Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiyaโฆsasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisaโฆ.papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!โฆBenedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaaโฆ
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!โฆโฆ..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!โฆ.ofa nyingineeee!”
Kimyaaaโฆ
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!โฆofa nyinginee!
Kimyaaaโฆ.
Kimyaaaโฆ.
๐๐๐โฆhapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balanceโฆsasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo๐(mama wee Mosha anachezea Simu!)โฆ..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)โฆ..mama weee๐
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maitiโฆ.kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena๐โฆMama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimiโฆ.Chicken wings zinataka kutokea Masikioniโฆ..Uuuuwiiiii,๐๐๐
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato๐๐๐๐๐.
chiel wie okee
Recent Comments