Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mapishi ya mboga ya mnavu

Viamba upishi

Mnavu mkono 1
Kitungu 1
Karoti 2
Maziwa kikombe 1
Mafuta vijiko viubwa 4
Karanga zilizosagwa kikombe 1
Chumvi kiasi ยฝ

Hatua

โ€ข Chambua mnavu, osha na katakata.
โ€ข Menya, osha na katakata kitunguu.
โ€ข Osha, menya na kwaruza karoti.
โ€ข Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike.
โ€ข Kaanga vitunguu na karoti mpaka zilainike ukikoroga.
โ€ข Weka mnavu na chumvi koroga sawa sawa, funika kwa dakika 5-10 (kama ni kavu weak maji kidogo).
โ€ข Changanya maziwa na karanga, ongeza kwenye mnavu ukikoroga kisha punguza moto kwa dakika 5.
โ€ข Onja chumvi na pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Weka nyanya kidogo.
Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa.
Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende Na Ufuta

MAHITAJI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Baking powder – 1 ยฝ Vijiko vya chai

Sukari – 1 Kikombe cha chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Mayai – 2

Maji – kiasi ya kuchanganyia

Tende – 1 Kikombe

ufuta – ยผkikombe

MAPISHI

  1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
  2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
  3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
  4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
  5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande.
  6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.
  7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele

Faida ya Mafuta Ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele.

1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara

2. Yanasaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa

3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele

4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.

5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.

NAMNA YA KUZIHUDUMIA NYWELE:

Unaweza kuchanganya na Mdalasini pamoja na Asali.

1. Olive oil vijiko 2 vya chakula

2. Asali kijiko 1 cha chakula

3. Mdalasini kijiko 1 cha chai

Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja pakaa kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka.

Ninashauri utumie mafuta haya kwenye nywele na ngozi ni mazuri sana. Ukiwa na mba pakaa kwenye ngozi mba itaisha na muwasho utaondoka.

Mambo 9 ya kuzingatia kuepuka ugonjwa wa saratani au Kansa

Tafiti nyingi zilizolizofanywa zinaonesha kuwa sababu kuu zinazosababisha saratani ni mtindo wa maisha usiofaa kama ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili.
Ili kuepukana na ugonjwa wa saratani au kupunguza uwezekano wa kupata saratani ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

1. Kula zaidi vyakula vya mimea na nafaka zisizokobolewa

Matokeo ya tafiti yanaonesha kuwa vyakula hivi vinapunguza uwezekano wa kupata saratani, Hakikisha unakula mboga mboga za kijani na rangi nyingine kama njano,zambara. Kula nafaka zisizokobolewa kama unga wa dona, mchele wa brauni,unga wa ngano usiokobolewa,mtama na ulezi.

2. Kuwa na Uzito Uliosahihi

Uzito mkubwa uliopitiliza ni hatari na husababisha saratani. Hakikisha uwiano wa urefu na uzito wako (BMI- Body -to-Mass Index) ni sahihi ambayo ni 18 -25 kwa mtu mzima na mwenye afya nzuri unashauriwa kuwa na uwiano wa 21-23.

Punguza vyakula vinavyonenepesha mwili kama vyenye mafuta na sukari kwa wingi. Vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama chipsi na vitumbua mfano ni hatari kwa afya yako.Vyakula vyenye sukari ni kama soda,chokoleti,keki,barafu na iskrimu na juisi bandia.

3. Fanya mazoezi ya mwili

Fanya mazozi ya mwili kila siku. Dakika 15-30 tu zinatosha kufanya mazoezi kwa afya njema. Ukikosa muda fanya anagalau mara 3 kwa wiki kwa muda usiopungua dakika 30.
Kukimbia(jogging) ni njia rahisi ya kufanya mazoezi yanayohusisha mwili mzima. Ukiweza jiunge katika timu ya mpira au klabu za mazoezi ya ndani.

Tembea kwa miguu pale inapobidi. Rafiki yangu mmoja ambaye ana gari ameweka ratiba ya kutotumia gari wakati wa mwisho wa juma. Anapanda dalala na kutembea kwa sehemu kubwa. Unaweza ukafanya hivyo pia.

4. Punguza au Acha kula Nyama nyekundu.

Ukiachia mbali saratani, nyama nyekundu imetambulika kusababisha madhara mengi na makubwa kwa binadamu.

Amua sasa kuachana nayo. Hamia katika samaki na kuku kwa kuanzia na baadae huenda ukaachana na hizo nyingine pia.
Nyama ya nguruwe maarufu kam Kitimoto ni nyama nyekundu na ni hatari kwa afya yako . Heri wale ambao hata dini zao zilikataza nyama hii ya Nguruwe kwani wameepuka hatari.

5. Epukana na Nyama za kusindikwa.

Nyama za makopo na soseji zinasababisha saratani kutokana na kemikali za kutunzia zisioze na pia huwekwa chumvi nyingi sana ambayo ni hatari kwa afya.

6. Punguza Matumizi ya Chumvi

Chumvi ya kupita kiasi inaongeza uwezekano wa kupata saratani hivyo ni hatari. Tumia chumvi kwa kiasi kidogo kwa afya njema. Binadamu anahitaji gramu 5 tu kwa siku sawa na kijoko kidogo cha chai.

Usiongeze chumvi wakati wa kula,chumvi isiyoyeyuka nia hatari zaidi.

7. Acha kula Vyakula vyenye Ukungu

Acha kula nafaka na kundekunde zilizootesha ukungu hasa kwa kutohifadhiwa vyema. Vyakula hivi vinatoa sumu ya aflatoxin

8. Usivute Sigara

Uvutaji wa sigara ni hatari na huenda ukakusababishia saratani ya koo,kinywa na mapafu. Acha kuvuta sigara ili kuepukana na ugonjwa wa saratani. Fikiria kidogo,kwanini ufe kwa sababu ya moshi tu?.

