Karibu AckySHINE
Karibu AckySHINE
Chagua Unachotaka Kusoma Hapa
Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.
Faida za kula karanga mbichi
Karanga ni muhimu sana katika afya ya mwili wa binadamu. Kiukweli karanga siyo chakula cha kupuuziwa iwapo utajua faida zake kama nitakavyokujuza leo katika makala haya.
1. Kwanza kabisa karanga husaidia katika kutibu magonjwa ya moyo.
Kama ilivyokuwa kwa korosho, karanga nazo ni chanzo kizuri cha mafuta mazuri aina ya monounsaturated fatsโ ambayo yanatiliwa mkazo kutumiwa kwa afya ya moyo. Kwa mujibu wa utafiti, watu wanaokula karanga mara kwa mara hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo (cardiovascular heart disease).
Aidha, katika taarifa iliyochapishwa kwenye jarida moja la Uingereza la โJournal of Nutritionโ ambako kuna matokeo ya taarifa nne za utafiti, imeonesha pia watu wanaotumia karanga mara kwa mara, angalau mara nne kwa wiki, hujipa kinga nyingine dhidi ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) kwa zaidi ya asilimia 37.
Mbali ya kuwa na mafuta mazuri yanayotoa kinga kwenye moyo, karanga pia, zinaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha virutubisho vinavyotoa kinga ya mwili (antioxidants) kuliko hata kile kinachopatikana kwenye tunda la epo na karoti!
Ili kupata kinga hiyo dhidi ya aina hizo mbili za ugonjwa wa moyo, ambao unatesa watu wengi duniani na kugharimu pesa nyingi kwa matibabu, unashauriwa kula karanga pamoja na bidhaa zake kama vile peanut butte, angalau kijiko kimoja cha chakula, mara nne kwa wiki.
2. Kinga dhidi ya kiharusi.
Ugonjwa mwingine hatari unaosumbua watu wengi hivi sasa ni kiharusi au strokeโ, lakini unaweza kujikinga nao kwa kuwa na mazoea ya kula karanga tu.
Utafiti umeonesha kuwa karanga ina kirutubisho aina ya Resveratrol ambacho hupatikana pia kwenye zabibu na mvinyo mwekundu (red wine). Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa maabara na kuchapishwa kwenye jarida la Kilimo na Kemia ya Chakula (Journal of Agricultural Food Chemistry),
umeonesha kuwa kirutubisho hicho huimarisha utembeaji wa damu kwenye mishipa inayokwenda kwenye ubongo kwa kiasi cha asilimia 30.
3. Kinga dhidi ya magonjwa ya moyo.
Faida nyingine inayoweza kupatikana kwenye mwili kutokana na ulaji wa karanga, ni kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, unaonesha kuwa virutubisho vya folic acid, phytosterols, phytic acidโ (inositol hexaphosphate) na resveratrolโ vinavyopatikana kwenye karanga, huweza kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya tumbo.
Zaidi utafiti huo umeonesha kuwa ulaji wa karanga hata mara mbili tu kwa wiki, una uwezo wa kupunguza uwezekano wa kupatwa na saratani ya tumbo kwa asilimia 58 kwa wanawake na asilimia 27 kwa wanaume. Kwa maelezo hayo kuhusu faida za karanga mwilini bila shaka chakula hiki kinapaswa kupewa kipaumbele katika orodha ya vyakula tunavyokula.
kila siku na hakika Mungu ametupenda sana kwakutupa kinga dhidi ya maradhi yote yanayotukabilikwa njia ya vyakula.
Kwa nini Wakatoliki wanaungama dhambi kwa Padri?
“Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungiwa dhambi wamefungiwa”(Yohane 20:22-23).
“Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako”
“Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana ‘leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu’ hapo akatoka nje,akalia sana.”
Mapishi ya Wali, samaki wa nazi na kisamvu
Mahitaji
Mchele
Kisamvu kilichotwangwa
Samaki
Mbaazi
Nyanya chungu
Vitunguu
Nyanya ya kopo
Tangawizi
Kitunguu swaum
Vegetable oil
Curry powder
Tui la nazi (kopo 2)
Chumvi
Pilipili
Limao
Matayarisho
Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.
Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.
SMS nzuri sana ya kutakia usiku mwema
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii, Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Maneno na matendo
Uwe mzuri kwenye kufanya kama ulivyo kwenye kufikiri. Matendo yako yafanane na maneno na maneno na matendo.
