Vichekesho Vya Jumapili

Cha kufanya msichana akikukimbia halafu atake kukurudia

……… Kama msichana atakutupa kwa sababu huna pesa, na baadaye unapopata pesa akarudi tena kuomba msamaha… Ndugu yangu….. Msamehe…. Mpe ahadi ya ndoa, mwambie utamuoa…. iambie familia yake unataka kufanya ukarabati wa nyumba yao…… Ondoa paa lote la nyumba yao halafu TOWEKA…..

šŸ˜‚ā€¦ā€¦ā€¦ šŸ˜‚ā€¦ā€¦.. šŸ˜‚

Kwa hiki kilichonikuta sitadanganya tena kuanzia leo

Juzi nikitoka church nilipanda kihiace na kulikuwa na mrembo mkali hujawahi kuona,kila kijana alikuwa akimtupia macho,so me nilikuwa na wepesi wa kuongea naye kirahisi coz nilikuwa kando yake,,, Sasa kama unavyojuwa wanaume kwa kujikosha Nikaimigine mtto ananiangalia so nikaamuwa kupiga fake phone
“Hello Mr. Supervisor,nitachalewa kidogo coz kuna mahali nitapitia, so nipelekee tu hyo Ferrari yangu nyumbani”

Nikaona mrembo ameniangalia kwa macho ya husda apo nkajua nimeuwa ndege kwa jiwe moja, nkaamua kujikosha mtt wa kiume , “niaje mrembo”, akanikazia macho kisha akaniambia,
“Shika battery yako uliangusha ukitoa simu”

Icho kicheko watu walicheka hujawahi ona jooo adi ikabidi dereva aegeshe gari watu wacheke kwanza šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
Nikaona isiwe tabu nikashukia pale palešŸš¶šŸæšŸš¶šŸæšŸš¶šŸæ

Tujifunze kusema ukweli kwani uongo sio mzuri hata kwa Mungu… šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™šŸ™

Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata

Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!

Wachaga wana mambo mbele ya hela, angalia hii bili ilivyomchanganya MASSAWE

MASSAWE alienda na marafiki zake bar kunywa, baada ya kumaliza kutumia akaletewa bili kama ifuatavyo:
Manka 35,000
Marieta 20,000
Kekuu 30,000

Kitime 15,000
Kinabo 10,000
TOTAL 110,000/=
MASSAWE akaicheki akasema “Wote nitawalipia lakini huyo “TOTAL” Yesuu simlipii.
Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa bongo. Shensi taip ! Na amekunywa nyingi kuliko wote alipe mwenyewe…

Utani wa wahindi, cheka kidogo

Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili

(1) Mfa maji ?……………….. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?………… Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?……….. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?……………… Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?……. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?……… Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?…….. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?…… Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?……… Takosa guo ya sikukuu…
(10) Kila ndege ?………….. …Hutua Airport
(11) Bandu bandu ?….. …….Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?… Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?….Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?………. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?…….. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?…. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? …….. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? …………..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?…….. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?….Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?…….. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? ……….Taenda Chadema
(23) Bendera ?……………. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?……. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?………. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? …….. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.

Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure

Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :Ā Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :Ā Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :Ā Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:Ā Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :Ā Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.

Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?

Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.

SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!

Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu…”

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”

šŸƒšŸƒšŸƒšŸƒšŸƒšŸƒšŸƒšŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

Madenge hakosi visa. Soma hii

MADENGE
HAKOSI
VISA

baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo
MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake.
BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa.
MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    šŸ  Home šŸ“– Reading šŸ–¼ļø Gallery šŸ’¬ AI Chat šŸ“˜ About