9. Punguza au Acha Pombe Kabisa

Ukiacha pombe utapunguza uwezekano wa kupata saratani na hivyo kuwa salama zaidi.
Achana na pombe, kuna madhara mengi sana ya kunywa pombe ukiachia ya saratani.

Badilisha Mtindo wa Maisha na Uwe Salama na Saratani
Namna ya kuishi kunachangia kwa kiasi kikubwa kupata saratani au la. Chagua mtindo ulio bora na salama kama ilivyoshauriwa katika mada hii juu ya kuepukana na ugonjwa wa saratani.

Afya yako ni jukumu lako mwenyewe na kupanga ni kuchagua. Panga kuishi mtindo wa maisha ulio bora na salama chagua kuishi bila saratani.

Faida ya kuabudu Ekaristi Takatifu

1.Kila saa moja tunayotumia kuabudu, inafurahisha moyo wa Yesu na hivyo majina yetu huandikwa mbinguni kwa ajili ya uzima wa milele (Mama Thereza wa Calcuta)
2.Maisha ya kiroho ya familia zetu yanaimarishwa kwa njia ya saa ya kuabudu (John Paul II)
3. Saa takatifu ya kuabudu ni ya muhimu sana kiasi kwamba roho za waamini wengi huenda kwenye uzima (mbinguni) badala ya motoni (ufunuo wa Yesu kwa Dina Belanger)
4. Wakati pekee ambao Yesu aliwaomba kitu wanafunzi wake ni wakati anakaribia mateso na hakuomba chochote isipokua saa moja ya kukesha nae (Askofu Mkuu Fulton Sheen)
5.Saa moja takatifu ya kuabudu ni kushiriki katika harakati za ukombozi (Askofu mkuu Fulton Sheen)
6. Neema ya kuabudu Ekaristi iko juu ya watu wote (St Peter Julian Eymard)
7.Bwana wetu Yesu husikia maombi yetu yote na popote lakini amewafunulia watu wake kuwa wale watakaokwenda kukaa nae katika kuabudu Ekaristi wanapata neema zaidi (Mtakatifu Alphonsus Ligoria)
8.Kila saa unapokwenda kuabudu kumbuka kwamba Yesu amekusubiria wewe binafsi kwenda kumtembelea kwa karne ishirini (St Josemaria scavia)
9.Kuabudu kwa dhati kuna neema na manufaa makubwa ambayo huzidi kwa wale wanaoabudu, hupanuka na kugusa nyumba zao familia zao na mpaka katika parokia zao (Pope Paul VI)
10. Saa moja takatifu mbele ya Ekaristi ni muhimu kuliko miaka elfu moja ya utukufu wa mwanadamu (Mtakatifu Padre Pio)

Mapishi ya Chicken Curry

Leo wapendwa nitaenda kuzungumzia mapishi ya mchuzi wa kuku (chicken curry).

Mahitaji

Kuku mzima
Nyanya kubwa 3
Karoti mbili
Pilipili hoho
Kotmiri
Tangawizi
Kitunguu maji
Kitunguu saumu kidogo
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Chumvi (pilipili ukipenda)

Matayarisho

1. Menya vitunguu saumu na tangawizi na uvitwange pamoja.
2. Katakata kuku vipande vidogo kisha ukamulie ndimu na kupaka mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu (kiasi tu).
3. Katakata vitunguu maji na pilipili hoho uweke pembeni.
4. Grind (Kwangua) kwenye grater nyanya na karoti pia uweke pembeni.
5.Katakata kotmiri vipande vidogo uweke pembeni.
6. Andaa kikaango na jiko.

Mapishi

1. Bandika kikaango jikoni na mafuta kiasi, yakishachemka weka vitunguu maji na kaanga hadi vimelainika na kuiva (hakikisha haviungui).
2. Weka pilipili hoho na karoti na endelea kukoroga hadi vyote viive na kulainika, Kisha weka chumvi.
3. Sasa weka vipande vya nyama koroga na funikia kwa dakika 3, kisha weka nyanya zako ulizo grind na koroga ili zichanganyike vizuri, vikishachanganyika weka kotmiri na pilipili kama utapenda. Acha vichemke kwa dakika 5. Hakikisha moto sio mkali sana.
4. Angalia kama nyama zimeiva vizuri kisha epua mchuzi wako.
5. Pakua kwenye bakuli na katakata kotmiri uweke kwa juu.
Unaweza kula kwa ugali, wali, ndizi rost au chipsi.

Mambo ya Msingi kuyajua kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu

Mojawapo kati ya magonjwa yanayohusishwa na umaskini na uchafu wa kupindukia ni ugonjwa wa Kipindupindu. Inaripotiwa kuwa Kipingupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huathiri jamii maskini zaidi kwa kiasi kikubwa hasa hasa kwenye nchi zinazoendelea, kiasi kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeuweka ugonjwa huu kama mojawapo ya viashiria vya maendeleo ya jamii husika.

Kwanini nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na ugonjwa huu?

Moja wapo ya changamoto zinazokabili nchi zinazoendelea ni jamii kutokuwa na uhakika wa kupata Maji safi na salama, pamoja na kutokuwa na mazingira safi kwa ujumla. Ndio maana mpaka leo nchi zinazoendelea ndizo zinazokumbwa na mlipuko wa kipundupindu au huwa katika hatari ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Kipindupindu husababishwa na nini?

Ugonjwa huu hutokana na maambukizi katika utumbo mdogo wa binadamu uletwao na vimelea vya bacteria vijulikanavyo kitaalamu kama Vibrio cholerae.

Jinsi unavyoweza kuambukizwa

Kwa kawaida vimelea hawa hupendelea kuishi katika kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu kwa kunywa maji ama chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea hivi vya kipindupindu.

