1. Ticha:”Punda ni mnyama anaefugwa nyumbani,lakini akiwa mwituni anaitwa pundamilia….Je sungura anayeishi mwituni anaitwaje?”
ZUZU:”Sunguramilia.”
2.Ticha:”Rais wa kwanza wa kenya aliitwa KENYATTA…Je rais wa kwanza wa
Tanzania aliitwaje?”
ZUZU:”TANZANIATTA.”
3. Ticha:”Kuku yuko katika jamii ya NDEGE…Je samaki yuko katika jamii ya nini?”
ZUZU:”MELI.”
4. Ticha:”Coach wa Arsenal anaitwa ARSENE,wa Man-city anaitwa MANCINI….Je wa
Liverpool anaitwaje?
ZUZU:”LIVER.”
5 Ticha:”Ukiwa na mbuzi 10,wezi waje waibe 5,utabaki na nini?”
ZUZU:”Hasira nyingi sana!”
Hii kichekesho itaingia moja kwa moja kwenye vipendwa vyangu! 😂
😂 Siwezi kuacha kucheka!
🤣 Hii imenigonga vizuri!
🤣👍👌
Nilihitaji kicheko hiki, asante kwa kushiriki! 😅