Maswali na Majibu kuhusu Hukumu ya Mwisho
2. Hukumu
3. Jehanamu (Motoni)
4. Paradiso. (Toharani/Mbinguni)
Ahadi kumi na mbili za Moyo Mtakatfu wa Yesu
Na kwa maneno yake mwenyewe, Bwana Yesu aliahidi:
1. โNitawajalia neema zote watakazozihitaji katika hali yao ya maisha
2. Nitawajalia amani katika familia zao
3. Nitawafariji katika magumu yao yote
4. Nitakuwa kimbilio lao salama wakati wa maisha yao, na zaidi sana katika saa yao ya kufa
5. Nitawapa baraka tele katika shughuli zao zote
6. Wakosefu watapata katika Moyo wangu chanzo na bahari ya huruma isiyo na mwisho
7. Waumini walio vuguvugu watakuwa na bidii
8. Waumini wenye bidii watakwea kwa upesi katika ngazi za juu za ukamilifu
9. Nitabariki kila mahali ambapo picha au sanamu ya Moyo wangu Mtakatifu itawekwa na kuheshimiwa
10. Nitawajalia mapadre karama ya kuigusa mioyo migumu
11. Wale wote watakaoeneza Ibada hii kwa wengine majina yao yataandikwa ndani ya Moyo wangu na sitawasahau kamwe
12. Wale wote watakaopokea Sakramenti ya Ekaristi kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi kwa miezi tisa mfululizo wakiwa katika hali ya neema ya utakaso, hawatakufa wakiwa na uadui nami, nitawapa neema ya kudumu katika uaminifu hadi mwisho na hawatakufa bila kupokea Sakramenti za mwishoโ.
Faida na namna ya kutumia mafuta ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele
Faida ya Mafuta Ya Zaituni Olive Oil kwenye nywele.
1. Yanasaidia kufanya mzunguko wa damu kufanya kazi vizuri kwenye ngozi ya kichwa na kupenyeza hadi kwenye shina ya nywele kisha kuifanya nywele inayoota kuwa imara
2. Yanasaidia kupambana na mba kwenye ngozi ya kichwa
3. Yanasaidia uzalishwaji wa mzizi au shina ya nywele
4. Yanasaidia uzalishwaji wa melanin ambayo inafanya kazi ya kutoa rangi ya nywele inayotakiwa.
5. Yanasaidia kuifanya nywele isiwe kavu sana.
NAMNA YA KUZIHUDUMIA NYWELE:
Unaweza kuchanganya na Mdalasini pamoja na Asali.
1. Olive oil vijiko 2 vya chakula
2. Asali kijiko 1 cha chakula
3. Mdalasini kijiko 1 cha chai
Pasha moto olive oil kisha changanya vyote kwa pamoja pakaa kwenye nywele acha kwa muda wa dakika 20 kisha osha nywele zako na upakae mafuta zikishakauka.
Ninashauri utumie mafuta haya kwenye nywele na ngozi ni mazuri sana. Ukiwa na mba pakaa kwenye ngozi mba itaisha na muwasho utaondoka.
Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga
Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-
1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!
Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng’ombe Karoti Na Zabibu
Vipimo – Nyama
Nyama ngโombe ya mifupa ilokatwa vipande – 1 kilo
Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa – 2 vijiko vya supu
Bizari mchanganyiko/garama masala – 1 kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Vipimo – Wali
Mchele – 4 glass
Mbatata/viazi menya katakata – 3 kubwa
Vitunguu katakata – 5
Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) – 1 kijiko cha supu
Hiliki ya unga – 1 kijiko cha chai
Bizari nzima ya pilau/cumin – 1 mti
Samli au mafuta – 2 Vijiko vya supu
Karoti zilokatwakatwa nyembamba – 6-7
Zabibu – Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake.
kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele.
Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto.
Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo.
Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive.
Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu.
Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.
Madhara ya kumlaza mtoto kifudifudi, kumlaza kwa tumbo
Unafahamu nini kuhusu suala la kumlaza mwanao? Maana Mapokeo tuliyo yapokea enzi na enzi ni kuwa ukitaka mtoto wako alale bila kushtuka basi alalie tumbo. Bado watu wengi wanaendelea kufanya hivyo hata sasa hivi unaposoma makala haya.
Je madaktari wanasemaje kuhusu suala hili?
Sayansi inashauri kuwa ni hatari kumlaza mtoto kwa tumbo. Visa kadhaa vya watoto kupoteza maisha vimehusishwa na watoto kulalia tumbo.
Kuanzia mwaka 1992 Madaktari wa watoto nchini Marekani walipendekeza kuwa watoto wachanga walale chali ( walalie Mgongo) ili kuepuka vifo vya ghafla vya watoto. Kifo cha ghafla hutokea pale ambapo mtoto mchanga anakutwa amefariki akiwa usingizini.