Mara baada kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa, baadhi ya vimelea hivi huuwawa kwa tindikali iliyopo kwenye tumbo (stomach) pindi chakula au maji haya yanapoingia tumboni. Hata hivyo baadhi ya vimelea hawa hufanikiwa kukwepa ukali wa hii tindikali na hivyo kuendelea kuishi.

Vimelea waliofanikiwa kuepukali tindikali ya tumbo la binadamu, hujongea kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia โ€˜maumboโ€™ maalum yaliyo kwenye miili ya ambayo huwawezesha kusafiri ama kwa kitaalamu huitwa flagella. Wawapo kwenye ukuta wa utumbo mdogo Vibrio cholerae hutoa sumu iitwayo CTX au CT (cholera Toxin) ambayo husababisha mtu kuharisha choo chenye majimaji, papo hapo kuendelea kutoa kizazi kingine cha vimelea hao nje kwa njia ya haja kubwa.

Iwapo choo hicho cha mtu aliyeambukizwa kipindupindu kitachanganyika na chanzo cha maji au chakula, watu wengine huambikzwa kirahisi. Hali kadhalika iwapo ni kwenye choo ambacho hakipo kwenye mazingira ya usafi kuna hatari ya choo cha mwambukizwa kuchanganyika na chanzo cha maji au chakula na hivyo kupelekea watu wengi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu.

Dalili za kipindupindu ni zipi?

Dalili za mwanzo kabisa za kipindupindu ni

โ€ข Kuanza Kuharisha ghafla choo chenye majimaji (ambacho rangi yake ni kama maji ya mchele) na chenye harufu mbaya kama shombo ya samaki.
โ€ข Kutapika

Aidha mgonjwa wa kipindupindu huonesha dalili zakupungukiwa maji mwilini kama vile

โ€ข ngozi huwa kavu,
โ€ข midomo kukauka,
โ€ข mgonjwa kuhisi kiu kikali,
โ€ข machozi kutoweza kutoka,
โ€ข kupata mkojo kidogo sana,
โ€ข Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana.
โ€ข Macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto.

Vipimo vya utambuzi wa Kipindupindu

Kwa kawaida kipindupindu huweza kugunduliwa na kutambuliwa kwa kutumia dalili. Hata hivyo ili kuthibitisha kuwa mlipuko uliotokea ni kweli kipindupindu, vipimo vifuatavyo huweza kufanyika;

Kupima damu kwa ajili ya kuotesha vimelea vya kipindupindu maabara.
Kuchunguza choo kwa kutumia darubini (dark field microscope) ambapo vimelea hivi vya V. cholerae huweza kuonekana. Vile vile choo hiki hutumika kuotesha vimelea vya v. cholerae kwa ajili ya utambuzi zaidi.

Tiba ya Kipindupindu

Lengo kuu katika kutibu kipindupindu ni kurejesha maji na madini ambayo mgonjwa wa kipindupindu hupoteza kwa wingi baada ya kuharisha na kutapika.

Njia kuu zitumikazo katika kumrejeshea mgonjwa wa kipindupindu maji na madini aliyopoteza ni kwa kumpatia maji maalum yenye madini hayo kwa njia ya mdomo, yaani kwa kumpa anywe au kwa njia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu huitwa intravenously (i.v).

ORS
Pamoja na ORS hiyo ambayo imetengenezwa na kuwekwa kwenye paketi tayari kwa matumizi, Shirika la afya duniani (WHO) limetoa pia mwongozo wa kutengeneza maji yenye madini yanayohitajika mwilini (oral rehydration fluid) ambao ni rahisi na usio na gharama.
ORS ya kutengeneza nyumbani kwa kadiri ya muongozo huo huitaji kuchanganya na
โ€ข Lita moja ya maji safi na salama,
โ€ข Changanya na vijiko vidogo vinane vya sukari, kisha
โ€ข Ongeza na kijiko kidogo kimoja cha chumvi
โ€ข Aidha, unaweza kuongeza nusu glasi ya juice ya machungwa au nusu ya ndizi (tunda) lilipondwapondwa kwa kila lita, ili kuongeza madini ya potassium na pia kuboresha ladha.

Kwa wagonjwa wenye hali mbaya na wale wasioweza kunywa wenyewe, hupewa maji yenye madini mbambali kwa njia ya mshipa wa damu. Maji haya huitwa kitaalamu kama Ringerโ€™s Lactate.

Mwongozo wa kufuata katika kutibu kipindupindu

Baada wa mgonjwa kuwasili katika kituo cha afya, hupimwa kiwango cha upungufu wa maji kilichopo mwilini.

Kisha muhudumu wa afya husahihisha upungufu wowote wa maji utakaonekana kwa awamu mbili. Kwanza kwa kati ya masaa 4-6 ya kwanza tangu kuwasili kituoni na kuendelea mpaka hali ya kuishiwa kwa maji mwilini itakapoonekana imekwisha.

Mhudumu wa afya hutakiwa kurekodi kwenye cheti maalum kiasi cha maji anayokunywa mgonjwa na kiasi cha mojo anachokojoa.

Njia ya mshipa hutumika pale tu, hali ya mgonjwa inapokuwa mbaya sana au pale ambapo mgonjwa hawezi kunywa chochote mwenyewe. Aidha kiasi cha maji kitolewacho kwa njia hii ya mshipa wa damu hwa ni kati ya 50-100 mL kwa kilo za uzito wa mgonjwa kwa saa.

Baada ya hapo, mgonjwa huendelea kupewa ORS anywe kwa kiwango cha 800 mpaka lita moja kwa saa.

Matumizi ya dawa katika kutibu kipindupindu

Ieleweke kuwa tiba sahihi na makini ya ugonjwa huu wa kipindupindu ni kumrejeshea mgonjwa maji na madini aliyopoteza wakati wa kuharisha na kutapika kwa njia ambazo zimeelezwa hapo juu. Matumizi ya dawa (antibayotiki) husaidia tu kufupisha muda wa kuwatoa wadudu na wala yasitumike kama tiba kuu ya ugonjwa huu.

