa au akitamani kubatizwa
3. Ubatizo wa Damu – Mtu akiifia Imani japo hajabatizwa


Nani aweza kubatiza?

Mwenye mamlaka ya kubatiza kwa kawaida ni yule mwenye dataja takatifu katika Kanisa, lakini katika hatari ya kufa kila mtu anaweza kubatiza.


Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?

Kwa sababu wanazaliwa na dhambi ya asili hivyo wanahitaji kuwekwa huru kutoka mamlaka ya yule mwovu na kuingizwa katika ufalme wa uhuru wa wana wa Mungu


Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?

Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo


Anayebatizwa yampasa nini?

Yampasa kuungama imani yake ama mwenyewe akiwa mtu mzima ama kupitia wazazi kama akiwa mtoto mdogo


Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni nini?

Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni kumwagia maji katika panda la uso na kutamka maneno “Fulani (jina lake linatajwa) nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” (Mt 28:19)


Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?

Msimamizi wa ubatizo ana wajibu hizi;
1. Kutoa mfano mzuri wa maisha ya Kikristo
2. Kumuongoza mbatizwa katika maisha ya Ukristo
3. Kumuombea mbatizwa
4. Kushirikiana na wazazi katika malezi

Amri ya Tano ya Mungu: Kutunza uhai wetu na wa watu wengine

Katika Amri ya Tano ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tutunze uhai wetu na wa watu wengine tangu mwanzo hadi mwisho. (Mwa 4:10-11)


Kwa nini ni lazima kutunza uhai wetu na wa wenzetu?

Kwa sababu uhai wa watu wote umetoka kwa Mungu


Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?

Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba


Nani anatenda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu? Mambo yanayovunja Amri ya Tano ya Mungu

Anayetemda dhambi dhidi ya amri ya tano ya Mungu ni yule;-

1. Anayemuua mtu au anayejiua mwenyewe
2. Anayemdhuru mwingine kwa namna yoyote ile
3. Anayeua Mimba na kuharibu nguvu za uzazi
4. Anayesaidia kuua, kumdhuru mtu au anayesaidia kutoa/kuharibu mimba
5. Anayeharibu mazingira yaliyomuhimu kwa uhai
6. Anayetetea au kuendeleza mifumo ya ya dhuluma, uhasama na vita.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu ngono na maadili ya kijinsia?

Kanisa Katoliki ni moja ya madhehebu makubwa duniani, na imani yake juu ya ngono na maadili ya kijinsia ni muhimu sana. Kanisa hili linazingatia mafundisho ya Biblia na Catechism ya Kanisa Katoliki katika kuelezea maadili ya kijinsia na ngono.

Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki, ngono ni kitendo kinachofanywa kati ya mwanamume na mwanamke, ambao wamefunga ndoa. Ni kitendo kitakatifu kinachopaswa kufanywa kwa upendo na kwa lengo la kuwaleta watoto duniani. Ni dhambi kufanya ngono kabla ya ndoa au kufanya ngono bila lengo la kuzaa watoto.

Kanisa Katoliki linasisitiza kuwa wanaume na wanawake wote ni sawa mbele ya Mungu na wanapaswa kutendewa kwa heshima na upendo. Uhusiano wa kimapenzi kati ya wanaume ama kati ya wanawake una kinyume na mafundisho ya Kanisa. Hata hivyo, Kanisa Katoliki linapenda na kuheshimu watu wote bila kujali kama wana tabia za kimapenzi ama la.

Kanisa Katoliki linasisitiza kuwa ngono inapaswa kutendeka kwa heshima na utu wa binadamu. Ni muhimu kufuata maadili ya kijinsia kwa kuepuka dhambi ya uzinzi, ngono haramu, na ukahaba. Kila mtu anapaswa kuishi maisha yenye maadili ya kijinsia, na kuhakikisha wanapata elimu ya kutosha juu ya maadili haya.

Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunasoma "Maadili ya kijinsia ni sehemu ya maadili ya kichungaji yanayohusiana na afya ya mtu na pia kuhusiana na maadili ya ndoa inayohusisha upendo wa kudumu kati ya mume na mke." (CCC 2351)

Kanisa Katoliki linasisitiza umuhimu wa kutumia njia za uzazi wa mpango ambazo hazimzuia Mungu kwa kuua mimba. Kanisa linapendekeza njia za uzazi wa mpango kama vile uzazi wa mpango wa asili, kufahamu kwa kina kuhusu mzunguko wa hedhi, na njia za uzazi wa mpango zinazorejesha udhibiti wa uzazi kwa mwanamke.

Kanisa Katoliki linakemea ngono kwa ajili ya kufurahisha nafsi ama kwa ajili ya ngono yenyewe, bila lengo la kuzaa watoto. Ngono inapaswa kuwa kwa lengo la kuunganisha mume na mke na kuwaleta watoto duniani kama zawadi kutoka kwa Mungu.

Hatimaye, Kanisa Katoliki linasisitiza umuhimu wa kuishi maisha ya utakatifu. Wanawake na wanaume wote wanapaswa kuishi maisha safi ya kijinsia, kufuata maadili ya kijinsia, kuheshimiana, na kuepuka kila aina ya dhambi. Kwa kufuata mafundisho ya Kanisa na kufuata Biblia na Catechism, tunaweza kuishi maisha yenye maadili ya kijinsia na mafanikio katika maisha.

