Vichekesho Vya Jumapili

Mtoto ni wa baba au wa mama? Angalia hoja za baba na mama kila mmoja anadai ni wake

Mtoto ni wa baba au wa mama?

Mume alimpa mkewe talaka wakaenda mahakamani ili hakimu aamue nani akae na mtoto.

MME: Akasimama akauliza hivi: Mheshimiwa hakimu hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye mashine ikatoa pesa, sasa pesa zitakuwa ni za ATM au zakwangu?

MKE: Akasimama na kusema: Mheshimiwa hakimu hivi ukimwaga mbegu ktk shamba la mtu mti ukiota utakuwa wa kwako au wa mwenye shamba?.

Hebu tumsaidie hakimu aamue kesi hii…

Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…”

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipo…!!!

Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE

MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000

Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyewe…

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About