Baadhi ya dawa ambazo hutumika katika matibabu ya ugonjwa huu ni Azithromycin na Tetracycline.

Jinsi ya kuzuia kipindupindu

Mara kwa mara serikali na taasisi zake zimekuwa zikihimiza watu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huu wa kupindupindu. Miongoni mwa njia zinazofaa katika kuzuia milipuko ya ugonjwa huu ni
Upatikanaji wa maji safi na salama, watu hawana budi kuhakikisha kuwa maji ya kunywa yanachemshwa vyema kabla ya kuyanywa. Vile vile wanaweza kutumia chlorine katika maji ambayo huua vimelea hawa wa V. cholerae.

Ni muhimu kunawa mikono baada ya kutoka chooni na kabla ya kula

Tunashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasitue juu yake

Inashauriwa kujenga choo umbali wa angalau mita 30 kutoka chanzo cha maji
Inashauriwa kwa wasafiri watokao nchi zilizoendelea kupata chanjo iitwayo Dukoral, pindi wanaposafiri kwenda nchi zinazoendelea.

Kauli 10 za mtu ambaye unatakiwa umuepuke maishani

Kauli 10 za mtu asiye na malengo wala uthubutu
1)Sina mtaji
2)Sina Connection
3)Nitaanza rasmi kesho
4)Mimi ni wa hivihivi tu

5)Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
6) Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo
7)Kupata ni majaliwa
8)Usilazimishe mambo
9)Kuna watu special siyo mimi.
10)Sina bahati

KAA MBALI NA HUYO MTU. NI HATARI KWA NDOTO ZAKO!!!!

Mwenendo Unaongozwa na Roho Mtakatifu

Basi, nasema hivi: Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. Maana tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na Tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamuwezi kufanya yale mnayotaka nyinyi wenyewe.

(Wagalatia 5:16-22)

Mwenendo Unaongozwa na Roho Mtakatifu

Basi, nasema hivi: Mwenendo wenu na uongozwe na Roho, nanyi hamtafuata tena tamaa za kidunia. Maana tamaa za kidunia hupingana na matakwa ya Roho; na matakwa ya Roho hupingana na tamaa za kidunia. Mambo hayo mawili hayaafikiani; kwa sababu hiyo hamuwezi kufanya yale mnayotaka nyinyi wenyewe.

“Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa maana mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.” (Wagalatia 5:16-17)

Maana ya Kuongozwa na Roho Mtakatifu

Kuongozwa na Roho Mtakatifu maana yake ni kuacha maisha yetu yaongozwe na maadili na kanuni za kiroho zinazotoka kwa Mungu. Roho Mtakatifu hutupa nguvu, hekima, na mwongozo wa kila siku katika safari yetu ya kiroho. Tunapoongozwa na Roho, tunakuwa na uwezo wa kupambana na tamaa za kidunia ambazo zinatufanya tuwe mbali na Mungu.

“Lakini Roho wa kweli atakapokuja, atawaongoza awatie kwenye kweli yote. Kwa maana hatasema kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayasema, naye atawapasha habari za mambo yajayo.” (Yohana 16:13)
“Basi, kama mlivyopokea Kristo Yesu Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye mizizi na kujengwa ndani yake, na kuthibitishwa katika imani, kama mlivyofundishwa, mkizidi kutoa shukrani.” (Wakolosai 2:6-7)
“Basi, enendeni kama watoto wa nuru, kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli.” (Waefeso 5:8-9)

Kupambana na Tamaa za Kidunia

Tamaa za kidunia ni yale mambo yanayotupotosha na kutufanya tuishi kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni lazima tujifunze kuzishinda kwa kuimarisha uhusiano wetu na Mungu kupitia maombi, kusoma Neno la Mungu, na kushirikiana na wengine waaminio. Roho Mtakatifu hutusaidia kuona na kutambua uovu na udanganyifu wa tamaa za kidunia na kutupa nguvu ya kuzishinda.

“Basi, ndugu zangu, sisi tuna deni, si kwa mwili, kufuatana na mwili; kwa maana kama mkiishi kufuatana na mwili, mnakufa; bali kama mkiyaangamiza matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.” (Warumi 8:12-13)
“Wala msiifanye miili yenu kuwa silaha za dhambi kwa kutenda uovu, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama watu waliotolewa katika wafu na kupewa uhai, na miili yenu iwe silaha za haki kwa Mungu.” (Warumi 6:13)
“Kwa maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukibomoa mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinue juu ya elimu ya Mungu; tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo.” (2 Wakorintho 10:4-5)

Kutembea Katika Nuru ya Roho

Kutembea katika nuru ya Roho Mtakatifu ni kuishi maisha yaliyojaa matunda ya Roho, kama vile upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi. Tunapojitahidi kuishi kwa njia hii, tunakuwa mashahidi wa kweli wa Kristo na tunavutia wengine kwake. Ni muhimu kufahamu kwamba hatuwezi kutembea katika nuru ya Roho kwa nguvu zetu wenyewe, bali kwa neema na uwezo wa Roho Mtakatifu ndani yetu.

“Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” (Wagalatia 5:22-23)
“Nanyi mkivumiliana na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo nanyi. (Wakolosai 3:13)
“Tazama ni jinsi gani upendo wa Baba alivyotupa, kwamba tuitwe watoto wa Mungu; na ndivyo tulivyo.” (1 Yohana 3:1)

Hitimisho

Kuongozwa na Roho Mtakatifu ni wito wa kila Mkristo. Ni mwaliko wa kuacha maisha yetu yaongozwe na Mungu, na kuishi kulingana na mapenzi yake. Tamaa za kidunia ni kikwazo kikubwa kwa uhusiano wetu na Mungu, lakini kwa nguvu na mwongozo wa Roho Mtakatifu, tunaweza kuzishinda na kuishi maisha yaliyojaa matunda ya Roho. Tuishi maisha ya kuongozwa na Roho, tukijua kwamba Mungu yupo nasi na anatupatia nguvu ya kushinda kila jaribu na changamoto.