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi upendo na huruma kwa wengine kama Kristo alivyofanya?

Je, Kanisa Katoliki linawahimiza waamini kuishi upendo na huruma kwa wengine kama Kristo alivyofanya?

Ndio, Kanisa Katoliki linafanya hivyo. Kwa maana hiyo, linatukumbusha kwamba upendo na huruma ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Upendo ni kitu ambacho kinapaswa kushinda yote, na ni muhimu sana kwa Wakristo kuonyesha upendo kwa wengine kama vile Kristo alivyofanya.

Kwa mujibu wa Biblia, Mathayo 22:37-40 inasema "Yesu akamwambia, ‘Mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote. Hii ndiyo amri ya kwanza na kubwa. Nayo amri ya pili ni hii, Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. Katika amri hizi mbili zote hutegemea torati na manabii.’ "

Kanisa Katoliki linatufundisha kwamba upendo na huruma ni msingi wa maisha ya Kikristo. Ni wajibu wetu kama Wakristo kuishi kwa upendo na kufanya kazi kwa ajili ya wengine, kama Kristo alivyofanya. Ni kwa njia hii tu tunaweza kufikia ushirika na Mungu na kupata amani ya kweli.

Katika Waraka wa Kitume wa Papa Fransisko "Misericordia et Misera", aliandika "Upendo ni moyo wa imani na imani ni mwanga wa upendo. Kwa hiyo, Kanisa inatualika kuishi kwa upendo na huruma kwa wengine, hasa kwa maskini na walio na shida. Hii inamaanisha kutoa msaada kwa wale wanaohitaji, kutembelea wagonjwa na wafungwa, na kuwa tayari kusamehe wale ambao wametukosea."

Kwa mujibu wa Kanisa Katoliki, upendo na huruma ni sehemu ya maisha ya kila siku ya kila Mkristo. Ni wajibu wetu kuonyesha upendo na huruma kwa wengine katika kila nafasi tunayokutana nao. Katika Kitabu cha Wagalatia 5: 22-23, tunasoma kwamba "Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi."

Pia, Katika Catechism of the Catholic Church, kifungu 1822 kinasema "Upendo wa Mungu ni msingi wa kila tendo la wema kwa wengine. Katika Kanisa, upendo ni sehemu muhimu sana ya huduma kwa wengine na ni wajibu wa kila mmoja kwa ajili ya wengine."

Kwa hiyo, ni muhimu kwa Wakatoliki kuishi maisha ya upendo na huruma kwa wengine kama vile Kristo alivyofanya. Kwa njia hii tu tunaweza kufikia utimilifu wa maisha yetu ya Kikristo na kufikia ushirika wa milele na Mungu.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu viongozi wa kidini na maaskofu?

Katika imani ya Kanisa Katoliki, viongozi wa kidini na maaskofu ni watu muhimu sana katika kufikisha ujumbe wa Mungu kwa wengine. Wao ni wawakilishi wa Kristo duniani na wanapaswa kufuata mfano wake wa kuwatumikia wengine kwa upendo na unyenyekevu.

Kanisa Katoliki linatambua kwamba maaskofu ni watendaji wa ngazi ya juu kabisa na wanayo mamlaka ya kufundisha, kuongoza, na kuwatawala waumini wa Kanisa. Kwa hivyo, wanapaswa kuwa na uadilifu wa hali ya juu na kuwa na uwezo wa kuonyesha mfano wa maisha ya Kikristo kwa waumini wao.

Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, maaskofu ni wachungaji ambao wanahusika na huduma ya kufundisha, kuongoza, na kuwatawala waumini wa Kanisa. Wanapaswa kufanya hivyo kwa kuzingatia kanuni za Injili na kufuata mfano wa Kristo mwenyewe.

Maaskofu wanapaswa kuwa wakarimu, wanyenyekevu, na kuwatendea watu kwa upendo na huruma. Kwa kufanya hivyo, wanaweza kuwaongoza waumini wao kwa njia ya dhati na kuwasaidia kufikia ukamilifu wa maisha yao ya Kikristo.

Biblia inatupa mifano mingi ya jinsi viongozi wa kidini wanavyopaswa kuwa. Kwa mfano, Mtume Paulo alisisitiza umuhimu wa uadilifu katika uongozi wa kidini katika 1 Timotheo 3:2-3: "Basi askofu imempasa awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, na mwenye kiasi, mwenye kujidhibiti, mwenye adabu, mwenye kupokea wageni, mwenye uwezo wa kufundisha; si mlevi, si mtu wa kujipenda mwenyewe, si mwenye hasira kali, si mtu wa kujitokeza sana, si mpiga-mkono".

Kanisa Katoliki linatambua kwamba hakuna kiongozi wa kidini au askofu anayeweza kuwa mkamilifu. Kwa hiyo, wanapaswa kuwa watu ambao daima wanatafuta kukua katika imani yao na kufanya kazi kwa bidii kumtumikia Mungu na waumini wao.

Kwa kweli, viongozi wa kidini na maaskofu ni watu muhimu sana katika Kanisa Katoliki. Kwa kufuata mfano wa Kristo na kuwa na uadilifu wa hali ya juu, wanaweza kuwa viongozi bora na kuwahudumia waumini wao kwa upendo na unyenyekevu.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About