Tangu pendekezo hilo la madaktari idadi ya vifo vya ghafla vya watoto imepungua zaidi ya nusu ya vifo vyote vya watoto vinavyotokea wakiwa usingizini.
Ni vizuri kuhakikisha kuwa kila mtu anayekusaidia kulea mtoto anajua jinsi ya kumlaza mtoto chali.
Muhimu
Hata hivyo kuna baadhi ya watoto unaweza kushauriwa na daktari iwapo mwanao usimlaze chali na alalie tumbo.
Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai
Viambaupishi
- Mchele (Basmati) – 3 vikombe
- Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) – 1 kikombe
- Kuku Kidari – 1 LB (ratili)
- Mayai – 2 mayai
- Vitunguu (vikubwa) – 2 au 3 vidogo
- Pili pili manga – 1 kijiko cha chai
- Paprika – 1 kijiko cha chai
- Chumvi – Kiasi
- Mafuta – 1/3 kikombe cha chai
- Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
- Tangawizi – 1 kijiko cha chai
- Kidonge cha supu – 1
- Soy sauce – 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku
Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.
Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)
Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.
Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.
Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali
Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.
Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi
Wacha uchemke asilimia 70%
Chuja maji na weka kando
Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu
Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)
Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga
Kisha tia wali changanye vizuri
Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive
Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.
Mapishi ya Sponge keki
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) 100g
Sukari (sugar) 100g
Siagi isiyokuwa na chumvi (unsalted butter) 100g
Mayai (eggs) 2
Vanila 1 kijiko cha chai
Chumvi pinch
Warm water 3 vijiko vya chakula
Matayarisho
Kwanza washa oven moto wa 200ย C. Baada ya hapo saga butter na sukari mpaka viwe laini kisha tia mayai na uendelee kusaga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia unga, vanila, chumvi na na maji na usage mpaka upate uji usiokuwa mzito sana au mwepesi sana. Baada ya hapo utie kwenye baking tin na u bake kwa muda wa dakika 25 na mpaka cake yako iive yani juu na chini iwe ya brown na ukidumbukiza kijiti katikati kinatoka kikiwa clean. Baada ya hapo itoe kwenye tin na uiache ipoe. Ikisha poa itakuwa tayari kwa kuliwa.
Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51
Mchanganuo wa Tsh 300,000/= kwa uzalishaji wa kuku wa kienyeji kwa faida
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina kilo 70.
– paraza kilo 25 = 700×25 =17500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
-mashudu ya alizeti kilo 15. 700×15=10500
– layer’s consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga
Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2×2 au 4×2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator).
Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200.
Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200.
Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.
ย
Namna ya kupika Vitumbua
Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi
Mahitaji:
Unga wa mchele ยฝ kg
Sukari vijiko 4 vya mezani
Tui bubu la nazi
Mafuta ya kupikia
Unga wa hiliki ยฝ kijiko cha chai
Hamira kijiko 1 cha chai
Chuma cha vitumbua
Maandalizi:
Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja
Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako
Weka hiliki koroga hadi view uji mzito
Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa,
Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto Kisha kaanga virumbua vyako
Duh, hii sasa kazi
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ #Hatutaki ujinga
Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
Sababu 5 zinazosababisha wanawake warembo wazuri wasiolewe
Wanawakeย wengi warembo husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu tofauti.
Wengi huwa na tabia za kuudhi hali ambayo huwafukuza wanaume walio na uwezo wa kuwaoa
Umewahi kushangaa sababu za wanawake warembo zaidi kutoolewa? Kuna sababu tano ambazo huwafanya wanawake warembo kusalia wapweke.
1. Tabia mbaya
Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya na kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani.
2. Baadhi ya wanawake hao huwa na maringo sana
eti hawawezi kuosha nyumba kwa kuogopa kucha zao zisikatike. Wengine hawaju kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.
3. Ghali kuwatunza
Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.
4. Wabinafsi na wenye chuki
Wanawake wa aina hiyo hufikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuhusiana na wanawake wa aina hiyo, ambao huwadharau kutokana na kuwa โwanapendwaโ na wanaume wengi.
Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa.
5. Hawataki kuwa wazazi
Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wa kupendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika.
Kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume.
I’m so happy you’re here! ๐ฅณ














































































Recent Comments