Mapishi ya tambi za kukaanga

Kupika tambi ni kama ifuatavyo

VIAMBA UPISHI

Tambi pakti moja

Sukari ยพ kikombe cha chai

Mafuta ยฝ kikombe cha chai

Iliki kiasi

Maji 3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose 1-2 Tone

Zabibu Kiasi (Ukipenda)

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZAKO

1. Zichambue tambi ziwe moja moja.

2. Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina
tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

3. Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

4. Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki
na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari
koroga kidogo na punguza moto.
5. Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili zikaukie vizuri.

6. Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

Kidokezi: Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.

Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ngโ€™ombe

Mahitaji

Mpunga – 4 vikombe

Nyama – 1 kilo moja

Kitunguu maji – 3

Mbatata/viazi – 7 vidogodogo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu

Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 3 vipande

Hiliki – 7 punje

Pilipili manga nzima – 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Mafuta – ยฝ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele weka kando
Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.

Mapishi ya Wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

Wali Wa Nazi

Mpunga – 4 vikombe

Tui la nazi – 6 vikombe

Chumvi – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha
Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi Wa Samaki Nguru

Samaki – 4

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 2 viijiko vya supu

Kitunguu maji kilokatwakawa – 2 slice ndogo

Nyanya/tungule – 4

Nyanya kopo – 3 vijiko vya supu

Pilipili mbichi – 2

Kotmiri ilokatwakatwa – 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) – I kijiko cha chai

Ndimu – 1 kamua

Mafuta – ยผ kikombe

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katakata samaki mkaange kwa kumtia viungo.
Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi thomu na tangawizi mbichi, nyanya, nyanya kopo, kitunguu na bizari ya mchuzi endelea kukaanga.
Tia maji kiasi na ndimu, pilipili mbichi ilosagwa kisha tia kotmiri.
Mwisho tia nusu ya samaki alokaangwa ukiwa tayari

Bilingani Za Kukaanga Na Viazi

Bilingani – 4 madogodogo

Viazi/mbatata – 3

Nyanya – 3

Majani ya mchuzi/mvuje/curry leaves – kiasi 6-7

Nnyanya kopo – 2 vijiko vya supu

Methi/uwatu ulosagwa – 1 kijiko cha chia

Rai/mustard seeds – 1 kijiko cha supu

Bizari ya manjano/haldi/turmeric – 1 kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Weka mafuta ya kukaangia katika karai

2. Katakakata bilingani vipande vipande vya mraba (cubes) kaanga katika mafuta ya moto hadi yageuke rangi. Eupa weka kando.

3. Katakataka viazi/mbatata vipande vidogodogo vya mraba (cubes) Kaanga hadi viive epua weka kando.

4. Ondosha mafuta yote katika karai bakisha kidogo tu kiasi ya vijiko 2 vya supu.

5. Kaanga rai kisha majani ya mchuzi, na methi/uwatu kisha kaanga nyanya.

6. Tia nyanya ya kopo kisha changanya pamoja bilingani na viazi ikiwa tayari.

Njia za kutunza nywele zako

Suala la kutunza nywele za asili wengi hutamani japokuwa ukweli kwamba kuna changamoto kadhaa, lakini kwa mtu aliye makini anao uwezo wa kupata kilicho bora katika nyewle zake. Leo tunaangazia vitu vya kufanya ili kukuza na kutunza nywele za asili.

Kwanza kabisa unapaswa kuzikubali nywele zako na kuzipenda , jambo hilo litapelekea mahusiano mazuri, kuelewa tatizo la nywele zako na kuanza kuchukua hatua taratibu ya kuzipatia uvumbuzi tatizo hilo.

Pili, unapaswa kufanya usafi wa kina wa ngozi na nywele zenyewe kwasababu endapo nywele zitaachwa chafu, basi ule uchafu unaziba matundu ya nywele na kuzuia njia kama vile ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata chunusi.

Tatu, ni kulinda unyevu wa nywele . pale zinapooshwa, yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu. Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyoo vizuri na zikikauka zinakuwa kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri, zikafanyiwa โ€˜conditionโ€™ , kwa zile nywele ambazo ni nyepesi na chache pia kuna bidhaa zinasaidia kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

Hatua nyingine ni ya kupaka mafuta kichwani, kwani mafuta yana umuhimu mno katika ukuaji wa nywele na mafuta mazuri ni ya nazi ambayo yamewafaa baadhi ya watumiaji wengi .

Njia nyingine ni ya kuzichambua vizuri nyele kabla ya kuzichana, hapa mtu anatakiwa kuwa na subira na nywele zake , asifanye pupa kuzichana na ikiwezekana aziloweshe maji kidogo halafu ndipo azichane kwa chanuo kubwa lenye upana wa kutosha (wide toothed comb) ili kuzipa afya na kuepuka kujiumiza wakati wa kuzichana.

Pia mtu anayetunza nywele za asili anatakiwa kupunguza matumizi ya vitu vyenye moto katika nywele zake kama vile pasi ya nywele na vingine kama hivyo. Nywele zinatakiwa zichanwe kawaida na ziachwe zikauke zenyewe kwa hewa bila kuzilazimisha.

Maswali na Majibu kuhusu Sala

Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;
โ€œNiite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua”.(Yeremia 33:3)
Vile tunavyokuwa na juhudi ya kusali kwa kusema mbele ya Mungu ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa tuwe na juhudi ya kumsikiliza Mungu kile anachotuambia.
Tunaweza kumsikiliza Mungu ndani kabisa ya Mioyo yetu, mara nyingine kwa kupitia dhamira zetu, kupitia watu wengine na kupitia neno lake (Biblia). Tuombe neema ya kutambua sauti yake anaposema nasi ili tuweze kumsikiliza na kutengeneza mahusiano mazuri kati yetu na yeye.
Mungu ni Baba yetu, anatupenda sana na yupo tayari kutusikiliza wakati wote ndio maana Mungu anatualika kwa kutuambia;
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Tudumu katika sala daima kwa sababu njia ya sala ndipo tunaweza kusema yale tunayotaka mbele ya Mungu na kusikia yale anayotaka Mungu.


Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;
  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu

1. Kumwabudu Mungu

Tunasali ili kumwabudu Mungu, yaani kumpa heshima ya mwisho juu ya kila kitu. Kuonyesha kuwa ni mkuu na wa kipekee kuliko mtu au kitu chochote.

2. Kumshukuru Mungu

Tunasali ili kumshukuru Mungu kwa yale yote aliyokwisha kuyatenda, anayoyatenda na yale atakayoyatenda. Tunamshukuru Mungu kwa yote kwa kuwa yote anayoyafanya anayafanya kwa Mapenzi/ Matakwa yake Matakatifu. Nia ya Mungu ni njema daima ndio maana tunapoona ameruhusu mambo ambayo kwa akili zetu tunayaona ni magumu na sio mema tunapaswa kushukuru kwa sababu ameyafanya kwa makusudi mema.
Biblia inatuambia hivi;
16 Furahini siku zote; 17ombeni bila kukoma; 18shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. (1 Wathesalonike 5:16-18)
Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa Kila jambo na kumshukuru huku ni kwa njia ya sala.

3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu

Tunasali kwa kuomaba neema na baraka kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya wenzetu. Tunamuomba Mungu baraka na Mkono wake katika yale tunayoyafanya na kwa yale wanayoyafanya wengine.
Maombi yetu ili ykubalike mbele ya Mungu ni lazima yawe katika mapenzi yake na yawe na nia njema. Tunafundishwa hivi katika biblia;
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. (Yakobo 4:3)
Tunatakiwa tusali kwa kuomba mema na kwa nia njema ili tuweze kupata yale tunayoyaomba kwa Mungu.

4. Kuomba Msamaha

Tunasali ili kuomba msamaha mbele ya Mungu kwa yote mabaya tuliyoyafanya. Mungu ni mwaminifu hasa kwenye kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu.
9Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:9)
Vilevile Tunatakiwa kusali katika mapungufu yetu na kuwa na matumaini.
9Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. (2 Wakorinto 12:9)

6. Kumsifu na kumtukuza Mungu

Tunasali ili kusifu na kumtukuza Mungu. Mungu anapenda kusifiwa na kutukuzwa. Kwa njia ya sifa tunapokea neema na baraka hata ambazo hatujaziomba.
1Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (Zaburi 100:1-4)


Nani anapaswa kusali?

Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Sala ndiyo njia pekee ya kumuunganisha Mwanadamu na Mungu. Tunapaswa kusali Katika hali yoyote. Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali vivyo hivyo tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali.
Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kudumu katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona hali yetu ya kiroho ipo vizuri. Hatupaswi kuacha kusali kama tumepata neema ya kusimama vyema mbele ya Mungu.
Tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kurudi katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona tupo katika hali ya dhambi. Kwa njia ya sala ndipo tutakapoweza kutoka katika hali ya dhambi.
Mungu yupo tayari kusikiliza ukiwa katika hali ya neema au kama ukiwa katika hali ya dhambi. Ndio maana tunapaswa kumwelekea Mungu katika hali yoyote tulio nayo.
14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. (1 Yohane 5:15)
Tena Mungu anasubiri tumuombe ili furaha yetu itimilike.
24Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. (Yohane 16:24)
Hata kama tuna dhambi Mungu yupo tayari kutupokea na kutusikiliza.
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Mungu yupo tayari kutusikiliza hata tunapokuwa wadhambi kwa kuwa haziweki dhambi zetu na makosa yetu mbele yetu. Huruma yake ni kubwa kushinda dhambi zetu.
12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. (Zaburi 103:12-13)
Mungu anatuwazia mema daima ndio maana tunapaswa kusali kwake
11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 12Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. (Yeremia 29:11-13)


Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu.
Tunatakiwa tusali daima Kama Yesu alivyotuhimiza kwa mfano huu;
1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? 
(Lk 18:1-8)
Kwa hiyo basi, Tusali daima kila siku, kila saa na katika hali yoyote. Tusichoke kusali hata kama maombi Yetu hayajajibiwa. Mungu ni mwenye Hekima na anajua lini hasa akujibu kile unachokiomba kwa manufaa yako wewe. Usipopewa Leo kile ukiombacho unaweza kukipata kwa wakati ufaao tena bila ya Kukiomba.

Sala ni Hazina

Sala ni hazina. Kusali ni kujiwekea hazina. Sala unayosali leo inaweza kukunufaisha wakati usioutarajia.

Maana ya Sala kwa Mkristo Mkatoliki

Maana ya sala kwa Mristu Mkatoliki sio kuomba tuu. Sala kwa Mkatoliki ni zaidi ya kuomba. Kwa Mkatoliki sala inamaanisha kufanya haya;
  1. Tunasali kushukuru,
  2. Tunasali kuomba,
  3. Tunasali kusifu na Kutukuza,
  4. Tunasali kumshirikisha Mungu Furaha zetu na huzuni zetu,
  5. Tunasali kuomba Toba na Msamaha,
  6. Tunasali kumshirikisha Mungu Juhudi zetu na Mipango yetu,
  7. Tunasali kumshirikisha Mungu changamoto zetu.
Tuna kila sababu ya Kusali kila Siku na Kila saa. Maisha yetu yote yanatakiwa yawe Maisha ya Sala. Usifikiri kwamba Wakati wote unaposali lazima utamke maneno Mengi sana ili uwe umesali, Sala haipimwi kwa Maneno. Sala inapimwa kwa nia yake na Kujiweka wazi mbele ya Mungu.
Kila Usalipo Jijengee Tabia ya kunuia, kuwa wazi na kusali kwa ukweli wa Moyo wako. Hata kama ni sentesi Moja fupi Kabisa itamke kwa Upendo na Imani. Kwa Mfano, kuna wakati inatosha kabisa kusema Ee Mungu wangu ninakushukuru kwa hili, hii inaweza kuwa sala Yenye nguvu Kama imetamkwa kwa Imani, Shukrani na Mapendo ya Kweli. Maneno machache yanayotamkwa kwa Imani na Mapendo yanaweza kuzidi Mkesha wa Kusali Usiku Mzima huku unasinzia.
Pamoja na kwamba sala fupi ni nzuri na inafaa sana, kuna haja pia ya kujitengea Muda wa Kutosha Kusali na Kutafakari Huku tukiungana na Mungu. Kila siku tunanye mambo yote mengine lakini tusisahau kuwa Tunahitaji kuwa na Muda wa Kusali.
Tusali daima, Kila wakati na Maisha yetu yawe ni Maisha ya Sala.
Mungu Akubariki sana, Azijibu sala zako na Akujalie Neema ya Kuwa Mtu wa Sala.


Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;
9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 
Luka 18:9-14
Tunatakiwa tusali kwa nia njema na kwa kufuata Mapenzi ya Mungu ili sala zetu zipate kibali mbele za Mungu. Tunapoomba kwa nia mbaya ya tamaa na majivuno hatuwezi kupata kile tukiombacho.
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Yakobo 4:3
Mungu anajibu sala zetu kulingana na nia ya kile tunachokiomba. Watu wote waliofanikiwa Katika sala zao walifanikiwa kwa sababu ya nia ya kile walichokiomba.
Sala sio kutamka manano tuu, sala ni kutamka maneno kwa kunuia. Tena tusalipo yatupasa kujua kuwa tunaongea na Mungu na sio tuu kwamba tunatamka maneno. Tusisahau nia kuu ya kusali ambayo ni mawasiliano Yetu na Mungu.
Tunaposali Tunapaswa Kukumbuka na kuzingatia haya;
  1. Nia na Imani (Kuamini na Kuwa na Uhakika na Unachokifanya)
  2. Unyenyekevu wa Kweli
  3. Ibada na Uchaji
  4. Upendo na Uwazi (Honest)
  5. Matumaini na Saburi (Subira)
Kila unaposali jiulize unasali kwa kwa sababu gani? Kila ubapoomba, jiulize unamuomba Mungu ili nini? Sababu yako ndio kibali cha sala yako.
Mungu Akubariki kwa Kukujalia Imani, Unyenyekevu, Ibada, Uwazi na Matumaini Usalipo. Uwe na Amani.


Sala zipo za namna ngapi?

Sala zipo za namna tatu,
1. Sala ya sauti
2. Sala ya fikara
3. Sala ya taamuli


Sala ya Taamuli ni nini?

Sala ya taamuli ni sala ya kumtazama tuu Mungu kwa upendo mkubwa moyoni


Sala ya sauti ni nini?

Sala ya sauti ni sala asaliyo mtu au kundi kwa kutamka maneno


Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu


Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Ni nyakati gani zafaa kwa sala?

Nyakati zote zafaa kwa sala hasa:
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila Dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi


Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13)


Je, yatupasa kuombea wengine?

Ndiyo. Yatupasa kuwaombea watu wote hasa wenye shida, wakosefu na hata maadui zetu.


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,โ€œTazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.โ€™โ€™ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, โ€œBaba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.โ€™โ€™ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, โ€œJe, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41โ€˜โ€˜Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.โ€™โ€™ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, โ€œBaba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.โ€™โ€™ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: โ€˜โ€˜Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.โ€™โ€™ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: โ€œMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.โ€
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, โ€œBaba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.โ€™โ€™ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, โ€œJe, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41โ€˜โ€˜Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.โ€™โ€™ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, โ€œBaba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.โ€™โ€™ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, โ€œKatika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, โ€˜Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.โ€™ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4โ€œKwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, โ€˜Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!โ€™ โ€ 6Bwana akasema, โ€œSikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?โ€ (Luka 18:1-8)


Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambiaโ€ฆ
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;
1. Misa Takatifu
2. Baraka ya Sakramenti Kuu
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari Takatifu
6.Novena


Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala


Mahali gani panafaa kwa sala?

Mtu anaweza kusali mahali popote lakini Kanisani ndipo mahali Rasmi pa sala


Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;
1. Mtawanyiko wa Mawazo
2.Ukavu wa moyo
3. Uvivu na Uregevu
Ndiyo maana kwa Wakatoliki sala nyingi zimeandikwa ili kutuongoza hasa tunapokuwa majaribuni katika sala.


Neno “Amina” katika sala lina maana gani?

Neno “Amina” katika sala lina maanisha “Na iwe Hivyo” (Hesabu 5:22)


“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maanisha “Msifuni Mungu”


Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?

Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?

Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?

Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili kushinda vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
โ€œEwe pepo mchafu, mtoke mtu huyuโ€ (Mk 5:8).
โ€œEwe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!โ€ (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
โ€œAliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafuโ€ (Mk 6:7).
โ€œPaulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, โ€˜Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyuโ€™. Akamtoka saa ileileโ€ (Mdo 16:18).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
โ€œNena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikiaโ€ (1Sam 3:10).
โ€œNakutafakari Wewe makesha yote ya usikuโ€ (Zab 63:6).
โ€œSheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwaโ€ (Zab 119:97).
โ€œManeno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wanguโ€ (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
โ€œIkawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, โ€˜Bwana, tufundishe sisi kusaliโ€ (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
โ€œBaba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze weweโ€ (Yoh 17:1).
โ€œAba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo weweโ€ (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
โ€œWazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuuโ€ (Lk 2:41-42).
โ€œSaa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, โ€˜Eloi, Eloi, lama sabakthani?โ€™โ€ (Mk 15:34).
โ€œEe Baba, mikononi mwako naiweka roho yanguโ€ (Lk 23:46).


Je, sala ya Yesu inatokana na utu wake tu?

Hapana, sala ya Yesu haitokani na utu wake tu, bali katika huo Mwana wa milele ndiye anayemuelekezea Baba yake sala kamili ya kitoto.
โ€œSaa ileile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, โ€˜Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendezaโ€ (Lk 10:21).
โ€œBaba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzoteโ€ (Yoh 11:41- 42).
โ€œBaba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendaloโ€ (Lk 23:34).


Yesu alisali vipi?

Yesu alisali kila mahali na kila wakati, akidumisha ushirika wa upendo kati yake na Baba katika Roho Mtakatifu.
โ€œSaa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabuduโ€ (Yoh 4:23).
Pamoja na kushiriki kiaminifu ibada za taifa lake, mara nyingi alijitafutia mahali pa faragha.
โ€œAliongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikaniโ€ (Lk 4:1).
โ€œAlikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaombaโ€ (Lk 5:16).
โ€œAliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Munguโ€ (Lk 6:12).
Ndiyo sababu ametuambia,
โ€œWewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye siriniโ€ (Math 6:6).
Tusipojua kuongea na Baba moyo kwa moyo, tutawezaje kuongea naye kati ya umati?


Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo.
โ€œUpatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yakoโ€ฆ Waombeeni wanaowaudhiโ€ฆ Msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watuโ€ (Math 5:24,44; 6:5).
โ€œMtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, โ€˜Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambiโ€™. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa hakiโ€ (Lk 18:13-14).
Hasa ametutia Roho Mtakatifu atuongoze kama alivyomfanyia yeye.


Je, Yesu ametufundisha maneno ya sala pia?

Ndiyo, Yesu ametufundisha maneno ya sala ya โ€˜Baba Yetuโ€™, kamili kuliko zote. Maombi yake saba yanategemea utangulizi ambao tunamuendea Mungu kwa ujasiri na furaha kama watoto wake, ndugu kati yetu.
Maombi matatu ya kwanza yanalenga atukuzwe, atawale, apate ushirikiano wetu. Maombi manne ya mwisho yanalenga tupate chakula cha roho na cha mwili, msamaha wa dhambi, ushindi katika vishawishi, usalama dhidi ya yule Mwovu.
โ€œBaba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hiviโ€ฆโ€ (Math 6:8-9).


Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga
โ€œjuu ya imaniโ€ฆ na kuomba katika Roho Mtakatifuโ€ (Yud 20).
โ€œMkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana hao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengiโ€ (Math 6:7).
Hii haituzuii tusirudie maneno yetu kwa dhati zaidi na zaidi.
Yesu โ€œalikwenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yaleyaleโ€ (Math 26:44).
Tunaweza kusali kimoyomoyo pia.
โ€œHana alikuwa akinena moyoni mwake, midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiweโ€ฆ โ€˜Nimeimimina roho yangu mbele za Bwanaโ€™โ€ (1Sam 1:13,15).
โ€œManeno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwanaโ€ (Zab 19:14).


Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba.
โ€œHata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifuโ€ (Yoh 16:24).
Lakini Baba, kwa ujuzi na upendo usio na mipaka, anaweza akatupatia mambo tofauti na yale tuliyomuomba.
โ€œKama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, โ€˜Nipe maji ninyweโ€™, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo haiโ€ (Yoh 4:10).
โ€œIkiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?โ€ (Lk 11:13).
Imani yetu ikubali kwamba aliyotupatia ni bora zaidi.


Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani.
Mhalifu alisema,
โ€œโ€˜Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wakoโ€™. Yesu akamwambia, โ€˜Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponiโ€ (Lk 23:42-43).
Stefano aliomba,
โ€œโ€˜Bwana Yesu, pokea roho yanguโ€™. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, โ€˜Bwana, usiwahesabie dhambi hiiโ€™โ€ (Mdo 7:59-60).
โ€œRoho na Bibi arusi wasema, โ€˜Njoo!โ€™. Naye asikiaye na aseme, โ€˜Njoo!โ€™โ€ฆ Na uje, Bwana Yesu!โ€ (Ufu 22:17,20).


Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
โ€œMungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, โ€˜Aba!โ€™ yaani, โ€˜Baba!โ€™โ€ (Gal 4:6).
โ€œRoho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwaโ€ฆ huwaombea watakatifu kama apendavyo Munguโ€ (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, โ€˜Njoo, Roho Mtakatifu!โ€™ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.


Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
โ€œYeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Munguโ€ (Ef 3:16-19).
โ€œHuyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yoteโ€ (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.


Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote.
โ€œKwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetuโ€ (Rom 8:38-39).
โ€œKwangu mimi kuishi na Kristo, na kufa ni faidaโ€ฆ Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristoโ€ (Fil 1:21,23)
.
Kwa kuwa hao wako na Kristo mbinguni, wanatuombea mfululizo pamoja naye.
โ€œNiliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, โ€˜Ee Mwenyezi, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata liniโ€ฆโ€™โ€ (Ufu 6:9-10).
Tunawaomba wazidi kutuombea kwa Mungu, kama tunavyowaomba wenzetu waliopo duniani.
โ€œMkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimiโ€ (Ef 6:18-19).


Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Mabinti wengine kwa kupenda hela! cheki huyu anachokifanya

Phone call
gal: hellow
Boy: sweety mambo vipi?
Girl: poa
Boy: utakuwa free weekend? nilikuwa nataka uje nyumbani
Girl: oh sorry ctoweza kuja sababu kuna haruc ya aunt yangu
Boy: kama ni hivyo sawa nilikuwa nataka nikufanyie sapraiz nimekununulia BLACKBERRY.
Girl: oh ucjal ntakuja na hata ntalala huko huko
Boy: na haruc je?
Girl: nilikuwa nakutania
Boy: hata mi nilikuwa nakutania

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About